AI-assisted research summary: Rais ametangaza tarehe 23 Agosti 2022 kuwa siku ya mapumziko.
Tamko la Siku ya Sensa ya Watu na Makazi Kuwa Siku ya Mapumziko ISSN 0856 - 034X Tangazo la Serikali Na. 521 (Linaendelea.) THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA Supplement No. 32 19th August, 2022 SUBSIDIARY LEGISLATION To The Gazette Of The United Republic Of Tanzania No. 33 Vol. 103 Dated 19th August, 2022 Printed By The Government Printer, Dodoma By Order Of Government TANGAZO LA SERIKALI Na. 521 la Tarehe 19/8/2022 SHERIA YA SIKUKUU ZA KITAIFA, (SURA YA. 35) ______ TAMKO ______ (Limetungwa chini ya kifungu cha 3) TAMKO LA SIKU YA SENSA YA WATU NA MAKAZI KUWA SIKU YA MAPUMZIKO LA MWAKA 2022 Sura ya 35 KWA KUWA, kifungu cha 3 cha Sheria ya Sikukuu za Kitaifa, kinampa mamlaka Rais, kwa Tamko, kutangaza siku yoyote kuwa siku ya mapumziko ya nyongeza kwenye siku zilizoainishwa katika Jedwali au kwa kubadilishwa kwa siku yoyote kati ya siku hizo na siku hiyo kuwa ni siku ya mapumziko kama vile ilikuwa imeainishwa kwenye Jedwali; NA KWA KUWA, Sensa ya Watu na Makazi ni zoezi muhimu kwa maendeleo ya nchi na itafanyika kuanzia Siku ya Jumanne tarehe 23 Agosti, 2022 ambayo ni siku ya kazi; NA KWA KUWA, kuifanya siku hiyo ya tarehe 23 Agosti, 2022 kuwa siku ya mapumziko kutawezesha wanakaya wengi kushiriki kikamilifu katika siku hii ya kwanza ya zoezi la Sensa ya Watu na Makazi; 1 Tamko la Siku ya Sensa ya Watu na Makazi Kuwa Siku ya Mapumziko Tangazo la Serikali Na. 521 (Linaendelea.) KWA HIYO BASI, MIMI, SAMIA SULUHU HASSAN, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika utekelezaji wa Mamlaka niliyopewa chini ya kifungu cha 3 cha Sheria ya Sikukuu za Kitaifa, ninatoa Tamko kuwa tarehe 23 Agosti, 2022 itakuwa siku ya mapumziko. Tamko hili limetolewa na kuwekewa Lakiri ya Umma leo tarehe 19 Agosti, 2022. L.S Dodoma, SAMIA SULUHU HASSAN, 19 Agosti, 2022 Rais 2