Tanzania Regulation

Parliament of Tanzania

KANUNI ZA MSAMAHA WA RIBA YA MALIMBIKIZO YA KODI YA PANGO LA ARDHI ZA MWAKA 2022

Kanuni hizi zinaweka utaratibu wa kuomba na kupata msamaha wa riba ya malimbikizo ya kodi ya pango la ardhi, na zinahitaji kodi ya msingi kulipwa ndani ya siku 90 baada ya msamaha kutolewa.

interest remissionland renttax relief applications

Publicly available, excluded from search-engine indexing

This page remains available for direct research for the following reasons:

  • The record does not meet this release's canonical indexing criteria. (market-indexing-disabled)
  • The record does not meet this release's canonical indexing criteria. (emergency-noindex)

Professional statute overview

Enactment structure, operative effect and source provenance

Official source

01

Purpose and legislative effect

“Kanuni hizi zinaweka utaratibu wa kuomba na kupata msamaha wa riba ya malimbikizo ya kodi ya pango la ardhi, na zinahitaji kodi ya msingi kulipwa ndani ya siku 90 baada ya msamaha kutolewa.”

Use this record to locate individual provisions, understand the instrument’s recorded structure, and move from a research summary to the exact source text.

02

How the instrument operates

  1. 01

    Start with the recorded version

    Legal dates not recorded. The date shown identifies this source expression and should not be treated as proof that no later change exists.

  2. 02

    Locate the controlling provision

    Use the provision map, part headings and full-text filter to move from the broad subject to the exact legal language.

  3. 03

    Read conditions and exceptions together

    Keep subsections, definitions, provisos and cross-references in context before drawing a legal conclusion.

  4. 04

    Verify currency and official wording

    Confirm later legislation, commencement notices and corrections with the official publisher before advice, filing or reliance.

03

Research entry points

Selected provisions across the instrument. Open any row to continue with the exact stored text.

Document text

Kanuni hizi zinaweka utaratibu wa kuomba na kupata msamaha wa riba ya malimbikizo ya kodi ya pango la ardhi, na zinahitaji kodi ya msingi kulipwa ndani ya siku 90 baada ya msamaha kutolewa.

Section document

04

Source and current-law status

Source record view

Source record from oagmis.oag.go.tz · Legal dates not recorded

Verify current force

The source record does not state a definitive current-law status. Check the official publisher and later amendments before relying on this text.

Source-indexed provision map

Sections and provisions

Search by section, heading, part or exact legal wording. Every result remains linked to the stored source record.

Showing 1 of 1 provisions

Provision
§ documentDocument textProvision

Kanuni hizi zinaweka utaratibu wa kuomba na kupata msamaha wa riba ya malimbikizo ya kodi ya pango la ardhi, na zinahitaji kodi ya msingi kulipwa ndani ya siku 90 baada ya msamaha kutolewa.

Msamaha wa Riba ya Malimbikizo ya Kodi ya Pango la Ardhi TANGAZO LA SEIKALI NA.537B Supplement No. 34 31st August, 2022 ISSN 0856 – 034X SUBSIDIARY LEGISLATION to the Gazette of the United Republic of Tanzania No. 34 Vol. 103 dated 31st August,2020 Printed by the Government Printer, Dodoma by Order of Government TANGAZO LA SERIKALI NA. 537B la tarehe 31/08/2022 SHERIA YA ARDHI, (SURA YA 113) ________ KANUNI ________ (Zimetengenezwa chini ya vifungu vya 33 (14) na 179) _________ KANUNI ZA MSAMAHA WA RIBA YA MALIMBIKIZO YA KODI YA PANGO LA ARDHI ZA MWAKA 2022 Kanuni Maelezo MPANGILIO WA KANUNI SEHEMU YA KWANZA MASHARTI YA AWALI 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. Jina la Kanuni. Matumizi. Tafsiri. SEHEMU YA PILI MSAMAHA Maombi ya msamaha. Sifa za kupata msamaha. Vigezo vya msamaha. Mapendekezo. Uamuzi. Malipo ya kodi. 1 Msamaha wa Riba ya Malimbikizo ya Kodi ya Pango la Ardhi TANGAZO LA SEIKALI NA.537B SEHEMU YA TATU MASHARTI YA JUMLA 10. Usitishaji wa msamaha. 11. Msamaha kutolewa mara moja. 12. Makosa. ________ JEDWALI __________ SHERIA YA ARDHI, (SURA YA 113) _________ KANUNI _________ (Zimetengenezwa chini ya vifungu vya 33(14) na 179) _________ KANUNI ZA MSAMAHA WA RIBA YA MALIMBIKIZO YA KODI YA PANGO LA ARDHI ZA MWAKA 2022 SEHEMU YA KWANZA MASHARTI YA AWALI Jina la Kanuni 1. Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Msamaha wa Riba ya Malimbikizo ya Kodi ya Pango la Ardhi za Mwaka 2022. Matumizi 2. Kanuni hizi zitatumika kwa ardhi zote zinazotambulika chini ya Sheria. Tafsiri Sura ya 113 3. Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “kodi ya msingi” maana yake ni kodi ya pango la ardhi inayolipwa kwa mwaka kwa mujibu wa kifungu cha 33 cha Sheria; “Sheria” maana yake ni Sheria ya Ardhi; “mwombaji” maana yake ni mtu yeyote anayemiliki sehemu ya ardhi inayoombewa msamaha wa riba ya malimbikizo ya kodi ya ardhi; “msamaha” maana yake ni msamaha wa riba au sehemu 2 Msamaha wa Riba ya Malimbikizo ya Kodi ya Pango la Ardhi TANGAZO LA SEIKALI NA.537B riba ya malimbikizo ya kodi ya pango la ardhi; “Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana na masuala ya ardhi; na “riba ya malimbikizo ya kodi ya pango la ardhi” maana yake ni riba katika kiwango cha asilimia sifuri nukta tano kwa mwezi katika kipindi cha miezi sita tangu tarehe ya kodi hiyo ilipotakiwa kulipwa, na riba katika kiwango cha asilimia moja kwa mwezi baada ya miezi kumi na mbili tangu tarehe ya kodi hiyo ilipotakiwa kulipwa. SEHEMU YA PILI MSAMAHA Maombi ya msamaha 4.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya Kanuni hizi, mtu yeyote ambaye amefanyiwa ukadiriaji wa kodi ya pango la ardhi ambao una riba ya malimbikizo, anaweza kuomba msamaha wa riba kwa Waziri kwa kujaza fomu ilivyoainishwa katika Jedwali la Kanuni hizi. (2) Maombi chini ya kanuni hii yatapaswa kuainisha sababu ya kuomba msamaha. Sifa za kupata msamaha 5. Mtu atastahili kupata msamaha chini ya Kanuni hizi endapo- (a) mtu huyo ni mmiliki wa ardhi isipokuwa kwamba ardhi hiyo haikuwa katika himaya na matumizi yake kwa sababu ya maamuzi ya mamlaka za usimamizi kwa kipindi chote kinachoombewa msamaha; (b) mtu huyo amerejesha ardhi au sehemu ya ardhi na hana maslahi yoyote na nia ya kuendelea kumiliki ardhi hiyo; au (c) kuna utaratibu uliowekwa na kuamuliwa na Serikali kuwezesha utekelezaji wa mikakati yenye maslahi mapana kwa Taifa. 6.-(1) Wakati wa kushughulikia maombi chini ya Kanuni hizi, Waziri atazingatia vigezo vifuatavyo: (a) endapo mwombaji anastahili kupata msamaha kwa mujibu wa kanuni ya 5; (b) maombi yamewasilishwa kwa mujibu wa utaratibu ulioainishwa katika Kanuni hizi; (c) mwombaji amethibitisha kwa hiyari yake 3 Vigezo vya msamaha Msamaha wa Riba ya Malimbikizo ya Kodi ya Pango la Ardhi TANGAZO LA SEIKALI NA.537B kuwa yuko tayari kulipa kodi ya msingi ndani ya muda utakaoainishwa katika hati ya msamaha; na (d) mwombaji hana shauri lolote mahakamani linalohusiana na madai ya kodi ya pango la ardhi ambayo inaombewa msamaha. (2) Hali ngumu ya kifedha, kufilisika, umaskini au majanga ya asili hayatakuwa kigezo cha kupata msamaha chini ya Kanuni hizi isipokuwa kama mwombaji atathibitisha kwamba- (a) hali hiyo ilijitokeza katika kipindi ambacho kodi ya pango la ardhi ilistahili kulipwa; (b) hali hiyo ni sababu pekee iliyopelekea mwombaji kushindwa kulipa kodi ya pango la ardhi katika tarehe iliyopangwa chini ya Sheria; au (c) hali hiyo ilitolewa taarifa kwa Waziri wakati ambapo kodi ya pango la ardhi ilipaswa kulipwa. 7. Baada ya kupokea maombi ya msamaha, Waziri atawasilisha mapendekezo yake kwa Waziri mwenye dhamana na masuala ya fedha kwa ajili ya uamuzi. 8.-(1) Waziri mwenye dhamana na masuala ya fedha anaweza, baada ya kupokea mapendekezo kutoka kwa Waziri- (a) kutoa msamaha; au (b) kukataa kutoa msamaha. (2) Uamuzi uliotolewa chini ya kanuni hii hautarejewa kiutawala au kukatiwa rufaa. (3) Bila kuathiri masharti ya kanuni hii, mtu yeyote ambaye hataridhika na uamuzi wa Waziri anaweza kutafuta suluhu katika Mahakama Kuu. Mapendekezo Uamuzi Malipo ya kodi 9. Mara baada ya kutolewa kwa msamaha, mwombaji atapaswa kulipa kodi ya msingi ndani ya kipindi cha siku tisini tangu kutolewa kwa msamaha. 4 Msamaha wa Riba ya Malimbikizo ya Kodi ya Pango la Ardhi TANGAZO LA SEIKALI NA.537B SEHEMU YA TATU MASHARTI YA JUMLA Usitishaji wa msamaha 10.-(1) Endapo mwombaji atabainika kutoa taarifa za udanganyifu kwa lengo la kupata msamaha chini ya Kanuni hizi, Waziri atapendekeza kwa Waziri mwenye dhamana na masuala ya fedha kufuta msamaha uliotolewa. (2) Endapo mwombaji amepewa msamaha na ameshindwa kulipa kodi ya msingi katika muda uliotolewa, msamaha uliotolewa utachukuliwa kuwa umesitishwa na atapaswa kulipa kodi ya msingi na riba ya malimbikizo. Msamaha kutolewa mara moja 11. Msamaha wa riba ya malimbikizo ya kodi ya pango la ardhi utatolewa mara moja tu kwa ardhi husika. Makosa 12. Mtu yeyote ambaye, kwa njia ya ulaghai au udanganyifu, amepata msamaha chini ya Kanuni hizi atakuwa atakapotiwa hatiani ametenda kosa na ataadhibiwa kwa mujibu wa masharti ya Sheria. __________ JEDWALI ___________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 4(1)) Fomu ya Ardhi Na. 74 FOMU YA MAOMBI YA MSAMAHA WA RIBA YA MALIMBIKIZO YA KODI YA PANGO LA ARDHI Kwa: KAMISHNA WA ARDHI wa Sanduku la Posta…………………………………… Mimi/Sisi…………………………………………………………………………………… wa………………………………………………………...………………………………… Naomba/tunaomba msamaha wa riba ya malimbikizo ya kodi ya pango la ardhi kuhusu ardhi inayotajwa hapa chini: 5 Msamaha wa Riba ya Malimbikizo ya Kodi ya Pango la Ardhi TANGAZO LA SEIKALI NA.537B NA. TAARIFA ZA KIWANJA/ SHAMBA 1. TAREHE YA MALIPO YA MWISHO KODI YA MSINGI RIBA JUMLA SABABU ZA MAOMBI YA MSAMAHA WA RIBA: …………………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………………………… (Tafadhali ambatisha nyaraka zote muhimu zinazothibitishwa sababu zilizotolewa hapo juu) TAMKO: Ninatamka kwamba taarifa zilizotolewa katika fomu hii na nyaraka yoyote iliyoambatishwa ni sahihi, kamili na imejumuisha maelezo ya kweli ya deni langu la kodi ya pango la ardhi kwa kadiri ya ufahamu wangu; Mimi ……………………………………….. ninatambua kwamba, msamaha wa riba ya malimbikizo ya kodi ya pango la ardhi ambayo haijalipwa utatolewa kwa masharti ya kulipa kodi yote ya msingi ya kiasi cha Tsh. …………………… kabla ya kuisha kwa muda wa msamaha uliotolewa; Tarehe ……………Mwezi ……………. Mwaka ……………….. …………………………………………………………………………………………. Jina na sahihi ya Mwombaji na muhuri ikiwa ni taasisi/kampuni Ziwasilishwe nakala tatu 1. MAPENDEKEZO YA KAMISHNA WA ARDHI Ardhi Mimi……………………………………………………. ninapendekeza kwa kuwa, maombi yaliyowasilishwa yakubaliwe/yasikubaliwe kwa Kamishna wa 6 Msamaha wa Riba ya Malimbikizo ya Kodi ya Pango la Ardhi TANGAZO LA SEIKALI NA.537B sababu yanakidhi/hayakidhi vigezo vilivyoainishwa katika Kanuni za Msamaha wa Riba ya Malimbikizo ya Kodi ya Pango la Ardhi. Saini …………………………………………………………………………………… Tarehe ………………………………………………………………………………… Dodoma, ANGELINA S.L. MABULA 30th August, 2022 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi 7
Section documentVerify source

Legislative relationships

0 referenced instruments

Names are derived from the stored provision headings and citation-enrichment layer. Treat this as a research index and verify each relationship against the source text.

No structured legislative relationships were detected

The statute remains fully searchable by provision. Consult the source text for amendments and cross-references that have not yet been indexed.

Recorded versions and source checkpoint

1 version available in this collection

Current-law checkpoint
  • Undated version · currentSwahili

Source-linked research

Ask AI about this statute

The overview, provisions, and source records above are public. Continue in a separate conversation with this statute’s jurisdiction and source version attached.

About this LexChat collection

Statute information is organised from identified legislative sources for professional research. Corrections can be reported to hello@esheria.ai.