abdallah a almas na wenginao dhidi ya a one products and bottles ltd na mwenzake 2023 tzhcld 1194 14 machi 2023
The court is barred from entertaining an application for extension of time to file a matter already dismissed for being time-barred; the present application seeks to revive what has already been dismissed, and the court is functus officio.
Source-derived case information.
- Citation
- abdallah a almas na wenginao dhidi ya a one products and bottles ltd na mwenzake 2023 tzhcld 1194 14 machi 2023
- Parties
- Applicant: Abdallah A. Almas; Applicant: Odilo Kyahe; Applicant: Said Magoma; Applicant: Zuhura Yusufu; Applicant: Halima Ayuni; Applicant: Salim Yahya; Applicant: Lucy Mwami; Applicant: Mohamed Haji; Applicant: Ilaila Nampokela; Applicant: Mohamed Kaniki; Applicant: Janeth Anthoni; Applicant: Secilia Mogela; Applicant: Primitiva Kahigi; Applicant: Mwanaidi Omary; Applicant: Hadija Salim; Applicant: Asumini Hussein; Applicant: Zuwena Juma; Applicant: Cosmas Lupande; Applicant: Ally Hamisi; Applicant: Ramadhan Forgo; Applicant: Hemed Said; Applicant: Samson Nyabange; Applicant: Iddy Amin; Applicant: Jastine Kaoneka; Applicant: Nasra Abdul; Applicant: Sharifa Yasini; Respondent: A-One Products and Bottles Ltd; Respondent: Peter Fidelis Mnyanyi
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2023
- Procedural Posture
- Labour Miscellaneous Application / Preliminary Objection Ruling
- Outcome
- Preliminary objection upheld; application dismissed.
- Legal Topics
- Res Judicata, Extension of Time, Dismissal Vs Strike Out, Enforcement of Settlement, Jurisdictional Bar
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Abdallah A. Almas
Applicant
Odilo Kyahe
Applicant
Said Magoma
Applicant
Zuhura Yusufu
Applicant
Halima Ayuni
Applicant
Salim Yahya
Applicant
Lucy Mwami
Applicant
Mohamed Haji
Applicant
Ilaila Nampokela
Applicant
Mohamed Kaniki
Applicant
Janeth Anthoni
Applicant
Secilia Mogela
Applicant
Primitiva Kahigi
Applicant
Mwanaidi Omary
Applicant
Hadija Salim
Applicant
Asumini Hussein
Applicant
Zuwena Juma
Applicant
Cosmas Lupande
Applicant
Ally Hamisi
Applicant
Ramadhan Forgo
Applicant
Hemed Said
Applicant
Samson Nyabange
Applicant
Iddy Amin
Applicant
Jastine Kaoneka
Applicant
Nasra Abdul
Applicant
Sharifa Yasini
Applicant
A-One Products and Bottles Ltd
Respondent
Peter Fidelis Mnyanyi
Respondent
Procedural Posture
Labour Miscellaneous Application / Preliminary Objection Ruling
Legal Issues
- 1 Whether the court is barred from entertaining an application for extension of time to file a matter already dismissed for being time-barred
- 2 Whether there is a distinction between the present application and the previously dismissed application No. 56 of 2021
Ratio Decidendi
The court is barred from entertaining an application for extension of time to file a matter already dismissed for being time-barred; the present application seeks to revive what has already been dismissed, and the court is functus officio.
Court Disposition
Preliminary objection upheld; application dismissed.
Orders
- Application dismissed for being res judicata and barred by law.
- No order as to costs; each party to bear its own costs.
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA MAHAKAMA KUU DIVISHENI YA KAZI PAR ES SALAAM MAOMBI ANUAI YA KIKAZI NA. 314 YA 2022 ABDALLAH A. ALMAS......................................... MLETA MAOMBI WA 1 ODILO KYAHE................................................. MLETA MAOMBI WA 2 SAID MAGOMA.................................................... MLETA MAOMBI WA 3 ZUHURA YUSUFU................................................ MLETA MAOMBI WA 4 HALIMA AYUNI.................................................. MLETA MAOMBI WA 5 SALIM YAHYA............................................... MLETA MAOMBI WA 6 LUCY MWAMI.................................................. MLETA MAOMBI WA 7 MOHAMED HAJI.................................................. MLETA MAOMBI WA 8 I LAI LA NAMPOKELA......................................... MLETA MAOMBI WA 9 MOHAMED KANIKI........................................... MLETA MAOMBI WA 10 JANETH ANTHONI............................................. MLETA MAOMBI WA 11 SECILIA MOGELA............................................. MLETA MAOMBI WA 12 PRIMITIVA KAHIGI......................................... MLETA MAOMBI WA 13 MWANAIDI OMARY......................................... MLETA MAOMBI WA 14 HADIJA SALIM.................................................. MLETA MAOMBI WA 15 ASUMINI HUSSEIN........................................... MLETA MAOMBI WA 16 ZUWENA JUMA................................................. MLETA MAOMBI WA 17 COSMAS LUPANDE........................................... MLETA MAOMBI WA 18 ALLY HAMISI.................................................. MLETA MAOMBI WA 19 RAMADHAN FORGO............................................... MLETA MAOMBI WA 20 HEMED SAID.................................................... MLETA MAOMBI WA 21 SAMSON NYABANGE MLETA MAOMBI WA 22 IDDY AMIN .............. MLETA MAOMBI WA 23 JASTINE KAONEKA .. MLETA MAOMBI WA 24 NASRA ABDUL......... MLETA MAOMBI WA 25 SHARIFA YASINI .... MLETA MAOMBI WA 26 1 DHIDI YA A-ONE PRODUCTS AND BOTTLES LTD....................... MJIBU MAOMBI WA 1 PETER FIDELIS MNYANYI..........................................MJIBU MAOMBI WA 2 UAMUZI MDOGO K.T. R Mteule, J 06 Machi, 2023 & 14, Machi 2023 Huu ni uamuzi wa pingamizi la awali kuhusu uwezo wa maombi haya kusimama kisheria kutokana na hoja ya mleta maombi wa kwanza kwamba maombi kama haya yalishasikilizwa na kufanyiwa uamuzi na Mahakama hii. Waleta maombi ni washinda tuzo katika Mgogoro wa Kazi Na. CMA/DSM/ILA/287/12/93. Walifungua maombi ya utekelezaji wa tuzo inayotokana na mgogoro huu wa kikazi. Baada ya ushindi wa waleta maombi katika ngazi mbalimbali za Mahakama kuanzia Tume ya Usuluhishi na Uamuzi, Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani, waleta maombi walifungua shauri la utekelezaji deni tuzo No. 609 la mwaka 2018 katika mahakama hii. Kupitia aliyekuwa mwakilishi wa waleta maombi Bwana Peter Mnyanyi ambaye ni mjibu maombi wa pili, makubaliano yalifanyika kumaliza mgogoro na 2 kutokana na mapatano hayo, Mahakama ilimaliza shauri la ukazaji deni tuzo No.609 la mwaka 2019. Waleta maombi hawakukubaliana na mapatano hayo wakidai kuwa hawakuruhusu mapatano yoyote kufanyika kwa niaba yao. Kwa mujibu wa kiapo cha waleta maombi, walibaini kwamba Mleta maombi wa pili kumbe alikuwa ameshalipwa fedha za mapatano toka tarehe 20.12.2021 na aliamua kukaa kimya bila kuwajulisha lolote kinachoendelea kama kuna mapatano ya kumaliza shauri. Katika kupata tafsiri ya hatma ya haki zao, waleta maombi walifungua maombi Na. 56 ya 2021 katika Mahakama hii wakiomba Mahakama kutengua hati ya makubaliano iliyoingiwa na Mjibu maombi wa pili kwa niaba ya waleta maombi. Mamo tarehe 03.08.2022 maombi hayo yalitupiliwa mbali kwa sababu hayakuzingatia muda. Wakiwa bado na nia ya kupata ufumbuzi wa makubaliano ambayo wanaamini hayakuwa na baraka zao, waleta maombi wanataka kuleta tena maombi ya marejeo dhidi ya makubaliano hayo. Kwa vile muda umepita, wameleta maombi haya ili kuomba kuongezewa muda ili kuleta maombi hayo ya marejeo dhidi ya hati ya makubaliano. 3 Wajibu maombi wameleta viapo kinzani na wote wakaja na mapingamizi ya awali. Pingamizi la awali la mjibu maombi wa pili lilitupwa kutokana na yeye kutokuwepo. Katika pingamizi la Mjibu maombi wa kwanza, anapinga maombi haya kusimama kisharia kwa hoja kwamba maombi kama haya yalishafunguliwa kupitia Maombi No. 56 ya 2021 na kutupiliwa mbali na hivyo mahakama imefungwa mkono. Kutokana na hoja hii, Mleta maombi wa kwanza anaiomba mahamama ione kuwa imefungwa mikono kwa kuwa shauri kama hili limeshaamuliwa. Hoja iliyopo mbele yangu ni kama maombi kama haya yalishatupiliwa mbali na hivyo Mahakama kufungwa mikono kuendelea na maombi yaliyopo sasa. Pingamizi lilisikilizwa kwa njia ya mdomo. Mleta maombi wa kwanza aliwakilishwa na Bi Ndehorio Ndessamburo ambaye aliwasilisha kwamba amri ya kutupilia mbali shauri (dismissal order) inamaliza shauri hilo na kulifanya kufikia hatma. Alirejea kesi ya Yahaya Hamisi versus Hamida Haji Iddi and 2 Others, Civil Appeal No 225 of 2018, CAT. Kwa mujibu wa Ndehorio, Mahakama ya Rufani katika kesi hii imetoa tofauti kati ya kesi kutupiliwa mbali (dismissal) na kesi kufutwa (strike out) ambapo tafsiri ya kesi kutupiliwa mbali madhara yake ni kesi 4 kufikia hitimisho. Alireje pia kesi ya East Africa Development Bank versus Blue Line Enterprises Limited, Civil Appeal No. 161 pf 2009. Alisema kwa tafsiri ya Mahakama ya Rufani, Mahakama inafungwa mikono kusikiliza shauri ambalo imewahi kulitupilia mbali. Akirejea kesi hiyo hiyo ya Blue Line, Ndehorio alieleza kuwa waleta maombi hawawezi kuomba kuongezewa muda kuleta shauri ambalo tayari limeshatupiliwa mbali. Upande wa waleta maombi umewakilishwa na mwakilishi binafsi Bw. Michael Mgombozi ambaye amesema kwamba kuna tofauti kati ya maombi haya na maombi Na. 56 ya 2021 ambayo yalitupiliwa mbali. Kwa maoni yake, maombi Na 56 ya 2021 yaliomba marejeo ya hati ya makubaliano wakati maombi haya yanaomba marejeo ya uamuzi wa msajili. Nimeangalia kilichoombwa katika maombi haya; ipo wazi kwamba waombaji wanaomba kuongezewa muda ili kuleta maombi ya marejeo dhidi ya hati ya makubaliano. Nimeangalia pia katika maombi Na. 56 ya 2021 na kuthibitisha kwamba maombi yale yaliomba Mahakama ifanya marejeo dhidi ya hati ya makubaliano kati ya mjibu maombi wa kwanza na mjibu maombi wa pili. Kesi ya Blue Line ambayo wakili wa mjibu maombi ameirejea imeweka wazi kwamba Mahakama haiwezi kusikiliza 5 maombi ya kurejesha shauri ambalo limetupiliwa mbali kutokana na kupitwa na muda. Kutokana na kesi hiyo, natofautiana na Bw. Mgombozi kwamba kuna tofauti inayoondoa kifungo katika mikono ya Jaji kuruhusu usikilizwaji wa maombi yanayoombewa ongezeko la muda wa kuleta shauri ambalo limeshatupiliwa mbali. Bado mahakama itaendelea kufungwa mikono kwani maombi haya yakiruhusiwa, kitakacholetwa ni kile kilichokwisha kutupiliwa mbali. Kwa kuongozwa na uamuzi wa Mahakama ya Rufani wa kasi ya Blue Line, nakubaliana na wakili wa mjibu maombi wa kwanza kwamba Maombi haya yapo kinyume na sheria kwa kuomba jambo ambalo limeshatupiliwa mbali. Kutokana na sababu hizi, pingamizi la Awali linakubaliwa na Maombi haya yanatupiliwa mbali. Mjibu maombi wa kwanza ameomba gharama. Nakubaliana na Bw. Mgombozi kwamba kwa kuwa ni shauri la kazi, hakuna gharama. Kila upande utashughulika na gharama zake. KATARINA REVOCATI MTEULE JAJI 14/3/2023 Vi ^// 6