alliance one tobacco tanzania ltd vs halfan abdallah 2021 tzhcld 140 2 juni 2021
The court held that requiring vehicle registration cards as security was inappropriate due to potential disruption and depreciation of the vehicles. A bank guarantee is a suitable alternative, balancing the interests of both parties.
Source-derived case information.
- Citation
- alliance one tobacco tanzania ltd vs halfan abdallah 2021 tzhcld 140 2 juni 2021
- Parties
- Applicant: Alliance One Tobacco Tanzania Ltd; Respondent: Halfan Abdallah
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2021
- Procedural Posture
- Review Application / Final Judgment
- Outcome
- Registrar's order set aside; applicant to provide bank guarantee as security.
- Legal Topics
- Stay of Execution, Security for Judgment, Execution of Arbitral Award
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Alliance One Tobacco Tanzania Ltd
Applicant
Halfan Abdallah
Respondent
Procedural Posture
Review Application / Final Judgment
Legal Issues
- 1 Whether the Registrar's order requiring the applicant to deposit vehicle registration cards as security for stay of execution was lawful and appropriate
Ratio Decidendi
The court held that requiring vehicle registration cards as security was inappropriate due to potential disruption and depreciation of the vehicles. A bank guarantee is a suitable alternative, balancing the interests of both parties.
Court Disposition
Registrar's order set aside; applicant to provide bank guarantee as security.
Orders
- Applicant to deposit a bank guarantee of TZS 20,979,125 within 21 days from the date of judgment.
- Each party to bear its own costs.
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
KATIKA MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DIVISHENI YA KAZI ILIYOKETI MOROGORO MAREJEO NA. 19 YA 2020 KATI YA ALLIANCE ONE TOBACCO TANZANIA LTD..................... MLETA MAOMBI NA HALFAN ABDALLAH......................................................... MJIBU MAOMBI HUKUMU Tarehe ya Amri Ya Mwisho: 19/05/2021 Tarehe ya Hukumu: 02/06/2021 A.E MWIPOPO, J. Shauri hili la marejeo limefunguliwa dhidi ya Amri ya Naibu Msajili, Mhe. Mtarania, katika Shauri la Utekelezaji Hukumu Na. 6 la 2020. Alliance One Tobacco Tanzania Limited ambaye ni mleta maombi anaomba Mahakama ifanye marejeo na kuiweka pembeni (set aside) Amri hiyo ya Mahakama iliyotolewa tarehe 03 Machi, 2020. Shauri hili limeungwa mkono na kiapo cha Sabatho Musombwa ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa Mleta Maombi. Katika aya ya 9 ya kiapo Mleta Maombi ametaja hoja ya kisheria (legal issue) inayotokana na maelezo ya shauri. Hoja hiyo ni kuwa Amri ya Mhe. i Naibu Msajili katika Maombi ya Utekelezaji Na. 6 ya 2020 haikuwa sahihi na ilipatikana isivyo halali. Historia fupi ya shauri hili ni kwamba Mjibu Maombi aitwaye Halfan Abdallah alifungua mgogoro Tume ya Usuluhishi na Uamuzi kupinga kuachishwa kazi na Mleta Maombi. Tume ilitoa uamuzi kuwa aliachishwa kazi isivyo halali na alipwe jumla ya shilingi 20,979,125/=. Mjibu Maombi alifungua Shauri la Utekelezaji (Execution Application) Na. 6 la 2020 kwa ajili ya kukazia tuzo ya Tume akiomba kukamata na kuuza magari mawili yenye namba za usajili T 210 CJA aina ya Toyota Land Cruiser na T 589 BXP aina ya Tata. Baada ya kuwasikiliza pande zote, mnamo tarehe 03 Machi, 2020 Naibu Msajili alitoa amri ya kusitisha utekezaji (stay of execution) kwa sharti kuwa kadi za magari hayo ya Mleta Maombi ziwasilishwe Mahakamani kama dhamana wakati wanasubiria shauri la marejeo namba 59 la 2019 lililofunguliwa na Mleta Maombi lisikilizwe na Mahakama hii. Mleta Maombi hakuridhika na uamuzi huo ndipo amefungua shauri hili la marejeo. Akiwasilisha hoja za kuunga mkono maombi haya, wakili wa Mleta Maombi aitwaye Boniface Uiso alieleza kuwa Katika shauri la utekezaji Na. 6 la 2020 Mhe. Msajili alitoa amri ya kusitisha utekelezaji wa tuzo ya Tume (stay of execution) kwa masharti 2 kwamba Mleta Maombi aweke kadi halisi ya gari Na. T 210 CJA aina ya Toyota Land Cruiser na T 589 BXP aina ya Tata. Ni msimamo wa kisheria kuwa dhamana ya utekelezaji wa hukumu isiwe adhabu au isababishe usumbufu kwa mtoa dhamana. Msimamo huo umetolewa katika kesi ya Africhick Hatchers Ltd dhidi ya CRDB Bank PLC, Maombi ya Madai Na. 98 ya 2016, Mahakama ya Rufani ya Tanzania, iliyoketi Dar es Salaam. Msajili alitoa amri hiyo ili kuzuia kuuzwa au kubadili umiliki wa magari hayo wakati ikisubiriwa shauri la marejeo baina ya wadaawa ambalo lipo mbele ya Mahakama hii liweze kusikilizwa na kutolewa uamuzi. Mhe. Msajili hakuwa sahihi kwa kuwa Mleta Maombi anaendelea na shughuli zake vizuri hapa Tanzania na Mkoani Morogoro na hakuna kiashiria chochote cha kuonesha kuwa atafunga au kuhairisha biashara zake. Mleta Maombi anao uwezo wa kulipa deni tuzo kupitia biashara zake iwapo shauri la marejeo mbele ya Mahakama hii halitakubaliwa. Wakili ameeleza kuwa amri ya kuweka kadi za magari kama dhamana litamsababisha hasara kwa kuwa magari hayo yanaendelea kutumika kila siku na hivyo kadi hizo zinahitajika. Kuwepo kwa kadi hizo Mahakamani kunaweza kuleta usumbufu pale kadi halisi itakapohitajika na Mamlaka nyingine. Alieleza kuwa Mleta Maombi anazo mali nyingine na anaweza kulipa deni husika pale 3 itakapohitajika kulipa. Wakili aliomba amri ya Mahakama ya kuweka kadi halisi ya gari husika kama dhamana iwekwe pembeni na kama Mahakama itaona kuna haja ya kuweka dhamana basi anaomba waruhusiwe kuweka dhamana ya benki (Bank Guarantee) ya kuweza kulipa kiasi chote cha deni tuzo ili pale shauri la marejeo litakapokataliwa Mjibu Maombi aweze kulipwa deni hilo. Akijibu mawasilisho ya Mleta Maombi, Bw. Emmanuel Zongwe ambaye ni Mwakilishi Binafsi wa Mjibu Maombi alieleza kuwa Mjibu Maombi alifungua Maombi ya kukazia hukumu Na. 6 ya 2020 akikazia tuzo ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi katika Shauri Na. CMA/MORO/149/2018 ambapo Tume iliamuru alipwe kiasi cha shilingi 20,979,125/= mnamo tarehe 04 Disemba, 2019. Mjibu Maombi aliomba katika shauri la utekelezaji wa tuzo ya Tume lenye Na. 6 la 2020 kukamatwa kwa magari yenye namba za usajili T 210 CJA aina ya Toyota Land Cruiser na T 589 BXP aina ya Tata ili yauzwe kwa ajili ya kulipa deni husika. Licha ya kwamba Mleta Maombi hakupeleka Maombi ya kuzuia utekelezaji wa hukumu, Mhe. Msajili alitoa amri ya kusitishwa ukamataji na uuzaji wa magari hayo na kuweka sharti la Mleta Maombi kuweka kadi halisi za magari hayo kama dhamana. Mhe. Msajili alikuwa sahihi kutoa masharti hayo baada ya kuzuia utekelezwaji wa tuzo. 4 Aliendelea kueleza kuwa masharti yaliyotolewa na Msajili sio adhabu hasa ukizingatia Mleta Maombi hakuwa amewasilisha maombi ya kuzuia utekelezaji wa tuzo ya Tume. Kampuni ya Mleta Maombi kuwa Nchi nzima na kuendelea na shughuli zake vizuri hakumuondolea wajibu wake wa kuweka dhamana pale kunapokuwa na shauri la ukaziaji wa hukumu. Kwa sababu hiyo aliomba Mahakama isikubaliane na Mjibu Maombi kutengua uamuzi wa Msajili kwa kuwa shauri la utekelezaji Na. 6 la 2020 litakuwa limesitishwa bila kuwa salama kwa kuwa dhamana haijawekwa. Aliomba kama kuna haja ya kuweka dhamana nyingine Mahakama itoe amri kuwa Mleta Maombi atoe fedha taslimu na kuweka katika akaunti ya Mahakama kama dhamana. Kuweka fedha taslimu hakutaleta usumbufu kwa upande wowote. Mleta Maombi katika mawasilisho yake ya nyongeza alirudia maelezo ya mawasilisho yake ya msingi. Kutokana na mawasilisho ya wadaawa, nimeona hoja ya kisheria inayotakiwa itolewe uamuzi na Mahakama ni iwapo amri ya Mahakama kuwa Mleta Maombi aweke dhamana kama sharti la kusitisha utekelezaji wa tuzo ilikuwa sahihi. Rekodi iliyopo inaonesha kuwa Naibu Msajili alisimamisha utekelezaji wa tuzo ya Tume katika shauri la utekelezaji (execution 5 application) Na. 6 la 2020 kwa masharti kwamba Mleta Maombi awasilishe kama dhamana kadi halisi za magari mawili, gari lenye namba za usajili T 210 CJA aina ya Toyota Land Cruiser na T 589 BXP aina ya Tata ambayo Mjibu Maombi alikuwa ameomba yakamatwe na kuuzwa ili kulipa deni tuzo. Naibu Msajiri alifikia uamuzi huo baada ya kuona kuwa kitendo cha Mleta Maombi kufungua shauri la marejeo Na. 59 la 2019 Mahakamani hakufanyi shauri la utekelezaji wa tuzo ya Tume lisimame lenyewe, bali Mleta Maombi alitakiwa afungue shauri la kusimamisha utekelezaji wa tuzo. Hivyo ili kulinda haki za pande zote hadi pale shauri la marejeo litakaposikilizwa aliamua kuwa Mleta Maombi aweke kadi hizo za magari kama dhamana. Mleta Maombi ana maoni kuwa dhamana ya utekelezaji wa tuzo hiyo ya Tume itasababisha usumbufu kwake kwa sababu magari hayo yanatumika kila siku na kadi hizo zinaweza kuhitajika na mamlaka nyingine. Wakili wa Mleta Maombi alieleza kuwa Mleta Maombi ni taasisi ya kimataifa inayoendesha biashara zake mkoani Morogoro na nje ya nchi hivyo inaaminika na ina mali nyingine nyingi zinazoweza kutumika kama dhamana. Kwa upande mwingine, Mjibu Maombi aliona kuwa ili haki ya Mjibu Maombi iweze kulindwa ni vizuri kukawa na dhamana na kama Mahakama itaona kuna haja ya kubadili dhamana basi Mleta Maombi aweke fedha taslimu. 6 Nakubaliana na maoni ya Mjibu Maombi kwamba kuna haja ya kulinda haki yake pale ambapo atashinda shauri lililopo Mahakama Kuu ili aweze kufurahia matunda yake. Hivyo ni muhimu wakati tunaangalia haki za Mleta Maombi, basi haki ya Mjibu Maombi pia iangaliwe. Mleta Maombi alieleza kuwa taasisi yake inaaminika na ina mali nyingi. Lakini ukiachia maelezo yaliyopo katika kiapo, hakuna kielelezo chochote kilichowasilishwa na Mleta Maombi kuonesha kuwa anafanya shughuli zake vizuri na anamiliki mali nyingine ambazo zinaweza kutumika kama dhamana. Ni maoni yangu kuwa kwa gari ambalo linatumika kila siku kutokuwa na kadi halisi ya gari kunaweza kusababisha usumbufu kwa anayeweka dhamana kwa kuwa kadi hiyo inaweza kuhitajika na Mamlaka nyingine. Na kama ilivyoelezwa katika kesi iliyonukuliwa na Mleta Maombi ya Africhick Hatchers Ltd dhidi ya CRDB Bank PLC, (supra), ni msimamo wa kisheria kuwa dhamana inayowekwa wakati wa utekelezaji wa hukumu inatakiwa isiwe adhabu au isisababishe usumbufu kwa mtoa dhamana. Na kwa kuwa magari hayo yanaendelea kutumika kila siku, kuna uwezekana kuwa mpaka wakati mashauri baina ya Mleta Maombi na Mjibu Maombi yanafikia mwisho magari hayo yanaweza kuwa hayana thamani ya kulipa deni tuzo husika kwa sababu ya kuchakaa, kuharibika au ajali. 7 Katika kesi ya Mantrac Tanzania Limited dhidi ya Raymond Costa, Maombi ya Madai Na. 11 ya 2010, Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Mahakama iliona kuwa mojawapo ya sharti la kusimamisha utekelezaji wa hukumu ni kuweka dhamana kwa ajili ya utekelezaji wa uamuzi wa kusimamisha utekelezaji wa amri/ tuzo ambapo Mahakama itaweka muda wa kuweka dhamana husika. Kama ilivyokuwa amri ya Naibu Msajili kuwa lazima kuwa na dhamana wakati wa usimamishaji wa utekelezaji wa hukumu, Mleta Maombi inabidi aweke dhamana nyingine badala ya kadi ya gari husika. Hivyo, kama kuna dhamana nyingine ambayo Mleta Maombi anaiweka badala ya kadi husika ya gari ni maoni yangu kuwa kwa ajili ya kutenda haki dhamana hiyo inaweza kuwekwa. Nia hasa ni kuona kuwa Mleta Maombi hapati usumbufu na Mjibu Maombi anapata haki yake ya kulipwa mara tu shauri la marejeo litakapoisha. Mleta Maombi aliomba aweke dhamana ya benki (bank guarantee) kama dhamana na Mjibu Maombi aliomba iwekwe fedha taslima kwa kiasi cha tuzo ya Tume. Dhamana ya Benki ni dhamana nzuri kwa kuwa benki inathibitisha kuwa ipo tayari kutoa malipo kwa muhusika pale ambapo itatakiwa kufanya hivyo. Hivyo, aliomba atumie dhamana ya benki badala ya kadi ya gari na ombi lake nakubaliana nalo. Hivyo, nafuta amri ya Naibu Msajili aliyoitoa tarehe 8 03 Machi, 2020 kuwa Mleta Maombi aweke kadi halisi ya gari lenye namba za usajili T 210 CJA aina ya Toyota Land Cruiser na T 589 BXP aina ya Tata na badala yake Mleta Maombi awasilishe Mahakamani dhamana ya benki ya kiasi cha shilingi 20,979,125/= ndani ya siku 21 toka tarehe ya uamuzi huu. Kila upande utalipa gharama zake za kuendesha shauri hili. Hii ndio amri ya Mahakama. A. E. MWIP JAJI 02/06/2021 9