aneth farady waya na wenzake 2 vs insurance group of tanzania 2022 tzhcld 996 12 oktoba 2022
Applicants were employed under fixed-term contracts which expired by effluxion of time; respondent followed legal procedures for non-renewal, provided required notice and terminal benefits; termination was lawful and applicants' claims lack merit.
Source-derived case information.
- Citation
- aneth farady waya na wenzake 2 vs insurance group of tanzania 2022 tzhcld 996 12 oktoba 2022
- Parties
- Applicant: Aneth Farady Waya; Applicant: Sarah Ramadhani Chalamila; Applicant: Neema Raphael Bisaya; Respondent: Insurance Group of Tanzania
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2022
- Procedural Posture
- Labour Revision / Final Judgment
- Outcome
- application dismissed
- Legal Topics
- Termination of Employment, Fixed Term Contracts, Procedural Fairness, Contractual Interpretation
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Aneth Farady Waya
Applicant
Sarah Ramadhani Chalamila
Applicant
Neema Raphael Bisaya
Applicant
Insurance Group of Tanzania
Respondent
Procedural Posture
Labour Revision / Final Judgment
Legal Issues
- 1 Whether applicants were employed under permanent or fixed-term contracts
- 2 Whether termination of applicants' employment was lawful
- 3 Whether respondent followed proper procedures in terminating employment
Ratio Decidendi
Applicants were employed under fixed-term contracts which expired by effluxion of time; respondent followed legal procedures for non-renewal, provided required notice and terminal benefits; termination was lawful and applicants' claims lack merit.
Court Disposition
application dismissed
Orders
- Application dismissed for lack of merit
- Respondent to provide certificate of service to applicants as required by law
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
KATIKA MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DIVISHENI YA KAZI PAR ES SALAAM MAREJEO NA. 147 YA MWAKA 2022 (Inatokana na Tuzo ya mgogoro namba CMA/DSM/ILA/206/21 mbele ya Mhe. Kiangi, Muamuzi) KATI YA ANETH FARADY WAYA................................. MLETA MAOMBI 1 SARAH RAMADHANI CHALAMILA........................ MLETA MAOMBI 2 NEEMA RAPHAEL BISAYA........................ MLETA MAOMBI 3 DHIDI YA INSURANCE GROUP OF TANZANIA................................... MJIBU MAOMBI HUKUMU S.M. MAGHIMBI, J; Katika shauri hili waleta maombi wanapinga maamuzi ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ('Tume') yaliyotolewa tarehe 13/02/2021 na Mh. Kiangi. N, Muamuzi katika mgogoro wa kazi Na. CMA/DSM/ILA/206/21. Waleta maombi walikuwa waajiriwa wa mjibu maombi walioajiriwa kwa nafasi mbalimbali na siku tofauti. Mnamo tarehe 01/03/2021 ajira za waleta maombi zilisitishwa hivyo baada ya kutoridhishwa na maamuzi hayo ya mjibu maombi waliwasilisha mgogoro wao dhidi ya mjibu maombi mbele ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ("Tume") wakipinga uachishwaji kazi usio halali. Walieleza kuwa mjibu maombi hakuwa na sababu za msingi za kuwaachisha kazi na kwamba hakufuata taratibu zilizowekwa kisheria. Tume baada ya kupitia Ushahidi wa pande zote mbili ilifikia maamuzi kuwa uachishwaji kazi wa waleta maombi ulikuwa i halali hivyo maombi mbele ya Tume yakatupiliwa mbali. Baada ya kutoridhika na maamuzi hayo ya Tume waleta maomba wakafungua tena shauri mbele ya mahakama hii wakiomba amri zifuatazo:- i. Kwamba iipendeze mahakama kurejea na kutengua uamuzi nambari CMA/DSM/ILA/206/21 ambao ulitolewa tarehe 13/12/2021 mbele ya Mheshimiwa Kiangi, Muamuzi ii. Kwamba mahakama itowe amri nyingine yoyote ambayo itaona inafaa. Pamoja na maombi haya waleta maombi waliiiomba mahakama itengue maamuzi hayo tajwa kutokana na hoja zifuatazo:- i. Kwamba muamuzi alikosea kwa hoja na sheria kwa kushindwa kuoanisha Ushahidi uliotolewa na pande zote husika. ii. Kwamba muamuzi alikosea kwa hoja ya sheria kwa kushindwa kuchambua na kutathmini Ushahidi uliotolewa. iii. Kwamba muamuzi alikosea kwa hoja na sheria kwa kuingiza na kuongelea hoja mpya ambazo hazikujadiliwa mbele ya Tume. iv. Kwamba muamuzi alijielekeza vibaya kwa kwenda kinyume na sheria ya kazi na kuamua kuwa mikataba ilikuwa ya muda mfupi na sio ya kudumu. 2 v. Kwamba muamuzi alikosea kwa hoja na sheria kwa kujielekeza kwenye dhana kwamba saini zilizokuwa katika mikataba ya muda mfupi ni ya waleta maombi. vi. Kwamba muamuzi alikosea kwa hoja na sheria kwa kukataa Ushahidi wa muhimu wa waleta maombi. Katika hoja ya kwanza wakili Garran aliiambia mahakama kuwa muamuzi alijielekeza vibaya kwa kutokuoanisha ushahidi wa pande zote mbili ila yeye aliamua kwa kutumia busara yake yeye mwenyewe suala ambalo waleta maombi hawakutendewa haki. Alieleza kuwa uamuzi wa Tume hauelezi Ushahidi ulivyokuwa umewasilishwa katika majumuisho ya mwisho ya waleta maombi ambao ulikuwa ni Ushahidi toshelevu wa Ushahidi wa kuachishwa kazi waleta maombi pasipo kufuata utaratibu. Katika hoja ya pili wakili Garran alieleza kuwa muamuzi hakuchambua na kufafanua sawasawa na kubainisha nini maana ya mkataba wa muda mfupi na mkataba wa kudumu. Alieleza kuwa waleta maombi walitoa mkataba wa kudumu (kielelezo Pl na P2) na mjibu maombi alitoa mkataba wa muda maalumu wa miaka miwili (kielelezo DI na D2) ambapo ilikuwa ni jukumu la muamuzi kufafanua kipengele cha 11 cha mikataba hiyo kinachoeleza wazi kuwa umri wa kustaafu ni miaka 55. Kuyapa nguvu mawasilisho yake wakili alirejea maamuzi mbalimbali ya 3 kesi za jinai ambazo zitazingatiwa katika maamuzi haya. Kesi hizo ni Pamoja na kesi ya Mohamedi Manila Vs. Republic (1995) TLR 3. Iliendelea kuelezwa kuwa muamuzi katika aya ya nne ukurasa wa pili anakiri kuwa waleta maombi walikuwa na mikataba ya kudumu lakini hailezi vyema kuwa ule mkataba wa kudumu uliishaje mpaka kuingia mkataba wa kudumu. Katika hoja ya tatu wakili Garran alieleza kuwa muamuzi alishindwa kutenda haki kwa kuingiza mambo ambayo hayakujadiliwa mbele ya Tume na kufanya kuwa sababu ya kuachishwa kazi waleta maombi. Alieleza kuwa mbele ya Tume hapakuwa na hoja ya kinidhamu ambayo iliongelewa lakini jambo hilo lilijadiliwa katika maamuzi. Kuhusu hoja ya nne wakili alieleza kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 15(4) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini ni takwa la kisheria kama kuna mabadiliko yoyote katika mikataba ya kazi kati ya mwajiri na mwajiriwa basi mabadiliko hayo yafanyike kimaandishi. Alisisitiza kuwa muamuzi alipaswa kuonesha kisheria mkataba wa awali ambao ni wa kudumu uliisha kwa namna gani. Iliongezwa kuwa mwajiri alipaswa kuthibitisha ni haki ipi iliifuata katika kusitisha mkataba wa muda maalumu wa waleta maombi kama ambavyo imeaninishwa katika vifungu vya 8(2)(c) 4 na 9(5) vya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini (Kanuni za Utendaji Bora) TS Na. 42 la mwaka 2007. Katika hoja ya tano wakili Garran alieleza kuwa muamuzi hakufanya uhakiki wa kutosha kujiridhisha saini zilizopo katika mikataba ya muda maalumu ni za waleta maombi kama ambavyo ni matakwa ya sheria katika kifungu cha 75(1)(2) vya Sheria ya Ushahidi No. 6 ya mwaka 2019. Katika hoja ya mwisho ilielezwa kuwa waleta maombi waliwasilisha Ushahidi wao mbele ya Tume lakini chakushangaza muamuzi alikataa Ushahidi huo bila kutoa sababu zozote za msingi. Alieleza kuwa kwa kufanya hivyo muamuzi aliwanyima waleta maombi haki yao ya msingi ya kikatiba ya kusikilizwa kama ambavyo imeelezwa katika Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Aliongeza kuwa katiba hiyo katika ibara ya 107A(2)(e) imezuia mahakama kujikita katika makosa ya kiufundi. Wakili Garran aliendelea kueleza kuwa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini kifungu cha 88(4)(b) kinaelekeza kuwa Tume inatakiwa kushughulikia undani wa mgogoro bila kujali sana taratibu za kisheria. Mwisho kabisa aliiomba mahakama ione kuwa hoja za waleta maombi ni za msingi na kuomba kupitisha maombi yaliyo katika wito wa faragha na kwenye kiapo. 5 Akijibu hoja ya kwanza Wakili Mwanri alieleza kuwa haifai kuwa sababu ya marejeo kwakuwa maamuzi ya Tume hayakatiwi rufaa. Alieleza kuwa muamuzi alichambua kwa usahihi Ushahidi uliotolewa na pande zote mbili. Alieleza kuwa mkataba wa waleta maombi uliisha baada ya kufikia ukomo kama ambavyo imeelezwa katika mkataba wa ajira (klielelezo DI). Aliongeza kuwa waleta maombi walipewa taarifa ya kutohuishwa kwa mikataba yao (kielelezo D2) kwamujibu wa Kifungu cha 4(2) cha Kanuni za utendaji bora. Kuyapa nguvu pia mawasilisho yake wakili alirejea kesi ya Serenity on the Lake Ltd vs Dorcas Martin Nyanda (Civil Appeal 33 of 2018) [2019] TZCA 64 (11 April 2019). Katika hoja ya pili wakili Mwanri alieleza kuwa uchambuzi wa Ushahidi katika kesi za jinai ni tofauti na kesi za madai hivyo kesi alizorejea wakili wa waleta maombi hazina mantiki katika kesi hii. Alieleza kuwa katika kesi hii muamuzi alichambua kwa usahihi Ushahidi ulioletwa na pande zote mbili na wala hakukuwa na mgongano wa Ushahidi wa mjibu maombi. Kuhusu hoja ya tatu ilielezwa kuwa akijibu hoja kinzani PW1 alieleza kuwa waleta maombi hawakuwa na nidhamu ndio maana mikataba yao ikasitishwa hivyo si kweli kuwa hoja hiyo iliibuliwa na muamuzi katika maamuzi yake. 6 Kuhusu hoja ya nne wakili Mwanri alieleza kuwa haiwezekani mfanyakazi akawa na mikataba ya aina mbili kwa wakati mmoja. Kwamba waleta maombi waliposaini tu mkataba wa muda maalumu. Alieleza kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 15(4) hakuna utaratibu maalumu wa namna ya kubadilisha vipengele katika mkataba hivyo kitendo cha waleta maombi kusaini mikataba mipya kinaonesha waliridhia mikataba hiyo. Akijibu hoja namba tano wakili Mwanri alieleza kuwa muamuzi alijiridhisha Saini ni za waleta maombi kwa kuangalia mikataba yao ya ajira (kielelezo DI kwa pamoja). Kwamba waleta maombi hawakutoa uthibitisho wowote mbele ya Tume kuwa Saini katika mikataba hiyo sio za kwao. Alisisitiza kuwa Saini hizo ni za waleta maombi hata kwa kuoanisha na Saini zilizopo katika CMA Fomu namba 1 pamoja na kwenye taarifa yao ya uwakilishi. Aliongeza kuwa japo waleta maombi wanalalamika kuwa Saini zao zimeghushiwa lakini hawajatoa taarifa yoyote juu ya hilo katika kituo cha polisi au sehemu nyingine yoyote kwaajili ya uchunguzi. Kuhusu hoja ya mwisho wakili Mwanri alieleza kuwa waleta maombi hawajaeleza ni Ushahidi gani uliokataliwa na muamuzi. Alieleza kuwa vielelezo vyote vya waleta maombi vilipokelewa isipokuwa 7 kielelezo ambacho hakikufuata utaratibu. Kutokana na mawasilisho yake wakili Mwanri aliomba mahakama itupilie mbali maombi haya kwa kukosa mashiko. Katika mawasilisho ya nyiongeza wakili Garran alirudia yaleyale aliyoeleza awali. Baada ya kupitia Ushahidi wa pande zote mbili, kumbukumbu za mahakama na sheria mbalimbali naona mahakama inatakiwa kutatua hoja zifuatazo; endapo waleta maombi walikuwa na mkataba wenye masharti ya kudumu, endapo mjibu maombi alikuwa na sababu za msingi za kuwaachisha kazi waleta maombi, endapo mjibu maombi alifuata taratibu za kuwaachisha kazi waleta maombi na nini stahiki za pande zote mbili. Katika hoja ya kwanza waleta maombi wameeleza kuwa walikuwa na mkataba wa masharti ya kudumu na wala si wa muda maalumu kama ambavyo imeamuriwa na Tume. Mbele ya Tume waleta maombi waliwasilisha mikataba yao ambayo imeeleza wazi kuwa mikataba hiyo ilikuwa ya kudumu (kielelezo Pl na P2). Mkataba wa Aneth Farady Waya (mleta maombi wa kwanza) unaonesha kuwa ulisainiwa tarehe 21/09/2011 na ulieleza kuwa utasitishwa pale ambapo mleta maombi huyo atafikisha miaka 55. Vivyo hivyo mkataba wa Sarah Chalamila 8 (mleta maombi wa pili) unaonesha kuwa ulisainiwa tarehe 28/01/2013 na kipengele cha 11 kimeeleza bayana kuwa mkataba huo utakoma pale ambapo mleta maombi huyo atafikisha umri wa miaka 55. Kwa upande wa mjibu maombi yeye aliwasilisha mikataba ya muda maalumu (kielelezo DI kwa Pamoja) iliyosainiwa tarehe 22/01/2019 na kukubalika kuanza mnamo tarehe 01/03/2019. Kipengele cha 17.1 cha mikataba hiyo kimeeleza bayana kuwa mikataba hiyo ni ya muda wa miaka miwili. Pande zote mbili yaani waleta maombi na wajibu maombi wanaonesha kuwa wametia saini katika mikataba hiyo. Waleta maombi wanaiambia mahakama kuwa Tume haikujiridhisha kuwa Saini zilizopo katika mikataba hiyo kama ni za waleta maombi. Kiutaratibu vielelezo vyote vinavyotarajiwa kutumiwa na wadaawa mbele ya Tume ni lazima viwasilishwe kabla ya shauri hilo kuanza kiusikilizwa. Kumbukumbu za Tume zinaonesha kuwa vielelezo vya mjibu maombi ikiwa ni pamoja na mikataba tajwa viliwasilishwa Tume tarehe 11/06/2021. Lakini pia kumbukumbu mbele ya Tume zinaonesha kuwa Ushahidi wa mjibu maombi ulisikilizwa mnamo tarehe 29/09/2021. Hivyo basi waleta maombi walikuwa na muda wa kupitia vielelezo vya mjibu maombi kabla ya shauri kusikilizwa na kutambua kuwa Saini zilizopo katika mikataba ya mjibu maombi sio za kwao. Lakini hata hivyo 9 kumbukumbu zinaonesha kuwa siku ya kusikilizwa kwa shauri hilo wakili wa waleta maombi alipinga mikataba ya muda maalumu isipokelewe kwa sababu moja tu ya kuwa mikataba hiyo ni yam waka 2019 na wao waleta maombi wanamikataba ya kudumu. Pingamizi la kuwa Saini zilizopo katika mikataba ya muda maalumu si za waleta maombi liliibuliwa tu wakati wa kutoa Ushahidi wao. Mahakama inaona jambo hilo si la kweli na liliibuliwa tu kupotosha Tume. Kama nilivyoeleza hapo awali kama kweli Saini si za kwao walikuwa na muda mrefu wa kuwasilisha pingamizi hilo lakini hawakufanya hivyo. Hivyo basi mahakama hii inaitambua mikataba yote miwili iliyotolewa mbele ya Tume ya kwamba hapo awali wadaawa waliiingia katika makubaliano ya mkataba wa kudumu kama ambavyo inaonesha katika kielelezo DI na D2. Lakini ilipofika tarehe 22/02/2019 waliingia tena katika mkataba wenye masharti ya muda maalumu wa miaka miwili. Mahakama imezingatia mawasilisho ya waleta maombi kuwa hakukuwa na majadiliano kabla ya kusaini mkataba wenye masharti ya muda maalumu. Ni mtazamo wa mahakama kuwa kitendo cha waleta maombi kusaini mikataba hiyo kinathibitisha kulikuwa na mawasiliano na makubaliano ya pande zote bili hivyo matakwa ya kifungu cha 15(4) cha 10 Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini yalitimizwa. Hakuna namna ya jinsi ya kuvunja aina moja ya mkataba na Kwenda nyingine. Pale tu wadaawa wanapoamua kuingia mkataba mpya basi mkataba walioingia zamani unaisha tokea siku wamesaini mkataba mpya. Katika shauri hili mkataba wa kudumu ulikoma kuanzia tarehe 01/03/2019 pale ambapo wadaawa walikubaliana kuingia katika mkataba mwingine wa masharti ya kudumu. Kwa kuzingatia Ushahidi uliotolewa na pande zote mbili mahakama inaungana mkono na maamuzi ya Tume kuwa wakati wa kuachishwa kazi waleta maombi walikuwa katika mkataba wa muda maalumu na si wa kudumu kama wanavyodai. Hoja ya pili na ya tatu zitajadiliwa kwa pamoja, waleta maombi wanadai kuwa waliachishwa kazi isivyo halali. Kwamba wao walitegemea kufanya kazi mpaka pale watakapofikisha miaka 55 kama ambavyo imeelezwa katika kifungu cha 13.1 cha mikataba yao. Kifungu hicho kinanukuliwa ifuatavyo:- "Retirement age is 55 (fifty five years) at which the employee's contract will automatically terminate, unless otherwise decided by the employer." Kwa tafsiri isiyo rasmi ya kifungu hicho ni kwamba muda wa kustaafu ni miaka 55 na mkataba wa mwajiriwa utakuwa umeisha labda ii tu pale itakapoamuriwa vinginevyo na mwajiri. Ni mtazamo wangu kuwa kifungu nukuliwa hapo juu kinaelezea muda wa kustaafu wa mwajiriwa ambao hauna mgongano wowote na muda wa mkataba utakaokubaliwa na pande zote mbili. Kifungu husika kinaeleza muda ambao pande zote mbili wamekubaliana kutoingia katika mkataba wa aina yoyote labda tu itakapoamuriwa vinginevyo, Kama ilivyoelezwa katika hoja ya kwanza mikataba ya waleta maombi ilieleza wazi kuwa ni ya muda wa miaka miwili (kipengele cha 17.1 cha kielelezo DI kwa pamoja) hivyo kifungu nukuliwa hapo juu kiliwekwa kizingatiwe hata katika kuhuisha mkataba husika. Mkataba wa waleta maombi haukuweka kifungu cha lazima kwa mjibu maombi kuhuisha mkataba huo pale utakapokwisha. Kumbukumbu zinaonesha kuwa mnamo tarehe 01/02/2021 mjibu maombi aliandika taarifa iliyopokelewa na waleta maombi wa kwanza na wa pili mnamo tarehe 15/02/2021 (kielelezo D2) ikieleza kuwa mikataba yao itakapokwisha mnamo tarehe 01/03/2021 haitahuishwa tena. Vilevile kwa mleta maombi wa kwanza taarifa yake ya kutohuishwa kwa mkataba iliandikwa tarehe 26/02/2021 ikieleza wazi kama walivyoelezwa waleta maombi wengine. Ni matakwa ya sheria kuwa pale ambapo muda wa makubaliano huisha katika mkataba wa muda maalumu basi mkataba huo utakuwa umekwisha moja kwa moja haya yameelezwa katika kifungu cha 4(2) cha Kanuni za Utendaji Bora. Hii imeelezwa pia 12 katika kesi ya Tunakopesha Ltd Vs. Moses Mwasiposya, Labour Revision No. 17 of 2011 (haijataarifiwa) ambapo mahakama ilieleza yafuatayo:- "... if the contract had indeed been for a fixed specific period, there would have been no need for notice of termination." Hivyo basi kutokana na maelezo hapo juu pamoja na kesi iliyonukuliwa ni wazi kuwa katika mkataba wa muda maalumu pande zote mbili zinatambua mwisho wa mkataba husika. Hata kama hakutakuwa na taarifa ya ukomo wa mkataba huo basi taarifa iliyopo katika mkataba husika inatosha kumtaarifa mwajiriwa kuwa mkataba wake utakwisha siku fulani. Katika shauri hili ni wazi kuwa mikataba ya waleta maombi ilifika ukomo na walipewa taarifa kuwa haitahuishwa. Kutokana na mazingira hayo nakubaliana na maamuzi ya Tume kuwa uachishwaji kazi katika shauri hili ulikuwa ni halali na ulizingatia matakwa ya sheria. Katika hoja ya mwisho ya nafuu, mahakama imepitia CMA Fl inayoanziashia shauri Tume na kuona kuwa waleta maombi waliomba kulipwa mshahara wa mwezi mmoja badala ya taarifa ya kuachishwa kazi, posho ya likizo, fidia ya miezi 12 kiinua mgongo na cheti cha utumishi. Kwakuwa mahakama hii haijatofautiana na maamuzi ya Tume 13 inaona kuwa madai ya waleta maombi hayana msingi. Taarifa za kuachishwa kazi (kielelezo D2 kwapamoja) kimeeleza wazi watalipwa mshahara wa mwezi mmoja badala ya notisi, posho ya likizo pamoja na kiinua mgongo. Hivyo basi fidia zote wanazostahili walilipwa mjibu maombi anaamuriwa tu kuwapa na cheti cha utumishi ambacho ni haki ya kila mtumishi kwa mujibu wa kifungu cha 44(2) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini. Kutokana na maelezo hapo juu Mahakama inaona kuwa maombi haya hayana mashiko na yanatupiliwa mbali. Mahakama inaunga mkono maamuzi ya Tume. Imeamuriwa hivyo. Imesainiwa leoTarehe 12 Mwezi Oktoba Mwaka 2022. S.M. MAGHIMBI JAJI 14