KESI KUMBUKUMBU NO 15637 OF 2024 CHRISTIAN FANDE MAPUNDA VRS LAKE OIL LTD
- Citation
- KESI KUMBUKUMBU NO 15637 OF 2024 CHRISTIAN FANDE MAPUNDA VRS LAKE OIL LTD
- Status
- Judgment
- Jurisdiction
- Tanzania
- Court
- TANZLII
- Decision
- 1 January 2024
- Posture
- Labour Revision / Judgment
- Language
- English
More details
- Court
- TANZLII
- Decision
- 1 January 2024
- Posture
- Labour Revision / Judgment
- Language
- English
On this page
Professional case brief
Research organized from the available case record
01
Holding and result
Applicant is not entitled to salary arrears for months not worked after settlement agreement and knowledge of termination; however, he is entitled to payment in lieu of notice and leave pay for the last contract period, but not severance pay as his contract was only for one year.
Court disposition
Partly allowed
Orders
- Applicant to be paid TZS 1,800,000, inclusive of TZS 1,200,000 previously awarded and an additional TZS 600,000 for payment in lieu of notice and leave pay.
- Other claims dismissed.
02
Material facts
Parties
Christian Fande Mapunda
Applicant Counsel: Majaliwa MusaLake Oil Ltd
Respondent Counsel: Heriolotu BonifaceAmounts and remedies
- Salary Per Month: TZS 300,000
- Salary Arrears Claimed: TZS 4,200,000
- Settlement Amount (cma F6): TZS 700,000
- Additional Awarded (notice + Leave): TZS 600,000
- Total Awarded by Court: TZS 1,800,000
03
Procedural history
Posture
Labour Revision / Judgment
04
Questions and positions
Legal issues
- 01
Whether the applicant is entitled to salary arrears for the period under disciplinary process
- 02
Whether the applicant is entitled to leave pay and payment in lieu of notice
- 03
Whether the applicant is entitled to severance pay
Party arguments
- Applicant
- Applicant argued he was entitled to 14 months' salary arrears and leave pay for the period under disciplinary process, as well as payment in lieu of notice and severance pay, since his employment was terminated on 07/05/2021, not 30/05/2020.
- Respondent
- Respondent argued applicant had already been paid as per settlement agreement (CMA F6), that termination was effective 30/05/2020, and that no further payments were due.
05
Court’s reasoning
Legal principles
- 01
Section 41(3) Employment and Labour Relations Act, 2004; Director Gema Security v Joshua Gombanila, High Court Labour Revision No. 192/2011
Notice of termination must be in writing and limitation period runs from date of written notice.
- 02
Section 41 Employment and Labour Relations Act
Payment in lieu of notice is due if notice is not given.
- 03
Section 44(1) Employment and Labour Relations Act
Leave pay is due for the last contract period if not taken.
- 04
Section 42(2)(a) Employment and Labour Relations Act
Severance pay is only due for contracts exceeding one year.
06
Ratio, limits and disposition
Ratio decidendi
Applicant is not entitled to salary arrears for months not worked after settlement agreement and knowledge of termination; however, he is entitled to payment in lieu of notice and leave pay for the last contract period, but not severance pay as his contract was only for one year.
Obiter and limits
- Settlement agreements before the Commission are enforceable as awards.
- Employees cannot claim salary for periods not worked after termination is agreed.
Court disposition
Partly allowed
- Applicant to be paid TZS 1,800,000, inclusive of TZS 1,200,000 previously awarded and an additional TZS 600,000 for payment in lieu of notice and leave pay.
- Other claims dismissed.
Source and reliance status
TANZLII · 1 January 2024
This page organises the available record for research. Confirm quotations, current status, and subsequent treatment against the official source before relying on the case.
Judgment reading view
Judgment text
The complete available source text.
TANZLII
Judgment· 1 January 2024
KATIKA MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
DIVISHENI YA KAZI
DAR ES SALAAM MAREJEO NA. 15637 YA MWAKA 2024 KES1 KUMBUKUMBU NA. 202407021000015637 CHRISTIAN FANDE MAPUNDA.................................... MLETA MAOMBI
DHIDI YA LAKE OIL LTD ................................................................... MJIBU MAOMBI
HUKUMU Tarehe ya Amri ya Mwisho\16/ 08/2024 Tareheya Hukumu: 03/ 09/2024 MLYAMBINA, J. Baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (itakjulikana kama Tume) katika Mgogoro wa Kazi Na. CMA/DSM/TMK/103/2021/201/117/2021, MIeta Maombi amewasilisha maombi haya mbele ya Mahakama akijikita katika hoja zifuatazo: i. Kwamba, mheshimiwa Mwamuzi al/kosea kisheria na k/uha/isia kuacha kujumuisha mafimbikizo ya mishahara ambayo hakulipwa kipindi chote cha mchakato wa hatua za kinidhamu afizokuwa akifanya Mwajiri Hadi ukomo wa Ajira, miezi 14 na Likizo. if. Kwamba, Mheshmiwa Mwamuzi al/kosea kisheria na kiuhafisia kushikiiia kwamba madai mengine hakustah/ii wakati dai fa mishahara na likizo vipo kisheria kwakuwa ailikuwa kazini chini ya taratibu ya hatua za kinidhamu. Shauri hili liliendeshwa kwa njia ya maandishi. Mbele ya Mahakama hii Mleta Maombi aliwakilishwa na Bw. Majaliwa Musa, Mwakilishi Binafsi. Ilihali Wakili Heriolotu Boniface alimwakilisha Mjibu Maombi. Mahakama imezingatia mawasilisho ya pande zote mbili na kuona kuwa katika shauri hili kuna hoja kuu moja ya msingi ya kutatua. Endapo Mleta Maombi alithibitisha mbele ya Tume madai yake ya malimbikizo ya mishahara na posho ya Hkizo. Katika mawasilisho yake, Bw. Musa alieleza kuwa Mleta Maombi aliajiriwa na Mjibu Maombi mnamo tarehe 01/09/2016 kwa mkataba wa muda maalumu wa mwaka mmoja. Kwamba, ilipofika
tarehe 06/04/2020 Mleta Maombi alipokea barua ya kusimamishwa kazi na kutakiwa kufika kwenye kikao cha nidhamu mnamo tarehe 8/04/2020. Alifika tarehe husika lakini kikao kiliahirishwa na kumtaka Mleta Maombi kuhudhuria tena kikao tarehe 11/04/2020. Kwamba, tarehe hiyo tena kikao hakikufanyika na Mleta Maombi alipewa ahirisho la mdomo kwa muda mrefu hadi pale alipoachishwa kazi mnamo tarehe 07/05/2021. Bw. Musa aliendelea kueleza kuwa Mleta Maombi alisimamishwa kazi kuanzia tarehe 06/04/2020 hadi tarehe aliyopewa barua ya ukomo wa ajira na cheti cha utumishi yaani tarehe 07/05/2021. Hivyobasi, alikuwa anastahili kulipwa mishahara ya miezi 14 kiasi cha TZS 4,200,000/= kwa kuwa alikuwa analipwa mshahara kwa mwezi kiasi cha TZS 300,000/= x 14 = 4,200,000/= hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini. Mwakilishi alisisltiza kuwa, ajira ya Mleta Maombi ilisitishwa tarehe 07/05/2021 ambapo ndio siku aliyopokea barua hiyo na sio tarehe 30/05/2020 kama ilivyoandikwa kwenye barua hiyo. Mwakilishi allkazia mawasilisho yake kwa kuiomba Mahakama irejee kwenye kesi ya Mahakama kuu ya Tanzania Kitengo cha Kazi kupitia marejeo na. 192/2011 kati ya Director Gema Security dhidi ya Joshua Gombanila iliyoamuriwa tarehe 31/01/2013 mbele ya S.C. MOSHI, J ambapo katika ukurasa wa 3 iliamuriwa ifuatavyo: I concede, with the reasoning of the Mediator at p. (3), that the law under section
41 (3) of Employment and Labour Relations Act, 2004 requires the notice of termination to he in writing. The period of limitation of time to institute the proceedings of this nature start to run from the day the employee is served with the notice of termination in writing. Pia, Mleta Maombi aliturejesha kwenye Kifungu cha 31(1) na (8) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini [Sura 366 Kama itivyorejewa 2019] (Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini). Pamoja na mengine, Mleta Maombi anadai malipo ya mshahara mmoja badala ya taarifa ya kuachishwa kazi pamoja na malipo ya posho ya likizo. Mjibu Maombi kupitia wakili Boniface alieleza kuwa, Mleta Maombi alishalipwa madai yake kama inavyoonesha kwenye hati ya makubaliano (CMA F6). Wakili huyo alipinga vikali madai ya kuwa Mleta Maombi aliachishwa kazi tarehe 07/05/2021 kama anavyodai. Alisisitiza kuwa Mleta Maombi aliachishwa kazi tokea tarehe 30/05/2020 kama barua ya kuachishwa kazi inavyojieleza. Hivyobasi, aliiomba Mahakama itupilie mbali madai yake. Baada ya kupitia kumbukumbu, Mahakama imeona ya kuwa mnamo tarehe 20/04/2020 Mleta Maombi aliwasilisha madai yake mbele ya Tume dhidi ya Mjibu Maombi akidai malimbikizo ya mshahara wa mwezi wa Machi, 2020 TZS 211,000/= na malimbikizo ya sikukuu za Kitaifa TZS 634,590/=. Mgogoro huo ulifanyiwa suluhu na kufikia makubaliano kama yanavyoonekana katika hati ya makubaliano CMA F6 (kielelezo Dl) mnamo tarehe 06/07/2020: 1. Mlalamikiwa atamlipa mlalamikaji jumla ya shilingi laki saba (700,000).
2. Malipo yatafanyika tarehe 14/07/2020 mbele ya Tume.
3. Mlalamikiwa atampatia Mlalamikaji barua yake ya ukomo wa ajira. Hivyobasi, kupitia makubaliano hayo, ni wazi Mleta Maombi alikubaliana na kukoma kwa ajira yake na jukumu la Mjibu Maombi ilikuwa ni kumpatia barua ya kumwachisha kazi kama walivyokubaliana. Baada ya Mjibu Maombi kushindwa kutimiza makubaliano hayo, ndipo Mleta Maombi alipofungua shauri la ukaziaji hukumu na kukabidhiwa barua yake ya kuachishwa kazi iliyokuwa imeandaliwa tokea tarehe 30/05/2020. Kwa mazingira hayo, kwakuwa Mleta Maombi alijua wazi kuwa ajira yake ilikuwa imekoma tokea walipofikia makubaliano husika, ni wazi kuwa hastahili malipo ya malimbikizo ya mishahara anayodai. Kwanza, ni miezi ambayo hajafanya kazi hivyo hawezi kulipwa ujira kwa kazi ambayo hajaifanya. Pili, kupitia makubaliano alijua fika ajira yake imekoma na ilikuwa ni kumalizia hatua za utekelezaji wa makubaliano ambayo pia yanaheshimika kama Tuzo ya Tume. Kuhusu madai ya likizo, Mahakama inaungana mkono na maamuzi ya Tume kuwa Mleta Maombi alishindwa kuthibitisha madai hayo. Pia, Mleta Maombi amedai madai ya mshahara wa mwezi mmoja badala ya notisi ya kuachishwa kazi pamoja na kiinua mgongo. Kuhusu mshahara mmoja badala ya taarifa ya kuachishwa kazi, Mleta Maombi anastahili malipo hayo kwa mujibu wa Kifungu cha 41 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini. Hivyo, muamuzi alikosea kutompa madai hayo. Vilevile, Mleta Maombi pia anastahili
madai ya malipo ya likizo kama ilivyoelekezwa katika kifungu cha 44(1) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Likizo anayostahili Mleta Maombi ni ya kwenye mkataba wa mwisho tu kwakuwa likizo nyingine ameshindwa kuzithibitisha. Kuhusu madai ya kiinua mgongo, Mahakama inaona hastahili madai hayo kwakuwa alikuwa na mkataba wa muda maalumu wa mwaka mmoja. Kwa mujibu wa kifungu cha 42(2)(a) cha Sherla ya Ajira na Mahusiano Kazini, fao hilo hulipwa kwa mfanyakazi mwenye mkataba wa kuvuka mwaka mmoja. Mleta Maombi mkataba wake ulikuwa wa mwaka mmoja tu. Kwa kumalizia, Mahakama Inaona ya kuwa shauri hili limefanikiwa kiasi kwakuwa madai mengine ya Mleta Maombi yamekataliwa. Pamoja na fidia aliyoamuriwa na Tume, Mahakama inamuongezea Mleta Maombi malipo ya mshahara mmoja badala ya taarifa ya kuachishwa kazi kiasi cha TZS 300,000/= pamoja na mshahara mmoja kama malipo ya likizo. Hivyo, jumla ya kiasi atakachoongezewa ni TZS 600,000/= zikijumuishwa na fedha alizoamuriwa na Tume TZS 1,200,000/= Mahakama inaamuru Mleta Maombi alipwe jumla ya kiasi cha TZS 1,800,000/=. Imeamuriwa hivyo. YJ. MLYAMBINA
JAJI 03/09/2024 Maamuzi haya yamesomwa tarehe 3 Septemba 2024 saa nane na nusu mchana mbele ya Majaliwa Musa, Mwakilishi Binafsi wa Mleta Maombi na Diana Frank, Afisa Mwandamizi wa Mjibu Maombi. Haki ya kukata rufaa imeelezwa.
JAJI 03/09/2024
Case-aware research
Ask AI about this case
The judgment and available research above are public. New questions open in a separate private conversation grounded in this case.