christian mwesiga michael vs board of governors of st peters junior seminary 2021 tzhcld 149 4 juni 2021
The applicant's claims for extension of time and reliefs against the respondent had already been heard and determined in previous proceedings involving the same parties and issues, thus barred by res judicata. The error regarding representation did not affect the applicant's rights or the validity of the...
Source-derived case information.
- Citation
- christian mwesiga michael vs board of governors of st peters junior seminary 2021 tzhcld 149 4 juni 2021
- Parties
- Applicant: Christian Mwesiga Michael; Respondent: Board of Governors of St. Peter's Junior Seminary
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2021
- Procedural Posture
- Labour Revision / Final Judgment
- Outcome
- dismissed
- Legal Topics
- Res Judicata, Unfair Termination, Extension of Time, Representation
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Christian Mwesiga Michael
Applicant
Board of Governors of St. Peter's Junior Seminary
Respondent
Procedural Posture
Labour Revision / Final Judgment
Legal Issues
- 1 Whether the applicant's claims before the Commission had already been heard and determined (res judicata)
- 2 Whether the Commission's decision was erroneous regarding representation
Ratio Decidendi
The applicant's claims for extension of time and reliefs against the respondent had already been heard and determined in previous proceedings involving the same parties and issues, thus barred by res judicata. The error regarding representation did not affect the applicant's rights or the validity of the Commission's decision.
Court Disposition
dismissed
Orders
- Each party to bear its own costs
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DIVISHENI YA KAZI ILIYOKAA MOROGORO MAREJEO NA. 46 OF 2020 BAINA YA CHRISTIAN MWESIGA MICHAEL................................................. MLETA MAOMBI NA BOARD OF GOVERNORS OF ST. PETER'S JUNIOR SEMINARY................................................ MJIBU MAOMBI HUKUMU Tarehe ya Mwisho ya Amri: 25/05/2021 Tarehe ya Hukumu: 04/06/2021 A. E. MWIPOPO, J. CHRISTIAN MWESIGA MICHAEL ambaye ni Mleta Maombi katika shauri hili la Marejeo ameleta shauri hili akiomba Mahakama ifanyie marejeo Uamuzi Mdogo wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi uliotolewa katika mgogoro wa kikazi Na. CMA/MORO/18/2020 wa tarehe 17 August, 2020. Mleta Maombi anaomba yafuatayo:- 1. Kwamba, Mahakama hii ikipendezwa itoe Amri ya kurekebisha na kuuweka pembeni uamuzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi katika mgogoro wa kikazi Na. CMA/MORO/18/2020 wa tarehe 17 Agosti, 2020, uliotolewa na Mhe. Kayugwa, H., Msuluhishi, kwa sababu uamuzi huo haukuwa wa haki na ni kinyume na sheria. i 2. Kwamba, Mahakama hii ikipendezwa isikilize mgogoro huu na kuamua kwa mujibu wa sheria. Maombi haya yameambatana na kiapo cha Mleta Maombi. Aya ya 4 ya kiapo imebeba hoja mbili (2) za kisheria zinazotokana na ushahidi. Hoja hizo ni kama zifuatazo;- 1. Kwamba Muamuzi alikosea kisheria, badala ya kuangalia sababu zilizosababisha kuchelewa na makosa ya kisheria yaliyofanywa na Mjibu Maombi ikiwa ni pamoja na kukamata mali zangu kinyume na sheria, alikimbilia kutafsiri kuhusu hoja kuwa maombi haya yalishasikilizwa na kutolewa uamuzi (res judicata) kinyume cha sheria. 2. Kwamba Muamuzi alikosea kisheria kwa kuona kwamba Mh. Boniface Basesa alikuwa mwakilishi wangu katika maombi hayo. Kwa kifupi, Mleta Maombi alikuwa ameajiriwa na St. Peters Junior Seminary, ambaye ni Mjibu Maombi, kama mwalimu mnamo tarehe 6 Juni, 2013. Aliachishwa kazi mnamo tarehe 26 April, 2017. Mleta Maombi hakuridhika na uamuzi wa Mjibu Maombi ndipo alipeleka mgogoro huo mbele ya Tume ambapo ulisajiliwa kwa Na. RF/CMA/MOR/96/2017 na shauri hilo kutupiliwa mbali na Tume. Ndipo alifungua tena shauri Na. CMA/MOR/18/2020 mbele ya Tume akiomba kuongezwa muda wa kufungua malalamiko yake lakini maombi yake yalitupiliwa mbali 2 (dismisses) kwa kuwa tayari mgogoro kama huu ulifunguliwa na Mleta Maombi mbele ya Tume, ukasikilizwa na kumalizika. Mleta Maombi hakuridhika na Uamuzi huo ndipo akafungua shauri hili la marejeo Mahakamani. Katika shauri hili, Mleta Maombi hakuwa na mwakilishi na aliwasilisha hoja zake mwenyewe ambapo Mjibu Maombi alikuwa anawakilishwa na Bw. Asifiwe Alinanuswe, Wakili. Akifanya mawasilisho ya msingi kuunga mkono maombi haya, Bw. Christian Mwesiga Michael alieleza ya kwamba, Mgogoro huu ulitokea tarehe 09 Februari, 2018 ambapo Mjibu Maombi alifungua nyumba anayokaa na kuchukua vitu vyote. Vitu hivyo bado vinashikiliwa na Mjibu Maombi hadi sasa hivi. Ameeleza kuwa alifungua shauri Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ya kudai kulipwa fidia ya kuachishwa kazi na kulipwa malipo ya madhara aliyopata kwa kuachishwa kazi. Msuluhishi aliyafuta madai hayo kwa kuwa yalishawahi kusikilizwa na kutolewa uamuzi na Tume katika Shauri Na. CMA/MORO/96/2017. Hivyo, Tume ilikosea kwa kushindwa kuonyesha ni madai yapi kati ya madai yake yaliyowasilishwa na kushughulikiwa na Tume. Kwa sababu hiyo, anaona kuwa uamuzi wa Tume hauonyeshi sababu ya Tume kufikia uamuzi kuwa shauri hilo limewahi kusikilizwa na kuamriwa na Tume katika shauri jingine. 3 Aidha, Mleta maombi alieleza kwamba katika uamuzi wa Tume, Muamuzi alieleza kuwa alikuwa anawakilishwa na Bw. Boniface Edward Basesa wakati sio kweli. Katika shauri lilokuwa mbele ya Tume amekuwa analiendesha mwenyewe na hakuwahi kutoa taarifa ya uwakilishi wa Bw. Basesa mbele ya Tume. Hivyo, anaona hajatendewa haki kwa mtu mwingine kwenda Tume na kumuongelea. Hivyo Mleta Maombi anaomba shauri lililokuwa mbele ya Tume libatilishwe kwa sababu halikuzingatia haki. Akijibu mawasilisho ya Mleta Maombi, Wakili wa Mjibu Maombi alieleza kuhusu uamuzi uliofanywa na Tume ya kwamba maombi ya Mleta Maombi yalishasikilizwa na kumalizika ("Res Judicata"). Tume ilikuwa sahihi kuona kuwa shauri liliopo mbele yake lilikuwa tayari limeshasikilizwa na kutolewa uamuzi. Ameeleza kuwa Mleta Maombi alifungua mashauri kadhaa ya aina hiyo hiyo ili kuomba ongezeko la muda la kuwasilisha mgogoro wake mbele ya Tume. Alifungua shauri la kwanza lenye Na. CMA/MORO/1/2019 ambalo pamoja na mambo mengine aliwasilisha maombi ya kuongezewa muda wa kufungua shauri na la kuomba arudishiwe vitu vyake vilivyoshikiliwa na mwajiri wake. Tume iliona kuwa sababu zilizotolewa hazina mashiko katika uamuzi uliotolewa tarehe 27 Septemba, 2019 na Msuluhishi Kayungwa. Mleta Marejeo akarudi tena Tume akafungua Mgogoro Na. CMA/MORO/29/2019 na akiomba nafuu 4 zilezile kwa chanzo cha mgogoro uleule na Msuluhishi Mwakyusa alitoa uamuzi tarehe 18 Oktoba, 2019 na kutupilia mbali maombi hayo. Mleta maombi akafungua tena mgogoro ule ule Tume na ukapewa Na. CMA/MORO/38/2019 mbele ya Mhe. Simba ambaye alitoa Uamuzi tarehe 26 Machi, 2020. Baada ya hapo, Mleta Maombi akafungua tena mgogoro namba CMA/MOR/18/2019 ambapo walisikilizwa na uamuzi ulitolewa tarehe 17 Agosti, 2020 na Mhe. Kayuga, Msuluhishi. Katika shauri hilo, Msuluhishi akiongozwa na Kifungu cha 9 cha Sheria ya madai alieleza kuwa mgogoro huo haupo kihalali kwa sababu ulishasikilizwa na kutolewa uamuzi na Tume hapo kabla hivyo shauri hilo jipya haliwezi kufunguliwa tena dhidi ya mtu yuleyule, kuomba nafuu zilezile kutokana na chanzo cha mgogoro uleule. Fomu Na. 2 ya Tume aliyowasilisha Mleta Maombi mbele ya Tume kuwa anayo maombi mengi hakuondoi msingi wa maombi yake. Maana maombi yake ya msingi ni kuongezwa muda. Wakili akiendelea kueleza ya kwamba Mleta Maombi katika mawasilisho yake anadai Msuluhishi alikosea kunukuu maombi yake Na. CMA/MORO/96/2017 kati ya Wadaawa hawa. Maamuzi hayo yalifika hadi katika Mahakama hii ambayo iliyatolea Uamuzi na hakuna rufaa iliyokatwa kwenda Mahakama ya Rufaa. Na katika marejeo hayo Mleta Maombi aliomba nafuu hiyo hiyo. 5 Wakili alieleza kanuni ya kisheria inaelekeza wazi kuwa hakuna mgogoro utakaosikilizwa kuhusu wadaawa walewale, akiomba nafuu lie lie katika Mahakama yenye Mamlaka ambayo tayari yamesikilizwa na kutolewa Uamuzi ambayo yataruhusiwa kufunguliwa tena. Mahakama hii ilikuwa na msimamo huo katika kesi ya Athamasic T. Masinde T/A Abeti Primary School dhidi ya NBC, kesi ya Biashara Na. 34 ya 2016, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi iliyoketi Dar es Salaam. Hivyo, msuluhishi alikuwa sahihi kuona kuwa shauri lililokuwa mbele yake lilikuwa limefunguliwa kinyume na sheria. Kuhusu hoja ya pili kwamba Msuluhishi alikosea kusema Bw. Boniface Basesa alikuwa mwakilishi wake, Wakili wa Mjibu Maombi alieleza kuwa matendo ya Mleta Maombi ndio yaliyopelekea Msuluhishi kuona kuwa Bw. Boniface Basesa alikuwa mwakilishi wake. Bw. Basesa ndiye aliyepokea nakala ya hukumu ya mgogoro uliokuwa mbele ya Tume na katika shauri hili alipokea majibu ya Mleta Maombi. Kusomeka kwa Bw. Basesa kama mwakilishi binafsi wa Mleta Maombi kwa namna yoyote hakujaathiri haki ya Mleta Maombi. Wakili anaomba Mahakama ione kuwa sababu ya Tume kusema Bw. Basesa alikuwa mwakilishi wa Mleta Maombi haiwezi kufanya uamuzi wa Tume uwe batili. Wakili wa Mjibu Maombi aliomba shauri hili la marejeo litupiliwe mbali kwa kukosa mashiko. 6 Akifanya mawasilisho ya nyongeza (rejoinder submission) Mleta Maombi alieleza Mashauri yaliyoorodheshwa Mjibu Maombi pia yalirejelewa na Msuluhishi lakini haukuwa msingi wa uamuzi wake hivyo anaomba yasizingatiwe. Shauri Na. CMA/MORO/96/2017 ndilo lilikuwa msingi wa uamuzi wa Tume. Katika uamuzi huo msuluhishi hakueleza iwapo nafuu zilizoombwa katika shauri hilo na shauri lililokuwa mbele ya Tume kama ziliwahi kushughulikiwa. Katika shauri ambalo Msuluhishi alilirejea waadawa walikuwa ni Christian Mwesiga Michael na Bodi ya Maaskofu. Katika mgogoro huu ni kati ya Christian mwesiga Michael dhidi ya Bodi ya Magavana wa St. Peters Junior Seminary. Pia nafuu zilizoombwa zinatofautiana. Katika mgogoro wa awali ilikuwa ni uachishwaji kazi usio halali (unfair termination) na katika mgogoro uliokuwa mbele ya Tume sio uachishwaji kazi usio halali. Hivyo, Mahakama hii inayo mamlaka ya kunisikiliza kwa kuwa bado kuna mgogoro. Kuhusu uwakilishi wa Basesa Mleta Maombi alieleza hilo ni suala la kisheria. Na hakuna uthibitisho wa kumteua Bw. Basesa kuwa mwakilishi wake. Mahakama baada ya kupokea mawasilisho ya pande zote mbili inaona wazi ya kwamba hoja zinazobishaniwa ambazo Mahakama inabidi izitolee uamuzi ni mbili. Hoja hizo ni kama ifuatavyo:- i) Iwapo maombi ya Mleta Maombi mbele ya Tume yaliwahi kusikilizwa na kutolewa maamuzi na Tume hapo kabla. 7 ii) Iwapo uamuzi wa Tume ulipatikana kimakosa. Kwa kuanza na hoja ya kwanza, Mahakama inajielekeza katika kifungu cha 9 Sheria ya Mwenendo wa Madai, Sura ya 33 ya Sheria, kama ilivyorejewa mwaka 2019, (Civil Procedure Code Act, Cap. 33 of the Laws R.E. 2019) ambacho kinakataza Mahakama kusikiliza shauri ambalo tayari limesikilizwa kikamilifu na Mahakama yenye mamlaka. Kifungu hicho kinasomeka kama ifuatavyo, nanukuu kwa lugha ya kiingereza:- "9. No court shall try any suit or issue in which the matter directly and substantially in issue has been directly and substantially in issue in a former suit between the same parties or between parties under whom they or any of them claim litigating under the same title in a court competent to try subsequent suit or the suit in which such issue has been subsequently raised and has been heard and finally decided by such court” Kifungu tajwa hapo juu kinaizuia Mahakama kusikiliza shauri au hoja ambayo moja kwa moja au maudhui yake ni hoja katika shauri kati ya wadaawa walewale au baadhi ya wadaawa kwa jina hilo hilo na shauri hilo likawa limesikilizwa kikamilifu na kutolewa uamuzi na Mahakama hiyo. Katika kesi ya George Shambwe dhidi ya Tanzania Italian Petroleum Company Ltd [1995] TLR 21, ilielezwa kwamba, nanukuu: - "For res judicata to apply not only it must be shown that the matter directly and substantially in issue in the contemplated suit is the same parties but also it must be shown that the matter was finally heard and determined by a competent court". 8 Katika kesi tajwa hapo juu Mahakama iliona kuwa ili kanuni ya res judicata itumike inatakiwa ionekane kuwa suala husika ni hoja ya moja kwa moja au kuna maudhui yanafanana na yale katika shauri linalotegemewa kuendelea kusikilizwa kuhusu wadaawa wale wale Ila pia lazima shauri hilo liwe lilisikilizwa na kutolewa uamuzi na Mahakama yenye mamlaka. Mahakama ilikuwa na msimamo kama huo katika kesi ya Gerald Chuchuba dhidi ya Rector, Itaga Seminary [2002] TLR 213. Mleta Maombi ameelezea kuwa maombi haya hayajawahi kutolewa uamuzi na Tume kwa kuwa mgogoro uliopo mbele ya Tume hahusiani na uachishwaji kazi usio halali. Maombi ya awali yalihusu uachishwaji kazi usio halali. Mjibu Maombi kwa upande wake ameeleza kuwa Mleta Maombi amekuwa akifungua mashauri kadhaa mbele ya Tume akiomba nafuu zile zile kuhusu mwajiri wake. Baada ya kupitia kumbukumbu zilizopo ninaona kwamba Mleta Maombi alishawahi fungua mgogoro mbele ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi dhidi ya mwajiri wake kuomba Maombi ya msingi yafunguliwe nje ya muda. Mleta Maombi katika shauri hili anapinga uamuzi wa Tume kukataa maombi yake ya kuongezwa muda wa kufungua mgogoro mbele ya Tume kwa kuwa iliona madai kama haya yaliwahi kufunguliwa na Mleta Maombi katika Mgogoro Na. CMA/MOR/96/2017 na Tume ilitoa uamuzi ambao Mleta Maombi aliukatia rufaa kwenda Mahakama ya Kuu, Divisheni 9 ya Kazi katika Marejeo Na. 31 ya 2020 kupinga uamuzi huo wa Tume na Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi ilitoa uamuzi wake. Maombi ya msingi ya Mleta Maombi mbele ya Tume ilikuwa ni kuongezwa muda ili afungue Mgogoro dhidi ya Mjibu Maombi kuhusu kuvunjwa kwa mkataba wake wa ajira, kuvunjiwa nyumba, kushikiliwa mali zake na kuharibiwa mali zake. Aidha, nafuu alizoomba ni kurudishiwa mali zake, kulipwa shilingi 10,000,000/= kufidia mali zilizoharibika na kupotea, kulipwa shilingi 20,000,000/= fidia ya kuvunjiwa mkataba, kulipwa shilingi 25,000,000/= fidia ya madhara ya jumla na kupewa posho ya gharama ya kila siku (subsistence allowance). Tume iliona kuwa madai ya msingi ya Mleta Maombi yalishatolewa uamuzi na Tume katika mgogoro Na. CMA/MOR/96/2017 katika shauri baina ya Mleta Maombi na Bodi ya Maaskofu (Board of Bishops). Nimepitia uamuzi wa Tume katika mgogoro Na. CMA/MOR/96/2017 na kuona kuwa Mleta Maombi alifungua mgogoro huo kuwa ameachishwa kazi isivyo halali na kuwa alikuwa anaomba nafuu ya kulipwa fidia ya mshahara wa miezi 36 kwa kuachishwa kazi isivyo halali au kurudishwa kazini bila kupoteza haki zake na apatiwe na haki nyingine. Ushahidi unaonesha kuwa Mleta Maombi aliajiriwa na Bodi ya Maaskofu ya St. Peters Junior Seminary kama Mwalimu wa somo la Kiswahili na kiingereza tarehe 6 Juni, 2013. Hivyo, hii inathibitisha kuwa wadaawa katika kesi hizi io mbili ni walewale pamoja na kuwa majina ya Mjibu Maombi yanatofautiana. Katika mgogoro Na. CMA/MOR/96/2017 Mjibu Maombi anaitwa Bodi ya Maaskofu na katika Mgogoro Na. CMA/MOR/18/2020 Mjibu Maombi anaitwa Bodi ya Magavana wa St. Peters Junior Seminary. Hivyo Migogoro yote miwili ilihusu mwajiri ambaye ni St. Peters Junior Seminary na tarehe ya kuajiriwa na kuachishwa kazi ni ileile. Katika mgogoro Na. CMA/MOR/96/2017 Tume iliwasikiliza wadaawa wote na kuona kuwa Mleta Maombi hakuachishwa kazi na Mjibu Maombi bali mkataba wake ulifikia ukomo. Aidha, Tume iliona kuwa Mleta Maombi stahili pekee anayotakiwa kulipwa ni fedha ya nauli na fedha ya mizigo kwa ajili yake na familia yake kiasi cha shilingi 1,640,000/=. Mleta Maombi aliwasilisha marejeo namba 31 ya 2020 mbele ya Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi iliyoketi Morogoro kupinga Uamuzi wa Tume. Mahakama Kuu iliamua kuwa Mjibu Maombi amlipe Mleta Maombi fedha ya nauli na fedha ya mizigo kiasi cha shilingi 1,640,000/= na fedha ya kujikimu kuanzi tarehe mkataba ulipofikia ukomo hadi tarehe ya kulipwa kwa fedha ya nauli. Hivyo, ni wazi kuwa madai ya msingi ya Mleta Maombi kuwa mkataba wake ulivunjwa na anadai alipwe posho ya kujikimu tayari yalishatolewa uamuzi na Tume na Mahakama hii katika hoja ya kuachishwa kazi isivyo halali. Kuhusu malalamiko ya kuvunjiwa nyumba, kushikiliwa mali zake na kuharibiwa mali zake ambayo ni sehemu ya Madai yake katika Mgogoro Na. ii CMA/MOR/18/2020, haya hayakuwa sehemu ya madai katika Mgogoro Na. CMA/MOR/96/2017. Hata hivyo, kwa kuwa alichanganya madai ambayo tayari yalishasikilizwa na kutolewa uamuzi na Tume, nakubaliana na uamuzi wa Tume kuwa baadhi ya hoja tayari zilikuwa zimeshasikilizwa na Tume na kutolewa uamuzi. Kwa sababu hiyo naona kuwa mgogoro wa msingi unaoombewa kuongezwa muda na Mleta Maombi ulikuwa umewasilishwa kinyume cha sheria kwa kuwa uliwahusu wadaawa walewale, baadhi ya hoja zilikuwa ni zilezile kuhusiana na nafuu ambazo baadhi ni zilezile. Kuhusu Muamuzi kuandika katika uamuzi wa Tume kuwa Mleta Maombi aliwakilishwa na Mwakilishi Binafsi aitwaye Basesa, naona hayo ni makosa kwa upande wa Muamuzi. Mwenendo wa Tume (Commission proceedings) inaonesha kuwa Mleta Maombi alijiwakilisha mwenyewe na hakuna siku aliyowakilishwa na mtu mwingine. Hata siku ya kusikilizwa kwa pingamizi lililopelekea uamuzi wa Tume tarehe 03 Juni, 2020 Mleta Maombi alijiwakilisha na kuwasilisha majibu yake kuhusu pingamizi. Hata hivyo, pamoja na Tume kukosea kuandika kuwa Mleta Maombi aliwasilishwa na Bw. Basesa, sioni kwa namna gani Mleta Maombi alikosa haki zake kwa kuwa alipata nafasi ya kusikilizwa kama rekodi ya mwenendo wa mgogoro mbele ya Tume inavyoonesha. Kosa la Muamuzi ni dogo ambalo linatibika na halifanyi uamuzi wake kuwa batili. 12 Hivyo, kwa ujumla wake naona shauri hili la marejeo halina mashiko na nalitupilia mbali (dismissed). Kila upande utabeba gaharama zake za kuendesha shauri hili. A. E. MWIPOPO* x JUDGE 04/06/2021 13