crane transport agent co ltd vs juma mwipi na mwenzake 2022 tzhcld 997 19 oktoba 2022
The conciliator lacked authority to decide both the extension of time and the one-sided award; thus, the applicant is granted extension of time to challenge the award, and the matter is remitted to the Commission for proper hearing.
Source-derived case information.
- Citation
- crane transport agent co ltd vs juma mwipi na mwenzake 2022 tzhcld 997 19 oktoba 2022
- Parties
- Applicant: Crane Transport Agent Co. Ltd; Respondent: Juma Mwipi; Respondent: Omary Mrisho
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2022
- Procedural Posture
- Application for Revision / Judgment
- Outcome
- application allowed
- Legal Topics
- Revision of Arbitral Award, Authority of Conciliator, Right to Be Heard, Extension of Time
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Crane Transport Agent Co. Ltd
Applicant
Juma Mwipi
Respondent
Omary Mrisho
Respondent
Procedural Posture
Application for Revision / Judgment
Legal Issues
- 1 Whether the conciliator had authority to decide the application for extension of time and the one-sided award
- 2 Whether evidence was taken without oath
- 3 Whether applicant should be granted extension of time to challenge the one-sided award
Ratio Decidendi
The conciliator lacked authority to decide both the extension of time and the one-sided award; thus, the applicant is granted extension of time to challenge the award, and the matter is remitted to the Commission for proper hearing.
Court Disposition
application allowed
Orders
- Decision denying extension of time is set aside
- Applicant is granted extension of time to file application to set aside one-sided award
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
KATIKA MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA D1VISHENI YA KAZI PAR ES SALAAM MAOMBI YA MAREJEO NA. 181 YA MWAKA 2022 (Inatokana na maombi Na. CMA/DSM/MISC/64/2020 Mhe. Lemwely, Muamuzi) KATI YA CRANE TRANSPORT AGENT CO. LTD, .................................... MLETA MAOMBI DHID1 YA JUMA MWIPI ............................................. MJIBU MAOMBI 1 OMARY MRISHO ................................................ MJIBU MAOMBI 2 HUKUMU S.M, MAGHIMBI, J: Hukumu inatokana na maombi yaliyoletwa na Mleta Maombi chini ya kifungu cha 91(l)(a)(b),(2)(a)(b)(c) & 94(1) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Sura ya 366, iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019, pamoja na Kanuni ya 24(l),24(2)(a)(b)(c)(d)(e)(f), 24(3)(a)(b)(c)(d), 24(11), 28(l)(a)(b)(c)(d) & 55(1)(2) ya Kanuni za Mahakama ya Kazi, Tangazo la Serikali Na. 106 ya mwaka 2007. Katika Hati yake ya Faragha, mleta maombi ameleta maombi kwa Mahakama hii kutoa amri zifuatazo: (i) Kwamba iipendeze Mahakama yako tukufu KUREJEA NA KUTENGUA Uamuzi uliyotolewa kwenye maombi No. CMA/DSM/MISC/64/2020) na kutengua TUZO ILIYOTOLEWA i U PAN DE MMOJA KWENYE MGOGORO NA. CMA/DSM/ILA/R. 1104/17 uliyotolewa kinyume na sheria mbele ya Mheshimiwa D. Lemwely, Msuluhishi). (ii) Mahakama hii tukufu itamke kwamba uamuzi kwenye maombi Na. CMA/DSM/MISC/64/2020) ni batili pia itengue mwenendo, uamuzi pamoja na ifute uamuzi wa TUZO YA UPANDE MMOJA katika Mgogoro Na. CMA/DSM/ILA/R.1104/17 kwa sababu ya kwama Tume ilikiuka utaratibu na Kwenda kinyume na matakwa kisheria ya haki ya kusikilizwa pamoja na Kwenda kinyume na matakwa ya sheria ya Ushahidi. (iii) Gharama itolewe na wajibu maombi wote (iv) Mahakama hii tukufu itoe nafuu yoyote itaona inafaa kutolewa. Maombi hayo yaliambatana na kiapo kilichoapwa na Bwana Mahmood Ally, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ambaye ni mleta maombi. Kiapo hicho kiliapwa siku ya tarehe 03 mwezi Juni, 2022. Kwa upande wao, Wajibu Maombi waliyapinga maombi haya kwa kuleta kiapo kinzani kilichoapwa na Steven Jamson Shitindi, ambaye ni mwakilishi wao, siku ya tarehe 28/06/2022. 2 Historia fupi ya maombi haya inatupeleka siku ya tarehe 18 Oktoba, 2017 pale ambapo wajibu maombi walifungua mgogoro dhidi ya Mleta Maombi katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Kanda ya Dar es Salaam ("Tume") wakilalamikia kuachishwa kazi bila ya kufuata utaratibu. Kutokana na kutohudhuria kwa mleta maombi mbele ya Tume, mgogoro huo ulisikilizwa kwa upande mmoja mbele ya Mheshimiwa Doroth Lemwely, Msuluhishi na ambaye alitoa Tuzo ya Upande mmoja tarehe 06/08/2018. Baada ya muda wa miaka zaidi ya miwili kupita, Mleta Maombi alipeleka mbele ya Tume maombi ya kuongezewa muda ili aweze kuomba kuondoloewa kwa Tuzo ya Upande mmoja. Baada kusikiliza sababu zake za kuchelewa mnamo tarehe 08/01/2022, Tume ilitoa uamuzi wake ambapo haikuridhishwa na sababu za mleta maombi na kupelekea kutupiliwa mbali kwa maombi haya na kuleta hoja zifuatazo za kisheria: (i) Tuzo ilitolewa kwa kukiuka Kanuni ya 28(2) ya Sheria ya Taasisi za Kazi (Miongozo ya Usuluhishi na Uamuzi) la Tangazo la Serikali Na. 67 ya 2007. (ii) TUZO YA UPANDE MMOJA ulitolewa kwa ulaghai katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Kanda ya Dar es Salaam. 3 (iii) TUZO YA UPANDE MMOJA bila ya kufuata sheria ya Ushahidi na pasipo kufuata utaratibu wa Ushahidi (iv) Nafuu zilitolewa pasipo kuzingatia Ushahidi wowote. (v) TUZO YA UPANDE MMOJA ilitolewa kinyume, bila ya kuangalia uwiano wa malalamiko na nyingi kupitiliza uhalisia ya malalamiko yaliyokuwa mbele ya Tume. (vi) Msuluhishi aliyeshindwa kusuluhisha mgogoro ndiye aliyetoa TUZO YA UPANDE MMOJA pasipo kuzingatia kanuni na sheria za kazi (viii) Tume ilitaka Ushahidi wa kwenye msingi wa mgogoro zilitwe kwenye maombi ya kutengua Tuzo prematured imeamuliwa na Tume kwamba, Mleta Maombi kwenye maombi ya kutengua Tuzo ya Upande mmoja ameshindwa kuleta uthibitisho kama wajibu maombi walikuwa wafanyakazi au la, mishahara yao ilikuwa ni kiasi gani. (viii) Tume imeleta hoja mpya na kuiamulia pasipo Mleta Maombi kupewa nafasi ya kusikilizwa kwenye hoja uhusika. Siku ambapo shauri lilikuja kwa ajili ya kusikilizwa, mleta maombi aliwasilishwa na Bwana Gidion Opande, Wakili Msomi na upande wa wajibu maombi uliwakilishwa na Bwana David Ndosi, Wakili Msomi. 4 Baada ya kupitia hoja za pande zote mbili, nimeona kuna hoja moja ya msingi ambayo imeletwa na Mleta Maombi ambayo inagusa moja kwa moja Mamlaka ya Msuluhishi wa Tume kufanya maamuzi yanayohusiana na Mgogoro. Bwana Opande alileta hoja mbili, moja ni kuwa aliyetoa maamuzi ya upande mmoja na pia aliyetoa maamuzi kuhusiana yanayopingwa sasa alikuwa ni Msuluhishi na sio muamuZi. Vilevile alipinga kuwa wakati wa kusikiliza ushahidi, ushahidi ulitolewa bila ya mashahidi kula kiapo. Kwa hoja hiyo Bwana Opande alinukuu uamuzi wa Mahakama ya rufani kwenye shauri la North Mara Gold Mine Vs. Khalid Abdallah Salum, Civil Appeal No. 463/2020 ambapo Mahakama ya Rufaa ilipokaa Musoma iliweka msimamo kwamba ushahidi unaochukuliwa bila ya shahidi kula kiapo ni batili. Kwenye hoja yake ya pili, alisema kuwa maamuzi ya upande mmoja pamoja na uamuzi wa kutupilia mbali kuongezewa muda pia yalisikilizwa na msuluhishi ambae hakuwa na mamlaka ya kufanya mammuzi hayo. Kwenye hoja hii Bwana Opande alinukuu maamuzi ya Mahakama ya Rufani kwenye shauri kati ya Barclays Bank (T) Limited Vs. Ayyam Matessa, Civil Appeal No. 481/2020 ambapo katika ukurasa wa 13 wa maamuzi yake, Mahakama ilisisitiza kuwa Mamlaka ya kusema kwamba uachishwaji kazi wa mtumishi ulikuwa ni wa halali au la yako kwa Muamuzi tu na sio Msuluhishi. 5 Kutokana na hoja hizi, Bwana Opande aliiomba Mahakama hii ione kwamba Msuluhishi hakuwa na Mamlaka ya kutoa maamuzi aliyotoa na hivyo iyafute maamuzi yake. Kwa upande wake, Bwana Ndosi hakuwa na lolote la msingi la kujibia kwenye hoja hii muhimu zaidi ya kusema kwamba kabla Bwana opande hajakwenda kwenye misingi ya Mamlaka ya Msuluhishi, ni lazima apate ruhusa ya kuongezewa muda. Kwa upande wangu nitaanzia hapa alipoishia Bwana Ndosi ambapo amedai kuwa Mleta Maombi alitakiwa kwanza kuthibitisha sababu za kuchelewa kuleta maombi haya kabla hajaleta hoja za kwamba msuluhishi hakuwa na mamlaka. Nimeona nianzie na hili kwakuwa linanipa fursa ya ' kuweka msisitizo na kukumbusha kuwa kuna maamuzi mengi ya Mahakama hii na Mahakama ya Rufani yanayosisitiza kuwa suala linaloombewa kuongezewa muda kama linahusu ubatili wa maamuzi yaliyotolewa, basi ni sababu tosha ya kuongeza muda hata kama hakuna sababu za msingi za ucheleweshwaji huo zilizotolewa. (Angalia maamuzi ya Mahakama ya Rufani kwenye shauri la D.P. VHALAMBIA). Hivyo basi kazi kubwa iliyopo mbele yangu ni kuona kweli hoja inayohusu mamlaka ya muamuzi kuamua 6 mgogoro ni hoja inoyokwenda kwenye uhalali au ubatili wa maamuzi ya Tume kuwezesha Mahakama hii kuongeza muda. Katika kupitia rekodi za Tume nimeona kuwa ni kweli uamuzi wa upande mmoja ambao ndio ulikuwa ukiombewa kuongezewa muda ili yafanyike maombi ya kuutengua, ulikuwa umeamuliwa na Msuluhishi. Lakini kwakuwa hii si hoja ya msingi iliyoko mbele yangu, sitalisemea sana. Kwangu ninaangalia shauri linaloombewa marejeo ambalo ni Shauri Na. CMA/DSM/MISC/64/2020. Katika shauri hilo, nimeona kuwa ni kweli kama alivyoleta hoja Bwana Opande kuwa yale maombi yanayoombewa muda yanahusisha hoja za kisheria ikiwemo ushahidi kuchukuliwa bila ya kiapo na msuluhishi kufanya maamuzi ya upande mmoja. Hizi ni hoja za kisheria ambazo zingeweza kumfanya muamuzi aongeze muda. Nibali ya hayo yaliamuliwa hapo juu, lakini vilevile kuna suala la kisheria lililoko mbele yangu, baada ya mleta maombi kupeleka maombi yake mbele ya Tume ya kuongezewa muda, maombi hayo yalisikillzwa na kuamuliwa na Msuluhishi na sio muamuzi. Katika uamuzi ulionukuliwa wa Barclays Bank, Mahakama ya Rufani iliweka wazi kuwa kazi ya msuluhishi ni kusuluhisha migogoro tu na sio kufanya maamuzi yoyote. Ukiangalia kumbukumbu za shauri hili, ni msuluhishi ambaye alifanya maamuzi ya maombi hayo ni 7 yuleyule ambaye aliamua shauri upande mmoja. Sasa kutokana na ukweli huu bayana na kwa msimamo uliowekwa na Mahakama ya Rufani katika kesi ya Barclays Bank, ni maamuzi yangu kuwa msuluhishi huyo hakuwa na mamlaka ya kusikiliza maombi hayo wala kuyatupilia mbali. Hivyo basi maombi haya yanakubaliwa na uamuzi wa kumnyima mleta maombi kuongezewa muda yanatupiliwa mbali, badala yake, mleta maombi anaongezewa muda ili akapeleke maombi yake ya kuomba uamuzi wa upande mmoja uwekwe pembeni ili wasikilizwe pande zote mbili. Kutokana na maamuzi hayo, shauri linarudishwa Tume ili kusikiliza maombi ya kuondoa uamuzi wa upande mmoja. Imesainiwa leo tarehe 19 mwezi Oktoba 2022 hapa Dar-es-salaam. S.M. MAGHIMBI JAJI 8