deodatus ujuma mwanja na mwingine vs shule ya sekondari charlote 2021 tzhcld 148 4 juni 2021
The retrenchment of the applicants was based on valid structural and operational requirements, and the respondent followed the required legal procedures for notice and consultation. The applicants were given notice and opportunity to participate in consultations. Therefore, the retrenchment was both substantively...
Source-derived case information.
- Citation
- deodatus ujuma mwanja na mwingine vs shule ya sekondari charlote 2021 tzhcld 148 4 juni 2021
- Parties
- Applicant: Deodatus Ujuma Mwanja; Applicant: Raphael Mapendo Simba; Respondent: Shule ya Sekondari Charlote
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2021
- Procedural Posture
- Labour Revision Application / Judgment
- Outcome
- Application dismissed
- Legal Topics
- Unfair Termination, Retrenchment Procedures, Employment Contracts
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Deodatus Ujuma Mwanja
Applicant
Raphael Mapendo Simba
Applicant
Shule ya Sekondari Charlote
Respondent
Procedural Posture
Labour Revision Application / Judgment
Legal Issues
- 1 Whether the retrenchment of the applicants was substantively and procedurally fair
- 2 Whether proper procedures for retrenchment were followed
- 3 What remedies are available to the parties
Ratio Decidendi
The retrenchment of the applicants was based on valid structural and operational requirements, and the respondent followed the required legal procedures for notice and consultation. The applicants were given notice and opportunity to participate in consultations. Therefore, the retrenchment was both substantively and procedurally fair.
Court Disposition
Application dismissed
Orders
- The decision of the Commission for Mediation and Arbitration remains undisturbed
- Each party to bear its own costs
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DIVISHENI YA KAZI ILIYOKAA MOROGORO MAOMBI YA MAREJEO NA. 43 YA 2020 BAINA YA DEODATUS UJUMA MWANJA............................................... MLETA MAOMBI NA.l RAPHAEL MAPENDO SIMBA.................................................MLETA MAOMBI NA.2 NA SHULE YA SEKONDARI CHARLOTE...............................................MJIBU MAOMBI HUKUMU Tarehe ya mwisho ya Amri: 24/05/2021 Tarehe ya Hukumu: 04/06/2021 A. E. MWIPQPO, J. DEUDATUS UJUMA MWANJA na RAPHAEL MAPENDO SIMBA ambao ni Waleta Maombi katika shauri hili wameleta Maombi haya ya Marejeo wakiiomba Mahakama irekebishe uamuzi wa Tume ya Usuluhishi uliotolewa katika mgogoro wa kikazi Na. RF/CMA/MORO/30/2018 wa tarehe 12/04/2019 na Mhe. KIOBYA, Z., Muamuzi. Waleta maombi wanaomba yafuatayo: 1. Kwamba, Tuzo iliyotolewa na Tume Morogoro katika shauri Na. CMA/MOR/30/2018 ya tarehe 12/02/2019 ina mapungufu makubwa ya kisheria kulingana na kifungu cha 86 (6) (a) (b) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6 ya 2004 pia Kanuni Na. 23 (1) (2) ya Kanuni za Taasisi za Kazi (Usuluhishi na Uamuzi), Tangazo la Serikali Na. 64 la 2007. 2. Kwamba, Ushahidi wa maelezo na vielelezo vya mlalamikiwa mbele ya Tume havikuwa na Uhalali. 3. Kwamba, Tume haikuwa na muda wa kujiridhisha na ushahidi wa vielelezo vya mlalamikiwa kabla ya Uamuzi. 4. Kwamba, Uamuzi wa Tume uliegemea sana upande mmoja. 5. Kwamba, Waleta Maombi wataiomba Mahakama nafuu nyingine yoyote katika maombi haya. Historia fupi ya shauri hili ni kuwa Waleta Maombi waliajiriwa na Charlote Secondary School ambaye ni Mjibu Maombi katika shauri hili katika nafasi ya Ulinzi kwa tarehe tofauti. Mnamo tarehe 02 Januari, 2018 Waleta Maombi walipunguzwa kazini kwa sababu ya kutaka kuboresha muundo wa Taasisi (Structural improvement). Waleta Maombi hawakuridhika na kupunguzwa huko kazi, hivyo walifikisha mgogoro mbele ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (hapa itajulikana kama Tume). Baada ya kuwasikiliza pande zote, Tume iliona kuwa zoezi la upunguzwaji kazi lilikuwa halali (fair) kisababu na kiutaratibu. Maamuzi ya Tume 2 hayakuwaridhisha Waleta maombi na waliamua kufungua shauri hili la marejeo katika Mahakama hii. Wakati wa usikilizwaji wa shauri hili, pande zote mbili zilikuwa zinawakilishwa. Waleta Maombi waliwakilishwa na Bw. Bilali Msaka, Mwakilishi Binafsi na Mjibu Maombi aliwakilishwa na Bw. Benjamin! Jonas, Wakili. Akifanya mawasilisho ya msingi kuunga mkono maombi haya, Mwakilishi Binafsi wa Waleta Maombi alieleza kwamba Waleta Maombi walikuwa wameajiriwa na Mjibu Maombi kama walinzi kwa Mkataba wa mwaka mmoja mmoja. Mikataba hiyo ilidumu kwa zaidi ya mwaka mmoja kabla ya kupunguzwa kazi na Mjibu Maombi. Sababu ya kupunguzwa kazi ni kubinafsishwa kwa idara ya ulinzi ya Mjibu Maombi baada ya kuingia mkataba na kampuni ya ulinzi ya Ruge. Akiendelea kuwasilisha alieleza kuwa upunguzwaji huo haukuwa halali kwa sababu Waleta Maombi walikuwa na mikataba ya muda maalum na ilikuwa imebakia muda mfupi ili mikataba yao ifikie ukomo. Waleta Maombi wanaona kuwa taratibu za sheria ya ajira zilikiukwa kwa kuwa taarifa ya kusitisha ajira yao ilikuwa ya muda mfupi sana wakati ajira zao zilikuwa za muda maalum. Alieleza kuwa Mjibu Maombi alikubali kuwalipa mishahara ya waliyoifanyia kazi na kiinua mgongo. 3 Mwakilishi alieleza ya kwamba Waleta Maombi hawaoni uhalali wa kubinafsishwa shughuli za ulinzi ambapo hadi muda huu hakuna kampuni ya ulinzi inayoendelea kulinda kwa Mjibu Maombi. Pia, utaratibu wa kupunguzwa kazi haukufuatwa kwa sababu hawakuwa wanawakilishwa katika vikao vya majadiliano na Wajumbe kutoka Chama cha Wafanyakazi. Mwakilishi aliyeteuliwa katika kikao cha majadiliano alikuwa ni miongoni mwa wafanyakazi wa Mjibu Maombi hivyo hakuwa katika nafasi ya kutetea maslahi ya watumishi watakaopunguzwa. Hivyo zoezi halikuwa halali na mwakilishi wa wafanyakazi hakuwa na uelewa wa sheria na taratibu za kazi ili kutetea maslahi yao. Baada ya kuachishwa kazi waleta maombi, Mjibu Maombi aliajiri watumishi wengine kuchukua nafasi zao jambo linaloonyesha kuwa kuwapunguza kazi ilikuwa ni sababu tu ya kuwaachisha kazi. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 38(1) (a) (b) (c) (i) (iii) (xi) (v) (d) (i) (ii) (iii) na (2) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Sura ya 366 ya Sheria kama Ilivyorejewa mwaka 2019. Pia ni kinyume cha Kanuni 23 (1) na (2) ya Kanuni za Ajira na Mahusiano Kazini (Kanuni za Utendaji Bora), Tangazo la Serikali Na. 42 la 2007. Hivyo Walete Maombi waliiomba marejeo haya yakubaliwe, Mahakama imwamuru Mjibu Maombi awalipe malipo ya taarifa ya kuachishwa Kazi na fidia ya kuachishwa kazi isivyohalali na uamuzi wa Tume uwekwe pembeni. 4 Akijibu mawasilisho ya Waleta Maombi, Wakili wa Mjibu maombi alieleza kuwa maelezo yaliyotolewa na Mwakilishi Binafsi wa Waleta maombi hayakuwa sehemu ya kiapo chao. Aya ya nne ya kiapo imeeleza mambo ambayo ndio sababu za kuomba Marejeo. Kwa kifupi sababu hizo ni kuwa Tume ilikosea kuruhusu mtu kuwa Mwakilishi Binafsi wa Waleta Maombi isivyo halali, mkataba na kampuni ya ulinzi ulikuwa batili, Tume ilikataa kupokea ushahidi wa Waleta Maombi na kiasi cha malipo ambayo walistahili kulipwa. Hivyo masuala mengine yaliyowasilishwa ambayo hayapo katika kiapo Wakili wa Mjibu Maombi hakuwa amejiandaa nayo na akaomba hoja hizo ambazo sio sehemu ya kiapo cha Waleta Maombi zisingatiwe. Wakili alieleza masuala yote ambayo yamewasilishwa na Waleta Maombi Tume tayari ilishayatolea Uamuzi. Kuhusu uhalali wa sababu za kuachishwa kazi, Tume iliona kuwa sababu hiyo ni halali na ilikuwa na nia ya kuboresha huduma na ufanisi wa kitengo cha Ulinzi. Hivyo sababu ya kuwaachisha kazi ni ya msingi inayoendana na Kanuni ya 23(c) ya Tangazo la Serikali (T.S.) Na. 42 la 2007. Wakili wa Mjibu Maombi alieleza ya kwamba utaratibu wa kuwapunguza kazi chini ya kifungu cha 38(1) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini zilifuatwa. Taarifa ya kuwapunguza kazi ilitolewa mapema, majadiliano yalifanyika, na sababu za kuwapunguza zilitolewa. s Ushahidi uliotolewa ulithibitisha kufuatwa na kuzingatiwa kwa taratibu hizo. Aidha, kulikuwa na makubaliano ya malipo yao. Wafanyakazi wote waliwakilishwa na mwakilishi wao waliyemchagua. Hivyo, hoja la Waleta Maombi haina mashiko. Wakili aliiomba Mahakama ione Marejeo haya hayana mashiko na yatupiliwe mbali (dismissed) kwa kuwa hayana msingi. Akifanya mawasilisho ya nyongeza (rejoinder submission), Mwakilishi wa Waleta Maombi alirudia mawasilisho yao ya msingi. Mjibu Maombi wakati akiwasilisha majibu ya hoja za Waleta Maombi ameibua hoja ya kwamba mawasilisho yaliyofanywa na Waleta Maombi yanatofautiana na hoja za kisheria zilizopo katika kiapo chao. Hata hivyo, ninaona kuwa kilichoandikwa katika Aya 4.2, 4.3 na 4.4 ya kiapo cha Waleta Maombi kwa kiasi kikubwa kinahusiana na mawasilisho yaliyofanywa na Waleta Maombi. Hivyo, Mahakama hii wakati ikifanya uamuzi itaangalia kama katika mawasilisho ya Waleta Maombi kuna hoja zilizowasilishwa nje ya kiapo chao basi hazitapewa uzito. Kutokana na mawasilisho ya pande zote mbili, Mahakama hii inaona hoja za msingi za kutolewa maamuzi ni kama zifuatazo:- i) Iwapo upunguzwaji wa kazi wa Waleta Maombi ulikuwa na sababu na za haki. ii) Iwapo utaratibu wa kuwapunguza kazi ulikuwa halali. iii) Nini nafuu za kila upande? 6 Kifungu cha 37(1) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Sura ya 366 ya Sheria kama Ilivyorejewa mwaka 2019, kinaeleza kuwa itakuwa ni kinyume na sheria kwa mwajiri kumwachisha kazi mwajiriwa isivyo halali. Na uachishwaji kazi utakuwa sio halali iwapo mwajiri atashindwa kuthibitisha kuwa kulikuwa na sababu halali na ya haki ya kumwachisha kazi mwajiriwa na taratibu halali za kumwachisha kazi zilifuatwa. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 37 (2) (a) (b) (c) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Sura ya 366 ya Sheria. Katika kesi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania dhidi ya Andrew Mapunda, Marejeo Na. 104 ya 2014, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, iliyokaa Dar Es Salaam, Mahakama hii ilkuwa na mtazamo kuwa ni kanuni ya kisheria kwamba ili uachishwaji kazi uweze kuchukuliwa ni wa haki unatakiwa utokane na sababu halali na taratibu za haki za uachishwaji kazi. Tukianza na hoja ya kwanza iwapo sababu ya kuwaachisha kazi Waleta Maombi ilikuwa halali na ya haki, kifungu cha 37(2) (a) (b) (iii) kinaeleza kuwa ili uachishaji kazi huo uwe halali ni lazima mwajiri athibitishe kuwa sababu za kumwachisha kazi zilikuwa halali na za haki zinatokana na mahitaji ya kiuendeshaji ya mwajiri. Sheria tajwa hapo juu inasomwa pamoja na Kanuni ya 23 (1) na (2) ya Kanuni za Ajira na Mahusiano Kazini (Kanuni za Utendaji Bora), Tangazo la Serikali Na. 42 la 7 2007. Kanuni ya 23(2) inaeleza mazingira ambayo ya mahitaji ya kiutendaji ambayo yanaweza kujenga msingi wa kuachisha kazi. Kanuni hiyo inaeleza kuwa, nanukuu:- '23.-(2) Kama kanuni ya jumia, mazingira ambayo yanaweza kujenga msingi wa kuachisha kazi kihaiaii ni - a) Mahitaji ya kiuchumi ambayo yanahusiana na usimamizi wa fedha za kampuni; b) Mahitaji ya kiteknoiojia ambayo yanahusu utumiaji wa teknoiojia mpya ambayo inaathiri mahusiano ya kikazi ama kwa kufanya kazi ziiizopo kutohitajika au kwa kuwataka wafanyakazi wajirekebishe na kuendana na teknoiojia mpya au marekebisho ya mahaia pa kazi. c) Mahitaji ya kimuundo ambayo yanatokana na marekebisho ya kibiashara kutokana na sababu mbaiimbaii zinazohusiana na biashara kama vile kuunganisha boashara, kubadiii aina ya biashara, njia za kufanya kazi zenye ufanisi Zaidi, kuhamisha biashara au sehemu ya biashara." Katika kesi ya Bakari Athumani Mtandika dhidi ya Superdoll trailer Ltd, Maombi ya Marejeo Na. 171 of 2013, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, iliyokaa Dar Es Salaam, Mahakama ilieleza kwamba jukumu la mfanya maamuzi katika mgogoro wa uachishwaji kazi usio halali kwa mahitaji ya kiutendaji inabidi mojawapo ya hoja ya kuamuliwa itakayotengenezwa iwe iwapo mahitaji ya kiutendaji ni sababu halisi ya kuhalalisha uachishwaji kazi na sio ni kisingizio. Katika maombi haya sababu ya upunguzwaji kazi kwa Waleta Maombi ni maboresho au kuongeza ufanisi katika vitengo mbaiimbaii ikiwepo 8 kitengo cha Ulinzi kwa kubinafsisha kwa kampuni binafsi kama ilivyoelezwa katika tangazo la upunguzaji kazi (notice of retrenchment) - Kielelezo MKW1 na muhtasari wa kikao kikao ambacho kilifanyika tarehe 28/11/2018 ambacho ni Kielelezo MKW2. Sababu hiyo inaangukia katika kanuni ya 23(2) (c) ya Tangazo la Serikali Na. 42 la 2007. Ushahidi wa DW1 unaonesha kuwa Waleta Maombi walipunguzwa kazi kutokana na nia ya Mjibu Maombi kuboresha huduma na ufanisi Zaidi katika kitengo cha ulinzi na vitengo vya jikoni na mazingira. Hivyo aliamua kutafuta kampuni ya ulinzi kusimamia ulinzi na pale inapofanya vibaya kampuni hiyo itawajibika. Na kwa sababu hiyo Waleta Maombi walipunguzwa kazi. Sababu hit inatosha kuthibitisha kuwa uachishwaji kazi wa Waleta Maombi ni mahitaji ya kimuundo ambayo yanatokana na marekebisho ya njia za kufanya kazi zenye ufanisi zaidi. Waleta Maombi walieleza kwamba kulikuwa hakuna Kampuni iliyopewa mkataba wa kulinda kwa Mjibu Maombi na kuwa walitumia Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (Tukururu) kuchunguza suala hilo. Hata hivyo madai haya hayakuweza kuungwa mkono na ushahidi mwingine wowote. Hivyo, ni maoni yangu kuwa ushahidi huo wa Mjibu Maombi ulikuwa unathibitisha kwamba sababu za kuwaachisha kazi waleta Maombi ni halali. 9 Hoja ya pili ya kuamuliwa ni iwapo taratibu za kuwapunguza kazi Waleta Maombi zilikuwa halali. Kifungu cha 37(2) (c) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Sura ya 366 ya Sheria, kinaeleza kuwa uachishwaji kazi utakuwa sio halali iwapo mwajiri atashindwa kuthibitisha kuwa taratibu za kumwachisha kazi mwajiriwa zilikuwa halali. Taratibu za kufuatwa wakati wa kumwachisha kazi mwajiriwa kwa mahitaji ya kiutendaji zinapatikana katika kifungu cha 38(1) cha sheria hiyo. Kifungu hicho kinaeleza kuwa mwajiri anatakiwa kutoa taarifa ya nia yake ya kupunguza wafanyakazi mapema kadli ilivyopangwa au kudhamiliwa, kutoa taarifa muhimu za upunguzwaji wafanyakazi kunakotarajiwa kufanyika kwa madhumuni ya majadiliano, kushauriana na wafanyakazi kabla ya upunguzwaji wa wafanyakazi na kutoa taarifa, kuweka wazi na kujadiliana na chama cha wafanyakazi cha mahala pa kazi au waajiriwa ambao hawana uwakilishi wa chama cha wafanyakazi. Waleta maombi walieleza kuwa utaratibu wa kuwaachisha kazi haukufuatwa kwa sababu hawakuwa wanawakilishwa katika vikao vya majadiliano na Wajumbe kutoka Chama cha Wafanyakazi na mwakilishi aliyeteuliwa katika kikao cha majadiliano alikuwa ni miongoni mwa wafanyakazi wa Mjibu Maombi hivyo hakuwa katika nafasi ya kutetea maslahi ya watumishi watakaopunguzwa. Hata hivyo DW2 ambaye ni mmoja ya wafanyakazi waliopunguzwa ameeleza kuwa walipewa tangazo io la kuhudhuria kikao cha kujadili upunguzwaji kazi mnamo tarehe 28/11/2017 na yeye ndiye alitia saini kumbukumbu za kikao kwa niaba ya wafanyakazi. Muhtasari wa Mkutano wa tarehe 28/11/2017 - kielelezo MKW2 unaonesha mojawapo ya agenda zilizojadiliwa ni upunguzwaji wa wafanyakazi , mafao watakayolipwa na sababu za upunguzwaji ambayo ni kubinafsisha wa baadhi ya idara. Aidha, waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Mleta Maombi Namba mbili ambaye katika ushahidi wake mbele ya tume alisema kuwa hakuhudhuria kikao hicho. Aidha, muhtasari huo unaonesha kuwa Mleta Maombi namba moja hakuhudhuria na katika ushahidi wake ameeleza kuwa hakuhudhuria sababu siku hiyo hakuwa zamu na kesho yake alipewa taarifa ya kilichojiri katika mkutano huo. Ni maoni yangu kuwa ushahidi huo unathibitisha kuwa Waleta Maombi walipewa taarifa ya kikao cha upunguzwaji kazi kilichofanyika tarehe 28/11/2018 hivyo ilikuwa ni wajibu wao kuhudhuria. Aidha, kielelezo MKW2 kinaonesha kuwa Mleta Maombi Na. 2 alihudhuria. Na muhtasari huo unaonesha kuwa majadiliano yalifanyika kama sheria inavyotaka. Kwa sababu hiyo naona ushahidi uliotolewa unathibitisha kuwa upunguzwaji kazi wa waleta maombi ulikuwa halali. ii Kwa sababu hiyo, mahakama hii inatupilia maombi haya. Uamuzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi utaendelea kubakia kama ulivyoamriwa. Kila upande utajigharamia gharama zake za kuendesha shauri hili. 04/06/2021 12