diana c ngalomba vs crdb bank plc 2022 tzhcld 1081 9 novemba 2022
The respondent proved valid reasons for termination and followed all statutory disciplinary procedures. The applicant was heard on the relevant charges, and the CMA's decision was correct. There was no procedural or substantive unfairness.
Source-derived case information.
- Citation
- diana c ngalomba vs crdb bank plc 2022 tzhcld 1081 9 novemba 2022
- Parties
- Applicant: Diana C. Ngalomba; Respondent: CRDB Bank PLC
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2022
- Procedural Posture
- Labour Revision / Final Judgment
- Outcome
- application dismissed
- Legal Topics
- Unfair Termination, Disciplinary Procedures, Burden of Proof, Right to Be Heard
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Diana C. Ngalomba
Applicant
CRDB Bank PLC
Respondent
Procedural Posture
Labour Revision / Final Judgment
Legal Issues
- 1 Whether the Commission for Mediation and Arbitration (CMA) properly evaluated evidence from both parties
- 2 Whether the applicant was heard on the charges leading to termination
- 3 Whether the employer followed proper disciplinary procedures
Ratio Decidendi
The respondent proved valid reasons for termination and followed all statutory disciplinary procedures. The applicant was heard on the relevant charges, and the CMA's decision was correct. There was no procedural or substantive unfairness.
Court Disposition
application dismissed
Orders
- Application for revision dismissed
- CMA award upheld
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
KATIKA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA DIVISHENI YA KAZI PAR ES SALAAM MAREJEO NA. 212 YA MWAKA 2022 (yatokanayo na maamuzi ya Mgogoro wa Kikazi Na. CMA/DSM/KIN/714/20/15/21/ mbele ya Mhe. Willbard G.M. Muamuzi) DIANA C. NGALOMBA......................................................... MLETA MAOMBI DHIDI YA CRDB BANK PLC................................................................. MJIBU MAOMBI HUKUMU S, M, MAGHIMBI, J: Hukumu hii inatokana na maombi yaliyoletwa na Mleta Maombi chini ya kifungu cha 91(l)(b), 91(2)(b) & 94(l)(b)(i) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Sura ya 366, iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019 ("Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini"), pamoja na Kanuni ya 24(1), 24(2)(a) (b) (c) (d) (e) (f), 24(3)(a) (b) (c) (d), 28(l)(c) (d) (e) ya Kanuni za Mahakama ya Kazi, Tangazo la Serikali Na. 106 ya mwaka 2007. Katika Taarifa yake ya maombi, mleta maombi ameleta maombi haya akiiomba Mahakama hii kutoa amri zifuatazo:- i. Kwamba mahakama hii iitishe jalada, kurejea mwenendo wa shauri na hatimaye kubatilisha na/au kurekebisha maamuzi yaliyotolewa na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Dar es salaam katika mgogoro wa Kazi Na. CMA/DSM/KIN/714/20/15/21 i yaliyotolewa na Mh. Wilbard G.M, Muamuzi mnamo tarehe 24/05/2022. ii. Amri zingine zozote Mahakama itakavyoona inafaa kwa mujibu wa sheria. Kiini cha mgogoro huu kimetokana na uvunjaji wa Mkataba wa Ajira wa Mleta maombi uliovunjwa na Mjibu Maombi. Kwa mujibu wa rekodi zilizopo, mahusiano kati ya wadaawa yalianza mnamo tarehe 17/09/2013 pale ambapo mleta maombi aliajiriwa na mjibu maombi kama afisa wa Benki. Mleta maombi aliaachishwa kazi na mjibu maombi/muajiri kwa kosa la uzembe uliokithiri mnamo tarehe 29/04/2020. Kutokana na kutoridhika na kuachishwa kazi, Mleta maombi aliawasilisha mgogoro wa kazi mbele ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi wilaya ya Ubungo ("Tume") ambao ulipokelewa na kusajiliwa kama Mgogoro wa kazi Na. CMA/DSM/KIN/714/20/15/21 akipinga uachishwaji kazi usio halali. Baada ya kusikiliza Ushahidi wa pande zote mbili Tume ilifikia maamuzi kuwa uachishwaji kazi katika shauri hili ulikuwa halali hivyo madai ya mleta maombi likatupiliwa mbali. Uamuzi wa Tume ulitolewa tarehe 24/05/2022. Mleta maombi hakuridhika na maamuzi ya Tume, 2 hivyo amewasilisha maombi haya akipinga maamuzi ya Tume kutokana na sababu zifuatazo: - i. Kwamba Tume imetumia mamlaka iliyopewa isivyo halali na kinyume cha sheria. ii. Kwamba, kumekuwa na makosa ya dhahiri ya kisheria ndani ya Tuzo ya Tume yaliyopelekea kuminywa kwa haki ya muombaji. Pamoja na hoja hizo, mleta maombi anaiomba mahakama itatue maswali ya kisheria yafuatayo:- i. Je, Tume ilijielekeza vyema kisheria katika kupima uzito wa ushahidi uliotolewa na pande zote mbili na hatimae kupata majibu sahihi kulingana na viini vya mgogoro? ii. Je, Tume ilikuwa sahihi au la kutozingatia Ushahidi uliotolewa na muombaji halali iliyopelekea Tuzo kukosa ubora unaotakiwa kwa mujibu wa sheria. iii. Je, Tume ilikuwa sahihi kisheria au la kutozitolea maamuzi hoja zote zilizowasilishwa na muombaji katika hoja zake za mwisho (final submission) hivyo kuacha hoja hizo bila majibu ya kisheria. iv. Je, Tume ilikuwa sahihi kisheria au la kwa kuamua kuwa muombaji alisikilizwa katika kosa la kufungua akaunti ya uongo (fictitious 3 account) kwa niaba ya kumrubuni mjubu maombi na hivyo kuwa sababu tosha kwa mjibu maombi kumuachisha kazi muombaji? v. Je, Tume ilikuwa sahihi au la kwa kuyachukulia makosa mawili ya uzembe uliokithiri (gross negligence) na kufungua akaunti ya uongo kwa nia ya kumrubuni mwajiri (opening of fictitious account with intention to defraud the bank) kuwa ni kosa moja? Shauri hili liliendeshwa kwa njia ya maandishi. Mbele ya Mahakama hii mleta maombi aliwakilishwa na wakili Litete Haji Ndugo ilihali mjibu maombi aliwakilishwa na wakili Juvenalis Ngowi. Katika swali la kwanza wakili Ndungo alieleza kuwa muamuzi hakijuielekeza vyema katika kupima uzito wa ushahidi uliotolewa na pande zote mbili ili kuamua mgogoro kwa mujibu wa sheria. Alieleza kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 39 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, ni jukumu la mwajiri kuthibitisha kuwa alimuachisha kazi kihalali mwajiriwa lakini muamuzi alijielekeza vibaya kwa kuhamisha jukumu hilo kwa mleta maombi ambaye ni mfanyakazi. Aliongeza kuwa katika ukurasa wa 7 mstari wa kwanza katika Tuzo Tume imehamisha jukumu la kuthibitisha kama msimamizi wa mleta maombi bado yupo kazini jambo ambalo ni kinyume na kifungu kilichonukuliwa. 4 Wakili Ndugo aliendela kueleza kuwa mjibu maombi alishindwa kuthibitisha ni kwa namna gani mleta maombi alihusika katika kufungua akaunti ya mtu feki kwa nia ya kuitapeli taasisi kwa maslahi yake. Kwamba, katika taarifa ya uchunguzi (kielelezo Cll) mjibu maombi amewataja wahusika wa wizi na namna walivyofaidika na wizi huo lakini jina la mleta maombi halikutajwa huko hivyo ni wazi kuwa hakushiriki katika wizi huo. Iliongezwa kuwa mjibu maombi alishindwa kuthibitisha kuwa jukumu la kufungua akaunti ni la mleta maombi kwani mleta maombi alieleza kuwa jukumu lake mteja anapotaka kufungua akaunti ni kukagua nyaraka, kuzituma kwenye mfumo kisha kuzituma kwa msimamizi wake aliyekuwa ni Bi. Happy Mwakitalu. Wakili alisistiza kuwa aliyeruhusu kufunguliwa kwa akaunti husika ni msimamizi wa mleta maombi alietajwa hapo juu lakini chakushangaza msimamizi huyo hakuchukuliwa hatua yoyote kwa uzembe husika. Kuhusu swali la pili na la tatu wakili Ndungo alieleza kuwa mleta maombi alifukuzwa kwa kosa ambalo uchunguzi ulikuwa ukiendelea polisi kama ambavyo imeelezwa katika kielelezo Cll. Alieleza kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 37(5) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini imezuiliwa mfanyakazi kuchukuliwa hatua za kinidhamu endapo kuna kesi ya jinai imeripotiwa katika kituo cha polisi nab ado ipo katika 5 uchunguzi. Aliongeza kuwa hayo yameamuriwa pia katika kesi ya Stella Manyahi & another Vs. Shirika la Posta, Reference No. 2 of 2010 [2013] LCCD 1. Kuhusiana na taratibu za kuachishwa kazi, wakili Ndungo alieleza kuwa mbele ya Tume kulikuwa na hoja kuwa mjibu maombi hakufuata taratibu ya kumsimamisha kazi (suspension) kwanza mleta maombi ili kupisha uchunguzi lakini hoja hiyo haikujibiwa na Tume. Aliongeza kuwa muamuzi hakufanya uchambuzi wa taratibu za kuachishwa kazi kama zilivyoainishwa katika Kanuni ya 13 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini (Kanuni za Utendaji Bora) Tangazo la Serikali Na. 42 la mwaka 2007 ("Kanuni za Utendaji Bora"). Akijibu swali la nne na la tano wakili Ndungo alieleza kuwa mleta maombi hakusikilizwa kwa kosa alilofukuzwa nalo kazi ambalo ni kuwezesha ufunguaji wa akaunti Na. 0152462132400 kwa mteja kivuli kwa nia ya kumtapeli mwajiri. Alifafanua kuwa mleta maombi alisikilizwa kwa kosa la ukiukaji wa utaratibu wa kufungua akaunti, yaani uzembe uliokithiri (gross negligence). Alisema kuwa chakushangaza muamuzi aliyaona makosa yote mawili tajwa ni kosa moja jambo ambalo ni kinyume na sheria. Hivyo basi kwakuwa mleta maombi alifukuzwa kwa kosa ambalo hakusikilizwa, alisema Wakili Ndungo, ni wazi kuwa 6 alinyimwa haki ya kusikilizwa jambo ambalo ni kinyume na haki za binadamu kama ambavyo imeamuriwa katika kesi ya Gideo Robert Mbalase Vs. Researchers Academicians and Allied Workers Union (RAAWU) and Prof. Kilo F.S Hamza, Misc. Application No. 313 ya mwaka [2015] LCCD 1. Mwisho kabisa wakili alimalizia kwa kuiomba mahakama ibatilishe maamuzi ya Tume kwakuwa hayakuzingatia hoja zote zilizojadiliwa hapo juu. Akijibu hoja ya kwanza wakili Hassan alieleza kuwa hoja hiyo haina mashiko kwakuwa jukumu la kuthibitisha kama mleta maombi aliachishwa kazi kihalali lilikuwa la mjibu maombi na alikamilisha jukumu hilo mbele ya Tume. Kwamba kwa ushahidi uliotolewa mjibu maombi alithibitisha kikamilifu kuwa mleta maombi alifanya uzembe uliokithiri kwa kupokea nyaraka za kughushi na kufungua akaunti feki iliyopelekea kuipatia benki hasara ya takribani shilingi milioni mia tatu sabini na mbili elfu na laki mbili arobaini na saba elfu. Iliendela kuelezwa kuwa ilikuwa ni jukumu la wadaawa kujikita katika hoja bishaniwa mbele ya Tume hivyo, suala la msimamizi wa mleta maombi kuwepo au kutokuwepo ofisini haikuwa hoja ya msingi ya kujadiliwa mbele ya Tume lakini hata hivyo hoja hiyo ilijibiwa. 7 Wakili Hassan aliendelea kueleza kuwa mleta maombi ameibua hoja kuwa kielelezo Cll hakijamtaja lakini hoja hiyo haikuibuliwa mbele ya Tume hivyo hakutakiwa kuiibua katika mahakama hii. Katika kutilia mkazo mawasilisho yake, wakili alirejea maamuzi mbalimbali ikiwemo kesi ya Mahakama ya Rufani ya Paulina Samson Ndawavya Vs. Theresia Thomas Madaha, Civil Appeal No. 45 of 2017 ambako iliamriwa hoja ambayo haikuibuliwa wakati wa usikilizwaji kesi haiwezi kuibuliwa katika hatua hii. Wakili aliongeza kuwa katika kielelezo Cll, ni dhahiri mleta maombi alikiri kuwa alishindwa kukagua kwa makini nyaraka alizopokea ambazo zilikuwa za kughushi hivyo ni wazi kuwa alikuwa mzembe. Kuhusu hoja ya endapo jukumu la kufungua akaunti lilikuwa la mleta maombi, wakili Hassan alieleza kuwa kwa kuzingatia Ushahidi uliotolewa na mjibu maombi, jambo hilo limeweza kuthibitishwa. Kuhusu hoja ya pili na ya tatu Wakili Hassan alieleza kuwa mleta maombi ameshindwa kutoa Ushahidi kuwa kesi husika ilifunguliwa katika kituo cha polisi hivyo hoja hiyo haina mashiko kwakuwa haina uthibitisho wowote. Alisisitiza kuwa kosa ambalo mleta maombi alifukuzwa nalo kazi ndilo hilohilo alilosikilizwa katika kikao cha nidhamu hivyo ya kuwa haku hakupewa haki ya kusikilizwa haina mashiko. 8 Kuhusu mjibu hoja ya kutoanza na hatua ya kumsimamisha kazi mleta maombi wakili Hassan alieleza kuwa hoja hiyo haina mashiko kwakuwa mjibu maombi alifuata utaratibu wa kuachisha kazi ulioanishwa katika Kanuni ya 13 ya Kanuni za Utendaji Bora. Aliongeza kuwa Sheria za kazi hazimlazimu mwajiri kumsimamisha kazi mwajiriwa wakati wa uchunguzi kama ilivyoelezwa katika Kanuni ya 27(1) ya Kanuni za Utendaji Bora. Pia wakili alisisitiza kuwa hoja ya kuwa mleta maombi hakusimamishwa kazi wakati wa uchunguzi na kuwa alifukuzwa wakati kesi ikiendelea polisi hazina mashiko kwakuwa ziliibuliwa tu wakati wa majumuisho na sio wakati wa kusikiliza Ushahidi mbele ya Tume hivyo haziwezi kuibiliwa katika hatua hii ya marejeo kama ilivyoamuriwa katika kesi ya Jeremiah Issangaya na wenzanke dhidi ya Malaki Longosua, Miscellaneous Land Application No. 17 of 2020. Wakili Hassan alipinga vikali mawasilisho ya mleta maombi kuwa Tume haikujadili taratibu za kuachisha kazi alisisitiza kuwa Tume ilijadili hoja hiyo kama ambavyo inaonekana katika ukurasa wa 8 wa Tuzo. alieleza kuwa Tuzo imefuata matakwa ya kisheria. Kuhusu hoja ya nne na ya tano wakili Hassan alieleza kuwa mleta maombi alisikilizwa kwenye kikao cha nidhamu kwa kosa alilofukuzwa 9 nalo kama inavyothibitishwa katika muhtasari wa kikao cha nidhamu (kielelezo C14) pamoja na barua ya kuachishwa kazi (kielelezo C6). Mwisho kabisa aliiomba mahakama itupilie mbali maombi hay ana kuthibitisha maamuzi ya Tume. Baada ya kupitia mawasilisho ya pande zote mbili Mahakama inaona ya kuwa inatakiwa kuchambua na kutoa ufumbuzi kwenye hoja zifuatazo; endapo mjubu maombi alikuwa na sababu ya msingi ya kumuachisha kazi mleta maombi, endapo mjibu maombi alifuata taratibu za kumuachisha kazi mleta maombi na nini nafuu ya pande zote mbili. Katika hoja ya kwanza kama kulikuwa na sababu ya msingi ya kumuachisha kazi mleta maombi, ni matakwa ya sheria kwa mujibu wa kifungu cha 37 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini kuwa mwajiri anatakiwa kumwachisha kazi mwajiriwa endapo anasababu za msingi na amefuata taraibu zilizopo za kumuachisha kazi. Hayo yamezaliwa kutoka kwenye mkataba wa Kimataifa wa Shirika la kazi duniani yaani inayohusiana na usitishwaji/uvunjwaji wa Mikataba ya Ajira, yaani "ILO Convention on Termination of Employment, 1982 (No. 158)" ambayo imebatilisha muajiri kusitisha mkataba wa ajira wa muajiriwa kama hakuna sababu za msingi zinazohusiana na uwezo au utendaji kazi wa muajiwa, au matakwa ya kimuundo/kiutendaji "operational io requirement". Katika shauri hili mleta maombi alifukuzwa kazi kwa sababu ifuatayo kama ambavyo imeandikwa katika barua ya kufukuzwa kazi (kielelezo C6): - '"That on 03rd October, 2019 while working as a Bank Officer at Mbezi Branch you facilitated opening of account number 0150462132400 to a fictitious customer with the intention to defraud the bank. The said process was not supported by the required valid documents thus, facilitated fraudulent transaction to be perpetuated causing financial loss to the Bank of Tanzania Shillings of Three Hundred Seventy - Two Million, Two Hundred and Forty - Seven Thousand (TZS 372,247,000.00)". Kwa tafsiri isiyo rasmi kosa nukuliwa hapo juu linaweza kutafsiriwa kama ifuatavyo:- "Kwamba tarehe 03 Oktoba, 2019 wakati unafanya kazi kama Afisa wa Benki katika Tawi ia Mbezi uliwezesha kufunguliwa kwa akaunti namba 0150462132400 kwa mteja wa uongo kwa nia ya kuilaghai benki. Mchakato huo haukuungwa mkono na nyaraka halali zinazotakiwa hivyo, kuwezesha miamala ya udanganyifu kuendelezwa na kusababisha hasara ya kifedha ii kwa Benki Kuu ya Tanzania Shiiingi Mia Tatu Sabini - Miiioni Mbiii, Mia Mbiii na Arobaini - Eifu Saba (TZS 372,247,000.00)". Kama ilivyoelezwa hapo juu kosa alilofanya mleta maombi ni kuwa alisaidia ufunguzi wa akaunti tajwa hapo juu. Mleta maombi amepinga vikali kushiriki katika zoezi hilo na kwamba mjibu maombi hajathibitisha kama lilikuwa ni jukumu lake kufungua akaunti husika. Katika maelezo yake wakati wa uchunguzi (kielelezo CIO) mleta maombi alieleza wazi kuwa moja ya majukumu yake ni kufungua akaunti. Kuhusu akanti husika mleta maombi alikiri kuwa katika tarehe tajwa mteja mwenye jina la Anzerani alifika sehemu yake ya kazi na kumkabidhi nyaraka za zinazotakiwa kwaajili ya kufungulia akaunti. Kwamba alizipokea nyaraka husika na kuziona ziko sawa. Kuhusu kufanya uchunguzi BRELA, Mleta maombi alieleza kuwa hakufanya hivyo kwakuwa aliamini msimamizi wake angefanya hivyo kwakuwa kazi yake ilikuwa ni kupokea nyaraka tu. Utetezi huo wa mleta maombi hauna mantiki, ni wazi kuwa kwakuwa yeye ni mtu wa kwanza kupokea nyaraka za mteja husika ,alitakiwa kuzikagua na kuhakiki kama ni sahihi lakini hakufanya hivyo. Katika jalada la nyaraka (kielelezo C8) kuna makosa ya wazi kabisa ambayo mleta maombi angekuwa makini angeweza kuyabaini. Katika leseni ya biashara nambari ya ushuru wa 12 mapato ni 137-557-746 wakati katika hati ya ushuru wa mapato namba iliyoandikwa ni 136-557-246. Lakini hata hivyo katika kielelezo CIO mleta maombi amekiri kuwa hakufanya uchunguzi BRELA jambo ambalo si sahihi. Maelezo hayo yanaonesha wazi kuwa mleta maombi alikuwa mzembe katika kufungua akaunti husika ambayo ilimsababishia haasara muajiri wake. Hivyo mjibu maombi aliweza kuthibitisha kosa la mleta maombi. Hata muhutasari wa kikao cha nidhamu (kielelezo C4) unaonesha kuwa wakati wa kusikiliza shauri la mleta maombi, mjibu maombi alipeleka Ushahidi wa kuthibitisha kosa alilofanya mleta maombi. Mahakama imezingatia mawasilisho ya mleta maombi kuwa muamuzi alimpa jukumu la kuthibitisha kama aliachishwa kazi kihalali. Madai hayo sio ya kweli kwakuwa hakuna mahali katika Tuzo muamuzi ameeleza hayo, na wala rekodi hazionyeshi kuwa jukumu hilo lilihama. Hivyo basi, kwa Ushahidi uliopo kwenye rekodi zilizoletwa mbeye ya Mahakam hii, ni wazi kuwa mjibu maombi alithibitisha shtaka dhidi ya mleta maombi. Mahakama hii inaungana mkono na maamuzi ya Tume kuwa mjibu maombi alikuwa na sababu za msingi za kumuachisha kazi mleta maombi. 13 Katika hoja ya pili mahakama inajiuliza kama mjibu maombi alifuata taratibu za kumuachisha kazi mleta maombi. Kama ilivyoelezwa hapo awali, mleta maombi alifukuzwa kazi kwa kosa la utovu wa nidhamu. Taratibu za kufuata katika kosa hilo zimeainishwa katika Kanuni ya 13 ya Kanuni za Utendaji Bora. Mleta maombi anaeleza kuwa taratibu ya kwanza iliyokiukwa na mjibu maombi ni kuwa hakumsimamisha kazi mleta maombi wakati wa uchunguzi. Kama ilivyoelezwa na wakili Hassan hakuna sharia wala kanuni yoyote ya kazi na ajira inayomlazimisha muajiri kumsimamisha kazi muajiriwa endapo uchunguzi unaendelea. Mwajiri anahaki ya kuangalia mazingira ya kazi kama yanamlazimu kumsimamisha mwajiriwa au la. Katika shauri hili mjibu maombi hakuona ulazima wa mleta maombi kusimamishwa kazi kwakuwa hakuathiri chochote katika uchunguzi huo hivyo madai ya kuwa utaratibu huo ulikiukwa hayana mantiki. Mleta maombi anadai pia kuwa alifukuzwa kazi kwa kosa ambalo hakusikilizwa katika kikao cha nidhamu. Nimeangalia rekodi zilizopo na katika wito wa kuhudhuria kikao cha nidhamu (kielelezo C3) mleta maombi alielezwa kuwa anaitwa katika kikao hicho kwa tuhuma ambazo aliambiwa ajielezee na ni baada ya maelezo yake kutojitosheleza ndipo alisitishiwa ajira. Katika barua ya tuhuma (kielelezo Cl), mleta maombi 14 alituhumiwa kwa kosa la uzembe uliokithiri na maelezo ya kosa hilo yalikuwa kama ifuatavyo:- "(9/7 03rd October, 2019 while working as a Bank Officer at Mbezi Branch you facilitated opening of account number 0150462132400 to a fictitious customer with the intention to defraud the bank. The said process was not supported by the required valid documents. This facilitated fraudulent transactions, causing of financial loss to the Bank of Tanzania Shillings of Three Hundred Seventy - Two Million, Two Hundred and Forty - Seven Thousand (TZS 372,247,000.00)". Ni wazi kuwa maelezo hayo ya kosa ni sawa na yale yaliyoandikwa katika barua ya kuachishwa kazi ambayo tayari imeshatafsiriwa hapo juu. Hivyo baso madai ya kuwa mleta maombi hakusikilizwa kwa kosa ambalo ameachishwa kazi mahakama inaona ni kinyume na Ushahidi uliopo mbele ya mahakama hii. Kwakusema hayo mahakama inaona kesi alizorejea wakili Ndungo zinazohusiana na haki ya kusikilizwa hazina mantiki katika shauri hili kwakuwa mleta maombi alipewa kikamilifu haki ya kusikilizwa. Mahakama imepitia pia taratibu nyingine za kufukuzwa kazi kwa kosa la utovu wa nidhamu na imeona kuwa zote zilizingatiwa na mjibu 15 maombi kama ambavyo imeamuriwa na muamuzi. Hivyo mjibu maombi alifuata taratibu za usitishaji wa ajira. Katika hoja ya mwisho mahakama inajiuliza nafuu za kila upande. Kama ilivyoamriwa hapo juu kuwa mjibu maombi alikuwa na sababu za msingi za kusitisha ajira ya mleta maombi na alifuata taratibu zinazotakiwa. Hivyo basi, mleta maombi hastahili malipo yoyote kwakuwa wakati anaachishwa kazi alilipwa stahiki zake zote kama ambavyo imeainishwa katika kielelezo C7. Mahakama inaona maombi haya hayana mantiki hivyo basi yanatupiliwa mbali. Imesainiwa leo Tarehe 9 Mwezi Novemba, Mwaka 2022 16