dolphin filaments t limited vs janeth muro 4 others 2022 tzhcld 1087 12 december 2022
The applicant failed to prove that the termination was due to genuine retrenchment and did not follow the required legal procedures. Evidence from one respondent was sufficient as the claims were identical. The application for revision lacked merit and was dismissed.
Source-derived case information.
- Citation
- dolphin filaments t limited vs janeth muro 4 others 2022 tzhcld 1087 12 december 2022
- Parties
- Applicant: Dolphin Filaments (T) Limited; Respondent: Janeth Muro; Respondent: Neema Ally Ramadhani; Respondent: Salma Abdallah Chororo; Respondent: Hamisa Abdallah Maganga; Respondent: Mohamed A. Ngoto
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 12 December 2022
- Procedural Posture
- Labour Revision / Final Judgment
- Outcome
- application dismissed
- Legal Topics
- Unfair Termination, Retrenchment Procedures, Burden of Proof in Termination, Representation in Labour Disputes
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Dolphin Filaments (T) Limited
Applicant
Janeth Muro
Respondent
Neema Ally Ramadhani
Respondent
Salma Abdallah Chororo
Respondent
Hamisa Abdallah Maganga
Respondent
Mohamed A. Ngoto
Respondent
Procedural Posture
Labour Revision / Final Judgment
Legal Issues
- 1 Whether the Commission erred in law and fact by failing to reconcile the evidence from both parties
- 2 Whether the Commission erred by awarding relief based on the testimony of one complainant without individual evidence from all complainants
Ratio Decidendi
The applicant failed to prove that the termination was due to genuine retrenchment and did not follow the required legal procedures. Evidence from one respondent was sufficient as the claims were identical. The application for revision lacked merit and was dismissed.
Court Disposition
application dismissed
Orders
- The application for revision is dismissed.
- The Commission's award stands as is.
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
MAHAKAMA KUU YA TANZANIA DIVISHENI YA KAZI PAR ES SALAAM MAREJEO NA. 204 YA 2022 DOLPHIN FILAMENTS (T) LIMITED.................. MLETA MAOMBI DHIDI YA JANETH MURO............................ MJIBU MAOMBI NAMBA MOJA NEEMA ALLY RAMADHANI......... MJIBU MAOMBI NAMBA MBILI SALMA ABDALLAH CHORORO..... MJIBU MAOMBI NAMBA TATU HAMISA ABDALLAH MAGANGA.... MJIBU MAOMBI NAMBA NNE MOHAMED A. NGOTO................. MJIBU MAOMBI NAMBA TANO (Kutokana na Uamuzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Kanda ya DSM- Temeke) (Mikidadi: Muamuzi) Tarehe 18.05.2022 Katika CMA/DSM/TEM/6/2021/42/2021 HUKUMU 15.11 & 12.12.2022 Rwizile, J Mleta maombi ameleta maombi haya akipinga uamuzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ('Tume'). Ameomba Mahakama kurejea na kutengua uamuzi katika mgogoro wa kikazi Na. CMA/DSM/TEM/6/2021/42/2021 wa tarehe 18.05.2022. Maelezo ya jumla ni kwamba wajibu maombi waliajiriwa na mleta maombi kwa m kata ba wa kudu mu. i Imeelezwa kuwa ajira yao ilisitishwa kwa makubaliano ya pande zote mbili baada ya kampuni kuyumba kiuchumi. Inasemekana kuwa wajibu maombi walilipwa stahiki zao ambazo ni kiinua mgongo, notisi, likizo, siku walizofanya kazi kwa mwezi husika na mkono wa kwakheri. Hata hivyo, makubaliana yaliyotajwa waliyakana na hatimaye walifikisha mgogoro wao mbele ya Tume kwa madai ya fidia ya kuachishwa kazi isivyo halali na baada ya kusikilizwa walishinda tuzo. Mleta maombi hakuridhishwa na maamuzi hayo na hivyo akafikisha maombi ya marejeo katika Mahakama haya. Kama taratibu zinavyoelekeza, maombi haya yameletwa kwa kiapo cha Msami Frank Mduma kwa niaba ya mleta maombi. Kiapo hicho kimeeleza sababu za maombi haya kama ifuatavyo; /. Kwamba muamuzi a/ikosea kwa hoja na sheria kwa kushindwa kuoanisha ushahidi uliotolewa na pande zote husika. ii. Kwamba muamuzi aiikosea kwa hoja na kisheria kwa kutoa tuzo kupitia ushahidi uliotolewa na mlalamikiwa mmoja bila kuzingatia kwamba walalamikiwa walikuwa watano na kila mmoja alitakiwa kutoa ushahidi wake. 2 Mawakili wasomi waliwawakilisha wadaawa. Bi Victoria G. Mgonja kwa niaba ya mleta maombi na Bwana Fortunatus Masurura Maricha kwa niaba ya wajibu maombi. Bi mgonja katika hoja ya kwanza alieleza kuwa ushahidi wa mleta maombi haukuzingatiwa. Alieleza kuwa, katika ushahidi wake Dwl alisema walikubaliana na wajibu maombi kuhusu kuachishwa kazi kama kielelezo D4 kinavyoonyesha. Katika hoja ya pili alisema kuwa hakuna ushahidi ulioonyesha kuwa Pwl alipata nguvu ya kisheria kutoa ushahidi kwa niaba ya wenzake. Katika kuipa nguvu hoja yake alirejea shauri la Shoppers Supermarket v James Anthony & 2 Others, Revision No. 635 of 2019, High Court - Dar es Salaam. Kwa mtazamo wake kila shahidi alitakiwa kutoa ushahidi wake mbele ya Tume. Hivyo aliomba uamuzi wa Tume utenguliwe. Katika kujibu hoja ya kwanza Bwana Maricha aliwasilisha kuwa, mleta maombi alishindwa kuthibitisha kufuata taratibu katika kuwapunguza kazi wajibu maombi kama inavyoelekezwa katika kifungu cha 38cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini [sura ya 366 kama kilivyorejewa mwaka 2019] na kanuni ya 23(4) ya TLS. Na. 42 ya mwaka 2007. Katika kushajihisha hoja yake alirejea shauri la Sharaf Shipping Agency (T) LTD v Bacilia 3 Constantine na wenzake, Civil Appeal Na. 56 ya mwaka 2019, Mahakama ya Rufaa ya Tanzania. Katika hoja ya pili alieleza kuwa katika shauri la Shoppers Supermarket v James Anthony & 2 Others ilielezwa kuhusiana na hoja ya kukosekana kwa ushahidi na sio kila mtu atoe ushahidi. Aliendelea kueleza kuwa Pwl aliruhusiwa na wajibu maombi wengine kuwawakilisha kwa kujaza fomu. Kwa mtazamo wake, Pwl alikuwa na mamlaka ya kutoa ushahidi Katika mawasilisho ya nyongeza, Bi Mgonja alisema kuwa pande zote mbili zilikubaliana kama kielelezo D3 kinavyothibitisha na kuwa fomu iliyojazwa na Pwl ilikuwa ni katika utaratibu wa kufungua shauri na kuweka sahihi nyaraka kwa niaba ya wengine na sio kutoa ushahidi. Baada ya kupitia hoja za pande zote, Mahakama inaona hakuna ubishi < \ ■ ■ kuwa wajibumaombi walikuwa wafanyakazi wa mleta maombi (kielelezo Dl) na kuwa waliachishwa kazi (kielelezo D3). Hata hivyo, kifungu 39 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, kama kilivyorejewa mwaka 2019 kinamtaka mwajiri (mleta maombi) kuthibitisha uachishwaji kazi kwa waajiriwa (wajibu maombi) kuwa ni halali. 4 Katika kupitia ushahidi na vielelezo vilivyotolewa mbele ya Tume, hakuna kielelezo chochote kinachoonyesha kazi za mleta maombi zilipungua, ili kuthibitisha sababu za kuwaachisha kazi wajibu maombi. Kuachisha kazi kwa njia ya Kupunguza wafanyakazi inatakiwa kutokana na sababu mbalimbali. Sababu hizo ni za kiuchumi, kiteknolojia, kimuundo au mambo mengine yanayoendana na hayo kama inavyoelezwa katika kanuni ya 23(1) ya Employment and Labour Relations (Code of Good Practice) TLS. Na. 42 ya mwaka 2007. Katika shauri hili mleta maombi ameeleza kuwa alikuwa na sababu ya kupunguza wafanyakazi ambayo ni upungufu wa kazi. Mahakama imebaini, mleta maombi alitoa ushahidi wa maneno pekee. Hali hiyo imeifanya kuamini kuwa mleta maombi kwa kushindwa kwake kuthibitisha upungufu wa kazi hakuwa na sababu za kupunguza wafanyakazi. Pia katika ushahidi uliotolewa mbele ya Tume hakuna kielelezo chochote kinachonyesha kama taratibu za uachishwaji kazi zilifuatwa kwani pamoja na sababu za kupunguza kazi wafanyakazi lakini pia taratibu za kupunguzwa huko lazima zifuatwe. Kifungu cha 38 cha sheria hii, na kanuni ya 23(4) ya TLS. Na. 42 ya mwaka 2007, vinaeleza taratibu za kufuatwa na mwajiri anapotaka kupunguza wafanyakazi. 5 Taratibu hizo ni kutoa taarifa kwa wafanyakazi juu ya nia ya kupunguza wafanyakazi, kutoa taarifa muhimu katika upunguzaji huo kwa ajili ya majadiliano, kueleza sababu, njia na taratibu pamoja na muda kuhusiana na kupunguza wafanyakazi. Kielelezo D2, kinaonyesha mahudhurio na dhumuni la kikao lakini hakuna sehemu inayoonyesha nini kilijiri, taratibu gani zilifuatwa kufikia maamuzi ya kuwapunguza kazi wajibu maombi na nini makubaliano ya kikao hicho. Kielelezo D3 (barua ya kuachishwa kazi) kinaeleza kuhusiana na makubaliano ya kikao chao cha tarehe 31.12 2020(D2)z lakini muhtasari wenyewe hauonyeshi makubaliano hayo. Kwa rahisi ya rejea: - "YAH: KUACHISHWA KAZI "...Husika na somo tajwa hapo juu, kama tulivyokubaliana katika kikao chetu cha Pamoja tuiichokifanya tarehe 30/12/2020, kuanzia ieo 31/12/2020 utakuwa umeachishwa kazi kutokana upungufu wa kazi..." Kwa kielelezo hicho Mahakama imeona kuwa muamuzi aliweza kuoanisha ushahidi uliotolewa na pande husika. Haya yanathibitika katika aya ya nne ya ukurasa wa 5 wa tuzo: - 6 "...Vile vile mlalamikiwa ameshindwa kuithibitishia Tume kuwa ni kweii uzaiishaji uiipungua maana hakuna kielelezo chochote kilichotolewa mbele ya Tume kuonesha hiio." katika aya ya nne ya ukurasa wa 6 pamoja na aya ya kwanza ukurasa wa saba wa tuzo alisema: - "kifungu cha 38(1) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Sura 366 R.E. 2019 ... Pamoja na kanuni ya 23 ya GN 47/2007 pia kimetoa utaratibu wa kufuata katika kuendesha zoezi la kupunguza kazi wafanyakazi kuwa ni wajibu uiiowekwa kwa waajiri ni wa kiutaratibu na wa kudumu na ni kuruhusu pande zote mbiii yaani mfanyakazi na mwajiri kwa njia ya Pamoja kutatua tatizo na kufikia makubaliano na kufuata taratibu kama niiizoziorodhesha hapo awaii. Hivyo ni wazi walalamikaji waiiachishwa kazipasipo kufuatwa kwa utaratibu wowote kama niiivyoainisha hapo juu." Katika hoja ya pili, hati ya uwakilishi iliyotolewa mbele ya Tume inaonyesha Pwl aliruhusiwa na wajibumaombi wengine kupokea na kuweka sahihi nyaraka zote. Lakini ushahidi unaonyesha kuwa Pwl alitoa ushahidi kwa niaba ya wenzake. Kwenye kesi ya Security Group Tanzania Ltd v Samson Yakobo and 10 Others (Civil Appeal 76 ya mwaka 2016) ukurasa wa 16 na 17 imeeleza kuwa kama wajibu maombi 7 wana mgogoro wa aina moja, ushahidi hauhitaji kutolewa na wote bali unaweza kuthibitishwa na baadhi yao. Kama uamuzi hapo juu unavyooeleza, katika shauri hili pia wajibu maombi walikuwa na mgogoro wa kufanana yaani wa uachishwaji kazi isivyo halali. Na Pwl katika ushahidi wake amethibitisha malalamiko ya wajibu maombi wote kwa kueleza muda wa ajira wa kila mmoja na namna ya uachishwaji kazi wa kila mmoja ulivyofanyika. Hivyo ilitosha kwa Pwl kutoa ushahidi kwa niaba ya wajibu maombi wengine kama alivyofanya. Hoja hii haina mashiko. Kwa sababu zilizobainishwa hapo juu, ni vema na haki, kuyaona maombi haya hayana msingi na hivyo yanatupiliwa mbali. Uamuzi wa Tume unabaki kama ulivyo na, kila upande utajilipia gharama zake. ^c°urt A.K. Rwizile * JUDGE 12.12.2022 8