emmanuel biengo vs seif kaduguda 2023 tzhc 20921 14 august 2023
- Citation
- emmanuel biengo vs seif kaduguda 2023 tzhc 20921 14 august 2023
- Status
- Judgment
- Jurisdiction
- Tanzania
- Court
- TZHC
- Decision
- 14 August 2023
- Posture
- Criminal Appeal / Second Appeal at High Court
- Language
- English
More details
- Court
- TZHC
- Decision
- 14 August 2023
- Posture
- Criminal Appeal / Second Appeal at High Court
- Language
- English
On this page
Professional case brief
Research organized from the available case record
01
Holding and result
The court held that the elements of obtaining money by false pretence under Section 304 of the Penal Code were not proved beyond reasonable doubt. The dispute was contractual and should be resolved through civil proceedings, not criminal prosecution.
Court disposition
appeal dismissed
Orders
- Appeal is dismissed for lack of legal merit.
- Right of further appeal explained to parties.
02
Material facts
Parties
Emmanuel Biengo
AppellantSeif Kaduguda
RespondentAmounts and remedies
- Amount in Dispute: TZS 1,500,000
03
Procedural history
Posture
Criminal Appeal / Second Appeal at High Court
04
Questions and positions
Legal issues
- 01
Whether the elements of obtaining money by false pretence were proved
- 02
Whether the dispute was criminal or civil in nature
- 03
Whether the lower courts erred in law and fact in acquitting the respondent
Party arguments
- Applicant
- The appellant argued that the elements of obtaining money by false pretence were proved as the respondent took TSH 1,500,000 without having a plot to sell, failed to transfer ownership, and did not refund the money. He relied on documentary evidence including the sale agreement and arbitration certificate.
- Respondent
- The respondent argued that the transaction was conducted legally, witnessed by a lawyer, and that the proper remedy for the appellant was a civil claim, not a criminal case.
05
Court’s reasoning
Legal principles
- 01
Penal Code, Section 304
Criminal cases require proof beyond reasonable doubt of all elements of the offence charged.
- 02
Law of Contract Act, Cap 345
Disputes arising from contracts should be resolved under contract law, not criminal law, unless clear criminal intent is established.
06
Ratio, limits and disposition
Ratio decidendi
The court held that the elements of obtaining money by false pretence under Section 304 of the Penal Code were not proved beyond reasonable doubt. The dispute was contractual and should be resolved through civil proceedings, not criminal prosecution.
Obiter and limits
- The appellant is advised to pursue a civil claim for recovery of money or specific performance under the contract.
Court disposition
appeal dismissed
- Appeal is dismissed for lack of legal merit.
- Right of further appeal explained to parties.
Source and reliance status
TZHC · 14 August 2023
This page organises the available record for research. Confirm quotations, current status, and subsequent treatment against the official source before relying on the case.
Judgment reading view
Judgment text
The complete available source text.
TZHC
Judgment· 14 August 2023
KATIKA MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA
KANDA YA TABORA RUFAA YA JINAI NAM BA 2 YA MW AKA 2023 (Imetokana Shauri la Jinai Namba 386 la Mwaka 2022 katika Mahakama ya Mwanzo Mjini Tabora na Rufaa ya jinai namba 1 ya Mwaka 2023 katika Mahakama ya Wiiaya Tabora) EMMANUEL BIENGO........................................ MWOMBA RUFAA
DHIDIYA SEIF KADUGUDA......................................... MJIBU RUFAA
HUKUMU Date: 14/08/2023 & 01/09/2023 BAHATI SALEMA, JAJI: Hii ni rufaa ya pili iliyotokana na Shauri la Jinai Namba 386 la mwaka 2022 katika Mahakama ya Mwanzo Mjini, Tabora ambapo mjibu rufaa Seif Kaduguda alishtakiwa kwa kosa moja la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu dhidi ya kifungu namba 304 cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 iliyorejelewa mwaka 2022. Katika mahakama hiyo, mwomba rufaa Emmanuel Biengo alilalamika kuwa mnamo tarehe 26/10/2021 majira ya saa tisa mchana huko maeneo ya Kata ya Kanyenye Manispaa ya Tabora bila halali na kwa makusudi mjibu rufaa alichukua kiasi cha pesa shilingi milioni moja na laki tano (TSH. 1,500,000) kutoka kwa mwomba rufaa kwa lengo la kumpatia kiwanja lakini hakufanya hivyo huku akijua kuwa ni kosa kisheria. i Mahakama iliweza kusikiliza pande zote mbili na mwisho kufikia uamuzi kwamba, mlalamikaji(mwomba rufaa) ameshindwa kuthibitisha shitaka dhidi ya mshtakiwa(mjibii rufaa) hivyo akaachiliwa huru. Kutokana uamuzi huo, mwomba rufaa hakuridhika hivyo akakata rufaa ya kwanza katika Mahakama ya Wilaya ya Tabora kupitia Shauri la Rufaa Namba 23 la Mwaka 2023. Katika sababu za rufaa alizoziorodhesha mwomba rufaa, sababu kuu ambayo ilibeba sababu zote ilikuwa kwamba shitaka dhidi ya mjibu rufaa lilithibitishwa pasi na kuacha shaka yoyote hivyo Mahakama ya Mwanzo ilipaswa kumtia hatiani. Baada ya pande zote mbili katika rufaa kupata nafasi ya
kuzielezea sababu za rufaa na zile za kupinga rufaa, Hakimu wa Mahakama ya Wilaya alikubaliana na uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Mwanzo kwamba shitaka dhidi ya mjibu rufaa halikuthibitishwa hivyo akaitupilia mbali rufaa hiyo. Kwa mara nyingine tena, Mwomba rufaa hakuridhika na uamuzi uliotupilia mbali rufaa yake hivyo akakata tena rufaa hii akieleza sababu tatu za kutokuridhishwa kama ifuatavyo; 1. Kwamba Hakimu aiikosea kisheria na kimantiki aiipoamua kwamba viini vya kosa la kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu havikuthibitishwa.
2. Kwamba Hakimu aiikosea kisheria na kimantiki kwa kuamua kwamba kosa halikuthibitishwa na ushahidi iihaii hakuzingatia ushahidi wa nyaraka "AA"na "BB"ambazo ni mkataba wa mauzo na had ya usuiuhishi ambazo ziiithibitisha kuwa mjibu rufaa aiipokea Shiiingi 1,500,000/ ingawa hana kiwanja.
3. Kwamba, Hakimu aiikosea kisheria na kimantiki kwa kutokuzingatia ushahidi kwamba mjibu rufaa aiikubaii kuwa 2 alipokea fedha na mpaka sasa ameshindwa kukabidhi kiwanja alichouza au kurudisha pesa hail inayoonyesha kwamba uiikuwa ni utapeli unaostahili adhabu. Tarehe 14/08/2023 rufaa hii ilipoitwa kwa ajili ya kusikilizwa mbele yangu, mwomba rufaa alifika yeye mwenyewe bila ya kuwa na uwakilishi wa kisheria, vivyo hivyo mjibu rufaa naye alikuwa mwenyewe bila uwakilishi wa mwanasheria. Katika mawasilisho yake, mwomba rufaa aliiambia mahakama kuwa viini vya kosa la kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu vilithibitishwa kwa sababu mjibu rufaa alichukua pesa yake bila ya kuwa na kiwanja na hiyo ilithibitishwa na kushindwa kwake kuhamisha umiliki wa kiwanja hicho kupitia Manispaa. Katika sababu ya pili ya rufaa mwomba rufaa alieleza kwamba Baraza la Kata lilithibitisha kuwa mjibu rufaa aliuza kiwanja ambacho tayari kilikuwa na mwenyewe. Kwa kumalizia alieleza kuwa mahakama haikuzingatia ushahidi kwamba mjibu rufaa alipokea pesa lakini mpaka sasa ameshindwa kukabidhi kiwanja au kurudisha pesa. Mwomba rufaa aliiomba mahakama ikubali rufaa yake na kumtia mjibu rufaa hatiani na kisha aamriwe kurudisha pesa pamoja na riba au akabidhi kiwanja. Kwa upande wake mjibu rufaa akipinga sababu za rufaa zilizowasilishwa na mwomba rufaa alieleza kuwa Mahakama haikukosea kwa sababu biashara kati
yao ilifanyika kwa mujibu wa sheria, walienda kwa Mwanasheria ambaye aliletwa na Mwenyekiti wa mtaa na kumtambulisha kwake. Mwisho mjibu rufaa alieleza kuwa Mahakama ilimshauri mwomba rufaa afungue shauri la madai dhidi yake na sio shauri la jinai kama alivyofanya. 3 Mahakama hii kabla ya kuchanganua sababu za rufaa zilizowasilishwa na mwomba rufaa nimeona ni vyema niweke bayana mambo mawili ambayo yalijitokeza wakati wa usikilizaji wa shauri la awali katika Mahakama ya Mwanzo mjini. Kati ya vielelezo vilivyowasilishwa katika mahakama ya mwanzo ni Mkataba wa kuuziana kiwanja (Kielelezo Pl) kati ya mwomba rufaa na mjibu rufaa, mkataba ambao unaonesha ulisainiwa tarehe 26/10/2021 mbele ya wakili wa kujitegemea Bw. A. G Katabazi. Katika mkataba huo kipengele cha tano kinaeieza, nanukuu; 5. KWAMBA, kwa sasa MUUZAJI na MNUNUZI wanakubaliana kama itatokea mgogoro wowote juu ya kiwanja hicho basi sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zitatumika katika utatuzi wake. Pia katika kileiezo "Pl" ndani yake kilijumuisha Cheti cha Usuluhishi wa Mgogoro wa Ardhi kilichotolewa na Baraza la Kata ya Malolo tarehe 13/09/2022. Katika usuluhishi huo wa ardhi uliofanyika baina ya Emmanuel Z. Biyengo(mwomba rufaa) na Damiano Manus Makunga(ambaye siyo mhusika katika shauri hili). Kielelezo kinaonyesha kwamba Baraza la Kata liliweza kupitia vielelezo vilivyowasilishwa mbele yake na kujiridhisha
kwamba Ndugu Damiano Manus Makunga ndiye aliyeidhinishwa na Ofisi ya Ardhi na kupewa hati ya kiwanja ambacho ndicho chenye mgogoro. Kuhusu Seif Rajab aliyeuza kiwanja kwa mwomba rufaa Baraza lilibaini kuwa alikuwa na malalamiko kwa Mkurugenzi kuhusu kupunjwa viwanja na alikuwa bado hajajibiwa lakini akauza kiwanja ambacho hajamilikishwa. Baada ya kuchunguza kwa makini kesi hii, inaonekana wazi kuwa mwomba rufaa alichagua kufungua kesi ya jinai dhidi ya mjibu rufaa 4 jambo ambalo haliendani na masharti ya mkataba. Mkataba baina ya wawili hawa unasema wazi kwamba migogoro inayotokana na mkataba huo inapaswa kutatuliwa kupitia sheria za Tanzania. Katika nchi ya Tanzania sheria inayosimamia mikataba ni Sheria ya Mikataba, Sura ya 345 kwa mantiki hiyo mgogoro uliojitokeza baina ya mwomba rufaa na mjibu rufaa ulipaswa kutatuliwa kwa mujibu wa sheria tajwa hapo juu. Kesi za jinai kwa kawaida zinahusiana na uvunjaji wa sheria za jinai, kama wizi au mashambulizi na siyo njia sahihi ya kutatua migogoro ya kimkataba inayohusiana na haki za mali. Kwa kuwa mkataba baina ya mwomba rufaa na mjibu rufaa ulihusisha umiliki wa ardhi, utaratibu aliouanza mwomba rufaa wa kwenda katika Baraza la Kata ya Malolo kwa ajili ya usuluhishi wa mgogoro wa ardhi ndiyo uliokuwa utaratibu sahihi na kupitia utaratibu huo Baraza la Ardhi lingekuwa katika nafasi nzuri ya kutafsiri Mkataba wao na kisha kueleza
stahiki za haki baina ya wote watakaokuwa wamehusishwa katika shauri hilo. Kifungu cha 304 cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 2022 alichoshitakiwa nacho mjibu rufaa kinaeleza kuwa; 304. Mtu yeyote ambaye, kwa njia yoyote ya hila au udangayifu, anapata kutoka kwa mtu mwingine yeyote kitu chochote ambacho kinaweza kuibiwa au anamshawishi mtu mwingine yeyote kuwasiiisha kwa mtu yeyote kitu chochote ambacho kinaweza kuibiwa au kuiipa au kuwasiiisha kwa mtu yeyote fedha yoyote au bidhaa au kiasi chochote kikubwa cha fedha au idadi kubwa zaidi ya bidhaa kuiiko ambavyo angeiipa kama isingekuwa hi!a au 5 mbinu hiyo, atakuwa anatenda kosa na atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha miaka mitatu." Baada ya kuchunguza kwa makini ushahidi na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani, nakubaliana na maamuzi yaliyotolewa na waheshimiwa Mahakimu wa mahakama zote mbili kwamba viini vya kosa la kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu kama vinavyoelezwa kwenye kifungu cha 304 hapo juu havikuweza kuthibitishwa, hivyo mahakama zote mbili zilikuwa sahihi katika maamuzi yake. Mahakama hii inamshauri mwomba rufaa kufuata njia sahihi ya kisheria ambayo ni kufungua kesi ya madai dhidi ya mjibu rufaa kulingana na masharti ya mkataba. Kupitia njia hiyo mahakama itakuwa na mamlaka ya kuchunguza uhalali wa madai ya mwomba rufaa na kutoa uamuzi kuhusu masuala yanayohusiana na mkataba huo. Baada ya kusema hayo, rufaa hii inatupiliwa mbali kwa kutokuwa na mashiko kisheria. Mahakama: Uamuzi umesomwa/umepokelewa mbele ya mwomba rufaa na mjibu rufaa. A. BAHATI SALEMA
JAJI 01/09/2023 Rufaa: Haki ya rufaa imeelezwa A. BAHATI SALEMA
JAJI 01/09/2023 6
Case-aware research
Ask AI about this case
The judgment and available research above are public. New questions open in a separate private conversation grounded in this case.