EMMANUEL PAUL
- Citation
- EMMANUEL PAUL
- Status
- Judgment
- Jurisdiction
- Tanzania
- Court
- TANZLII
- Decision
- 20 September 2024
- Posture
- Criminal Appeal / Judgment on Appeal
- Language
- English
More details
- Court
- TANZLII
- Decision
- 20 September 2024
- Posture
- Criminal Appeal / Judgment on Appeal
- Language
- English
On this page
Professional case brief
Research organized from the available case record
01
Holding and result
The court found that the identification of the appellant was reliable as he was well known to the victim and her mother, the incident occurred in sufficient light, and the medical evidence corroborated the victim's account. The prosecution proved the offence of rape beyond reasonable doubt, and the trial court properly evaluated all evidence. The appeal lacked merit and was dismissed.
Court disposition
Appeal dismissed
Orders
- Conviction and sentence of 30 years imprisonment upheld
02
Material facts
Parties
Emmanuel Paul
AppellantJamhuri
Respondent Counsel: Geofrey MlagalaAmounts and remedies
- Sentence: years 30
03
Procedural history
Posture
Criminal Appeal / Judgment on Appeal
04
Questions and positions
Legal issues
- 01
Whether the identification of the appellant was proper and reliable
- 02
Whether the prosecution proved the offence of rape beyond reasonable doubt
- 03
Whether the trial court properly evaluated the evidence from both sides
Party arguments
- Applicant
- The appellant argued there was no proper identification as required by law, the ingredients of rape were not proved, the prosecution evidence was unreliable, the trial court failed to analyze all evidence, and the conviction was based on weakness of the defence rather than strength of the prosecution case.
- Respondent
- The respondent argued that identification was proper as the appellant was known to the victim and her mother, the ingredients of rape were proved by medical and eyewitness evidence, the trial court properly analyzed all evidence, and the prosecution case was strong and credible.
05
Court’s reasoning
Legal principles
- 01
Waziri Amani v. Republic [1980] TLR 250
Proper identification requires consideration of time, distance, conditions, and prior acquaintance between witness and accused.
- 02
Seleman Makumba v. Republic [2006] TLR 379
In sexual offences, the victim's evidence alone can be sufficient for conviction if credible.
06
Ratio, limits and disposition
Ratio decidendi
The court found that the identification of the appellant was reliable as he was well known to the victim and her mother, the incident occurred in sufficient light, and the medical evidence corroborated the victim's account. The prosecution proved the offence of rape beyond reasonable doubt, and the trial court properly evaluated all evidence. The appeal lacked merit and was dismissed.
Obiter and limits
- There is no legal bar to relatives testifying as witnesses if their evidence is credible.
- If the accused was innocent, he would have assisted the victim rather than fleeing the scene.
Court disposition
Appeal dismissed
- Conviction and sentence of 30 years imprisonment upheld
Source and reliance status
TANZLII · 20 September 2024
This page organises the available record for research. Confirm quotations, current status, and subsequent treatment against the official source before relying on the case.
Judgment reading view
Judgment text
The complete available source text.
TANZLII
Judgment· 20 September 2024
KATI KA MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA
MASIJARA NDOGO YA DODOMA ILIYOPO DODOMA RUFAA YA JINAI NA. 46 YA 2023 (Inatokana na Shauri La Jinai Na. 45 La 2021 Katika Mahakama ya WHaya ya Iramba Inayoketi Kiomboi) EMMANUEL PAUL.................................................................... MRUFANI
DHIDI YA JAMHURI......................................................................... MRUFANIWA
HUKUMU Tarehe ya Amri ya mwisho: 22/8/2024 Tarehe ya Hukumu: 20/9/2024. KHALFAN, J. Emmanuel Paul, mrufani katika shauri hili, alishtakiwa katika mahakama ya wilaya ya Iramba iliyoketi Kiomboi kwa kosa moja la ubakaji kinyume ya vifungu vya 130 (1) (2) (e) na 131 (1) vya Kanuni ya Adhabu [Sura ya 16 Marejeo ya 2019 (sasa 2022)]. Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, mnamo siku ya tarehe 05/05/2021 usiku huko katika Kijiji cha Malaja wilayani Mkalama mkoani Singida, mrufani alimuingilia kimwili msichana wa miaka 15 aliyekuwa anasoma katika shule ya msingi Malaja. Hi kulinda faragha, binti huyo atarejewa kama mhanga au SM2. Mrufani alikana shtaka, ndipo shauri liliendelea katika ngazi ya usikilizwaji. Kumbukumbu inaonesha kwamba, hili ni jaribio la pili baada ya rufaa ya kwanza mbele ya Mhe. Nzowa-Hakimu mwenye mamlaka ya ziada) kutengua hatia na adhabu za mahakama ya wilaya na kisha kuamuru uchukuliwaji wa ushahidi wa mhanga kwa kuwa awali ulichukuliwa kinyume cha sheria. Kwa ufupi, shauri hili lilianzia majira ya saa moja jioni ya siku ya tukio pale mama wa mhanga aliposikia kelele za bintiye SM2, zikitokea upande mwingine wa nyumba yao alikokuwa amemtuma akachukue taa ya sola. Kufika pale, alimuona jirani yao ambaye ni mrufani akikimbia, japo alimuita na kumuuliza ni kwa nini anakimbia, mrufani hakujibu na kisha kutokomea. Mhanga alimueleza mama yake kuwa mrufani alikuwa amembaka
baada ya kumuangusha chini. Kwamba, baada ya kumkagua na kumuona mhanga anatokwa damu na ana manii ukeni, alimpeleka kwa mama wa mrufani kuthibitisha. Naye mama wa mrufani alipothibitisha, ndipo wakamuita mwenyekiti wa kitongoji cha Mwinyi, SM4 pale nyumbani kwa wazazi wa mrufani. Aidha, ni mwenyekiti wa kitongoji cha Mwinyi SM4, ndiye aliyeripoti suala la ubakaji kwa mtendaji wa kijiji cha Malaja baada ya mrufani 2 kukiri kumbaka mhanga kwa vile aliona jambo hili like nje ya uwezo wake. Akiwa chini ya ulinzi wa mgambo SM5, mrufani alifikishwa ofisi ya mtendaji wa kijiji na hatimaye katika kituo cha polisi. Katika uchunguzi wa kitababu uliofanywa siku ya pili na kujazwa katika kielelezo P2 ambayo ni PF3 iliyotolewa na SM6, daktari alibaini mhanga alikuwa ameingiliwa kimwili kwa kuwa nguo zake za ndani zilikuwa na mabaka meupe, alikuwa hana bikra na alikuwa akitokwa ute ute mithili ya shahawa na michubuko katika sehemu za uke na kwenye makalio. Katika utetezi wake, mrufani yeye alidai kuwa siku ya tukio akiwa kijiweni huko Jenga Lambulu katika Kijiji cha Malaja, alipigiwa simu na mdogo wake Daniel Paul akimtaka arejee nyumbani. Mrufani aliongeza kuwa, alipofika nyumbani, aliwakuta mhanga na wazazi wake na mwenyekiti. Alidai kuwa watu hao walimueleza tuhuma za kubaka naye alikanusha. Mrufani alimalizia kuwa baada ya hapo, alikamatwa na kupelekwa kituo cha polisi. Ni katika
ushahidi huo, mahakama ya chini iliridhika na ushahidi uliotolewa hivyo ilimtia hatiani na kuamuru mrufani kutumikia kifungo cha miaka 30 gerezani. Akigadhabishwa na uamuzi huo wa mahakama ya wilaya, mrufani amekata rufaa katika mahakama hii akiegemea hoja tano za rufaa; ambazo ni: 3 1. Hakukuwa na ushahidi madhubuti wa utambuzi kama ilivyoelekezwa katika shauri la Waziri Amani dhidi ya Jamhuri [1980] TLR 250.
2. Kwamba, Hakimu alipotoka kumtia hatiani mrufani pasipo kuthibitisha viini vya kosa fa ubakaji.
3. Kwamba, hakimu alipotoka kwa kuzingatia ushahidi wa upande wa mashtaka ambao sio wa kuaminika na thabiti.
4. Kwamba, hakimu alipotoka kwa kushindwa kuchambua ushahidi uiiotoiewa na pande zote.
5. Kwamba, hakimu alipotoka kisheria na kimantiki kwa kuamua shauri kwa sababu ya udhaifu wa upande wa mshtakiwa badaia ya uimara wa ushahidi wa upande wa mashtaka. Katika usikilizwaji wa rufaa hii, mrufani hakuwakilishwa na wakili ilhali upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Bw. Geofrey Mlagala, wakili msomi mwandamizi wa serikaii. Mrufani alipopewa nafasi ya kufafanua sababu zake za rufaa, aliiomba mahakama hii kuchukulia sababu zake za rufaa kuwa ndio majumuisho yake. Hakuwa na jambo la ziada la kuelezea. Akijibu sababu ya kwanza ya rufaa, Bw. Mlagala, wakili msomi wa serikaii, alirejea kesi ya Waziri Amani tajwa hapo juu. alidai kuwa katika kesi zinazohusiana na utambuzi kwa kuona, mahakama lazima ijionye ili isije mtia hatiani mtuhumiwa kwa utambuzi uliokosewa. Wakili alidai kuwa katika shauri hili, hakukuwa na utata katika utambuzi wa uono kwa mrufani katika eneo la tukio. Wakili alieleza kuwa katika ushahidi wake, SM2 alieleza namna alivyobakwa siku ya tukio na mtu anayemfahamu na hata alimtajia mama yake, SMI punde tu alipofika. Wakili aliongeza kuwa, hata SMI katika ushahidi wake, aliieleza Mahakama namna alivoitikia kilio cha SM2 ambapo alipofika, alimuona mrufani akikimbia kisha akamuuliza kwa nini alikuwa akimkimbia ilhali SM2 analia. Bw. Mlagala alidai zaidi kuwa mrufani alitambuliwa kwa usahihi kwani hata alipoitwa na mwenyekiti wa kitongoji SM4, mwanzoni alikataa;
lakini baadaye alikiri kubaka. Aidha, kuhusu umbali, wakili alidai kitendo cha ubakaji kinatokea mkiwa jirani, hivyo, mrufani alitambuliwa kirahisi na SM2. Isitoshe, huko nyuma, alishawahi kumtaka kimapenzi, hivyo SM2 alimtambua mrufani kiurahisi. Wakili alimalizia kuwa ushahidi upande wa mashtaka uliondoa wasiwasi wa kukosea kutambua na mahakama ya wilaya ilijionya. Katika sababu ya pili ya rufaa, Bw. Mlagala alidai kuwa kifungu cha 130 (1) na (2) (e) cha Kanuni ya Adhabu, kinaelezea viini vya kosa la kubaka na kifungu cha 130 (4) kinaeleza kuwa hata kama uingiliaji ulikuwa wa 5 / juu juu, hilo ni kosa tosha. Wakili alidai kuwa SM2 alieleza kuwa alibakwa na mrufani. Na SMI alidai kumkuta SM2 na damu na shahawa. Wakili aliongeza kuwa ushahidi wa daktari SM6, uliungana na ushahidi wa SMI na SM2 kwani kwa kueleza kuwa SM2 alikuwa hana kizinda (ubikira) lakini akawa na shahawa na michubuko katika uke wake, kulithibitisha kuwa SM2 aliingiliwa. Wakili alidai zaidi kuwa pia ushahidi wa mwenyekiti wa kitongoji SM4, kuwa mrufani alikiri kutenda kosa; kote huko kulithibitisha viini vya kosa bila kuacha shaka kama inavyotakiwa na sheria. Katika sababu ya tatu, Bw. Mlagala alidai kuwa alirejea majumuisho yake hapo juu na kudai sababu hiyo haina mashiko. Wakili aliieleza mahakama hii kuwa kwa kitendo cha mhanga kumtaja haraka mbakaji yaani mrufani, kinathibitisha kuwa mrufani ndiye
aliyetenda kosa. Wakili aliegemea katika majumuisho yake kwenye kesi ya Marwa Wangiti Mwita na Mwenzake dhidi ya Jamhuri, Rufaa Ya Jinai No. 6 ya 1995. Kwa upande wa sababu ya nne ya rufaa, wakili msomi alieleza kuwa mahakama ya wilaya katika hukumu yake ilichambua kwa undani ushahidi wa pande zote mbili, wa mashitaka na utetezi. 6 Akimalizia kujumuisha katika sababu ya tano, Bw. Mlagala, alidai kuwa ushahidi wa upande wa mashitaka ulikuwa imara. Isitoshe, mrufani alipewa nafasi ya kuwahoji maswali na mwishowe alipewa nafasi ya kujitetea. Wakili alidai kuwa katika hukumu yake, Mahakama ya wilaya ilichambua kwa kina ushahidi wa pande zote. Kwamba, endapo ushahidi wa utetezi ulikuwa dhaifu; hiyo ni shauri yake. Wakili alimaliza kwa kuiomba mahakama hii kutupilia mbali rufaa hii kwa kukosa mashiko. Katika hoja za nyongeza, mrufani aliiomba mahakama hii kutoa uamuzi wa haki. Nimepitia sababu za rufaa, kumbumbu za mahakama ya wilaya na majumuisho ya wahusika katika rufaa hii, hoja kuu niionayo ni je rufaa hii ina mashiko? Nikianza na sababu ya kwanza ya rufaa, mrufani anadai kuwa vipengele vya utambuzi sahihi kwa kuona vilivyoainishwa katika kesi ya Waziri Amani dhidi ya Jamhuri, havikuzingatiwa na mahakama ya wilaya. Sababu hii inanifanya kuainisha vipengele vya utambuzi sahihi kwa kuona ambavyo mahakama ya Rufani katika kesi ya Waziri Amani iliona ni miongoni mwa ambavyo mahakama
inayosikiliza shauri inaweza jiuliza na kujibu, navyo ni: 1. Muda ambao shahidi alimtazama mtuhumiwa, 7 2 UmbaH tokea kwa shahidi a/ipokuwa hadi kwa mtuhumiwa, 3 . Mazingira aiipokuwa shahidi akimtazama mtuhumiwa, kwa mfano je i/ikuwa muda wa mchana au usiku?je kuiikuwa mwanga wa kutosha au hafifu kwenye eneo ia tukio? Na zaidi, 4 .Je shahidi aiimfahamu au aiimuona mtuhumiwa kab/a au la? Mahakama ya Rufani ilisema kuwa endapo mwishoni katika uchunguzi hakimu atakuwa ameridhika na ubora wa utambuzi kwa mfano utambuzi ulifanywa na shahidi baada ya kumtazama mtuhumiwa kwa muda mrefu au katika mazingira mazuri na ndugu, jirani, rafiki wa karibu, mfanyakazi mwenza na vitu kama hivyo, basi anaweza akamtia hatiani mtuhumiwa kupitia ushahidi wa utambuzi. Kwa upande mwingine, Mahakama ya Rufani ilisema, endapo ubora wa ushahidi wa utambuzi ni mdogo kwa mfano ulitokana na muda au kipindi kifupi au kutazama kwa muda mrefu kupitia hali au mazingira magumu mfano utambuzi kwa njia ya kuona kupitia mwanga hafifu wa mtaani; basi hakimu atatakiwa kumuachia mtuhumiwa. Nikija katika shauri hili, kama ilivyosemwa kwa usahihi na wakili wa serikali, mhanga (SM2) katika ushahidi wake, alieleza kuwa tukio lilitokea muda wa saa 12:00 jioni kuelekea saa 1:00 usiku akiwa njiani 8 I akirudi kwenye nyumba yao nyingine akiwa ametokea katika nyumba nyingine alikutana na mrufani. SM2 alidai kuwa kabla ya hiyo
siku, mrufani alishawahi kumtaka kimapenzi lakini alimkatalia. Kwamba, ndipo muda huo mrufani alimuangusha chini mhanga kisha akamvutia kwenye shamba la mahindi. Huko mrufani akamvua nguo na kuanza kumuingilia kimwili kinguvu. Ni kelele za SM2 ndizo zilimleta mama wa mhanga, SMI kwenye eneo la tukio. SMI alidai kuwa alipofika eneo la tukio, alimuona mrufani ambaye ni jirani yao, kisha akakimbia. Akamuita "Emma, Emma kwa nini unakimbia wakati SM2 analia?" Hata hivyo, mrufani hakujibu. SM2 alipomueleza SMI kuwa alikuwa amebakwa, ndipo alipomchunguza SM2 na kumkuta ana shahawa na damu kwenye nguo yake ya ndani na sketi. Hili lilimfanya SMI ampeleke SM2 nyumbani kwa mrufani. Ambapo, mama wa mrufani alimkagua na akathibitisha kuingiliwa kimwili kwa SM2. Mrufani katika utetezi wake alidai kuwa alipopigiwa simu na kwenda nyumbani aliwakuta SM2 na wazazi wake na mwenyekiti. Akijibu hoja, mrufani alikiri kuwa anamfahamu SM2 kwa kuwa ni jirani yao. Kwa ushahidi huo, ni dhahiri kwamba vipengele vilivyoainishwa katika kesi ya Waziri Amani hapo juu vimethibitishwa. Ilikuwa sahihi kwa mahakama ya wilaya kuridhika na ushahidi wa utambuzi wa SM2 na SMI 9 kwa kuwa wanajuana wakiwa kama majirani. Isitoshe, mrufani tayari alikwisha wahi mtaka kimapenzi SM2. Aidha, kwa muda wa saa 12 hadi saa 1 jioni kwa hapa Afrika Mashariki, giza linakuwa bado halijaingia. Zaidi ni kwamba, kitendo cha SM2
kukutana na mrufani na mrufani kumuangusha, kumvutia kwenye mahindi, kumvua nguo hadi kuanza kumwingilia na kisha kumaliza haja yake, kwa maoni yangu, kilichukua muda kulikopelekea SM2 kumtambua vizuri mrufani ambaye anamfahamu siku nyingi. Aidha, ni mtazamo wangu pia, kwa kuwa SMI na mrufani ni majirani na nikizingatia na muda wa tukio, naamini kuwa SMI aliweza kumtambua kwa usahihi mrufani na ndio maana alipomuona anakimbia, alimuita kwa jina lake. Kulingana na uchambuzi hapo juu, mahakama hii imeridhika kuwa mahakama ya wilaya ilikuwa sahihi kuona kuwa hakukuwa na upungufu au makosa ya utambuzi wa kumuona mrufani. Hivyo, sababu ya kwanza ya rufaa; mahakama hii inaona haina mashiko na inatupiliwa mbali. Katika sababu ya pili, tatu, nne na tano; kusema kuwa ushahidi upande wa mashitaka haukuwa madhubuti na wa kuaminika; mrufani hakueleza ni kwa nini anaona ushahidi upande wa mashtaka hauaminiki. Ijapo SMI ni mama wa SM2 na SM3 ni baba wa SM2 na mume wa SMI; je hii ndio tuseme ushahidi wao hauaminiki? Jibu ni Hapana. Hi ni kwa kuwa mashahadi hawa walieleza yale yaliyotokea. Mahakama hii haioni mahala pa kutilia shaka ushahidi wao. Hata tukisema ushahidi wa mama wa mhanga, SMI na baba, SM3 kuwa uwe una mashaka, bado ushahidi wa mhanga, SM2 unajitosheleza ukiungwa mkono na PF3. Hii ni kwa kuwa katika makosa yanayohusu makosa ya kingono, ushahidi wa mwathiriwa pekee unatosha
kumtia hatiani mtuhumiwa. Rejea kesi ya Seleman Makumba dhidi Jamhuri [2006] TLR 379. Hata hivyo, kama mtu umeshuhudia tukio kama vile ilivyokuwa kwa SMI, hakuna sheria inayozuia kutoa ushahidi eti tu kwa sababu ni ndugu au wana uhusiano. Isitoshe, nje ya SMI na SM3, kuna mwenyekiti wa kitongoji SM4 aliyefika nyumbani kwa wazazi wa mrufani na baada ya kumhoji mrufani aliyekana lakini baadaye akakiri kubaka na kuona tukio lipo nje ya uwezo wake, ndipo alimuarifu Afisa Mtendaji wa Kijiji. Pia askari mgambo SM5 aliyedai kupigiwa simu na SM3 kuwa aende nyumbani kwa wazazi wa mrufani ambako aliwakuta SM2 na mrufani pamoja na familia zao. Hawa wote, SM4 na SM5, hakuna ubishi siyo ndugu wa SM2. Sanjari na hayo, mrufani mwenyewe anaonyesha kuwa familia yake na ile ya SM2 hawakuwa na visirani kwani alipofika nyumbani kwao alidai 11 kumkuta SM2 akiwa na wazazi wake. Hii yote inaashiria kuwa hakuna namna kuwa kulikuwa na chuki ya kumkomesha mrufani. Kwa upande mwingine, ushahidi wa kitabibu na PF3 unaonyesha kuwa katika uchunguzi, SM2 alikutwa na michubuko na alikuwa akitokwa na ute ute mithili ya shahawa katika sehemu zake za siri na hakuwa na kizinda/ubikira. Hii kwa maoni ya daktari ni kuwa SM2 aliingiliwa kimwili ukeni kwake. Mahakama hii imeridhika na uamuzi wa mahakama ya wilaya kuwa kosa la ubakaji lilithibitishwa kwamba SM2 aliingiliwa kimwili na alimtaja mrufani kuwa ndiye
aliyembaka, na SMI alimuona mrufani akikimbia akimuacha SM2 anapiga kelele. Hata hivyo, kama mrufani alikuwa ni mtu mwema, ilibidi atoe msaada kwa SM2 labda kungeleta taswira tofauti. Hii inaashiria kwamba huenda mrufani aliamua kukimbia moja kwa moja hadi huko alikoita kijiweni ili kupoteza ushahidi. Isitoshe, mahakama hii inaona kama ilivyoona mahakama ya wilaya kuwa ushahidi upande wa utetezi haukuyumbisha hata kidogo ushahidi thabiti wa upande wa mashtaka kwani kama kweli alikuwa kijiweni kutazama bao, hakuita mtu yoyote kumtolea ushahidi. 12 Ni kwa sababu hizo hapo juu, mahakama hii inaona rufaa hii haina mashiko na hivyo inatupilia mbali kwa ujumla wake. Hatia na adhabu ya mrufani inaendelea kusimama. Imeamriwa hivyo. Imetolewa Dodoma leo tarehe 20 Mwezi Septemba, 2024. 20/9/2024 13
Case-aware research
Ask AI about this case
The judgment and available research above are public. New questions open in a separate private conversation grounded in this case.