george muhewa 3others vs nimrod elirehema mkono advocates 2021 tzhcld 2090 5 novemba 2021
The Commission erred in holding it was functus officio for all claims after dismissing condonation for salary arrears; only the salary arrears claim was time-barred, but the unfair termination claim was filed within time and should be heard.
Source-derived case information.
- Citation
- george muhewa 3others vs nimrod elirehema mkono advocates 2021 tzhcld 2090 5 novemba 2021
- Parties
- Applicant: George Mhewa; Applicant: Kahazi Opulukwa; Applicant: Sylivester Feston; Applicant: Victoria Shayo; Respondent: Nimrodi Elirehema Mkono t/a Mkono & Advocates
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2021
- Procedural Posture
- Labour Revision / Final Judgment
- Outcome
- decision reversed
- Legal Topics
- Unfair Termination, Condonation, Limitation Period
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
George Mhewa
Applicant
Kahazi Opulukwa
Applicant
Sylivester Feston
Applicant
Victoria Shayo
Applicant
Nimrodi Elirehema Mkono t/a Mkono & Advocates
Respondent
Procedural Posture
Labour Revision / Final Judgment
Legal Issues
- 1 Whether the Commission was functus officio regarding unfair termination claims after dismissing condonation for salary arrears
- 2 Whether claims for unfair termination were filed within statutory time limits
Ratio Decidendi
The Commission erred in holding it was functus officio for all claims after dismissing condonation for salary arrears; only the salary arrears claim was time-barred, but the unfair termination claim was filed within time and should be heard.
Court Disposition
decision reversed
Orders
- The Commission's decision of 25/03/2020 is set aside.
- The Commission is ordered to hear the applicants' unfair termination claims on merits.
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
MAHAKAMA KUU YA TANZANIA DIVISHENI YA KAZI DAR ES SALAAM MAOMBI YA MAREJEO NA. 162 YA 2020 KATI YA GEORGE MHEWA......................................... MLETA MAOMBI WA KWANZA KAHAZI OPULUKWA........................................... MLETA MAOMBI WA PILI SYLIVESTER FESTON........................................ MLETA MAOMBI WA TATU VICTORIA SHAYO................................................MLETA MAOMBI WA NNE DHIDIYA NIMRODI ELIREHEMA MKONO t/a Mkono & Advocates...................................... MJIBU MAOMBI HUKUMU YA UPANDE MMOJA Tarehe ya Amri ya Mwisho: 23/09/2021 Tarehe ya Hukumu: 05/11/2021 I. Arufani, J. Waombaji katika shauri hili wanaomba mahakama iitishe kumbukumbu za mgogoro wa kazi namba CMA/DSM/ILALA/916/18/154 wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (itakayojulikana kama tume) na kufanyia marejeo uamuzi uliotolewa na tume tarehe 25/03/2020. Katika uamuzi huo Tume ilikataa kusikiliza madai ya waleta maombi ya kuwa waliachishwa kazi isivyo halali yaliyokuwa yamelekezwa dhidi ya mjibu maombi. Tume iliamua kuwa haiwezi kusikiliza madai yao kwa msingi kuwa madai hayo yalishatupiliwa mbali na tume kwa sababu ya kupelekwa mbele ya 1 tume nje ya muda uliowekwa kisheria kupita na hayakuombea msamaha (condonation). Maeleza ya maombi haya kwa ufupi ni kwamba waleta maombi walieleza kuwa waliajiriwa na mjibu maombi kwa nyakati tofauti na wote kwa pamoja wakaachishwa kazi tarehe 03/08/2018 kwa utovu wa nidhamu. Baada ya waleta maombi kutoridhishwa na uamuzi wa kuachishwa kazi walipeleka malalamiko yao mbele ya tume wakidai waliachishwa kazi bila ya kufuata matakwa ya sheria wala taratibu na kanuni za ajira kazini. Waliomba tume imwamuru mjibu maombi awalipe malimbikizo ya mishahara yao pamoja na madai mbalimbali yanayotokana na kuachishwa kazi isivyo halali. Kwa kuwa madai ya waleta maombi ya kulipwa malimbikizo ya mashahara yalikuwa ni ya zaidi ya siku sitini waliambatanisha madai yao na maombi ya msamaha (condonation) wa muda waliochelewa. Kwa mujibu wa uamuzi uliotolewa na tume tarehe 08/03/2019 maombi yao ya msamaha wa muda waliochelewa kupeleka madai ya malimbikizo ya mishahara yao mbele ya tume hayakufanikiwa. Walipotaka kuendelea na madai yatokanayo na kuachishwa kazi isivyo halali upande wa mjibu maombi uliweka pingamizi kuwa tume haiwezi kusikiliza madai ya waleta maombi kwa sababu uamuzi 2 uliotolewa na tume tarehe 08/03/2019 ulitupilia mbali madai yao yote. Katika uamuzi uliotolewa tarehe 25/03/2020 Tume ilikubaliana na pingamizi la upande wa mjibu maombi na kutupilia mbali madai ya waleta maombi na kueleza kuwa tume haikuwa na uwezo wa kusikiliza madai mengine ya waleta maombi. Baada ya uamuzi huo waleta maombi walifungua maombi haya mbele ya mahakama hii wakiiomba mahakama ifanyie marejeo uamuzi huo wa tume na kama 4-. '% itaridhika hauko sawa kisheria au una kasoro ifute uamuzi huo. Baada ya mjibu maombi kupelekewa wito wa kuja mahakamani kwa njia ya kutangaziwa kupitia kwenye gazeti la Mwananchi la tarehe 23/10/2020 na kushindwa kufika mahakamani, mahakama iliombwa na kuridhia kuwa maombi haya yasikilizwe upande mmoja (ex-parte) xk Is kwa njia ya n Waleta maombi waliomba kiapo chao kiwe sehemu ya mawasilisho yao. Waliendelea kueleza kuwa msuluhishi alikosea kutafsiri sheria alipoeleza kwamba tume imefungwa (functus officio) kuendelea kusikiliza madai yao ya kuachishwa kazi isivyo halali. Walieleza kuwa madai ya malimbikizo ya mishahara yaliyoelezwa kuwa yaliwasilishwa nje ya muda yalikuwa tofauti na madai 3 yaliyotokana na kuachishwa kazi isivyo halali. Walieleza kuwa kimsingi wanakubaliana na hoja kuwa madai ya malimbikizo ya mishahara yalitakiwa kwa mujibu wa kanuni ya 10 (2) ya Tangazo la Serikali Na. 64 la 2007 yawasilishwe mbele ya tume ndani ya siku sitini kuanzia siku ya kuanza kwa mgogoro lakini yalipelekwa zikiwa zimeshapita siku mia moja na ishirini mbili. Waliendelea kufafanua kuwa msuluhishi Alfred Massay alishindwa kujielekeza vizuri kuhusu uamuzi uliotolewa na msuluhishi Mahindi, P. P. kwani ulihusiana na malalamiko ya malimbikizo ya mishahara ambayo yaliwasilishwa mbele ya tume zikiwa zimepita siku 122 kinyume na siku 60 zilizowekwa kisheria. Walieleza kuwa kimsingi na kama inavyoelezwa katika kanuni ya 10 (1) ya Tangazo la Serikali Na. 64 la 2007 madai ya kufukuzwa kazi isivyo halali yalipaswa kuwasilishwa ndani ya siku 30 kuanzia siku ya kuachishwa kazi. Walieleza kuwa waliachishwa kazi tarehe 03/08/2018 kama inavyoonyeshwa kwenye barua ya kuachishwa kazi na waliwasilisha malalamiko yao mbele ya tume tarehe 31/08/2018 ambayo ni ndani ya siku 30 zilizoainishwa kwenye sheria tajwa hapo juu. Waliiomba mahakama ione kuwa uamuzi wa tume wa tarehe 25/03/2020 ulikosewa kisheria kwani hauhusiani na madai ya 4 kuachishwa kazi isivyo halali kisheria ambayo yaliwasilishwa ndani ya muda badala yake unahusiana na madai ya malimbikizo ya mishahara ambayo yaliwasilishwa nje ya muda. Mwisho waliiomba mahakama iweke kando uamuzi wa tume ulioamua kuwa tume haiwezi kuendelea kusikiliza madai yao ya kuachishwa kazi isivyo halali na iamuru tume iendelee kusikiliza madai yao ya msingi ya kuachishwa kazi kinyume na sheria. * Baada ya kutafakari kwa kina mawasilisho ya waleta maombi na baada ya kupitia kumbukumbu za tume mahakama imeona hoja ya kuamuliwa katika marejeo haya ni kama msuluhishi alikosea kuamua kuwa baada ya tume kuamua madai ya malimbikizo ya mishahara ya waleta maombi yalikuwa nje ya muda basi tume ilikuwa haiwezi kuendelea kusikiliza madai ya waleta maombi ya kuachishwa kazi v ■ V.-. isivyo halali. Mahakama imepitia madai ya waleta maombi kama yalivyowasilisha mbele ya tume kupitia fomu CMA Fl na ikaona kuwa waleta maomba walikuwa wanaomba tume iamue kuwa usitishwaji wa ajira yoa ulikuwa siyo wa halali (unfair termination) na iamuru walipwe malimbikizo ya mishahara yao, kiinua mgongo, malimbikizo ya likizo ambazo hawakuchukua, malipo ya mshahara badala ya ilani 5 ya kuachishwa kazi, posho ya chakula cha mchana kwa mleta maombi wa tatu, malipo ya mishahara ya miezi kumi na miwili kama fidia ya kuachishwa kazi isivyo halali na cheti cha utumishi bora. Pamoja na madai hayo waleta maombi walipeleka pia maombi ya kuongezewa muda wa kusikilizwa kwa maombi ya malipo ya malimbikizo ya mishahara ambayo walieleza yalikuwa yamechelewa kwa muda wa siku 122. Kama ilivyoelezwa hapo juu maombi hayo ya kuongezewa muda kwa ajili ya kusikilizwa kwa madai ya malimbikizo ya mishahara nje ya muda ulioweka na sheria yalikataliwa katika uamuzi uliotolewa na tume tarehe 08/03/2019. Baada ya mahakama kupitia uamuzi wa tume uliotolewa tarehe 25/03/2020 ambao ndiyo waleta maombi wanaomba mahakama hii iufanyie marejeo mahakama imeona kuwa, kama walivyoelezea waleta maombi katika । ■ mawasilisho yao msuluhishi alijielekeza vibaya kueleza kuwa tume ilikuwa imezuiliwa (fanctus officio) na uamuzi huo kusikiliza madai yao yanayotokana na kuachishwa kazi isivyo halali. Mahakama imekuwa na maoni hayo baada ya kuona hoja iliyokuwa inaamuliwa katika uamuzi wa tarehe 08/03/2019 ni kuhusu kukubaliwa kusikilizwa kwa madai ya malimbikizo ya mishahara nje ya muda na sio madai yote ya waleta maombi yaliyoamuriwa kuwa yako 6 nje ya muda na hayawezi kusikilizwa na tume. Mahakama imeona kuwa, kwa kuwa maombi ya kuongezewa muda yalikuwa yanahusu madai ya malimbikizo ya mishahara peke yake na siyo madai yote ya waleta maombi na kwa kuwa msuluhishi alieleza kwenye uamuzi wa tarehe 08/03/2019 kuwa maombi hayo ya kuongezewa muda yametupiliwa mbali basi haikuwa sahihi kwa msuluhishi kuamua katika uamuzi wa tarehe 25/03/2020 kuwa tume haikuwa na uewezo wa kusikiliza maombi ya madai mengine ya waleta maombi ambayo hayakuwa nje muda. Kwa msingi huo mahakama inaona kuwa msuluhishi alikosea kueleza katika uamuzi wa tarehe 25/03/2020 kuwa tume haikuwa na uwezo wa kusikiliza madai ya waleta maombi ambayo yalikuwa ndani ya muda na ambayo hayakuwa yamejadiliwa na kutolewa uamuzi katika uamuzi wa tume uliotolewa tarehe 08/03/2019. Kwa hiyo uamuzi wa tume uliotolewa tarehe 25/03/2020 unabatilishwa na kuwekwa kando na Mahakama inaagiza tume isikilize malalamiko ya waleta maombi yanayohusu kuachishwa kwao kazi isivyo halali na kuamuliwa kwa mujibu wa sheria. Inaamriwa hivyo. 7 Imesainiwa hapa Dar es Salaam leo tarehe 05 ya mwezi Novemba, 2021 I. Arufani JAJI 05/11/2021 Mahakama: Hukumu imesomwa leo tarehe 05 ya mwezi Novemba, 2021 akiwepo mleta maombi wa kwanza na waleta maombi wengine wakiwa hawapo na akiwepo pia Wakili Elia Mpinga akishika mikoba ya Wakili Greyson Laizer anayemwakilisha mjibu maombi. Haki ya rufaa imeelezwa kwa wadaawa kikamilifu . Arufani JAJI ^^5/11/2021 8