MAOMBI YA MAREJEO 17491 YA MWAKA 2024 HAMIS SHABNI KITIBWI DHIDI YA IRONSIDS LIMITED
Applicant failed to prove the exact date and circumstances of termination due to conflicting evidence and lack of corroboration; the burden of proof was not discharged, and the Commission's decision to dismiss the claim was correct.
Source-derived case information.
- Citation
- MAOMBI YA MAREJEO 17491 YA MWAKA 2024 HAMIS SHABNI KITIBWI DHIDI YA IRONSIDS LIMITED
- Parties
- Applicant: Hamisi Shabani Kitibwi; Respondent: Ironsides Limited
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2024
- Procedural Posture
- Labour Revision / Final Judgment
- Outcome
- application dismissed
- Legal Topics
- Unfair Termination, Burden of Proof, Procedural Fairness
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Hamisi Shabani Kitibwi
Applicant
Ironsides Limited
Respondent
Procedural Posture
Labour Revision / Final Judgment
Legal Issues
- 1 Whether the applicant was unfairly terminated without written notice
- 2 Whether oral termination suffices as proof of dismissal
- 3 Whether the applicant discharged the evidentiary burden
Ratio Decidendi
Applicant failed to prove the exact date and circumstances of termination due to conflicting evidence and lack of corroboration; the burden of proof was not discharged, and the Commission's decision to dismiss the claim was correct.
Court Disposition
application dismissed
Orders
- Commission's award upheld
- No relief granted to applicant
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
KATIKA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA DIVISHENI YA KAZI DAR ES SALAAM MAOMBI YA MARE3EO NA. 17491 YA MWAKA 2024 KESI NAMBA: 202407221000017491 HAMIS SHABANI KITIBWI.......................................................... MLETA MAOMBI DHIDS YA IRONSIDES LIMITED............................................................................ ........ ......... MJIB HUKUMU Tarehe ya Amri ya Mwisho:30/ 09/2024 Tarehe ya Hukumu: 15/ 10/2024 MLYAMBINA, J. Katika shauri hili Mleta Maombi anapingamaamuzi yaliyotolewa na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (itajulikana kama Tume)yaliyotolewa katika Mgogoro wa Kazi Namba CMA/DSM/KIN/88/2023/188/2023. Katika shauri hili, Mleta Maombi aliwasilisha mgogoro mbele ya Tume akidai kuachishwa kazi isivyo halali. Shauri hilo lilisikilizwa upande mmoja baada ya Mjibu Maombi kushindwa kuhudhuria mbele ya Tume. Hata hivyo Tume baada ya kuzingatia Ushahidi wa Mleta Maombi ilitupilia mbali shauri lake kwa kushindwa kuthibitisha madai husika. Baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya Tume, Mleta Maombi amewasilisha maombi haya akijikita katika hoja zifuatazo: i. Kwamba, Mwamuzi hakuzingatia Ushahidi wa Mlalamikaji kuhitaji barua ya kuachishwa kazi ya maandishi wakati n i wajibu wa Mwajiri kutoa barua na Mwajiriwa hawezi kujiandikia barua ya kujiachisha kazi mwenyewe baii ameachishwa kazi kwa taarifa ya mdomo. ii. Kwamba, Mwamuzi alishindvza kumrekodi vizuri ushahidi hata kwenye maswa/i ya dodoso kwamba, kie/e/ezo ki/ichopoke/ewa na Tume ambacho n i naka/a ya hukumu kutoka Mahakama ya Mwanzo Kawe inaonyesha kulikuwa na mgogoro wa Mwajiri kwa makusudi kumpeleka Mahakamani kwa makosa ya kubarnbikiwa (jinai), Mla/amikiwa hakuwahi kunilipa mishahara yangu hata baada ya kumaliza kesi kwakuwa tayari alikuwa ameniondoa kwenye list ya wafanyakazi. iii. Kwamba, Mwamuzi ameshindwa kuzingatia taarifa za Mwombaji (ex- parte hearing) biia ya Miaiamikiwa kuja kukanusha na hakufika biia udhuru wa kisheria iicha ya kuwa na taarifa. Shauri hili liliendeshwa kwa njia ya maandishi. Mbele ya Mahakama hii, Mleta Maombi aliwakilishwa na Bw. Fadhili Fredrick Rithe, Mwakilishi Binafsi. Ilihali Bw. Antony Kalinga alimwakilisha Mjibu Maombi. Katika mawasilisho yake Bw. Rithe aliachana na hoja ya 2 na 3 na kubakiwa na hoja ya kwanza pekee. Alieleza kuwa, Mwamuzi hakuzingatia ushahidi wa Mleta Maombi ambaye muda wote alieleza kuwa aliachishwa kazi kwa mdomo kwa hiyo asingeweza kuwasilisha barua ya kuachishwa kazi ya maandishi kwa sababu hakupewa barua hiyo bali alitaarifiwa kwa mdomo. Aliongeza kuwa haikuwa sahihi kuhitaji barua kama uthibitisho wa kuachishwa kazi kwakuwa hata katika fomu namba 1 ameeleza wazi kuwa aliachishwa kazi kwa mdomo. Ilielezwa na Mleta Maombi kuwa, katika kiapo kinzani cha Mjibu Maombi aya ya 1 Mjibu Maombi amekubali maudhui yote yaliyomo katika aya ya 1, 2, 3, 4, 5 na 6 ya kiapo cha Mleta Maombi. Hivyo amekubali kuwa Mleta Maombi aliachishwa kazi bila sababu na bila kufuata utaratibu. Katika kuyapa nguvu maelezo yake, Mleta Maombi alirejea kesi ya Atuwonekye IMwenda Hezron Mangula Misc Land Application No. 05 ya 2020 (haijaripotiwa) Mahakama Kuu ya Tanzania Kitengo cha Ardhi Iringa. Kwamba katika kesi iliyorejewa ukurasa wa 16 aya ya kwanza Mahakama ilikuwa na haya ya kusema miongoni mwa mambo mengine: Three, it is a principle of law as stated in the case of East African Cables [T] Limited v Spenncon Services Limited, that where the fact sworn to or affirmed is not controverted then it is deemed to be admitted. Kwa kuzingatia mawasilisho yaliyotolewa hapo juu, Mleta Maombi anaiomba Mahakama ikubali maombi na itengue Tuzo iliyotolewa na Tume tarehe 27/06/2024 na kumwagiza Mjibu Maombi kumlipa Mleta Maombi jumla ya Shilingi za Kitanzania 17,891156 kama inavyoonekana kwenye fomu namba Mahakama inatambua ya kuwa shauri hili liliendeshwa mbele ya Tume upande mmoja bila ya Ushahidi wa Mjibu Maombi. Na hata baada ya maamuzi ya upande mmoja, Mjibu Maombi hakuwasilisha maombi ya kutengea maamuzi hayo mbele ya Tume. Hivyo katika Mahakama hii alitakiwa kujibu hoja za kisheria pekee na sio maelezo mengine. Katika mawasilisho yake, Mahakama imeona ya kuwa hakuna hoja yoyote ya kisheria iliyojibiwa au kuibuliwa na Mjibu Maombi. Hivyo basi, maelezo yake hayajazingatiwa mbele ya Mahakama Mleta maombi anaomba Mahakama izingatie maelezo yake kuwa aliachishwa kazi kwa mdomo, hivyo hakuna uthibitisho wowote ule wa maandishi. Katika fomu ya kuanzishia mgogoro madai ya Mleta Maombi yalikuwa ni kuachishwa kazi isivyo halali na migogoro mingine. Katika fomu hiyo Mleta Maombi alieleza kuwa mgogoro ulizuka tarehe 29/09/2022. Vilevile katika fomu hiyo kwenye kipengele cha kuonesha tarehe Mleta Maombi alipopewa taarifa ya kuachishwa kazi aliandika kuwa alipewa taarifa ya kuachishwa kazi tarehe 26/09/2022. Hivyo katika fomu hiyo kuna mkanganyiko wa taarifa za madai ya Mleta Maombi. Katika Ushahidi wake mbele ya Tume Mleta Maombi ameeleza kuwa alikamatwa na Polisi tarehe 27/09/2022 na alifukuzwa kazi tarehe 30/10/2022. Hivyo kwa kupitia Ushahidi wa Mleta Maombi Mahakama inajiuliza; ni ipi siku sahihi ambapo alifukuzwa kazi? Kwakuwa Mleta maombi ndiye eliyedai kuwa aliachishwa kazi basi ilikuwa ni jukumu lake kuthibitisha kuwa ni kweli aliachishwa kazi na kwa tarehe ambazo anadai. Huu ni msimamo wa kisheria uliowekwa katika Kifungu cha 110 cha Sheria ya Ushahidi [Sura 6 Kama i/ivyorejewa 20/P/kinaeleza ifuatavyo: 110. -(1) Whoever desires any court to give judgement as to any legal right or liability dependent on the existence o f facts which he asserts must prove that those facts exist Katika kifungu tajwa hapo juu imeelezwa kuwa yeyote anayetamani Mahakama iamue upande wake juu ya jambo fulani ni lazima kuthibitisha jambo hilo. Katika shauri hili hakuna uthibitisho wowote ni lini Mleta Maombi alipofukuzwa kazi. Kama nilivyoeleza hapo juu, ushahidi wake una mkanganyiko hata yeye mwenyewe hajui siku sahihi alipoachishwa kazi hivyo kufanya maelezo yake kuwa na walakini. Mahakama imezingatia maelezo kuwa katika kiapo kinzani Mjibu Maombi hapingi kumuachisha kazi Mleta Maombi, lakini kwakuwa shauri liliendeshwa upande mmoja ni wazi kuwa Mahakama haiwezi kuzingatia Ushahidi mpya unaoletwa mbele ya mahakama hii. Ushahidi huo ulitakiwa kuwasilishwa mbele ya Tume. Lakini Mleta Maombi alipewa nafasi ya kuthibitisha maelezo yake na alishindwa. Ni kweli kuwa hata bila uwepo wa barua ya kuachishwa kazi dai la kuachishwa kazi linaweza kuthibitishwa. Lakini dai hilo ni dhahiri kuwa litathibitishwa kutokana na mazingiza husika. Mazingira ya shauri hili ambapo kuna ushahidi uliokinzana wa Mleta Maombi, ni ngumu kuthibitisha dai lake la kuachishwa kazi kwa njia ya mdomo. Hivyo basi, kutokana na maelezo hapo juu, Mahakama hii inaona ya kuwa shauri hili halina mantiki. Tume iliamua shauri hili kwa usahihi. Hivyo basi maamuzi ya Tume yanaendelea kushikiliwa. Shauri hili linatupiliwa mbali. Imeamuriwa hivyo. JAJI 16/10/2024 Uamuzi huu umesomwa na kutolewa leo tarehe 16/10/2024 mbele ya Bw. Fadhili Fredrick Rithe, Mwakilishi Binafsi na Bw. Herry Makomba, Afisa Zamu wa Mjibu Maombi. JAJI 16/10/2024