MAREJEO NA
- Citation
- MAREJEO NA
- Status
- Judgment
- Jurisdiction
- Tanzania
- Court
- TANZLII
- Decision
- 1 January 2024
- Posture
- Labour Revision / Final Judgment
- Language
- English
More details
- Court
- TANZLII
- Decision
- 1 January 2024
- Posture
- Labour Revision / Final Judgment
- Language
- English
On this page
Professional case brief
Research organized from the available case record
01
Holding and result
The applicant's claim for salary arrears was time-barred as it was not filed within 60 days from the accrual of the cause of action. The applicant, being on probation, was not entitled to compensation for unfair termination, and only entitled to arrears for the last two months worked.
Court disposition
application dismissed
Orders
- Respondent to pay applicant TZS 300,000 as arrears for last two months worked
02
Material facts
Parties
Idd Martin Nyinyoo
Applicant Counsel: Muhindi SaidiManangwa na Baraka Po R K
Respondent Counsel: Kelvin MundoAmounts and remedies
- Salary Arrears Awarded: TZS 300,000
03
Procedural history
Posture
Labour Revision / Final Judgment
04
Questions and positions
Legal issues
- 01
Whether the applicant's claim for salary arrears was time-barred
- 02
Whether the applicant was entitled to compensation for unfair termination during probation
Party arguments
- Applicant
- The applicant argued that the arbitrator erred in finding his claim for salary arrears time-barred and in awarding only two months' salary, asserting entitlement to compensation for unfair termination and arrears due to underpayment.
- Respondent
- The respondent contended the claim was filed out of time per Rule 10(2) of GN No. 64/2007 and that the applicant, being on probation, was not entitled to compensation for unfair termination under section 40 of the Employment and Labour Relations Act.
05
Court’s reasoning
Legal principles
- 01
Rule 10(2) of GN No. 64/2007
Claims other than unfair termination must be filed within 60 days
- 02
Section 40 of Employment and Labour Relations Act; David Nzaligo v. National Microfinance Bank Plc [2019] TZCA 540
Probationary employees are not entitled to compensation for unfair termination
06
Ratio, limits and disposition
Ratio decidendi
The applicant's claim for salary arrears was time-barred as it was not filed within 60 days from the accrual of the cause of action. The applicant, being on probation, was not entitled to compensation for unfair termination, and only entitled to arrears for the last two months worked.
Obiter and limits
- Probationary employees must file claims under unfair labour practice, not unfair termination.
Court disposition
application dismissed
- Respondent to pay applicant TZS 300,000 as arrears for last two months worked
Source and reliance status
TANZLII · 1 January 2024
This page organises the available record for research. Confirm quotations, current status, and subsequent treatment against the official source before relying on the case.
Judgment reading view
Judgment text
The complete available source text.
TANZLII
Judgment· 1 January 2024
KATIKA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA
DIVISHENI YA KAZI
DAR ES SALAAM MAREJEO NA. 27598 YA MWAKA 2024 KESI KUMBUKUMBU NA. 202411011000027598 IDD MARTIN NYINYOO............................................... MLETA MAOMBI
DHIDI YA MANANGWA NA BARAKA PO R K...................................MJIBU MAOMBI
HUKUMU Tarehe ya Amri ya Mwisho :20/12/2024 Tarehe ya Hukumu: 24/12/2024 MLYAMBINA, J. Mleta Maombi amewasilisha shauri hili baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (itajulikana kama Tume). Kumbukumbu zinaonesha kuwa, Mleta Maombi alikuwa Mwajiriwa wa Mjibu Maombi katika nafasi ya ulinzi. Kwamba alifukuzwa kazi mnamo tarehe 10/07/2023. Baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya kuachishwa kazi, Mleta Maombi aliwasilisha malalamilo yake mbele ya Tume pamoja na madai mengine aliomba malimbikizo ya mishahara. Madai hayo yalikataliwa na Tume na ndio msingi wa marejeo haya akijikita katika hoja zifuatazo: i. Kwamba, Muamuzi hakuwa sahihi kwa kuamua na kusema madai ya Mleta Maombi yalikuwa nje ya muda na kuyatupilia mbali kwa kukosa mashiko wakati madai yake yalikuwa ni mapunjo. i ii. Kwamba, Muamuzi alikosea kwa hoja na sheria kwa kusema kwamba madai yapo nje ya muda na kutoa amri ya Mleta Maombi kulipwa miezi miwili ya mshahara, na je ni zipi stahiki za kuachishwa kazi bila sababu za msingi na ambapo utaratibu haukufuatwa na upi ushahidi uliomuongoza katika uthibitisho? Shauri hili liliendeshwa kwa njia ya maandishi. Katika kuendesha shauri hili, Mleta Maombi aliwakilishwa Muhindi Saidi, Mwakilishi Binafsi, ilihali Mjibu Maombi aliwakilishwa na Bw. Kelvin Mundo, Mwakilishi Binafsi. Katika hoja ya kwanza, Mleta Maombi alisimamia msimamo wake kuwa Muamuzi alikosea
kusema kuwa madai yake ya mapunjo yalikuwa nje ya muda. Alieleza kuwa madai yake yalikuwa ni mapunjo yaliyotokana na Mwajiri kulimbikiza mapunjo ambayo hakuwa analipwa badala yake kulipwa kama vile kiasi cha TZS 50,000/= au 20,000/ =. Aliongeza kuwa kama alivyoeleza katika ushahidi ndani ya ukura wa 5 wa maamuzi husika, wakati wa kuanza kazi tarehe 13/10/2022 Paulo ambaye ndiyo Mwajiri alitoa kama kianzio kiasi cha shilingi 20,000/=. Alieleza kuwa alikuwa analipwa mshahara kidogo kidogo kuanzia kiasi cha TZS 20,000/=, 30,000/= na 10,000/= hivyo anastahili malimbikizo ambayo alipunjwa. Ili kuyapa nguvu mawasilisho yake Mleta Maombi alirejea katika kesi Baina ya Tanzania China Friendship Textle Co. Ltd na Mada Hason Na Wenzake 1360, Maombi ya Marejeo Na. 88 ya Mwaka 2008. Katika kujibu, Bw. Mundo alipinga vikali hoja ya kwanza kwamba haina mashiko. Alieleza kuwa Mleta Maombi aliwasilisha maombi yake nje ya muda. Alieleza kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 10(2) cha Sheria ya Taasisi za Kazi (Kanuni za Usu/uhishi na Uamuzi) Tangazo la Serika/i Na. 64 la mwaka 2007madai hayo yaliwasilishwa nje ya muda kwani yalitakiwa kuwasilishwa ndani ya siku 60 tokea mapunjo hayo. Lakini kwa upande wa Mleta Maombi aliwasilisha nje ya siku zilizopangwa kisheria. Mahakama imepitia hoja hii na kuona ya kuwa, katika CMA FI Mleta Maombi alieleza kuwa anaomba kulipwa malimbikizo ya mishahara yake kiasi
cha shilingi laki nane na sabini (TZS 870,000/=). Katika fomu hiyo, Mleta Maombi hakueleza madai hayo yameanza lini. Lakini katika Ushahidi wake Mleta Maombi alieleza kuwa madai hayo yameanza tokea alipoajiriwa kwani alikuwa akipewa mshahara kidogo kidogo na si kama ambavyo walikubaliana. Tukirejea, inaonesha Mleta Maombi alianza kazi tarehe 13/10/2022. Hivyo madai yake ya mapunjo ni tokea wakati huo ameajiriwa. Kama alivyoeleza Mjibu Maombi, madai hayo ya mapunjo ya mshahara yanaangukia katika Kanuni ya 10(2) ya TS. Na. 64/2007 ambapo kanuni hiyo imeelekeza madai mengine yote isipokuwa mgogoro wa kuachishwa kazi yawasilishwe ndani ya siku 60. Tukihesabu tokea tarehe 13/10/2022 hadi tarehe 10/08/2023 Mleta Maombi alipowasilisha madai yake mbele ya Tume ni wazi kuwa madai hayo yalikuwa nje ya muda. Muamuzi alilizingatia hilo na kumpa Mleta Maombi madai ya mshahara ya miezi miwili ya mwisho. Mahakama inaona maamuzi hayo yalikuwa ni sahihi kwa kuzingatia kifungu cha sheria tajwa. Mleta Maombi angetaka madai hayo yashughulikiwe alitakiwa kuomba nyongeza ya muda ya kuwasilisha maombi hayo. Lakini kwakuwa hakufuata huo utaratibu ilikuwa ni sahihi kwa madai yake kutupiliwa mbali. Katika hoja ya pili, Mleta Maombi alieleza kuwa muamuzi alikosea kutoa tuzo ya malipo ya miezi miwili tu wakati katika tuzo hiyo kwenye ukurasa wa 15, Tume ilithibisha kwamba uachishwaji kazi haukuwa halali
bila kutoa fidia iliyoombwa na Mleta Maombi. Kama ilivyoelezwa kuanzia Kifungu cha 39 hadi 41(1), (2) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini [Sura ya 366 Kama iiivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019] Katika kujibu hoja hiyo, Bw. Mundo alieleza kuwa Mleta Maombi alikuwa kwenye muda wa majaribio hivyo hakustahili kuliwa fidia ya mishahara ya miezi 12 kwa mujibu wa kifungu cha 40 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini. Hi kuyapa nguvu maelezo yake, Mjibu Maombi alirejea kesi ya David Nzaligo v. National Microfinance Bank Pic, (Civil Appeal 61 of 2016) [2019] TZCA 540 (09 September 2019). Mahakama pia imepitia na kuona kuwa ilikuwa ni maamuzi ya Tume kuwa Mleta Maombi alikuwa katika muda wa uangalizi (probation) na mbele ya Mahakama hii Mleta Maombi hajapinga hoja hiyo. Hivyo basi, kwakuwa imekubalika kuwa Mleta Maombi alikuwa katika muda wa matazamio naungana mkono na Bw. Mundo kuwa hastahili kulipwa fidia ya miezi 12 ya mshahara kwa kuachishwa kazi kwakuwa vifungu vinavyohusiana na uachishwaji kazi usio halali havimlindi mfanyakazi alie katika kipindi cha uangaliazi. Haya pia ni maamuzi ya Mahakama ya Rufani yaliyoamuriwa katika kesi ya David Nzaligo (supra) ambapo Mahakama iliamuru ifuatavyo: We find that the import of section 35 o f ELRA though it addresses the period of employment and not the status of employment, a fact that a probationer is under assessment and valuation can
in no way lead to circumstances that can be termed unfair termination. Katika kesi nukuliwa hapo juu, Mahakama ya Rufani iliamuru kuwa, pamoja na kwamba kifungu cha 35 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini kimeelezea suala la muda wa ajira, kitendo cha mfanyakazi kuwa katika muda wa majaribio hakipelekei mazingira ya kuachishwa kazi isivyo halali. Kama ilivyoelezwa hapo juu, Mleta Maombi alikuwa katika muda wa matazamio hivyo hastahili kulipwa madai hayo kama ilivyoamuriwa na Tume. Vilevile ni msimamo wa Mahakama kuwa pale ambapo Mfanyakazi anakuwa katika kipindi cha matazamio anatakiwa kufungua shauri lake chini ya kanuni iitwayo uonevu katika ajira "unfair labour practice" na si ufukuzwaji kazi usio halali. Kwakuwa Mleta Maombi katika shauri hili alifungua shauri la ufukuzwaji kazi usio halali, hawezi kufaidika na fidia zozote. Hivyo basi Mahakama inaona shauri hili kwa ujumla halina manktiki. Muamuzi aliamua shauri hili kwa usahihi na Mahakama inakubaliana na maamuzi ya Tume. Mjibu Maombi anaamuriwa kumlipa Mleta Maombi kiasi cha Shilingi Laki Tatu (T7S 300,000/=) kama mapunjo ya mishahara ya miezi miwili ya mwisho aliyoifanyia kazi. Imeamuriwa hivyo.
JAJI 24/12/2024 Uamuzi huu umesomwa na kutolewa leo tarehe 24/12/ 2024 mbele ya Muhindi Saidi Mwakilishi Binafsi wa Mleta Maombi na Bw. Kelvin Mundo, Mwakilishi Binafsi wa Mjibu Maombi. Haki ya Rufaa imeelezwa. \
Case-aware research
Ask AI about this case
The judgment and available research above are public. New questions open in a separate private conversation grounded in this case.