iron and steel limited dhidi ya martine kumalija na mwenzake 2022 tzhcld 953 21 oktoba 2022
The preliminary objection is dismissed because the issue of when the applicant became aware of the award is a factual matter requiring evidence, not a pure point of law suitable for determination as a preliminary objection.
Source-derived case information.
- Citation
- iron and steel limited dhidi ya martine kumalija na mwenzake 2022 tzhcld 953 21 oktoba 2022
- Parties
- Applicant: Iron and Steel Limited; Respondent: Martine Kumalija na mwenzake
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2022
- Procedural Posture
- Labour Revision Application / Ruling on Preliminary Objection
- Outcome
- Preliminary objection dismissed
- Legal Topics
- Limitation Periods, Review of Arbitration Awards, Preliminary Objection
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Iron and Steel Limited
Applicant
Martine Kumalija na mwenzake
Respondent
Procedural Posture
Labour Revision Application / Ruling on Preliminary Objection
Legal Issues
- 1 Whether the revision application was filed out of time
- 2 Whether the preliminary objection on limitation is sustainable
Ratio Decidendi
The preliminary objection is dismissed because the issue of when the applicant became aware of the award is a factual matter requiring evidence, not a pure point of law suitable for determination as a preliminary objection.
Court Disposition
Preliminary objection dismissed
Orders
- Preliminary objection is dismissed
- Main application to proceed to hearing on merits
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
IN THE HIGH COURT OF TANZANIA LABOUR DIVISION AT PAR ES SALAAM MAOMBI YA MAREJEO NA. 188 YA MWAKA 2022 (Maombi ya Marejeo yanatokana na uamuzi wa Tume ya Usuluhishi Tarehe 23 Mei 2021 katika Mgogoro Na, CMA/DSM/KIN/R.573/8284) IRON AND STEEL LIMITED..................................................... MLETA MAOMBI DHIDI YA MARTINE KUMALIJA NA MWENZAKE.................... WAJIBU MAOMBI UAMUZI MDOGO K, T, R- MTEULE, J, 19/10/2022 & 21/10/2022 Uamuzi huu mdogo unatokana na pingamizi la awali lililoletwa dhidi ya maombi haya ya Marejeo yanayotokana na Tuzo ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi katika Mgogoro Na. CMA/DSM/KIN/R.573/8284 uliyoamriwa tarehe 23/05/2020 na Mhe. Urassa, E, F. IRON AND STEEL LIMITED, ambaye ni mwombaji katika shauri hili anaiomba Mahakama nafuu zifuatazo:- 1) Mahakama hii iite kumbukumbu, kutathmini usahihi na uhalali wa Tuzo ya mchanganuo wa hesabu ya Tume Usuluhishi na Uamuzi iliyotolewa na Mheshimiwa E.F. Urassa (Mwamuzi) i tarehe 23/05/2017 mchanganuo ambao mleta maombi alipewa na kuufahamu uwepo wake tarehe 09/05/2022. 2) Na nafuu nyingine ambazo Mahakama hii itaona busara kuzitoa kwa mleta maombi. Maombi haya yameambatana na kiapo cha Bw. Idrissa Ally ambaye ni Afisa Mwandamizi wa Mleta Maombi. Hata hivyo Mjibu maombi amepinga maombi haya kwa kuwasilisha kiapo kinzani alichoapa Bw. Omar Abubakar Ahmed. Pingamizi la awali lililowasilishwa na mjibu maombi lina hoja kwamba maombi haya ya marejeo yamefunguliwa nje ya muda. Katika hatua ya usikilizwaji wa shauri mleta maombi aliwakilishwa na Wakili Gilbert Mushi, na Wakili George Shayo na kwa upande wa mjibu Maombi aliwakilishwa na Bw. Juma Nassoro. Usikilizwaji wa maombi haya ulifanyika kwa mawasilisho kwa njia ya mdomo. Bw. Nassoro akifanya mawasilisho ya pingamizi la awali alieleza ya kwamba kwa mujibu wa kifungu Na. 91(10(a) ya sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, sura 366 kama ilivyorejewa 2019, Mahakama hii ina mamlaka ya kufanya mapitio ya tuzo iliyotolewa na Tume ndani ya wiki 6 kutoka tarehe ambayo maamuzi hayo yaliwasilishwa kwa mleta maombi. Na endapo anapinga tuzo hiyo kwa hoja kuwa tuzo ilipatikana 2 kinyume cha utaratibu, basi maombi yawasilishwe ndani ya wiki 6 toka tarehe aliyogundua kuwa tuzo ilipatikana kinyume na utaratibu. Bw. Juma Nassoro alieleza ya kwamba Tuzo inayolalamikiwa iiitolewa tarehe 23/5/2017 wakati kila upande ukiwa umewakilishwa Tume tuzo hiyo kuwasilishwa katika maombi ya ukazaji hukumu "Execution No. 247 of 2019" kati ya Julai 2021 na Agosti 2021 na usikilizwaji kuendelea Mei 2022. Kwa mujibu wa Wakili Nassoro, waleta maombi tokea wakati huo 2017 kule Tume, mpaka 2021 wakati wa usikilizwaji wa maombi ya kukaza hukumu, walikuwa na ufahamu wa uwepo wa Tuzo bishaniwa na hivyo kwa kitendo cha kusajili maombi haya mwezi wa sita 2022 walikuwa nje ya muda. Bw. Juma Nassoro alirejea aya ya 3.10, 3.11 na 3.12, pamoja na kwamba mleta maombi ameeleza kufahamu uwepo wa tuzo hii tarehe 9/5/2020 na kwamba aliomba apatiwe nakala na baadaye akaipata 20/5/2022, mleta maombi hasemi aliipata tarehe ngapi hiyo tuzo na wala hakuonyesha ushahidi wa ni lini aliipata, hivyo inaunga mkono maoni yake kwamba mleta maombi ameamua kwa makusudi kuficha ukweli wa lini aliipata hiyo nyaraka kwa sababu angetaja tarehe rasmi ukweli ungekuwa dhidi yake. 3 Bw. Nassoro alieleza Kanuni ya kisheria pale ambapo mdaawa kwenye shauri anapotakiwa kuleta ushahidi na akaamua kuuficha huo ushahidi bila kutoa sababu yoyote Mahakama inayo haki ya kuchukulia kwa uhasi dhidi ya mdaawa huyo kuwa ushahidi huo ungeletwa ungekuwa dhidi yake. Wakili Nassoro alisema kuwa, waleta maombi wanatumia mbinu za kuchelewesha haki kuwanyima haki wateja wake. Hivyo aliomba maombi haya yatupiliwe mbali, chini ya kifungu No. 3 (1) cha sheria ya ukomo wa muda (law of Limitation Act). Akijibu mawasilisho ya mjibu maombi Bw. Gilbert Mushi alikubaliana na mawasilisho ya Wakili wa mjibu maombi kwamba maombi ya marejeo hufanyika kwa mujibu wa kifungu cha 91(l)(a) cha sheria ya Kazi na Usalama Kazini, Sura ya 366 Marekebisho ya 2019, maombi haya yanatakiwa yafunguliwe ndahi ya siku 42 tangia siku ambayo wahusika wamepewa nakala ya tuzo. Hivyo alieleza swali la msingi katika maombi haya ni, lini mleta maombi alipewa nakala ya maombi yanayoombewa marejeo. Bw. Gilbert Mushi alieleza ni jukumu la mleta pingamizi kuijulisha Mahakama ni lini mleta maombi alipewa nakala ya tuzo. Alisema katika kiapo kinzani hakuna mahali ambapo imeelezwa hiyo tuzo ilitolewa lini kwa mleta maombi. Aliendelea kueleza ya kwamba kwenye aya ya 3.10, 4 3.11 na 3.12 kiapo chake mleta maombi ameeleza namna ambavyo aligundua uwepo wa tuzo, mnamo tarehe 9/5/2022 wakati wa kusikiliza maombi ya ukazaji Tuzo No. 247 ya 2019 na kwamba mleta maombi aliitaarifu Mahakama kuwa kiapo kilieleza kuwa hakuwa na ufahamu wa tuzo hiyo kabla ya tarehe 9/5/2022. Kwa mujibu wa Wakili Mushi, baada ya kutoridhika na tuzo alifungua marejeo haya kati ya tarehe 10/6 - 19/6/2022 kwa njia ya mtandao au "online" ambayo yalisajiliwa, tarehe 20/6/2022 na nakala ngumu kuwasilishwa hapa mahakamani. Kwa maoni yake, tata ikichukuliwa tarehe ya kuleta maombi kuwa 20/6/2022, sheria ya ukomo sura ya 89 iliyorejewa 2019, kifungu 19 (1) kinaondoa siku ya kwanza kwenye hesabu ya muda na hivyo ukiondoa tarehe 9/5/2022 ambayo ndiyo tarehe mleta maombi aligundua uwepo wa tuzo hiyo hadi tarehe 20/6/2022 ambapo nakala ngumu zililetwa, ni siku 42. Kwa maoni yake maombi haya yapo ndani ya muda. Wakili Mushi alipinga tuhuma kuwa ameficha taarifa za ni lini alijua uwepo wa tuzo. Ni Maoni ya Wakili Mushi kwamba maombi haya yamefunguliwa ndani ya muda na yameletwa ili kuweza kufichua ubatili wa tuzo iliyotolewa na Tume tarehe 23/5/2017 na siyo mbinu za ucheleweshaji. Katika majumuisho Bw. Nassoro alisisitiza ya kwamba mwenye wajibu wa kusema ni lini aligundua uwepo wa tuzo ili kufanya maombi hayo 5 yawe ndani ya muda ni mleta maombi na siyo wajibu maombi na hiyo hoja ya kulaumu kiapo kinzani kutokueleza ni lini walipelekewa nakala haiwezi kuwa na mashiko. Kwa mujibu wa Bw. Nassoro, hakuna mahali kiapo cha waleta maombi kimesema ni lini waligundua upatikanaji wa hii tuzo kuwa imepatikana kinyume cha taratibu. Baada ya kuzingatia na kuchambua kilichopo ndani ya kiapo, kiapo kinzani pamoja na mawasilisho yaliyofanywa na pande zote na kumbukumbu za Tume, ninaona hoja bishaniwa ni je pingamizi la awali lililo ibuliwa na Mjibu maombi lina misingi ya kisheria. Kinachoangaliwa katika kujibu swali hili ni kama maombi yaliletwa nje ya muda. Kifungu cha 91 (a) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini, Sura ya 366 kinaeleza wazi ya kwamba hesabu ya muda itahesabiwa kuanzia siku ambayo mleta maombi amepatiwa nakala ya uamuzi. Katika maombi haya kumbukumbu zinaonyesha maamuzi ya ukokotozi/udadavuzi Na. CMA/DSM/KIN/R.573/8284 ambayo ndiyo yanayoombewa marejeo yalitolewa na CMA tarehe 23/05/2020. Mleta maombi anaeleza kwamba alipata uelewa wa uwepo wa maamuzi hayo tarehe 09/05/2022 ndipo alipoomba nakala hiyo na baada ya kuipitia aliandika kiapo cha tarehe 20/05/2022 na kuwasilisha mbele ya 6 Mahakama hii wakati wa kusikiliza maombi ya kukazia hukumu Na. 247 ya 2019. Jambo hili linabishaniwa na mjibu maombi ambaye anasema kuwa waleta maombi walijua uwepo wa uamuzi huo mara baada ya kutolewa CMA. Mabishano haya yapo katika viapo vyao. Na huu ndiyo mgogoro wa msingi katika maombi haya. Kwa vile kiini cha marejeo haya kimelala katika hoja ya uelewa wa mleta maombi kuhusu uwepo wa tuzo inayobishaniwa. Kwa vile tarehe ya ufahamu wa uwepo wa tuzo ni moja ya hoja inayohitaji kuthibitishwa katika maombi ya msingi, nina maoni kuwa hoja hii haiwezi kumalizwa kwa pingamizi la awali. Ni msimamo wa kisheria ya kwamba suala linalohitaji ushahidi au kuthibitishwa haliwezi kusimama kama pingamizi la awali au hoja ya kisheria, kama ilivyojadiliwa katika kesi ya Mukisa Biscuit Manufacturing Co. Ltd v. West End Distributors Ltd (1969) EA 696. Kutokana na msimamo wa kesi tajwa ni wazi kwamba ili pingamizi la awali liweze kusimama kisheria ni lazima iwe hoja ya msingi ya kisheria tu. Katika maombi haya hakuna ubishi kwa pande zote mbili za wadaawa ya kwamba haijulikani ni lini mleta maombi alipewa nakala ya maamuzi ya ukokotoaji Na. CMA/DSM/KIN/R.573/8284. Nakala halisi 7 haionyeshi ni lini wadaawa walipatiwa nakala hiyo nah ii ni hoja ya msingi katika maombi ya marejeo. Kutokana na msimamo wa kisheria hapo juu ni wazi ya kwamba pingamizi la awali la mjibu maombi linakosa sifa ya kisheria kusimama kama pingamizi la kisheria. Hivyo Mahakama hii inatupilia mbali pingamizi hili, shauri la msingi lisikilizwe na kuamriwa. Kila upande utajigharamia gharama za kesi. Imeamriwa hivyo. Imetolewa Leo tarehe 21 Oktoba 2022 KATARINA REVOCATI MTEULE JAJI 21/10/2022 8