MAREJEO NA
The applicant was not unfairly terminated; the evidence, including CCTV footage, sufficiently proved he refused to sign the suspension letter, and hearsay evidence was properly disregarded.
Source-derived case information.
- Citation
- MAREJEO NA
- Parties
- Applicant: Joseph Dickson Maringo; Respondent: Eldride Investment Tanzania Ltd
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2024
- Procedural Posture
- Labour Reference / Final Judgment
- Outcome
- dismissed
- Legal Topics
- Unfair Termination, Evidence Admissibility, Oral Contract, Hearsay Evidence
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Joseph Dickson Maringo
Applicant
Eldride Investment Tanzania Ltd
Respondent
Procedural Posture
Labour Reference / Final Judgment
Legal Issues
- 1 Whether the applicant was unfairly terminated from employment
- 2 Whether the evidence relied upon by the Commission was properly evaluated
- 3 Whether hearsay evidence was admissible and given proper weight
Ratio Decidendi
The applicant was not unfairly terminated; the evidence, including CCTV footage, sufficiently proved he refused to sign the suspension letter, and hearsay evidence was properly disregarded.
Court Disposition
dismissed
Orders
- The reference is dismissed.
- The Commission's decision is upheld.
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
KATIKA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA DIVISHENI YA KAZI DAR ES SALAAM KESI REFERENCE NA. 20240108000000305 MAREJEO NA. 305 YA MWAKA 2024 JOSEPH DICKSON MARINGO............................................MLETA MAOMBI DHIDI YA ELDRIDE INVESTMENT TANZANIA L T D ........................... MJIBU MAOMBI HUKUMU Tarehe ya Amri ya Mwisho: 12/ 03/2024 Tarehe ya Hukumu: 05/ 04/2024 MLYAMB1NA, J. Katika shauri hili ni madai ya Mleta Maombi kuwa aliajiriwa na Mjibu Maombi kwa mkataba wa mdomo usio na muda maalumu mnamo tarehe 01/05/2015 katika nafasi ya Mkaguzi wa ndani na baadae kupandishwa cheo kama Meneja wa duka kwa mshahara wa shilingi laki nane na hamsini (TZS. 850,000/=). Ni dai la Mleta Maombi kuwa mgogoro huu ulizuka pale ambapo Maafisa wa Mfuko wa Hifadhi wa Jamli NSSF walipokwenda kutembelea eneo la kazi la Mjibu Maombi na kuongea na Wafanyakazi. Kwamba, Maafisa hao walimuuliza Mleta Maombi kama wamejiunga na mfuko huo naye akajibu hawajajiunga na i akaeleza pia kuwa hawana mikataba ya ajira ya maandishi. Kwamba, baada ya ukaguzi huo, Mleta Maombi alipewa jukumu la kumtaarifu Mjibu Maombi juu ya kuwapa mikataba ya ajira pamoja na kuwaunga katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii. Kwamba, baada ya Mjibu Maombi kufikishiwa taarifa hiyo alikasirika na kumtaka Mleta Maombi akabidhi funguo ya ofisi na kumuachisha kazi tokea siku hiyo. Baada ya kutoridhika na uachishwaji kazi huo, Mleta Maombi alipeleka malalamiko yake mbele ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (itajulikana kama Tume) ambapo mgogoro wake ulitupiliwa mbali. Tume iliamua kuwa madai ya Mleta Maombi kuwa aliachishwa kazi sio ya kweli. Kwamba siku anayodai Mleta Maombi aliachishwa kazi ni siku aliyopewa barua ya kusimamishwa kazi kwa muda (suspension), lakini alikataa kupokea barua hiyo na kukimbilia kupeleka mgogoro Tume. Baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya Tume, Mleta Maombi ameamua kuleta mgogoro huu mbele ya Mahakama akiiomba Mahakama kutatua hoja zifuatazo: i. Kwamba, Mheshimiwa Muamuzi alikosea kimantiki na kisheria kuamua kuwa Mleta Maombi alikana kupokea barua ya kusimamishwa kazi wakati ushahidi wa picha mjongeo (CCTV footage) ulishindwa kuthibitisha hilo. ii. Kwamba, Mheshimiwa Muamuzi alikosea kisheria na kimantiki kwa kushindwa kuelezea na kuchanganua ushahidi wa shahidi wa upande wa Mleta Maombi (PW2) bila sababu za msingi. iii. Kwamba, Mheshimiwa Muamuzi alikosea kimantiki na kisheria kwa kushindwa kurekodi majina ya mashahidi kwa ufasaha. Shauri hili liliendeshwa kwa njia ya maandishi. Bw. Carlos J. Cathbert, wakili, ilihali Bw. Edward Simkoko, Mwakilishi Binafsi alimwakilisha Mjibu Maombi. Katika hoja ya kwanza, Mleta Maombi alieleza kuwa Muamuzi alitumia ushahidi wa picha mjongeo (CCTV footage) kuthibitisha yeye kukataa kupokea barua ya kusimamishwa kazi. Aliupinga ushahidi huo kuwa hakuithibitisha tukio hilo kwani hauonyeshi tukio hilo na wala hauna sautl kuthibitisha Mleta Maombi alikataa kupokea barua hiyo. Alifafanua zaidl kuwa, katika kielelezo E l, Mleta Maombi alisimamishwa kazi lakini barua hiyo ilimtaka atoe maelezo kutokana na kosa alilokuwa amefanya, Mleta Maombi alikataa kupokea barua hiyo. Bw. Simkoko alieleza kuwa, wakati Mleta Maombi anakataa kupokea barua hiyo (kielelezo E l), kulikuwa na watu walioshuhudia tukio hilo na waliandika barua za kutoa maelezo juu ya tukio husika. Kwamba, chakushangaza watu hao hawakufika mbele ya Tume kutoa ushahidi. Mwakilishi alieleza kuwa, licha ya uthibitisho huo kutokuwepo, Muamuzi aliamua kuwa ushahidi wa picha mjongeo unathibitisha kuwa Mleta Maombi alikataa kupokea barua ya kusimamishwa kazi. Mjibu Maombi yeye alieleza kuwa video iliyonyesha tukio la Mleta Maombi kukataa kupokea kielelezo E l tarehe 17/3/2016. Alieleza zaidi kuwa, video hiyo inaonesha Mleta Maombi akipokea nyaraka na akiisoma kisha akirudi na kueleza kuwa ameongea na Wakili wake katika simu na amemshauri asitie sahihi katika barua hiyo. Alifafanua zaidi kuwa, Mleta Maombi anaonekana akihesabu na kuthibitisha mauzo na kukabidhi funguo na kuondoka. Mahakama imepitia kwa kina Kielelezo E2 (CCTV footage), inaonesha Mleta Maombi alipewa bahasha, alipokea bahasha hiyo, akaifungua na kutoa karatasi. Pia kinaendelea kuonesha akiisoma karatasi hiyo na kuandika na kisha akarudisha kwa aliyempatia karatasi hiyo, huku akitamka maneno ya kuhusu mwanasheria wake. Mahakama hii katika kujibia hoja hiyo imeangalia na kusikiliza kwa makini kielelezo E2 imebaini kusikika kwa sauti ingawa kwa umbali na kubaini kwa Mleta Maombi kuongelea kuhusiana na Wakili wake. Hivyo basi, kulingana na ushahidi wa DW1, pamoja na maelezo yaliyoandika katika kielelezo E l na Mariamu, vinashabihiana na tukio husika la maelezo ya kwamba Mleta Maombi alipatwa barua husika ya kusimamishwa kazi, na alikataa kuipokea. Alipowasilisha madai yake mbele ya Tume, Mleta Maombi alieleza kuwa aliachishwa kazi na Mjibu Maombi mnamo tarehe 17/03/2016, siku ambayo ndio tukio la kukataa kupokea barua lilitokea kama ilivyoainishwa hapo juu. Kama ilivyoelezwa, tukio la siku hiyo halithibitishi Mleta Maombi kuachishwa kazi kama ambayo iliamuriwa kwa usahihi na Tume. Lakini pia hakuna ushahidi wowote wakuthibitisha baada ya tukio elezewa hapo juu endapo Mleta Maombi alienda tena ofisini na kupewa barua ya kuachishwa kazi. Mahakama imezingatia hoja za Mleta Maombi kuwa Mjibu Maombi hawakuwaleta mashahidi waliokuwepo eneo la tukio. Mahakama haikubaliani na hoja hizo za Mleta Maombi. Kama ilivyoelezwa hapo juu, Mjibu Maombi alitoa Ushahidi wa picha mjongeo (CCTV footage) kuthibitisha tukio lote lililotokea siku husika. Hivyo basi, hata bila kuwaleta mashahidi hao, ushahidi huo wa picha mjongeo unatosha kuthibitisha kuwa Mleta Maombi alipelekewa barua na kukataa kuisaini kwa madai kuwa amepokea maelekezo kutoka kwa Wakili wake. Hivyo basi, kwakuwa hakuna uthibitisho wowote uliotolewa, Mahakama inaona madai yake ya kuwa ameachishwa kazi hayana mantiki. Katika hoja ya pili, Mleta Maombi alieleza kuwa Muamuzi hakueleza ushahidi wa P2 ameuchukuliaje kwakuwa hakusema chochote kama amekubaliana nao au hajakubaliana nao. Kwamba, kwa maelezo ya Muamuzi kuwa ushahidi huo haukuthibitishwa. Hoja hiyo ilipingwa vikali na Mjibu Maombi ambaye alieleza kuwa ushahidi wa P2 ni wa kusikia hivyo haukuthibitishwa mbele ya Tume. Hivyo, Muamuzi alikuwa sahihi kutozingatia Ushahidi huo. PW2 alieleza kuwa siku hiyo hakuwepo kabisa ofisini, hivyo hakushuhudia chochote bali alipata taarifa kutoka kwa wafanyakazi wenzake pamoja na Mkurugenzi Carlos. Ushahidi huo unadhihirisha wazi shahidi huyo hakuwepo siku ya tukio bali alipewa taarifa tu na wafanyakazi wenzake. Hivyo basi, ushahidi wake hauwezi kuthibitisha chochote na Tume ilikua sahihi kutozingatia ushahidi huo. Hayo pia ni maamuzi ya Mahakama katika kesi ya Jongo Mwikola v. Geita Gold Mining Limited, Civil Appeal No. 344 ya mwaka 2020, Court of Appeal, Mwanza, Mahakama iliamua ifuatavyo: We are mindful that section 62 of the Evidence Act provides for the inadmissibility of hearsay evidence and that even if it is admitted it would be of no significance or no evidential value in proving a fact in issues. Katika kesi hiyo hapo juu, Mahakama iliamuru kuwa kifungu cha 62 cha Sheria ya Ushahidi kinakataza upokeaji wa Ushahidi wa kusikia lakini kifungu hicho kimeongeza kuwa Ushahidi huo hata ukipokelewa usipewe nguvu. Na hata katika shauri hili, Ushahidi wa P2 ulipokelewa lakini haukupewa nguvu kwakuwa ni Ushahidi wa kusikia ambao hauna uthibitisho wowote. Mleta Maombi hakusema chochote kuhusiana na hoja ya mwisho hivyo Mahakama inaona kuwa aliamua kuachana na hoja hiyo. Hivyo basi, kutokana na maelezo hapo juu, Mahakama hii inaona ya kuwa shauri hili halina mantiki. Tume iliamua shauri hili kwa usahihi. Hivyo basi maamuzi ya Tume yanaendelea kushikiliwa. Shauri hili linatupiliwa mbali. Imeamuriwa hivyo. Y. J. MLYAMBINA JAJI 05/04/2024 Hukumu hii imesomwa leo tarehe 05/04/2024 mbele ya Edward Simkoko Mwakilishi Binafsi wa Mleta Maombi na Wakili Carlos Cuthbert kwa ajili ya Mjibu Maombi. Rufaa iko wazi. JAJI 05/04/2024