justine s lengai na wengine vs shirika la usambazaji umeme tanzania tanesco 2021 tzhcld 147 4 juni 2021
Applicants were employed under specific task contracts, not permanent contracts. Their contracts ended upon completion of tasks, so they are not entitled to terminal benefits or remedies for unfair termination. Standing Orders for Public Servants do not apply to their employment type.
Source-derived case information.
- Citation
- justine s lengai na wengine vs shirika la usambazaji umeme tanzania tanesco 2021 tzhcld 147 4 juni 2021
- Parties
- Applicant: Justine S. Lengai; Applicant: Maulid Ayub; Applicant: Maltin Mkude; Applicant: Ramadhani Kingi; Applicant: Dickson Kessy; Applicant: Tino Kasiani; Applicant: Itovela Tungwa; Applicant: Ally Kibwana; Applicant: Salvatory John; Applicant: Juma K. Tambi; Applicant: Emmanuely Ng'oa; Applicant: Yona Stanley; Applicant: Majuto Ramadhani; Applicant: Gidioni Kitea; Applicant: Joseph Henry; Applicant: Clevian Adomary; Applicant: Gerald T. Roman; Applicant: Majuto Mkude; Applicant: Thobias J. Luhanga; Applicant: Rashidi Bakari; Applicant: Kulwa Mhina; Applicant: Abdallah Said; Respondent: Shirika la Usambazaji Umeme Tanzania (TANESCO)
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2021
- Procedural Posture
- Labour Revision / Final Judgment
- Outcome
- application dismissed
- Legal Topics
- Employment Contracts, Termination, Public Service Standing Orders, Fixed Term Contracts, Specific Task Contracts
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Justine S. Lengai
Applicant
Maulid Ayub
Applicant
Maltin Mkude
Applicant
Ramadhani Kingi
Applicant
Dickson Kessy
Applicant
Tino Kasiani
Applicant
Itovela Tungwa
Applicant
Ally Kibwana
Applicant
Salvatory John
Applicant
Juma K. Tambi
Applicant
Emmanuely Ng'oa
Applicant
Yona Stanley
Applicant
Majuto Ramadhani
Applicant
Gidioni Kitea
Applicant
Joseph Henry
Applicant
Clevian Adomary
Applicant
Gerald T. Roman
Applicant
Majuto Mkude
Applicant
Thobias J. Luhanga
Applicant
Rashidi Bakari
Applicant
Kulwa Mhina
Applicant
Abdallah Said
Applicant
Shirika la Usambazaji Umeme Tanzania (TANESCO)
Respondent
Procedural Posture
Labour Revision / Final Judgment
Legal Issues
- 1 Whether applicants had permanent employment contracts
- 2 Whether applicants are entitled to terminal benefits for unfair termination
Ratio Decidendi
Applicants were employed under specific task contracts, not permanent contracts. Their contracts ended upon completion of tasks, so they are not entitled to terminal benefits or remedies for unfair termination. Standing Orders for Public Servants do not apply to their employment type.
Court Disposition
application dismissed
Orders
- Each party to bear its own costs
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DIVISHENI YA KAZI ILIYOKAA MOROGORO MAOMBI YA MAREJEO NA. 41 YA 2020 BAINA YA JUSTINE S. LENGAI. ■ MLETA MAOMBI NA. 1 MAULID AYUB. MLETA MAOMBI NA. 2 MALTIN MKUDE. MLETA MAOMBI NA. 3 RAMADHANI KINGI. MLETA MAOMBI NA. 4 DICKSON KESSY. MLETA MAOMBI NA. 5 TINO KASIANI. MLETA MAOMBI NA. 6 ITOVELA TUNGWA. MLETA MAOMBI NA. 7 ALLY KIBWANA. MLETA MAOMBI NA. 8 SALVATORY JOHN MLETA MAOMBI NA. 9 JUMA K. TAMBI. MLETA MAOMBI NA. 10 EMMANUELY NG'OA. MLETA MAOMBI NA. 11 YONA STANLEY. MLETA MAOMBI NA. 12 MAJUTO RAMADHANI. MLETA MAOMBI NA. 13 GIDIONI KITEA. MLETA MAOMBI NA. 14 JOSEPH HENRY. MLETA MAOMBI NA. 15 CLEVIAN ADOMARY. MLETA MAOMBI NA. 16 GERALD T. ROMAN MLETA MAOMBI NA. 17 MAJUTO MKUDE. MLETA MAOMBI NA. 18 THOBIAS J. LUHANGA. MLETA MAOMBI NA. 19 RASHIDI BAKARI. MLETA MAOMBI NA. 20 KULWA MHINA. MLETA MAOMBI NA. 21 ABDALLAH SAID. MLETA MAOMBI NA. 1 ABDALLAH SAID. MLETA MAOMBI NA. 1 ABDALLAH SAID. MLETA MAOMBI NA. 1 1 NA SHIRIKA LA USAMBAZAJI UMEME TANZANIA (TANESCO).................................................. MJIBU MAOMBI HUKUMU Tarehe ya Mwisho ya Amri: 28/05/2021 Tarehe ya Hukumu: 04/06/2021 A. E. MWIPOPO, J. JUSTINE lengai na Wenzake 20 ambao ni Waleta Maombi katika shauri hili la Marejeo wameleta maombi haya wakiomba Mahakama irekebishe Uamuzi wa Tume ya Usuluhishi uliotolewa katika mgogoro wa kikazi Na. CMA/MORO/128/2016 wa Tarehe 26 Machi, 2020, na Mhe. Hilary N.J., Muamuzi. Waleta Maombi wanaomba yafuatayo: 1. Mahakama hii ikipendezwa iitishe kumbukumbu za Tume ya Usuluhishi na Uamuzi iliyoketi Morogoro kwa ajili ya kurekebisha mwenendo mzima na uamuzi wa Tume katika mgogoro wa kikazi Na. CMA/MORO/128/2016 kati ya ABDALLAH SAID NA WENZAKE dhidi ya SHIRIKA LA USAMBAZAJI UMEME TANZANIA (TANESCO). 2. Gharama ya fidia 3. Nafuu yoyote ambayo Mahakama itapendezwa. 2 Maombi haya yanaungwa mkono na kiapo cha pamoja cha Waleta Maombi. Katika aya ya 4 ya kiapo kuna hoja 2 za kisheria zinazotokana na shahidi. Hoja hizo ni kama zifuatazo:- i. Iwapo Mjibu Maombi alitakiwa kutoa taarifa ya kuwaachisha kazi Waleta Maombi. ii. Iwapo Muamuzi alikuwa sahihi kisheria na kiushahidi kutupilia mbali (dismiss) madai ya Waleta Maombi. Historia ya mgogoro huu kwa ufupi ni kuwa, Waleta Maombi waliajiriwa na Mjibu Maombi kuanzia mwaka 2009 hadi 2016 kufanya kazi za kujenga njia za umeme na kukarabati njia hizo za umeme. Mnamo tarehe 1 Julai, 2016 Mjibu Maombi aliwapatia Waleta Maombi Mkataba wa kazi wa siku 4 unaoisha tarehe 04 Julai, 2016. Waleta Maombi hawakuridhika na mkataba huo na ndipo waliwasilisha mgogoro huo mbele ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi. Katika uamuzi wake, Tume ilitupilia mbali (dismissed) mgogoro huo kwa kuwa iliona Waleta Maombi walikuwa na mikataba ya kazi maalum ambapo kazi hiyo ilikuwa imekamilika. Waleta Maombi walifungua maombi ya marejeo Na. 29 ya 2019 na maombi ya marejeo Na. 14 ya 2020 ambayo yalifutwa na Mahakama hii kwa kuwa yalikuwa na makosa na walipewa kibali cha kuwasilisha maombi mengine ya marejeo yaliyo sahihi. Ndipo Waleta Maombi waliwasilisha maombi haya ya marejeo. 3 Wakati wa usikilizwaji wa maombi haya, pande zote mbili zilikuwa zinawakilishwa. Waleta Maombi wanawakilishwa na Prof. Binamungu, Wakili, na Mjibu Maombi alikuwa anawakilishwa na Bw. Norbet Beda, Wakili. Akifanya mawasilisho ya kuunga mkono marejeo haya, Wakili wa Waleta Maombi alieleza kuwa Waleta Maombi wanaomba kulipwa malipo ya taarifa ya kuachishwa kazi, likizo na kiinua mgongo. Alieleza kuwa Mjibu Maombi hajapinga maombi yao kama kiapo kinzani chao kinavyoonesha. Waleta Maombi walikuwa wakilipwa kutokana na kazi walizokuwa wakifanya mfululizo kuanzia mwaka 2009 hadi 2016. Jambo hilo pia halijapingwa na Mjibu Maombi. Tatizo lilitokea pale Mjibu Maombi alipotoa mkataba wa siku 4 kuanzia Tarehe 01/07/2016 na ulikuwa unaisha tarehe 04/07/2016. Hii ndio nyaraka iliyowafanya Waleta Maombi kuona kuwa wanaachishwa kazi isivyo halali. Wakili aliendelea kueleza kuwa pande zote mbili walikubaliana kuwa Waleta Maombi walikuwa wanafanya kazi kwa mikataba na hawakuwa wafanyakazi wa muda. Kanuni za kudumu za Utumishi wa Umma, 2009 katika kipengele D.33 kinaonesha malipo hayo yaliyoombwa na Waleta Maombi. Mjibu maombi alikuwa anawachukulia waleta maombi kama wafanyakazi wa muda ambayo sio sahihi. Na hivyo kushindwa kuona kuwa masharti ya mikataba ya Waleta Maombi yapo hata kama hayakuwa 4 yametajwa katika mikataba yao ya kazi. Mbele ya Tume kulikuwa na hoja ya malipo yao wanayodai. Ni maoni ya Waleta Maombi kuwa Muamuzi alikosea kuona Waleta Maombi hawastahili malipo hayo kwa kuwa hawakuwa wameyaomba katika shauri la mgogoro uliofungua mbele ya Tume. Mjibu Maombi hakutakiwa kufanya vile alivyofanya. Hivyo, wanaiomba Mahakama ifanyie marejeo ya Uamuzi wa Tume. Akijibu mawasilisho ya Waleta Maombi, Wakili wa Mjibu Maombi alieleza kuwa ni kweli Waleta Waombi walikuwa ni waajiriwa wa Mjibu Maombi kwa mikataba. Na mikataba - kielelezo MK1 ilipokuwa' ikiisha ilikuwa inaongezwa na walikuwa wakilipwa kwa siku kama kielelezo MK2 kinavyothibitisha. Chanzo cha mgogoro huu ni kitendo cha Waleta Maombi kugoma kufanya kazi baada ya kupewa mkataba wa siku 4. Waleta Maombi baada ya kugoma walileta madai ya likizo, kiinua mgongo na taarifa ya kuachishwa kazi. Muamuzi aliliona jambo hili katika ukurasa 12 wa Tuzo kuwa hakukuwa na uachishwaji kazi bali Waleta Maombi waliamu?i kuacha kazi baada ya kutoridhika na mkataba mpya. Wakili akiendelea kuwasilisha alieleza ya kwamba katika kiapo cha Waleta Maombi hakukuwa na suala la kuachishwa kazi. Mjibti Maombi anashangaa madai ya taarifa ya kuacha kazi yanatoka wapi. Kwa msirigi huu Waleta Maombi ndio waliotakiwa kumlipa Mjibu Maombi ifialipo ya taarifa ya kuacha kazi kwa siku 4. 5 Kuhusu likizo, Waleta Maombi walikuwa hawaendi likizo na aina ya mikataba yao ni kulipwa kwa siku na hawakuwa wakiomba likizo kwa kuwa wasingelipwa. Hata madai ya kiinua mgongo hayastahili kwa kuwa mikataba yao haikuwa inasema walipwe kiinua mgongo. Kuhusu malipo yanayotokana na kanuni za kudumu za Utumishi wa Umma Wakili wa Mjibu Maombi alieleza kuwa kanuni za kudumu za Watumishi wa Umma, 2009 (Standing Orders for Public Servants, 2009) hazitumiki kwa aina ya ajira ya Waleta Maombi. Sheria inayotumika ni Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Sura ya 366 ya Sheria, kama ilivyorejewa mwaka 2019, ndio maana walifungua shauri mbele ya Tume. Hivyo, wanaiomba Mahakama ikubaliane na Uamuzi wa Tume na kutupilia mbali maombi haya. Akifanya mawasilisho ya nyongeza (rejoinder submission), Wakili wa Waleta Maombi alieleza kuwa Mjibu Maombi ameeleza kuwa walikuwa wakiongeza mikataba yao hivyo walikuwa na mategemeo ya kdongezwa mkataba. Kuhusu maelezo kuwa Waleta Maombi waligoma kufanya kazi, Wakili alieleza kuwa hiyo inaonyesha kuwa walikuwa wanaendelea na kazi. Na alieleza kuwa maelezo hayo hayapo katika kiapo kinzani cha Mjibu Maombi. Alieleza kuwa Mjibu Maombi ni shirika la Umma hivyo hawezi kusema kuwa Kanuni za Utumishi wa Umma, 2009, hazitumiki kwa watumishi wa umma wa aina Fulani, labda sheria husika ieleze tofauti. Pia 6 Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini haiondoi matumizi ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma, 2009. Wakili wa Waleta Maombi aliona kuwa hoja hii inataka kuwanyima haki Waleta Maombi. Kutokana na mawasilisho ya pande zote mbili, naona kuwa kuna hoja mbili ambazo zinabishaniwa ambazo Mahakama hii inatakiwa izitolee uamuzi. Hoja hizo ni kama zifuatazo:- i) Iwapo waleta maombi walikuwa na mikataba ya kazi ya kudumu. ii) Nini nafuu za kila upande? Kwa kuanza kujibu hoja ya kwanza iwapo waleta maombi walikuwa na mikataba ya kazi ya kudumu, ni vema kuangalia aina za mikataba ambayo inatambulika na sheria za kazi. Kifungu cha 14(1) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Sura ya 366 ya Sheria, kama ilivyorejewa Mwaka 2019, inaelezea aina ya mikataba ya kazi. Kifungu hicho cha sheria kinaeleza kuwa kuna aina tatu za mikataba ya kazi ambayo ni mkataba usio na muda maalum, mkataba wa muda maalum na mkataba wa kazi maalum. Kifungu hicho kinaeleza kama ifuatavyo, nanukuu:- "14. -(1) Mkataba na mfanyakazi utakuwa wa aina zifuatazo- (a) mkataba kwa kipindi cha muda usiotajwa; (b) mkataba kwa kipindi cha muda kiiichotajwa kwa kada za wataaiamu na mameneja (c) mkataba wa kazi maaiumu." 7 Katika kesi ya Mtambua Shamte na Wenzake 64 dhidi ya Care Sanitation and Supplies, Marejeo Na. 154 ya 2010, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, iliyokaa Dar Es Salaam, Mahakama hii ilieleza kuwa kanuni zip! za kisheria zitatumika kuhusu uachishaji wa kazi inategemea na aina ya mkataba. Mkataba utachukuliwa kuwa ni wa masharti maalum wakati mkataba wa kufanya kazi unahusiana na muda maalum au kazi maalum. Na mkataba unachukuliwa kuwa ni wa kudumu wakati makubaliano ya kufanya kazi hayahusiani na muda au kazi maalum. Mkataba wa kazi maalum unaisha wakati kazi maalum inapokamilika. Mahakama hii ilitoa tafsiri kama hiyo katika kesi ya Abel Kikoti na Wenzake 5 dhidi ya Tropical Contractors Ltd, Marejeo Na. 305 ya 2019, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, iliyokaa Dar Es Salaam. Katika shauri hili, Waleta Maombi wameeleza kuwa walikuwa na mikataba ya kazi ambayo ni ya kudumu na kuwa walifanya kazi mfululizo kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka 2016. Hivyo wanaomba walipwe malipo ya taarifa ya kuachishwa kazi, likizo na kiinua mgongo. Kanuni za kudumu za utumishi wa umma za 2009 katika kipengele D.33 kinaelezea kuhusu malipo hayo. Kwa upande wa Mjibu Maombi ameeleza kuwa Waleta Maombi walikuwa ni wafanyakazi wao lakini walikuwa na mikataba ya kazi maalum ambayo kila ikiisha walikuwa wakipewa mikataba mingine. Na 8 kuwa Waleta Maombi waligoma kuongeza mikataba yao baada ya kuwa imeisha kutokana na Mjibu Maombi kuwaongeza kazi maalum ya siku 4. Mahakama hii imepitia kumbukumbu za Tume na inaona kuwa kulikuwa na mikataba ya ajira baina ya Waleta Maombi na Wajibu Maombi - kielelezo MK2. Kielelezo MK2 kinaeleza katika kifungu cha 1 kwamba Mkataba ni wa kazi maalum na malipo ya kazi hiyo ni ya kutwa. Na malipo hayo yatalipwa kila baada ya wiki mbili kwa kuzingatia siku mwajiriwa alizofanya kazi. Mkataba huo unaonesha siku za kufanya kazi na eneo la kufanyia kazi. Mkataba huo katika kifungu cha 2 unaeleza kuwa mwisho wa kazi katika eneo hilo ndio mwisho wa mikataba. Aidha, karatasi ya malipo ya Waleta Maombi - Kielelezo MK1 kinaonesha kuwa Waleta Maombi walikuwa wakilipwa kwa idadi ya siku ambazo walifanya kazi. Hivyo ni wazi kuwa Mkataba baina ya waleta maombi na wajibu Maombi ulikuwa ni wa kazi maalum na haukuwa wa kudumu. Kuhusu hoja ya Waleta Maombi kuwa walifanya kazi mfululizo kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka 2016 hivyo kwa muda waliofanya kazi unawafanya kuwa na mikataba ya kudumu, ni maoni yangu kuwa mahusiano ya kiajira yanayotokana na makubaliano baina ya mwajiri na mwajiriwa ndio na yanayoamua aina ya mkataba baina yao. Kazi za Waleta Maombi ni kazi maalumu na ukomo wake ulitegemea ukamilifu wa kazi na sio muda waliofanya kazi kama Kielelezo Mk-2 ambacho ni mikataba ya 9 kazi ya Waleta Maombi inavyoonesha. Katika kesi ya Group Six International dhidi ya Musa Maulid & another, Marejeo Na. 428 ya 2015, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, iliyokaa Dar Es Salaam, Mahakama ilieleza kuwa, nanukuu kwa lugha ya Kiingereza: - "Basically, the law does not provide that if an employee worked for a long period of time under one kind of the employment contract it automatically changed the kind of the employment relationship, changed from a contract for a specific task to a contract of an unspecified period of time." Kwa ufupi, Mahakama katika kesi tajwa hapo juu ilikuwa na matazamo kuwa sheria haielezi kuwa mwajiriwa aliyefanya kazi kwa muda mrefu chini ya aina moja ya mkataba wa ajira haifanyi aina ya mahusiano yake ya kikazi kubadilika moja kwa moja kutoka kuwa mkataba wa kazi maalum na kuwa mkataba usiokuwa na muda maalum. Kwa mtazamo huu, ni maoni yangu kuwa hoja ya Waleta Maombi kwamba walikuwa walifanya kazi kwa muda mrefu na walikuwa wakiongezwa mikataba mara kwa mara haiwafanyi kuwa na mikataba ya kudumu ya ajira. Kuhusu hoja ya Waleta Maombi kuwa Kanuni za kudumu za Utumishi wa Umma, 2009 katika kipengele D.33 kinaonesha malipo hayo yaliyoombwa na Waleta Maombi hivyo wanastahili kulipwa, na kuwa Mjibu Maombi ni shirika la Umma hivyo hawezi kusema kuwa Kanuni za Utumishi wa Umma, 2009, hazitumiki kwa watumishi wa umma wa aina fulani. Mjibu io Maombi alikuwa na Maoni kuwa Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma hazitumiki kwa Waleta Maombi. Nakaubaliana na Mjibu Maombi kuwa Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za mwaka 2009 hazitumiki kwa watumishi wa Taasisi ya Umma waliona na mikataba ya kazi maalum au mikataba ya kazi ya muda maalum. Kwa mujibu wa kifungu cha 3 cha Sheria ya Utumishi wa Umma, watumishi wa Taasisi za Umma ambao wanalipwa kwa siku au wana mikataba ya muda maalum huwa hawashughulikiwa chini ya sheria zinazoongoza watumishi wa umma. Hivyo Kanuni za kudumu za utumishi wa umma za 2009 haziwezi kutumika kwa Waleta Maombi katika kudai mafao yao. Kuhusu hoja ya Waleta Maombi kuwa kulikuwa na mategemeo ya kuongezwa mikataba, hoja hii haina msingi kwa kuwa ushahidi uliopo unaonesha kuwa mikataba ya Waleta Maombi ilikuwa ni ya kazi maalum na sio mikataba ya muda maalum. Hivyo, mikataba hiyo ilifikia mwisho baada ya kazi husika kukamilika kama mikataba yenyewe inavyoonesha. Ushahidi uliopo pia unaonesha kuwa tarehe 01/07/2016 Mjibu Maombi aliwapatia Waleta Maombi mkataba wa kazi maalum ya siku nne ambao unaisha tarehe 04/07/2016 lakini waleta Maombi waliukataa mkataba huo. Aidha, hakuna Ushahidi ya kwamba Waleta Maombi waliendelea na kazi au walipewa mkataba mwingine wa kudumu au wa muda ili kuwa na hoja n kuwa Waleta Maombi walikuwa na mategemeo ya kawaida ya kuongezwa mkataba. Kwa sababu hii, hoja ya kuwa matarajio ya kuongezwa mkataba haijathibitishwa. Kwa sababu hiyo, ninaona kuwa Waleta Maombi walikuwa na mikataba ya kazi maalum ambayo ilifika mwisho baada ya kukamilisha kazi husika. Hivyo Waleta Maombi hawakuwa na mikataba wa kazi wa kudumu. Hoja ya mwisho ni nini nafuu za kila upande. kwa kuwa Waleta Maombi walikuwa wanafanya kazi chini ya mkataba wa kazi maalumu hivyo ni wazi kuwa hawahusiki na haki zinazotokana na uachishwaji kazi usio halali. Suala hili lilijadiliwa Mahakama hii katika kesi ya ambayo nimeinukuu ya Mtambua Shamte na Wenzake 64 dhidi ya Care Sanitation and Suppliers, ambapo Mahakama hii ilieleza kuwa, nanukuu kwa lugha ya Kiingereza:- "It is now a principle of unfair termination under the Act, do not apply to specific task or fixed term contract which come to an end on the specified time or completion of a specific task. Under the latter, such principles apply under conditions specified under Section 36(a)(iii) read together with Rule 4(4) o the Code." Kwa kifupi, Mahakama ilieleza kuwa kwa sasa ni msimamo wa kisheria kuwa kanuni za uachishaji kazi usio halali hazitumiki kwa mikataba ya kazi maalum au ya muda maalum ambayo imefikia ukomo kutokana na kufikia mwisho muda maalum uliotajwa au kukamilika kwa kazi maalum. 12 Kwa msimamo huii wa kisheria, ni wazi kuwa Waleta Maombi hawachostahili kulipwa chochote kwani hawakuwa wameajiriwa kwa mkataba wa kudumu au kuachishwa kazi isivyo halali, bali mkataba wao ulifika mwisho baada ya kukamilisha kazi maalum waliokuwa wakiifanya. Hivyo naona hakuna sababu ya kupingana Uamuzi wa Tume na natupilia mbali maombi haya ya marejeo. Kwa kuwa huu ni mgogoro wa kazi kila upande utagharamia gharama zake za kuendesha shauri hili. 04/06/2021 13