kassim engineering company limited vs david saliva komba 2023 tzhcld 1285 19 mei 2023
The respondent failed to prove continued employment after expiry of the initial fixed-term contract. The work permit did not constitute or prove an employment contract, and payments made after contract expiry were for arrears, not for a renewed contract. The Commission's reliance on the work permit as evidence of...
Source-derived case information.
- Citation
- kassim engineering company limited vs david saliva komba 2023 tzhcld 1285 19 mei 2023
- Parties
- Applicant: Kassim Engineering Company Limited; Respondent: David Saliva Komba
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2023
- Procedural Posture
- Labour Revision / Final Judgment
- Outcome
- application allowed
- Legal Topics
- Employment Contract, Renewal by Default, Proof of Employment Relationship, Evidence Admissibility
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Kassim Engineering Company Limited
Applicant
David Saliva Komba
Respondent
Procedural Posture
Labour Revision / Final Judgment
Legal Issues
- 1 Whether there was an employment relationship after expiry of the initial fixed-term contract
- 2 Whether the work permit (kibali) can substitute an employment contract
- 3 Whether the respondent was entitled to salary and transport allowances for the alleged renewed period
Ratio Decidendi
The respondent failed to prove continued employment after expiry of the initial fixed-term contract. The work permit did not constitute or prove an employment contract, and payments made after contract expiry were for arrears, not for a renewed contract. The Commission's reliance on the work permit as evidence of employment was legally incorrect. The applicant demonstrated grounds for revision, and the Commission's award was set aside.
Court Disposition
application allowed
Orders
- The Commission's award in CMA/DSM/KIN/603/432/20 is set aside.
- Each party to bear its own costs.
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA DIVISHENI YA KAZI ILIYOKETI PAR ES SALAAM MAOMBI YA MAREJEO NA. 10 YA 2023 (Kutokana na Uamuzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ya DSM HiyoketiIlala Tarehe 29 Novemba 2022 katika Mgogoro wa Kazi Na. CMA/DSM/KIN/603/432/20. KASSIM ENGINEERING COMPANY LIMITED................ MLETA MAOMBI Dhidi ya DAVID SALIVA KOMBA................................................... MJIBU MAOMBI HUKUMU K. T. R MTEULE, J 11/05/2023 & 19/05/2023 Shauri hili la marejeo limefunguliwa dhidi ya Uamuzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi katika Mgogoro wa Kazi Na. CMA/DSM/KIN/603/2020/432/20. KASSIM ENGINEERING COMPANY LIMITED ambaye ni mleta maombi anaiomba Mahakama itoe amri zifuatazo: - i. Kwamba Mahakama hii tukufu ipendezwe kuitisha na kupitia kumbukumbu za Tume ya Usuluhishi na Uamuzi na Amri iliyotolewa kwenye Tuzo tarehe 29/11/2022 na Mh. Massawe, Muamuzi kwenye Mgogoro wa Kikazi Na. CMA/DSM/ILA/603/432/2020 kwa ajili ya kujiridhisha i kuhusu uhalali wa kisheria Pamoja na usahihi, na kama hayapo sahihi basi kuyatengua. ii. Amri yoyote ambayo Mahakama hii itaona inafaa. Shauri hili limeungwa mkono na kiapo cha mleta maombi amacho katika aya ya 4 kuna hoja tano za kisheria (legal issues) kama ifuatavyo: - i. Kwamba Mheshimiwa Muamuzi alikosea kimantiki na kisheria kuamua kuwa Mjibu Maombi alikuwa na mkataba mwingine baada ya ule wa kwanza kuisha na hivyo kumstahilisha alipwe nauli na mishahara kwa kuegemea kwenye kibali cha kazi ambacho hakikutolewa na mleta maombi bila uthibitsho wa uwepo wa mahusiano ya ajira kati ya wadaawa. ii. Kwamba Mheshimiwa Mwamuzi alikosea kimantiki na kisheria kwa kuamua kwamba, Pamoja na kutokuwa na uthibitisho wa uwepo wa mkataba mwingine wa pili wa muda maalumu wa miezi (3) [kati ya Aprili hadi Juni 2021] na bila kuthibitishwa mjibu maombi alifikaje Msumbiji, eti mjibu maombi alikuwa akiendelea kufanya kazi, hivyo kumstahilisha alipwe mshahara na nauli ya kurudi Tanzania. iii. Kwamba Pamoja na Ushahidi wa upande wa mleta maombi wakiwepo wahusika wakuu wa masuala ya malipo ya mishahara walioleza kwa kiapo utaratibu wa kulipana na 2 mazingira yaliyosababisha ukosefu wa ushahidi wa mjibu maombi kulipwa mishahara yake, mheshimiwa muamuzi alikosea kimantiki na kisheria kuamua kuwa mjibu maombi amepunjwa mshahara wa kiasi cha TZS 2,500,000/=(Millioni mbili na laki Tano) kwenye mkataba wa tarehe 26/09/2018 na 26/06/2018 uliosainiwa kati yake na mleta maombi hivyo kumstahilisha mjibu maombi alipwe kiasi cha TSH 2,500,000/=(Millioni mbili na laki Tano) tu. iv. Kwamba Mheshimiwa muamuzi alikosea kimantiki na kisheria kwa kuukubali Ushahidi wa maneno wa DW2 bila kuwa na uthibitsho wowote hasa kwa kuzingatia utaratibu na wajibu maombi katika utendaji kazi wa shahidi huyo ambaye ni afisa wa polisi. v. Kwamba Mheshimiwa muamuzi alikosea kimantiki na kisheria kwa kutoa Tuzo aliyoitoa Pamoja na hata yeye mwenyewe kuzingatia vifungu husika vya kisheria vinavyothibitisha kuwa mleta maombi alitimiza majukumu yake kama mwajiri wa mjibu maombi haya. Historia fupi ya shauri hili ni kwamba Mjibu Maombi aliajiriwa na Mleta maombi tarehe 26/09/2018 kwa mkataba wa muda maalumu wa miezi (3) mitatu, kama Fundi Mchundo. Katika mahusiano haya, ilidaiwa 3 na mjibu maombi kwamba baada ya kuisha mkataba ulioanza tarehe 26/09/2018 hadi tarehe 26/12/2018, mahusiano ya kiajira yaliendelea na mleta maombi hakuweza kulipa baadhi ya mishahara kwa muda aliofanya kazi mjibu maombi, jambo lililopelekea kufunguliwa kwa mgogoro huu mbele ya Tume. Tume iliyakubali madai ya mleta Maombi kwa kigezo kwamba ushahidi unaonyesha mjibu maombi alifanya kazi kwa mleta maombi kwa muda wa miezi sita, hivyo kufanya madai haya kuwa ya msingi, ambapo mleta maombi aliamriwa kumlipa mjibu maombi fidia ya mapunjo ya mshahara na nauli jumla ya kiasi cha TSH 7,400,000/= (Milioni saba na laki nne). Maamuzi hayakumpendeza mleta maombi, jambo hivyo kusababisha kufunguliwa kwa shauri la Marejeo mbele ya Mahakama hii. Pamoja na maombi ya faragha, mleta maombi aliambatanisha kiapo chake, ambacho kinaeleza mtririko mzima wa mgogoro huu uliopelekea maombi haya kama ilivyoelezwa hapo juu, ambapo mleta maombi anadai fidia ya mapunjo ya mshahara na stahiki za usafiri. Maombi haya yalipingwa na Mjibu Maombi Kupitia kiapo kinzani kilichoapwa na David Saliva Komba, Mjibu Maombi ambaye alidai mkataba wa mwanzo ulijihuisha wenyewe. Kiapo kinzani kimesisitiza kuwa mjibu maombi alikoma kulipa mishahara kwa mjibu maombi kwa 4 mujibu wa makubaliano yao. Kiapo kinzani kimekanusha maelezo yote ya msingi kuhusu yaliyosemwa katika kiapo cha mleta maombi. Shauri hili lilisikilizwa kwa njia ya mdomo ambapo, mleta Maombi aliwakilishwa na Wakili Mrs. Makalle, na Mjibu Maombi aliwakilishwa na Muwakilishi binafsi Bw. Pascal Temba. Katika mawasilisho wakili wa mleta maombi aliziunganisha hoja zote nne za kisheria katika hoja kuu mbili. Katika hoja ya kwanza, kama kulikuwa na mahusiano ya kiajira, Bi. Makalle akirejea kifungu cha 61 cha Labour Institutions Act Cap 300 R.E 2019, kinachotoa vigezo vya mtu kuonekana kuwa mwajiriwa, alieleza kigezo mojawapo ni kama mtu anafanya kazi kwa maelekezo ya mtu mwingine, na kama mtu amefanya kazi kwa masaa 45 kwa mwezi kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita. Bi. Makalle alieleza kuwa mahusiano yaliyokuwepo kati ya mleta maombi na mjibu maombi yalitokana na mkataba wa tarehe 26/9/2018 mpaka tarehe 26/12/2018. Aliwasilisha ya kwamba Mkataba wa wadaawa unaongozwa na kifungu cha 14 (1) (a) & (b) cha sura ya 366 kinachoeleza aina za mikataba, ambapo ni wazi mkataba wa mjibu maombi ulikuwa ni wa kazi maalum, muda maalum na ulikuwa ni wa maandishi. Aliendelea kueleza kwamba pande zote zilitimiza masharti na mjibu maombi alitoa kielelezo DI ambacho ni mkataba wa ajira wa 5 kuanzia tarehe 26/9/2018 hadi tarehe 26/12/2018. Kwa mujibu wa Mrs Makale, kwa vile kazi ilifanyika na kumalizika hii inatafsirika kwamba Mkataba uliheshimiwa. Mrs Makale aliendelea kuwasilisha kwamba baada ya tarehe 26/12/2018, hakuna Ushahidi wowote wa kuwepo kwa mahusiano ya kikazi kati ya wadaawa hawa wawili na kwamba mjibu maombi kwamba kulikuwa na mkataba mwingine kati ya April 2019 na June 2019. hayajathibitishwa na ushahidi wowote kama inavyotakiwa na Sheria ya Ushahidi, Sura ya 6 iliyorejewa 2022 kinachomtaka yeyote mwenye madai kuyathibitisha. Alipinga usahihi wa kibali ambacho kimeandikwa kireno na kufanyiwa tafsiri (kielelezo D-2). Kwa mujibu wa Mrs Makale, kibali siyo mkataba kwa tafsiri ya Kifungu cha 14 (2) sura ya 366 R.E 2019 na isitoshe kibali hicho hakikuandikwa kwa mleta maombi Kassim Engineering Co. Ltd. Amepinga tume kupokea kibali hicho kama mkataba wakati hata kibali chenyewe hakina mahusiano na mleta maombi kwani kilitolea kwa Camel Oil na siyo kwa mleta maombi. Aliendelea kupinga kibali hicho kwa kukosa kuonyesha ni kipindi gani ambacho mjibu maombi amefanya kazi. Kibali hicho kielelezo D-2 kilisema tu alifanya kazi toka April na June 2019. Alisizitiza kwamba itoshe kusema kwamba Tume haikuwa sahihi kupokea kibali hiki kama mkataba kwa sababu nilizotamka. 6 Mrs Makale alikosoa kibali kusomeka kutolewa tarehe 10/6/2019 wakati mjibu maombi anadai kufanya kazi kati ya April 2019 na June 2019. Alihoji kibali kupokelewa kama kielelezo wakati kilitolewa mwishoni mwa muda wa unaosemekana kuwa mkataba unaodaiwa kuwa hai. Kwa maoni yake, kibali hutolewa kabla ya kuanza kazi na siyo mwishoni, na alihoji mjibi maombi aliwezaje kwenda Msumbiji wakati kibali hakijatolewa. Mrs. Makale alieleza kuna ushahidi kuwa mjibu maombi alikuwepo Dar es Salaam baada ya Disemba 2018 na kuhoji aliondokaje na kurudi bila maandishi ya makubaliano kama kweli kulikuwa na mahusiano ya ajira. Alirejea ukurasa wa 10 wa Tuzo aya ya 2, ambapo inaonyesha kuwa kibali kilitolewa na mamlaka ya Malawi. Alisisitiza vibali ni jukumu la mwajiri na siyo la mfanyakazi na Mwajiri alipopata kazi aliorodhesha watu wote wanaohitajika, na kuingia nao mkataba na nyaraka zote zinakuwa za mleta maombi na vibali vinatakiwa kuwa vya aina tatu ambavyo ni; (1) cha kuingia chini Msumbiji (2) kibali cha kazi (3) kibali cha kufanyia kazi bandarini. Alisisitiza kuwa bila vibali hivi mfanyakazi haruhusiwi kufanya kazi bandarini na hivyo Mleta maombi asingeweza kuruhusu kazi ifanyike bila kibali na kwamba mwaka 2018 vibali vyote hivi vilipatikana lakini hakukuwa na kibali cha kufanya kazi bandarini hadi 2021 na kilihusu Tanzania tun a siyo bandarini Msumbiji. Mleta 7 maombi anaamini Tume ilikosea kukubali hiki kibali na kukitumia kama ushahidi unaothibitisha mahusiano ya kiajira. Mrs. Makale, akirejea Ukurasa wa 3 wa Tuzo aya ya 5, alieleza kuwa wakati wa Ushahidi wa mwajiri, alisema anayetafuta kazi ambaye ni mwajiri, anawasiliana na mteja, safari hii Camel Oil, na vibali hutolewa kwa mwajiri maana yeye ndiye mwenye mkataba na passport na hivyo hakuna mawasiliano ya moja kwa moja kati ya mwajiriwa na mteja. Alihoji ni kwa nmana gani mjibu maombi alipata kibali na kwa mkataba upi. Aliongeza kuwa hata wakiaminishwa kwamba kibali ni sahihi, bado hakitoshi kuthibitisha mahusiano ya kiajira kwani kilitolewa wakati hakuna mkataba. Mrs Makella aliwasilisha kuwa kwa vile hakuna mkataba uliotolewa na mleta maombi kuthibitisha ajira na mjibu maombi baada ya tarehe 26/12/2018 basi Mahakama itamke kuwa kibali hicho siyo mkataba. Kuhusu dai la kupunjwa malipo ya TZS 7,400,000/= kama ilivyoorodheshwa katika ukurasa wa 14 wa Tuzo, Mrs. Makella alieleza ya kwamba mashahidi wakiwa kwenye kiapo walitambua matakwa ya kifungu cha 15 (15) cha sura ya 366 ya 2019 kwamba ni jukumu la mwajiri kuweka nyaraka lakini walieleza haikuwezekana nyaraka kutolewa kutokana na ugumu wa mazingira. Aliendelea kueleza kwamba mashahidi walithibitisha kuwa malipo yalifanyika baada ya mkataba wa 8 kwanza na waajiriwa wote kurudishwa Dar es salaam isipokuwa malipo ya mwezi mmoja na nusu ambayo yalifanyika kwa mikupuo kwani mteja alipata changamoto za fedha na kuzitoa kidogo kidogo hivyo kusababisha malipo ya mwisho kuwa March 2019 wakati wafanyakazi wote wakiwa Dar es salaam. Mrs Makella amenaomba Mahakama iyapitie maombi na kukubaliana na hoja za kwenye kiapo na mawasilisho ya mdomo na kutengua uamuzi wa Tuzo iliyotolewa na Tume kwani ni batili na pia aliomba nafuu nyingine yoyote. Akijibu hoja bishaniwa, Bw. Temba aliwasilisha ya kwamba kwa mujibu wa kifungu cha 61 (a) (b) & (g) cha sura ya 366, ni ukweli kulikuwa na mahusiano ya kiajira kama inavyoonekana katika Kielelezo D-l ambacho ni Mkataba wa ajira uliosainiwa tarehe 26/09/2018 ambao ulienda hadi tarehe 26/12/2018. Kwa maoni yake, Mkataba huu ulihuishwa tena (by default) baada ya kuisha muda wake na mahusiano yale yaliendelea kwa masharti yale yale, na hii inathibitishwa na malipo yaliyokuwa yakiendelea kufanyika kutoka kwa mleta maombi wenda kwa mjibu maombi kama invyoonekana katika Exhibit D-3 ambayo inaonyesha miamala ya Tigo Pesa iliyofanywa baada ya mkataba wa awali kuisha. Aliongeza kuwa kielelezo D-2, ambacho ni kibali cha tarehe 10/6/2019 kutoka Msumbiji ni uthibitisho kuwa 9 kulikuwa na mahusiano ya kiajira kati ya pande mbili. Akirejea ukurasa wa 10, aya ya 3 ya tuzo, alisema vibali vya kazi huandaliwa na kampuni yenye kazi Msumbiji kwa maana hiyo kibali kusoma jina la Camel Oil ni sahihi kwani kilitolewa kwa taarifa zilizotumwa na mleta maombi. Bw. Temba alieleza vibali havikupatikana vyote kwa mujibu wa DW1 na ndicho kilichosababisha kazi kushindwa kufanyika na kurudi tena April 2019 hadi June 2019. Akirejea ushahidi wa PW1, Bwana Temba alieleza kuwa ilithibitika kuwa awali vibali havikutolewa na kusababisha mjibu maombi kukamatwa na uhamiaji Msumbiji na ndipo mteja Camel Oil alifuatilia vibali hivyo na kuwakabidhi wafanyakazi. Kwa maoni yake mahusiano yalikuwepo ndiyo maana malipo yaliendelea kufanyika kama ilivyo katika kielelezo D-3 kwa pamoja ambacho ni miamala ya Tigo Pesa iliyolipwa kwa mjibu maombi. Bw. Temba alisema hakuna kielelezo chochote kutoka kwa mleta maombi kilichothibitisha ukomo wa mkataba wa ajira, na hivyo ana maoni kuwa kulikuwa na mwendelezo wa mkataba mwingine baada ya ule wa kwanza kuisha. Akijibu hoja kama kibali cha kazi kinaweza kuwa mbadala wa mkataba wa ajira, Bw. Temba alirejea kifungu cha 15 cha sura ya 366 iliyorejewa 2019, na kusema kuwa mwajiri anatakiwa kuandaa taarifa zote zinazohusiana na ajira ya mfanyakazi na kwamba Mleta maombi alishindwa kutekeleza kifungu hicho kwa kushindwa kutoa taarifa hizo io au maelezo ya kina ambapo hata katika kielelezo DI ambacho ni mkataba ulioandaliwa na mleta maombi, hakuna maelezo kama inavyotakiwa na kifungu cha 15 (a)-(i). Alirejea kielelezo P-3 kwa Pamoja ambacho ni kibali kinachoonyesha mahusiano ya ajira kati ya mleta maombi na mjibu maombi. Akirejea ukurasa wa 10 wa tuzo aya ya 3 Bw. Temba aliifahamisha Mahakama kuwa kibali Exhibit P3 kilichotolewa kwa Camel Oil kwa lugha ya kireno kinathibitisha mahusiano ya mleta maombi na mjibu maombi. Bw. Teemba alikataa matumizi ya kifungu 110 cha sura ya 6 ya Sheria ya Ushahidi iliyorejewa 2022, dhidi ya Mjibu maombi na kusema kwamba Kifungu cha 15 (5) cha sura ya 366 kinamtaka mwajiri atunze kumbukumbu za mwajiriwa kwa muda usiopugua miaka mitano na hivyo kwa mleta maombi kushindwa kuwa na vielelezo vya mahusiano ya kiajira, ni wazi kuwa maelezo ya mjibu maombi yanapaswa kupokelewa kama yalivyo na jukumu la kuthibitisha kurudi kwa mleta maombi. Kwa mujibu wa Bw Temba, ni wazi kuwa mleta maombi hakuwa akikamilisha taratibu zote za upatikanaji wa vibali jambo lililoleta madhila na manyanyazo kwa mjibu maombi katika serikali ya Msumbiji ambapo alikamatwa na kuwekwa kizuizini. Aliiomba Mahakama ikubaliane na ii uamuzi wa CMA wa tarehe 29/11/2022 na kutupilia mbali maombi ya marejeo kwa kuwa hayana mashiko. Wakili Makale aliwasilisha hoja jazilishi akisema kuwa mikataba ya ajira inaongozwa na Sura ya 366 iliyorejewa 2019 vifungu vya 14 na 15 kwa ujumla wake na hakuna mahali panaposema kuwa vibali vya ajira ni sehemu ya mkataba. Kuhusu matakwa ya kifungu cha 15 cha Sura ya 366, Wakili Makale alisema kuwa mwajiri alionyesha mkataba ambao mjibu maombi aliridhika nao na kwenda kufanya kazi Msumbiji akiamini kwamba matakwa yote ya Mkataba wa ajira yamezingatiwa. Aliendelea kusisitiza kuwa kibali chenyewe hakimhusu mleta maombi, kwani hakikutolewa kwa Kassim Engineering ambaye ndiye alikuwa mjibu maombi. Alisema kuwa Mjibu maombi alirudi Msumbiji kivyake na kuishi kivyake ndiyo maana anashindwa kuthibitisha mkataba. Mrs Makale alisisitiza kuwa malipo ya mwezi wa tatu hayana uhusiano na Mkataba wa Aprili kwani malipo ya mwisho yalikuwa Machi. Baada ya kuzingatia mawasilisho ya pande zote mbili Mahakama inaona kuna hoja mbili (2) zinazobishaniwa ambazo ni:- 1. Je Waleta Maombi wameweza kuibua hoja ya msingi itakayoifanya Mahakama hii ifanye marejeo katika uamuzi uliotolewa na tume katika Mgogoro wa Kikazi Na. CMA/DSM/KIN/603/2020/432/20 12 2. Nini nafuu za kila upande? Katika kuanza kujibu hoja ya kwanza, Mahakama itazingatia hoja zilizoibuliwa na mleta Maombi katika kiapo chake, ikiwepo hoja ya kwamba ni je palikuwepo na uhusiano wa kiajira kati ya wadaawa, na je Muamuzi alikuwa sahihi kwa kutumia Kielelezo D-2 (kibali cha kazi) katika kutoa uamuzi. Kwa kuanza na hoja endapo palikuwepo na uhusiano wa kiajira kati ya wadaawa Wakili Mrs Makalla anakataa uwepo wa uhusiano huo akiwa na hoja kwamba mahusiano yaliisha na mkataba wa ajira ya muda ulioanza tarehe 26/9/2018 mpaka tarehe 26/12/2018 kwa kazi maalumu. Upande wa pili ulipinga na kudai kuwepo kwa mahusiano ya kiajira, ambapo Bw. Temba alieleza ya kwamba baada ya mkataba wa maandishi wa awali, mkataba ulihuishwa tena mara mbili hivyo kupelekea kuwa na mda wa miezi sita. Katika ngazi ya Tume, muamuzi aliona kuwa mkataba ulihuishwa na kwamba madai ya mjibu maombi ni ya msingi. Baada ya kuzingatia hoja za wadaawa, inaonekana kuwa mgogoro mkubwa upo katika hoja ya endapo kulikuwa na mahusiano ya kiajira yatokanayo na mkataba kujihuisha (Renewal by default). Mahusiano ya kiajira yanasimamiwa na mkataba ambao mwajili ameingia na mwajiriwa Pamoja na sheria za ajira. Katika shauri hili, hakuna ubishi mkataba 13 ulikuwa wa maandishi na wa muda maalumu. Katika hali ya kawaida, mkataba wa muda maalumu hufika ukomo siku ya mwisho ya makataba. Mkataba huo unaweza kujihuisha wenyewe (renewal by default) kutokana na mazingira fulani. Mazingira hayo yameelelezewa katika Kanuni ya 4 ya T.S Na. 42 la 2007 ambayo inaeleza kwamba; - 4(3) Subject to sub rule (2) a fixed term contract may be renewed by default if an employee continues to work after the expiry ofthe fixed term contract and circumstances warrants it. ( 4) Subject to sub-rule (3), the failure to renew a fixed-term contract in circumstance where the employee reasonably expects a renewal of the contract may be considered to be an unfair termination." Kutokana na kifungu tajwa ni wazi kwamba mkataba unaweza huishwa iwapo mwajiriwa ataendelea kufanya kazi baada ya mkataba wake wa awali kuisha. Swali linalojitokeza ni kama mjibu maombi aliendelea kufanya kazi baada ya mkataba wa awali kuisha. Kwa mujibu wa mjibu maombi, kulikuwa na mwendelezo wa ajira baada ya mkataba wa awali kuisha na alithibitisha hili kwa kuonyesha kibali cha ajira (Kielelezo D2) kilichotolewa na Serikali ya Msumbiji kwa Kampuni ya Camel Oil ambayo ilikuwa mteja wa mleta maombi. Alionyesha pia malipo yaliyofanyika mwezi March 2019 (Kielelezo D3) baada ya Mkataba wa awali kuwa 14 umeisha mwezi December 2018. Akijibu ushahidi huu, mleta maombi alitoa ushahidi kukataa uhusika wa kampuni yake na upatikanaji wa kibali cha ajira. Pia alitoa ushahidi kueleza kwamba malipo ya mishahara yalikuwa ni amlipo ya mishahara wa mkataba wa awali ambao ulimalizika mwezi December 2018. Kwa vile mleta maombi alikanusha kwa ushahidi kuhusu uhusika wake na kibali cha ajira na suala la uhusika wa malipo ya March 2023 na mkataba mpya, lilibaki kuwa ni jukumu la mjibu maombi au mwajiriwa kuwasilisha ushahidi zaidi kuonyesha mahusiano ya kiajira. Haswa ushahidi zaidi unahitajika kuonyesh ni namana gani mjibu alihusika katika kupata kibali cha ajira, na kuonysa kama malipo yaliyoishia March 2019 hayana uhusiano na mkataba uliopita ambao unaosemekana kuwa malipo hayakukamilika. Kielelezo DI kina kiambatanisho cha mchanganuo wa malipo yote ya mkataba wa awali amboyo jumla yake ni TZS 4,500,000 ambayo ni jumbla ya miezi mitatu ya makataba wa awali. Pia natofautiana na maoni wa muamuzi kwamba kibali cha ajira (Kielelezo D-2) kinaweza kusimama badala ya mkataba wa ajira. Kibali cha ajira na mkataba wa ajira ni vitu viwili tofauti. Kibali kinatolewa na mamlaka husika serikalini kuruhusu mtu kufanya kazi lakini hakiingilii mahusiano ya wahusika katika ajira hiyo. Mahusiano ya ajira yanatafsiriwa kutokana na sheria inayosimamia ajira husika na mkataba 15 wa mwajiri na mwajiriwa. Hi mkataba uonekane umeuhishwa lazima kuwepo na matarajio ya uhuishwaji huo kutoka kwa mwajiriwa kwa mujibu wa Kanuni ya 4 ya T.S Na. 42 la 2007 kama ilivyonukuliwa hapo juu. Narejea kesi ya Miriam E. Maro vs. Bank of Tanzania, (Civil Appeal 22 of 2017) [2020] TZCA 1789 (30 September 2020). Ilijadiliwa kwamba; - "It is the law that parties are bound by the terms of the agreement they freely enter into. We find solace on this stance in the position we took in Unilever Tanzania Ltd v. Benedict Mkasa t/a Bema Enterprises, Civil Appeal No. 41 of 2009 (unreported) in which we relied on a persuasive decision of the supreme court of Nigeria in Osun State Government v. Daiami Nigeria Limited, Sc. 277/2002 to articulate: Strictly speaking, under our laws, once parties have freely agreed on their contractual clauses, it would not be open for the courts to change those clauses which parties have agreed between themselves, it was up to the parties concerned to negotiate and to freely rectify clauses which find to be onerous. It is not role of the courts to re-draft clauses in agreements but to enforce those clauses where parties are in dispute." 16 Katokana na mkataba wa maandishi kati ya wadaawa (Exhibit DI), na kuzingatia mazingira yaliyoghubika mahusiano ya kiajira kwa kipindi hicho cha mkataba wa awali, sijaona ni masuala gani yaliweza kumshawishi mjibu maombi awe na matarajio ya kuhuishwa kwa mkataba huo wa miezi mitatu na hivyo kuendelea kufanya kazi msumbiji, tena akiwa hana hata vibali vya ajira. Nasema hivyo kwani kibali cha ajira kilitoka mwishoni mwa mkataba anaodai kuwa ni uliohuishwa na ni wazi katika kumbukumbu kwamba kibali hicho kilitafutwa na mteja wa mleta maombi na ni cha tarehe 10/06/2019 mwishoni mwa kipindi cha mkataba baada ya kuhuishwa kama anavyodai mjibu maombi. Naungana na hoja ya mleta maombi aliyohoji kama mjibu alifanyaje kazi bila kibali?. Baada ya kusema hayo, ninaomna mleta maombi ameweza kuleta hoja zinazoonyesha umuhimu wa Mahakama hii kufanya marejeo katika uamuzi wa Tume. Ni maoni yangu kwamba mjibu maombi hakuweza kuthibitisha uwepo wa mahusiano ya kiajira kati yake na mleta maombi. Hivyo ni vema mahakama hii ikaruhusu maombi haya. Kutokana na kilichojadiliwa hapo juu, nafanya marejeo katika uamuzi wa CMA katika Mgogoro wa kazi Na. CMA/DSM/KIN/603/432/20 na kutengua tuzo iliyotolewa. Maombi haya yanaruhusiwa. Katika mazingira 17 haya maombi haya ya Marejeo yamekubaliwa. Kila upande utajigharamia gharama zake katika shauri hili. Amri hii imetolewa Dar es salaam leo Tarehe 19 May 2023 KATARINA REVOCATI MTEULE JAJI 19/05/2023