kessy dickson udoba vs ukod international co ltd 2023 tzhcld 1415 11 septemba 2023
The applicant proved the existence of an employment relationship and entitlement to terminal benefits through documentary evidence, and the respondent's written promise to pay was binding. The arbitrator erred by failing to consider this evidence and by dismissing the claim in the absence of any rebuttal from the...
Source-derived case information.
- Citation
- kessy dickson udoba vs ukod international co ltd 2023 tzhcld 1415 11 septemba 2023
- Parties
- Applicant: Kessy Dickson Udoba; Respondent: Ukod International Co. Ltd
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2023
- Procedural Posture
- Labour Revision / Judgment
- Outcome
- Application for revision allowed; CMA decision set aside.
- Legal Topics
- Unfair Termination, Employment Contract, Employee Entitlements, Non Appearance of Respondent
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Kessy Dickson Udoba
Applicant
Ukod International Co. Ltd
Respondent
Procedural Posture
Labour Revision / Judgment
Legal Issues
- 1 Whether the applicant proved his claims before the Commission for Mediation and Arbitration (CMA)
- 2 Whether the arbitrator considered all evidence presented by the applicant
Ratio Decidendi
The applicant proved the existence of an employment relationship and entitlement to terminal benefits through documentary evidence, and the respondent's written promise to pay was binding. The arbitrator erred by failing to consider this evidence and by dismissing the claim in the absence of any rebuttal from the respondent.
Court Disposition
Application for revision allowed; CMA decision set aside.
Orders
- The decision of the CMA is set aside.
- The applicant is entitled to payment of TZS 1,230,500 as terminal benefits.
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DIVISHENI YA KAZI ILIYOKETI DAR ES SALAAM MAOMBI YA MAREJEO NA. 163/2023 (Marejeo yanatokana na uamuzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ya DSM iliyoketi Temeke) Tarehe 28 Mei 2023 katika Mgogoro wa Kazi Na. CMA/DSM/TEM/223/2022/149/2022 BAINA YA KESSY DICKSON UDOBA...................................... MLETA MAOMBI NA UKOD INTERNATIONAL CO. LTD.................................... MJIBU MAOMBI HUKUMU Tarehe ya mwisho ya Amri: 05/09/23 Tarehe ya Hukumu: 11/09/2023 OPIYO, J Shauri hili la marejeo limefunguliwa dhidi ya Uamuzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi katika Mgogoro wa Kazi Na. CMA/DSM/TEM/2022/149/2022. KESSY DICKSON udoba ambaye ni Mleta maombi anayeomba Mahakama itoe amri zifuatazo: - 1. Kwamba, iiependeze Mahakama yako tukufu kurejea na kutengua uamuzi wenye usajiri Na. CMA/DSM/TEM/233/2022/149/2022 ambao ulitolewa Tarehe 28/4/2023 na Mh. Nyang'uye-Muamuzi. i 2. Kwamba, Mahakama hii tukufu itoe amri nyingine yoyote ambayo inafaa kutolewa. Historia fupi ya shauri hili ni kwamba mleta maombi aliajiriwa kama Dereva kwa mkataba wa mwaka mmoja. Mahusiano ya kiajira yalikoma tarehe 31/03/2022 baada ya mwajiri kusitisha ajira ya mwombaji kwa kisingizio cha upungufu wa kazi baada ya kufungwa kwa baadhi ya vituo vya biashara. Mleta Maombi hakulizika na maaumuzi, jambo lililopelekea kufunguliwa kwa mgogoro huu mbele ya Tume. Hata hivyo Tume ilitupilia mbali madai ya Mleta Maombi kwa kigezo kwamba ameshindwa kuithibitishia Tume kuhusu madai yake, hivyo kupelekea kufunguliwa kwa maombi haya marejeo. Pamoja na hati ya faragha, Mleta Maombi aliambatanisha kiapo chake, ambacho kinaeleza mtririko mzima wa mgogoro huu uliopelekea maombi haya kama ilivyoelezwa hapo juu, ambapo Mleta maombi anadai muamuzi alikosea kisheria kwa kutozingatia uhusiano wa kiajira ambao mwenyewe alithibitisha katika uamuzi wake, pia alikosea kisheria kwa kutozingatia baadhi ya vielelezo alivyovitoa mbele ya Tume. 2 Shauri hili lilisikilizwa upande mmoja, kwa njia ya mdomo baada ya mjibu maombi kushindwa kuhuduria mahakamani kwa wito uliotolewa mara ya mwisho tarehe 03/08/2023. Mleta Maombi aliwakilishwa na Bw. Francis Mwakibinga, Mwakilishi Binafsi. Hi kutetea maombi haya mwakilishi Binafsi alianza na hoja ya kwanza ya kwamba muamuzi alishindwa kutumia vielelezo vya mleta maombi vizuri. Bw. Mwakibinga alieleza kwamba katika ukurasa wa pili, Muamuzi alijiridhisha kuwa mleta maombi alikuwa na mausiano ya kiajira na mjibu maombi kupitia kielelezo Pl(mkataba wa ajira). Aliendelea kueleza kuwa kupitia ukurasa huo huo muamuzi alikuwa na kielelezo P3 (barua ya kusitisha ajira). Katika kielelezo cha kusitisha ajira mjibu maombi alimweleza Mleta maombi kuwa atamlipa stahiki zake kwa mjibu wa sheria No. 4/2004 lakini pamoja na hayo hakuna mahali aliponyesha kutekeleza tamko au ahadi hiyo, kwani mleta maombi hakulipwa chochote. Kuhusu hoja ya pili ya kutupilia mbali maombi ya mleta maombi mbele ya Tume, Bw. Mwakibinga alieleza kwamba Muamuzi alikosea kutupilia mbali maombi ya mleta maombi ilihali mjibu maombi hakuwahi kuja mbele ya Tume kujibu chochote na katika kutupilia mbali maombi hayo 3 Mheshimiwa Mwamuzi alitumia kielelezo P4 (stahiki za uachishwaji kazi) ambacho kilikuwa ni mchanganuo wa malipo ambayo mwajiri alikubali kulipwa kama stahiki zake. Kwa maoni yake Kielelezo P4 kilichopokelewa na tume kinaonyesha hilo. Bw. Mwakibinga aliendelea kueleza kinacholalamikiwa na Mleta maombi ni kuwa hakukuwa na upingwaji wowote wa mjibu maombi, kwenye madai haya, lakini Mheshimiwa Muamuzi alivaa uhusika wa mjibu maombi na kutupilia mbali maombi hayo aliyokwisha kubali kulipa lakini yakakwama kwenye utekelezaji tu. Sababu ya tatu ni ya mjibu maombi kutotii wito wa tume, Bw. Mwakibinga alieleza kwanba Mjibu maombi alijinyima haki yake ya kutokufika mbele ya Tume. Pia Mheshimiwa Muamuzi katika uamuzi wake ukurasa wa 1 aya ya kwanza amekiri kwamba mjibu maombi alipelekewa wito ambao ulimfikia mara kadhaa lakini hakuweza kufika mbele ya Tume, na tabia hiyo ni kielelezo mpaka mbele ya Mahakama hii, ambapo ilipelekea wito wa Mahakama hii bado ameendelea kutofika na kutokutiii Mahakama kutokana na sababu ambazo zimeelezwa hapo juu. Hivyo ni maombi yao kwamba maaumuzi ya Tume yatenguliwe na mwombaji kupewa haki yake ya msingi kisheria ambayo imeelezwa kwenye sheria sawa sawa na ahadi ya mjibu Maombi._.x 4 Kwa kumalizia Bw. Mwakibinga alieleza kwamba kwakuwa mkataba wa mlalamikaji ulikuwa wa muda maalumu na ulivunjwa anaiomba Mahakama hii itengue uamuzi wa Tume na kumpatia haki zake kama alivyoomba. Baada ya kuzingatia mawasilisho ya Mleta Maombi, Mahakama inaona kuna kuwa hoja mbili (2) zinazobishaniwa ambazo Mahakama inatakiwa izitolee uamuzi ambazo ni kama mwombaji aliweza kuthibitisha maombi yake mbele ya tume na kama muamuzi alizingatia vielelezo vyote vya mwaombaji. Hoja zote mbili zitajibiwa kwa pamoja, na katika kufanya hivyo Mahakama itazingatia hoja zilizoibuliwa na Mleta Maombi katika kiapo chake. Hoja hizo ni kwamba mwajiri alikosea kisheria kwa kuona muombaji hakuthibitisha maombi yake na kutozingatia vielelzo vya mwombaji hata baada ya kubaini uwepo wa mahusiano ya kiajira kati ya Mleta maombi na mjibu Maombi. Katika kujibu hoja hizo ni wazi kwa mujibu wa kielelezo P-l(mkataba wa ajira) palikuewepo na mahusiano ya mkataba wa ajira wa mwaka mmoja ambao ulitakiwa kukoma 15/07/2021, hata hivyo kwa mujibu wa kielezo P-2 (barua ya kusitisha ajira) inaonyesha Mleta Maombi alisitishiwa ajira yake kwa ofa ya 7/ 5 kulipwa stahiki zake kwa mjibu wa Sheria ya ajira na Mahusiano Kazini, No. 4/2004 kama kielelezo P4 (stahiki za usitishwaji ajira) kinavyoonyesha, na kwa upande wa mleta maombi aliikubali ofa hiyo. Lakini pamoja na hayo hakuna mahali ilipoonyeshwa utekelezaji wa tamko hilo. Katika kesi ya Hotel Sultan Palace Zanzibar vs, Daniel Laizer & Another, Civil. Appl. No. 104 of 2004, ambayo ilirejewa katika kesi ya Ofgang Cornel Basi v. Budget Entertainment Resort Limited, Marejeo Na. 135 of 2021, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, iliyoketi Dar es salaam (haijalipotiwa) ilijadiliwa ya kwamba:- "It is elementary that the employer and employee have to be guided by agreed terms governing employment. Otherwise, it would be a chaotic state of affairs if employees or employers were left to freely do as they like regarding the employment in issue. " Kwa tafsiri isiyo rasmi ni kwamba: "/V/ muhimu kuwa mwajiri na mwajiriwa waongozwe na yaiiyomo kwenye taratibu yanayoongoza ajira. Vinginevyo itakuwa ni vurugu kama waajiriwa na waajiri wakiachwa huru kufanya wanachotaka kuhusiana na suaia ia ajira." py 6 Kutokana na kesi twajwa hapo juu ni wazi mleta maombi alikubali kulipwa stahiki zake za kuachishwa kazi kama ilivyopendekezwa na mjibu maombi, madai haya yameweza kuthibitishwa na mleta maombi kama Kielelezo Pl(barua ya usitishaji kazi) na P4 (stahiki za uachishwaji kazi) zinavyoonyesha. Ni msimamo wa kisheria ya kwamba, kwa mtu yeyote anayeahidi jambo na kumfanya mwingine aamini na kulitekeleza basi mtu huyo hubanwa na ahadi hiyo, kama ilivyojadiliwa katika kesi ya Edwin Simon Mamuya v. Adam Jona Mbala [1983 T.L.R 410 at 414 Lugakingira J (as then was) quoting Lord Denning J (as then was) in the case of Robertson & Minister of Pension (1949) 1 KB 227. Msimamo tajwa hapo juu ni wazi unambana mdaiwa kwa kuwa alishaahidi kwa maandishi kulipa stahiki za uachishwaji kazi kwa mjibu wa sharia na hata kutoa mchanganuo. Ukizingatia kuwa hakuna uthibitisho kuwa kuna stahiki yoyote aliyokwisha kulipwa kwa uachishwaji huo, kwa maoni yangu ni haki mleta maombi alipwe madai hayo ya TZS 1,230,500.00/=. Kwa maana hiyo ni dhahiri muamuzi alikosea kusema kuwa mwombaji hakuthibitisha madai yake kwa kuhoji uhalali wa kielelezo P4 kilichowasilishwa mbele yake wakafi hakuna hoja pinzani iliyoletwa na mwajiri dhidi yake. 7 Kwa kuwa sababu hizi mbili zimeweza kuthibitisha madai ya mleta maombi, mahakama inaona wazi hakuna haja ya kujadili hoja zingine, kwani ni wazi vielezlezo ikiwepo kielelezo P4 havikuweza kuzingatiwa na Muamauzi baada ya kuvipokea. Katika mazingira haya nayakubali maombi haya ya Marejeo kwa kuwa yana nguvu ya kisheria, na inatengua na kutupilia mbali maamuzi ya Tume yaliyoamua kwamba mleta maombi hakuthibitisha maombi yake. Na badala yake ninaona kwamba mwombaji aliweza kuthibitisha maombi yake na anastahili kulipwa kiasi cha shilingi za kitanzania 1,230,500/- kama alivyoomba. Kila upande utajigharamia gharama zake katika shauli hili. M. P. OPIYO, JAJI 11/09/2023 8