kk security co ltd vs majariwa musa kagoma 2021 tzhcld 353 23 agosti 2021
Termination of the respondent was procedurally unfair due to the chairperson's improper involvement in both initiating and adjudicating disciplinary proceedings, violating statutory requirements. However, reinstatement is not appropriate given the nature of security work and loss of trust; compensation for 19...
Source-derived case information.
- Citation
- kk security co ltd vs majariwa musa kagoma 2021 tzhcld 353 23 agosti 2021
- Parties
- Applicant: K.K Security Co. Ltd; Respondent: Majariwa Musa Kagoma
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2021
- Procedural Posture
- Labour Revision / Final Judgment
- Outcome
- partially allowed
- Legal Topics
- Unfair Termination, Remedies for Unfair Dismissal, Procedural Fairness in Disciplinary Proceedings
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
K.K Security Co. Ltd
Applicant
Majariwa Musa Kagoma
Respondent
Procedural Posture
Labour Revision / Final Judgment
Legal Issues
- 1 Whether the termination of the respondent was lawful
- 2 What remedies are appropriate for each party
Ratio Decidendi
Termination of the respondent was procedurally unfair due to the chairperson's improper involvement in both initiating and adjudicating disciplinary proceedings, violating statutory requirements. However, reinstatement is not appropriate given the nature of security work and loss of trust; compensation for 19 months' salary is confirmed as the proper remedy.
Court Disposition
partially allowed
Orders
- Order for reinstatement set aside
- Order for payment of TZS 3,097,000 to respondent confirmed
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA YA TANZANIA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA DIVISHENI YA KAZI ILIYOKETI PAR ES SALAAM MAOMBI YA MAREJEO NA. 822 YA 2019 BAINA YA K.K SECURITY CO. LTD.................................................................MLETA MAOMBI NA MAJARIWA MUSA KAGOMA......................................................... MJIBU MAOMBI HUKUMU Tarehe ya mwisho ya Amri: 02/08/2021 Tarehe ya Hukumu: 23/08/2021 B. E. K. MGANGA J. Shauri hili la marejeo limefunguliwa dhidi ya Uamuzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi katika Mgogoro wa Kazi Na. CMA/DSM/KIN/R.328/18/131. K.K SECURITT CO. LTD ambaye ni mleta maombi anaomba Mahakama itoe amri ya kurekebisha tuzo ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi iliyotolewa tarehe 19 Septemba, 2019 na Mhe. Mbeyale, Mwamuzi, katika Mgogoro wa Kazi Na. CMA/DSM/KIN/R.328/18/131 na kwamba Mahakama baada ya kurekebisha mwenendo, uamuzi na tuzo hiyo itoe amri ya kuiweka pembeni (set aside) tuzo hiyo. i Maombi haya yameungwa mkono na kiapo cha Mleta Maombi ambacho katika aya ya 5 kuna hoja tatu za kisheria zifuatazo: - kama Muamuzi alikuwa sahihi kisheria kuamua kwamba uachishwaji kazi wa Mjibu maombi haukuwa haiari. kama iiikuwa sahihi kisheria Muamuzi kutoa amri ya kumrudisha kazini Mjibu maombi. kama iiikuwa ni haki ya kisheria kwa Muamuzi kutoa fidia ya TZS 3,097,000/= kwa Mjibu maombi. Historia fupi ya shauri hili ni kwamba, Mjibu Maombi aliajiriwa na Mleta Maombi kama Mlinzi (Security) tarehe 25/02/2012. Inadaiwa kuwa tarehe 19/02/2019 Mjibu maombi alifukuzwa kazi kwa kigezo cha utovu wa nidhamu yaani kulala kazini na kutompigia saluti kiongozi wake wa kazi. Mjibu Maombi hakuridhika na uamuzi huo, hivyo alipeleka malalamiko yake mbele ya Tume ambayo katika uamuzi wake ilikubaliana na Maombi yake kwamba aliachishwa kazi isivyo haiari. Tume iliamuru Mjibu maombi arejeshwe kazini na alipwe Shilingi Milioni Tatu Tisini na Saba Elfu ikiwa ni stahiki yake ya mishahara ya miezi 19 alipokuwa amefukuzwa kazi. Kutokana na uamuzi huo wa Tume, Mleta Maombi (Mwajiri) amelete maombi haya akiomba uamuzi huo ubatilishwe. 2 Wakati wa kusikiliza shauri hili, Mleta Maombi alikuwa anawakilishwa na Bw. Magirari John, Wakili wa kujitegemea, na Mjibu Maombi alijieleza mwenyewe. Akifanya mawasilisho ili kuunga mkono marejeo, Wakili wa Mleta Maombi alieleza kuwa Mjibu maombi aliachishwa kazi kwa kutofuata sheria na taratibu za kazi ikiwemo kulala akiwa kazini (lindoni) na kutompigia saruti kiongozi wake wa kazi. Alidai kuwa uthibitishwaji wa tuhuma hizi uliungwa mkono na vielelezo mbalimbali ikiwemo Kielelezo R-3 (picha ya mlalamikaji), R-4 (maelezo ya wafanyakazi wengine). Hata hivyo, DW1 aliieleza Tume tuhuma mbalimbali ambazo Mjibu maombi aliwahi kuwa nazo hadi kusababisha kupewa onyo kama Kielelezo R-2 (onyo) kinavyounga mkono Ushahidi huo. Kuhusu muda wa onyo hilo kuisha, Wakili wa mleta maombi alieleza kuwa onyo la mwisho lilitolewa tarehe 15/09/2017 na Mjibu maombi alikutwa na kosa lingine tarehe 05/02/2018 ikiwa na maana kuwa kosa lilitendeka ndani ya muda kama inavyooonyesha katika ukurasa wa 5 Aya 1 ya Tuzo. Hivyo, kwa maoni ya Wakili, muamuzi alikosea kuanza kuhesabu tarehe ya mwisho ya onyo hadi tarehe ya kuachishwa kazi. Wakili wa mleta maombi alieleza kuwa, kwa hoja hii Muaamuzi alishindwa kuchambua vizuri 3 Ushahidi. Katika kuipa nguvu hoja hii, Wakili alirejea kesi mbalimbali ikiwemo kesi ya Salum Bugu v. Mariam Kibwana [1980] TLR 31. Wakili wa Mleta Maomba alidai kuwa Muamuzi alikosea kutojadili hoja inayohusiana na utaratibu uliotumiwa na Mleta Maombi kumuachisha kazi Mjibu Maombi. Maoni ya wakili ni kuwa kulikuwa na sababu ya msingi ya usitishwaji ajira tofauti na Muamuzi alivyosem? kuwa usitishwaji wa hajira haukuwa halali. Wakili alieleza kuwa ni jukumu la kisheria kwa Muamuzi kujibu hoja bishaniwa ili kuweza kuamua na kutoa Tuzo sahihi. Alirejea kesi ya Sosthenese Bruno & Diana Rose Bruno v. Flora Shauri, Rufaa ya Madai Na. 81 ya 2016, iliyoamriwa na Mahakama ya Rufani, (haijaripotiwa) wakati Mahakama hiyo iliporejea kesi ya Kukal Properties Development Ltd v. Maloo & Other [1990-1994] EA 281. Kuhusu nafuu aliyopewa Mjibu Maombi, Wakili wa Mleta Maombi alidai kuwa hata kama uachishwaji kazi haukuwa halali, muamuzi alikosea kisheria kutoa amri ya kurudishwa kazini na kulipwa stahiki zote pasipo kuzingatia mazingira ya kesi hii na hivyo kumpa mzigo mkubwa Mwajiri. Katika kuipa nguvu hoja yake, Wakili wa mleta maombi alirejea kesi ya Kirobe Mwita v. AAA Drill Manager (2014) LCCD na Kanuni ya 32(5) Taasisi ya Kazi (Miongozo ya Usuluhishi na Uamuzi). Alihitimisha kwa kusema kuwa, Muamuzi angezingatia mazingira ya shauri hili, asingetoa 4 amri ya fidia kandamizi na kumrejesha mjibu maombi kazini. Hivyo, aliomba maombi haya ya marejeo yakubal:we na uamuzi wa Tume utenguliwe na kutupiliwa mbali. Akijibu hoja za Wakili, Mjibu Maombi alijibu kwa kueleza kuwa Kielelezo R-3 (picha) kilichopokelewa na Tume, hakina uthibitisho wa kitaalamu kuwa picha hiyo muhusika ni Mjibu Maombi. Alidai kuwa hiyo ni kinyume na matakwa ya kisheria kama inavyohitajika kwa mujibu wa Kifungu cha 18(2)(a) and (b) cha Sheria ya Kieletroniki Na. 13 ya 2015 na kama ilivyojadiliwa katika kesi ya Simbanet Tanzania Limited v. Sahara Media Group, shauri la kibiashara Na. 2 la mwaka 2016. Mjibu maombi alisisitiza kuwa, katika msimamo huu wa kisheria, Muamuzi aliona picha hii haiaminiki kwa kuwa imeonyesha mtu amekaa akiwa amejiegemeza kwenye kiti na siyo kulala kama alivyodai Mleta maombi. Kuhusu heshima mbele ya viongozi (saluti), Mjibu maombi alieleza kuwa mwajiri alikuwa hana sera inayohusiana na hoja hii kinyume na Kanuni ya 11(1) ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini (Code of Good Practice) G.N No. 42 ya 2007. Katika hoja inayohusu utaratibu uliotumika kuachishwa kazi, Mjibu Maombi alieleza kuwa, Mleta Maombi katika kikao cha nidhamu kilichoketi tarehe 19/02/2018 mwenyekiti wa kikao alikuwa Madali Morice na ndiye aliyeshughulikia mgogoro huu kabla ya kufika 5 kwenye Kamati ya nidhamu. Alidai kuwa pia ndiye aliyetoa onyo tarehe 15/09/2017 na barua ya wito ya tarehe 05/02/2018 ya kuhudhuria kikao cha nidhamu cha tarehe 08/02/2018 kinyume na Kanuni ya 4(2) ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini (Code of Good Practice) G.N No. 42 ya 2007. Kuhusu nafuu, Mjibu maombi alieleza kuwa amri iliyotolewa kuwa mlalamikaji arudishwe kazini na alipwe fidia inatokana na uachishwaji kazi usio halali na ni matakwa ya kisheria chini ya Kifungu cha 40(1) cha Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini, Sura ya 366 Marekebisho ya 2019. Hivyo anaiomba Mahakama kutupilia mbali maombi haya. Katika mawasilisho ya nyongeza mleta maombi alirudia mawasilisho yake ya awali. Baada ya kusikiliza mawasilisho ya pande zote mbili naona kuna hoja mbili (2) zinazobishaniwa ambazo Mahakama inatakiwa izitolee uamuzi. Hoja hizo ni kama zifuatavyo: - 1. Je uachishwaji kazi wa mjibu maombi ulikuwa wa halali? 2. kila upande unastahili nafuu zipi? Katika kuanza kujibu hoja hii ni vyema kujielekeza katika matakwa ya Kifungu cha 37 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Sura ya 366 kama ilivyorekebishwa mwaka 2019. Kifungu hiki ndicho kinachoongoza uachishwaji kazi usio halali. Kifungu cha 37(1) cha sheria hiyo kinaeleza kuwa itakuwani kinyume cha sheria kwa mwajiri kumuachisha kazi 6 mwajiriwa isivyo halali. Na kifungu kidogo cha (2) cha kifungu hicho kinaeleza kuwa mwajiri atakuwa amemwachisha kazi mwajiriwa isivyo halali iwapo atashindwa kuthibitisha kuwa sababu za kumwachisha kazi zilikuwa za haki na halali na taratibu za kumwachisha kazi zilikuwa halali. Kwa mujibu wa kifungu tajwa hapo juu, ni wazi kuwa jukumu la kuithibitishia Mahakama kuwa uachishwaji kazi ulikuwa halali ni la mwajiri kama inavyoelekezwa katika kifungu cha 39 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini. Suala hili pia limejadiliwa katika kesi ya Tanzania Railway Limited dhidi ya Mwajuma Said Semkiwa, Marejeo Na. 239 ya 2014, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, iliyokaa Dar Es Salaam. Katika shauri hili, kumbukumbu zinaonesha kuwa Mjibu maombi aliachishwa kazi kwa utovu wa nidhamu (misconduct) kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo kushindwa kufuata taratibu zilizowekwa na mwajiri na kulala kazini kama inavyoshuhudiwa na kielelezo R-l(Barua ya kusitisha ajira). Hata hivyo, kwa mujibu wa kumbukumbu za Tume, ni wazi hakuna ubishi kuwa Mjibu maombi ameshawahi kupewa maonyo mbalimbali ikiwemo onyo la tarehe 14/03/2017. Aidha, ilidaiwa kuwa Mjibu maombi aliandika barua R2 kukiri kuchelewa kufika kazini. Nimesoma barua hiyo na kubaini kuwa Mjibu maombi alisema alichelewa kutokana na afya yake kutokuwa vizuri. Barua hiyo imetoa sababu za msingi kwa binadamu yeyote 7 kuweza kuchelewa au kutofika kazini. Ilidaiwa pia kuwa Mjibu maombi alikiri kwa barua kutofika kazini tarehe 9/9/2017. Nimesoma barua hiyo na kubaini kuwa mjibu maombi alisema hakufika kazini kwani alikwenda CMA kuhudhuria kesi Na. 653/17 kati yake na KK Security na kuwa ofisi inalifahamu suala hilo isipokuwa kiongozi wake wa Impala ndiye halifahamu. Pamoja na maelezo hayo kwenye barua hiyo, mjibu maombi alimuomba kiongozi huyo msamaha kuwa hatorudia. Hivyo, kumuachisha kazi mujibu maombi kwa kuegemea barua hizi siyo sahihi. Kwa mazingira ya shauri hili, nakubaliana na uamuzi wa Tume kuwa haukutolewa ushahidi unaothibitisha sababu za msingi za kumuachisha kazi mjibu maombi. Katika Marejeo haya Mjibu maombi alidai kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu za uachishaji kazi ambapo mwenyekiti wa kikao cha nidhamu ndiye aliyeshughulikia mgogoro huu hata kabla ya kikao cha nidhamu. Baada ya kupitia kumbukumbu za Tume, ni wazi, Mwenyekiti wa kikao kama anavyoonekana kwenye fomu ya kikao cha nidhamu ndiye pia aliyesaini barua ya tarehe 13/09/2017 na ya tarehe 14/03/2017 zote zikiwa ni onyo na zilipokelewa kama kielelezo R-l kwa pamoja. Kutokana na hayo, ni wazi Mwenyekiti alikwenda kinyume na Kanuni ya 4(2) ya Miongozo ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, TAngazo la Serikali Na. 42 la 2007 ambayo inamtaka Mwenyekiti kuwa mtu huru katika kikao cha nidhamu na 8 awe hajajihusisha na uanzishwaji wa tuhuma za mlalamikiwa. Hivyo, kitendo kilichofanywa na mwenyekiti katika maombi haya ni ukiukwaji wa taratibu za uachishaji kazi na ni kinyume na kanuni ya 13(4) ya Kanuni za Ajira na Mahusiano Kazini (Kanuni za Utendaji Bora), Tangazo la Serikali Na. 42 la 2007 kama ilivyojadiliwa na kuamriwa katika kesi ya Lucy Mandara v. Tanzania Cigarette Company Limited, Maombi ya Marejeo Na. 185 of 2020, Mahakama Kuu Dar es salaam( haijaripotiwa). Katika mazingira haya, Mahakama hii haina kigugumizi kusema kuwa palikuwa na ukiukwaji wa utaratibu wa uachishwaji kazi dhidi ya mjibu maombi. Kuhusu nafuu za kila upande, Kifungu cha 40(1) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini, Sura ya 366 Marekebisho ya 2019 kinaeleza nafuu zinazostahili kutolewa paleTume au Mahakama inapoona kuwa uachishwaji kazi haukuwa sahihi. Katika maombi haya, Tume iliamru Mjibu maombi arejeshwe kazini na alipwe Shilingi Milioni tatu na Elfu Tisini na saba (TZS 3,097,000/=). Kwa kuangalia aina ya kazi yaani shughuli za ulinzi ambapo Mjibu maombi na mleta maombi wanatakiwa kuwa na kiwango cha juu kabisa cha kuaminiana, na kwa mazingira haya ambayo kiwango hicho kimeshuka, haitakuwa busara kumrejesha Mjibu maombi Kazini. Hii ni kwa sababu, Mleta maombi anayo dhamana ya kulinda mali za wateja wake bila 9 kuvunja imani hiyo kwao na hilo litafanyika tu endapo atakuwa na wafanyakazi anao waamini kuwa nao hawatasababisha imani hiyo ivunjike kwa kuhujumiwa kwa njia moja au nyingine. Aidha, katika mazingira ambayo wafanyakazi wanatumia silaha katika shughuli zao na kukawa na uhusiano usio wa kuridhisha miongoni mwao au na mwajiri wao, kama ilivyo katika maombi haya, siyo busara kumrejesha mfanyakazi katika ajira hiyo. Hii ni kwa sababu tayari kutakuwa na kinyongo kati ya mwajiri na mwajiriwa au mwajiriwa na waajiriwa wenzake kuwa wamechangia kuhatarisha ajira yake na kuanza kulipiza kisasi. Aidha Mahakama ya Rufani kataika kesi ya National Microfinance Bank dhidi ya Leila na wenzake 2, Shauri la Rufaa ya Madai Na. 30 ya mwaka 2018, na National Microfinance Bank dhidi ya Victor Modest Banda, Shauri la rufaa ya madai Na. 29 ya Mwaka 2018, Mahakama ya Rufani iliamua na kutoa msimamo kuwa Kifungu cha a0(l) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini, Sura ya 366 Marekebisho ya 2019 kinataka mwajiriwa arudishwe kazini au alipwe mishahara isiyopungua miezi kumi na mbili na siyo yote kwa pamoja. Aidha Mahakama ya Rufani ilisema kuwa uamuzi wa Mahakama hii (Kuu) katika kesi ya Kirobe Mwita v. AAA Drill Manager iliyorejelewa katika maombi hay ana Wakili wa mjibu maombi iliamuliwa na mahakama hii kimakosa. io Kutokana na yote niliyoyajadili hapo juu, nimetengua amri ya kumrudisha kazini Mjibu maombi. Kwa kuwa nimebaini kuwa hapakuwa na sababu za msingi za kuachishwa kazi mjibu maombi, nathibitisha amri iliyotolewa na Tume kuwa Mjibu maombi alipwe Shilingi Milioni tatu na Elfu Tisini na saba (TZS 3,097,000/=) ikiwa ni stahili yake ya mishahara ya miezi 19. Hivyo maombi ya marejeo haya yamekubaliwa kwa kiasi nilichojadili na kueleza hapo juu. Kwa kuwa hili ni shauri la kikazi, kila upande utabeba gharama za kuendesha shauri hili. n