moja mapunda vs tanzania railways corporation trc 2023 tzhcld 1144 8 machi 2023
The applicant is not entitled to gratuity payments under the second and third contracts because the law prohibits double benefits for employees who are members of a social security fund. The contract terms must be interpreted in light of the governing statutes, which require that gratuity be deducted and remitted to...
Source-derived case information.
- Citation
- moja mapunda vs tanzania railways corporation trc 2023 tzhcld 1144 8 machi 2023
- Parties
- Applicant: Moja Mapunda; Respondent: Tanzania Railways Corporation (TRC)
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2023
- Procedural Posture
- Labour Revision / Judgment
- Outcome
- application dismissed
- Legal Topics
- Employment Contracts, Gratuity, Public Service Employment, Social Security Contributions, Double Benefit Prohibition
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Moja Mapunda
Applicant
Tanzania Railways Corporation (TRC)
Respondent
Procedural Posture
Labour Revision / Judgment
Legal Issues
- 1 Whether the applicant is entitled to gratuity payments under the second and third employment contracts
- 2 Whether the respondent lawfully deducted gratuity payments and remitted them to the social security fund
- 3 Whether the Commission for Mediation and Arbitration (CMA) erred in dismissing the applicant's claim
Ratio Decidendi
The applicant is not entitled to gratuity payments under the second and third contracts because the law prohibits double benefits for employees who are members of a social security fund. The contract terms must be interpreted in light of the governing statutes, which require that gratuity be deducted and remitted to the social security fund if the employee is a member. The respondent acted lawfully in making the deductions, and the applicant failed to prove entitlement to additional gratuity beyond what was remitted to the fund.
Court Disposition
application dismissed
Orders
- Each party to bear its own costs
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
MAHAKAMA KUU YA TANZANIA DIVISHENI YA KAZI PAR ES SALAAM MAREJEO NA. 364 YA 2022 MOJA MAPUNDA............................................. MLETA MAOMBI DHIDI YA TANZANIA RAILWAYS CORPORATION (TRC)................. MJIBU MAOMBI (Kutokana na Uamuzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi -1lala Katika Shauri Na. CMA/IIA/413/18/21 HUKUMU Tarehe ya amri ya mwisho: 02/03/2023 Tarehe ya hukumu: 08/03/2022 MLYAMBINA, J. Mleta maombi ameleta maombi haya ya marejeo kuiomba Mahakama hii kutengua uamuzi uiiotolewa na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (itakayojulikana kama 'TUNE') katika Shauri Na. CMA/ILA/413/18/21 uiiotolewa tarehe 16/09/2022 mbele ya Mhe. Mbeyale R. Historia ya mgogoro huu kwa ufupi ni kuwa, Mleta maombi aliajiriwa na Mjibu maombi katika nafasi ya Mkaguzi wa ndani mnamo tarehe 09/03/2009 katika mkataba wa muda wa miaka mitatu. Baada ya mkataba huo kuisha walihuisha na kuingia tena mkataba wa miaka mitatu. Hata hivyo, baada ya mkataba tajwa kuisha, wadaawa waliingia tena katika makubaliano ya mkataba mwingine wa muda wa miaka miwili ulioanza mnamo tarehe 26/03/2015 na kuisha mnamo tarehe 08/03/2016. Kumbukumbu zinaonesha kuwa katika mkataba wa pili na watatu Mjibu i maombi aliyakata malipo ya kiinua mgongo "gratuity" ya Mleta maombi tofauti na makubaliano yaliyopo katika mkataba. Hivyo basi, Mleta maombi alifikisha mgogoro huo Tume, ambapo ulisikilizwa na shauri likafukuzwa kwa kukosa mashiko. Baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya Tume, ndipo Mleta maombi amewasilisha mgogoro huu mbele ya Mahakama. Maombi haya yameambatanishwa na kiapo cha Mleta maombi, sababu za maombi za kisheria zikiwa ni zifuatazo: i. Kwamba Muamuzi alikosea kwa hoja na sheria kwa kushindwa kuoanisha ushahidi uiiotoiewa na vifungu vi/ivotajwa na pande zote husika. ii. Kwamba Mheshimiwa Muamuzi alikosea kwa hoja na sheria kwa kukiri kuwa katika mkataba wa piH kipengeie 5.5 kinampa haki Mleta maombi kuiipwa gratuity na mwisho kukataa maombi yake kuwa hastahiii kuiipwa. Hi. Kwamba Mheshimiwa Muamuzi alikosea kwa hoja na sheria kwa kuamua kuwa, kitendo cha Mleta maombi kutia Saini mkataba wa mwisho alikubali masharti ya mkataba bila kuzingatia pia kitendo cha Mjibu maombi kutia Saini kwenye mikataba yote mitatu. Pia Muamuzi anakubaii vipengele vya mkataba huo ikiwemo kum/ipa gratuity mleta maombi. iv. Kwamba Mheshimiwa Muamuzi alikosea kwa hoja na sheria kwa kuyapokea maelezo yanayohusu mwongozo wa hazina yaani barua/waraka wa tarehe 22/11/2016 ambao ulikataliwa na 2 haukupokelewa kama kielelezo kwani haukukidhi vigezo vya nyaraka stahiki zinazopaswa kupoke/ewa kwenye ushahidi. v. Kwamba Mheshimiwa Muamuzi ah'kosea kwa hoja na sheria kwa kuzingatia kielelezo DI pekee alicholeta Mjibu maombi kama ushahidi wa kumnyima gratuity M/eta maombi kisha kutoa maamuzi bila kuangalia sheria ya hitimisho la kazi Sura ya 371 Hiyotajwa kwenye barua hiyo ya kuzuia gratuity kwa Mieta maombi kuwa haikumhusu Mieta maombi. vi. Kwamba Mheshimiwa Muamuzi aiikosea kwa hoja na sheria kwa kushindwa kuchanganua kanuni D 33 kwa umoja wake na kanuni D 2 kifungu kidogo cha 1 na 2 cha Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma (Standing Orders for Public Service) kama kilivyochambuliwa kwenye maelezo ya mwisho ya Mieta maombi kule Tume na badala yake kutoa uamuzi ambao sio sahihi. vii. Kwamba Mheshimiwa Muamuzi ah'kosea kwa hoja na sheria kwa kuamua kuwa, kitendo cha Mjibu maombi kukata gratuity za M/eta maombi kwa ajili ya kujifidia michango ya mfuko wa jamii kama Mwajiri Hikua sahihi bila kutamka ni sheria ipi i/iyomuongoza kuamua hivyo. viii. Kwamba Mheshimiwa Muamuzi aiikosea katika hoja na sheria kwa kuutolea uamuzi mkataba wa mwisho pasipo kuutolea uamuzi mkataba wa pili ambao moja kwa moja aya ya 5.5 inae/eza Mieta maombi ah'pwe gratuity. ix. Mheshimiwa Muamuzi aiikosea kwa hoja na sheria kwa kusema kuwa hakuna ushahidi wowote kuwa M/eta maombi alidai gratuity katika mkataba wake wa pili kwa wakati huo kabla ya kusaini mkataba wa tatu. 3 Maombi haya yalisikilizwa kwa njia ya maandishi. Mleta maombi alijiwakilisha mwenyewe wakati Bi. Adelaida Ernest Masaua, Wakili wa Serikali akisimama kwa ajili ya Mjibu maombi. Mleta maombi alieleza kuwa kulingana na mkataba wa pili (wa tarehe 9/3/2012 ulioisha 8/3/2015) na watatu (wa tarehe 1/4/2015 ulioisha 31/3/2016), Mjibu maombi alitakiwa amlipe Mleta maombi asilimia 25% ya mshahara wake kama kiinua mgongo lakini hakufanya hivyo katika mikataba yote miwili. Aliendelea kueleza kuwa Mjibu maombi alimkata kiinua mgongo "gratuity" cha jumla ya TZS 19,656,000 (TZS 14,724,000 zilikatwa kwenye malipo ya vocha Na. 7397 ya tarehe 2/4/2015 katika mkataba wa pili na TZS 4,932,000 kwenye malipo ya vocha Na. 9488 ya tarehe 4/2016 katika mkataba wa tatu). Mleta maombi alieleza kuwa Mjibu maombi alipeleka michango ya Mleta maombi katika mfuko wa wa hifadhi ya jamii wakati kifungu cha 8(2) cha PPF Pensions Act [R.E. 2015] kinachomtaka Mwajiri kuchangia. Alifafanua zaidi kuwa Muamuzi alikosea kueleza kuwa Mleta maombi hakustahili kuiipwa kiinua mgongo na Mjibu maombi kwa kuzingatia Kanuni D33 ya Kanuniza Kudumuza Utumishi wa Umma (Standing Orders for the Public Service) za mwaka 2009 bila kusoma kanuni hiyo ambayo husomwa pamoja na Kanuni D2 (1) na (2) ya sheria hiyo. 4 Mleta maombi alieleza zaidi kuwa Mjibu maombi na Muamuzi walikosea kusema kuwa yeye alikuwa Mtumishi wa Umma. Kwa maoni yake, Mleta maombi hakuwa Mtumishi wa Umma kwa kuwa aliajiriwa kwa mkataba wa muda kulingana na Kifungu cha 3 cha Sheria ya Utumishi wa Umma (Public Service Act [PSA] Namba 8 ya Mwaka 2002). Alieleza zaidi kuwa katika mwaka 2008 hadi 2018 Mwajiriwa wa sekta yoyote alikuwa na haki ya kuchagua mfuko wa hifadhi ya jamii. Katika kuipa nguvu hoja yake alirejea Kifungu 30, 3 vyote vya Mamiaka ua udhibiti wa Mifuko ya Jamii ya mwaka 2008 na Kanuni ya Social Security Schemes (Pension Benefits Harmonization) Rules za mwaka 2014. Kwa maelezo ya Mleta maombi, kwa kupitia sheria hizo, Mleta maombi alichagua mfuko wa jamii wa PPF Pension Fund na hivyo alifungwa tu sheria hiyo na sio sheria za mifuko mingine ya jamii. Kwa maoni yake, Muamuzi hakukielewa Kifungu cha 23 cha Sheria ya Mafao ya Hitimisho la Kazi la Utumishi wa Umma [Sura ya 371 Marejeo ya Mwaka 2015]. Pia alieleza kuwa, kwa mujibu wa Vifungu Namba 3 na 5 vya Sheria ya Mafao ya Hitimisho ia Kazi, Sura 371 Mwaka 2015, Mleta maombi asingeweza pia kuwa mwanachama wa Public Service Pensions Fund (PSPF) kwa wakati mmoja. 5 Mieta maombi aliendelea kueleza kuwa Muamuzi hakutofautisha malipo ya kiinua mgongo ya kwenye mkataba na yale yanayolipwa na mfuko wa jamii. Kuipa nguvu hoja yake alirejea Vifungu vya 39(1), 3(1), 10(1), 7 vyote toka katika sura ya 371 Marejeo ya Mwaka 2015 na Kifungu cha 7(3)(h) na 7(2) vyote vya Sheria ya Kodi ya Mapato Marejeo ya Mwaka 2019. Kwa maoni yake, malipo ya kiinua mgongo ya Mwajiri kwa Mwajiriwa sio moja ya mafao yaliyotajwa katika Kifungu cha 23 cha Sheria ya Mafao ya Hitimisho ia Kazi kwa Utumishi wa Umma [Sura ya 371 marejeo ya mwaka 2015]. Akafahamisha zaidi kuwa, kifungu hicho pia hakimuhusu Mieta maombi. Mieta maombi alielezea zaidi kuwa, mikataba yote, ya kwanza, pili na tatu iliwabana wote Mieta maombi na Mjibu maombi. Kwa maoni yake, mjibu maombi kukiuka Kifungu cha 5.5 cha mkataba ni ukiukwaji wa mkataba na ukiukwaji wa Kifungu cha 8(2) Sura 372 Marejeo ya mwaka 2015. Kwa maoni yake, Mjibu maombi alitakiwa na sheria kumchangia Mieta maombi na sio Mieta maombi kujichangia mwenyewe kupitia mshahara na kiinua mgongo chake. Hivyo aliongeza; Mjibu maombi kwa kitendo hicho amevunja mkataba chini ya sheria ya Mikataba (Law of Contract Act) na hivyo anastahili kulipwa fidia ya TZS 25,000,000/=. 6 Katika kujibia hoja, Bi. Adelaida alieleza kuwa mkataba wa ajira wa Mleta maombi wa mwaka 2015-2016 uliruhusu kuiipwa kwa kiinua mgongo lakini sheria na kanuni zilibadilisha msimamo huo kwakua pia alikuwa akilipwa malipo ya pensheni. Aliendelea kueleza kuwa, mkataba huo wa Mleta maombi ulieleza wazi kuwa Mwajiriwa anayechangiwa katika mfuko wa jamii, Mwajiri angekata pesa hiyo katika malipo yake ya kiinua mgongo. Akakazia hoja yake kwa kurejea Kifungu cha 23 cha Sura ya 371 na kueleza kuwa mwajiriwa aliajiriwa kwa mkataba wa kiinua mgongo hawezi kuajiriwa tena kwa masharti ya pensheni. Aliendelea kueleza kuwa Mjibu maombi hakukiuka haki ya Mleta maombi kwani hakumkata kimakosa bali alikatwa kite kilichostahili. Kuhusiana na PPF na PSPF, alifahamisha kuwa hii yote ni mifuko ya hifadhi ambayo inapaswa kuzingatia taratibu na kwa kipindi hicho mifuko yote ya hifadhi ilikuwa imeshaunganishwa. Akaeleza kuwa hoja ya Mleta maombi haikuwa ya msingi. Bi Adelaida aliendelea kuwasilisha kuwa, wakati wa kuweka sahihi mkataba wa mwaka 2015-2016, Mleta maombi alifahamu mabadiliko hayo ya kukatwa pesa na akaweka sahihi yake. Akahitimisha kwa kuomba maombi haya yafutwe kwa kukosa mashiko ya kisheria. 7 Katika mawasilisho ya nyongeza, Mleta maombi aliwasilisha kuwa Mjibu maombi katika kutetea hoja amejikita zaidi katika mkataba wa tatu na kuuacha ule wa pili. Alieleza kuwa, Mjibu maombi hajafahamisha ni sheria au kanuni ipi iliyomuongoza kukiuka mkataba. Akaendelea kueleza kuwa mkataba wa Mleta maombi ulikoma mwaka 2016 na sheria aliyoitaja Mjibu maombi ilianza mwaka 2018 na hivyo haimfungi Mleta maombi. Aliendelea kueleza kuwa, Mjibu maombi hajaweza kueleza taratibu na sheria zipi zinazostahili kufuatwa na mifuko ya hifadhi na kisha akarudia yale aliyoyaeleza katika mawasilisho yake ya awali. Baada ya kupitia hoja za kisheria, mawasilisho ya pande zote mbili na kumbukumbu za Tume, Mahakama hii imekuwa na hoja zifuatazo za kujiuliza: i. Kama Tume Hikuwa sahihi kutokutoa amri ya malipo ya kiinua mgongo kwa mleta maombi na ii. Nini stahiki za kila upande. Katika kujibia hoja ya kwanza, hakuna ubishani kama Mleta maombi aliajiriwa na Mjibu maombi. Kulingana na mawasilisho ya pande zote mbili, mikataba iliyozua hoja ni miwili (wa mwaka 2012-2015 na 2015-2016) ambayo ni mkataba wa pili na wa tatu iliyoingiwa kati ya Mjibu maombi na Mleta maombi. 8 Mkataba wa pili katika kipengele cha 5.5 unaeleza moja kwa moja kuwa Mwajiriwa atalipwa kiinua mgongo kwa asilimia 25% na hakuna maelezo mengine yoyote yaliyoeleza kuhusiana na makato. Kwa rahisi ya rejea kipengele hicho kinasomeka kama ifuatavyo: Upon completion of the contract period the employee will be entitled to a gratuity payment calculated as 25% of the total of basic salaries paid to the employee during the contract period. (emphasis is mine) Kifungu cha 10 cha Sheria ya Mikataba [Sura ya 345 Marejeo ya Mwaka 2019] kinaeleza wazi kuwa makubaliano ni mkataba kama yatafikiwa kwa ridhaa ya wadaawa wanaotambulika kisheria. Ni vizuri kuheshimu mkataba na makubaliano yake kama ambavyo imeelezwa katika kesi ya Hotel Sultan Pares v. Daniel Laizer & Another, Civil Application No. 104 of 2004 kuwa mkataba unapaswa uheshimiwe kama wadaawa walivyokubaliana ili kukwepa migogoro. Mjibu maombi anapinga vikali madai ya Mieta maombi kwa maelezo kuwa Sheria zinakataza malipo ya kiinua mgongo mara mbili kwa mtumishi mmoja. Alirejea sheria ya mafao Kifungu cha 23 cha Sura ya 371 ya Mwaka 2015 kinachokataza malipo ya kiinua mgongo mara mbili kwa mtumishi. Kifungu hicho kinaeleza ifuatavyo: 9 No person being a member shall be entitled at any time to receive more than one benefit and in the event of a member qualifying for more than one benefit at the same time, the Board may in its discretion approve or seek the opinion of a member so qualified as to which one of the benefits was suitable to a member and the decision of the Bord shall be final. Kwa mujibu wa kifungu nukuliwa hapo juu, Mfanyakazi anatakiwa kuiipwa aina moja tu ya mafao na sio mafao yote ya kiinua mgongo kama ambavyo Mleta maombi anataka Mahakama hii iamini. Japokuwa kulikuwa na kifungu cha malipo ya asilimia 25 ya kiinua mgongo kwenye mkataba lakini masharti hayo ya kwenye mkataba yalitakiwa kuzingatia sheria zinazowaoongoza pande zote mbili katika kuingia mkataba huo. Vilevile katika mkataba husika, kipengele cha 12 cha mkataba huo pande zote mbili zimekubaliana kuongozwa na Sheria za Tanzania. Sheria ya Mafao Kifungu cha 23 cha Sura ya 371 ya Mwaka 2015 kama ilivyonukuliwa hapo juu, inakataza malipo ya kiinua mgongo mara mbili kwa Mtumishi. Hivyo basi kwa tafsiri hiyo Mahakama hii inaungana na maamuzi ya Tume kuwa Mleta maombi hastahili malipo ya gratuity anayodai katika mkataba wa pili. Pia, katika mkataba wa tatu kipengele cha 5.5 cha mkataba kinaeleza wazi kuwa endapo mwajiriwa atakuwa katika mfuko wa hifadhi io ya jamii kiinua mgongo chake kitakatwa na muajiri na kuwekwa katika mfuko huo. Kwa rahisi ya rejea kinaeleza kuwa: Upon completion of the contract period the employee will be entitled to a gratuity payment calculated as 25% of the total of basic salaries paid to the employee during the contract period. If the employee is a member of any social security fund, then the employer's contributions to social security should be deducted on payment of gratuity accordingly. [Msisitizo ni wangu] Hivyo katika mazingira hayo, mkataba wa tatu wa mwaka 2015 - 2016 ilikuwa sahihi kukatwa kwani hakuna ubishi kuwa Mleta maombi alikuwa katika mfuko wa hifadhi wa PPF na hivyo makato ya kiinua mgongo chake yalistahili kukatwa. Kwani kipengele katika mkataba kinaeleza kiinua mgongo kingekatwa na kupelekwa kwenye mfuko wowote wa hifadhi; haukuainisha ni mfuko gani wa hifadhi ambao ungekatwa na upi ambao usingekatwa. Katika kujibia hoja ya pili ya nini stahiki za kila upande, baada ya maamuzi ya hapo juu Mahakama hii inaona kuwa shauri hili halina msingi kwakuwa mleta maombi ameshindwa kuthibitisha madai yake kama ambavyo iliamuriwa na Tume. Hivyo basi shauri hili linatupiliwa mbali kwa kukosa mashiko. Kila upande utajilipia gharama zake. ii JAJI 08/03/2023 Hukumu imesomwa leo tarehe 8 Mwezi Machi, 2023 mbele ya Mieta Maombi na Wakili wa Serikali Francis Wisdom kwa niaba ya Mjibu Maombi. JAJI 08/03/2023 12