mustaquim murtaza darugar na wanzagi selemani makongoro na wenzake 2 2022 tzhcld 802 12 agosti 2022
Applicant remains liable as judgment debtor for the arbitral award since BRELA records and court findings confirm his status as director/shareholder at the relevant time; the registrar's order for imprisonment cannot be enforced due to respondent's inability to pay prison costs; court order for imprisonment is set...
Source-derived case information.
- Citation
- mustaquim murtaza darugar na wanzagi selemani makongoro na wenzake 2 2022 tzhcld 802 12 agosti 2022
- Parties
- Applicant: Mustaquim Murtaza Darugar; Respondent: Wanzagi Selemani Makongoro; Respondent: First Observer Security Ltd; Respondent: YONO Auction Mart & Co. Ltd
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2022
- Procedural Posture
- Labour Revision / Final Judgment
- Outcome
- application allowed in part
- Legal Topics
- Execution of Arbitral Awards, Director Liability, Judgment Debtor Identification
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Mustaquim Murtaza Darugar
Applicant
Wanzagi Selemani Makongoro
Respondent
First Observer Security Ltd
Respondent
YONO Auction Mart & Co. Ltd
Respondent
Procedural Posture
Labour Revision / Final Judgment
Legal Issues
- 1 Whether the applicant is liable as a director/shareholder for the arbitral award debt
- 2 Whether the registrar's order for imprisonment of the applicant as a judgment debtor is enforceable
- 3 Whether the applicant ceased to be a director/shareholder before the award was issued
Ratio Decidendi
Applicant remains liable as judgment debtor for the arbitral award since BRELA records and court findings confirm his status as director/shareholder at the relevant time; the registrar's order for imprisonment cannot be enforced due to respondent's inability to pay prison costs; court order for imprisonment is set aside as unenforceable.
Court Disposition
application allowed in part
Orders
- Order for imprisonment of applicant as judgment debtor set aside as unenforceable.
- Applicant remains liable for payment of award debt; execution to proceed by lawful means if respondent fulfills statutory requirements.
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
MAHAKAMA KUU YA TANZANIA DIVISHENI YA KAZI DAR ES SALAAM MAOMBI YA MAREJEO NA. 43 YA 2022 BAINA YA MUSTAQUIM MURTAZA DARUGAR ........................................ MLETA MAOMBI NA 1. WANZAGI SELEMANI MAKONGORO ……………….…….... MJIBU MAOMBI 2. FIRST OBSERVER SECURITY LTD ……………………..….... MJIBU MAOMBI 3. YONO AUCTION MART & CO. LTD …………..……...……… MJIBU MAOMBI HUKUMU Tarehe ilipotolewa Amri ya mwisho: 19/7/2022 Tarehe ya Hukumu: 12/8/2022 B. E. K. Mganga, J. Maelezo mafupi kuhusiana na shauri hili ni kuwa, Wanzagi Selemani Makongoro, Mjibu Maombi Na. 1 aliajiriwa tarehe 23/3/2006 na First Observer Security Ltd ambaye ni Mjibu Maombi Na. 2 katika Shauri hili kama Mlinzi. Mnamo tarehe 23/5/2017, Wanzagi Selemani Makongoro, Mjibu Maombi Na. 1 alifungua Mgogoro wa Kazi Na. CMA/DSM/ILA/R.514/2017 katika Baraza la Usuluhishi na Uamuzi (CMA) akidai kuwa Mjibu Maombi Na. 2 alimfukuza kazi tarehe 7/5/2017 bila kuwa 1 na sababu na wala bila kufuata utaratibu. Wakiwa katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Mjibu Maombi Na. 2 licha ya kuwa alikuwa na taarifa ya Mgogoro huu wa kazi, alishindwa kuhudhuria na matokeo yake Mgogoro ukasikilizwa upande mmoja. Baada ya kusikiliza ushahidi wa Mjibu Maombi Na.1, Muamuzi alitoa Tuzo kuwa Mujibu Maombi Na. 2 hakumfukuza kazi kihalali Mjibu Maombi Na. 1. Hivyo, Muamuzi alimwamuru Mjibu Maombi Na. 2 amlipe Mjibu Maombi Na. 1 jumla ya Shilingi 12,284,615/=. Mjibu maombi Na. 2 hakuridhika na Tuzo aliyopewa Mjibu Maombi Na. 1 hivyo, alifungua shauri la Marejeo Na. 310 la 2018. Mnamo tarehe 11/4/2019 Mahakama (Jaji I. D. Aboud) ilitupilia mbali Shauri hilo la Marejeo baada ya Mjibu Maombi Na. 2 kutofika mahakamani. Mnamo tarehe 4/5/2020 Mjibu Maombi Na. 1 alifungua Shauri Na. 377 la 2019 dhidi ya Mjibu Maombi Na. 2 akiomba kukamata na kuuza Nyumba ya Mleta Maombi iliyopo katika Mtaa wa Nianjema /Upendo nyuma ya Msikiti wa Udongo Bagamoyo Mjini ili kukazia Deni Tuzo. Mnamo tarehe 22/6/2020, Mheshimiwa F.A. Mtarania, Naibu Msajili alitoa amri Nyumba hiyo iuzwe. Mnamo tarehe 20/11/2020 Mahakama hii (Jaji A.E. Mwipopo) ilitengua Uamuzi huo wa Naibu Msajili baada ya Saada Abdulaziz Rais 2 kupinga na kuthibitisha kuwa Nyumba hiyo ni yake na si mali ya Mleta Maombi. Mnamo tarehe 4/11/2021, Mjibu Maombi Na. 1 aliwasilisha maombi ya kutaka kukamata na kuuza (i) Gari Na. T888 BUJ, (ii) Gari Na. T135 DAK na (iii) Gari Na. T.173 BZJ mali ya Mleta Maombi akionesha kuwa Mleta Maombi ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mjibu Maombi Na. 2. Maombi hayo yalitupiliwa mbali na Mahakama (A. Teye, Naibu Msajili) mnamo tarehe 17/7/2021 baada ya Mjibu Maombi Na.1 kushindwa kumpatia Hati za Wito Mjibu Maombi Na. 2. Mnamo tarehe 11/11/2021, Mjibu Maombi Na. 1 aliwasilisha tena maombi ya kukazia Deni Tuzo akiomba Mleta Maombi amlipe kiasi kilichotajwa kwenye Tuzo na kama akishindwa akamatwe na kufungwa kama Mfungwa wa madai. Katika maombi hayo, Mjibu Maombi Na. 1 alionesha kuwa Mleta Maombi ni Mkurugenzi Mwendeshaji na Mmiliki wa Mjibu Maombi Na. 2. Kwa upande wake, Mleta Maombi alipinga akidai kuwa aliacha kuwa Mkurugenzi na Mmiliki wa Mjibu Maombi Na. 2 tangu tarehe 24/10/2018. Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Mahakama (E.M. Kassian, Naibu Msajili) alitoa Uamuzi kuwa Deni Tuzo lilitolewa wakati Mleta Maombi ni Mkurugenzi na Mmiliki wa Mjibu Maombi Na. 2 na 3 hivyo anawajibika kulipa kiasi cha Shilingi 12,284,615/= ndani ya siku 14 na akishindwa, akamatwe na kufungwa kwa muda wa miezi sita(6). Baada ya kutoridhika na Uamuzi huo, Mleta Maombi ameleta maombi haya akiomba Mahakama itengue Uamuzi huo. Mleta Maombi katika kiapo chake amewasilisha sababu tatu (3) akiomba Uamuzi huo utenguliwe. Sababu hizo ni:- 1. Kwamba, Mheshimiwa Msajili Kassian alikosea kisheria kufuta uamuzi wa msajili wa kwanza. 2. Kwamba, Mheshimiwa Msajili alikosea kisheria kutokuonesha kuwa alilipekua na kulisoma Jalada la Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Mkoa wa Dar es Salaam na kugundua kuwa muombaji alishaondoka siku nyingi lakini kinyume na Sheria tarehe 11.11.2021 bado kwa hila anatajwa kuwa ni mmoja wa Wakurugenzi na pia kwa kushindwa kugundua kuwa Execution Na. 337/2019 ilikuwa kinyume na Sheria Mahakamani na hasa mbele ya Wasajili kwani maombi yake mengi yalifutwa kabisa hivyo hakupaswa tena kuingiza mengine mbele ya Wasajili walewale badala ya kupeleka mbele ya Mhe. Jaji na pia Msajili alipaswa kujiridhisha kama Muombaji alikuwa mmoja ya walio lalamikiwa CMA-Dar es Salaam. 3. Kwamba, Mheshimiwa Msajili alikosea kisheria kwa kutopitia karatasi ya BRELA kama inaonesha kuwa Muombaji ni mmoja ya Wakurugenzi wa Mjibu Maombi namba 2 na je mihtasari ya kumruhusu Muombaji kuondoka iliazimia kuwa Muombaji atawajibika na gharama au uwajibikaji wowote utakao jitokeza wakati wowote au la. Shauri lilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa, Mleta Maombi aliwakilishwa na Wakili Saiwello Kumwenda, wakati Mjibu Maombi Na. 1 aliwakilishwa na 4 Wakili Francis Munuo. Mjibu Maombi Na. 2 na 3 hawakuhudhuria licha ya kupewa taarifa kwa njia ya Magazeti baada ya jitihada za kuwapatia wito kwa njia ya kawaida kushindikana. Akitoa mawasilisho kwa niaba ya Mleta Maombi, Wakili Kumwenda aliiomba Mahakama itengue amri ya kutaka kumkamata Mustaquim Murtaza Darugar kutokana na Uamuzi ulitolewa tarehe 24/01/2022 na Mheshimiwa Msajili Kassian kwenye Shauri la kukazia Deni Tuzo Na. 337 la 2019. Akitoa hoja zake, Wakili wa Mleta Maombi alisema kuwa anapinga amri ya kukamatwa Mleta Maombi pamoja na amri ya kulipa kiasi cha Shilingi 12,284,615/= zinazotokana na Deni Tuzo ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA). Wakati wa mawasilisho yake, Wakili alikiri kuwa Uamuzi wa Tume (CMA) haujawahi kutenguliwa na kuwa Mahakama hii haiwezi kutengua Tuzo iliyotolewa na Tume (CMA) kupitia maombi haya bila kuwa na maombi ya kutengua Tuzo hiyo. Wakili Kumwenda alidai kuwa, Mleta Maombi alikuwa hausiki huko Tume na ndiyo maana ameleta maombi haya kupinga kukamatwa na kufungwa kama Mfungwa wa madai. Wakili alidai zaidi kuwa, aliyekuwa anahusika ni Mjibu Maombi Na. 2 ambaye ni Kampuni na kuwa mteja wake yaani Mleta Maombi siyo miongoni mwa Wakurugenzi wa Mjibu Maombi 5 Na. 2 Wakili aliendelea kufafanua kuwa, wakati Tuzo inatolewa na Tume (CMA), mteja wake alikuwa amekoma kuwa Mkurugenzi tangu tarehe 04/10/2018. Wakili Kumwenda aliongeza kuwa, Mleta Maombi siyo mdaiwa Tuzo, hivyo hawezi kukamatwa wala amri kutolewa dhidi yake. Kutokana na hayo, Wakili Kumwenda aliwasilisha kuwa Msajili alikosea kutengua Uamuzi wa Msajili mwenzake na alihitimisha kwa kuomba maombi haya yakubaliwe kwa kutengua Uamuzi wa Msajili. Kwa upande wake, Wakili Munuo kwa niaba ya Mujibu Maombi Na.1, aliwasilisha hoja kuwa, hakuna amri iliyotolewa tarehe 24/01/2022 iliyotaka Mleta Maombi kukamatwa. Wakili alifafanua zaidi kuwa, Msajili aliagiza Mleta Maombi alipe fedha na kuwa kama akishindwa akamatwe. Kwa maoni yake, Wakili wa Mjibu Maombi Na.1, hakuna amri iliyotolewa na Mahakama kumkamata Mleta Maombi. Aliendelea kufafanua kuwa mwenye uwezo wa kutoa amri ya kumpeleka Mleta Maombi Gerezani kama Mfungwa wa madai ni Jaji na siyo Msajili na kuwa Jaji hajawahi kutoa amri hiyo. Wakili Munuo aliendelea kuwasilisha hoja zake akisema kuwa, mnamo tarehe 25/02/2022 Mheshimiwa Msajili alipeleka Jalada kwa Jaji Mfawidhi ili Mleta Maombi akamatwe. Lakini wakati akiendelea na mawasilisho yake, 6 Wakili Munuo alisema kuwa Mjibu Maombi Na. 1 hana uwezo wa kulipia gharama za Magereza hivyo amri ya kukamatwa haiwezi kutekelezwa. Wakili Munuo kwa niaba ya Mjibu Maombi Na. 1 aliendelea kufafanua kuwa, hoja inayohusiana na maombi ya kupinga Tuzo ya CMA iliyoletwa na Wakili wa Mleta Maombi haiwezi kuwa sawa kwani Mleta maombi anapinga Uamuzi wa Msajili na siyo Tuzo iliyotolewa na Muamuzi (Arbitrator). Aidha, Wakili wa Mjibu Maombi Na. 1 aliendelea kufafanua kuwa, hoja kuwa Mleta Maombi hakuwa Mkurugenzi siyo sahihi kwani hiyo ilikuwa ni njia ya kukwepa Tuzo iliyotolewa na Tume. Wakili wa Mujibu Maombi Na. 1 alirejea Uamuzi wa Mahakama hii (Jaji A. Mwipopo) katika Shauri la Marejeo Na. 281/2020 (Revision No. 281/2020) uliotolewa na kuwa Mleta Maombi ni miongoni mwa Wadaiwa Tuzo (“judgment Debtor”). Wakili alihitimisha kwa kuomba maombi haya yatupiliwe mbali. Katika hoja jazilishi, Wakili wa mleta maombi alidai kuwa, maombi haya yapo sawa. Aidha, alikiri kuwa hakuna Uamuzi mwingine wa Mahakama ya juu uliotengua Uamuzi wa Mheshimiwa jaji A. Mwipopo, aliposema kuwa Mleta maombi ni Mdaiwa Tuzo. (“Judgment Debtor”). 7 Nimetathmini kwa kina hoja za pande zote katika Shauri hili ambapo Mleta Maombi anaomba amri ya kumkamata Mleta Maombi na kumfunga kama Mfungwa wa madai itenguliwe. Kwa upande mwingine, Wakili wa Mjibu Maombi Na. 1 anadai kuwa Mjibu Maombi Na. 1 hana uwezo wa kulipia gharama za Magereza na kuwa amri ya kukamatwa Mleta Maombi haiwezi kutekelezwa. Mwanzoni, Wakili wa Mjibu Maombi Na. 1 alidai katika mawasilisho yake kuwa hakuna amri iliyotolewa ya kukamatwa Mleta Maombi na kumfunga Gerezani kama Mfungwa wa madai. Nimesoma Uamuzi uliotolewa na Mheshimiwa Kassian, Naibu Msajili, ambao ndiyo chanzo cha maombi haya ya Marejeo na kubaini kuwa Mahakama ilitoa amri kuwa Mleta Maombi anatakiwa alipe kiasi cha shilingi 12,284,615/= ndani ya siku kumi na nne (14) na kuwa kama akishindwa, akamatwe na kufungwa kama Mfungwa wa madai. Kwa ufupi, amri hiyo ipo lakini utekelezaji wake utakamilika tu kama Mahakama hii (yaani Jaji wa Mahakama Kuu) atakaposaini Amri ya kumfunga Mleta Maombi kama Mfungwa wa madai hasa baada ya Mjibu Maombi Na.1 kutimiza matakwa yote ya Sheria ikiwa ni pamoja na kulipia gharama za kumtunza Mleta Maombi Gerezani. Katika mawasilisho yake, Wakili wa Mjibu Maombi Na.1 aliieleza Mahakama kuwa Mjibu Maombi Na.1 hana uwezo wa kulipa 8 gharama za kumtunza Mleta Maombi Gerezani kama Mfungwa wa madai. Kwa kuwa Mjibu Maombi Na. 1 anakiri kuwa hana uwezo wa kulipa gharama za kumtunza Gerezani Mleta Maombi kama Mfungwa wa madai, natengua amri iliyotolewa na Mheshimiwa Msajili kwani haiwezi kutekelezeka. Katika mawasilisho yake, Wakili Kumwenda kwa niaba ya Mleta Maombi, alidai kuwa Mleta Maombi siyo Mkurugenzi au Mmiliki wa Mjibu Maombi Na. 2 na hivyo hausiki na Deni Tuzo iliyotolewa na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi. Kwa upande mwingine, Wakili wa Mjibu Maombi Na.1 alidai kuwa Mleta Maombi anatumia ujanja kukwepa kutekeleza Deni Tuzo. Nimesoma Uamuzi uliotolewa na Mheshimiwa jaji Mwipopo katika Shauri kati ya Saadat Abdulaziz Rais (Mleta Maombi) na Wanzagi Selemani Makongoro na Wenzake Wawili (Wajibu Maombi), Shauri la Marejeo Na. 281/2020, Mahakama Kuu (halijaripotiwa) na kubaini kuwa Uamuzi huo unamtaja Murtakim Murtaza Daruga kuwa ni Mdeni Tuzo (Judgment debtor). Katika uamuzi huo, Pamoja na mambo mengine Mahakama hii ilisema:- 9 “…From the submissions of both parties it is clear that the plot No. 170, Block F, at Nia Njema, Bagamoyo which was attached for execution…was not a property of judgment debtor, Murtakim Murtaza Daruga”. Hakuna Uamuzi au Hukumu ya Mahakama ya Rufani iliyokwisha kutengua Uamuzi huo na kusema kuwa Murtakim Murtaza Daruga siyo Mdeni Tuzo katika shauri linalomuhusu Mjibu Maombi Na.1. Itakumbukwa kuwa Saadat Abdulaziz Rais alifungua Shauri la Marejeo Na. 281/2020, katika Mahakama hii baada ya Wanzagi Selemani Makongoro kufungua Shauri Na. 337 la 2019 akiomba nyumba iliyopo nyuma ya Msikiti wa Udongo Bagamoyo kukamatwa na kuuzwa akidai kuwa ni mali ya Murtakim Murtaza Daruga, Mdeni Tuzo. Katika Shauri hilo Mahakama iliridhika kuwa nyumba hiyo ni mali ya Saadat Abdulaziz Rais ambaye alikuwa Mleta Maombi ya pingamizi na si mali ya Murtakim Murtaza Daruga, Mdeni Tuzo. Nimesoma barua yenye Kumb. MITM/RC/113190/10 ya tarehe 04 Desemba, 2019 iliyosainiwa na Angela Kimario kwa niaba ya Msajili wa Makampuni kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kwenda kwa Msajili, Msajili Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi kuhusiana na umiliki wa “The First Observer Security Co. Limited” ambaye ni Mjibu Maombi Na. 2 katika Shauri hili na kubaini kuwa Mmiliki wake ni (i) 10 Christian Venance Kiponda (hisa 50) na (ii) Mustaquim Murtaza Daruga (hisa 50) na kuwa Wakurugenzi wake ni (i) Christian Venance Kiponda, na (ii) Mustaquim Murtaza Daruga. Barua tajwa ilieleza wazi kuwa Kampuni tajwa hapo juu haijawahi kubadilisha jina wala kupeleka kwa Msajili wa Makampuni maombi ya kubadilisha jina tangu isajiliwe tarehe 20 Novemba, 2014. Kutokana na hayo, maombi ya kutaka Mahakama hii itamke kuwa Mustaquim Murtaza Daruga siyo Mmiliki wa Mjibu Maombi Na. 2 na kuwa siyo Mdeni Tuzo, ni kuiomba Mahakama itengue Uamuzi wake kwa kupitia mlango wa nyuma. Hoja hiyo haiwezi kukubalika. Kama Mleta Maombi hakuridhika na Uamuzi wa Mahakama hii ilipomrejea kama mdeni tuzo (judgment debtor), alitakiwa kukata rufaa katika Mahakama ya Rufani. Sasa hivi Mahakama hii imefungwa mikono yake na haiweze kutamka kinyume na ilichowahi kusema. Nimesoma Hati ya Uwakilishi (Notice of Representation) ambayo Mustaquim Murtaza Daruga, Mleta Maombi, aliisaini mnamo tarehe 13/7/2020 kumteua Nyamachaguri Msamba Msenye na kuiwasilisha hapa Mahakamani tarehe 14/7/2020 na kubaini kuwa katika Hati hiyo ya Uwakilishi, Mustaquim Murtaza Daruga alionesha kuwa anuani yake ni 11 S.L.P. 21431 Dar es Salaam. Aidha alionesha kuwa Hati hiyo alipelekewa (i) Mjibu Maombi Na. 1 ambaye anuani yake haikuoneshwa, (ii) Mjibu Maombi Na. 2 ambaye anuani yake ni S.L.P. 21431 Dar es Salaam na (iii) Mjibu Maombi Na. 3 ambaye naye anuani yake haikuoneshwa. Kutokana na hayo, nimebaini kuwa wote Mleta Maombi na Mjibu Maombi Na. 2 wanatumia anuani moja. Hii inaendelea kuthibitisha kuwa Mleta Maombi na Mjibu Maombi Na. 2 wana mahusiano. Katika Hati ya Uwakilishi iliyosainiwa na Mleta Maombi na kuiwasilisha hapa Mahakamani tarehe 24/11/2021 bado inaonesha uhusiano huo kwenye anuani kati ya Mleta Maombi na Mjibu Maombi Na. 2. Mustaquim Murtaza Daruga, Mleta Maombi, alisema katika Aya ya 6 na 7 ya Kiapo chake kuwa mnamo tarehe 04/10/2018 alijiondoa katika nafasi ya Ukurugenzi wa The First Observer Security Co. Limited” ambaye ni Mjibu Maombi Na. 2 na kuwa alitoa taarifa ya maandishi TRA na Wakala wa Usajili wa Makampuni (BRELA) na kuwa tarehe 11/11/2021 alitajwa kimakosa kuwa ni mmoja wa Wakurugenzi wa Mjibu Maombi Na. 2. Kama nilivyoeleza hapo juu, barua kutoka Ofisi ya Wakala wa Usajili wa Makampuni ipo wazi kuwa Mleta Maombi ni Mwanahisa na Mkurugenzi wa Mjibu Maombi Na. 2, hivyo anawajibika na kilichofanywa na Mjibu Maombi 12 na. 2 na hawezi kukwepa. Kutokana na hayo, nakubaliana na Uamuzi wa Mheshimiwa Kassian, Naibu Msajili kuwa Mleta Maombi ni Mkurugenzi na Mwanahisa wa Mjibu Maombi Na. 2 na anawajibika kuhakikisha kuwa Deni Tuzo inatekelezwa. Maelezo ya Mleta Maombi kuwa alijiondoa kwenye Umiliki na Ukurugenzi wa Mjibu Maombi Na. 2 mwaka 2018 ni uongo. Maelezo hayo yanafanya kiapo chake chote kisiaminike. Kama nilivyoeleza hapo juu, hoja ya Wakili wa Mleta Maombi kuwa wakati Tume ya usuluhishi na Uamuzi (CMA) inatoa Tuzo iliyompa ushindi Mjibu Maombi Na. 1 alikuwa amejiuzuru nafasi ya Ukurugenzi na hakuwa Mwanahisa wa Mjibu Maombi Na. 2 si ya kweli na naitupilia mbali. Kutokana na hayo, hata Uamuzi wa W.S. Ng’humbu, Naibu Msajili uliotolewa tarehe 13/08/2021 katika Shauri kati ya Emmanuel Otto Chundu dhidi ya First Observer Security Co. Ltd, Shauri la Ukaziaji Deni Tuzo (Labour Execution) No. 309 la 2019 ambapo alisema kuwa Mleta maombi yaani Mustaquim Murtaza Daruga, hawezi kukamatwa na kufungwa kama Mfungwa wa madai kwa vile alikuwa amekoma kuwa Mkurugenzi au Mwanahisa wakati Tuzo ilikuwa imetolewa tarehe 26/10/2018, siyo sahihi. Wakili wa Mleta Maombi aliegemea katika Uamuzi huo kukosoa Uamuzi wa Mheshimiwa Kassian, Naibu Msajili ambao ndiyo chimbuko la maombi haya. Kama nilivyosema 13 Uamuzi wa Mheshimiwa Ng’humbu, Naibu Msajili haukuwa sahihi na ninakubaliana na Uamuzi wa Mheshimiwa Kassian, Naibu Msajili. Katika Uamuzi wake, Mheshimiwa Kassian, Naibu Msajili alisema kuwa Mleta Maombi alikuwa ni Mkurugenzi na Mmiliki wa Mjibu Maombi Na. 2 wakati Tuzo inatolewa nakubaliana naye. Katika Vielelezo D1 na D2 vilivyowasilishwa mbele ya Naibu Msajili, vinaonesha wazi kuwa Mleta Maombi alikuwa ni Mkurugenzi na Mmiliki wa Mjibu Maombi Na. 2. Baada ya kupitia kumbukumbu zilizomo ndani ya Jalada, nimebaini kuwa katika maombi ya kukamata Nyumba iliyopo Bagamoyo, niliyoilezea hapo juu, Mleta Maombi aliwakilishwa na Nyamachuguri Msamba Msenye na hakuna sehemu ambayo Mleta Maombi alionesha kuwa hakuwa Mkurugenzi au Mmiliki wa Mjibu Maombi Na.2. Katika maombi hayo, jambo lililopingwa ni umiliki wa Nyumba na si uhusika wa Mleta Maombi katika kuendesha au kumiliki Mjibu Maombi Na. 2. Kutokana na hayo, nakubaliana na hoja ya Wakili wa Mjibu Maombi Na. 1 kuwa Mleta Maombi anatumia mbinu kuhakikisha kuwa Deni Tuzo iliyotolewa na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi haitekelezeki. Nimebaini kuwa Mleta Maombi anatumia mbinu ya kujiondoa kwenye Ukurugenzi na Umiliki wa Mjibu Maombi Na. 2 ili kuhakikisha kuwa Tuzo iliyotolewa na Tume ya Ushuluhishi na Uamuzi 14 haitekelezeki. Jambo hili halikubaliki kwani amri ya Mahakama ikiwa ni pamoja na Tuzo zinazotolewa na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi lazima zitekelezwe. Ninakubaliana na alichokisema Mheshimiwa S.B. Fimbo, Naibu Msajili katika Uamuzi wake wa tarehe 21/4/2022 katika Shauri kati ya Wanzagi Selemani Makongoro dhidi ya First Observer Security Co. Ltd, shauri la kukazia Deni Tuzo (Execution) Na. 337 la 2019 linalowahusu wadaawa katika maombi haya aliponukuu Uamuzi wa Mahakama ya Rufani katika kesi ya TBL v. Edson Dhobe, Miscellaneous Civil Application No. 96 of 2006, kuwa:- “Court orders should be respected and complied with. Courts should not condone such failures, to do so is to set bad precedent and invite chaos” Nami naongeza kwa kusema kuwa, kutotekeleza Uamuzi wa Mahakama kunavunja utaratibu mzima wa utawala wa Sheria katika Nchi na kufanya taratibu zote za utoaji haki zionekane kuwa hazina maana na kuhatarisha mstakabali na utangamano wa Taifa. Jambo hilo halikubaliki na halivumiliki na Mahakama haiwezi kulifumbia macho. Ni vema Wadaawa wote wakafahamu kuwa hakuna hiari ya kutekeleza au kutotekeleza amri ya Mahakama mpaka pale amri hiyo itakapokuwa imetenguliwa na Mahakama ya juu. Mahakama imepewa jukumu hilo la kusimamia na kutoa 15 haki hapa Nchini kwa Mujibu wa Ibara ya 107A na 107B ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977. Jukumu hilo lazima litekelezwe bila kujali hali, jinsia, cheo, rangi, utaifa au kabila la mtu ili kulinda misingi ya Katiba ya Nchi yetu. Hivyo, kamwe mbinu zozote zenye lengo la kukwamisha utekelezaji wa amri za Mahakama hazitavumilika na lazima zipingwe kwa nguvu zote na hatua kuchukuliwa mapema iwezekanavyo dhidi ya wahusika. Kutokana na hayo, kama Mjibu Maombi Na. 1 angesema ana uwezo wa kutimiza matakwa ya Sheria ili kuwezesha Mleta Maombi afungwe kama Mfungwa wa madai, basi Mahakama hii ingetoa amri hiyo. Kwa kuwa Mjibu Maombi Na. 1 amesema hawezi kutimiza matakwa ya Sheria kumfunga Mleta Maombi, kama nilivyosema, natengua amri ya Mheshimiwa Naibu Msajili kwa sababu amri hiyo haitekelezeki. Kama Mjibu Maombi Na. 1 atakuwa tayari kukazia Deni Tuzo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria kwa kutafuta njia mbadala, basi afuate utaratibu huo. Katika shauri hili nimeona kuna mkanganyiko wa majina kwani wakati mwingine jina la mleta maombi linarejewa kama Mustaquim Murtaza Daruga na wakati mwingine kwenye maombi mengine kama Murtakim Murtaza Daruga. Kwa upande wangu naona kuwa makosa katika uandishi wa majina hayo haujaathiri na hautaathiri shauri kati ya wadaawa 16 hawa. Jambo la msingi ni kuwa majina hayo yanatakiwa kusomeka kama yanavyostahili baada ya kurekebishwa. Msimamo kama huo umewahi kuchukuliwa na Mahakama ya Rufani katika shauri kati ya Christina Mrimi v. Coca Cola Kwanza Bottlers Ltd, Shauri la rufaa (Madai) Na. 113 la mwaka 2011, ( haijaripotiwa) na Joseph Magombi v. Tanzania Natioanl Parks (TANAPA), shauri la rufaa (madai) Na. 114 la mwaka 2016, (harijaripotiwa). Kutokana na yote niliyosema hapo juu, nakubali maombi haya isipokuwa maombi kuhusiana gharama na natengua Uamuzi wa kutaka kumkamata Mleta Maombi na kumfunga kama Mfungwa wa madai kwa vile Mjibu Maombi Na. 1 hana uwezo wa kukidhi vigezo vilivyowekwa kwa Mujibu wa Sheria ili kuhakikisha Mleta Maombi anapelekwa Gerezani kama Mfungwa wa madai. Hukumu hii imetolewa leo tarehe 12 Agosti, 2022. B. E. K. Mganga JUDGE 17 Hukumu hii imesomwa leo tarehe 12 Agosti 2022 mbele ya Francis Munuo, Wakili wa Mjibu Maombi Na.1 bila kuwepo Mleta Maombi na Wajibu Maombi wengine. B. E. K. Mganga JUDGE NBN 18