ezekiah tom oluoch vs katibu mkuu kiongozi another 2022 tzhc 10420 1 july 2022
The applicant established a prima facie case for judicial review, showing arguable grounds that his dismissal violated principles of natural justice, was conducted by authorities lacking jurisdiction, and breached statutory and constitutional rights. The application was timely and the applicant has sufficient interest.
Source-derived case information.
- Citation
- ezekiah tom oluoch vs katibu mkuu kiongozi another 2022 tzhc 10420 1 july 2022
- Parties
- Applicant: Mwl. Ezekiah Tom Oluoch; Respondent: Katibu Mkuu Kiongozi; Respondent: Mwanasheria Mkuu wa Serikali
- Court
- TZHC
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 July 2022
- Procedural Posture
- Miscellaneous Civil Application / Ruling on Leave to Apply for Judicial Review
- Outcome
- Leave to apply for judicial review granted.
- Legal Topics
- Judicial Review, Natural Justice, Employment Termination, Freedom of Association
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Mwl. Ezekiah Tom Oluoch
Applicant
Katibu Mkuu Kiongozi
Respondent
Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Respondent
Procedural Posture
Miscellaneous Civil Application / Ruling on Leave to Apply for Judicial Review
Legal Issues
- 1 Whether the applicant was dismissed from public service in violation of principles of natural justice
- 2 Whether the authorities involved had jurisdiction to dismiss the applicant
- 3 Whether the applicant was denied the right to be heard
Ratio Decidendi
The applicant established a prima facie case for judicial review, showing arguable grounds that his dismissal violated principles of natural justice, was conducted by authorities lacking jurisdiction, and breached statutory and constitutional rights. The application was timely and the applicant has sufficient interest.
Court Disposition
Leave to apply for judicial review granted.
Orders
- Applicant granted leave to file substantive application for judicial review.
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA (MASIJALA KUU) DAR ES SALAAM MAOMBI MADOGO NA.10 YA MWAKA 2022 MWL. EZEKIAH TOM OLUOCH................. MLETA MAOMBI DHIDI KATIBU MKUUU KIONGOZI.....................MJIBU MAOMBI WA KWANZA NA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI................ MJIBU MAOMBI WA PILE. UAMUZI WA UPANDE MMOJA. Tarehe ya amri ya mwisho: 23/06/2022 Tarehe ya Uamuzi: 01/7/2022 BEFORE: 5.C. MOSHI, J. Maombi haya yameletwa kwa mujibu wa kifungu cha 2 (1) (3) cha the judicature and application of laws Act [sura ya 358 MAREJEO YA MWAKA 2019], kifungu cha 18(1), 19(2) na (3) cha the Law Reform (Fatal Accidents and Miscellaneous Provisions ) Act, [CAP 310 MAREJEO YA MWAKA 2019], Kanuni ya 5 (1), (2) na (3) ya the Law Reform (FatalAccidents and Miscellaneous Provisions) (Judicial Review Procedure and Fees) ya mwaka 2014 (Tangazo la serikali Na. 324 ya mwaka 2014 na l kifungu cha 95 cha the Civil Procedure Code, [Sura ya 33. MAREJEO YA MWAKA 2019]. Katika maombi haya Mwombaji anaomba mahakama itoe amri zifuatazo: 1. KWAMBA, ikiipendeza mahakama tukufu itoe kibali cha mahakama ill aweze kuleta maombi ya amri ya certiorari ya mahakama kufuta na kutupilia mbali barua ya Katibu Mkuu Kiongozi ya tarehe 06 Januari mwaka 2022 yenye Kumb. Na. CAB.30/536/PF.636/15, iliyomjulisha Mleta Maombi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitupilia mbali rufaa aliyokata kwake na kuthibitisha adhabu ya kufukuzwa kazi kwenye utumishi wa umma kama ilivyoamriwa na Tume ya utumishi wa walimu kama mamlaka ya kwanza ya rufaa. 2. KWAMBA, gharama za kesi itolewe kwa mieta maombi 3. KWAMBA, mahakama itoe nafuu yoyote ambayo itaona inafaa. Maombi haya yaliungwa mkono na kiapo cha mleta maombi Mwalimu Ezekiah Oluoch. Aidha aliwasilisha maelezo ya maombi kwa maandishi. Maelezo mafupi ya maombi haya ni kwamba, Mleta Maombi aliajiriwa kwenye utumishi wa umma tangu tarehe 01 Julai mwaka 1993 na mwajiri wake alikuwa ni Katibu Mkuu wa iliyokuwa wizara ya Elimu na utamaduni ambayo kwa sasa ni wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Tangu awe mtumishi wa umma, hakuwahi kujulishwa kuwa mwajiri wake aiibadilika na kuwa ni Manispaa ya Ilala kwa sasa ni Jiji la Dar es Salaam. Mleta maombi akiwa ni mtumishi wa umma, alijiunga na Chama cha Walimu Tanzania 2 (CWT) ambacho ni Chama cha Wafanyakazi. Akiwa kama mwanachama wa CWT, aligombea na kuchaguliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CWT kwa muda wa vipindi vinne mfululizo kuanzia Mei, 2000 (2000-2005). Mei 2005(2005-2010), Mei 2010(2010-2015) na Mei 2015(2015-2020). Tarehe 20 Februari mwaka 2017, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma alimwandikia barua ya kumtaka aidha aache nafasi yake ya Naibu Katibu Mkuu wa CWT ili arudi kwenye utumishi wa umma au aajiriwe na CWT. Katiba ya CWT hairuhusu Kiongozi wa kuchaguliwa kwenye nafasi ya Naibu Katibu Mkuu kuajiriwa na CWT katika masharti ya kudumu. Kwa kuwa yote yalikuwa hayatekelezeki, Mleta Maombi hakufanya uchaguzi wowote ule. Matokeo yake, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma alimwandikia barua ya kumwondoa kazini mnamo tarehe 16 Machi mwaka 2017 bila kuwa na mamlaka. Mleta Maombi hakuridhika na maamuzi hayo na alifungua shauri katika Mahakama hii kwa ajili ya kuomba kibali na baada ya kibali kutolewa, alifungua shauri la mapitio ya mahakama kupinga kuondolewa kwenye utumishi wa umma. Hata hivyo, maombi hayo yalitupiliwa mbali na Mahakama hii. Mleta Maombi hakuridhika alikata rufaa Mahakama ya Rufaa kwenye Civil Appeal No. 140 ya mwaka 2018. Tarehe 06 Januari mwaka 2020 Mahakama ya Rufani ya Tanzania ilifuta mchakato wote uliomwondoa Mleta Maombi kwenye utumishi wa umma kwa sababu alihukumiwa bila ya kusikilizwa na aliyefanya maamuzi ya kumwondoa Mlalamikaji hakuwa na Mamlaka ya kumwondoa kazini Mlalamikaji. Baada ya Mahakama ya Rufani kufuta mchakato mzima uliomwondoa Mleta Maombi kwenye utumishi wa umma, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma 3 hakuridhika na maamuzi ya Mahakama ya Rufani na matokeo yake, alianzisha upya mchakato wa kumfukuza kazi Mleta Maombi kwenye utumishi wa umma. Kwa kuanzishwa upya kwa mchakato huo, Mleta Maombi alifukuzwa tena kazi na Kamati ya Nidhamu ya Tume ya Utumishi wa Walimu ya Manispaa ya Ilaia tarehe 22 Mei mwaka 2020. Mleta Maombi hakuridhika na kufukuzwa kwake kazi na alikata rufaa kwenye Tume ya Utumishi wa Walimu kama sheria inavyoelekeza lakini rufaa yake ilitupiliwa mbali. Mleta Maombi hakuridhika na maamuzi ya Tume ya Utumishi wa Walimu na alikata rufaa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama Mamlaka ya mwisho ya Rufaa. Tarehe 06 Januari mwaka 2022, Katibu Mkuu Kiongozi kwa barua yake yenye Kumb. Na. CAB.30/536/PF.636/15, alimjulisha Mleta Maombi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametupilia mbali rufaa yake na ameridhia adhabu ya kufukuzwa kazi kwenye utumishi wa umma. Mleta Maombi hakuridhika na maamuzi hayo ya Rais na aliamua kuwasilisha maombi katika Mahakama hii ili kupata kibali cha kumwezesha kufungua shauri la mapitio ya Mahakama kupinga maamuzi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Shauri hili lilipangwa kusikilizwa kwa njia ya maandishi. Upande wa mleta maombi alijisimamia yeye mwenyewe, upande wa wajibu maombi waliwakilishwa na Daniel Nyakiha, wakili wa serikali. Hata hivyo shauri lilisikilizwa upande mmoja kwa kuwa Mahakama iliagiza kuwa Mleta Maombi awasilishe maombi yake tarehe 05 Mei mwaka 2022 na wajibu maombi wawasilishe Kiapo Kinzani tarehe 12 Mei mwaka 2022. Mleta maombi awasilishe majibu kama yapo ifikapo tarehe 19 Mei mwaka 2022. Waliamriwa ifikapo tarehe 23 Mei mwaka 2022 wahudhurie mahakamani. Mleta Maombi alitii maagizo ya Mahakama na kuwasilisha maombi yake tarehe 05 Mei mwaka 2022 na kupeleka nakala kwa Mwanasheria wa Walalamikiwa ambayo ni Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali na ilipokelewa tarehe 05 Mei mwaka 2022 saa 5:59 Asubuhi. Kiambatanisho cha Muhuri wa kuthibitisha kuwa nakala ilipokelewa imeambatanishwa kama Kiambatanisho ETO- 01. Alisema kigezo cha kuzingatiwa na mahakama ili iweze kutoa kibali kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha The Law Reform (Fatal Accidents and Miscellaneous Provisions) Act (Cap. 310 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019) maombi ya kuomba mapitio ya mahakama lazima kwanza yapate kibali cha Mahakama. "An application forjudiciai review shall not be made unless a leave to file such application has been granted by the court in accordance with these Rules." Mleta Maombi anawasilisha kuwa ana hoja za kisheria zinazokidhi vigezo vya kutolewa kwa Kibali cha mapitio ya mahakama. Sababu ya kuomba kibali cha Mahakama ni kusaidia Mahakama kufanya mchujo kwa kusoma Kiapo cha Mleta Maombi pamoja na vigezo vya maombi yake ili Mahakama ijiridhishe kama kutakuwa na kesi yenye matakwa kisheria hujulikana kama prima facie case au arguable case. Msimamo wa Mahakama hii katika maombi ya kibali cha Mapitio ya 5 mahakama yaliyowasilishwa ulielezwa katika shauri la Ezekiah Tom Oluoch dhidi ya Permanent Secretary, President's Office, Public Service Management (Misc. civil Application No.30 o f 2017-unreported) ukurasa wa 5 na 6 (Mhe. Jaji Kihio kama alivyokuwa wakati huo) alisema kuwa: - "It is the law that there has to be a prima facie case before leave to apply for prerogative orders o f certiorari, mandamus, and prohibition can be granted..... Having gone through the statement and the document (annexture OL-I11 annexed to the Affidavit) I am satisfied that there is a primafacie case established by the applicant, I, therefore, agree with Mr. Heri MbHo's submission that the scenario o f allegations available constitutes primafacie case or triable issues upon which leave should be granted." Katika maombi hayo, Mleta Maombi alijenga hoja zilizokubaliwa na Mahakama kuwa alihukumiwa bila ya kusikilizwa na kuwa maamuzi ya kumfukuza kazi yalifanywa na Mtu ambaye hakuwa na Mamlaka na hoja hizo zilizokubalika kuwa zilikidhi vigezo kwa Mahakama kutoa kibali Pia kama ilivyoamriwa kwenye kesi ya Republic ex-parte Shirima vs Kamati ya Ulinzi na Usalama, Wilaya ya Singida, The Area Commissionner and the Attorney General [1983] TLR 375 ukurasa wa 385 (Mhe. Jaji Lugakingira kama alivyokuwa wakati huo) mahakama iliamua kuwa:- "there has to be a prima facie case before leave can be granted" 6 Mleta Maombi anawasilisha hoja kwamba kwa kuangalia Kiapo chake pamoja na maelezo yake, ana sababu za kisheria ambazo zinaweza kusikilizwa na Mahakama hii na kuchambua namna alivyofukuzwa kazi kwenye utumishi wa umma bila ya kuzingatia sheria zinazotawala utumishi wa umma na misingi ya utoaji haki kama zilivyoelekeza. Anaomba mahakama iridhia kuwa hoja hizo zinakidhi vigezo vya kuonyesha kuwa kuna kesi ya msingi. Sababu yake ya kwamba Mleta Maombi alihukumwa kwa kukiukwa kwa kanuni za asili ya kutoa haki (in violation of principles of natural justices); (a) Mleta Maombi alihukumiwa bila ya kusikilizwa na Rais Katika aya ya 51 na 52 ya Kiapo chake, Mleta Maombi amedai kuwa wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anasikiliza rufaa yake ya kufukuzwa kazi kwenye utumishi wa umma, hakumpa fursa ya kumsikiliza licha ya kwamba aliomba kwa maandishi kuwa apewe fursa hiyo. Katika aya ya kwanza kwenye ukurasa wa 2 wa Kiambatanisho ETO - 20 kwa maneno yaliyokolezwa wino mweusi, Mleta Maombi aliwasilisha Maombi yafuatayo kwa Rais kama Mamlaka ya Rufaa:- "...Hata hivyo, ninaomba kwamba wakati wa kusikilizwa kwa rufaa hii na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama Mamlaka ya P ili na ya mwisho ya rufaar nipewe fursa ya kusikilizwa Hi nijiteee mbele ya Mheshimiwa Rais chiniya Ibaraya 13(6)(a) ya Katiba ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania" Pamoja na maombi hayo, Rais hakuzingatia ombi hilo la Mleta Maombi na kusababisha maamuzi kufanyika ya kumfukuza kazi bila ya kumsikiliza kinyume cha Ibara ya 13(6) (a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na Marekebisho yake inayokataza mtu kuhukumiwa bila ya kupewa fursa ya kusikilizwa. Mleta Maombi anaomba apewa kibali na mahakama afungue maombi yake ya mapitio. Aidha, mleta mao alidai kwamba, hakuitwa kujitetea mbele ya Kamati ya Nidhamu ya Tume ya Utumishi wa Walimu ya Manispaa ya Ilala iliyomfukuza kazi kwenye utumishi wa umma. Katika aya ya 41 ya kiapo chake, Mleta Maombi amedai kuwa alifukuzwa kazi na kamati ya Nidhamu ya Tume ya Utumishi ya Walimu ya iliyokuwa Manispaa ya Ilala kwa sasa ni jiji la Dar es Salaam bila ya kuitwa ajitetee. Tume iliegemea taarifa na mapendekezo ya Kamati ya Uchunguzi iliyoundwa kuchunguza tuhuma dhidi ya Mleta Maombi bila ya Mleta Maombi kujua nini kiliandikwa kwenye taarifa yao ya uchunguzi na hakupewa nafasi ya kupitia ushahidi uliomtia hatiani ili ajiridhishe kama ulikuwa ni ushahidi sahihi. Kwa kuwa Mleta Maombi anadai kuwa alifukuzwa kazi bila ya kusilizwa na Kamati ya Nidhamu, anaomba kupewa fursa ya kusikilizwa na Mahakama kuthibitisha kama kweli alisikilizwa au hakusikilizwa. Alisema, mleta Maombi hakupewa nakala ya Taarifa ya uchunguzi ya Kamati ya Uchunguzi iliyoundwa kuchunguza tuhuma dhidi yake. Mleta Maombi anadai kuwa Kitendo cha kunyimwa taarifa ya uchunguzi' iliyochunguza tuhuma dhidi yake iliyotumiwa na Kamati ya Nidhamu s kumfukuza kazi, taarifa iliyorejewa na Tume ya Utumishi wa Walimu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutupilia mbali rufaa yake, ni sawa na kuhukumiwa bila ya kusikilizwa. Kwa mujibu wa aya ya 43 ya Kiapo chake na Kiambatanisho ETO-17, Mleta Maombi aliwasilisha ombi la kupewa nakala ya Taarifa ya Kamati ya Uchunguzi kwa Kaimu Katibu Msaidizi wa Tume ya Utumishi wa Walimu ya Manispaa ya Ilala ili aisome kabla ya kukata rufaa kwenye Tume ya Utumishi ya Walimu, lakini hakupewa. Aya ya 44 na 45 pia zinaeleza kuwa Mieta Maombi aliomba nakala ya Taarifa ya Kamati ya Uchunguzi kwa Tume ya Utumishi wa Walimu ili aandae utetezi wake kwenye rufaa mbele ya Tume, nako alinyimwa. Mleta Maombi anaomba apewe kibali ili awasilishe hoja kuwa alihukumiwa bila ya kusikilizwa. Alisema, waendesha mashtaka ndiyo waliobadiHka kuwa mahakimu. Katika aya ya 42, 46 na 47 ya kiapo chake, mleta maombi amedai kuwa waliokuwa waendesha mashtaka dhidi yake ndio waliobadilika na kuwa mahakimu baada ya kumaliza kuendesha mashtaka dhidi yake. Katika aya ya 42, mleta maombi amedai kuwa Subira A. Mwakibete aliyekuwa Mwendesha Mashtaka mbele ya Kamati ya Uchunguzi akiwa amewaleta Mashahidi wanne kuthibitisha mashtaka dhidi ya Mleta Maombi pia alikuwa ni Katibu wa Kamati ya nidhamu iliyomfukuza kazi mleta Maombi alikuwa ameshiriki katika hatua zote za maamuzi kama Mtendaji mwenye nguvu na ushawishi mkubwa hivyo, alikuwa ni hakimu katika kesi aliyokuwa na maslahi nayo. 9 Katika aya ya 46 na 47 Mleta Maombi ameeieza kuwa Winifrida G. Rutaindurwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu ambaye barua yake ya tarehe 05 Februari mwaka 2020 yenye Kumb. Na. TSC/C/0.1409/22 alitumiwa na Kamati ya Nidhamu kumtia hatiani Mleta Maombi na kumfukuza kazi, alishiriki katika kuamua juu ya rufaa ya Mleta Maombi kwenye Tume ya Utumishi wa Walimu kama mjumbe licha ya Mieta Maombi kuomba kwa Mwenyekiti wa Tume kuwa asiwepo kwa kuwa alikuwa na maslahi ya matokeo katika rufaa hiyo. Misingi yote hiyo imekiuka Kanuni ya ruie against bias hivyo Mleta Maombi anaomba apewe kibali ili afungue shauri la maombi ya prerogative orders. Alisema, mleta Maombi alifukuzwa kazi na wahusika ambao hawana mamlaka katika mchakato huo. Mleta Maombi amewasilisha maombi haya kwa kujenga hoja kuwa waliofanya maamuzi dhidi yake hawakuwa na Mamlaka (jurisdiction) au walikuwa na Mamlaka lakini walifanya maamuzi nje ya Mamlaka yao kama inavyofafanuliwa hapa chini: - Alisema, mleta Maombi hakuwa mtumishi wa Manispaa ya llala Katika aya ya 3 na 35 ya kiapo Chake, Mlela Maombi amedai kuwa aiipoajiriwa kwenye utumishi wa umma tarehe 01 Julai mwaka 1993, mwajiri wake alikuwa ni Katibu Mkuu, wa iliyokuwa Wizara ya Elimu na utamaduni ambayo kwa sasa ni Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Mleta Maombi alichukuliwa hatua za kinidhamu, alikuwa ni mtumishi wa Wizara ambayo ilikuwa Dodoma na hajawahi kuwa mtumishi wa iliyokuwa Manispaa ya llala kwa sasa ni Jiji la Dar es Salaam. Tume ya Utumishi wa 10 Walimu ya Manispaa ya llala ina Mamlaka ya kuwachukulia hatua za kinidhamu walimu wale tu walioajiriwa na iliyokuwa Manispaa ya llala. Kwa kuwa Mleta Maombi hakuwa mtumishi wa Manispaa ya llala, Tume ya Utumishi wa Walimu ya Manispaa ya llala haikuwa na mamlaka kisheria kuanzisha mchakato wa hatua za kinidhamu na kumfukuza kazi Mleta Maombi. Mleta Maombi anaomba apewe fursa ya kusikilizwa na Mahakama. Alisema, barua zilizotumika kumtia hatiani Mleta Maombi ziliandikwa na watu ambao hakuwa na Mamlaka. Katika aya ya 39 ya Kiapo cha Mleta Maombi, amedai kuwa barua ya tarehe 05 Februari mwaka 2020 yenye Kumb. Na. TSC/C/0.1409/22 iliyoandikwa na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu iliyotumika kumtia hatiani Mleta Maombi na hatimaye kufukuzwa kazi na barua ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ya tarehe 27 Januari mwaka 2020 iliyomwagiza Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu kumchukulia hatua za kinidhamu Mleta Maombi ziliandikwa na watu ambao hawakuwa na Mamlaka ya kuandika barua hizo hivyo, zilikuwa ni barua batili. Kwa kuwa barua hizo ndizo zilizotumika kumfukuza kazi Mleta Maombi, Mahakama inaombwa kutoa ruhusa kwa Mleta Maombi kuwasilisha maombi yake Mahakamani kupinga kufukuzwa kazi kwenye utumishi wa umma ili athibitishe kuwa barua hizo zilikuwa batili kwa kuwa ziliandikwa na watu ambao hawakuwa na mamlaka. Alisema, mamuzi batili yaliyotolewa kumfukuza kazi. Moja ya sababu zinazomsukuma mleta maombi kuomba fursa ya kusikilizwa na mahakama juu ya kufukuzwa kwake kazi ni ubatili wa ii maamuzi yenye (illegality of the decision). Mleta maombi anadai kuwa maamuzi ya kumfukuza kazi ni maamuzi batili kutokana na sababu zifuatazo:- (a) Aliomfukuza kazi hawakuwa na mamlaka kama alivyoeza hapo juu. (b) Mleta maombi alihukumiwa bila ya kusikilizwa kama alivyoeleza hapojuu. (c) Barua iliyotumika kumfukuza kazi mleta maombi haikuwasilishwa kwenye kamati ya uchunguzi ili kupata uhalali wake kisheria. Katika aya 39 ya kiapo chake mleta maombi amedai kuwa barua ya tarehe 5 februari mwaka 2020 yenye kumb. Na.TSC/C/0.1409 iliyoandikwa na katibu wa Tume ya utumishi wa Walimu iliyotumika kama ushahidi wa kumtia hatiani mleta maombi, haikuwasilishwa na mwendesha mashtaka mbele ya kamati ya uchunguzi iliyoundwa kuchunguza tuhuma za kinidhamu dhidi ya mleta maombi ili kumpa fursa mleta maombi ya kuuliza hoja kinzani juu ya uhalali wake. Mleta maombi anashangaa ni kwa vipi nyaraka ambayo haikuwasilishwa wala kupokelewa na kamati ya uchunguzi kutoka kwa mwendesha mashtaka wa Tume ya utumishi wa walimu ya manispaa ya Ilala kutumika kama ushahidi wa kumtia hatiani mleta maombi? Mleta maombi ndiye aliyewasilisha barua hiyo katika utetezi wake akidai kuwa barua hiyo iliyotumika kumwandalia hati ya mashtaka ya kinidhamu haikuwa barua halali kwa kuwa iliandikwa na mtu asiye na mamlaka. Hakuna shahidi aliyepelekwa mbele ya kamati ya uchunguzi kutetea barua hiyo hivyo haina uhalali. 12 Alitoa hoja kwamba, uamuzi wa kumfukuza kazi mleta maombi ulikiuka sheria Katika aya ya 52 ya kiapo chake mleta maombi amedai kuwa kufukuzwa kwake kazi kwenye utumishi wa umma kwa kushiriki shughuli halali za chama cha walimu Tanzania kulikiuka Ibara ya 20(1) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na merekebisho yake juu ya Freedom of Association pamoja na mikataba mingine ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia (angalia uk.20 wa kiambatanisho ETO-20). Kifungu cha 9 cha sheria ya Ajira na Mahusiano kazini ya mwaka 2004 kimetoa haki kwa mleta maombi kushiriki kwenye shughuli halali za chama cha walimu Tanzania ikiwa ni pamoja na kushiriki kwenye uchaguzi. Section 9(1) every employee shall have the right - (b) to participate in lawful activities o f the trade union (3) No person shall be discriminated against an employee on the ground that the employee:- (a) exercised or or has exercised any right under this Act or any other written law administered by the Minister (c) participate or has participated in the lawful activities o f an office bearer o f a trade union or federation for representing it or participating in its lawful activities. Mleta maombi katika aya ya 52 ya kiapo chake amedai kuwa akiwa mwakilishi wa wafanyakazi aliyechaguliwa na wafanyakazi kuwa kiongozi wao, alikuwa na kinga ya kutofukuzwa kazi kwa kushiriki katika shughuli 13 halali za chama cha waiimu Tanzania kwa mujibu wa kifungu cha 37(1) (3) (a) (ii) (iv) na (v) cha sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004 pamoja na marekebisho yake uk 20 wa kiambatanisho ETO-20. S. 3 7(1) It shall be unlawful for an employer to terminate the employment o f an employee unfairly. (3) It shall not be a fair reason to terminate the employment o f an employee- (a) for reason that- (ii) fails or refused to do anything that an employer may not lawfully permit or required the employee to do; (Hi) Exercise any right conferred by agreement, this Act or any other law (iv)Belongs, or belonged, to any trade union; or (v) Participates in the lawful activities o f a trade union, including a lawful strike. Mleta Maombi alifukuzwa kazi kwa sababu alipochaguliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Waiimu Tanzania, alikuwa akiwatetea sana waiimu hali ilyoikera serikali kama alivyoeleza kwenye aya ya 6 ya Kiapo chake na kukubaiiwa na Wajibu Maombi kwa kutokuandika Kiapo Kinzani. Kwa kuwasemea sana waiimu na wakati fulani kuingia mgogoro na serikali. Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani ilimnyima kibali cha kufanya kazi CWT na badala yake ikampa masharti ambayo hayakuwa yanatekeleza ikiwa ni pamoja na sharti la kuacha kazi CWT na kurudi kwenye utumishi wa umma kinyume cha sheria. 14 Alisema, hoja za mleta maombi hazikuzingatiwa katika mchakato wa kumfukuza kazi. Katika aya ya 52, Mleta Maombi amedai kuw hoja zake alizowasllisha kwa rais kwenye refaa yake hazikuzingatiwa na rais katika kutooa hukumu ya kutupilia mbali rufaa yake. Hoja hizi ambazo hazikuzingatiwa na rais zimebainishwa kwenye kifungu cha 5(b) (i)-(xxii) cha maelezo yake (Statement) ambapo ameorodhesha vigezo vya maombi yake. Katika kesi - Ndesamburo vs Attorney General [1997] TLR 137 katika ukurasa wa 140 maamuzi bila ya kusikiliza upande mmoja ni sawa na kufanya Maamuzi bila kusikiliza upande mwingine ambapo maamuzi yanakuwa ni batili na ni sawa na kuwa upande ambao hoja zake hazikupewa nafasi, haukusikilizwa. The principle o f naturaljustice which requires a person to be afforded opportunity to defend himself necessarily implies that the person determining the matter will consider the party's defence before making a decision which affects the rights o f such party. Failure to consider such defence is as bad aas not affording the party an opportunity o f the right o f hearing. Kwakuwa Mleta Maombi amedai kuwa hoja zake hazikusikilizwa na Rais wakati wa kuamua rufaa yake, kuna haja kwa Mahakama kumpa fursa ya kumsikiliza katika kipengele hicho sawa na vipengele vingine. Aidha Mleta Maombi alisema kwamba, alihukumiwa kwa sheria isiyomhusu. 15 Katika aya ya 3, 21, 22 na 23 za Kiapo chake, Mleta Maombi amedai yeye alikuwa ni mtumishi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknoloji wakati the Teachers Service Commission Act, 2015 na kanuni zake za mwaka 2016 zilizotumika kumfukuza kazi zilikuwa zinawahusu walimu waliokuwa waajiriwa wa serikali za mitaa na si walimu waajiriwa wa wizara ya elimu sayansi na teknolojia kama yeye hivyo, alihukimiwa kwa sheria isiyomhusu na kufanya maamuzi hayo kuwa batili. Mieta maombi alitoa hoja kwamba, pale panapotokea maamuzi kulalamikiwa hakuwa ni batili, Mahakama inapaswa kutoa fursa ya kusikilizwa kwa anayetuhumu. Huo ndio msimamo wa mahakama hii katika kesi ya Said Juma Muslim Shekimweri dhidi ya Attorney General [1997] TLR 3 ambapo mahakama hii (Mhe. Jaji Sammata, J.K kama alivyokuwa) aliamua kama ifuatavyo, uamuzi unaoungwa mkono na mleta maombi haya:- "As I understand the law,, if a decision purportedly made by an the authority which falls under the supervisoryjurisdiction o f this court is challenged on the ground that it is not valid in law or it is null and void it becomes the boundly duty o f the court to hear the aggrieved party)" Hapo ndipo mwisho wa mawasilisho ya hoja zake na mleta maombi aliiomba Mahakama hii impe kibali cha kufungua shauri la maombi ya mapitio ya mahakama. Mwombaji ameleta maombi ya kuomba kibali cha kufungua shauri la mapitio ya mahakama. Mleta Maombi ameeleza kwamba, alihukumiwa bila ya 16 kusikilizwa na Rais baada ya kupewa barua yenye kumbukumbu Na.CAB.30/536/PF.636/15 licha ya kuomba kuwa ajitetee kabla ya kupewa barua hiyo. Ameieleza kwamba wakati anafukuzwa kazi maamuzi yaliyotolewa yalikuwa batili kwa kuwa waliomfukuza kazi hawakuwa na mamlaka, mleta maombi alihukumiwa bila ya kusikilizwa kama alivyoeleza, barua iliyotumika kumfukuza kazi mleta maombi haikuwasilishwa kwenye kamati ya uchunguzi ili kupata uhalali wake kisheria na kwamba waendesha mashtaka ndiyo waliobadilika kuwa mahakimu. Baada ya kuchambua hoja katika mawasilisho yake, mwombaji anatakiwa athibitishe mbele ya mahakama hii mambo makuu matatu ya kisheria kabla ya kupewa kibali cha kufungua shauri la mapitio ya mahakama, kama ilivyoamriwa kwenye kesi ya Emma Bayo vs. the Minister for Labour and Youths Development and 2 Others, Civil Appeal No. 79/2012, (Arusha Registry), (Unreported). Kwanza kabisa anatakiwa aonyeshe kuwa kuna kesi ya msingi, pili anatakiwa kuonyesha kuwa shauri lake iimefunguiiwa ndani ya miezi sita na miezi hiyo inaanza kuhesabika tangu chanzo cha mgogoro ulivyoanza, na tatu anatakiwa aonyeshe kuwa ana Maslahi muhimu katika maombi ya msingi. Baada ya maelezo ya mleta maombi mahakama hii inajielekeza kwenye mambo ya awali na siyo kulijadili shauri hili kiundani kwenye viini vinavyoijengea kesi hii, ufafanuzi huo ulitolewa kwenye kesi ya Re Bavic International SA (Bureau Vertas 2005)2 EA 42(HCK). Baada ya kuangalia aya ya 51, 52, 41,44,45,42,46,47,3,35,39,21, na 23 ya maelezo yake na mawasilisho yake hayakupingwa hapa mahakamani 17 nimeona kuwa maelezo yake yanajitosheleza kumpa kibali cha kufungua shauri la msingi la mapitio ya mahakama kwani kuna shauri la msingi kuhusu utaratibu uliotumika kumwachisha kazi, pia ana maslahi (Interest) kwa kuwa yeye ndiye aliyeachishwa kazi, Aidha maombi haya yamaletwa ndani ya muda, angalia Kanuni ya 6 ya Law Reform Fatal Accident Provisions Miscellaneous Provision (Judicial Review Procedure & Fees) 2014 inasema kuwa: - "The leave to apply for judicial review shall not be granted unless the application for leave is made within six months after the date of the proceedings, act or omission to which the application for leave relate" Aidha kwenye kesi ya Hezron Nyachiya vs Tanzania Union of Industrial and Commercial Workers and Organization of Tanzania Workers Union, Civil Appeal No. 79 of 2001, (Dar es Salaam Registry), (Unreported), mahakama ilisema kwamba, "the time for an application for leave for prerogative orders was declared to be six (6) months. " Kwa hiyo, maombi haya yamekubaliwa baada ya kuzinqatia mambo yote yaliyojadiliwa katika uamuzi huu. Inaamriwa hivyo. 18