oliver kiwale na 15 wengine vs manish home needs industries limited 2022 tzhcld 918 29 september 2022
There is no evidence that the applicants were terminated from employment by the respondent. The Commission's decision to dismiss the claim was correct.
Source-derived case information.
- Citation
- oliver kiwale na 15 wengine vs manish home needs industries limited 2022 tzhcld 918 29 september 2022
- Parties
- Applicant: Oliver Kiwale na 15 wengine; Respondent: Manish Home Needs Industries Limited
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 29 September 2022
- Procedural Posture
- Labour Revision / Final Judgment
- Outcome
- application dismissed
- Legal Topics
- Termination of Employment, Procedural Fairness, Employment Contracts
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Oliver Kiwale na 15 wengine
Applicant
Manish Home Needs Industries Limited
Respondent
Procedural Posture
Labour Revision / Final Judgment
Legal Issues
- 1 Whether applicants were terminated from employment by the respondent
- 2 Whether proper procedures were followed in termination
Ratio Decidendi
There is no evidence that the applicants were terminated from employment by the respondent. The Commission's decision to dismiss the claim was correct.
Court Disposition
application dismissed
Orders
- Commission's decision upheld
- Each party to bear its own costs
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
MAHAKAMA KUU YA TANZANIA DIVISHENI YA KAZI PAR ES SALAAM MAREJEO NA. 223 YA 2022 OLIVER KIWALE NA 15 WENGINE................... MLETA MAOMBI DHIDI YA MANISH HOME NEEDS INDUSTRIES LIMITED .. MJIBU MAOMBI (Kutokana na Uamuzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ya DSM - Ilala) (Mbeyale : Muamuzi) Tarehe 09.10.2020 Katika CMA/DSM/ILA/1116/19/25 HUKUMU 12 & 29.09.2022 Rwizile, J Waleta maombi wameiomba Mahakama kutengua amri na uamuzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (Tume). Imeelezwa kuwa waleta maombi waliajiriwa na mjibu maombi kwa nyakati tofauti katika mikataba ya kudumu. Waliajiriwa katika nafasi tofautitofauti katika kuaendesha mashine na katika usambazaji. Mnamo mwezi Oktoba, 2019, mjibu maombi alihamisha mashine kutoka sido - Dar es Salaam Kwenda Vikindu (wilaya ya Mkuranga) bila ya kushirikisha waleta maombi. Hivyo suala hili likazua sintofahamu baina i yao. Hii ilipelekea Mwezi Desemba, 2019 waleta maombi kuomba kikao na mjibu maombi ili waweze kujua hatma yao. Mjibu maombi aliwataka waleta maombi kukaa nyumbani kwa muda wa miezi mitatu huku akiwalipa mshahara wa shilingi 100,000/=. Hawakufikia makubaliano yoyote ingawa walilipwa mshahara wa mwezi mmoja pekee. Kutoka na kutoelewa huko, mnamo tarehe 24.12.2019 waleta maombi wakafungua mgogoro wao mbele ya Tume, wakidai kwamba ajira yao ilisitishwa bila ya kufuata taratibu za kisheria. Baada ya tume kusikiliza maombi yao, iliona hayana mashiko na kwahiyo maombi yao yalitupwa kwasababu mjibu maombi hakusitisha ajira zao. Hawakuridhika na uamuzi wa Tume, maombi haya yakazaliwa. Maombi haya yameambatana na kiapo cha Oliver R. Kiwale kwa niaba ya wenzake, kikieleza sababu za maombi haya kama ifuatavyo; a. Kama waleta maombi walifukuzwa kazi b. Kama kiini cha kwanza ni ndiyo, je kulikuwa na sababu za msingi na kama taratibu zilifuatwa kuwafukuza kazi? c. Sababu muhimu za kisheria zilizojitokeza katika mwenendo mzima wa shauri na tuzo iliyotolewa na Tume ya usuluhishi na uamuzi nazo ni: - 2 i. Kwamba, muamuzi alikosea kuamua kuwa mjibu maombi hakuvunja mkataba wa ajira na waleta maombi. ii. Kwamba, muamuzi alishindwa kuuchambua ushahidi walio utoa waleta maombi mbele ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (Tume) ambapo waleta maombi walisema kuwa mjibu maombi aliwafukuza kazi kwa maneno yake mwenyewe. Bwana Ambrose Menance Nkwera aliwawakilisha waleta maombi na Bwana Mlyambelele Abedinego Levi Ng'weli alikuja kwa niaba ya mjibu maombi. Bwana Nkwera alieza kuwa mjibu maombi alivunja mkataba kwa kuwazuia waleta maombi kwenda kazini bila kuwapa stahiki zao. Alieleza kuwa ajira yaweza kisitishwa kwa njia mbili; ya maneno na maandishi. Na akaifahamisha kuwa mkataba wa waleta maombi ulisitishwa kwa maneno kama walivyoeleza katika CMAF1. Aliendelea kuwasilisha kuwa ushahidi uliotolewa na waleta maombi mbele ya Tume haukuzingatiwa. Alifafanua kuwa waleta maombi walithibitisha kufukuzwa kazi tena bila ya kufuata taratibu. Kwa maoni yake, kama wangekuwa hawajafukuzwa kazi mjibu maombi angewachukulia hatua za kinidhamu kwakuwa walikuwa na mkataba wa kudumu. Akaeleza pia 3 kuwa kwa kitendo hicho inathibitisha, waleta maombi hawajalipwa stahiki zao. Akamalizia kwa kueleza kuwa waleta maombi wote walipwe jumla ya shilingi 118,892,308.00. Bwana Mlyambelele katika kujibu hoja za waleta maombi alisema kuwa ushahidi mbele ya Tume umeeleza vizuri kuwa tarehe 22.12.2019 mjibu maombi alikuwa na kikao na waleta maombi kuhusiana na masuala yao ya kazi. Akaendelea kusema wakakubaliana kutafuta mtaalam kuhusiana na mambo yaliyojiri siku hiyo (kielelezo DI na D2). Alieleza kuwa tarehe 23.12.2019 waleta maombi wakafikisha mgogoro mbele ya Tume. Kwa maoni yake hakukuwepo na uvunjwaji wa mkataba. Aliendelea kuwasilisha kuwa kwakuwa mjibu maombi hakuwafukuza kazi waleta maombi hivyo ni jukumu lao (waleta maombi) kuthibitisha kuwa walifukuzwa kazi. Aliwasilisha pia kuwa ushahidi ulichambuliwa vema na Tume. Na akaifahamisha kuwa kiwango kilichodaiwa hakiwezi kulipwa kwakuwa waleta maombi mbele ya Tume walikuwa 39 na hapa Mahakamani wapo 16 pekee. Katika mawasilisho ya nyongeza, waleta maombi waliileza Mahakama kuwa mgogoro uliwasilishwa tarehe 24.12.2019 na sio tarehe 23.12.2019. Nakwamba watumishi 9 hawakufungua shauri, hivyo hakuna haja ya 4 kuendelea na shauri lao. Alihitimisha kwa kuomba waleta maombi walipwe stahiki zao. Baada ya kupitia mawasilisho ya pande zote mbili, Mahakama inaona kuna hoja kubwa mbili zinazobishaniwa; /. Kama ajira za waleta maombi ziiisitishwa na mjibu maombi ii. Kama taratibu ziiifuatwa katika kusitisha ajira yao Katika hoja ya kwanza, hakuna ubishi kuwa waleta maombi waliajiriwa na mjibu maombi. Pia hakuna ubishi kuwa kuna mgogoro baina yao kwa madai ya kufukuzwa kazi isivyo halali. Kifungu cha 36(a)(i)(ii)(iii)(iv) na (v) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, [Sura ya 366 Marejeo ya mwaka 2019] kinaeleza hali mbalimbali za usitishwaji wa ajira. Hali hizo ni: - /. Katika "common law" ii. Mwajiri kuweka mazingira yasiyoweza kuvumiiika kwa mwajiriwa Hi. Kushindwa kuhuisha mkataba katika masharti ya awaii au mapya iv. Kushindwa kumruhusu mfanyakazi kufanya kazi baada ya kupata Hkizo ya uzazi na v. Kushindwa kumrudisha kazini mfanyakazi 5 Waleta maombi wameieleza Mahakama kuwa ajira yao ilisitishwa tena kwa kutokufuata utaratibu. Wakati huohuo mjibu maombi alisema kuwa hakusitisha ajira yao bali hawakuelewana katika kikao na ikashauriwa kufuata ushauri wa mtaalam wa kazi lakini waleta maombi wakapeleka mgogoro mbele ya Tume. Katika kupitia nyaraka zilizowasilishwa mbele ya Tume hakuna kielelezo chochote kinachoonyesha, waleta maombi walifukuzwa kazi. Katika maelezo ya Pwl alisema kuwa ajira yao ilisitishwa kwa mdomo, ushahidi ambao ndio ulioandikwa katika CMA Fl. Mahakama imebaini katika maelezo yao, walisema ajira yao ilisitishwa katika kikao cha tarehe 22.12.2019 (kielelezo D3). Lakini kielelezo hicho hakionyeshi sehemu yoyote ambayo waleta maombi walifukuzwa kazi. Kielelezo hicho kinaonyesha kuwa waleta maombi na mjibu maombi hawakuelewana katika kikao kuhusiana na likizo na malipo ya mwezi mmoja. Kwa rahisi ya rejea kinasema: - "MUHTASARI WA KIKAO CHA WAFANYAKAZI NA MKURUGENZI WA KAMPUNIKILICHOFANYIKA KIWANDANISIDO TAREHE 22/12/2019 AGENDA: 1. UTANGULIZI 2. TAARIFA YA KUSUDIO LA KUHAMA ENEO LA OFISI 6 3. TAARIFA YA BAADHI YA MASHINEKWENDA MATENGENEZO 4. LIKIZO 5. KUFUNGA KIKAO NA. Agenda Majadiiiano Mapendekezo 1. ... ... ... 2. ... ... ... 3. ... ... ... 4. Mengineyo N/A Mkurugenzi aiiwasihi wafanyakazi kuendeiea na kazi na kuchaguana wawakiiishi wachache kuomba ufafanuzi wa kisheria idara ya kazi kuhusu hoja yoyote ambayo haijaeieweka na wengine kuendeiea na kazi kwa utaratibu wa kawaida na Mkurugenzi aiiwahakikishia wafanyakazi kuwa tayari kushiriki katika mazungumzo na chombo hicho cha Serikaii." 7 Katika kupitia kielelezo hiko hakuna sehemu yoyote ambayo inaonyesha kuwa waleta maombi walifukuzwa kazi na mjibu maombi. Kielelezo hicho kinaonyesha kuwa walishindwa kuelewana na hivyo ikashauliwa kuwa waende idara ya kazi kupata ufafanuzi wa kisheria. Baada ya waleta maombi kufanya kama ambavyo ilikubaliwa kwenye kikao wao walienda kufungua mgogoro mbele ya Tume na kufungua mgogoro wa kazi tarehe 24.12.2019. Ikumbukwe kuwa, waleta maombi walikuwa na kikao na mjibu maombi tarehe 22.12. 2019. Mgongoro wao mbele ya Tume ulifunguliwa siku mbili baadaye. Kwa kielelezo hiki, ninashawishika kusema kwamba ajira ya waleta maombi haikusitishwa. Tume ilikuwa sahihi kuamua hivyo. Hakuna ushahidi wa kuthibitisha hayo. Katika hoja ya pili, kwakuwa imethibitika kuwa waleta maombi hawakufukuzwa kazi, hakuna haja ya kushughulika na hoja ya pili. Itoshe kusema kuwa maombi haya hayana mashiko na hivyo yametupiliwa mbali. Maamuzi ya Tume, kwa mtazamo wangu yalikuwa sawa. Kwakuwa hili ni shauri la masuala ya kiajira, kila upande utajilipia gharama zake. AJGRWIZIEE------ JUDGE 29.09.2022 8