omary kombo kijangwa vs mtibwa sugar estate ltd 2021 tzhcld 138 2 juni 2021
The termination of the applicant was substantively and procedurally unfair because the reason given in the termination letter was not proven, the investigation report was not provided, and the disciplinary committee was not impartial. The applicant is entitled to compensation for the remaining period of the contract.
Source-derived case information.
- Citation
- omary kombo kijangwa vs mtibwa sugar estate ltd 2021 tzhcld 138 2 juni 2021
- Parties
- Applicant: Omary Kombo Kijangwa; Respondent: Mtibwa Sugar Estate Ltd
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2021
- Procedural Posture
- Labour Revision / Final Judgment
- Outcome
- application granted
- Legal Topics
- Unfair Termination, Procedural Fairness, Employment Contract, Remedies for Unlawful Dismissal
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Omary Kombo Kijangwa
Applicant
Mtibwa Sugar Estate Ltd
Respondent
Procedural Posture
Labour Revision / Final Judgment
Legal Issues
- 1 Whether the reasons for termination of the applicant were valid and fair
- 2 Whether the procedures for termination were fair
- 3 What remedies are due to each party
Ratio Decidendi
The termination of the applicant was substantively and procedurally unfair because the reason given in the termination letter was not proven, the investigation report was not provided, and the disciplinary committee was not impartial. The applicant is entitled to compensation for the remaining period of the contract.
Court Disposition
application granted
Orders
- The decision of the Commission for Mediation and Arbitration is set aside.
- The respondent shall pay the applicant TZS 23,066,666.72 as compensation for unlawful termination.
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA YA TANZANIA MAHAKAMA KUU DIVISHENI YA KAZI ILIYOKETI MOROGORO MAOMBI YA MAREJEO NA. 07 YA 2020 BAINA YA OMARY KOMBO KIJANGWA........................................................ MLETA MAOMBI NA MTIBWA SUGAR ESTATE LTD..................................................... MJIBU MAOMBI HUKUMU Tarehe ya Amri ya Mwisho: 18/05/2021 Tarehe ya Hukumu: 02/06/2021 A. E. MWIPOPO, J. OMARY K. KIJANGWA, ambaye ni Mleta Maombi katika shauri hili la Marejeo, ameleta maombi haya akiomba Mahakama irekebishe uamuzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi uliotolewa katika mgogoro wa kikazi Na. CMA/MORO/666/11/748 wa tarehe 21 Januari, 2020, na Mhe. K. Haji, Msuluhishi. Mleta Maombi anaomba yafuatayo: 1. Mahakama hii ikipendezwa iitishe kumbukumbu za Tume ya Usuluhishi na Uamuzi iliyoketi Morogoro kwa ajili ya kurekebisha mwenendo mzima na uamuzi wa Tume katika mgogoro wa kikazi Na. CMA/MORO/666/11/748 ambao ulitolewa Tarehe 21 Januari, 2020, i na Mhe. K. Haji, Mwamuzi, ili kujiridhisha kuhusu usahihi, uhalali, utaratibu na ustahili wake. 2. Mahakama hii ikipendezwa ifafanue juu ya malipo ya mshahara ya Mleta Maombi ya Tsh 2,500,000/= ambayo ni ya kila mwezi tangu tarehe ya kuachishwa kazi isivyo halali mpaka tarehe ya malipo ya mwisho, malipo ya usafiri, malipo ya kujikimu tangu kuachishwa kazi na malipo ya mshahara ya miezi 13 yatokanayo na uvunjwaji wa mkataba na kutoa amri ya stahiki zingine tangu tarehe ya uachishwaji kazi isivyo halali mpaka tarehe ya kurudishwa kazini au ya malipo ya mwisho ikiwepo fidia ya madhara na unyanyaswaji na stahiki zote za ajira. 3. Mahakama hii ikipendezwa ifafanue juu ya malipo ya mishahara ya Mleta Maombi na kutoa amri ya Mleta Maombi kurudishwa kazini ikiwepo stahiki zake zote tangu tarehe ya uachishwaji kazi isivyo halali mpaka tarehe ya kurudishwa kazini au ya malipo ya mwisho ikiwepo fidia ya madhara na unyanyaswaji na stahiki zote za ajira. 4. Mahakama hii pia ikipendezwa iweze kutoa nafuu yoyote itakayoona inafaa. Historia fupi ya shauri hili ni kuwa Mleta Maombi aliajiriwa na Mjibu Maombi katika nafasi ya Meneja wa ulinzi, kwa mkataba wa miaka miwili kuanzia tarehe 01/03/2017 hadi tarehe 28/02/2019. Mnamo tarehe 2 05/02/2018 ajira ya Mleta Maombi ilisitishwa na Mjibu Maombi kwa sababu ya utovu wa nidhamu. Mleta Maombi hakuridhika na uamuzi huo wa kuachishwa kazi na hivyo alifikisha mgogoro wake katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (hapa itajulikana kama Tume). Tume iliamua kwamba Mleta Maombi aliachishwa kazi kihalali hivyo hastahili malipo yoyote. Maamuzi haya ya Tume hayakumridhisha Mleta Maombi jambo lilopelekea afungue shauri hili la marejeo hapa Mahakamani. Katika shauri hili, pande zote mbili zilikuwa zinawakilishwa. Mleta Maombi alikuwa anawakilishwa na Bw. Michael D. Mgombozi, Muwakilishi Binafsi, na Mjibu Maombi anawakilishwa na Bw. Philipo Mahenge, Mwanasheria Mwandamizi wa Mjibu Maombi. Akifanya mawasilisho ya msingi kuunga mkono maombi haya, Mwakilishi Binafsi wa Mleta Maombi alieleza kuwa Mwamuzi alijiongoza vibaya kwa kutupilia mbali madai yaliyofikishwa mbele ya Tume kutokana na Uamuzi huo wa Tume kujaa kasoro nyingi za kisheria. Mwamuzi alishindwa kuviangalia viini vya mgogoro wa shauri hili na ameshindwa kubainisha ni kosa lipi lililothibitishwa kutendwa na Mleta Maombi. Katika ushahidi uliotolewa, mwajiri alishindwa kuthibitisha tuhuma zote tisa (9) alizokuwa amemshitaki Mleta Maombi. Mwakilishi Binafsi akiendelea kuwasilisha alieleza kuwa Mwamuzi alishindwa kujiongoza vema kwa kuwa baadhi ya tuhuma hazikuwa 3 Sehemu ya Hati ya Mashitaka ya kinidhamu aliyopewa Mleta Maombi. Alieleza kuwa Mwamuzi alikiri katika ukurasa wa 22 wa Uamuzi wa Tume kuwa Shahidi DW1 alikuwa na Mgogoro wa Maslahi na Mleta Maombi na aliutupa Ushahidi wake. Hii inathibitisha kuwa uachishwaji kazi ulijaa uonevu uliokithiri. Tume iliona katika ukurasa 24 wa Tuzo kuwa Mjibu Maombi hakumpatia Mleta Maombi ripoti ya uchunguzi ili aweze kujiandaa. Pia DW2 hakutakiwa kuhusishwa katika jopo la kusikiliza rufaa na kutoa Maamuzi. Aidha, imeelezwa na Mwakilishi Binafsi kuwa Mwamuzi hakuzingatia vielelezo vilivyotolewa na mleta maombi. Fomu ya Mwenendo wa Shauri la Kinidhamu - Kielelezo DD10 kinaonesha waliohudhuria kikao hicho akiwemo Thadeo Ernest ambaye alikataliwa na Mleta Maombi, lakini wajumbe wa Kamati ya Nidhamu waliona kuwa ni utovu wa nidhamu kumkataa Mjumbe huyo na wakamfungulia shitaka la kinidhamu na kumkuta na hatia nalo. Hii ni kinyume na haki zake za kusikilizwa. Akiendele kuwasilisha alieleza kuwa Mleta Maombi alitegemea risiti kuthibitisha tuhuma za upotevu wa fedha bila kuleta shahidi yeyote. Kielelezo DD8 ambayo ni barua ya kumsimamisha kazi ili kupisha uchunguzi inaonesha makosa yake ni kudharau Mamlaka (insurbodination) na matumizi mabaya ya fedha za Mwajiri (Misuse of Employer's Fund) hata 4 hivyo Mleta Maombi hajawahi kutenda makosa hayo na hakuna ushahidi wa kuyathibitisha. Aidha Muwakilishi aliwasilisha kwamba Kanuni ya 11 ya Tangazo la Serikali Na. 42 ya 2007 imetoa mwongozo wa namna ya kumwachisha kazi mfanyakazi ikiwa ni pamoja na kupewa kwanza onyo kwa makosa aliyotenda kabla ya kuachishwa kazi. Katika shauri hili hakuna onyo au rekodi yoyote ya kinidhamu ya Mleta Maombi. Muwakilishi Binafsi wa Mleta Maombi akiendelea kuwasilisha alieleza kuwa Mleta Maombi alikuwa Meneja wa ulinzi kama mkataba wa ajira - Kielelezo DD1 kinavyoonyesha. Mkataba huo katika aya ya 1(a) kinaonesha kuwa Mleta Maombi anawajibika kwa Meneja Rasilimali watu na mtu mwingine anayehusiana na Rasilimali watu. Mleta Maombi hajawahi kuambiwa kuwa anawajibika kwa Meneja Udhibiti Majanga (Risk Management Manager). Kwa hali hiyo mgogoro kati ya Mleta Maombi na Meneja wa kudhibiti majanga haukuwa ni kosa la kudharau mamlaka (insurbordination) kwa kuwa Mleta Maombi na Meneja Udhibiti Majanga walikuwa na nafasi sawa hivyo Mleta Maombi hawajibiki kwake. Akiendelea kuwasilisha katika hoja hii alieleza kuwa Meneja Udhibiti Majanga alimtuhumu Mleta Maombi kushindwa kufanya kazi zake vizuri lakini hakuna ushahidi huo. Meneja Mdhibiti Majanga anasema Mleta Maombi hakuandaa viashiria muhimu vya kiutendaji (key performance indicators). 5 Kanuni ya 8 (2) ya Tangazo la Serikali Na. 2 42 la 2007 linaonesha kuwa ni mwajiri ndiye atatoa mwongozo wa ufanyaji kazi. Lakini hakuna sehemu inaonesha mwajiri akitoa mwongozo. Ameendelea kueleza kuwa utaratibu wa kumwachisha kazi Mleta Maombi haukuwa halali kwa kuwa mwenyikiti wa Kamati ya nidhamu, ambaye alikuwa ni Meneja Rasilimali watu, alitoa ushahidi wakati wa kikao na hivyo kuwa shahidi na Hakimu katika shauri analoliendesha. Aidha, Mleta Maombi alikuwa anawajibika kwa Meneja Rasilimali Watu. Hivyo, mwenyekiti wa kamati hakuwa mtu huru kwa kuwa Mjibu Maombi alikuwa anawajibika kwake, na pia ndiye aliyeandika barua ya kumsimamisha na kumfukuza kazi Mleta Maombi. Mwamuzi alitakiwa aone kuwa utaratibu wa kumwachisha Mleta Maombi haukuwa halali. Kuunga mkono maelezo yake amenukuu kesi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kesi ya Wonderwork shop dhidi ya Ciprian Bwire, Marejeo Na. 84 ya 2015, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi iliyoketi Dar es Salaam, Knight Support (T) Ltd dhidi ya Yahaya Aswad na Wenzake, Marejeo Na. 106 ya 2015, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi iliyoketi Dar es salaam, Sharifa Ahmed dhidi ya Tanzania Road Haullage (1980) Ltd, Marejeo Na. 299 ya 2014, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi iliyoketi Dar Es Salaam, na KCB (T) Ltd dhidi ya Dickson Mwikuka, Marejeo Na. 45 ya 2013, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, iliyoketi Mwanza. 6 Pia Mwakilishi alieleza kwamba Muamuzi alikosea kutozingatia namna Mleta Maombi alivyofanyiwa ikiwa ni pamoja na kutolewa vyombo vyake ndani ya nyumba ya kampuni na familia yake kulala mara baada ya kuachishwa kazi. Barua ya kusimamishwa kazi pia ilionesha kuwa hatakiwi kuonekana ndani ya kiwanda au kuongea na mfanyakazi wa kiwanda wakati huo akiwa anaishi katika nyumba za kiwanda zilizopo ndani ya eneo la kiwanda. Hivyo Mleta Maombi alidhurika kwa matendo ya Mjibu Maombi na alistahili malipo ya jumla kutokana na madhara aliyotendewa (General Damages). Aidha, Mleta Maombi ameeleza kuwa alistahili kulipwa fedha ya kujikimu kwa sababu alilipwa fedha pungufu za usafiri na ni kinyume cha kanuni ya 16 of Kanuni (za Jumla) za Ajira na Mahusiano Kazini, Tangazo la Serikali (T.S.) Na. 47 la 2017. Mleta Maombi aliajiriwa kutoka kwao hivyo anastahili kurejeshwa huko. Kuunga mkono maelezo hayo alinukuu kesi ya Kenya Kazi Security (T) Ltd vs. Nambeke Skawa, Marejeo Na. 37 ya 2016, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi iliyoketi Mwanza. Akijibu mawasilisho ya Mleta Maombi, Wakili wa Mjibu Maombi alieleza Tuzo ya Tume ipo sahihi kwa mujibu wa Sheria. Alieleza ya kwamba viini vya mgogoro katika shauri lilokuwa mbele ya Tume ni vitatu na Muamuzi alifanya Uamuzi baada ya kuchambua viini vyote vitatu vya mgogoro. Mwamuzi alibainisha kosa lililothibitishwa na Mleta Maombi ni dharau iliyozidi (gross insurbordination) kwa Mamlaka. Ushahidi 7 unaothibitisha kosa hilo ni Kielelezo DD 6 - barua pepe toka kwa Meneja Udhibiti wa Majanga kwenda kwa Mleta Maombi ikihoji sababu ya Mleta Maombi kutohamisha askari wanaojihusiha na uhalifu hata baada ya kupokea maelekezo ya kuwahamisha watu hao mara moja. Kielelezo DD 3 - barua pepe ya Meneja Udhibiti Majanga akimkumbusha Mleta Maombi kuwa amekiuka maelekezo ya kutotumia silaha za moto zisizo na kibali aliyokuwa amepewa. Pia kielelezo DD 7 - taarifa ya ndani inaoonesha Mleta Maombi aliandika barua ya kuomba kuajiri walinzi kwa Meneja Mkuu bila kupitisha kwa Meneja Mdhibiti majanga kama ulivyo utaratibu. Ushahidi huo unathibitisha kuwa Mleta Maombi alikataa kutii maelekezo halali ambayo aliyokuwa amepewa na pia alidharau mkubwa wake hivyo kuthibitisha kuwa Mleta Maombi alitenda makosa ya dharau iliyokithiri kwa mkubwa wake. Wakili alieleza ya kwamba kielelezo DD1 - Mkataba wa ajira katika aya 1(a) unaonesha kuwa Mleta Maombi atawajibika kwa Meneja Rasilimali Watu kiutawala au mtu mwingine anayehusika na masuala hayo. Mkataba huo ulisainiwa tarehe 15/03/2017. Wakati wa kusaini mkataba huo Meneja Usalama alikuwa anaripoti kwa Meneja Rasilimali Watu. Mwezi April!, 2017 ilitengenezwa Idara ya kudhibiti Majanga na suala la Usalama likawa ni sehemu katika muundo wa Idara ya kudhibiti Majanga. Na alipoanza kazi Mleta Maombi alikuwa akiripoti kwa Meneja Udhibiti Majanga. Kielelezo DD 8 4 - Muhtasari wa Utendaji wa Mleta Maombi unaonesha kuwa alipewa muda ajirekekebisha katika kuiongoza Sehemu (Section) ya Usalama. Na baada ya tamko hilo bado aliendelea kwenda kinyume cha tamko lake. Hivyo, Muamuzi alikuwa sahihi kuona kuona kuwa kosa la dharau iliyokithiri dhidi ya Mleta Maombi kwa kiongozi wake limethibitishwa. Kuhusu hoja ya Mwamuzi kukiri kuwa DW1 alikuwa na mgogoro wa maslahi, Wakili alieleza kuwa Mwamuzi amefafanua hoja hii katika ujumla wake kuanzia ukurasa wa 22-23 wa Tuzo lakini Muamuzi aliona kuwa Mleta Maombi alikuwa na wajibu wa kutekeleza maelekezo ya viongozi wake. Hii ilipelekea kukosana kwa Mleta Maombi na Meneja Udhibiti Majanga (Risk Management manager). Wakili aliendelea kuwasilisha kwamba taarifa ya uchunguzi ambayo ndio msingi wa tuhuma za Mleta Maombi zipo wazi katika Kanuni ya 11 na 13(1) kuwa wajibu wa mwajiri ni kufanya uchunguzi. Hivyo haitoi ulazima wa kumpatia ripoti ya uchunguzi Mleta Maombi. Alieleza kuwa barua ya kumsimamisha kazi Mleta Maombi ilikuwa na makosa machache, lakini baada ya uchunguzi makosa yaliongezeka kama inavyoonekana katika taarifa ya kuitwa katika Shauri la kinidhamu. Taarifa hiyo ilimpatia siku 3 za kujiandaa na kikao na iliorodhesha makosa yote anayotuhumiwa nayo. Tarehe 18/01/2018 Mleta Maombi alihudhuria kikao cha nidhamu na tarehe 19/01/2018 Mleta Maombi aliomba Msamaha kwa makosa aliyoyafanya 9 kupitia barua. Baada ya kutoka matokeo ya kikao cha kinidhamu alikata rufaa ambapo hakupinga makosa ila aliomba apunguziwe adhabu. Meneja Mkuu ambaye ndio mwenye Mamlaka ya kusikiliza rufaa aliwataka mwajiriwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu wawasilishe hoja zao mbele yake na kisha akatoa uamuzi wa Rufaa kama kielelezo DD 14 kinavyoonyesha. Ilielezwa kuwa Kikao cha nidhamu kilikuwa chini ya Meneja Rasilimali watu. Hivyo alisaini barua ya kumsimamisha kazi Mleta Maombi lakini hakuhusika na uchunguzi wa tuhuma dhidi ya Mleta Maombi. Katika kikao cha nidhamu Mwenyekiti wa kamati ya Nidhamu alikuwa na mamlaka ya kumuita mtuhumiwa katika kikao cha nidhamu na alisaini barua hiyo. Barua ya kuachishwa kazi pia ilisainiwa na Meneja Rasilimali Watu kwa kuwa ndio wajibu wake. Hivyo katika taarifa ya kuitwa katika kikao cha nidhamu na Muhtasari wa kikao cha kinidhamu alikuwa mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu na katika kumsimamisha kazi na kumfuta kazi Mleta Maombi aliandika barua kama Meneja Rasilimali watu. Muamuzi aliliongelea hili katika ukurasa wa 25 na 26 wa Tuzo. Hivyo hakukuwa na mgogoro wa kimaslahi. Pia Thadeo ambaye ni Mwanasheria wa Kampuni na Mjumbe wa kikao cha nidhamu hakuwa na maslahi na kikao hicho. Wakili alinukuu kesi ya Alliance One Tobacco (T) Ltd vs. George Masalo, Marejeo Na. 14 ya 2015, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi io iliyoketi Morogoro ambapo Mahakama iliona kuwa sio lazima kufuata kila kitu katika taratibu za kumwachisha mwajiriwa kwa makosa ya kinidhamu. Kanuni 13(1) ya T.S. Na. 42 ya 2007 sio kipimo pekee kuwa taratibu za kauchishwa kazi zilifuatwa. Inatakiwa ziangaliwa taratibu hizo zilizowekwa na kanuni kwa pamoja kama haziathiri haki ya mwajiriwa kujitetea. Hivyo Mwamuzi alikuwa sahihi katika Uamuzi wake. Kuhusu nafuu alizoomba Mleta Maombi, Wakili alieleza kuwa Mjibu Maombi alimpa Mleta Maombi stahili zake kama inavyoonekana katika DD 15 - mafao ya kuachishwa kazi na DD 16 - Mkataba wa Hali Bora. Alilipwa mshahara aliofanyia kazi, taarifa ya kuachishwa kazi, likizo na gharama ya kusafirishwa. Fedha nyingine zililipwa katika akaunti yake na fedha ya usafiri alilipwa fedha taslimu. Malipo hayo yalizingatia mkataba wa hali bora. Mwajiri alimpa taarifa ya siku 14 ya kutoka katika nyumba baada ya kuwa amelipwa fedha za mafao ya kuachishwa kazi. Siku 14 zilipita na Mleta Maombi hakutoka katika nyumba ndipo kampuni ilimtoa katika nyumba kupitia kwa walinzi. Wakati wa uchunguzi ni kweli Mleta Maombi, alizuiwa kufanya mawasiliano na watumishi wengine ili kuzuia asije kuharibu upelelezi. Hivyo, hoja ya malipo ya madhila ya Jumla Mleta Maombi hakuwahi kuomba nafuu hiyo mbele ya Tume. Kwa maelezo hayo naomba Mahakama izingaie kuwa kwa makosa aliyoyafanya ya kuruhusu silaha za moto zisizo na kibali kutumika, bado kusingeweza kumrudisha ii Mleta Maombi kazini. Na pia nafasi hiyo kwa sasa ilifutwa na shughuli za usalama zimetolewa kwa kampuni ya ulinzi. Kuhusu kesi alizozirejea mleta maombi, katika shauri hili kuna ushahidi wa kuthibitisha makosa ya kinidhamu dhidi ya Mleta Maombi. Pia kesi ya Kenya Kazi Security (T) Ltd vs. Nambeke Skawa (supra) Wakili alieleza ni tofauti na kesi hii kwa kuwa ilikuwa inahusu malipo ya kuachishwa kazi baada ya mwajiriwa kuomba kuhama kituo, wakati shauri hili linahusu malipo ya usafiri baada kuachishwa kazi. Mleta Maombi hakuacha kazi yake ill aje atende matukio ya kinidhamu. Hivyo wanaiomba mahakama itupilie mbali maombi haya. Akifanya mawasilisho ya mwisho (Rejoinder submission), Mwakilishi wa Mleta Maombi alirejea mawasilisho yake ya msingi ya awali ila alisisititiza kuwa jukumu la Meneja wa ulinzi ni ulinzi na sikutoa silaha. Aidha, alieleza kuwa suala la kuomba kibali cha kuajiri kutoka kwa Meneja Mkuu si dharau. Baada ya kusikiliza maelezo ya mawasilisho toka pande zote mbili, mahakama iliona kuwa hoja zifuatazo ndizo zinazotakiwa kufanyiwa uamuzi;- i. Endapo sababu za kumwachisha kazi Mleta Maombi zilikuwa halali na za haki. 12 ii. Endapo taratibu za kumwachisha kazi Mleta Maombi zilikuwa za haki. iii. Ni nafuu ipi ambayo kila upande unastahili? Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini inaeleza katika kifungu cha 37(1) inaeleza kuwa itakuwa ni kinyume cha sheria kwa mwajiri kumwachisha kazi mwajiriwa pasipo uhalali. Sheria hiyo inaeleza katika kifungu cha 37(2) (a) (b) (c) uachishwaji kazi utakuwa sio halali iwapo Mwajiri atashindwa kuthibitisha kuwa sababu za kumwachisha kazi mwajiriwa zilikuwa halali na za haki na kuwa taratibu za kumwachisha kazi zilikuwa halali. Katika kesi ya Tanzania Railway Limited dhidi ya Mwajuma Said Semkiwa, Marejeo Na. 239 ya 2014, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kai, iliyokaa Dar Es Salaam, Mahakama ilikuwa na maoni kwamba ni msimamo wa kisheria kuwa uachishwaji kazi ili uonekane kuwa ni halali unatakiwa uegemee katika sababu halali za kumwachisha kazi na ufuate taratibu halali. Kwa maneno mengine kuwe na uhalali wa kimaudhui (sababu) ya kumwachisha kazi na uhalali wa kiutaratibu ili uachishwaji kazi uwe halali. Katika kuamua hoja ya kwanza endapo kulikuwa na sababu halali na za haki za kumwachisha kazi Mleta Maombi, ushahidi uliopo katika rekodi unaonesha kuwa Mleta Maombi alikuwa ameajiriwa na Mjibu Maombi kwa mkataba wa kipindi maalum cha miaka miwili. Mkataba huo ilianza tarehe 13 01/03/2017 na ulitakiwa kufikia ukomo tarehe 28/02/2019. Hata hivyo aliachishwa kazi kutokana na makosa ya kinidhamu tarehe 05/02/2018. Kwa mujibu wa barua ya kumwachisha kazi Mleta Maombi - Kielelezo DD12 Mleta Maombi aliachishwa kazi kwa kosa la kuwa na tabia mbaya (Misbehaving) katika utendaji wake. Kosa hilo ni tofauti na makosa yaliyo katika hati ya wito wa kuhudhuria kikao cha nidhamu - Kielelezo DD9 ambayo inaonyesha mtuhumiwa anatuhumiwa kwa makosa mawili ambayo ni utendaji ulio chini ya kiwango na dharau iliyokithiri kwa kiongozi wake (gross insubordination). Kosa la kuwa na tabia mbaya na kosa la kudharau kiongozi au mamlaka ni makosa tofauti. Aidha, kosa la tabia mbaya ni kosa la kuwa na tabia au kitendo cha ukosefu wa maadili ya eneo husika au jamii husika. Na katika shauri hili kosa la tabia mbaya ya Mleta Maombi haliko wazi kuwa ni tabia gani hizo mbaya ambazo alizifanya katika utendaji wake. Kosa hili sio miongoni mwa makosa makubwa ya kinidhamu ambayo yanaweza kupelekea mwajiriwa kufukuzwa kazi akikutwa na hatia kwa mujibu wa kifungu cha 12(3) cha Tangazo la Serikali Na. 42 la 2007. Hivyo, ni wazi kuwa Mleta Maombi alitiwa hatiani kwa kosa ambalo hakushitakiwa nalo. Katika shauri hili mleta maombi akiwa Meneja wa Ulinzi wa Mjibu Maombi alishtakiwa kwa makosa mbalimbali ya kinidhamu. Tume iliona kuna ushahidi wa kuthibitisha kosa la kudharau viongozi wake au amri 14 halali kuliko kithiri (gross insurbordination). Kosa hilo likithibishwa linaweza kumfukuzisha kazi mwajiriwa kwa mujibu wa kanuni ya 12(3) (f) ya Kanuni za Ajira na Mahusiano Kazini (Kanuni za Utendaji Bora), Tangazo la Serikali Na. 42 la 2007. Hata hivyo kama nilivyoeleza hapo awali, kwa kuwa barua ya kumwachisha kazi inataja sababu ya kumwachisha kazi ambayo ni tofauti na makosa ya kinidhamu aliyoshitakiwa nayo, ni wazi kuwa sababu hiyo iliyo katika barua ya kumwachisha kazi haijathibitishwa kwa ushahidi mbele ya Kamati ya Nidhamu na mbele ya Tume. Hivyo, Mwamuzi hakuwa sahihi kuona kuwa sababu ya kuachishwa kazi Mleta Maombi ya dharau iliyokithiri kwa kiongozi wake ilithibitishwa. Pia Mjibu Maombi alieleza makosa aliyotuhumiwa wakati wa kusimamishwa kazi yaliongezeka baada ya kufanya uchunguzi. Hata hivyo, ripoti ya uchunguzi (investigation report) haikuweza kuletwa na Mjibu Maombi mbele ya kamati ya nidhamu wala Mleta Maombi kupewa ili kuweza kuitumia kujitetea dhidi ya tuhuma zinazomkabili. Huu ni ukiukwaji wa taratibu kama ulivyo katika kifungu cha 13(1) cha Tangazo la Serikali Na. 42 la 2007 inayotaka mwajiri kufanya uchunguzi kujiridhisha iwapo kuna sababu za kuitisha usikilizwaji wa shauri la kinidhamu. Kutotolewa kwa ripoti wakati wa usikilizwaji wa shauri la kinidhamu na mbele ya Tume kunafanya kusiwe na kielelezo cha kuthibitisha kuwa uchunguzi ulifanyika. 15 Aidha, kutompatia mwajiriwa ripoti ya uchunguzi ambayo ndio ilikuwa msingi wa mashitaka ya kinidhamu dhidi yake ni sawa na kumnyima haki yake kusikilizwa ambayo ni haki ya msingi na ya kiasili. Mahakama ya Rufaa ilikuwa na msimamo kama huo katika kesi ya Severe Mutegeki na Mwenzake dhidi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA), Rufaa ya Madai Na. 343 of 2019, Mahakama ya Rufani ya Tanzania, iliyokaa Dodoma, (haijaripotiwa). Hivyo hoja ya Mjibu Maombi kuwa sio lazima kila utaratibu wa kumwachisha kazi mwajiriwa uliowekwa na sheria ni lazima ufuatwe inakosa mashiko kwa kuwa taratibu ambazo hazikufuatwa na Mjibu Maombi zilikuwa zinamnyima haki ya kusikilizwa Mleta Maombi. Kwa sababu hiyo, kesi ya Alliance One Tobacco (T) Ltd dhidi ya George Masalo, Marejeo Na. 14 ya 2015, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi iliyoketi Morogoro, ambayo Mjibu Maombi aliinukuu ina mazingira tofauti na yaliyopo katika kesi hii. Vilevile taratibu za usikilizwaji wa shauri la kinidhamu zilikuwa nikinyume cha utaratibu kwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ambaye alikuwa ni Meneja Rasilimali watu ndiye alimsimamisha kazi Mleta Maombi, alimwandikia wito na hati ya mashitaka, aliongoza kikao cha kamati ya nidhamu na kumuandikia barua ya kumwachisha kazi. Hili linaonesha kuwa kikao cha usikilizwaji was shauri la kinidhamu hakikuwa 16 huru kwa kuwa kulikuwa na viashiria vya upendeleo na hivyo kuwa kinyume cha kanuni ya kisheria dhidi ya upendeleo (rule against bias). Muamuzi alikuwa na maoni kuwa Meneja Rasilimali Watu alifanya majukumu ya kuandika barua ya kumsimamisha kazi na kumwachisha kazi Mleta Maombi akiwa kama Meneja Rasilimali Watu na alisaini barua ya kumuita katika shauri la kinidhamu na kuongoza kikao cha kamati ya nidhamu akiwa kama Mwenyekiti wa Kamati. Hoja hii sio sahihi kwa kuwa mwongozo Na. 4 (2) wa Mwongozo wa Sera na Taratibu za Kushughulikia Nidhamu, Kukosa Uwezo na Kutohitajika ambao ni Kiambatisho katika Kanuni za Ajira na Mahusiano Kazini (Kanuni za Utendaji Bora), Tangazo la Serikali Na. 42 la 2007 unataka Mwenyekiti wa shauri la kinidhamu asiwe na upande wowote. Kwa Meneja Rasilimali kufanya mambo yote hayo kunaonesha alikuwa na upande wa mwajiri kwa kuwa baadhi ya majukumu aliyoyafanya kama kumsimamisha kazi na kumwachisha kazi Mleta Maombi ni ya mwajiri. Hivyo, Mwenyekiti alikuwa ni hakimu katika shauri lake mwenyewe. Kwahiyo, Mwenyekiti wa shauri hakuwa huru. Ni maoni yangu kuwa kwa Mleta Maombi kutopewa taarifa ya uchunguzi na Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu kutokuwa huru kunafanya taratibu za kumuachisha kazi Mjibu Maombi kutokuwa halali kwa sababu ziliathiri haki zake. 17 Hivyo Mahakama hii inaona sababu za uachishwaji wa kazi wa Mleta Maombi hazikuwa halali na haki na utaratibu za kumwachisha kazi haukuwa halali. Hoja ya mwisho katika shauri hili nini ni stahili za kila upande. Kwa kuwa Mleta Maombi na Mjibu Maombi walikuwa na mahusiano ya kimkataba yaani mkataba wa miaka miwili kuanzia tarehe 01/03/2017 hadi tarehe 28/02/2019 kama Kielelezo DD1- Mkataba wa Ajira kinavyoonesha na mkataba huo umesitishwa isivyo halali tarehe 05/02/2018, ni wazi kuwa Mleta Maombi aliachishwa kazi miezi 11 na siku 23 kabla ya kufikia ukomo wa mkataba wake. Hata hivyo, katika malipo ya kumwachisha kazi (terminal benefits) alilipwa mshahara wake hadi tarehe 12/02/2018. Hivyo, fidia anayostahili kulipwa Mleta Maombi ni mshahara wa muda uliokuwa umebakia katika mkataba wake kama ilivyoamuriwa na Mahakama hii katika kesi ya Good Samaritan dhidi ya Joseph Robert Savari Munthu, Marejeo. Na. 165/2011 Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, iliyoketi Dar Es Salaam, (haijaripotiwa). Kwa kuwa kielelezo pekee kinachoonesha mshahara wa Mleta Maombi ni Mkataba wa Ajira - Kielelezo DD1 ambao unaonesha kuwa alikuwa analipwa shilingi 2,000,000/= kwa mwezi, basi hesabu za malipo ya fidia zitafanywa kutumia mshahara huu. Kwa sababu hiyo, Mjibu Maombi atamlipa Mleta Maombi jumla ya shilingi 18 23,066,666.72 ikiwa ni mishahara ya kipindi kilichobaki cha mkataba wake kama fidia ya uachishwaji kazi usio halali. Kuhusu kulipwa pungufu malipo ya usafiri, Mleta Maombi hajathibitisha ni kiasi gani ambacho amepunjwa. Aidha, kwa kuwa malipo ya usafiri wake na mizigo ilishatolewa kwa mujibu wa kilelezo - DD16 ni wazi kuwa alikuwa na uwezo wa kuhama wakati akifuatilia fedha anazodai kuwa alipunjwa. Hivyo hastahili kulipwa fedha ya kujikimu na pia naona hakuna ushahidi wa tofauti ya malipo anayodai kuwa alipunjwa. Kuhusu malipo ya jumla ya madhara aliyoyapata kwa kutolewa ndani ya nyumba na kuzuiwa kuongea na watumishi wengine wa Mjibu Maombi, hakuna uthibitisho uliotolewa wa kuhamishwa kabla ya kulipwa fedha za usafiri na mizigo. Mleta maombi hajathibitisha ni lini alitolewa katika nyumba hiyo. Aidha, hoja ya Mjibu Maombi kuwa alimwandikia Mleta Maombi kutoongea na watumishi wengine ili kuzuia asije kuharibu upelelezi ambao ulikuwa unaendelea unaonekana kuwa na mashiko kwani bado Mleta Maombi angeweza kuwasiliana na watu ambao sio watumishi wa Mjibu Maombi. Hivyo madai ya malipo ya jumla ya madhara aliyoyapata (general damages) yameshindwa kuthibitishwa. Kwa sababu hiyo basi, mahakama hii inafuta uamuzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi na kuyakubali maombi haya ya Marejeo. Mjibu Maombi atamlipa Mleta Maombi jumla ya shilingi 23,066,666.72 ikiwa ni 19 fidia ya uachishwaji kazi usio halali. Na kila upande utajigharamia gharama za kuendesha shauri hili. JjW A. E. MWIPORQ JAJI 02/06/2021 20