oswald m mussa dhidi ya group six international limited 2023 tzhcld 1162 9 machi 2023
The applicant was presumed to be an employee under statutory criteria, and the respondent failed to rebut this presumption or produce employment records. The claim was not time-barred as extension had been granted. The applicant was unfairly terminated and is entitled to statutory compensation.
Source-derived case information.
- Citation
- oswald m mussa dhidi ya group six international limited 2023 tzhcld 1162 9 machi 2023
- Parties
- Applicant: Oswald M. Mussa; Respondent: Group Six International Limited
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2023
- Procedural Posture
- Labour Revision / Final Judgment
- Outcome
- application allowed
- Legal Topics
- Employment Relationship, Unfair Termination, Limitation Period, Employee Entitlements
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Oswald M. Mussa
Applicant
Group Six International Limited
Respondent
Procedural Posture
Labour Revision / Final Judgment
Legal Issues
- 1 Whether the applicant was an employee or independent contractor
- 2 Whether the claim was time-barred
- 3 Whether the applicant was unfairly terminated
Ratio Decidendi
The applicant was presumed to be an employee under statutory criteria, and the respondent failed to rebut this presumption or produce employment records. The claim was not time-barred as extension had been granted. The applicant was unfairly terminated and is entitled to statutory compensation.
Court Disposition
application allowed
Orders
- Decision of the Commission for Mediation and Arbitration set aside
- Applicant to be paid statutory entitlements under Section 44 of Cap 366
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA DIVISHENI YA KAZI ILIYOKETI PAR ES SALAAM MAOMBI YA MAREJEO NA. 337 YA 2022 (Kutokana na Mgogoro wa Kikazi No CMA/DSM/KIN/882/2022) OSWALD M. MUSSA...........................................................MLETA MAOMBI DHIDI YA GROUP SIX INTERNATIONAL LIMITED........................... MJIBU MAOMBI HUKUMU K.T.R, Mteuie, J 03 Machi, 2023 & 09 March, 2023 Maombi haya ya marejeo yanatokana na Mgogoro wa Kikazi Na. CMA/DSM/KIN/882/19 katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Dar es Salaam Kinondoni (Tume). Mleta maombi ndiye alifungua mgogoro huo Tume akidai kuachishwa kazi visivyo halali na kuomba Tume imwamuru Mjibu Maombi amlipe kiasi cha TZS 86,520,492.00. Kwa mujibu wa taarifa zilizopo Tume, mleta maombi alidai kuajiriwa na mjibu maombi kama msindikizaji wa malori yaliyokuwa yanapeleka mizigo katika maeneo ya ujenzi akiwa analipwa mshahara TZS 1200,000 kwa mwezi. Alidai kuachishwa kazi bila sababu wala kufuata utaratibu. Mjibu maombi alikataa kuwahi kumwajiri mleta maombi akidai kuwa alikuwa "independent contractor". i Baada ya kusikiliza shauri, muamuzi aliona hakukuwa na ushahidi unaothibitisha mahusiano ya kiajira. Na pia Tume iliona kuwa mgogoro ulikuwa umewasilishwa nje ya muda. Tume ilitupilia mbali madai ya mleta maombi na kusababisha afungue maombi haya ya marejeo. Katika kiapo cha Maombi haya ya marejeo kuna hoja kuu tatu ambazo ni:- 1. Muamuzi alikosea kwa hoja na sheria kwa kushindwa kuoanisha ushahidi 2. Muamuzi alikosea kwa hoja na sheria kwa kuamua kwamba hapakuwa na mahusiano ya kiajira kati ya mlalamikaji na mlalamikiwa 3. Muamuzi alikosea kwa hoja na sheria kwa kuamua kwamba madai ya mlalamikiwa yalikuwa yamepitwa na muda Usikilizwaji ulifanyika kwa mdomo ambapo Mleta maombi aliwakilishwa na Mwakilishi binafsi Bw. Said Muhindi wakati mjibu maombi akiwakilishwa na Wakili Stephen Mtui. Katika kusikiliza maombi haya, katika hoja ya kwaza, Bw. Muhindi Said, aliiambia Mahakama hii kwamba muamuzi alikosea kwa hoja na sheria kwa kushindwa kuoanisha ushahidi wa pande zote. Bw. Muhindi alisema kuwa Ajira ya mleta maombi ilisitishwa tarehe 2 30/1/2019. Bw. Muhindi alirejea ushahidi wa mlalamikiwa uliotolewa na Bw. Omar (DW1) akisema kwamba mjibu maombi anamtambua mlalamikaji kama aliyekuwa msimamizi binafsi aliyepewa zabuni ya kuhakikisha malori yanabeba mizigo ya site za wateja yanafika salama na kwamba alikuwa "independent contractor." Aliukosoa ushahidi huu kwa hoja kuwa shahidi alishindwa kutoa uthibitisho mahusiano hayo yanatokana na makubaliano yapi kama mleta mombi hakuwa mwajiri wake. Kwa mujibu wa Bw. Muhindi, mleta maombi aliomba nyaraka hizo ziwe faida kwa pande zote mbili lakini mlalamikiwa hakuleta nyaraka hizo. Kwa maoni ya Bw. Muhindi, kwa mazingira haya ya ushahidi ndiyo kasoro zilizosababisha kutokukubaliana na Uamuzi huo wa muamuzi. Bw. Muhindi alirejea pia ushahidi wa upande wa mlalamikaji aitwaye Yazidu Magimba ambaye pia ni mfanyakazi wa group six, ambaye alithibitisha kwamba anamtambua mlalamikaji kama mfanyakazi wa Group Six International Limited lakini aliachishwa kazi. Bwana Muhindi aliendelea kukosoa ushahidi wa upande wa mlalamikiwa kwa kutokuwa na nyaraka au uthibitisho wowote pamoja na kupewa taarifa ya kuleta nyaraka ("notice to produce") ikiwepo kitabu cha mahudhurio (occurance book) ili zitumiwe kama sehemu ya kutambua wafanyakazi. 3 Kuhusu hoja ya pili, kwamba muamuzi alikosea kwa hoja na sheria kwa kuamua kwamba hapakuwa na mahusiano ya kiajira kati ya mlalamikaji na mlalamikiwa, Bwana Muhindi aliwasilisha kwamba Tume kulikuwa na hoja kuhusu muhuri uliokuwepo katika barua ya kuachishwa kazi ambao mlalamikiwa aliupinga akidai kwamba umeandikwa received. Kwa mujibu wa Muhindi, mlalamikiwa hakukataa kama siyo wa Kampuni, ila tatizo kwake ni neno "received" ambalo lilipelekea mapungufu upande wa muamuzi kukubaliana na hoja ya mlalamikiwa. Bw. Muhindi alisema kuwa mlalamikaji aliweza kuthibitisha kuwa muhuri ulikuwa mali ya kampuni kwani nyaraka zote zinagongwa muhuri huo. Kuhusu hoja ya tatu kuhusu madai kupitwa na muda, Bwana Muhindi alikumbusha kuwa, awali shauri lilikuwa lilisikilizwa maombi na kuongezewa kubali cha kusikilizwa nje ya mud ana kibali hicho kiliongezwa. Alirejea kesi ya Tanzania China Friendship Textile Co. Ltd vs. Madaha Soni & Others, 1360, Maombi ya Marejeo No. 88 ya 2008, Mahakama Kuu Div. ya Kazi, ambapo Mahakama iliamua kuwa mapunjo hayapitwi na wakati. Ni mawasilisho ya Bw. Muhindi kwamba kutokana na hoja hizi tatu, mleta maombi hakutendewa haki Tume hivyo anaomba Mahakama hii ipitie na isahihishe mapungufu hayo ili kutoa haki kwa pande zote. 4 Akijibu hoja za mleta maombi, Wakili wa Mjibu maombi Bw. Stephine Mtui, akianza na hoja ya kwanza, kuhusu muamuzi kukosea katika kuoanisha ushahidi, alisema kwamba kulikuwa na ushahidi wa mjibu maombi kuthibitisha kwamba mleta maombi hakuachishwa kazi visivyo halali. Alirejea ushahidi wa Bw. Omar Mwita aliyekuwa Afisa Rasilimali watu ambaye alisema kuwa kulikuwa na makubaliano ya kazi maalum na siyo ajira. Aliongeza kuwa mleta maombi alikuwa "independent contractor" na kifungu cha 14 (1) (c) cha Sheria ya Mahusiano Kazini kinatambua aina hiyo ya makubaliano. Alirejea kesi ya Mahakama ya Rufani, Hamidu Abdallah na Wengine 11 dhidi ya B.E Forward Tanzania Co. Ltd uliotolwa mwaka huu na kuomba Mahakama izingatie busara iliyopo katika uamuza huo katika ukurasa wa 8 kwamba pale ambapo mlalamikaji anasema alikuwa ameajiriwa, ni wajibu wake kuthibitisha uhusiano huo wa kiajira. Ni hoja ya Wakili Mtui kwamba mleta maombi alishindwa kutekeleza jukumu lake la kuthibitisha mahusiano ya kiajira. Wakili Mtui aliendelea kuwasilisha kwamba mjibu maombi alithibitisha kuwa hakumwachisha kazi mlalamikiwa kwa kuwa hakuwa mwajiriwa wake. 5 Akishambiliwa uhalali wa hoja za Mleta Maombi, Wakili Mtui alisema mleta maombi hasemi kweli kwani kiapo chao cha kuomba kuongezewa muda Tume, kinasema aliajiriwa kwa njia ya mdomo wakati katika kiapo chake katika Mahakama hii, anadai aliajiriwa kwa maandishi. Wakili Mtui alikosoa ushahidi wa PW2 Azigu Mwagimba, na kutoa hoja kwamba alishindwa kuthibitisha ni kwa namna gani mleta maombi alikuwa mwajiriwa kwani hakuna nyaraka yoyote iliyotolewa kuhusu namna alivyojua taarifa hizo na wala hakusema kama alikuwepo wakati wa m kata ba. Kuhusu hoja ya pili juu ya mahusiano ya kiajira, Wakili Mtui alieleza kwamba hakukuwa na ajira bali mleta maombi alikuwa independent contractor na hivyo Tume ilikuwa sahihi kwa kuwa mleta maombi alishindwa kuthibitisha uhusiano huo. Alirejea tena uamuzi wa Mahakama ya Rufani katika kesi ya BE Forward, kwamba mwenye kudai uhusiano wa kiajira ndiye athibitishe. Kuhusu uwepo wa barua ya kumuachisha kazi iliyogongwa muhuri wa "received" Wakili Mtui alikuwa na maoni kuwa tume ilikuwa sahihi kuona kwamba barua hiyo haikuwa halali kwa kuwa muhuri haukuwa sahihi kwani Muhuri wa "received" unaonyesha upokelewaji wa 6 nyaraka wakati ule wa kutoa byaraka ni tofauti. Hivyo anaona Tume ilikuwa sahihi, kuona barua hii siyo halali. Kuhusu hoja ya tatu, kuhusu madai kupitwa na wakati, kwa kuwa mleta maombi hakuwa mwajiriwa, kwani hakuthibitisha hilo, hastahili stahiki alizoomba kwa mujibu wa kesi ya Hamidu Abdallah na wenzake 11 dhidi ya BE Forward. Hivyo kwa maoni yake, hoja kwamba mapunjo ya mishahara hayapitwi na muda haina mashiko kwa sababu mleta maombi hana stahiki hizo. Baada ya kupitia viapo vya wadaawa, na baada ya kupokea mawasilisho yao, hatua inayofuata ni kuamua hoja bishaniwa. Nitaanza na hoja ya madai kupitwa na muda kwani ni hoja ya kisheria. Nimepitia uamuzi wa tume na kuona kuwa baada ya kuchambua hoja zote za msingi, muamuzi aliibua hoja ya suala la kupitwa na muda mwishoni. Kisha alinukuu kurasa tatu za mawasilisho ya wakili wa mwajiri na kuhitimisha kuwa alikubaliana naye. Muamuzi hakusema sababu zilizomfanya akubaliane na mawasilisho ya wakili wa mwajiri na kuamua kuwa mgogoro ulikuwa umepitwa na muda. Kumbukumbu zinaonyesha kuwa suala la muda lilikuwa limeshaamuliwa kutokana na maombi yaliyowasilishwa Tume na mleta maombi kupitia CMA Form No. 1 ambayo yalifanyiwa uamuzi na 7 kuongezewa muda. Uamuzi huo ni wa tarehe 27/8/2021. Hivyo muamuzi alikuwa ameshafungwa mikono kuhusu suala la muda. Ni maoni yangu kuwa, kwa vile mleta maombi alikuwa ameshakubaliwa kufungua mgogoro nje ya muda, haikuwa sahihi kwa muamuzi kuamua tena hoja hii. Sasa inafuata hoja ya kwanza na ya pili ambazo nitazijibu kwa Pamoja. Hoja hizi ni kuwa muamuzi alikosea kuona kuwa hakuna mahusiano ya kiajira kati ya mleta maombi na mjibu maombi na kwamba hakuoanisha ushahidi ipasavyo. Utambuaji wa mahusiano ya kiajira unaongozwa na Kifungu cha 61 cha Sheria ya Taasisi za Kazi, Sura ya 300. Nanukuu:- "61. For the purposes of a labour law, a person who works for, or renders services to, any other person is presumed, until the contrary is proved, to be an employee, regardless of the form of the contract, if any one or more of the following factors is present- fa) the manner in which the person works is subject to the control or direction of another person; (b) the person's hours of work are subject to the control or direction of another person; 8 (c) in the case of a person who works for an organisation, the person is a part of that organization; (d) the person has worked for that other person for an average of at least forty five hours per month over the last three months; (e) the person is economically dependent on the other person for whom that person works or renders services; (f) the person is provided with tools of trade or work equipment by the other person; or (g) the person only works for or renders services to one person." Kutokana na kifungu kilichonukuliwa, ni dhahiri kwamba sheria inamchukulia mtu kuwa mwajiriwa wa mtu aliyemtumikia mpaka yaliyoorodheshwa yathibitike kutokuwepo. Kuna barua ya kuachishwa kazi (Kielelezo P-8) ambayo ilitoka kwa mjibu maombi kuonyesha kuwa mleta maombi aliachishwa kazi. Mjibu maombi anaikataa barua hii kusema ina muhuri wa "Received" Ni maoni yangu kuwa si kazi ya mjibu maombi kugonga mihuri. Kama kuna mtu aligonga muhuri wa received kimakosa, jambo hilo haliondoi hoja kuwa barua iliandikwa kutoka ofisi ya mjibu maombi. 9 Barua hii naichukua kama kiashiria cha kuwa mleta maombi aliwahi kufanya kazi katika ofisi za mjibu maombi. Kwa mujibu wa Kifungu cha 15 cha Sheria ya Ajira na Usalama Kazmi, Sura ya 366, ni jukumu la Mwajiri kutunza kumbukumbu za ajira. Kama mahusiano ya Mleta maombi na mjibu maombi yalikuwa ni ya kiajira au ni ya kazi maalumu, vigezo vilivyotajwa hapo juu vilitakiwa kuthibitishwa na mwajiri ambaye ndiye anapaswa kutunza mikataba na taarifa za ajira. Kutokuwepo kwa ushahidi huo, inamaana mleta maombi ataonekana kuwa alikuwa mwajiriwa wa njibu maombi mpaka ithibitishwe kinyume chake. Niliyosema hapo juu yanajibu hoja zote mbili. Kwa vile mjibu maombi alisisitiza kutokumtambua mleta maombi kama mwajiriwa wake, hakuna chochote kinachoonyesha kama alifuata taratibu za kumuachisha kazi. Hivyo natofautiana na uamuzi wa muamuzi. Alipaswa kuona uwepo wa uhusiano wa kiajira baina ya wadaawa na kwamba mleta maombi aliachishwa kazi bila utaratibu. Ni nafuu gani wadaawa wanastahili, katika CMA Form No 1, ameomba kulipwa stahiki zake. Nami naona mleta maombi anastahili kulipwa fidia na stahili zingine za kiajira. Hivyo basi, naona mleta maombi ameweza kuthibitisha kuwa alikuwa mwajiriwa na mjibu maombi na aliachishwa kazi bila kufuata 10 utaratibu na bila sababu. Hivyo maombi haya yanaruhusiwa. Kwa msingi huu, nafanya marejeo katika uamuzi wa Tume na kutengua uamuzi huo. Natoa amri mleta maombi alipwe stahili zake za kisheria kwa mujibu wa kifungu cha 44 cha Sura ya 366 na fidia ya mishahara ya miezi 12. Imeamriwa hivyo. Hakuna amri juu ya gharama. Imetolewa Dar es Salaam leo tarehe 9 Machi 2023 ii