MAOMBI YA MAREJEO NA
The applicant failed to provide any credible evidence or documentation to prove the existence of an employment relationship with the respondent. The Commission's decision to dismiss the claim was correct as the burden of proof was not discharged by the applicant.
Source-derived case information.
- Citation
- MAOMBI YA MAREJEO NA
- Parties
- Applicant: Peter Valentine Kim Ario; Respondent: Avelino George Tesha
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2024
- Procedural Posture
- Labour Revision Application / Judgment
- Outcome
- Application dismissed
- Legal Topics
- Unfair Termination, Employment Relationship, Standard of Proof
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Peter Valentine Kim Ario
Applicant
Avelino George Tesha
Respondent
Procedural Posture
Labour Revision Application / Judgment
Legal Issues
- 1 Whether the Commission erred in dismissing the applicant's claim for lack of proof of employment relationship
- 2 Whether the applicant proved existence of an employment relationship with the respondent
Ratio Decidendi
The applicant failed to provide any credible evidence or documentation to prove the existence of an employment relationship with the respondent. The Commission's decision to dismiss the claim was correct as the burden of proof was not discharged by the applicant.
Court Disposition
Application dismissed
Orders
- The application is dismissed.
- Right of appeal explained.
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
KATIKA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA DIVISHENI YA KAZI DAR ES SALAAM MAOMBI YA MAREJEO NA. 15642 YA MWAKA 2024 KUMBUKUMBU NA. 202407021000015624 PETER VALENTINE KIM ARIO.............................................. MLETA MAOMBI DHIDI YA AVELINO GEORGE TE S H A ........ ..............................................MJIBU MAOMBI HUKUMU Tarehe ya amri ya Mwisho: 13/ 08/2024 Tarehe ya Hukumu: 21/ 08/2024 MLYAMBINA, 3 . Mbele ya Mahakama hii Mleta Maombi anapinga maamuzi yaliyotolewa na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (itajulikana kama Tume) mnamo tarehe 10/10/2023 katika Mgogoro wa Kazi Na. CMA/DSM/UBG/58/2022/28/2022. Mbele ya Tume, Mleta Maombi aliwasilisha mgogoro wake akipinga uachishwaji kazi usio halali dhidi ya anayedaiwa kuwa Mwajiri wake, Mjibu Maombi katika shauri hili. Tume baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili iliona ya kuwa Mleta Maombi alishindwa kuthibitisha uwepo wa mahusiano ya kiajira baina yake na Mjibu Maombi. Hivyo basi, maombi yake yalitupiliwa mbali. Baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya Tume, Mleta Maombi amewasilisha Maombi haya kwa hoja zifuatazo: i. Kwamba, Tume i/ikosea kiukwefi na kisheria kwa kutozingatia na kufanyia kazi ushahidi uiiotoiewa mbele ya Tume. ii. Kwamba, Tume i/ikosea kiukweli na kisheria kutupilia mba/i mgogoro kwa hoja kwamba hapakuwa na ushahidi wa maandishi kuthibitisha uhusiano wa ajira baina ya Mfafamikaji na Mlalamikiwa. Hi. Kwamba, Tume ifikosea kiukweli na kisheria kutozingatia kwamba Mjibu Maombi a/ikiri Kufanya biashara ya marashi na jam ii ya udi katika Maeneo ya mchikichi na msimbazi. iv. Kwamba, Tume ifikosea kiukweli na kisheria kutozingatia kwamba Mjibu Maombi hakufeta wateja wake ambao afisema n i Wapemba kama mashahidi kuthibitisha kwamba hakuwa na eneo maaiumu ia biashara ya marashi na udi baii aiikuwa anawapeiekea wateja wake kwa oda ya mdomo. Shauri hili liliendeshwa kwa njia ya maandishi. Mbele ya Mahakama hii Mleta Maombi alijiwakilisha mwenyewe. Hoja zote zilijadiliwa kwa pamoja. Mleta Maombi alieleza kuwa aliajiriwa na Mjibu Maombi tokea tarehe 12/10/2012 kama Afisa Masoko katika biashara ya Duka la vipodozi la Mjibu Maombi lililopo llala, Dar es Salaam. Anadai kuwa aliachishwa kazi mnamo tarehe 01/08/2022 isivyo halali. Mleta Maombi alieleza kuwa ni wazi Tume haikuzingatia kwamba Mjibu Maombi alikiri kuwa anafanya biashara ya marashi na udi lakini hakuleta wateja wake kama mashahidi. Kuwa, aiikuwa hana duka na aliwapata wateja hao kwa njia ya mdomo tu. Aliongeza kuwa; mnamo tarehe 20/03/2024, Mjibu Maombi alimuomba afute shauri hili jambo linalothibitisha wazi kulikuwa na mahusiano ya kiajira baina yao. Hivyo aliiomba Mahakama izingatie ushahidi wake na kutupiiia mbali maamuzi ya Tume. Mjibu Maombi aliwakilishwa na Mawakili kutoka Ofisi ya Mawakili ijulikanayo kama Nzia. Walieleza kuwa Mleta Maombi alishindwa kuthibitisha madai yake mbele ya Tume. Kwamba hakuleta mkataba wowote wa ajira au nyaraka yoyote ya kuthibitisha madai yake. Kwamba hata benki alikokuwa anapeleka fedha alizodai alishindwa kuitambua. Waliongeza kuwa; umuhimu wa kuthibitisha uhusiano wa kiajira ulilezewa pia na Mahakama Kuu katika Shauri la Marejeo Na. 71 la 2018 kati ya ERPNESS EZEKIEL dhidi ya SBC LIMITED TANZANIA (Arusha) (ambapo ilielezwa kuwa: He did not even produce evidence to show the mode of payment of his salary. I find that there was no employer and employee relationship because the Applicant was never under direct control of the Respondent but Mbulu Trading Company. The first issue is answered in the negative. Mawakili hao pia walipinga vikali kutotambua barua iliyowasilishwa na Mleta Maombi akidai kuwa walimuomba kuondoa shauri hili. Mwisho, waliiomba Mahakama itupilie mbali shauri hili. Baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili, Mahakama inaona kuwa ina hoja moja ya msingi ya kutatua; endapo maamuzi ya Tume yalikuwa sahihi. Kama alivyowasilisha Mleta Maombi, madai yake ni kuwa aliachishwa kazi isivyo halali. Kwa kuwa Mjibu Maombi alimkana kuwa hamtambui kama Mwajiriwa wake, ilikuwa ni muhimu Tume ichunguze kama kulikuwa na mahusiano ya kiajira baina ya pande hizo mbili. Kumbukumbu za Tume zinaonesha kuwa hakuna kilelezo chochote kilichotolewa kuthibitisha mahusiano ya kiajira yanayodaiwa. Mleta Maombi anadai kuwa aliajiriwa tokea mwaka 2012 lakini hakuna kithibitisho cha aina yoyote kuthibitisha hilo. Pia, ameeleza tu kuwa Mjibu Maombi anafanya bishara ya vipodozi lakini hakuna kielelezo chochote kuthibitisha kama kweli alikuwa na duka na alikuwa akifanya biashara hiyo. Ni Dhahiri kuwa, endapo angekuwa Meneja Masoko kama anavyodai angekuwa anajua taarifa nyingi za biashara ya Mjibu Maombi kwakuwa amefanya kazi katika ofisi hiyo tokea mwaka 2012 kama anavyodai. Kwa mazingira hayo naunga mkono maamuzi ya Tume kwamba Mleta Maombi ameshindwa kuthibitisha madai yake. Mahakama imezingatia maelezo ya Mjibu Maombi kuwa anafanya bishara ya marashi, lakini biashara hiyo tajwa haijathibitishwa kuwa ndiyo aliyokuwa anasimamia Mleta Maombi. Hata mshahara anaodai kulipwa Mleta Maombi hakuna kithibitisho chochote ambacho kimeletwa, jambo ambalo Mahakama inaona sio la kawaida kwa Mwajiriwa wa zaidi ya miaka 10 kutokuwa na kielelezo cha aina yoyote ile kama ilivyo kwa Mleta Maombi. Katika kesi ya Paulina Samson Ndawavya v. Theresia Thomas Madaha, Civil Appeal No. 53 of 2017 (unreported), iliamuriwa ifuatavyo: ...It is equally elementary that since the dispute was in civil case, the standard of proof was on a balance of probabilities which simply means that the Court will sustain such evidence which is more credible than the other... Katika kesi nukuliwa hapo juu iliamuriwa kuwa katika kesi za madai Mahakama itapima ulinganifu wa ushaidi kuthibitisha madai. Msimamo huo pia hutumika katika migogoro ya kazi. Kwakuwa Mleta Maombi ndiye anayedai kuwa alikuwa Mwajiriwa wa Mjibu Maombi, ilikuwa ni jukumu lake kuthibitisha hilo na kama kumbukumbu zinavyoonesha ameshindwa kufanya hivyo. Mahakama haijazingatia kielelezo alichowasilisha Mleta Maombi mbele ya Mahakama hii kwakuwa kesi ilianzia Tume na Mahakama inatakiwa kuzingatia ushahidi uiiotoiewa tu Tume. Hivyo basi Mahakama hii inaendelea kushikilia maamuzi ya Tume. Shauri hili linatupiliwa mbali. Imeamuriwa hivyo. JAJI 21/08/2024 Uamuzi huu umesomwa leo tarehe 21/08/2024 saa nane na dakika therathini na tano mbele ya Mleta Maombi na Wakili Shundi Mrutu kwa niaba ya Mjibu Maombi. Haki ya rufaa imeelezwa.