products of nature company limited dhidi ya eliabu isaack mwita 2023 tzhcld 1158 7 februari 2023
The court found that the Commission for Mediation and Arbitration (CMA) failed to properly determine whether the respondent was terminated or resigned, which is a prerequisite before assessing the fairness of termination. The matter was remitted to the CMA for proper determination of this core issue.
Source-derived case information.
- Citation
- products of nature company limited dhidi ya eliabu isaack mwita 2023 tzhcld 1158 7 februari 2023
- Parties
- Applicant: Products of Nature Company Limited; Respondent: Eliabu Isaack Mwita
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2023
- Procedural Posture
- Labour Revision / Judgment on Application for Revision of Arbitration Award
- Outcome
- Application partly allowed; matter remitted to the CMA for rehearing on specific issues.
- Legal Topics
- Employment Relationship, Termination of Employment, Arbitration Award, Procedural Fairness, Limitation Period
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Products of Nature Company Limited
Applicant
Eliabu Isaack Mwita
Respondent
Procedural Posture
Labour Revision / Judgment on Application for Revision of Arbitration Award
Legal Issues
- 1 Whether there was an employment relationship between the applicant and the respondent
- 2 Whether the respondent was unfairly terminated or resigned voluntarily
- 3 Whether the arbitration award was issued within the proper legal framework
Ratio Decidendi
The court found that the Commission for Mediation and Arbitration (CMA) failed to properly determine whether the respondent was terminated or resigned, which is a prerequisite before assessing the fairness of termination. The matter was remitted to the CMA for proper determination of this core issue.
Court Disposition
Application partly allowed; matter remitted to the CMA for rehearing on specific issues.
Orders
- Records remitted to the CMA to determine whether the respondent was terminated or resigned and whether the dispute was filed within time.
- Each party to bear its own costs.
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA DIVISHENI YA KAZI PAR ES SALAAM MAOMBI YA MAREJEO NA. 280 YA 2022 (Kutokana na Tuzo ya Mgogoro Wa Kikazi Na. CMA/DSM/KIN/856/19/396 ya tarehe 15/7/2022) PRODUCTS OF NATURE COMPANY LIMITED.........................MLETA MAOMBI DHIDI YA ELIABU ISAACK MWITA ........................................ ............ MJIBU MAOMBI HUKUMU K.T.R, MTEULE, J 7 Februari 2023 & 7 Februari 2023 Haya ni maombi ya marejeo yanayotokana na Mgogoro wa kikazi uliofunguliwa katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Dar es Salaam Kinondoni (Tume) na Bw. Eliabu Isaack Mwita (ambaye hapa anatambulika kama Mjibu Maombi) dhidi ya aliyesemwa kuwa mwajiri wake, Products of Nature Limited (anayetambulika kama Mleta maombi). Kutokana na nilichojifunza baada ya kupitia kumbukumbu za Tume na nyaraka za wadaawa, inaonekana mleta maombi ni kampuni inayomilikiwa na Bi. Rose Anna Aziz akiwa ni miongoni mwa wamiliki wengine ambao taarifa zao hazipo wazi katika kumbukumbu za shauri. i Inaonekana pia kuwa utumishi wa mjibu maombi umekuwa na utata na kuwa kiini cha mgogoro kilichoacha swali kama ni nani hasa alikuwa mwajiri wa mjibu maombi kati ya Bi. Rose Anna Aziz na mleta maombi. Kwa mujibu wa CMA Fl iliyowasilishwa Tume, Mlalamikaji alidai kwamba alianza kazi kwa mlalamikiwa tarehe 01/07/2004 hadi tarehe 10/10/2019 pale mkataba wake wa ajira ulipositishwa. Jambo hili linapingwa na mleta maombi ambaye anadai kuwa hakuwahi kumwajiri mjibu maombi. Mleta maombi pia ana hoja kwamba mjibu maombi hakuachishwa kazi bali aliacha kazi mwenyewe. Kutokana na kutokuridhika na uhalali wa ukomo wa ajira yake, mlalamikaji aliwasilisha mgogoro katika Tume tarehe 22/10/2019. Hoja zifuatazo zilijadiliwa Tume:- 1. Endapo kulikuwa na uhusiano wa kiajira kati ya mlalamikaji na Mlalamikiwa, 2. Endapo kulikuwa na sababu za msingi za kumuachisha kazi Mlalamikaji, 3. Endapo taratibu zilifuatwa 4. Ni nini stahiki za kila upande katika mgogoro huu. 2 Baada ya Tume kusikiliza ushahidi wa pande zote, hoja zote zilijibiwa kwa ushindi wa upande wa mjibu maombi wa sasa. Tume ikiongozwa na kifungu cha 61(a) (b) (c) (d) (e) (f) na (g) cha Labour Institutions Act Cap. 300 [R.E 2019] kinachoelezea juu ya vigezo vya mtu kuwa mwajiriwa, Muamuzi alishawishika kuwa mleta maombi (DW1) alikiri kumuajiri mjibu maombi nyumbani kwake Mbezi Beach ambapo alifanya kazi za ufundi wa aina mbali mbali tangu mwaka 2004. Msuluhishi aliridhika kuwa kulikuwa na mahusiano ya kiajira kati ya mleta maombi wa sasa na mjibu maombi. Baada ya kuridhika na uwepo wa mahusiano ya kiajira, msuluhishi aliamua hoja zingine zote dhidi ya mleta maombi na hivyo kuona kuwa taratibu za kusitisha ajira hazikufuatwa kwa mujibu wa Kanuni ya 9(1) a Employment and Labour Relations (Code of Good Conduct) G.N. No. 42/2007 na hakukuwa na sababu halali. Tume inamuamuru Mlalamikiwa kumlipa Mlalalamikaji stahiki zifuatazo:- (a) Notisi sawa na Mshahara wa Mwezi mmoja Tshs. 400,000/= (b) Fidia sawa na mishahara ya miezi 12 Tshs. 400,000/= x 12=4,800,000/= (c) Kiinua mgongo cha miaka 10 Tshs. 400,000/= xl0x7/26=Tshs. 1,076,923/= 3 Jumla ya malipo yote ni Tshs. 6,676,923.00 Mwajiri hakuridhika na uamuzi wa Tume na hivyo kufungua maombi haya ya marejeo akiomba Mahakama hii iitishe kumbukumbu na kuangalia mwenendo mzima na tuzo iliyotolewa na Tume kuona kama iko sahihi. Mleta maombi ameomba mahakama itengue uamuzi wa Tume na kuibadili tuzo hiyo. Katika kiapo kilichawasilishwa pamoja na maombi haya, hoja zifuatazo zimeibuliwa:- (a) Endapo Mwamuzi amekosea kwa hoja na sheria kwa kuamua kuwa Miibu maombi alikuwa mwajiriwa wa Mleta maombi kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa na pande zote. (b) Endapo kufuatia jibu la (a) hapa juu Mwamuzi amekosea kwa hoja na sheria kwa kuamua kuwa Miibu maombi ameachishwa kazi pasipo sababu za msingi na/au pasipo utaratibu kufuatwa. (c) Endapo kufuatia jibu la (a) hapa juu Mwamuzi amekosea kwa hoja na sheria kwa kuamua kuwa Mjibu maombi anastahili malipo ya jumla ya 6,676,923.00 kama aliyoyaainisha. (d) Endapo Mwamuzi amekosea kwa kutouzingatia ushahidi uliotolewa na DW2 wa kupokea barua kutoka TllICO na kuitikia wito wa TUICO zilizopokelewa kama Kielelezo PN 6 ambacho 4 kilikuwa na barua ya TUICO ya tarehe 19/07/2019, na barua ya TUICO ya tarehe 30/7/2019 iliyoandikwa kufuatia barua ya Miibu maombi ya tarehe 25/7/2019) ushahidi ambao unathibitisha kuwa mgogoro uliwasilishwa mbele ya Tume nje ya muda Mleta maombi ameomba nafuu zifuatazo:- (a) Kwamba Mahakama hii tukufu iridhie kuamua kuwa hakukuwa na uhusiano wa kiajira kati ya Mleta maombi na Mjibu maombi hivyo Mjibu maombi hakuachishwa kazi na Mleta maombi (b) Kwamba Mahakama hii tukufu iridhie kuamua kuwa Mjibu maombi hastahili stahiki zilizobainishwa (c) Kwamba Mahakama hii tukufu iridhie kuamua kuwa Mgogoro uliwasilishwa mbele ya Tume nje ya muda (d) Kwamba Mahakama hi tukufu iridhie kutengua uamuzi wote wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi katika Mgogoro wa Kikazi Na. CMA/DSM/KIN/856/19/396 kwa kuwa Mwamuzi alishindwa kuuchambua ushahidi uliotolewa na hatimaye ameshindwa kutoa uamuzi wa haki. 5 Katika kiapo kinzani, mjibu maombi alikanusha hoja kwamba hakuwahi kuajiriwa na mleta maombi. Amesisitiza kuwa aliajiriwa na mleta maombi kwa ajira ya kudumu na siyo vinginevyo. Shauri lilisikizwa kwa mawasilisho ya hoja za maandishi. Mleta maombi aliwakilishwa na Wakili Stella Simkoko huku mjibu maombi akiwakilishwa na Mwakilishi binafsi Bw. Denise Mwamkwala. Nawashukuru wote kwa mawasilisho yao ambayo yamezingatiwa na yamekuwa muhimu katika uamuzi wa shauri hili. Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili na kuangalia kumbukumbu za Tume, hoja kuu iliyopo mbele yangu ni endapo kuna sababu za msingi kuishawishi Mahakama hii kufanya marejeo na kutengua uamuzi wa Tume ya Uamuzi na Usuluhishi. Hoja hii itajibiwa kwa kuangalia hoja zilizoibuliwa na mleta maombi katika maombi haya. Hoja ya kwanza katika maombi haya ni kama muamuzi alikuwa sahihi kuamua kwamba mjibu maombi alikuwa mwajiriwa wa mleta maombi. Kutokana na majibizano ya hoja za maandishi, inaonekana kiini kikuu cha mgogoro ni kwamba kati ya mleta maombi na Bi Rose Anna Aziz, ni nani hasa alikuwa mwajiri wa mjibu maombi. Kwa mujibu wa Wakili Simkoko, ushahidi katika Tume ulikuwa wazi kwamba kuna ushahidi unaoonyesha kuwa mjibu maombi hakumjua mwajiri wake kwani kuna 6 wakati alisema ameajiriwa na Rose Anna Aziz ila kitu kikiharibika kiwandani alikuwa anaenda kutengeneza. Hapa ni muhimu kuweka kumbukumbu sawa kwamba Kiwanda husika kinamilikiwa na mjibu maombi. Wakili Simkoko pia ana hoja kwamba, maelezo ya mjibu maombi yanaashiria kuwa siku ambazo hakuna kitu kilichoharibika kiwandani, mjibu maombi alifanya kazi nyumbani kwa Bi. Rose Anna Aziz na hivyo huyo ndiye aliyekuwa mwajiri wake na siyo mleta maombi. Akijibu hoja kuhusu ni nani mwajiri wa mjibu maombi, Bw. Denise Mwamkwala alieleza kuwa DW1 na DW2, wote wawili walitoa ushahidi kwamba wanamtambua mjibu maombi na kwamba wote walitoa kielelezo cha daftari la mahudurio ya mjibu maombi. Kwa maoni ya Bw. Denise, kwa ushahidi huo, ni dhahiri kuwa mjibu maombi alikuwa mwajiriwa wa mleta maombi. Baada ya kutafakari hoja za pande zote mbili, nimepitia pia kumbukumbu za ushahidi uliotolewa Tume na pande zote mbili kuhusiana na ni nani mwajiri wa mjibu maombi. Mfanyakazi wa mleta maombi Bw. Deo Vitalis Nyaulingo alitoa ushahidi Tume kama DW1. Yeye alieleza kuwa aliajiriwa na Kampuni (mleta maombi) kufanya kazi za nyumbani kwa mkurugenzi ambaye ni Engineer Rose Aziz. Kwa maelezo yake, nyumbani kwa mkurugenzi ni eneo moja na pale kilipo 7 kiwanda cha mieta maombi. Kwa mujibu wa ushahidi wake yeye na mjibu maombi walikuwa wafanyakazi nyumbani lakini mara nyingine walikuwa wanaitwa kufanya kazi za kampuni (mleta mambi) kiwandani. Shahidi wa pili Bi. Rose Aziz ambaye ni mkurugenzi anayemiliki sehemu kubwa ya hisa za mleta maombi naye alitoa ushahidi kama DW2 na alikanusha hoja kwamba mjibu maombi aliajiriwa na mleta maombi. Kwa maelezo yake, yeye ndiye aliyemwajiri mjibu maombi kufanya kazi za ndani. Alikanusha hoja kwamba mjibu maombi aliwahi kuachishwa kazi. Kwa mujibu wa maelezo yake, yeye ndiye aliyemwajiri mjibu maombi kumfanyia kazi za nyumbani na wala siyo mleta maombi. Na alikanusha hoja kwamba mjibu maombi aliwahi kuachishwa kazi. Kwa maoni yake, mlalamikaji aliacha kazi mwenyewe. Mlalamikaji Tume (mjibu maombi wa sasa) alionyesha barua ambayo ilipokelewa Tume kama kielelezo EMI ambayo inaonyesha maelezo ya mleta maombi akimwandikia barua ya utambulisho kwa yeyote anayehusika akielezea wasifu na utendaji wa mjibu maombi. Ni kutokana na ushahidi wa hapo juu Pamoja na barua ya wasifu wa mjibu maombi, muamuzi katika Tume aliridhika kuwa mjibu maombi alikuwa mwajiriwa wa mleta maombi kwa mujibu ya kifungu cha 61(a) 8 (b) (c) (d) (e) (f) na (g) cha Sura ya. 300 [R.E 2019]. Kifungu hicho kinasema:- 61. "For the purpose of a labour law, a person who works for, or renders services to, any other person Is presumed, until contrary is proved, to be an employee regardless of the form of the contract, if any one or more of the following factors are is present- (a) the manner in which the person works is subject to the control or direction of another person; (b) the person's hours of work are subject to the control or direction of another person; (c) in the case of a person who works for an organization, the person is part of that organization; (d) the person has worked for that other person for an average of at least forty five hours per month over the last three months; (e) the person is economically dependent on the other person for whom that person works or renders services; (f) the person is provided with tools of the trade or work equipment by other person, or (g) the person only works or renders services to one person. Kwa maoni yangu, kifungu hiki kinataka mahusiano yaonekane kuwa tu ni ya kiajira pale ambapo mtu anatoa huduma kwa anayedhaniwa kuwa mwajiri na vipengele 'a7 hadi 'g' katika kifungu tajwa hapo juu vikiwa vimetimizwa. Haina ubishi kuwa mjibu maombi, pamoja na kazi 9 alizofanya nyumbani kwa mkurugenzi, zipo nyakati ambazo alikuwa anafanya kazi za mleta maombi ikiwepo ujenzi wa jengo la kiwanda kama ilivyoelezwa katika barua (Kielelezo EMI). Kama ilivyo kwa kifungu cha 61z utoaji wa huduma uliofanywa na mjibu maombi utatafsiriwa kuwa ajira bila kujali aina ya mkataba uliohusika hadi hapo itakapothibitika tofauti. Haiko wazi katika kumbukumbu kama ni kwa muda gani mjibu maombi alihusika na kazi za mleta maombi. Hata hivyO/ kitendo cha kuwa aliwahi kuhusika kufanya kazi za mleta maombi kinaonyesha uwepo wa mahusiano ya kazi kati ya mleta maombi na mjibu maombi. Kama mahusiano haya yanatosheleza kuitwa mahusiano ya kiajira, hili ni jambo linalohitaji uchambuzi wa kisheria. Ni muhimu ikumbukwe kuwa ni jukumu la mwajiri kutunza kumbukumbu za mwajiriwa na pia mwajiri ana jukumu la kuthibibitisha aina ya ajiri kati yake na mwajiriwa. (Angalia Kifungu cha 15 (5) na (6) cha sura ya 366). Ushahidi wa mleta maombi kule Tume unaonyesha kuwa kuna nyakati mjibu maombi alikuwa anapewa kazi za kufanya katika kiwanda anachokimiliki. Ni kwa kiwango gani mjibu maombi alihusika na kazi hizi, hili ni jambo ambalo mwajiri au mleta maombi alipaswa kulifafanua na kulithibitisha. Ukosefu wa maelezo haya unafanya tafsiri ya haki ilalie upande wa mjibu maombi ambaye ndiye mwajiriwa kwani ni jukumu la 10 mwajiri kuthibitisha aina ya mahusiano ya kikazi aliyokuwa nayo na yeyote aliyefanya kazi kwake. Pamoja na kwamba muamuzi hakusema sababu zilizomfanya aamini kuwa kulikuwa na mahusiano ya kiajira kati yake na mjibu maombi, maelezo ya hapo juu yananifanya nikubaliane naye kuhusu hitimisho lake katika hoja hii kutokana na uwepo wa ushahidi kuonyesha kuwa kuna kazi za mleta maombi zilikuwa zinafanywa na mjibu maombi na hakuna ushahidi unaoonyesha kama kazi hizo hazikutosheleza kujenga mahusiano ya kiajira. Kutokutolewa kwa maelezo hayo na muamuzi hakujaathiri uhalisia wa haki hivyo sioni sababu ya kutofautiana na hitimisho lake katika hoja hii. Hoja nyingine iliyoibuliwa na mleta maombi ni endapo mwamuzi alikosea kuona kuwa mjibu maombi aliachishwa bila utaratibu na pasipo sababu halali. Mleta maombi anapinga hoja kwamba mjibu maombi aliachishwa kazi bila utaratibu kutokana akiendelea kushikilia msimamo wake kuwa hakumwajiri mjibu maombi. Mjibu maombi aliendelea kusisitiza kuwa aliachishwa kazi bila sababu na bila utaratibu kufuatwa. Mwamuzi alikuwa na maoni kuwa mleta maombi hakufuata utaratibu wakati wa kumwachisha kazi mlalamikaji. Katika ushahidi wake, mleta maombi alieleza kuwa mjibu maombi aliomba kuacha kazi yeye 11 mwenyewe. Jambo ninaloliona ni kwamba muamuzi hakuzingatia ushahidi uliotolewa kwamba mjibu maombi aliamua kuacha kazi yeye mwenyewe. Muamuzi alishawishiwa na barua iliyotolewa kama kielelezo EMI ambayo ni barua ya kumtambulisha mjibu maombi kwa yoyote atakayetaka kujua Habari zake. Nimeipitia barua hiyo lakini sikuona tafsiri yoyote inayoonyesha kuwa ilikuwa na lengo la kumwachisha kazi mjibu maombi. Kwa maoni yangu, naona mwamuzi alitakiwa kutafakari hoja ya muhimu kuangalia kama mjibu maombi aliachishwa kazi. Kitendo cha kwenda moja kwa moja kuangalia kama uchachishwaji wa kazi ulikuwa halali, kimetanguliza hitimisho dhaniwa kuwa kulikuwa na uachishwaji wa kazi. Kitendo cha kutokuwa na uchambuzi wa hoja ya endapo kulikuwa na uachishwaji wa kazi uliofanywa na mwajiri kinaacha shauri kuwa na hitimisho lisilotokana na uchambuzi sahihi. Kwa maoni yangu, endapo kulikuwa na uachishwaji kazi, hii ilikuwa ni hoja muhimu iliyopaswa kutazamwa na muamuzi kabla ya kuangalia kama kulikuwa na uhalali wa kuachishwa kazi. Nina maoni kuwa katika hili, muamuzi ali katika uundwaji wa hoja. Kabla ya kuhitimisha hoja endapo kulikuwa na sababu za kuachishwa kazi, lingetafutwa hitimisho kwanza kuhusu hoja ya endapo mlalamikaji aliachishwa kazi. Bila jambo hili kuhitimishwa, itakuwa vigumu kutathmini kama kulikuwa na sababu za kuachishwa kazi na kama utaratibu ulifuata. Kwa maoni yangu, ni jukumu la Tume 12 kuangalia hoja hii. Haitakuwa sahihi Mahakama hii kuibua hoja mpya na kuishughulikia kama haikufanyiwa kazi katika ngazi ya chini, yaani ngazi ya Tume. Kutokana na maoni yangu katika hoja ya pili, naona hoja ya msingi endapo kuna sababu za kuishawishi Mahakama hii kufanya marejeo na kutengua uamuzi wa tume imejibiwa kikamilifu kwama sababu hizo zipo. Nafuu iliyo sahihi kwa maoni yangu ni kurudisha shauri Tume ili muamuzi akaangalie na kuhitimisha hoja endapo mlalamikaji aliachishwa kazi au aliacha kazi mwenyewe. Lipo jambo linginelilioibuliwa ni kama shauri lilikuwa ndani ya muda. Kwa vile hili ni suala linalogusa mamlaka ya mahakama, ni muhimu likazingatiwa. Hata hili nalo kwa maoni yangu ni jambo la kuangalia katika ngazi ya baraza. Kutokana na uchambuzi wa hapo juu, nimeridhika kuwa kuna sababu za kutosha kuishawishi Mahakama kufanya marejeo ya uamuzi wa Tumen a hivyo hoja kuu katika maombi haya imejibiwa kikamilifu. Hivyo basi, ninarudisha kumbukumbu za shauri Tume ili hoja bishaniwa zikaundwe upya na kuangaliwa ili kuzingatia namna ambayo mlalamikaji katika tume ambaye ni mjibu maombi kwa sasa aliondoka kazini, endapo aliacha kazi au aliachishwa kazi pamoja na hoja endapo shauri 13 lilifunguliwa ndani ya muda. Ikithibitika kuwa aliachishwa kazi, ndipo Tume iangalie kama kulikuwa na sababu na kama taratibu zilizingatiwa. Maombi haya yanakubaliwa kwa kiasi hicho. Kila upande utashughulika na gharama zake. Imeamriwa hivyo. Imetolewa Dar es Salaam leo tarehe 7 Februari 2023. 14