Download PDF

Tanzania Judgment

TANZLII

MAOMBI YA MAREJEO NA 11431 OF 2024 RAJABU JUMA NYUMBA NA WENZAKE DHIDI YA WAMIUTA CO

On this page

Professional case brief

Research organized from the available case record

Source document

01

Holding and result

The court found that the evidence, particularly the service provision form (D1), established the applicants as casual service providers (kibarua) and not employees. The absence of an employment contract and the nature of payment (per service, not salary) supported the Commission's finding that no employment relationship existed. Thus, the application was dismissed for lack of merit.

Court disposition

application dismissed

Orders

  • Application is dismissed for lack of merit.
  • Right of appeal is granted.

02

Material facts

Parties

Rajabu Juma Nyumba

Applicant Counsel: Francis B. Mwakibinga

Ally Mohamed Matumla

Applicant Counsel: Francis B. Mwakibinga

Rashid Yusuph Mbonde

Applicant Counsel: Francis B. Mwakibinga

Shabani Waziri Makupete

Applicant Counsel: Francis B. Mwakibinga

Abdull Said Nyumba

Applicant Counsel: Francis B. Mwakibinga

Patrick John Mdee

Applicant Counsel: Francis B. Mwakibinga

Mohamed Salum Amour

Applicant Counsel: Francis B. Mwakibinga

Wamiuta Co. Ltd

Respondent Counsel: Avity Chrisostom Bakuza

03

Procedural history

  1. Posture

    Labour Revision / Final Judgment

04

Questions and positions

Legal issues

Party arguments

Applicant
Applicants argued they were employees of the respondent, performing cargo handling services at the port, and that the respondent failed to prove otherwise or provide employment contracts as required by law. They relied on statutory presumptions and cited relevant case law supporting their position.
Respondent
Respondent denied any employment relationship, asserting applicants were only issued introduction letters for port access, not employment contracts, and were paid allowances per service rendered, not salaries. The respondent maintained the applicants were independent service providers, not employees.

05

Court’s reasoning

  1. 01

    Section 61 of the Labour Institutions Act [Cap 300 R.E. 2019]

    Presumption of employment relationship based on control, economic dependence, and other statutory factors unless proven otherwise.

  2. 02

    Section 15 of the Employment and Labour Relations Act [Cap 366 R.E. 2019]

    Employer's duty to keep employment records and prove the nature of the relationship.

06

Ratio, limits and disposition

Ratio decidendi

The court found that the evidence, particularly the service provision form (D1), established the applicants as casual service providers (kibarua) and not employees. The absence of an employment contract and the nature of payment (per service, not salary) supported the Commission's finding that no employment relationship existed. Thus, the application was dismissed for lack of merit.

Obiter and limits

  • The employer's duty to keep employment records is recognized, but in this case, the contract was not of employment nature.

Court disposition

application dismissed

  • Application is dismissed for lack of merit.
  • Right of appeal is granted.

Source and reliance status

TANZLII · 1 January 2024

This page organises the available record for research. Confirm quotations, current status, and subsequent treatment against the official source before relying on the case.

Judgment reading view

Judgment text

The complete available source text.

Source document

TANZLII

Judgment· 1 January 2024

MAOMBI YA MAREJEO NA 11431 OF 2024 RAJABU JUMA NYUMBA NA WENZAKE DHIDI YA WAMIUTA CO

KATIKA MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA TANZANIA

DIVISHENI YA KAZI

DAR ES SALAAM MAOMBI YA MAREJEO NA. 11431 YA MWAKA 2024 RAJABU JUMA NYUMBA ................................... .......... MLETA MAOMBI 1 ALLY MOHAMED MATUMLA.......... ..................... .........MLETA MAOMBI 2 RASHID YUSUPH MBONDE.................................... . MLETA MAOMBI 3 SHABANI WAZIRI MAKUPETE......... ...........................MLETA MAOMBI 4 ABDULL SAID NYUMBA................ ................................ MLETA MAOMBI 5 PATRICK JOHN MDEE ...................................... .......... MLETA MAOMBI 6 MOHAMED SALUM AM OUR........ .............................................................. ..... MLETA

DHIDI YA WAMIUTA CO. LT D .... ............................ ................. ..... MJIBU MAOMBI

HUKUMU Tareheya amri ya mwisho: 05/ 07/2024 Tareheya hukumu: 23/ 07/2024 MLYAMBINA, J. Katika shauri hili, Waleta Maombi wanadai kuwa walikuwa ni Wafanyakazi wa Mjibu Maombi katika maridhiano ya kiajira kuanzia mnamo tarehe 12/07/2021 hadi siku ambayo waliachishwa kazi tarehe 24/10/2022. Kwamba, kazi hiyo ilikuwa ni utoaji wa huduma ya uchukuzi wa mizigo bandarini. Hivyo baada ya kuachishwa kazi walipeleka shauri lao mbele ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (itajulikana kama Tume). Baada ya Tume i kupitia ushahidi wa pande zote mbili ilitupilia mbali madai ya Waleta Maombi kwa kuamua kuwa kulikuwa hakuna mahusiano ya kiajira baina ya Waleta Maombi na Mjibu Maombi. Waleta Maombi hawakuridhishwa na maamuzi ya Tume, hivyo kuwasilisha maombi haya wakiomba Mahakama irejee maamuzi ya Tume na kuyatupilia mbali kwakuwa mahusiano ya kiajira yalikuwepo kwa wadaawa. Shauri hili limejikita katika hoja kuu mbili, ambazo ni: i. Kwamba, Muamuzi hakuzingatia ukweli dhidi ya mahusiano ya kiajira waliyokuwa nayo baina ya Waleta Maombi na Mjibu Maombi. ii. Kwamba, Muamuzi hakuzingatia ushahidi ambao muajiri hakuthibitisha kwamba walikuwa wanafanya kazi kwa malipo ya kamisheni bila ya uthibitisho wa mkataba ambapo mwajiri anaeleza hivyo wakati wajibu wa mwajiri ni kubainisha mkataba wa ajira na sio matatisho ya sheria ya kiufundi (technicality). Shauri hili liliendeshwa kwa njia ya maandishi. Mbele

ya Mahakama hii Waleta Maombi waliwakilishwa na Bw. Francis B. Mwakibinga, Mwakilishi Binafsi ilihali wakili Avity Chrisostom Bakuza alimwakilisha Mjibu Maombi. Kwakuwa hoja zilizowasilishwa mbele ya Mahakama hii zinaendana, zitatatuliwa zote kwa pamoja. Bw. Mwakibinga alieleza kuwa katika kifungu cha 61 cha Sheria ya Taasisi za Kazi[Sura ya 300 Kama ilivyorejewa mwaka 2019\ kinaeleza kwamba: For the purpose of a labour law, a person who works for, or renders service to, any other person is presumed, until the contrary is proved to be an employee, regardless of the form of the contract, if any one or more of the following factors is present; «)The manner in which the person works is subject to the control or Direction of another person; b)The person's hours of work are subject to the control or direction of another person; c)\n case of person who works for an - organization, the Person is part of that organization; d) The person has worked for that other person for an average of at lest 45 hours per month over the last three months; e)The person is economically dependent on the other person for whom of the person worker or renders services; f) The person is provided with tools of trade or work - equipment by the other person, or g) The person only works for or renders services to one person. Mwakilishi alirejea maamuzi mbalimbali yanayoelezea kwa kina mazingira nukuliwa hapo

juu ikiwa ni pamoja na Kesi ya Marejeo No. 11 ya 2019 ya madai iliyo amriwa Morogoro mbele ya Mh. Judge Z. G MURUKE J, baina ya ELIZABETH SILAYO (Mleta Maombi) dhidi ya HALMASHAURI YA MANISPAA MOROGORO (Mjibu Maombi), na pia vilevile katika kesi nyingine ya madai ya kikazi mbele ya Mahakama Kuu ya Tanzania Dar es Salaam, Marejeo Namba 291 ya 2009 baina ya DIRECTOR USAFIRISHAJI AFRICA dhidi ya HAMISI MWAKABALA and 25 OTHERS. Iliwasilishwa kuwa Waleta Maombi walikuwa na mahusiano ya kiajira na kesi hiso zinaunga mkono madai yao. Bw. Mwakibinga alieleza kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 15 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini[Sura ya 366 kama Hivyorejewa mwaka 2019], ni jukumu la Mwajiri kutunza kumbukumbu za ajira kama mahusiano ya Waleta Maombi na Wajibu Maombi yalikuwa ni ya kiajira au ni kazi maalum. Ilielezwa kuwa, vigezo vilivyotajwa hapo juu vilitakiwa kuthibitishwa na Mwajiri ambaye ndiye anapaswa kutunza mkataba na taarifa za ajira, kutokuwepo kwa ushahidi huo inamaana Waleta Maombi wataonekana kama walikuwa waajiriwa wa Mjibu Maombi mpaka ithibitishwe kinyume chake. Hivyo aliiomba Mahakama itupilie mbali maamuzi ya Tume. Malalamiko hayo yalipingwa vikali na Mjibu Maombi ambaye kupitia wakili Bakuza alikanusha vikali uwepo wa mahusiano ya kiajira baina yao. Alieleza kuwa, barua ya kusitisha utoji wa huduma (kielelezo D2) imetengenezewa mazingira ya kuachishwa kazi jambo

ambalo si kweli. Alifafanua kuwa Waleta Maombi walipewa tu barua za kuwatambulisha bandarini na sio barua za ajira kama ambavyo wanadai. Aliongeza kuwa aina ya kazi ya Waleta Maombi ilikuwa ni kubeba mizigo ya abiria bandarini hivyo, walikuwa wanalipwa posho tu na sio mshahara. Wakili Bakuza aliendelea kueleza kuwa, Mjibu Maombi alilazimika kuwafutia Waleta Maombi utambulisho (barua ya kusitisha utoaji huduma) bandarini kwakuwa walikuwa na mienendo mibaya. Aliendelea kuongeza kuwa, kwa mujibu wa kielelezo Dl, Waleta Maombi hawakuwa na mkataba wa ajira bali ilikuwa ni fomu tu ya makubaliano ya utoaji huduma. Kwa kifupi wakili huyo aliomba shauri hili litupiliwe mbali. Mahakama imepitia mawasilisho ya pande zote mbili pamoja na kupitia nyaraka za Tume na zile ambazo zimewasilishwa mbele ya Mahakama hii. Kifungu cha 61 cha Sheria ya Taasisi za kazi, [Sura ya 300 Kama Hivyorejewa 2019], kimeeleza mazingira mbalimbali yanayotumika kupima endapo kulikuwa na mahusiano ya kiajira au la kama walivyoeleza Waleta Maombi. Mazingira hayo yaliyoelezewa ni pamoja na namna ya ufanyaji kazi, masaa ya kazi, namna ya malipo, ugawiwaji wa vitendea kazi pamoja na mazingira mengine yanayoendana na hayo. Katika shauri hili, Waleta Maombi wamesisitiza kuwa walikuwa na mahusiano ya kiajira na Mjibu Maombi. Walieleza kuwa kwakuwa Mjibu Maombi ndiye mwenye jukumu la kutunza kumbukumbu za kiajira kama

ilivyoelezwa katika Kifungu cha 15 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini [Sura ya 366 Kama /iivyorejewa 2019] Hivyo basi, kwakuwa Mjibu Maombi ndiye alikuwa na mkataba alitakiwa kuutoa ili kuonesha mahusiano yao ya kiajira. Mojawapo ya kielelezo kilichotolewa mbele ya Tume ni kielelezo D1 (kinachosomeka kama Fomu ya Kujiunga na shughuli ya utoaji huduma ya uchukuzi kwa niaba ya Wamiuta Company Limited eneo la baggage room bandari ya Dar es Salaam). Kielezo hicho kilipokelewa na Tume bila ya pingamizi lolote. Sehemu ya kwanza ya fomu hiyo imeandikwa wazi kuwa atajaza kibarua (mtoa huduma). Hivyo, maneno hayo yaliyotumika yameweka wazi kabisa kuwa mahusiano sio ya mwajiri na mwajiriwa bali ni kibarua tu ambaye kitafsiri ya mwajiriwa hayumo katika kundi hilo. Katika fomu hiyo imeelezwa wazi pia kuwa kazi ya kibarua ilikuwa ni kupokea abiria wanaoingia na kutoka kwenye boti za kwenda Tanzania visiwani na kurudi Tanzania Bara na kubeba mzigo wa abiria endapo atakuwa nao na kuhitaji huduma ya kubebewa au kusafirishiwa mzigo huo kwa malipo watakayokubaliana na kibarua (mtoa huduma) ya uchukuzi kwa niaba ya Mjibu Maombi. Kwa misingi hiyo hapo juu, kwakuwa hakuna ubishi kuwa fomu hiyo ndiyo iliyotumika pia kufanya makubaliano ya kazi baina ya Waleta Maombi na Mjibu maombi, ni Dhahiri kuwa hapakuwepo na mahusiano ya kiajira. Hata mkataba huo bishaniwa umeeleza wazi kuwa ikitokea hakuna

abiria wanaohitaji kubebewa au kusafirishiwa mizigo yao, Mjibu Maombi hatowajibika kumlipa kibarua. Kwa msingi huo Waleta Maombi walikuwa wakijilipa wenyewe kutokana na kazi walizokuwa wanafanya kwa utaratibu wao. Mahakama imezingatia pia kielelezo D2 ambacho ni taarifa ya kusimamishwa kwa mtoa huduma kwa niaba ya Mjibu Maombi, Kama ambavyo imeamuriwa mbele ya Tume, kielelezo hicho hakielezi moja kwa moja mahusiano ya kiajira yaliyokuwepo baina ya wadaawa. Kielelezo hicho kikisomwa kwa pamoja na kielelezo D1 vinajieleza wazi kuwa kulikuwa hakuna mahusiano ya kiajira bali ni huduma ya uchukuzi ilikuwa ikitolewa kwa niaba ya Mleta Maombi. Nimezingatia pia kesi zilizorejewa na Waleta Maombi kuhusiana na uthibitisho wa uwepo wa mahusiano ya kiajira lakini mahusiano hayo hayajaweza kuthibitishwa. Pia, Mahakama inatambua ni jukumu la Mwajiri kutunza mikataba kama ilivyoelezwa kwa ufasaha na Bw. Mwakibinga lakini katika shauri hili, aina ya mkataba sio wa kiajira. Kwakuwa vigezo vyote vywa kuthibitisha mahusiano ya kiajira vimeshindwa kuthibitishwa katika shauri hili, Mahakama inaunga mkono maamuzi ya Tume kuwa kulikuwa hakuna mahusiano ya kiajira. Hivyo basi, maombi haya yanatupiliwa mbali kwa kukosa mashiko. Imeamuriwa hivyo. Y.J. MLYAMBINA

JAJI 23/ 07/2024 Hukumu hii imesomwa na kutolewa leo tarehe 23 Julai, 2024 mbele ya Francis Mwakibinga, Mwakilishi Binafsi wa Waleta Maombi na Avity Bakuza kwa niaba ya Mjibu Maombi. Haki ya rufaa imetolewa.

Source wording is retained. Consult the source document for its original formatting and pagination.

Authorities

Authorities used by the court

Cases, legislation, regulations, and constitutional provisions identified in the available record.

Elizabeth Silayo v. Halmashauri ya Manispaa Morogoro, Labour Revision No. 11 of 2019

Case cited

Director Usafirishaji Africa v. Hamisi Mwakabala and 25 Others, Labour Revision No. 291 of 2009

Case cited

Labour Institutions Act [Cap 300 R.E. 2019]

Legislation

Legislation referenced in the available case record.

Employment and Labour Relations Act [Cap 366 R.E. 2019]

Legislation

Legislation referenced in the available case record.

Case-aware research

Ask AI about this case

The judgment and available research above are public. New questions open in a separate private conversation grounded in this case.

About this LexChat collection

This page organizes the available case record for research. Verify quotations, current status, and subsequent treatment against the source document. Corrections can be reported to hello@esheria.ai.

Legal information, not legal advice. Research summaries do not replace the judgment.