rehema mafaume na wenzake wawili vs dar es salaam city council 2022 tzhcld 848 9 september 2022
The Commission for Mediation and Arbitration erred by relying solely on a report (R1) without producing the alleged forged certificate as evidence. The applicant possessed a valid technical certificate from Mgulani, and there was no sufficient proof of forgery. The dismissal was not justified under the applicable...
Source-derived case information.
- Citation
- rehema mafaume na wenzake wawili vs dar es salaam city council 2022 tzhcld 848 9 september 2022
- Parties
- Applicant: Rehema Mfaume; Applicant: Lucy Mongi; Applicant: Lydia Mwakasege; Respondent: Dar es Salaam City Council
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 9 September 2022
- Procedural Posture
- Labour Revision / Final Judgment
- Outcome
- application allowed in part
- Legal Topics
- Termination of Employment, Qualification Requirements, Forgery of Certificates, Public Service Regulations
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Rehema Mfaume
Applicant
Lucy Mongi
Applicant
Lydia Mwakasege
Applicant
Dar es Salaam City Council
Respondent
Procedural Posture
Labour Revision / Final Judgment
Legal Issues
- 1 Whether there was evidence to prove Rehema Mfaume forged a VETA certificate
- 2 Whether the applicants should have been reinstated based on qualification requirements
Ratio Decidendi
The Commission for Mediation and Arbitration erred by relying solely on a report (R1) without producing the alleged forged certificate as evidence. The applicant possessed a valid technical certificate from Mgulani, and there was no sufficient proof of forgery. The dismissal was not justified under the applicable public service regulations.
Court Disposition
application allowed in part
Orders
- The Commission's decision of 15 April 2020 against Rehema Mfaume is set aside.
- The Commission's decision of 31 October 2017 reinstating Rehema Mfaume remains in force.
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
MAHAKAMA KUU YA TANZANIA DIVISHENI YA KAZI PAR ES SALAAM MAREJEO NA. 94 YA 2022 REHEMA MAFAUME.................... MLETA MAOMBI NAMBA MOJA LUCY MONGI............................. MLETA MAOMBI NAMBA MBILI LYDIA MWAKASEGE................... MLETA MAOMBI NAMBA TATU DHIDIYA DAR ES SALAAM CITY COUNCIL........................ MJIBUMAOMBI (Kutokana na Uamuzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi na Uamuzi Kanda ya DSM - Ilala) (Massay: Muamuzi) ya tarehe 31.10.2017 na 15.04.2020 Katika CMA/DSM/ILALA/R.900/16/872 HUKUMU 25.08 & 09.09.2022 Rwizile, J Waleta maombi wameleta maombi haya wakiomba Mahakama kupitia Tuzo zilizotolewa na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (TUME), tarehe za 31 Oktoba, 2017 na 15 April!, 2020 na kuyatengua. i Katika maombi haya, inaelezwa kwamba waleta maombi waliajiriwa na Mjibumaombi kwa nafasi tofauti tofauti kati yam waka 1997 na tarehe 02 Juni, 2003. Waleta Maombi waliachishwa kazi kwa ukosefu wa ujuzi tarehe 31 Agosti, 2016. Walifikisha shauri mbele ya tume ambapo walalamikaji 10 kati yao walirudishwa kazini. Wajibumaombi hawakurudishwa kazi, hivyo walileta maombi ya maregeo Na. 548/2017, Mahakamani Kuu. Siku ya kusikiliza maombi yao, Mjibumaombi alikubali kuwarudisha kazini. Mahakama ikaamuru shauri kurudishwa Tume ili ikasikilize kuhusiana na suala la vyeti- bandia (vyeti feki). Mbele ya Tume, shauri lilisikilizwa na kuamriwa, kwakuwa Rehema Mfaume alikugshi cheti che Veta, hakutakiwa kurudishwa kazini. Alifungua maombi haya baada ya kutoridhika na uamuzi wa Tume. Maombi haya yameambatanishwa na kiapo cha pamoja cha waleta maombi, kikiainisha sababu za maombi haya kama ifuatavyo: - i. Muamuzi alitenda kosa kisheria kwa kutotoa amri ya kumrudisha kazini mieta maombi namba moja biia Ushahidi kwamba amegushi cheti. ii. Muamuzi alitenda kosa kisheria kwa kutotoa amri ya kurudishwa kazini kwa waleta maombi namba mbili na tatu kwa sababu ya kutokuwa na ujuzi na wakati muamuzi hakuuzingatia ushahidi wao. 2 Hi. Muamuzi aiikosea kwa kutokuzingatia muundo wa kazi wa tarehe 10.04.2004 amabo ulieleza kuwa wafanyakazi walioajiriwa kabia ya tarehe 20.05.2004 hawakuhitajika kuwa na eiimu ya kidato cha nne. Kila upande ulipata nafasi ya kuwakilishwa. Waletamaombi waliwakilishwa na Shafii Mafita, Wakili na Mjibumaombi aliwakilishwa na Wakili wa Serikali, Hussein Kambi. Wakati shauri likiendelea siku ya tarehe 15 Juni, 2022 bwana Kambi aliwasilisha pingamizi la awali akiifahamisha Mahakama kuwa waleta maombi namba mbili na tatu, maombi yao yapo nje ya muda. Bwana Shafii katika kujibu hilo alikubaliana na pingamizi hilo. Hivyo, maombi ya Waleta Maombi Na. 2 na 3 yafukuzwa. Hivyo maomba haya ni kwa ajili ya Mleta maombi Namba moja pekee. Bwana Mafita aliwasilisha kuwa mleta maombi namba moja aliajiriwa na mjibu maombi tarehe 01 Januari, 2001 kuwa ufundi umeme kwa cheti cha ufundi katika Chou cha Mgulani na akathibitishwa tarehe 26 Septemba, 2003. Aliendelea kueleza kuwa tarehe 31 Agosti, 2016, Mjibumaombi alimuachisha kazi kwa kukosa cheti cha kidato cha nne. Aliendelea kuwasilisha kuwa Mleta maombi na wenzake walipeleka mgogoro wao mbele ya Tume. Tuzo ilitolewa na Mjibu maombi 3 hakuridhika na Tuzo hiyo. Aliongeza kwa kusema kuwa Mjibumaombi alifungua shauri la Marejeo Mahakamani Kuu yaliyopewa Na. 548 ya 2019. Lakini shauri likiwa linaendeia Mjibumaombi alikubalina na Tuzo ya Tume na akaomba muongozo kuhusiana na vyeti bandia. Mahakama ikatoa uamuzi wa kurudisha shauri mbele ya Tume ili hoja hiyo isikilizwe. Bwana Mafita aliendelea kuwasilisha kuwa hoja hiyo ilisikilizwa na tume ikakataa kumrudisha kazini Mletamaombi kwa madai kuwa alikuwa na cheti bandia cha veta. Kwa maelezo yake, ni kuwa Mleta maombi alisoma chuocha ufundi Mgulani na cheti chake kimefanyiwa uhakiki na kuthibitika kuwa ni cheti halisi. Akaeleza kuwa Mleta maombi anaomba maombi yake kukubaliwa ili arudishwa kazini. Aliendelea kusema kuwa Mleta maombi aliachishwa kazi kwa kuwa hakuwa na sifa za ufaulu wa kidato cha nne. Wakati kwa maelezo yake sababu hiyo inakinzana na Waraka wa Utumishi wa Umma namba 1 wa mwaka 2004 kama ulivyofafanuliwa 10 Aprili, 2006. Waraka unaeleza kuwa kwa mtumishi aliyeajiriwa kabla ya tarehe 20 Mei, 2004 ulipoanza kutumika waraka 1 wa 2004, hatalazimika kuwa na cheti cha kidato cha nne ili kuendelea na ajira. Alieleza tena kuwa mleta maombi namba moja alishindwa kufikisha cheti cha Veta kilichodaiwa na Mjibumaombi kuwa kipo kwenye jarada kwakuwa yeye hakusoma Veta bali Mgulani. Aliifahamisha Mahakama 4 kuwa pamoja na maelezo ya mjibu maombi lakini hakufikisha hicho cheti aiichosema kipo kwenye jarada. Kisha akafahamisha kuwa cheti kilichowasilishwa na Mjibumaombi siku ya tarehe 13 Julai, 2022 mbele ya Tume hawajui amekitoa wapi. Alihitimisha kwa kuomba uamuzi wa Tume utenguliwe na Mjibumaombi arudishwa kazini. Katika kujibu hoja, Bw. Kambi Wakili wa Serikali alisema kuwa barua ya kufukuzwa kazi Mletamaombi haikinzani na Waraka wa Utumishi wa Umma namba 1 wa mwaka 2004 kama ilivyoamriwa na Tume katika tuzo ya tarehe 31 Oktoba, 2017 ambapo iliamriwa arudishwe kazini. Alieleza kuwa ilishindikana kurudishwa kazini kwakuwa iligundulika kuwa ana cheti bandia cha Veta (kilichokutwa kwenye faili binafsi la kazini) na hivyo akakosa sifa ya kurudishwa kazini. Aliifahamisha Mahakama kuwa mtumishi ndiye mwenye wajibu wa kuwasilisha cheti chake ofisini na endapo mwajiri akiwa na mashaka huwasilisha kwenye mamlaka husika kwa ajili ya uhakiki. Na hivyo madai ya Mletamaombi kuwa cheti hicho cha Veta hakikuwasilishwa Tume hayana msingi kwakuwa Veta walithibitisha kwa barua yao ya tarehe 10 Novemba, 2017. 5 Alimalizia kwa kuomba kuwa maombi haya yaondolewe kwakuwa yeye mwenyewe ndiye alipaswa kujilaumu kwa kuwasilisha kwa vyeti viwili vya ufundi vilivyotolewa na vyuo viwili tofauti vya ufundi. Alifafanua na kusema kuwa cheti cha veta kilikuwa namba ya usajili EL/99/383 kilichotolewa tarehe 15 Januari, 2000 na cheti cha Mgulani JKT chenye namba ya usajili MGVTC/98/0278 cha mwezi Agosti, 1999. Katika mawasilisho ya nyongeza Bwana Mafita alieleza kuwa suala la vyeti bandia halikuwa kiini cha mgogoro mbele ya Tume bali liliibuliwa wakati wa kusikiliza kesi ya marejeo yenye Na. 548/2017. Alieza zaidi kuwa mleta maombi hakuwasilisha vyeti viwili kwa mwajiri wake na kama angefanya hivyo cheti cha Veta kingepelekwa mbele ya Tume kama kielelezo. Na kisha akaendelea kuomba Tuzo hiyo kutenguliwa. Baada ya kupitia mawasilisho ya pande zote mbili, Mahakama hii imeona kuna hoja inayobishaniwa: - I. Iwapo kuna ushahidi wa kuthibitisha Mietamaombi aiigushi cheti cha Veta. Katika hoja hii, Mleta maombi kupitia mwakilishi wake ameeleza kuwa hakuwasilisha cheti cha Veta kwa Mjibumaombi wakati akiomba kazi na hivyo hakitambui. Mjibu maombi aliipinga hoja hiyo kwa kueleza kuwa mleta maombi alipokuwa akiomba kazi alitumia vyeti viwili, cha 6 Veta pamoja na Mgulani (JKT). Katika kupitia mwenendo wa mgogoro mbele ya Tume, Mahakama imebaini wazi bila ya shaka kuwa mleta maombi alipoajiriwa aliomba kazi kwa kutumia cheti. Hii imethibitishwa na kielelezo R1 ambacho kimeeleza wazi kuwa mleta maombi namba moja alitumia cheti cha kugushi. Kwa urahisi wa rejea: - 'YAH: UHAKIKI WA VYETI Katika kumbukumbu zetu inaonyesha: - NO. Jina Na ya usajiH Cheti No. Maelezo 1. Dotto S. Kitego MV/889/97 C011282 Cheti haiaii 2. ... 3. ... ... 4. ... ... 5. 6. ... ... ... 7. Rehema Hamadi Mfaume EL/99/383 A 064680 Cheti cha kughushi // Hivyo kwa uthibitisho huo kutoka katika Chuo cha Veta uliothibitishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Utahini na Vyeti. Mahakama hii imeridhika kulikuwa cheti cha Veta. Katika kuchunguaza hoji kwa undani, Mahakama imebaini kuwa Mleta maombi kutorudishwa kazini kulitoka na cheti cha Veta cha kughushi. Kama kilivyooneshwa kwenye taarifa Rl. Pia Mjibumaombi anaeleza kuwa Mletamaombi alipoajiriwa alipeleka vyeti viwili kimoja cha Chuo cha 7 Mgulani na cha Veta. Maelezo ambayo hata Mleta maombi kupitia mwakilishi wake anayakubali ni kuwa alipoajiriwa alifikisha kwa mwajiri cheti hicho cha Mgulani. Mahakama katika hilo ilipitia kielelezo cha barua ya ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa miundo ya utumishi inaeleza wazi kuwa kwa mtumishi ambaye hatakuwa na cheti cha kidato cha nne aweze kutambulika endapo atawasilisha cheti cha taaluma katika muundo wa utumishi wa kada yake. Kwa urahisi wa rejea: - ’’ 10 Apriii, 2006 UFAFANUZI KUHUSU UTEKELEZAJI IV/1 MIUNDO YA UTUMISHI YA KADA MBAUMBALIILIYOTOLEWA MWAKA 2002 PAMOJA NA WARAKA WA UTUMISHI NA. 1 IV4 A7I454/C4 2004 1. ... 2. ... 2.1 ... • Hi kuwatendea haki watumishi wa aina hii sasa imeamuiiwa kuwa mtumishi asiye na cheti cha kufauiu mtihani wa kidato cha Nne iakini baada ya kumaiiza eiimu ya msingi aiipata mafunzo ya stadi za kazi yanayohitajika katika 8 muundo wa utumishi wa kada yake na kupata cheti kinachotambulika katika kada yake na kupata cheti kinachotambulika katika kada yake atambulike kwamba ana sifa ya cheti inayolingana na kite cha kufauiu mtihani wa kidato cha nne. Watumishi wa aina hii waingizwe katika miundo iiiyohuishwa na pia kupandishwa vyeo iwapo sifa Hiyomkwamisha tangu kutoiewa kwa miundo mipya ni kutokuwa na cheti cha kufauiu mtihani wa kidato cha nne." Hivyo cheti cha chuo chochote cha taaluma katika kada husika kilikuwa kinakubalika. Kama ambavyo mwakilishi wa mleta maombi namba moja alivyoeleza kuwa mleta maombi alikuwa na cheti toka katika Chuo cha Mgulani na ndicho kilichotumiwa na mleta maombi namba moja katika kuajiriwa kwake. Maelezo hayo yanathibitishwa kwa ushahidi wa barua kutoka katika chou hicho. Kwa rahisi ya rejea: - "MGULANI CHUO CHA UFUNDI... Yah: Uhakiki wa weti wa Ufundi Rehema Mfaume Chuo kinathibitisha kuwa REHEMA MFAUME aiijiunga na chuo chetu mnamo mwaka 1998 na kuhitimu mwaka 1999 katika kozi ya "Electrical Installation 9 Kwa uthibitisho wa barua hii iliyotolewa na Mkuu wa chuo inathibitisha kuwa mleta maombi namba moja alikuwa na cheti halali kutoka katika Chuo tajwa. Cheti hicho kipo kama sehemu ya kumbukumbu na ni VTC No. 00185, na nambari ya usajili ni MGVTC/98/0278, cha August 1999. Mahakama hii katika kupitia ushahidi na vielelezo imebaini kuwa Mleta maombi alikuwa na kigezo cha kurudishwa kazini kwa kutumia cheti cha Mgulani kama ambavyo kimethibitika kuwa halali. Hakuna shaka katika hilo. Nimepitia ten na tena maelezo ya pande zote 2 na ushahidi uliopelekwa mbele ya Tume. Imebainika kwamba cheti kilichogushiwa ni chenye namba ya usajili EL/99/383 na namba ya cheti chenyewe ni A064680. Cheti hii kimetajwa tu kwenye taarifa kutoka Veta. Hakikutolewa kama kielelezo. Inamaana hakipo kwenye kumbukumbu za Tume au Mahakama. Hivyo ni dhahili Tume haikupata nafasi kuikiona cheti hicho na kuona usahihi wa taarifa ya Veta-Rl. Kama kweli kipo kwanlnl hakikutolewa kama kielelezo. Kwa mantiki hiyo, Mahakama inaona kuwa tume haikuwa sahihi kuamini tu taarifa kielelezo R1 bila kuona cheti chenyewe. Tume ilikuwa na wajibu wa kupima na kulinganisha taarifa zilizo katika R1 kama zinawiana na cheti halisi. Kwa kuwa cheti hizo ndicho kiini cha kumfukuza Mleta Maombi ni jambo la 10 kushangaza kuona nyaraka hiyo muhimu haipo katika kumbukumbu ya Tume. R1 siyo cheti chenyewe ni taarifa tu. Kwa mantiki hiyo uamuzi wa tume dhidi ya Reheme Mfaume, uliotolewa tarehe 15.4. 2020 unatenguliwa. Hii inamaanisha kuwa uamuzi wa Tume wa tarehe 31.10.2017, unabaki kama ulivyo tolewa. Kila upande utajilipia gharama zake. A.K. Rwizile JAJI 09.09.2022 ii