retone garage company ltd vs christian bernard milikioni na wenzake wawili 2022 tzhcld 847 29 august 2022
The applicant failed to provide evidence of the employment contracts' terms and remaining period at the time of dismissal. The Commission's award of 12 months' salary compensation stands, as the employer did not discharge the burden of proof regarding lawful termination or contract duration.
Source-derived case information.
- Citation
- retone garage company ltd vs christian bernard milikioni na wenzake wawili 2022 tzhcld 847 29 august 2022
- Parties
- Applicant: Retone Garage Company Ltd; Respondent: Christian Bernard Milikioni; Respondent: Solomon Frank Makala; Respondent: Pascal Gervas Mgamba
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 29 August 2022
- Procedural Posture
- Labour Revision / Final Judgment
- Outcome
- application dismissed
- Legal Topics
- Termination of Employment, Fixed Term Contracts, Compensation for Unfair Dismissal
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Retone Garage Company Ltd
Applicant
Christian Bernard Milikioni
Respondent
Solomon Frank Makala
Respondent
Pascal Gervas Mgamba
Respondent
Procedural Posture
Labour Revision / Final Judgment
Legal Issues
- 1 Whether the Commission was correct to award 12 months' salary compensation to respondents under a fixed-term contract
- 2 Whether the respondents were unfairly dismissed without following proper procedures
- 3 Whether the applicant proved the existence and terms of the employment contracts
Ratio Decidendi
The applicant failed to provide evidence of the employment contracts' terms and remaining period at the time of dismissal. The Commission's award of 12 months' salary compensation stands, as the employer did not discharge the burden of proof regarding lawful termination or contract duration.
Court Disposition
application dismissed
Orders
- Each party to bear its own costs
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
MAHAKAMA KUU YA TANZANIA DIVISHENI YA KAZI PAR ES SALAAM MAREJEO NA. 69 YA 2022 RETONE GARAGE COMPANY LTD .................... MLETA MAOMBI DHIDI YA CHRISTIAN BERNARD MILIKIONI................................I. MJIBU MAOMBI SOLOMON FRANK MAKALA............................................ 2. MJIBU MAOMBI PASCAL GERVAS MGAMBA................................. 3.MJIBU MAOMBI (Kutokana na Uamuzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Kanda ya DSM- Ilala) (Nyagaya: Muamuzi) Tarehe 31. 01. 2022 katika CMA/DSM/ILA/776/20/404 HUKUMU 02nd & 29th August 2022 Rwizile J Mleta maombi ameleta maombi haya akipinga uamuzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ('Turne'). Ameomba Mahakama ipitie jalada la Tume na kutengua uamuzi wa Tume katika mgogoro wa kazi Na. CMA/DSM/ILA/776/20/404 wa tarehe 31.01.2022. Maelezo ya jumla ni kwamba, mleta maombi ni mmiliki wa karakana ya kukarabati magari. Inaelekea wajibu maombi waliajiliwa kwa nyakati tofauti i kama mafundi sanifu. Ina semekana kwamba mikataba yao ya ajila ilianza kati ya waka 2014 mpaka 2016. Mnamo 03.10.2020, wajibu maombi walifukukuzwa kazi na mleta maombi. Kwa mujibu wa maelezo yao, hawakulipwa stahiki zao. Hii iliwafanya kufungua mgogoro wa kikazi katika Tume. Baada ya kusikiliza pande zote mbili. Tume iliona wajibu maombi walifukuzwa isivyo halili na bi la kufuata taratibu. Ilimwamuru mleta maombi kiwalipa kila mmoja wao fidia ya mishahara ya miezi 12. Mleta maombi hakuridhishwa na umauzi huo, akamua kuleta maombi haya mbele ya Mahakama. Kama ilivyo ada, maombi haya yameletwa kwa klapo cha mleta maombi kikiapwa na ndugu Zhang Chun Yu amabaye ni afisa mwandamizi. Katika kiapo, mleta maombi ameeleza sababu za maombi haya kama ifuatavyo; i. Kama Hikuwa sahihi kisheria kwa Muamuzi kutoa Tuzo bila kuzlnagatia aina ya mkataba wa ajira baina ya pande mbili. ii. Kama Hikuwa sahihi kwa muamuzi kuamua kwamba wajibu maombi walifukuzwa bila kufuata taratibu badala ya kuanagafi kama kulikuwepo tu na ujunjwaji wa mkataba wa kazi 2 Hi. Kama Hikuwa sahihi kwa muamuzi kuamru wajibu maombi walipwe fidia ya miezi 12 wakati walikuwa na mkataba wa kipindi maaium. Msomi, wakili Felix Makene, alimwakilisha mleta maombi, wakati wajibu maombi walijitetea wenyewe. Katika mawasilisha yake, Ndugu Makene aliimbia mahakama kwamba wajibu maombi walikuwa na mkataba wa mwaka mmoja. Hivyo haikuwa sahihi, tume kutoa fidia ya miezi 12 wakati walishatumikia miezi 10. Kwa hakika aliongeza kuwa walistahili kulipwa miezi 2 tu iliyokuwa imebaki katika maktaba wao. Hoja hii, alisema inaungwa mkono na shauri la Mtabwa Shamte dhidi ya Care Sanitation and Suppliers, Marejeo.Na 154/2010. Katika uk. 8-10, pamoja na kanuni ya 4 (1) ya Tangazo la Na 42/2007. Akifafanua hoja ya pili, Bwana Makene alisema hapakuwepo kuachishwa kazi isivyo halali labda kama ni kuvunja mkataba.Tume ilitakiwa kutofautisha, kati ya kuvunjwa na kusitishwa kwa mkataba. Hivyo itoshe kusema mkataba ulivunjwa na sio kuachishwa kazi bila kufuata utaratibu. Katika, hoja hii, wakili aliomba Mahakama kuangalia kanuni 8(2)(b) ya Tanagzo la Serikali 3 Na. 42/2007 ambapo mwajiri na mwajiriwa wanaweza kuvunja mkataba kwa makubaliano. Tarehe 03.10.2020, alitoa hoja kwamba wajibu maombi walikubaliana na mwajiri wao kuvunja mkataba. Walilipwa miezi 2 na zaidi, hawa ndio baada ya hapo waliamua kuja mbele ya Tume. Wakili aliomba Mahakama iamuru kwamba mkataba ulivunjwa na kama walistahili, walipwe kama wanavyostahili miezi 2 tu. Katika kujibu hoja, Bwana Christian alisema Mkataba wa kwanza ulikuwa wa maneno tangu 2014 -2017. Anafafanua, mwekezaji mpya aliingia na kuomba mkataba uliendelea kama zamani. Anasema, mkataba waliongia ulikuwa mwaka mmoja na kwamba ulianza 2017 japo hawakupewa nakala yake. Anaendelea kusema, hapakuwepo mkataba mwingine mpaka 2020. Aliseama, mwezi October asubuhi wakati anaingia kazini alisema alifukuzwa kazi bila malipo yoyote. Kwa upande wake Bwana Salomon, aliimbia mahakama kwamba alianza kazi tarehe 09.06.2016, kwa mwajiri wa zamani katika makataba wa mwaka mmoja. Mwaka 2018, Kampuni iliunzwa kwa mwajiri mpya, mleta maombi. Huyu mwajiri mpya alisema aliingia nao mkataba wa mwaka mmoja ambao 4 hata hivyo hakuwapa nakala. Aliendelea kujieleza kwamba tarehe 30.09.2020 alifukuzwa kazi baada ya kulipwa mshahara. Akihitimisha hoja za wajibu maombi bwana Mgamba, alisema alianza kazi 29.09.2016. Anasema mwaka 2018, alikuja mwekezaji mpya. Akiwa kwa mwekezaji mpya, aliingia mkataba mwaka mmoja 2018. Anasema hakupewa mkataba mwingine hadi alipoachishwa kazi. Bwana Makene alimazia kwa kusema kwamba, wajibu maombi walikuwa na mkataba wa muda maalum na ulikuwa umebakiza muda wa miezi 2. Hivyo kama wanastahili walipwe kiasi kilichobaki. Baada ya kupitia hoja za pande mbili. Itoshe kusema kwamba ni wajibu wa mwajiri kuthibisha kwamba waajiriwa walifukuzwa kazi kwa utaratibu. Hoja ya msigi inayopaswa kuamriwa ni kama Tume ilikuwa sahihi kuwalipa wajibu maombi fidia ya miezi 12 na hali kulikuwa na mkataba wa muda maalum. Wakati shahidi wa mleta maombi anatoa ushahid mbele ya Tume alisema kwamba hawatambui wajibumaombi na kwamba kampuni anayosimamia 5 ilianza kazi mwaka 2017. Hivyo kwa mujibu wa maelezo yake hatambui tuhuma za mwaka 2014 mpaka 2016. Hata hivyo hakuieleza tume yeye kama mwajiri mwenye wajibu wa kutunza taarifa za wafanayakazi wajibumaombi waliajiriwa lini. Ni ukweli usipongika kwamba wajibumaombi walikuwa wafanyakazi katika karakana hiyo kwa vipindi tofauti na kwa mujibu wa maelezo yao. Nasema kwa mujibu wa maelezo yao kwa sababu hakuna Ushahidi toka kwa mwajiri unatoapicha tofauti. Itoshe kusema kwamba kama mleta maomba hakuleta Ushahidi wowote wa maana kuthibitisha shauri mbele ya tume, ni dhahiri hana ushahidi zaidi wa wajibumaombi. Katika kupitia ushahidi wa pande zote mbili, ni dhahiri kwamba mwajiri ameshindwa kutoa mikataba ya ajira ya wajibu maombi. Hii ina maanisha ni kweli kwamba wajibu maombi walinyimwa mikataba yao pale baada ya kuitia Saini kama walinvyoeleza. La muhimu ni kwamba hata wao wanakili kwamba walikiwa na mkataba wa mwaka mmoja. Mkutaba huo, unasemekena ulikuwa kuanzia mwaka 2018. Lakini walifukuzwa kazi mwaka 2020. Hii inamaisha kwamba, kipindi hicho chote walikuwa na mkataba wa mmoja mmoja uliendelee mpaka walipo achishwa kazi. 6 Wakili wa mleta maombi alisema kwa kuwa wajibumaombi hawakubishia uwepo wa mkataba huo, basi walipwe stahili yao ya miezi 2 kwani ndiyo iliyokuwa imebaki. Hii hoja ni nzuri, lakini haina ushahidi unaooneshe mkataba ulianza tarehe ngapi mpaka wanafutwa kazi mwezi wa 10 kulikuwa kumebakia muda gani. Haya maneno kwa mtazamo wangu hayatokani na ushahidi mbele ya tume. Nashawishika kusema ni hoja ya wakili. Kimsingi mashauri hayaamriwi kwa mtiririko mzuri wa hoja bali mtiririko mzuri wa Ushahidi unaothibisha mnyororo wa matukio kabla na baada ya mikataba. Pamoja na ukweli kwamba ninaona kunautata katika ushahidi was wajibumaombi lakini ni lazima kikiri kwamba si kazi yao kuthibitisha walianza lini mkataba na ulitakiwa kuisha lini. Kama walivyo sema, ninakubaliana na maelezo yao na pia uamuzi wa tume kwamba, mleta maombi aliwafukuza kazi bila kuwalipa stahili zao zote. Wakiti ninafukuza maomba haya, ninawiwakusema kwamba hainamaana kwamba kwa kuwa wajibumaombi walifukuzwa mwezi 10, walikuwa wamebakiza miezi 2 tu kumaliza mkataba wao. Hili ni jambo amabalo linaweza kuthibitishwa kwa ushahidi tu, kitu ambacho mwajiri hakufanya. 7 Kwa sababu hiyo, mahakama haya, yanaona maombi haya hayana msingi yanatupiliwa mbali. Na kila upande utajilipia gharama zake. \ A.K. Rwizile V JAJI ; -{ ' ■ . ..... ' 29.08.2022 8