revocatus m mandago vs mazava fabrics production ea ltd 2021 tzhcld 142 3 juni 2021
The Commission lacked jurisdiction to entertain the applicant's dispute as he was terminated during a probationary period of less than six months, and the law does not provide protection or remedies for unfair termination in such circumstances.
Source-derived case information.
- Citation
- revocatus m mandago vs mazava fabrics production ea ltd 2021 tzhcld 142 3 juni 2021
- Parties
- Applicant: Revocatus M. Mandago; Respondent: Mazava Fabrics Production E.A. Ltd
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2021
- Procedural Posture
- Labour Revision / Judgment
- Outcome
- application dismissed
- Legal Topics
- Probationary Employment, Termination of Employment, Jurisdiction of Labour Commission
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Revocatus M. Mandago
Applicant
Mazava Fabrics Production E.A. Ltd
Respondent
Procedural Posture
Labour Revision / Judgment
Legal Issues
- 1 Whether the Commission for Mediation and Arbitration had jurisdiction to hear a dispute concerning termination of employment during probation period
- 2 Whether the applicant's claim was for breach of contract or unfair termination
Ratio Decidendi
The Commission lacked jurisdiction to entertain the applicant's dispute as he was terminated during a probationary period of less than six months, and the law does not provide protection or remedies for unfair termination in such circumstances.
Court Disposition
application dismissed
Orders
- application for revision dismissed
- decision of the Commission for Mediation and Arbitration upheld
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA DIVISHENI YA KAZI ILIYOKETI MOROGORO MAREJEO NA. 25 YA 2020 BAINA YA REVOCATUS M. MANDAGO............................................................ MLETA MAOMBI NA MAZAVA FABRICS PRODUCTION E.A. LTD............................... MJIBU MAOMBI HUKUMU Tarehe ya Amri ya mwisho: 19/05/2021 Tarehe ya Hukumu: 03/06/2021 A. E. MWIPOPO, J. REVOCATUS M. MANDAGO, ambaye ni Mleta Maombi katika shauri hili la Marejeo, ameleta maombi haya ya marejeo akiomba Mahakama irekebishe Uamuzi Mdogo wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi uliotolewa katika mgogoro wa kikazi Na. CMA/MORO/141/2019 wa tarehe 27 Januari, 2020. Mleta Maombi anaomba yafuatayo: 1. Mahakama hii ikipendezwa iitishe kumbukumbu za Tume ya Usuluhishi na Uamuzi iliyoketi Morogoro kwa ajili ya kurekebisha mwenendo mzima na uamuzi wa Tume katika mgogoro wa kikazi Na. CMA/MORO/141/2019 wa tarehe 27 Januari, 2020, uliotolewa Mhe. Kayugwa, H., Msuluhishi. i 2. Mahakama hii ikipendezwa itoe amri ya kurudishwa kwa Mgogoro wa Kikazi Na. CMA/MORO/141/2019 mbele ya Tume ili pande zote mbili ziweze kusikilizwa. 3. Mahakama hii ikipendezwa iweze kutoa amri yoyote itakayoona inafaa. Historia fupi ya shauri hili ni kuwa Mleta Maombi aliajiriwa na Mjibu Maombi aitwaye Mazava Fabrics Production EA Ltd katika nafasi ya Meneja wa Afya na Usalama wa Mazingira kwa mkataba wa mwaka mmoja. Mkataba huo ulianzia tarehe 17/04/2019 hadi tarehe 16/04/2020. Mnamo tarehe 07/10/2019 ajira ya Mleta Maombi ilisitishwa na mwajiri wake kwa sababu ya utendaji mbovu (Poor Perfomance). Mleta maombi hakuridhika na uamuzi wa Mjibu Maombi hivyo alifikisha mgogoro wake katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (hapa itajulikana kama Tume). Kabla ya usikilizwaji wa shauri la msingi, Mjibu Maombi aliweka pingamizi la awali kuwa Tume haikuwa na mamlaka ya kusikiliza maombi ya Mleta Maombi kwa sababu mgogoro huo uliibuka wakati wa kipindi cha majaribio ya kazi (Probation period). Pingamizi hilo lilikubaliwa na Tume na shauri lilikuwa mbele yake lilifutwa (struck out). Mleta Maombi hakuridhika na uamuzi wa Tume ndipo akafungua shauri hili Mahakamani. 2 Katika shauri hili, pande zote mbili zilikuwa zinawakilishwa ambapo Mleta Maombi anawakilishwa na Bw. Iddi Yassin, Wakili, na Mjibu Maombi anawakilishwa na Prof. Siriacus Binamungu, Wakili. Akifanya mawasilisho ya msingi kuunga mkono maombi haya, wakili wa Mleta Maombi alieleza kwamba Tume ilikosea kuona kuwa haikuwa na Mamlaka ya kusikiliza shauri lililowasilishwa mbele yake kwa kuwa Mleta Maombi alikuwa katika kipindi cha majaribio (probation). Katika shauri hili Mleta Maombi alikuwa na mgogoro na Mjibu Maombi kuhusu kuvunjwa kwa Mkataba wake wa kazi na sio uachishwaji kazi. Hivyo, Tume ilikosea kuona kuwa haikuwa na Mamlaka ya kusikiliza Shauri hilo chini ya Kifungu cha 35 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Sura ya 366, Marekebisho ya 2019. Kwa sababu hiyo anaiomba Mahakama ifute uamuzi wa Tume na kuona kuwa Tume ilikuwa na Mamlaka ya kusikiliza shauri lilokuwa mbele yake. Akijibu mawasilisho ya Mleta Maombi, Wakili wa Mjibu Maombi alieleza kuwa Tuzo ya Tume ipo sahihi kwa mujibu wa Sheria. Alieleza ya kwamba Tume ilifanya uamuzi sahihi katika shauri lililokuwa mbele yake kwa kuwa Mleta Maombi alikuwa ni mwajiriwa na aliachishwa kazi akiwa katika kipindi cha Majaribio (probation) kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yake kama Mkataba wake wa ajira unavyoeleza. Fomu ya Tume Na. 1 inaonesha kuwa malalamiko ya Mleta Maombi mbele ya Tume ni ya 3 kuvunjwa kwa masharti ya Mkataba lakini ukiangalia nafuu alizoomba utaona kuwa anachoomba sio kuvunjwa kwa mkataba ball ni kuwa ameachishwa kazi isivyo halali. Hivyo, Uamuzi wa Tume upo sahihi na unazuia mfanyakazi ambaye yupo katika kipindi cha majaribio kufungua shauri mbele ya Tume kupinga uachishwaji kazi usio halali. Aidha, Wakili wa mjibu aliwasilisha ya kwamba katika ukurasa wa 5 wa uamuzi Msuluhishi aliangalia hoja zilizowasilishwa na pande zote mbili kabla ya kufikia uamuzi. Madai ya Mleta Maombi mbele ya Tume na nafuu anazoomba zinaonesha kuwa madai yake ni ya namna gani. Hii inaonesha kuwa Mleta Maombi alikuwa amefungua shauri la kuvunjwa mkataba lakini akidai nafuu za kuachishwa kazi pasipo halali wakati alikuwa katika kipindi cha majaribio. Nafuu ndio zinatoa picha kuwa Mleta Maombi alikuwa amefungua shauri la kuachishwa kazi kwa kificho. Mleta Maombi hana pingamizi kuwa mfanyakazi aliye katika kipindi cha majaribio haruhusiwi kufungua shauri la kuachishwa kazi pasipo halali. Lakini Fomu Na. 1 ya Tume inaonesha wazi kuwa shauri hili ni la uachishwaji kazi pasipo halali. Mleta Maombi haoneshi ni kwa namna gani mkataba wake ulivunjwa. Hivyo, naomba shauri hili litupiliwe mbali na uamuzi wa Tume uendelee kuwa kama ulivyoamuliwa. Kurudisha tena Shauri husika mbele ya Tume ni wazi bado Tume haitakuwa na Mamlaka ya kusikiliza. 4 Akifanya mawasilisho ya nyongeza (Rejoinder submission), Wakili wa Mjibu Maombi alieleza kuwa mfanyakazi aliye katika kipindi cha majaribio anaweza kuwasilisha mgogoro mbele ya Tume kuhusu uhalali wa kuachishwa kazi. Fomu Na. 1 ya Tume inaonesha alifungua mgogoro wa kuvunjwa kwa mkataba wake ili apate nafuu zake. Kwa sababu hiyo Mleta Maombi hafungwi na katazo la kifungu cha 35 cha Sheria ya Mahusiano Kazini kufungua shauri la kuvunjwa kwa Mkataba wake wa ajira. Hivyo, Muamuzi alikosea kuona kuwa hana mamlaka ya kusikiliza shauri hilo. Hivyo anaomba uamuzi huo ufutwe na shauri lirejeshwe mbele ya Tume ili liweze kusikilizwa kwa ustahilifu. Baada ya kupokea mawasilisho ya pande zote mbili, naona hoja ya kufanyiwa uamuzi ni endapo Tume ilikuwa na mamlaka ya kusikiliza mgogoro uliofunguliwa na Mleta Maombi. Katika shauri hili hakuna ubishani kuwa Mleta Maombi aliachishwa kazi na Mjibu Maombi kwa kushindwa kufanya kazi vizuri wakati akiwa katika kipindi cha majaribio. Mleta Maombi anadai kuwa alifungua shauri la kuvunjwa kwa mkataba wake wa ajira. Ushahidi uliopo katika rekodi unaonesha kuwa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ilikubali pingamizi la Mjibu Maombi kuwa haikuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri la kuachishwa kazi isivyo halali kwa mfanyakazi ambaye bado yupo katika kipindi cha majaribio. Muamuzi katika Ukurasa wa 7 aya ya kwanza ya Uamuzi wa 5 Tume aliona kuwa Mleta Maombi hatakiwi kupinga usitishwaji ajira kwa sababu alikuwa bado yupo katika kipindi cha majaribio cha chini ya miezi 6. Nakubaliana na uamuzi wa Muamuzi kuwa mwajiriwa aliye katika kipindi cha majaribio halindwi na vifungu vinavyohusu uhalali wa kuachishwa kazi kama kifungu cha 35 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Sura ya 366, Iliyorejewa mwaka 2019 inavyoeleza. Katika kesi ya David Nzaligo dhidi ya NMB PLC, Rufaa ya madai Na. 61 ya 2016, Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, Mahakama iliona mwajiriwa aliye katika muda wa majaribio hawezi kunufaika na nafuu zilizopo katika sehemu ya III ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini. Sehemu hiyo ya III ya sheria hiyo inahusu kuachisha kazi isivyo halali. Aidha, kanuni ya 10 (8) ya Kanuni za Ajira na Mahusiano Kazini (Kanuni za Utendaji Bora), T.S. Na. 42 la 2007 inatoa utaratibu wa kuachishwa kazi mwajiriwa ambaye yupo katika kipindi cha majaribio kinachozidi miezi 6. Hivyo, kwa mwajiriwa aliye katika kipindi cha majaribio cha chini ya miezi sita sheria haijaweka utaratibu wa kumwachisha kazi (Angalia kesi ya Jane Chubruma dhidi ya NMB, Marejeo Na. 159 ya 2016, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi). Ushahidi uliopo katika shauri hili unaonesha kuwa Mleta Maombi alikuwa ameajiriwa na Mjibu Maombi kwa mkataba wa muda wa mwaka mmoja kuanzia tarehe 17 Aprili, 2019 hadi tarehe 16 Aprili, 2020. Mkataba 6 huo ulisitishwa tarehe 07 Oktoba, 2019 wakati bado Mleta Maombi yupo katika kipindi cha majaribio. Hii ina maana kuwa Mleta Maombi alifanya kazi kwa muda wa miezi mitano (05) na hivyo kuwa aliachishwa kazi wakati yupo katika kipindi cha majaribio cha chini ya miezi 6. Hivyo, kanuni ya 10 ya T.S. Na. 42 la 2007 haiwezi kumlinda. Kuhusu mawasilisho ya Mleta Maombi kuwa mgogoro aliouwasilisha mbele ya Tume ulihusu kuvunjwa kwa mkataba wake, nimeisoma Fomu Na. 1 ya Tume. Fomu hiyo inaonesha katika sehemu ya 3 kuwa kiini cha mgogoro ni kuvunjwa kwa mkataba. Hata hiyvo, sehemu ya muhtasari wa madai yake Mleta Maombi amejaza kuwa ameachishwa kazi wakati akiwa katika kipindi cha majaribio na uachishwaji kazi huo haukufuata utaratibu wa kisheria. Maelezo hayo ya madai yake yanaonesha kuwa mgogoro huo ulihusu kuachishwa kazi. Hivyo, nakubaliana na uamuzi wa Tume kuwa haikuwa na mamlaka ya kusikiliza mgogoro huo uliowasilishwa na Mleta Maombi. Kwa sababu hiyo, Mahakama hii inatupilia mbali (dismiss) maombi haya ya marejeo na Uamuzi Mdogo wa Tume unabakia kama ulivyo. Kila upande utabeba gharama zakq za shauri hili. v Q A*. E. MWIPOPO JAJI 03/06/2021 7