romanus j chumi na mwenzake dhidi ya scania tanzania ltd 2022 tzhcld 702 14 julai 2022
The dispute was filed within the prescribed 60-day period from the date the applicants were notified of the refusal to pay their entitlements (16 July 2019), thus the Commission erred in dismissing the claim as time-barred. The arbitrator further erred by proceeding to determine the merits after finding the dispute...
Source-derived case information.
- Citation
- romanus j chumi na mwenzake dhidi ya scania tanzania ltd 2022 tzhcld 702 14 julai 2022
- Parties
- Applicant: Romanus J. Chumi; Applicant: Peter Abduel; Respondent: Scania Tanzania Ltd
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2022
- Procedural Posture
- Labour Revision / Judgment on Application for Revision
- Outcome
- application allowed
- Legal Topics
- Limitation Period, Employee Benefits, Retirement Entitlements, Jurisdiction of Labour Commission
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Romanus J. Chumi
Applicant
Peter Abduel
Applicant
Scania Tanzania Ltd
Respondent
Procedural Posture
Labour Revision / Judgment on Application for Revision
Legal Issues
- 1 Whether the dispute was filed within the prescribed limitation period
- 2 Whether the arbitrator was correct to decide on the merits after finding the dispute out of time
Ratio Decidendi
The dispute was filed within the prescribed 60-day period from the date the applicants were notified of the refusal to pay their entitlements (16 July 2019), thus the Commission erred in dismissing the claim as time-barred. The arbitrator further erred by proceeding to determine the merits after finding the dispute out of time.
Court Disposition
application allowed
Orders
- Decision of the Commission in CMA/DSM/ILA/665/19/303 is set aside
- Matter remitted to the Commission for fresh hearing and determination on the merits
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA DIVISHENI YA KAZI ILIYOKETI DAR ES SALAAM MAOMBI YA MAREJEO NA. 36 YA 2021 (Kutokana na uamuzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ya DSM iiiyoketi Ilala Tarehe 14 Disemba 2019 katika Mgogoro wa Kazi Na. CMA/DSM/ILA/665/19/303) BAINA YA ROMANUS J. CHUMI....................... .MLET'A MAOMBI - 1 PETER ABDUEL .............................. .......MLETA MAOMBI - 2 NA SCANIA TANZANIA LTD................. ...MJIBU MAOMBI HUKUMU 14/06/2022 & 14/07/2022 K, T- R, MTEULE, 3, Maombi haya yamefunguliwa kuomba marejeo ya Uamuzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi katika Mgogoro wa Kazi Na. CMA/DSM/ILA/665/19/303. BWANA ROMANUS J. CHUMI NA PETER ABDUEL ambao ni waleta maombi wanaomba Mahakama itoe amri zifuatazo:- i. Kwamba Mahakama iitishe na kurekebisha tuzo ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi iliyotolewa tarehe 14 Disemba, 2020 na Mhe. Wilbard G.M. Mwamuzi, katika Mgogoro wa Kazi Na. CMA/DSM/ILA/665/19/303. ii. Na nafuu nyingine yoyote Mahakama itaona kuwa inafaa na ya haki (just). i in. Gharama yoyote Mahakama itaona inafaa kutolewa katika shauri hili. Maombi haya yameungwa mkono na viapo vya waleta maombi ambavyo katika aya ya 7 ya viapo hivyo, kuna hoja tatu za kisheria (legal issues). Ya kwanza inahoji usahihi wa kisheria wa uamuzi wa Tume ulioamua kwamba mgogoro ulikuwa nje ya muda na ya pili imehoji usahihi wa msuluhishi kuamua kwamba waleta. maombi hawastahili kulipwa stahiki za usafiri na fedha za kujikimiK wakati wakisubiri stahiki za usafiri. Historia fupi ya shauri hili ni kwamba waleta’ maombi waliajiriwa na Mjibu Maombi kwa nafasi tofauti na nyakati tofauti. Inadaiwa na waleta maombi kwamba waliomba kustaafu kutokana na umri wao, ambapo Mleta Maombi namba 1 alikubaliwa kustaafu tarehe 01 Januari 2018 na mwenzake alikubaliwa tarehe 28 Februari 2018. Baada ya hapo, ulifuatia mgogoro wa madai ya kuwasafirisha waleta maombi kuwarejesha walikotoka wakati wanaajiriwa na gharama za kujikimu kwa kipindi chote walichokuwa wakisubili stahiki za usafiri. Inadaiwa. na .Waleta Maombi ya kwamba Mjibu Maombi alishindwa kutekeleza makubaliano ya hiari, jambo lililosababisha kufunguliwa kwa mgogoro huu mbele ya Tume. Hata hivyo Tume iiitupilia mbali madai ya Waleta Maombi kwa kigezo kwamba yalifunguliwa nje ya muda. Kutokana na kutokuridhika na uamuzi wa Tume, waleta maombi waliamua kufungua maombi haya ya Marejeo. Pamoja na maombi ya faragha, Waleta Maombi waliambatanisha viapo vyao, ambavyo vinaeleza mtiririko mzima wa mgogoro hadi kuwepo kwa maombi haya. Katika viapo vyao Waleta Maombi 2 wanadai kwamba tangu walipostaafu ajira zao hawakulipwa stahiki za usafiri na za kujikimu. Waleta maombi wanadai pia kwamba mgogoro waoTume ulifunguliwa ndani ya muda lakini ulitupwa kimakosa. Maombi haya yalipingwa na Mjibu Maombi kupitia kiapo kinzani kilichoapwa na Cornelius Kasiya Kariwa, Wakili wa Mjibu Maombi. Shauri hili lilisikilizwa kwa njia ya maandishi ambapo, Walesa Maombi waliwakilishwa na Bw. Hemedi Omary, Muwakilishi Binafsi/na/Mjibu Maombi aliwakilishwa na Bw. Frank Kilian, Wakili. Mahakama hii inapokea mawasilisho yote yaliyofanywa na w^daawa na itayazingatia katika kuandaa uamuzi wake. x-, Baada ya kuzingatia mawasilisho ya pande zote mbili Mahakama inaona kuna hoja mbili (2) zinazbbishaniwa ambazo zinatakiwa zitolewe uamuzi. Hoja hizo ni kama zifuatavyo:- i) Je Waleta Maombi wana hoja ya msingi itakayoifanya Mahakama hii ifanye marejeo na kutengua uamuzi uliotolewa ha Tume katika Mgogoro wa Kikazi Na. CMA/DSM/ILA/665/19/303? ii) Nini hafuu za kila upande? Katika'.kujibu hoja ya kwanza, Mahakama itazingatia hoja zilizoibuliwa na Waleta Maombi katika viapo vyao, zikiwepo hoja kama mgogoro ulifunguliwa Tume nje ya muda, na kama Muamuzi alikuwa sahihi kwa kuamua ya kwamba wadaawa hawastahili stahiki za usafiri na fedha za kujikimu. Nikianza na hoja ya mgogoro kufunguliwa nje ya muda, Bw. Hemedi alieleza ya kwamba jukumu la kutunza kumbukumbu za mwajiriwa ni 3 la mwajiri na hii ni kwa mujibu wa Kifungu cha 15 Cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Sura ya 366 Marek. 2019. Aliongeza kuwa baada ya kustaafu, waleta maombi walipewa barua zilizoainisha stahili zao zikiwemo nauli na malipo ya kusafirishia mizigo kwa ajili yao na familia zao. Barua hizo zilipokelewa Tume kama Exhibit S2. Bw. Hemedi aliendelea kueleza kuwa baada ya kusubiri muda mrefu na kuona malipo ya kusafirishwa hayalipwi, waliamua kuandika barua ya kuhoji, na kujibiwa tarehe 16/7/2019 kwa kukataliwa stahiki hizo. Ni maoni ya Bw. Hemedi kwamba mgogoro uliibuka tarehe ambayo Mjibu Maombi alikataa kulipa stahiki za Waleta Maombi. Kwa maoni yake, kwa kuwa mgogoro wa Waleta Maombi hi wa kimaslahi hivyo ulitakiwa ufunguliwe kwa kufuata Kanuni ya 10 (2) ya Sheria za Taasisi ya Kazi, T.S. Na. 64 la 2007 ambayo inaeleza kuwa muda utahesabiwa kuanzia tarehe ambayo mgogoro umeibuka ambayo ni tarehe 16/7/2019. Mjibu maombi ana hoja kwamba waleta maombi hawajazingatia Kanuni ya muda kwani muda unatakiwa kuhesabiwa kuanzia tarehe ambayo waleta maombi walistaafu. Kwa maoni yake, kwa vile Mleta Maombi namba 1 alistaafu kazi rasmi tarehe 01 Januari 2018 na mwenzake 28 Februali 2019 na mgogoro kuwasilishwa Tume tarehe 26 Agosti 2019, haiwezekani mgogoro huo ukawa ndani ya muda wa siku 60 zilizotolewa na kanuni. Kwa msingi huu Wakili wa Mjibu Maombi alikuwa na mtizamo kwamba hoja ya Waleta Maombi kuwa mgogoro uliibuka tarehe 16 Julai 2019 pale walipojibiwa barua ya kukumbushia malipo ya stahiki zao inakosa mashiko. 4 Katika kuhesabu muda katika shauri hili, mwongozo muafaka ni Kanuni ya 10 (2) ya Sheria ya Taasisi za Kazi, T.S. Na. 64 la 2007 ambayo inaeleza ya kwamba:- "K.10 (2) Migogoro mingine yote iwasillshwe kwenye Tume ndani ya siku sitin/ kuanzia tarehe ya kuanza mgogoro" Kinachoonekana kutofautisha hoja za wadaawa nLtarelie ambayo siku zinatakiwa kuanza kuhesabiwa. Ni muhimu ijulikane tofauti iliyopo kati ya Kanuni ya 10 (1) na Kanuni ya 10 (2) ya “RS. No. 64 la 2007. Nanukuu kanuni ya 10 (1) inyosema:- "10. (1) Disputes about the fairnessof an employee’s termination of employment must be referred to the Commission within thirty days from the date of termination or the date that the employer made a final decision to terminate or uphold the decision to terminate." Ni Dhahiri kwamba Kanuni ya 10 (1) inahusika na mgogoro unaotokana na uhalali wa kusitisha ajira wakati Kanuni ya 10 (2) inazungumzia ukomo wa muda kwa migogoro mingineyo isiyohusiana na uhalali wa kusitisha ajira. Ni wazi kwamba kwa mujibu wa Kanuni ya 10 kuwa muda wa kufungua mgogoro unaohusiana na madai ya stahiki za usafiri hayahusiani na uhalali wa usitishwaji wa ajira, hivyo huangukia Kanuni ya 10 (2) na ni lazima yafanyike ndani ya siku (60) sitini tangia mgogoro huo uanze. Muda unaanza kuhesabiwa kuanzia tarehe ambayo mgogoro umeibuka. Na mgogoro huibuka siku ambayo imejulikana kwa wadaawa kuwa kuna kutokuelewana. 5 (Angalia kesi ya Mohamed Kigesu Mahegu vs. Laurence Asseli Nsanya (Appeal 53 of 2021) [2022] TZHCL and D 58). Tofauti hii ya kisheria ni ya muhimu kwani uachishwaji wa kazi uko wazi na unajulikana kwa pande zote mara tu unapotokea. Lakini yapo madai mengine ambayo mtu hawezi kuyajua mpaka kutokee kutokuelewana mfano madai ya sasa kuhusu usafirishaji wa waleta maombi. Hakuna namna ambayo wangejua kuwa kuriWngogoro kama mjibu maombi asingekuwa amewajulisha kuwa hatalipa<6 Hoja ya wakili wa mjibu maombi kwamba muda unataka uhesabiwe kuanzia tarehe ya kustaafu kwa waleta maombi. ingekuwa na mashiko kama kungekuwa na mgogoro kuhusu usitishaji wa ajira zao. Katika shauri lililokuwepo Tume, hakukuwa na mgogoro wa usitishwaji wa ajira. Pia mwajiri alishawaambia waleta maombi kupitia barua kwamba watalipwa stahili za usafiri baada ya kustaafu. Hivyo ilijuikana kuwa kuna mgogoro siku ambayo waleta maombi walipewa barua ya kukataliwa kulipwa stahiki zao kama walivyokuwa wameahidiwa hapo awali. Siku hii ni tarehe 16 na 18 Julai 2019. Hapa ndipo mgogoro unatakiwa uanze kuhesabiwa. Kuanzia tarehe hii 16 Julai 2019, siku 60 zingeisha tarehe 10/9/2019. Mgogoro tume uliwasilishwa tarehe 22/8/2019. Ni wazi kuwa mgogoro ulifunguliwa ndani ya muda. Hivyo hoja ya kwanza inapata majibu hasi kwamba mgogoro Tume haukuwa umepitwa na muda. Hoja inayofuata ni kama muamuzi alikuwa sahihi kuamua kuwa waleta maombi hawakustahili stahiki za kusafirishwa. Hapa naona kuna utaratibu haujakaa sawa. Baada ya msuluhishi kuona kuwa hakuna mgogoro ulikuwa nje ya muda, alipaswa kuutupilia mbali 6 kwani mgogoro uliochelewa unaondoa mamlaka ya Tume kuendelea kusikiliza. Tofauti na hili, muamuzi aliendelea kuamua kuhusu stahili za wadaawa. Katika kesi ya Tanzania Fish Processors Ltd. v. Christopher Luhangula, Madai ya Rufaa No. 161 of 1994, katika Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, iliyoketi Mwanza, ilijadiliwa kama ninavyonukuu:- "The question of Limitation of time is fundamental jssue involving jurisdiction ...it goes to the very root of deaiing with civil claims, limitation is a materia! point in the speedy administration ofjustice. Limitation is there to ensure that a party does not come to Court as and when he chooses..." Ni msimamo wa kisheria ya kwamba nafuu ya shauri linalofunguliwa nje ya muda ni kutupiliwa mbali kama ilivyojadiliwa katika kesi ya Anna Haule v. Salum Ally, Maombi ya Anuai Na. 250 ya 2004, Mahakama Kuu ya Tanzania, iliyoketi Dar es Salaam, (Haijaripotiwa). Katika kesi. hii, iliamuliwa kwamba nafuu ni rufaa kutupiliwa mbali kwa kuwa ilifunguliwa nje ya muda na pasipokuwepo na kibali cha Mahakama kufungua shauri nje ya muda. Kutokana na msimamo wa kesi tajwa ni matakwa ya kisheria kwamba shauri lililopitwa na muda linainyima Mahakama mamlaka ya kuendelea na utatuzi wa mgogoro wa msingi. Kitendo cha muamuzi kuendelea kushughulika na haki za msingi za wadaawa katika shauri alilokwisha kuliona kuwa liko nje ya muda, ni utaratibu usiokuwa 7 sahihi. Kwa hiyo, hoja ya pili nayo inajibiwa kuwa muamuzi hakuwa sahihi kuamua kuhusu stahili za waleta maombi. Baada ya kuona kwamba mgogoro uliwasilishwa Tume ndani ya muda, na kwamba tume haikuwa sahihi kusikiliza shauri la msingi baada ya kuona kuwa mgogoro ulifunguliwa nje ya muda, hii inatosha kujibu hoja ya kwanza ya maombi haya kwamba Waleta Maombi wana hoja ya msingi ya kuishawishi Mahakama hii.. kufanya marejeo na kutengua uamuzi wa Tume ya Usuluhishi katika Mgogoro wa Kikazi Na. CMA/DSM/ILA/665/19/303. Baada ya jibu la hapo juu, kinachofuata ni -hbja ya pili kuhusu nafuu wanazostahili wadaawa katika maombi haya. Nafuu pekee kuruhusu maombi haya na shauri kusikilizwa upya. Katika mazingira haya naruhusu maombi haya ya Marejeo. Natengua uamuzi wa Tum^, .katika Mgogoro wa Kikazi Na. CMA/DSM/ILA/665/19/303, Natamka kuwa mgogoro haukuwa nje ya muda. Narudisha jalada Tume mgogoro huu ukasikilizwe upya na kuamuliwa kuhusu madai ya msingi. Imetolewa leo Dar es Salaam tarehe 14th Julai, 2022. KATARINA REVOCATI MTEULE 14/07/2022 8