MAOMBI YA MAREJEO NA
Applicants failed to provide evidence of non-payment of salaries or any documentation supporting their claims of constructive dismissal; thus, the decision of the Commission for Mediation and Arbitration to dismiss their claims is upheld.
Source-derived case information.
- Citation
- MAOMBI YA MAREJEO NA
- Parties
- Applicant: Salim Abdallah Shiza; Applicant: Mohamedi Rashid Ally; Applicant: Raphael Lugendo Mkomwa; Applicant: Iddi Salehe Saboto; Applicant: Meshack Michael Sanga; Applicant: Stamili Ayubu Bakari; Applicant: Mikidadi Abuu Mikidadi; Applicant: Essau Boniface Sanga; Applicant: Antony Joseph Makarious; Applicant: Joseph Dausen Ndashau; Applicant: Nassoro Omary Salum; Applicant: Mohamed Jumanne Temba; Applicant: Hajj Omary Salum; Applicant: Athumani Ayubu Said; Applicant: Abdallah Amiri Sheshuda; Applicant: Salehe Hassani Feruzi; Applicant: Shabani Mohamed Ihaji; Respondent: Panone Company Limited
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2024
- Procedural Posture
- Labour Revision / Judgment
- Outcome
- Application dismissed
- Legal Topics
- Constructive Dismissal, Burden of Proof, Non Payment of Salary
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Salim Abdallah Shiza
Applicant
Mohamedi Rashid Ally
Applicant
Raphael Lugendo Mkomwa
Applicant
Iddi Salehe Saboto
Applicant
Meshack Michael Sanga
Applicant
Stamili Ayubu Bakari
Applicant
Mikidadi Abuu Mikidadi
Applicant
Essau Boniface Sanga
Applicant
Antony Joseph Makarious
Applicant
Joseph Dausen Ndashau
Applicant
Nassoro Omary Salum
Applicant
Mohamed Jumanne Temba
Applicant
Hajj Omary Salum
Applicant
Athumani Ayubu Said
Applicant
Abdallah Amiri Sheshuda
Applicant
Salehe Hassani Feruzi
Applicant
Shabani Mohamed Ihaji
Applicant
Panone Company Limited
Respondent
Procedural Posture
Labour Revision / Judgment
Legal Issues
- 1 Whether the applicants were subjected to intolerable working conditions amounting to constructive dismissal
- 2 Whether the applicants proved non-payment of salaries justifying constructive dismissal
Ratio Decidendi
Applicants failed to provide evidence of non-payment of salaries or any documentation supporting their claims of constructive dismissal; thus, the decision of the Commission for Mediation and Arbitration to dismiss their claims is upheld.
Court Disposition
Application dismissed
Orders
- The application is dismissed for lack of merit.
- The decision of the Commission for Mediation and Arbitration is upheld.
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
KATIKA MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DIVISHENI YA KAZI DAR ES SALAAM MAOMBI YA MAREJEO NA. 12793 YA MWAKA 2024 SALIM ABDALLAH SH IZA ..........................MLETA MAOMBI WA 1 MOHAMEDI RASHID A L L Y ........................MLETA MAOMBI WA 2 RAPHAEL LUGENDO M KO M W A................ MLETA MAOMBI WA 3 IDDI SALEHE SABO TO ..............................MLETA MAOMBI WA 4 MESHACK MICHAEL S A N G A .....................MLETA MAOMBI WA 5 STAMILI AYUBU BAKARI......................... MLETA MAOMBI WA 6 MIKIDADI ABUU M IKIDADI.................... MLETA MAOMBI WA 7 ESSAU BONIFACE S A N G A .........................MLETA MAOMBI WA 8 ANTONY JOSEPH MAKARIOUS................ MLETA MAOMBI WA 9 JOSEPH DAUSEN N DASHAU.................. MLETA MAOMBI WA 10 NASSORO OMARY S A LU M ..................... MLETA MAOMBI WA 11 MOHAMED JUMANNE T E M B A ................MLETA MAOMBI WA 12 HAJJ OMARY SA LU M ................. ........... MLETA MAOMBI WA 13 ATHUMANI AYUBU S A ID ....................... MLETA MAOMBI WA 14 ABDALLAH AMIRI SHESHUDA............... MLETA MAOMBI WA 15 SALEHE HASSANI FER U ZI..................... MLETA MAOMBI WA 16 SHABANI MOHAMED I H A JI.................. MLETA MAOMBI WA 17 DHIDI YA PANONE COMPANY LIM ITED............................. MJIBU MAOMBI HUKUMU Tarehe ya Amri ya Mwisho: 12/ 07/2024 Tarehe ya Hukumu: 23/ 08/2024 MLYAMBINA, J. Mbele ya Mahakama hii Waleta Maombi wanapinga maamuzi ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (itajulikana kama Tume) Dar es Salaam yaliyotolewa katika Mgogoro wa Kazi Na. CMA/DSM/ILA/113/22/103/2022. Katika shauri hilo, Waleta Maombi waliwasilisha mgogoro mbele ya Tume wakidai kuwa Mwajiri (Mjibu Maombi) amewawekea mazingira magumu yaliyowapelekea kuacha kazi (constructive termination). Baada ya Tume kupitia ushahidi wa pande zote mbili iliona ya kuwa Waleta Maombi walishindwa kuthibitisha madai yao. Hivyo basi, yalitupiliwa mbali. Baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya Tume Waleta Maombi wamefika tena mbele ya Mahakama hii wakljikita katika hoja zifuatazo: i. Kwamba, mheshmiwa Mwamuzi alikosea kisheria na kiuhalisia kuufuta mgogoro huu wakati Waleta Maombi walikuwa na uthibitisho wa kutolipwa mishahara kwa muda mrefu na Mjibu Maombi. ii. Kwamba, Mheshmiwa Mwamuzi alikosea kisheria na kiuhalisia kuufuta mgogoro huu wakati Tume imethibitisha vigezo vya (constructive termination) ambavyo ni pamoja na mazingira magumu (intolerable situation). iii. Kwamba, Mheshmiwa Mwamuzi alishindwa kutumia Kanuni ya 7(3) ya Sheria ya Ajira na mahusiano kazini (Code o f good Practice) TS. 42/2007 badala yake akajielekeza kwenye Kanuni ya 7(2) ya Kanuni tajwa na kuufuta mgogoro huu. iv. Kwamba, Mheshmiwa Mwamuzi alikosea kisheria na kiuhalisia kwa kushikilia kwamba kusababishiwa mazingira magumu ya kuacha kazi haikuwa sahihi isipokuwa kujiuzulu. Mahakama baada ya kupitia mawasilisho ya pande zote mbili inaona kuwa ina hoja kuu mbili za msingl za kutatua; endapo waieta maombi waiiwekewa mazingira magumu ya kupeiekea kuacha kazi na nini stahiki za pande zote mbiii. Tukianza na hoja ya kwanza, Waieta Maombi wanadai kuwa Mjibu Maombi alikuwa hawalipi mishahara yao hivyo ikawalazimu waache kazi. Ni kweli kuwa, kutomlipa Mfanyakazi mshahara ambao ndio tegemeo la kipato chake ni kumuwekea mazingira magumu yanayoweza kupeiekea kuacha kazi. Haya yameamriwa pia katika kesi ya Peter Rwegasira v. Northern Engineering Works Ltd, Revision Application No. 403 of 2022 uk. 13 ambapo iliamriwa ifuatavyo: withholding someone's payment which is important for his survival create intolerable condition of work. Ni msimamo uliowekwa kisheria kupitia maamuzi mbalimbali kuwa ni jukumu la Mwajiriwa kuthibitisha mazingira magumu aliyowekewa na kupeiekea kuacha kazi. Haya yameelezwa wazi katika kesi ya Kobil Tanzania Limited v. Fabrice Ezaovi, Civil Appeal No. 134 of 2017. Katika kesi hiyo, ambayo ilitumiwa na Muamuzi, imeainisha vigezo mbalimbali vywa kuzingatia kupima kama mwajiriwa aliwekewa mazingira magumu ya kupeiekea kuacha kazi. Vigezo hivyo vinanukuliwa kama ifuatavyo; .... there are three requirements for constructive dismissal to be established: i. That the Employee must have terminated the contract of employment. ii. The reason for termination of contract must be that continued employment has become intolerable for the employee. iii. It must have been the employee's employer who had made continued employment intolerable. Katika shauri hili, Waieta Maombi wamedai tu kuwa hawakulipwa mishahara yao. Lakini katika ushahidi wao hakuna kielelezo chochote cha kuthibitisha hilo. Wameeleza kuwa walikuwa wakilipwa mishahara kwa kutumia njia ya benki lakini hata hati za kibenki hazijawasilishwa mbele ya Tume kuthibitisha madai husika. Vilevile, katika kesi ya aina hii Mwajiri anatakiwa kuthibitisha kuwa hakukuwa na namna ya kutatua tatizo zaidi ya kuacha kazi. Kumbukumbu zinaonesha kuwa hata uthibitisho tu wa madai ya mishahara daiwa hakuna. Kwamba, Waleta Maombi wamewahi kudai mishahara yao kwa Mjibu Maombi bila ya mafanikio yoyote mpaka kupelekea wao kuachishwa kazi. Pia, hata katika kuacha kwao kazi, haieleweki ni lini wameacha na hata hakuna barua ya kuacha kazi inayoeleza wazi kuwa wameacha baada ya kutolipwa mishahara yao. Kwa mazingira hayo, Mahakama inaunga mkono maamuzi ya Tume kuwa Waleta Maombi walishindwa kuthibitisha madai yao. Hivyo basi, Mahakama inaendelea kushikilia maamuzi ya Tume kwakuwa hakuna sababu zozote za msingi za kubatilisha maamuzi hayo. Mgogoro huu unatupiliwa mbali kwa kukosa mantiki. Imeamriwa hivyo. JAJI 23/08/2024 Uamuzi huu umesomwa leo tarehe 23/08/2024 mbele ya Jimmy Mnkeni, Mwakilishi Binafsi kwa niaba ya Waieta Maombi na Wakili Engelbert Boniface na Nasri Juma (Meneja Rasilimaliwatu) kwa niaba ya Wajibu Maombi.