selemani athumani salehe and 7 others vs joiven investment t limited na mwenzake 2021 tzhcld 330 30 julai 2021
The applicants admitted their application before the Registrar was defective and failed to comply with mandatory procedural requirements. The proper legal avenues for challenging the Registrar's decision were not followed. The court will not entertain applications that are procedurally defective or fail to comply...
Source-derived case information.
- Citation
- selemani athumani salehe and 7 others vs joiven investment t limited na mwenzake 2021 tzhcld 330 30 julai 2021
- Parties
- Applicant: Selemani Athumani Salehe & 7 Others; Respondent: Joiven Investment (T) Limited; Respondent: Al-Hatimy Developers
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2021
- Procedural Posture
- Labour Revision Application / Judgment on Application to Set Aside Deputy Registrar's Decision
- Outcome
- Application dismissed
- Legal Topics
- Setting Aside Registrar's Decision, Application for Restoration of Struck Out Matter, Procedural Compliance, Right to Be Heard
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Selemani Athumani Salehe & 7 Others
Applicant
Joiven Investment (T) Limited
Respondent
Al-Hatimy Developers
Respondent
Procedural Posture
Labour Revision Application / Judgment on Application to Set Aside Deputy Registrar's Decision
Legal Issues
- 1 Whether the applicants provided sufficient grounds to set aside the Deputy Registrar's decision in Miscellaneous Application No. 636 of 2018
- 2 Whether the application for restoration was properly before the court
- 3 Whether procedural requirements regarding representation and affidavits were met
Ratio Decidendi
The applicants admitted their application before the Registrar was defective and failed to comply with mandatory procedural requirements. The proper legal avenues for challenging the Registrar's decision were not followed. The court will not entertain applications that are procedurally defective or fail to comply with statutory requirements. Therefore, there were no sufficient grounds to set aside the Registrar's decision.
Court Disposition
Application dismissed
Orders
- The decision of the Deputy Registrar in Miscellaneous Application No. 636 of 2018 is upheld.
- The application for revision is dismissed.
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
MAHAKAMA KUU YA TANZANIA DIVISHENI YA KAZI PAR ES SALAAM MAOMBI YA MAREJEO NA. 813 YA 2019 KATI YA SELEMANI ATHUMANI SALEHE & 7 OTHERS............... WALETA MAOMBI DHIDIYA JOIVEN INVESTMENT (T) LIMITED........................... MJIBU MAOMBI WA 1 AL-HATIMY DEVELOPERS .......................................... MJIBU MAOMBI WA 2 MAAMUZI Tarehe ya amri ya mwisho: 26/05/2021 Tarehe ya maamuzi: 30/07/2021 T. Mweneqoha, J. Katika shauri hili muombaji alifungua maombi ya kuiomba mahakama itengue maamuzi ya Naibu Msajili (Deputy Registrar) katika maombi ya kukazia hukumu (execution no 436 of 2017) na maombi ya anuwai (Miscellaneous application no 636 of 2018). Wajibu maombi walipinga vikali maombi hayo kwa kuleta pingamizi tatu ikiwemo, kwamba waombaji wameunganisha maombi ya kesi mbili tofauti kimakosa. Mnamo tarehe 16/04/2021 mahakama ilitolea maamuzi kuwa ni kweli mashauri hayo yaliunganishwa kimakosa hivyo maombi dhidi ya execution namba 436 ya 2017 yaliondolewa kwenye kumbukumbu za i mahakama hii. Hivyo basi maamuzi haya ni dhidi ya maamuzi katika maombi ya anuwai (Miscellaneous Application No. 636 of 2018). Mawasilisho ya maombi hayo yalifanyika kwa mdomo. Waombaji waliwakilishwa na Bw. Hemedi Omari, Muwakilishi binafsi ilihali wajibu maombi waliwakilishwa na Bw. Peter Nyange, Wakili. Katika mawasilisho yake mwakilishi wa waleta maombi alieleza kuwa, waleta maombi wanapinga uamuzi wa Mh. Simfukwe wa tarehe 22/09/2019 unaotokana na pingamizi za awali zilizowasilishwa na wajibu maombi. Alieleza kuwa kulingana na pingamizi la kwanza kwamba kulikuwa na mapungufu ya vifungu vya sheria si kweli kwani kwa kumbukumbu za waleta maombi, maombi hayo yaliletwa chini ya vifungu sahihi. Ilielezwa kuwa wajibu maombi katika shauri hilo walipinga ukomo wa muda, alisema kuwa sheria za mahakama hii zipo kimya kulingana na sheria ya ukomo wa muda. Alirejea Sheria ya Ukomo wa muda, Sura 89 KM 2002 kifungu cha 21 kinazungumza kuwa maombi yoyote ambayo hayakutajwa ukomo wake, mwombaji anayo haki ya kuleta kwenye mahakama ndani ya siku 60. Kwamba waleta maombi walileta maombi yao ndani ya muda. 2 Kwamba, kulikuwa na pingamizi kuwa kiapo cha waleta maombi hakikueleza chanzo cha taarifa. Ilielezwa kuwa, pingamizi hilo si la kweli kwakuwa ni kweli siku iliyotajwa katika kiapo hicho hawakuwahi kuitwa wala kupanga na mahakama kuwa shauri hilo litaitwa kwa msajili. Hivyo waliomba mahakama iitishe jalada hilo na kuangalia uhalisia wake na kuweza kufuta maamuzi ya msajili katika maombi hayo. Iliendela kuelezwa kuwa maombi yao pia yalifutwa na msajili kwa kutokuwa na taarifa ya uwakilishi. Mwakilishi huyo alisema, taarifa hiyo ilikuwepo kwa mujibu wa kanuni ya 43 (1) ya Kanuni za Mahakama ya Kazi, Tangazo la Serikali Na. 106 la 2007 (zitatambulika kama Kanuni za Mahakama ya Kazi). Kwamba taarifa hiyo iliwasilishwa kabla ya kusikiliza maombi hayo tarehe 22/08/2018 na tarehe 29/09/209. Ilisisitizwa kuwa maombi yaliyowasilishwa mbele ya msajili yalikuwa ni ya kufufua shauri ambayo yaliwasilishwa kwa mujibu wa kanuni ya 24 (1), 24 (2) (a) (b) (c) (d) (e) (f), 24 (3) (a) (b) (c) (d), 35 (1) (2) (3) na kanuni ya 36 (1) (2) (3) za Kanuni za Mahakama ya Kazi ambazo zinaipa mamlaka mahakama hii kufufua mgogoro uliofutwa. Iliendelea kuelezwa kuwa, Kanuni hizo zinasomwa pamoja na kifungu cha 94 (1) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, [Sura 366 KM 2019] (itatambulika kama Sheria ya ajira na mahusiano kazini), ilisisitizwa 3 kuwa kwakuwa vifungu hivyo vipo ni dhahiri kuwa maombi hayo yaliletwa chini ya vifungu sahihi. Aliomba mahakama ifute pingamizi hilo na kuruhusu maombi ya waleta maombi yasikilizwe kama ambavyo haki hiyo inapatikana katika ibara ya 13 (6) ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977. Mwakilishi wa wajibu maombi pia aliiomba mahakama isizingatie kiapo kinzani cha wajibu maombi katika maombi haya kwakuwa kimekiuka masharti ya kanuni ya 24 (2) ya kanuni za Mahakama ya Kazi. Alidai kuwa kiapo hicho kiliapwa na wakili wa wajibu maombi na sio wajibu maombi wenyewe. Hivyo basi kutokana na sababu zote hizo hapo juu aliiomba mahakama ikubali maombi haya. Akijibu hoja za wajibu maombi Bw. Peter Nyange aliieleza mahakama kuwa pingamizi la kwanza na la pili katika maombi namba 636 ya 2018 zilifutwa hivyo haoni haja ya kuzizungumzia tena. Kuhusu suala la uwakilishi alieleza kuwa ni kweli wakati wanafungua maombi yao waleta maombi hawakukuwa na taarifa ya uwakilishi kwamba, kuleta taarifa hiyo baadae bila ruhusa ya mahakama ilikuwa sio sahihi. Hivyo aliomba hoja hiyo itupiliwe mbali. 4 Katika hoja ya kuwa maombi yalikuwa na mapungufu alieleza kuwa, tukirejea katika maamuzi bishaniwa Msajili alisema wazi kuwa ambaye hakuridhika na maamuzi katika (execution) namba 436 ya 2017 alikuwa na uwezo wa kupinga maamuzi hayo kwa njia ya mapitio (reference) au marejeo (revision) na sio kufanya maombi ya kurejesha shauri hilo. Ilielezwa kuwa hoja hiyo ilisisitizwa pia katika kesi ya Blueberry Tanzania Services Ltd vs. Evarist Sesa, Lab. Div. DSM. Misc. Appl. No. 47 of 2010, (unreported) kama ilivyonukuliwa katika ukurasa wa 2 wa maamuzi bishaniwa. Ilielezwa kuwa waleta maombi walipewa haki ya kusikilizwa hivyo sababu zao walizozitoa mbele ya mahakama hii hazina mashiko. Katika hoja ya chanzo cha taarifa wakili wa wajibu maombi alieleza kuwa mwakilishi wa wajibu maombi ameshindwa kueleza vizuri hoja hiyo. Alisema hawakumaanisha kuwa walishindwa kufika ila walitakiwa waseme kilichopo kwenye aya husika katika kiapo chao ni taarifa wanazozijua wao au kwamba ni taarifa waliyoitoa mahali fulani kama inavyoelekeza katika Order 19 Rule (3) (1) ya Civil Procedure Code, Cap 33 RE 2019 pamoja na kesi ya Augustine Lyatonga Mrema vs. AG and others [1999] TLR 273 kama iliyonikuliwa katika maamuzi bishaniwa. 5 Kuhusu pingamizi aliloliibua mwakilishi wa waleta maombi kuhusiana na kiapo kinzani cha wajibu maombi ilielezwa kuwa, kifungu walichorejea cha 24 (2) cha Kanuni za Mahakama ya Kazi hakihusiani na kiapo kinzani bali ni taarifa ya maombi (Notice of application) ambayo huletwa na waleta maombi na sio wao wajibu maombi. Aliongeza kuwa lakini hoja hiyo ni mpya mbele ya mahakama hii ambayo haikuibuliwa katika maamuzi bishaniwa. Hivyo kutokana na hoja hizo aliiomba mahakama kutupilia mbali maombi haya. Katika mawasilisho ya nyongeza mwakilishi wa waleta maombi alieleza kuwa, wawakilishi wa wadaawa sio waleta maombi mbele ya mahakama hivyo wadaawa wanaweza kujiwakilisha wenyewe au watakavyoona inawapendeza. Ilielezwa kuwa wakili wa mjibu maombi amerejea Civil Procedure Code, Cap 33 RE 2019 lakini sheria hiyo hutumika tu pale sheria za kazi zinapokuwa kimya. Kuhusu kiapo kinzani ilisisitizwa kuwa kina mapungufu ya kutofuata matakwa ya sheria. Hivyo basi aliiomba mahakama ifutilie mbali mapingamizi yote yaliyowasilishwa na wajibu maombi na kuamuru maombi ya waleta maombi yakasikilizwe ili haki iweze kutendeka. Baada ya kupitia mawasilisho ya pande zote mbili, Mahakama imeachiwa hoja kuwa, endapo waleta maombi wameeleza sababu za 6 msingi za kuweza kutengua maamuzi ya Msajili katika maombi ya anuwai no. 636 ya 2018. Kumbukumbu zinaonesha kuwa katika maamuzi yanayobishaniwa wajibu maombi waliibua pingamizi tano juu ya maombi husika na hoja ya kwanza na ya pili waliiondoa kama alivyoeleza wakili wa wajibu maombi hivyo mahakama haioni haja ya kuiibua na kujadili tena pingamizi hizo ambazo hazikuwa sehemu ya hoja katika maamuzi bishaniwa. Katika maamuzi hayo pingamizi tatu zilijadiliwa ambazo ni kukosekana kwa taarifa ya uwakilishi, maombi hayakuwa sawa na kuwa kiapo cha waombaji hakikuelezea chanzo cha taarifa. Katika muenendo wa maombi Na. 636 ya 2018 kuhusiana na taarifa ya uwakilishi kumbukumbu zinaonesha kuwa mwakilishi wa waleta maombi alikiri mbele ya Msajili kuwa wakati wanapeleka maombi hayo hakukuwa na taarifa ya uwakilishi lakini ilipelekwa baadae tarehe 22/11/2018. Lakini katika pingamizi la kutokueleza chanzo cha taarifa mwakilishi huyo alipinga vikali pingamizi hili. Lakini pia maombi kutokuwa sahihi mwakilishi huyo alikubali pingamizi hilo kuwa ni kweli 7 maombi si sahihi lakini aliiomba mahakama iweze kuendelea na shauri hilo. Katika mazingira hayo ainishwa hapo juu, ni wazi kuwa mwakilishi alitambua ya kuwa maombi ya waleta maombi hayakuwa sahihi mbele ya Msajili na walikubali pingamizi hilo hivyo basi ni wazi msajili asingeweza kuendelea kusikiliza shauri hilo. Katika maamuzi hayo waleta maombi walielekezwa njia sahihi ya kufanya ili wapate haki ya kusikilizwa lakini wameamua kukazania wasikilizwe kupitia shauri ambalo hata wao walikubali lina mapungufu mbele ya mahakama. Ni msimamo wa mahakama katika maamuzi mbalimbali ya kuwa haitosikiliza shauri lolote lenye mapungufu au lililokiuka matakwa yoyote ya lazima ya kisheria. Hivyo maombi ya kuwa haki ya kusikilizwa itendeke mahakama inaelekeza kuwa wakati haki hiyo inapiganiwa mwombaji asikiuke taratibu zilizowekwa na sheria pamoja na mahakama. Lakini pia mahakama imepitia maombi hayo ya waleta maombi yaliyokuwa yamewasilishwa mbele ya msajili, kama walivyoeleza mbele ya mahakama hii ilikuwa ni maombi ya kuomba kurejeshwa kwa shauri lao lilokuwa limekwisha mbele ya msajili huyo (marked settled). Katika maombi yao waleta maombi walitumia kifungu cha 36 (1) (2) cha Kanuni za Mahakama ya Kazi. Vifungu hivyo vinaeleza ifuatavyo:- 8 'Rule 36 (1) Where a matter is struck off the file due to absence of a party who initiated the proceedings, the matter may be re-enrolled if that party proves the court with a satisfactory explanation by an affidavit, for his failure to attend the Court. (2) the affidavit shall be filed in Court and the Registrar shall place it to be heard by a Judge in chambers to decide whether the matter may be re enrolled or not.' Kifungu hapo juu kimeeleza wazi kuwa pale ambapo shauri linaondolewa kwa kutokuhudhuria kwa mleta maombi shauri hilo laweza kurejeshwa kama mleta maombi katika kiapo chake ataeleza sababu za mzingi zilizomfanya ashindwe kuhudhuria mahakamani. Kumbukumbu zinaonesha shauri lilokuwa linaombewa kurejeshwa mahakamani liliisha kwa pande zote mbili kukubaliana mbele ya msajili hivyo ni wazi kuwa msajili alikuwa tayari ameshalitolea maamuzi hivyo asingeweza kuendelea kusikiliza shauri hilo. Lakini pia shauri hilo lilikuwa na mapungufu mengi ya kisheria kama ilivyoainishwa hapo juu. Mahakama hii inasisitiza pia kuwa njia sahihi ya mwombaji kuweza kupata haki ya kusikilizwa ni kufuata yale yaliyoamuriwa katika kesi ya Blueberry Tanzania Services Ltd vs. Evarist Sesa, Lab. Div. DSM. Misc. Appl. No. 47 of 2010, (unreported) ambapo iliamuriwa kuwa:- 9 'After giving considerable thought of this issue and having failed to get a better instructive authority, my position is that a party aggrieved by the registrar's decision in execution of a CMA decree have 3 options; if the issue stems from any doubt regarding meaning of contents of the award, one of the options is one the aggrieved party to apply for revision of the award. An award is revisable on ground of ambiguity. Such an application would be brought under s. 94 (1) (e) (i) of the ELRA read together with Rule 24 and 28 of the Labour Court Rules. The second option would be to apply for review of the disputed award under the above cited section of the Act read together with Rule 26 of the Labour Court Rules. The third option is for the aggrieved party to put a machinery of reference under Order 41 of the Civil Procedure Code. That the aggrieved party may make an application to the registrar requesting a reference being made to the High Court on the matter on which doubt is entertainable.' Mahakama pia imezingatia hoja ya mwakilishi wa waleta maombi kuwa kiapo kinzani cha wajibu maombi kipo kinyume na kanuni ya 24 (2) ya Kanuni za Mahakama ya Kazi. Katika hili naunga mkono hoja ya wakili wa wajibu maombi kuwa kifungu hicho kinazungumzia taarifa ya maombi na sio kiapo kinzani. Hivyo basi mahakama inaona hoja hiyo ya 10 mwakilishi wa waleta maombi haina mashiko. Lakini pia ni rai ya mahakama kuwa endapo upande wowote umegundua mapungufu ya nyaraka yoyote iliyowasilishwa na upande mwingine basi mapungufu hayo/pingamizi ziibuliwe mapema kabla ya kuanza kusikilizwa maombi husika. Hivyo basi, kutokana na majadiliano yote hapo juu ni wazi kuwa waleta maombi wameshindwa kutoa sababu za msingi za kuifanya mahakama hii itupilie mbali maamuzi ya Msajili katika maombi ya anuwai na. 636 ya 2018. Mahakama inayatilia mkazo maamuzi hayo na kuagiza yafuatwe kama yalivyo. Aidha mahakama imeyametupilia mbali maombi haya ya marejeo. Imeamuriwa hivyo. wenegoha JAJI 30/07/2021 li