Download PDF

Tanzania Judgment

TANZLII

Selemani Juma Nyigo dhidi ya Jamhuri

On this page

Professional case brief

Research organized from the available case record

Source document

01

Holding and result

The prosecution failed to prove beyond reasonable doubt that the appellant committed the offences due to unreliable identification and inadmissible hearsay evidence; the trial court erred in rejecting the alibi defence without sufficient proof of guilt.

Court disposition

appeal allowed

Orders

  • Conviction and sentence quashed
  • Appellant to be released from prison forthwith unless lawfully held for another cause

02

Material facts

Parties

Selemani Juma Nyigo @ Mwanyigo

Appellant Counsel: Maula Tweve

Jamhuri

Respondent Counsel: Edna Mwangulumba

Amounts and remedies

  • Sentence for Robbery: years 15
  • Sentence for Rape: years 30
  • Amount Stolen: TZS 100,000

03

Procedural history

  1. Posture

    Criminal Appeal / Judgment

04

Questions and positions

Legal issues

Party arguments

Applicant
The prosecution failed to prove the charges beyond reasonable doubt; identification was unreliable; alibi defence was improperly rejected; procedural irregularities occurred.
Respondent
The prosecution evidence was sufficient; identification was proper; alibi defence was not properly notified; procedural irregularities did not affect the fairness.

05

Court’s reasoning

  1. 01

    Waziri Amani v Republic [1980] T.L.R 250

    Visual identification evidence must be reliable and free from possibility of error, especially where the accused and victim are strangers.

  2. 02

    Section 194(6) Criminal Procedure Act (SMMJ)

    Alibi defence can only be rejected if the prosecution evidence proves the charge beyond reasonable doubt.

  3. 03

    Section 62 Evidence Act

    Hearsay evidence is inadmissible unless exceptions apply.

06

Ratio, limits and disposition

Ratio decidendi

The prosecution failed to prove beyond reasonable doubt that the appellant committed the offences due to unreliable identification and inadmissible hearsay evidence; the trial court erred in rejecting the alibi defence without sufficient proof of guilt.

Obiter and limits

  • Daytime commission of an offence does not guarantee reliable identification, especially where the victim and accused are strangers.
  • Procedural irregularities in preliminary hearing did not affect the fairness of the trial.

Court disposition

appeal allowed

  • Conviction and sentence quashed
  • Appellant to be released from prison forthwith unless lawfully held for another cause

Source and reliance status

TANZLII · 1 January 2024

This page organises the available record for research. Confirm quotations, current status, and subsequent treatment against the official source before relying on the case.

Judgment reading view

Judgment text

The complete available source text.

Source document

TANZLII

Judgment· 1 January 2024

Selemani Juma Nyigo dhidi ya Jamhuri

MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA (MASIJALA NDOGO YA IRINGA) ILIYOPO IRINGA. RUFAA JINAI NA. 68 YA 2021 (Asilia Shauri la Jinai Na. 18/2020 la Mahakama ya WHaya ya Iringa mbe/e ya Mhe. E.A. Nsangatufu, HMM). SELEMANI JUMA NYIGO @ MWANYIGO.................... MRUFANI

DHIDIYA JAMHURI ............................................. MRUFANIWA

HUKUMU 23 & 30/05/2024 I.C. MUGETA, J: Kuna matukio katika maisha yangefaa kwa nadharia za kujifunzia katika mahakama za bandia (moot courts) vyuoni. Kinyume chake kwa baadhi ya watu siyo nadharia ni uhalisia. Tarehe 12/2/2021 binti bikra, raia wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 19 aliyekuwa akifanya kazi za kujitolea kama mwalimu hapa Iringa alibakwa na kuporwa mali zake mchana kweupe. Makazi yake yalikuwa eneo la Gangilonga na kazi alifanyia Ipogolo. Siku ya tukio alikuwa akitembea kurudi nyumbani kupitia njia ya mkato ya waenda kwa miguu itokayo Ipogolo hadi Gangilonga. Kwa ushahidi wake, njiani alikutana na mrufani ambaye alimfunga kamba mikononi, akambaka na kumpora mali zake ambazo ni simu Page 1 of 8 ya mkononi aina ya Samsung Galax C7, kadi ya ATM na fedha taslimu shilingi laki moja. Upelelezi ulifanyika na mrufani alikamatwa kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo. Hati ya mashtaka ina mashtaka mawili: unyang'anyi wa kutumia nguvu kinyume na fungu la 285 na 286 na kubaka kinyume na fungu la 130(1) & 2(a) na 131(1) vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu [Sura ya 16 Toleo Rekebu (T.R) la 2022] Mtawalia. Hi kulinda faragha ya mhanga, sitataja jina lake. Katika shauri hili alitoa ushahidi kama shahidi wa kwanza (SMI) wa upande wa mashtaka. Alieleza tukio lilivyotetendeka na kwamba lilidumu kwa dakika 30. Hakimu Mkazi Mwandamizi aliyesikiliza shauri hili aliridhika kuwa mhanga aliporwa

mali zake kwa nguvu na kubakwa na aliyembaka ni mrufani. Alimtia hatiani kwa makosa yote mawili na kumwadhibu kifungo cha miaka 15 kwa kosa la kwanza na miaka 30 kwa kosa la pili. Mrufani hakuridhika na hatia pamoja na adhabu. Rufaa yake ina sababu 13. Mbili kati ya hizo ziliamuliwa na mahakama hii (Mlyambina, J) tarehe 8/6/2022. Nazo zilihusu kukiukwa kwa vifungu 131 na 214 vya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai [Sura ya 20 T.R la 2022] (SMMJ). Mahakama hii, kwa ukiukaji huo, ilielekeza usikilizaji wa shauri hili uanze upya. Page 2 of 8 Mkurugenzi wa Mashtaka alikata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama hii. Rufaa hiyo ifishinda tarehe 21/3/2024. Mahakama ya Rufani iliagiza mahakama hii isikilize sababu zote 11 za rufani zilizobakia kwa sababu ukiukaji wa she ria, hata kama upo, haukuvunja misingi ya haki. Amri hiyo ndiyo iliyozaa hukumu hii. Kwa vile rufaa ilishasikilizwa jukumu langu ni kuandika hukumu kwa kuzingatia kumbukumbu zilizopo. Rufaa iliposikilizwa, mrufani aliwakilishwa na msomi wakili Maula Tweve. Mkurugenzi wa Mashtaka aliwakilishwa na Msomi Wakili wa Seri kali Edna Mwangulumba. Sababu zote za rufaa zilizobakia, isipokuwa moja inayohitaji kuamuriwa peke yake na ambayo nitaieleza baadaye, zinabeba lalamiko moja kuu la msingi. Kwamba, mashtaka hayakuthibishwa bila kuacha mashaka ya msingi. Nitazingatia lalamiko hilo kuu katika uamuzi huu. Kama mahakama ya

kwanza ya rufani, nitachambua upya ushahidi uliopo kuona kama mahakama ya chini ilifanya uamuzi sahihi. Ninakubaliana na Hakimu Mkazi Mwandamizi kuwa ushahidi wa SMI pamoja na daktari aliyemtibu slku ya tukio ndugu Shaban Likondongoma •(SM3) unathibitisha kuwa mhanga aliingiliwa kingono. Ripoti ya daktari ni kielelezo P2. SM3 aliona shahawa ukeni ha bikra iliyotobolewa na kuvuja damu. Kuhusu kuporwa mali kwa nguvu, sioni sababu ya msingi kutomwamini Page 3 of 8 mhanga kwamba mali zake ziliporwa. Hoja inayobishaniwa ni iwapo, mrufani ndiye aliyetenda matukio yote mawili anayoshitakiwa nayo. Ushahidi wa moja kwa moja wa tukio lilivyotendeka aliutoa mhanga. Mhanga (SMI) hakumfahamu mrufani kabla ya tukio. Katika ushahidi wake hakueleza wajihi wa mrufani wala kilichomsaidia kumtambua kwenye gwaride la utambulisho lililoendeshwa na ASP William Kilangi (SM2) na alipotoa ushahidi mahakamani mrufani akiwa kwenye kizimba. Rejesta ya gwaride la utambulisho ilitolewa na SM2 kama kielelezo Pl. Mhanga hafahamu ni namna gani polisi walifanikiwa kumkamata mrufani. Ushahidi unaomuunganisha mrufani na tukio ni uliotolewa na G. 4395, DC Lubeya (SM4) kama mpelelezi wa kesi. Kwamba, karibu na eneo la tukio korongoni, walikuta nguo za mtuhumiwa ambazo waosha magari wenzake wa eneo la Ndiuka walizitambua kama mali ya mrufani. Hata hivyo waosha magari hao hawakuletwa mahakamani kuthibitisha jambo

hili. Kinyume chake, mrufani aliwaleta mahakamani mshahidi watatu, SU2, SU3 na SU4 ambao walisema muda na siku inayodaiwa tukio kutendeka walikuwa na mrufani katika kijiwe chao cha kuosha magari katika eneo la Ndiuka. Ushahidi huu ulikataliwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi kwa vile mrufani hakutoa indhari ya kusudio la kutumia ushahidi wa alibi kama inavyotakiwa na kifungu cha 194(4) cha SMMJ. Je hakimu alikuwa sahihi? Page 4 of 8 Ushahidi wa upande wa mashtaka una matatizo makuu mawili ya msingi. Kwanza, mhanga katika ushahidi wake hakusema kuwa aliwaeleza polisi wajihi wa mtuhumiwa ambao uliwasaidia katika upelelezi na kumkamata mrufani na utambuzi wake kwenye gwaride la utambuzi lililoendeshwa na SM2. Kueleza wajihi na hata mavazi ya mtuhumiwa ni sharti la msingi la kisheria la kufanya mahakama imwamini shihidi mtambuzi aliyeona kwa macho na kuleta thamani ya kiushahidi linapofanyika gwaride la utambuzi. Haya yalielezwa kwenye shauri la Leonard Mathias Makami & Mwenzake dhidi ya Jamhuri, Rufaa Jinai Na. 579/2017, Mahakama ya Rufani - Dar es Salaam (isiyoripotiwa) ukurasa 16 -18. Kwa msingi huo utambuzi wa mrufani kwenye gwaride la utambulisho na mahakamani bila ushahidi wake wa jinsi alivyomwelezea mtuhumiwa baada ya tukio kwa watu wengine na gwaride lenyewe la utambuzi havina thamani kiushahidi. Ninatambua katika ushahidi wake, SM4 alisema mhanga alimweleza kuwa mnyanganyi na

mbakaji alikuwa mweusi, mwenye pua kubwa na mrefu wastani. Hata hivyo, SM4 hakueleza kuwa mrufani ndiye mtu pekee ambaye ni mweusi, mwenye pua kubwa na mrefu wastani na ni kwa namna gani wajihi huo ulimsaidia yeye kubaini mhalifu na SMI kumtambua kwenye gwaride la utambuzi. Page 5 of 8 Tatizo la pili ni namna polisi walivyombaini mtuhumiwa. Kwamba, walitumia utambuzi wa nguo zake zilizokutwa korongoni jirani na eneo la tukio bila kuwaleta mahakamani mashahidi waliotambua nguo hizo. Kutokufika kwa mashahidi hao kunafanya ushahidi wa mpelelezi (SM4) kuwa nguo zilizokutwa karibu na eneo la tukio ni za mrufani kuwa ushahidi wa kuambiwa. Ushahidi wa kuambiwa hauna nguvu kisheria chini ya kifungu cha 62 cha Sheria ya Ushahidi [Sura ya 6 T.R la 2022]. Kwa ajili ya mambo hayo mawili, nimeridhika kwamba utambuzi wa mrufani kama mkosaji unatia mashaka. Kwa mashaka hayo hakimu hakuwa na sababu ya kukataa utetezi wa mrufani kwa msingi wa sheria aliyoitumia. Chini ya kifungu cha 194(6) cha SMMJ, wajibu wa mahakama kukataa au kukubali utetezi wa "alibi" uliotolewa bila indhari unakuja pale tu tuhuma zinapokuwa zimethibitika. Katika shauri hili mrufani hakutambuliwa ipasavyo hivyo asingetiwa hatiani hata bila ya kujitetea. Kwa msingi huo, licha ya kuhuzunishwa na tukio lililompata mhanga, siyo halali wala haki kisheria mrufani abebe msalaba kwa tuhuma ambazo hazina ushahidi wa kuzithibitisha.

Ninahitimisha kwamba licha ya tukio kufanyika mchana, hakuna ushahidi toshelevu kuthibitisha kuwa lilitendwa na mrufani. Utambuzi wa kuona (visual identification) ni ushahidi dhaifu ambao utatumika dhidi ya mtuhumiwa pale tu ambapo hakuna uwezekano wa Page 6 of 8 utambuzi kukosewa. (Waziri Amani dhidi ya Jamhuri [1980] T.L.R 250). Katika shauri hili, uwezekano wa utambuzi kuwa na makosa ni mkubwa. Nimeridhika kuwa uamuzi wa mahakama ya chini kuwa kwa vile tukio lilifanyika mchana SMI hakukosea katika utambuzi wake siyo sahihi. Ni makosa kuamini kuwa kila tukio linalofanyika mchana mtambuzi hawezi kukosea katika utambuzi wake hasa kwenye mazingira ambayo mhanga na mtuhumiwa hawafahamiani. Sababu ya rufaa ambayo inahitaji kuamriwa peke yake inahusu hoja ya kisheria. Kwamba, usikilizaji wa awali haufufanyika vizuri. Hii ilikuwa ni moja ya sababu iliyopelekea mahakama iagize shauri hili lisikilizwe upya. Ni kweli kwamba usikilizaji wa awali uliborongwa. Maelezo ya tukio hayapo kwenye kumbukumbu za shauri na hata mambo ya msingi yasiyobishaniwa hayakuorodheshwa. Hakika huo ni ukiukaji wa sheria. Hata hivyo, nimeridhika kuwa ukiukwaji huo haukusababisha haki kutotendeka kwa upande wowote. Lalamiko katika sababu hiyo ya rufaa halina msingi. Mwisho, kwa vile nimefikia hitimisho kuwa mhanga hakueleza wajihi wa mtuhumiwa mahakamani na kwa watu wengine ipasavyo hivyo gwaride la utambuzi

(kielelezo P2) na utambuzi wake mahakamani ni batili na kwa vile ushahidi wa SM4 kuhusu nguo zilizokutwa eneo la tukio kuwa ni za mrufani ni ushahidi wa kuambiwa, mahakama ya chini ilijipotosha kumtia hatiani. Hivyo, Page 7 of 8 hatia hiyo ninaifuta na adhabu yake nimeibatilisha. Rufaa imeshinda. Mrufani aachiliwe huru kutoka gerezani anakoshikiliwa mara moja isipokuwa kama kuna sababu nyingine nje ya shauri hili inayohalalisha kuendeleza kushikiliwa kwake. I.C. MUGETA

JAJI 30/5/2024 Mahakama: Hukumu hii imesomwa wakiwepo Muzzna Mfinanga, Wakili wa Serikali na mrufani. Isw. I.C. MUGETA

JAJI 30/5/2024 Page 8 of 8

Source wording is retained. Consult the source document for its original formatting and pagination.

Authorities

Authorities used by the court

Cases, legislation, regulations, and constitutional provisions identified in the available record.

Waziri Amani v Republic [1980] T.L.R 250

Case cited

Leonard Mathias Makami & Another v Republic, Criminal Appeal No. 579/2017

Case cited

Penal Code Cap 16 R.E 2022

Legislation

Legislation referenced in the available case record.

Criminal Procedure Act Cap 20 R.E 2022

Legislation

Legislation referenced in the available case record.

Evidence Act Cap 6 R.E 2022

Legislation

Legislation referenced in the available case record.

Case-aware research

Ask AI about this case

The judgment and available research above are public. New questions open in a separate private conversation grounded in this case.

About this LexChat collection

This page organizes the available case record for research. Verify quotations, current status, and subsequent treatment against the source document. Corrections can be reported to hello@esheria.ai.

Legal information, not legal advice. Research summaries do not replace the judgment.