shirika la reli tanzania vs revocatus mgawe another 2022 tzhcld 929 28 septemba 2022
The applicant failed to demonstrate sufficient cause for the delay in seeking extension of time. The alleged illegalities were not apparent on the face of the record and the dispute regarding limitation was a factual issue, not a clear illegality. The delay of over five years was not justified.
Source-derived case information.
- Citation
- shirika la reli tanzania vs revocatus mgawe another 2022 tzhcld 929 28 septemba 2022
- Parties
- Applicant: Shirika la Reli Tanzania; Respondent: Revocatus Mgawe; Respondent: Stephen Mdachi
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2022
- Procedural Posture
- Labour Application / Ruling on Application for Extension of Time
- Outcome
- application dismissed
- Legal Topics
- Extension of Time, Review of Arbitral Award, Jurisdiction of Commission for Mediation and Arbitration, Limitation Period
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Shirika la Reli Tanzania
Applicant
Revocatus Mgawe
Respondent
Stephen Mdachi
Respondent
Procedural Posture
Labour Application / Ruling on Application for Extension of Time
Legal Issues
- 1 Whether sufficient cause was shown to warrant extension of time to file an application for review of the CMA award
- 2 Whether the CMA had jurisdiction to entertain the dispute filed by the respondents
- 3 Whether the dispute was filed out of time before the CMA
Ratio Decidendi
The applicant failed to demonstrate sufficient cause for the delay in seeking extension of time. The alleged illegalities were not apparent on the face of the record and the dispute regarding limitation was a factual issue, not a clear illegality. The delay of over five years was not justified.
Court Disposition
application dismissed
Orders
- Application for extension of time is dismissed.
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
MAHAKAMA KUU YA TANZANIA DIVISHENI YA KAZI DAR ES SALAAM MAOMBI MADOGO YA KAZI NA 200 YA 2022 [Yatokanayo na Tuzo ya Tume ya Usuluhishi na uamuzi iliyotolewa na Mh. Msuri,Muamuzi katika CMA/DSM/ILA/290/12/243] KATI YA SHIRIKA LA RELI TANZANIA.......... ....................... MLETA MAOMBI DHIDI REVOCATUS MGAWE.................................. MJIBU MAOMBI WA KWANZA STEPHEN MDACHI...................... MJIBU MAOMBI WA PILI UAMUZI S.M. MAGHIMBI, J: Mleta Maombi ambaye ni Shirika la Reli Tanzania (TRC) ameleta maombi haya chini ya Kanuni ya 24(1), 24(2)(a) (b)(c)(d)(e) & (f) na 24(3)(a)(b)(c) & (d) na Kanuni 55 (1)(2) na (3) ya Kanuni za Mahakama ya Kazi, Tangazo la Serikali Na. 106 la mwaka 2007 ("Kanuni"). Katika Maombi yake ya Faragha, mleta maombi ambaye hakuridhishwa na maamuzi ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi kanda ya Ilala ("Tume"), ana nia ya kuleta maombi ya mapitio ya uamuzi hil lakini yuko nje ya muda. Hivyo basi kwenye taarifa yake ya maombi anawasilisha maombi ya kuongezewa muda wa mapitio, hivyo anaiomba Mahakama itoe amri zifuatazo: (a) Kwamba, Mahakama hii tukufu iongeze muda wa kuita na kupitia muenendo na tuzo ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi i iliyotolewa tarehe 16/12/2017 mbele ya Mhe. Msuri Muamuzi, katika Maombi ya mgogoro wa Kazi Na. 290/12/243 ya Mwaka 2019. (b) Na amri nyingine yeyote Mahakama hii tukufu itawiwa kuitoa. Maombi haya yaliambatana na kiapo cha Bwana Hangi Chang'a, Wakili wa Serikali Mkuu kilichoapwa tarehe 01 mwezi wa 06 mwaka 2022. Kwa upande wao, wajibu maombi walipinga maombi kwa kiapo kinzani kilichoapwa nao kwa pamoja wakiiomba Mahakama hii kutupilia mbali maombi hayo. Shauri hili lilisikilizwa kwa njia ya maandishi. Kwa ufupi historia ya shauri hili ni kwamba wajibu maombi walikuwa waajiriwa wa Shirika la Reli la Afrika Mashariki. Baada ya kuvunjika kwa Shirika la Reli la Afrika Mashariki wajibu maombi walihamishiwa shirika la reli Tanzania -TRC. Ilipofika tarehe 31/08/2007, wajibu maombi walipunguzwa kazini na kulipwa malipo yao ya kuachishawa kazi pamoja na malipo mengine ya Pensheni. Kwa mujibu wa wajibu maombi, malipo hayo hayakufuata utaratibu hivyo kupelekea kukatwa makato ambayo hayakuwepo na waliahidiwa kulipwa na mfuko wa pensheni wa PPF. Mnamo mwaka 2012, wajibu walifungua shauri la kazi Na. CMA/DSM/IAL/290/12/243 mbele ya Tume, wakidai mapunjo ya malipo 2 yao ya pensheni kutokana na kutoridhishwa na malipo ya pensheni ambayo yalilipwa baada ya kupunguzwa kazi tarehe 31/08/2007. Kwa upande wake Tume iliridhika na uthibitisho wa madai hayo na kuamuru mleta maombi awalipe stahiki zao na hivyo kwa kutoridhika, mleta maombi ameleta madai haya ya kuongezewa muda ili alete maombi ya mapitio. Katika kiapo chao pamoja na mawasilisho yao, sababu kuwa ya uchelewaji iliyotolewa na TRC ni kuwa baada ya Tuzo kutolewa, pamoja na mambo mengine, mleta maombi aliomba ushauri wa kisheria kwa Ofisi ya Wakili Mkuu (Kiambatisho TRC 1 kwenye kiapo). Kwamba, baada ya ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kupata barua ya kuomba ushauri wa kisheria kutoka kwa mleta maombi ilifanyiwa kazi pasipo kuchelewa na baada ya kupitia jalada na nyaraka zinahusiana na mgogoro, Wakili Mkuu wa Serikali aligundua makosa ya kisheria (illegalities) katika Tuzo iliyotolewa na Tume. Mleta maombi alidai kuwa makosa hayo ya kisheria yanakinzana na maslahi mapana ya Serikali. Katika hati ya kiapo sababu zifuatazo za makosa ya kisheria zimeainishwa kwa ajili ya kusikilizwa na mahakama hii pamoja na kwamba Tume haikuwa na Mamlaka kisheria ya kusikiliza na kuamua mgogoro kwa kuwa ulikuwa nje ya muda. Vile vile mleta maombi amedai 3 kuwa Tume haikuwa na Mamlaka Kisheria ya kuamua mgogoro ambao ulikuwa chini ya msingi wa kutoridhiishwa na malipo ya pensheni (PPF). Vilevile, mleta maombi alidai kuwa kabla ya maombi haya alishawahi kuleta maombi ya kuomba kuongezewa muda namba 425 ya mwaka 2021 na tarehe 21/04/2022 Mleta maombi aliomba kuyaondoa na kuomba kuruhusiwa kuleta maombi mengine haya nje ya muda. Akinukuu maamuzi ya Mahakama ya Rufani kwenya Rufaa ya Jamhuri dhidi ya Yonakapona na wenzake 9 [1985] T.L.R 84, mleta maombi aliwasilisha kwamba kwenye maamuzi haya mahakama ilisema katika kuamua kama kuna uwezekano wa kukubali maombi ya kukata rufaa nje ya muda,Mahakama itazingatia kama kuna sababu zenye mashiko,sio tu kwa kuchelewa bali pia kuwe na sababu za kuongezewa muda wa kusikiliza rufaa. Vile vile mleta maombi alidai kwamba alileta hoja kuwa maombi ya kuongezewa muda yanaweza kutolewa pale kunapokuwa na makosa ya kisheria katika tuzo iliyotolewa. Mahakama kuu na Mahakama ya Rufaa katika kesi mbalimbali zilishawahi kutoa maamuzi kuwa makosa ya kisheria ni kigezo kizuri cha kuongezewa muda. Alisisitiza wasilisho hili kwa kuilekeza Mahakama hii kwenye maamuzi ya Mahakama ya Rufani katika shauri la KATIBU MKUU, WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA 4 KUJENGA TAIFA DHIDI YA DEVRAN VALAMBHIA, [1992JT.L.R 182 ambapo Mahakama ya Rufani iliamua kwamba Mahakama iliweka msimamo ya kwamba kunapokuwa na makosa ya kisheria katika maamuzi yanayobishaniwa, mahakama inajukumu hata inapobidi kuongeza muda ili kushughulikia makosa ya kisheria. Mleta maombi aliendelea kuwasilisha kuwa wajibu mahombi walifukuzwa kazi tarehe 31/08/2007, miaka mitano baadae wajibu maombi walifungua mgogoro Tume bila kuomba nafuu ya Tume kuongeza muda ili kuleta kesi yao nje ya muda wa kisheria. Akasisitiza kwamba Tume ilisikiliza na kuamua mgogoro huo ambao ulikuwa nje ya muda wa kisheria ambao ni miezi sita tangu kutokea kwa mgogoro. Alihitimisha kuwa kosa hilo la Tume ni sababu ya msingi kwa Mahakama hii kuzingatia na kuona umuhimu wa kuongeza muda ili kosa hilo liweze kurekebishwa, huku akiiomba Mahakama hii kutumia kigezo hiki kuongeza muda kama walivyoomba. Kwa upande wao, wajibu maombi walieleza kwamba waliingiza mgogoro wao katika Tume mnamo tarehe 16/05/2012, kwa sababu mgogoro huo ndio ulianza na sio kwamba mgogoro huu ulianza siku ya tarehe 31/08/2007 siku ambayo wajibu maombi waliachishwa kazi kama hoja za mleta maombi zinavyosema. Walifafanua kuwa hawajawahi 5 kuwa na mgogoro juu ya kuachishwa kazi na mwajiri wao TRC na mgogoro haukuanza tarehe na siku ambayo wajibu maombi waliashishwa kazi. Waliendelea kufafanua kuwa mgogoro baina yao na mwajiri TRC ulianza pale TRC ilipowapa barua ya mwisho ya kuonyesha hawatolipa pesa ambayo walikata kwenye mafao yao kama wafanyakazi mnamo tarehe 30/03/2012. Vilevile wajibu maombi wameeleza kuwa hawajawahi kuwa na mgogoro wowote na PPF, kwani walipata michango yao yote na ile waliyochangiwa na mwajiri wao TRC kwa mujibu wa sheria na hapo hapakuwa na mgogoro kabisa. Walieleza kuwa mgogoro kati ya wajibu maombi na mwajiri wao TRC ulianza pale Jumuiya ya Afrika Mashariki ilipowalipa wajibu maombi pesa za mafao yao kwa kupitia mwajiri wao ambapo baadaya malipo hayo, mwajiri huyu aliwakata kiasi cha shilingi 13,452,308/- pesa ya Kitanzania kwa mjibu maombi wa kwanza (Stephen Mdachi), na mjibu maombi wa pili (Revocatus Mgawe) kiasi cha shilingi 20,240,772/- pesa ya Kitanzania. Walilalamika kuwa pesa walizokatwa wajibu maombi si pesa za PPF ni pesa zao za mafao yao kutoka kwa muajiri wa zamani na wala wajibu maombi hawakuwa na mgogoro au kudai pesa za PPF. Kwamba, barua ya mwisho iliyotolewa na TRC ya tarehe 30/03/2012 ndio ilileta mgogoro na sio tarehe ya 6 kusimamishwa kazi kama mleta maombi alivyoeleza katika hoja zake na wala mgogoro haukuwa wa kuachishwa kazi bali mgogoro ulikuwa juu pesa zilizokatwa na mwajiri. Kwa mantiki hiyo, wajibu maombi wlileta hoja kuwa walikuwa ndani muda kwa kuwa shauri lao waliingiza katika Tume ya usuluhishi na uamuzi mnamo tarehe 16/05/2012. Baada ya kueleza hoja zao, wajibu maombi walikataa vikali hoja ya mleta maombi ya kwamba wajibu maombi waliingiza shauri hili wakiwa nje ya muda. Walidai kuwa hoja hizo hazina msingi wowote na kwamba maombi haya hayana miguu ya kusimamia. Kwenye hoja ya pili ya waleta maombi kuwa Tume haikuwa na mamlaka kisheria kuamua mgogoro ambao ulikuwa chini ya misingi ya kutoridhishwa na malipo ya pension (PPF), wajibu maombi walieleza kuwa kama walivyojieleza hapo juu kwenye sababu ya kwanza, mgogoro haukuhusu malipo ya PPF ila ni makato yalifanywa na mwajiri kwa kudai ni makato ya PPF. Wakijibu kuhusu kesi aliyo itumia mleta maombi kukazia hoja zake, lie ya Republic Vs Yonakapona and 9 Others (1985) T.L.R. 84, kwamba kunapaswa kuwa na sababu za msingi za kupewa muda wa ziada kukata rufaa pia unapaswa kuwa na sababu za kupewa muda huo, wajibu maombi walisema kwamba uamuzi huo unamaanisha kuwa na sababu ya kuchelewa na kwa nini upewe muda wa nyongeza 7 kwa kuonyesha mapungufu ya kisheria ambayo hayakuwepo, ila kesi tajwa hapo juu inataka vyote kwa pamoja sababu ya kuchelewa na kwa nini uongezewe muda ambacho mleta maombi hakutekeleza. Kwa kumalizia, waleieleza kuwa shauri lao ni la muda mrefu na uceleweshwaji wa waleta maombi umelenga kutowapatia haki yao ya msingi na maombi haya hayana uhalali, Kwa upande wangu, baada ya kupitia maombi haya nimeona kuwa hakuna sababu yoyote ya msingi iliyoletwa juu ya uchelewaji huo. Sababu ambayo mleta maombi amelalia ni kuwa uamuzi wa Tume ni batili kwa sababu mbili. Sababu ya kwanza ilikuwa kwamba wajibu maombi walifungua mogogoro huo nje ya muda. Lakini katika majibu yao wajibu maombi wamesema kiini cha mgogoro hakikuwa kuachishwa kazi bali ilikuwa ni mapungufu ya malipo yao huku wakiainisha kuwa barua ya kuwanyimwa malipo ya pungufu ilikuwa ni ya tarehe 30/03/2012. Hivyo basi ni wazi kuwa suala la kuwa shauri lilikuwa nje ya muda ni suala la kubishaniwa kiushahidi na sio suala la "illegality" moja kwa moja kama mleta maombi anavyotaka Mahakama hii ione. Hivyo basi hoja hii haitoshelezi kuwa sababu ya kuongeza muda. Hoja ya pili iliyoletwa na mleta maombi ni kuwa Tume haikuwa na Mamlaka Kisheria ya kuamua mgogoro ambao ulikuwa chini ya msingi 8 wa kutoridhiishwa na malipo ya pensheni (PPF). Ukiangalia rekodi na uamuzi wa Tume, kama walivyoeleza wajibu maombi, Tume haikuamuru kulipwa makato yao ya Pensheni bali ilieleza kuwa muajiri alikata makato ya pensheni zaidi ya yale ambayo wajibu maombi walitakiwa kulipwa. Hivyo basi hoja hii pia ni ambayo imetengenezwa na mleta maombi ili kuonyesha kuwa kuna illegality kwenye maamuzi lakini ni hoja ambayo ukiangalia rekodi haina ukiukwaji wa sharia wa moja kwa moja kuwezesha kuhalalisha kuongeza muda wa kuleta maombi baada ya kuchelewa kwa zaidi ya miaka mitano. Kutokana na sababu hizo, Mahakama hii imejiridhisha kuwa mleta maombi hajaleta sababu zote za msingi za kuhalalisha uongezwaji wa muda. Kinachooneka ni uzembe na sasa baada ya miaka mitano kupita ndio mleta maombi anadai kuwa alipitia uamuzi na kuona mapungufu, sababu iliyoletwa kwanini ilichukua miaka mitano kuona mapungufu hayo hazikuwa na msingi wowote na kwakuwa hakuna sababu za ucheleweshwaji wala Mahakama haina illegality kwenye maamuzi hayo, hoja hizo hazina mashiko. Kutokana na uchambuzi hapo juu, ni uamuzi wa Mahakama kuwa Mleta maombi ameshindwa kuleta sababu za msingi za kuifanya 9 Mahakama iongeze muda wa kuleta maombi ya mapitio. Hivyo basi maombi haya yanatupiliwa mbali. Imetolewa leo Tarehe 28 Mwezi Septemba, 2022. 10