tanzania electric supply company limited vs ramadhani m mgaya 2021 tzhcld 301 20 agosti 2021
The applicant proved, on the balance of probabilities, that the respondent submitted a forged certificate and that proper procedures for dismissal were followed, making the termination lawful.
Source-derived case information.
- Citation
- tanzania electric supply company limited vs ramadhani m mgaya 2021 tzhcld 301 20 agosti 2021
- Parties
- Applicant: Tanzania Electric Supply Company Limited; Respondent: Ramadhani M. Mgaya
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2021
- Procedural Posture
- Labour Revision / Final Judgment
- Outcome
- Application allowed; award of reinstatement set aside.
- Legal Topics
- Unlawful Termination, Employment Certificate Forgery, Procedural Fairness in Dismissal
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Tanzania Electric Supply Company Limited
Applicant
Ramadhani M. Mgaya
Respondent
Procedural Posture
Labour Revision / Final Judgment
Legal Issues
- 1 Whether the respondent was unlawfully terminated
- 2 Whether proper procedures were followed in the dismissal
- 3 Whether the respondent submitted a forged certificate
Ratio Decidendi
The applicant proved, on the balance of probabilities, that the respondent submitted a forged certificate and that proper procedures for dismissal were followed, making the termination lawful.
Court Disposition
Application allowed; award of reinstatement set aside.
Orders
- Award of reinstatement is quashed.
- If respondent was not paid arrears for May-August 2017 as claimed in CMA Fl, he is entitled to those payments.
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
MAHAKAMA KUU YA TANZANIA DIVISHENI YA KAZI PAR ES SALAAM MAOMBI YA MAREJEO NA. 827 YA 2019 KATI YA TANZANIA ELECTRIC SUPPLY COMPANY LIMITED........... MLETA MAOMBI DHIDI YA RAMADHANI M. MGAYA MJIBU MAOMBI HUKUMU Tarehe ya Amri ya Mwisho: 02/08/2021 Tarehe ya Hukumu: 20/08/2021 I. Arufani, J. Katika shauri hili mleta maombi aliiomba Mahakama hii ifanye marejeo na kutengua tuzo iliyotolewa na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ya Kinondoni, Dar es Salaam (itakayokuwa inarejewa kama Tume) katika mgogoro wa ajira namba CMA/KIN/R1047/17/1013, ambao ulifikishwa mbele ya tume na mjibu maombi baada ya kutoridhishwa na kusitishiwa ajira yake. Baada ya kusikiliza mgogoro huo Tume iliamua kuwa, mjibu maombi aliachishwa kazi isivyo halali na kutoa amri ya kuwa arejeshwe kazini chini ya kifungu cha 40 (1) (a) ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Sura ya 366 marejeo ya 2019 (itakayokuwa inarejewa kama Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini). i Mleta maombi hakuridhishwa na uamuzi wa Tume na hivyo akafungua maombi haya kuiomba mahakama hii ifanye marejeo ya tuzo hiyo kwa sababu zifuatazo:- /. Kwamba mwamuzi alikosea kisheria na kiuhalisia kwa kusikiliza malalamiko ambayo hayako ndani ya mamlaka yake. ii. Kwamba mwamuzi alikosea kisheria na kiuhalisia aiipoamua kwamba, sababu za kumuachisha kazi mjibu maombi hazikuwa na mashiko. Hi. Kwamba mwamuzi alikosea kisheria na kiuhalisia aiipoamua kwamba, mleta mombi aiikuwa na wajibu wa kufanya uchunguzi Hi kuhakiki uhalali wa cheti. iv. Nafuu zozote Mahakama hii itakavyoona inafaa. Maombi haya yaliambatanishwa na kiapo cha Farida Adam Sued, Afisa Mwandamizi wa Mleta maombi, wakati kwa upande wake mjibu maombi alipinga maombi haya kwa kuwasilisha mahakamani kiapo kinzani kilichoapwa na Stanley Kalanje, mwakilishi binafsi wa mjibu iB . . . maombi. Maelezo mafupi ya shauri hili ni kwamba, mleta maombi alimwajiri mjibu maombi toka mwaka 1991 kama mlinzi na baadaye mwaka 2000 alibadilishiwa kazi na kuwa msoma mita. Mahusiano yao ya kiajira yalidumu mpaka tarehe 15 Agosti, 2017 ambapo mjibu maombi 2 alisitishiwa ajira yake baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kuwasilisha kwa mwajiri wake ambaye ni mleta maombi cheti cha kidato cha nne (form four) kilichoghushiwa. Ilielezwa kuwa kosa hilo liligundulika baada ya zoezi la uhakiki wa vyeti vya kitaaluma vya watumishi wote wa umma nchini, lililoendeshwa na Serikali kupitia Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, na kupelekea kusitishwa kwa ajira za watumishi wote walioghushi vyeti akiwemo dBk mjibu maombi. Shauri hili lilisikilizwa kwa njia ya maandishi ambapo mleta maombi aliwakilishwa na Wakili Farida Adam Sued, Afisa Mwandamizi kutoka idara ya sheria ya mleta maombi. Kwa upande wa mjibu maombi aliwakilishwa na Stanley Kalanje, mwakilishi binafsi. Kwa kuwa wawakilishi wa pande zote mbili walileta mawasilisho yao kwa lugha ya Kiswahili na kwa kuwa kanuni ya 4 (1) na (2) ya Kanunu za Mahakama ya Kazi, Tangazo la Serikali Na. 106 la 2007 inaruhusu mahakama kutumia lugha ya Kiswahili au Kiingereza katika kuandika hukumu zake basi nimeona ni vyema nitumie Kiswahili katika kuandika hukumu hii ili kuwawezesha wadaawa kuisoma na kuielewa hukumu hii kwa ufasaha zaidi. 3 Katika mawasilisho yake mwakilishi wa mleta maombi aliachana na sababu ya kwanza ya marejeo na kuwasilisha katika sababu zilizobaki. Alieleza kuhusiana na sababu ya pili kwamba, mwamuzi alikosea kisheria na kiuhalisia kwa kuamua kuwa, mleta maombi hakuwa na sababu za msingi za kumwachisha kazi mjibu maombi kwa sababu mjibu maombi hakuhitaji cheti cha kidato cha nne kupata ajira yake. Alieleza zaidi kuwa, mwamuzi alikosea kuamua kwamba cheti hicho cha kidato cha nne hakikuwasilishwa na mjibu maombi bila kuzingatia kwamba, mfanyakazi anaweza kujiendeleza wakati wowote na kuwasilisha cheti chake kwa mwajiri. Ilielezwa zaidi na mwakilishi wa mleta maombi kwamba, mwamuzi hakuzingatia ushahidi uliotolewa na DW1 ambao ni kielelezo D2, barua ya mjibu maombi akiomba kubadilishiwa kazi toka kuwa mlinzi kuwa M % fundi umeme na kujibiwa kuwa ni lazima awe na elimu ya kidato cha nne, kielelezo D3 ambacho ni cheti cha usomaji mita na cheti cha kidato cha nne ambavyo vyote vilihakikiwa na kupokelewa na Afisa Rasilimali Watu kwa mujibu wa utaratibu uliokuwepo katika ofisi ya mleta maombi. Alieleza pia kuwa kielelezo hicho D3 kilikuwa na namba ya ajira R. 955 ambayo mjibu maombi alikiri kuwa ni namba yake. 4 Katika sababu ya tatu ilielezwa na mwakilishi wa mleta maombi kwamba, muamuzi alikosea kisheria na kiuhalisia kuamua kuwa mleta maombi alikuwa na wajibu wa kufanya uchunguzi wa uhalali wa cheti cha mjibu maombi. Kama ilivyoelezwa na DW1 katika ushahidi wake, kuwa zoezi la kutambua uhalali wa vyeti lilifanywa na mamlaka husika kama ilivyoagizwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Baada ya kurejesha majina ya wenye vyeti vya kughushi akiwemo mjibu maombi alikata rufaa bila mafanikio kama inavyoonekana katika vielelezo D5 na D6. < Aliendelea kuwasilisha kuwa, jukumu la kuchunguza uhalisia wa J cheti hicho halikuwa la mleta maombi kwa kuwa hana utalamu wala mamlaka ya kuchunguza vyeti vya kitaaluma. Kwamba, kwa kuamuru mjibu maombi arejeshwe kazini, ni kama mwamuzi alithibitisha kuwa cheti hicho ni halali wakati hana mamlaka wala ujuzi wa kufanya hivyo. Alimalizia kwa kuiomba mahakama izingatie na kukubali maombi yao. Kwa upande wake mjibu maombi, mwakilishi wake aliiomba mahakama ikubali kiapo kinzani alichoapa yeye kiwe sehemu ya mawasilisho yake. Alieleza katika sababu ya pili ya marejeo kwamba, mwamuzi alikuwa sahihi katika kuamua kwamba mjibu maombi 5 aliachishwa kazi isivyo halali. Alieleza kuwa mwamuzi alizingatia ushahidi uliotolewa mbele ya Tume na aliamua shauri lake kwa mujibu wa sheria. Katika hoja ya tatu mwakilishi wa mjibu maombi alieleza kwamba sababu hiyo haina mashiko kwa sababu, mleta maombi alikuwa na wajibu wa kuchunguza nyaraka zote za mjibu maombi kwa wakati. Alieleza pia kuwa uamuzi wa kumrejesha kazini mjibu maombi ulitolewa na mwamuzi kwa mujibu wa sheria na sio vinginevyo. Mwisho aliiomba mahakama itupilie mbali maombi haya kwa gharama. Baada ya kupitia maelezo ya pande zote mbili pamoja na f ■ kumbukumbu za shauri toka tume, mahakama imeona kuwa hoja za kuamuliwa katika maombi haya ni kama zifuatavyo:- i. Endapo muamuzi alizingatia ushahidi uliotolewa na wadaawa Hi katika kufikia uamuzi kuwa mjibu maombi hakuachishwa kazi kihalali. % ii. Nini nafuu ya kila upande. Katika kujibu hoja ya kwanza, mahakama imeona Tume iliamua kuwa mleta maombi hakuwa na sababu za msingi za kumuachisha kazi mjibu maombi na mleta maombi hakufuata taratibu za kisheria katika kumwachisha kazi mjibu maombi. Mwakilishi wa mleta maombi 6 ameeleza kwamba, uamuzi huo haukuwa wa haki kwa kuwa mwamuzi hakuzingatia ushahidi uliotolewa na DW1 hasa vielelezo D2 na D3. Madai haya yalikanushwa na mjibu maombi kwa kueleza kwamba, uamuzi ulikuwa ni wa haki na maamuzi ya tume yalizingatia misingi ya kisheria. Ni msingi wa kisheria kwamba, ili uachishwaji kazi uwe ni wa % halali na haki, mwajiri anapaswa kuthibitisha kuwa alikuwa na sababu halali na ya haki ya kumuachisha kazi muajiriwa, na pia awe amefuata taratibu zilizoainishwa kisheria. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 37(2) cha sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini na kama ilivyosisitizwa na gr mahakama hii katika mashauri mbalimbali likiwemo shauri la Tanzania Railways Limited V. Mwinjuma Said Semkiwa, [2015] LCCD 3. Pamoja na mambo mengine mahakama ilieleza katika shauri hilo kwamba, ni msingi wa kisheria kuwa ili usitishwaji wa ajira uwe halali, ni % w 1 lazima kuwe na sababu halali na taratibu za usitishaji wa ajira zilizowekwa na sheria lazima zizingatiwe. Kama ilivyoelezwa mwanzoni mwa hukumu hii ni kwamba mjibu maombi alisitishiwa ajira yake kwa sababu ya kutenda kosa la kuwasilisha kwa mwajiri wake ambaye ni mleta maombi cheti cha kidato cha nne kilichoghushiwa. Mwakilishi wa mleta maombi alieleza ili kuthibitisha kosa hilo, shahidi wa mleta maombi aliyetoa ushahidi mbele 7 ya Tume kama DW1 alitoa kielelezo D2 ambacho ni barua ya mjibu maombi akiomba kubadilishiwa kada na kuwa fundi umeme, iliyoandikwa tarehe 15 Desemba, 1995. Alitoa pia kielelezo D3 ambavyo ni nakala ya cheti cha kidato cha nne kinachodaiwa kughushiwa kinachoonyesha kilitolewa mwaka 2007 pamoja na cheti cha Msoma Mita (meter Reader) kilichotolewa tarehe 28 Februari, 2001. Mwakilishi wa mleta maombi alieleza katika mawasilisho yake ..ft, kuwa, ushahidi huo wa mleta maombi haukuzingatiwa na mwamuzi katika uamuzi alioutoa. Baada ya kupitia tuzo ya Tume ambayo mleta maombi anaomba ifanyiwe marejeo na mahakama hii, mahakama 1 imeona kuwa mwamuzi alieleza sababu zilizomfanya afikie uamuzi wa kuona kuwa mleta maombi hakuwa na sababu halali ya kusitisha ajira ya mjibu maombi ni kuwa mleta maombi alishindwa kuthibitisha ni jinsi gani mjibu maombi alivyowasilisha cheti kinachodaiwa kughushiwa kwa mleta maombi na kama mpokeaji alihakiki uhalali wa cheti hicho kwa kutumia cheti halisi. Baada ya kupitia vielelezo hivyo mahakama imeona kuwa vielelezo hivyo ambavyo ni nakala za cheti cha kidato cha nne na cheti cha Msoma Mita vilipokelewa, kusainiwa na kugongwa muhuri na Afisa Rasilimali Watu wa mleta maombi mnamo tarehe 3 Januari, 2011 na 8 kuandikwa juu yake namba R.955 ambayo mjibu maombi alikiri katika ushahidi wake kuwa ni namba yake ya ajira akiwa kwa mleta maombi. Kwa hiyo mwamuzi alijipotosha kwa kueleza kuwa mleta maombi hakueleza ni kwa namna gani cheti hicho kinachodaiwa kughushiwa kuliwasilishwa na kupokelewa na mleta maombi na kuwa hakikuhakikiwa. Mahakama imeona shahidi wa mleta maombi, DW1 Ik alieleza katika ushihidi wake alioutoa mbele ya Tume kuwa mjibu maombi ndiye aliyewasilisha cheti hicho kwa mleta maombi na Wk W^ kilipokelewa tarehe 3 Januari, 2011 na kugongwa mhuri na kusainiwa na Afisa Rasilimali Watu wa mleta maombi kuthibitisha ni nakala ya cheti halisi. Kwa hiyo kama alivyoeleza mwakilishi wa mleta maombi katika O' mawasilisho yake ni kweli mwamuzi hakuzingatia ushahidi uliotolewa na DW1 mbele ya Tume. Mahakama imeona sababu nyingine aliyoitumia mwamuzi kufikia uamuzi unaobishaniwa mbele ya mahakama hii ni kuwa mjibu maombi hakutumia cheti hicho cha kidato cha nne kujipatia ajira aliyokuwa nayo. Mahakama hii inakubaliana na mwamuzi kuwa ni dhahiri kwamba mjibu maombi hakujipatia ajira aliyokuwa nayo kwa kutumia cheti hicho kinachodaiwa kughushiwa. Hii ni kwa sababu mjibu maombi aliajiriwa 9 mwaka 1991 kwa sifa ya kuwa na elimu ya darasa la saba na cheti kilichoghushiwa kinaonyesha ni cha mwaka 2007. Kama mwamuzi alivyoeleza kwa usahihi katika tuzo ya Tume, mjibu maombi haiingii katika kundi la watumishi waliopaswa kuwa na elimu ya kidato cha nne ndipo waajiriwe kwa sabau yeye aliajiriwa kabla ya Waraka namba 1 wa mwaka 2004 uliotolewa na Serikali kupitia . Menejiment ya Utumishi wa Umma uliotaka watumishi wote wa umma Jr , wawe na elimu ya kuanzia kidato cha nne, na kufafanuliwa kwa barua iliyotolewa na Menejimenti ya Utumishi wa Umma ya tarehe 10 Aprili, 2006. Hata hivyo Mahakama inaona kuwa Mwamuzi hakuwa sahihi kueleza katika uamuzi wake kuwa mjibu maombi aliachishwa kazi kwa sababu ya kutumia cheti kilichoghushiwa kujipatia ajira kwa mleta maombi. Badala yake Mahakama imeona kuwa, Pamoja na kuwa ni K W kweli mjibu maombi alishitakiwa kwa kosa la kughushi cheti cha kidato cha nne na kukitumia kujipatia ajira kwa mleta maombi lakini mhutasari wa kikao cha kamati ya nidhamu kilichosikiliza shauri lake pamoja na barua ya kusitisha ajira yake ya tarehe 15 Agosti, 2017 zinaonyesha mjibu maombi aliachishwa kazi baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kuwasilisha cheti cha kughushi kwa mleta maombi. io Kwa hiyo mjibu maombi hakuachishwa kazi kwa sababu ya kujipatia ajira kwa kutumia chetu kilichoghushiwa kama alivyoeleza mwamuzi bali kwa sababu ya kuwasilisha kwa mwajiri wake cheti kilichagundulika kuwa kimeghushiwa. Kosa hilo la kughushi linaangukia katika makosa yaliyoainishwa katika kanuni ya 12 (3) (a) ya Tangazo la Serikali Na. 42 la 2007 kuwa ni sababu ya haki inayokubalika kusitisha ajira ya mtumishi. Ikiwa hivyo ndivyo ilivyo na kwa kuwa mjibu maombi alieleza katika ushahidi wake na katika mawasilisho yake kuwa hakuwasilisha f % W cheti kinachodaiwa kughushiwa kwa mleta maombi, mahakama imeona suala la kuamua hapa ni kama cheti hicho ni cha mjibu maombi na ni yeye aliyekiwasilisha kwa mwajiri wake. Baada ya Mahakama hii kupitia mwenendo wa shauri la tume pamoja na kumbukumbu zake, imekuwa na maoni tofauti na ya mwamuzi kwamba, sio kweli kwamba hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa mjibu maombi ndiye aliyewasilisha kwa mleta maombi cheti hicho kinachodaiwa kughushiwa. Mahakama imekuwa na maoni hayo baada ya kuona kuwa hakuna ubishi wowote kutoka kwa mjibu maombi kuwa majina yaliyopo katika cheti hicho ya Ramadhani M. Mgaya ni majina yake. Aidha mahakama imeona pia kuwa hakuna ubishi wowote kuwa namba R.955 iliyoandikwa li juu ya cheti hicho ni namba ya utambulisho ya ajira ya mjibu maombi alipokuwa anaajiriwa na mleta maombi. Hayo yote pamoja na niliyoeleza hapo awali yanaifanya mahakama hii ione kuwa, pamoja na kuwa mjibu maombi alieleza kuwa cheti hicho sio chake na hajawahi kuandika barua ya kuwasilisha cheti hicho kwa mleta maombi lakini hakuna ushahidi wowote unaonyesha ni kwa vipi cheti hicho chenye majina yake na namba yake ya ajira kiliweza kufika kwa mwajiri wake na kuingizwa katika jalada lake la ajira tofauti na ilivyoelezwa na DW1 katika ushahidi wake kuwa mjibu maombi ndiye aliyekiwasilisha cheti hicho kwa mleta & Aidha pamoja na kuwa Kumbukumbu za Tume zinaonyesha mjibu maombi alieleza katika utetezi wake kuwa kulikuwa na mtumishi mwenzake aliyekuwa na majina kama ya kwake katika ofisi yao lakini huyo mtumishi hakuitwa kutoa ushahidi mbele ya Tume kuthibitisha hayo aliyoyasema mjibu maombi. Kwa maoni ya mahakama hii mjibu maombi alipaswa kuthibitisha mbele ya tume hayo aliyoyasema kama inavyoelezwa katika kifungu cha 110 cha Sheria ya Ushahidi, Sura ya 6, Marejeo ya Mwaka 2019. Kwa kushindwa kufanya hivyo kunaifanya mahakama ione kuwa mjibu maombi hakuweza kuthibitisha mbele ya Tume kuwa cheti hicho sio cha kwake na kuwa kiliwasilishwa kwa mleta 12 maombi na mtu mwingine na kuweka katika jalada lake la ajira kwa makosa kama alivyoeleza. Hayo yote yanaifanya mahakama hii ione kwamba, ushahidi uliotolewa mbele ya Tume na shahidi wa mleta maombi, DW1 na kuungwa mkono na vielelezo vilivyotajwa hapo juu vilitosha kuonyesha kwamba mleta maombi alitimiza jukumu lake la kuthibisha uhalali wa sababu ya kusitisha ajira ya mjibu maombi, kwa uzani wa uwezekano kama alivyoelezwa katika kifungu cha 39 cha sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini kikisomwa pamoja na kanuni ya 9 (3) ya Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini (kanuni za utendaji bora), Tangazo la Serikali Na. 42 la 2007. Kuhusu kuzingatiwa au kutokuzingatiwa kwa utaratibu wa kusitisha ajira ya mjibu maombi, mahakama imeona mwamuzi alieleza katika tuzo inayobishaniwa mbele ya mahakama hii kwamba, utaratibu uliopaswa kufuatwa kisheria kama ulivyoelezwa katika kanuni ya 13 (1) • .V ya Tangazo la Serikali Na. 42 la 2007 haukuzingatiwa na mleta maombi katika kusitisha ajira ya mjibu maombi. Mwamuzi alieleza kwamba mleta maombi alishindwa kufanya uchunguzi kuona kama cheti kinachodaiwa kughushiwa kilikuwa cha mtumishi wao mwingine mwenye majina sawa na ya mjibu maombi na kiliwekwa katika jalada la mjibu maombi kwa 13 makosa au la na taarifa ya uchunguzi huo apewe mjibu maombi kabla shauri lake kuanza kusikilizwa na kamati ya nidhamu. Mahakama imejaribu kutafakari hoja ya mwamuzi katika kufikia uamuzi wake na kuona alijipotosha kwa kueleza kuwa kanuni ya 13 (1) ya Tangazo la Serikali Na.42 la 2007 haikuzingatiwa kabla ya kusitisha ajira ya mjibu maombi. Mahakama imeona hivyo baada ya kuona kanuni hiyo inataka mwajiri afanye uchunguzi na kujiridhisha kama kuna sababu ya haki ya kuanzisha usikilizaji wa shauri la nidhamu dhidi ya mtumishi anayetakiwa kusitishiwa ajira yake. Mahakama imeona kama It ilivyoelezwa na mwakilishi wa mleta maombi katika maombi haya, ni kwamba uchunguzi wa kughushiwa kwa cheti kilichosababisha ajira ya mjibu maombi isitishwe ulifanywa na Tume ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taarifa yake kuwasilishwa kwa mleta maombi na mjibu ■ ■ 4; maombi alipata nakala yake ndiyo sababu alikata rufaa dhidi ya uchunguzi huo japo rufaa yake haikufanikiwa. Kwa mazingira hayo mahakama imeona sababu ya kuanzishwa usikilizwaji wa shauri la nidhamu dhidi ya mjibu maombi ilikuwa inajulikana na hakukuwa na sababu ya kufanya uchunguzi mwingine ili kuona kama kulikuwa na sababu ya kuanzisha usikilizaji wa shauri lake kwa sababu uchunguzi wake ulikuwa tayari umeshafanywa na Tume ya 14 Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Mahakama imeona hoja ya mwamuzi kwamba mleta maombi alipaswa kufanya uchunguzi kujiridhisha kama cheti hicho sio cha mtumishi mwingine aliyekuwa na majina yanayofanana na majina ya mjibu maombi haikuwa na mashiko kwa sababu hoja hiyo ilipaswa kuthibitishwa kwa kutolewa ushahidi mbele ya kamati ya nidhamu na sio kufanyiwa uchunguzi na mleta maombi kabla ya usikilizwaji wa shauri lake haujaanza. Kuhusu mashauri aliyoyatumia mwamuzi kufikia uamuzi aliufikia % mahakama hii haikuweza kupata nakala zake ili iweze kuyapitia kuona kama kilichakuwa kinazungumziwa katika mashauri hayo kinafanana na kinachozungumziwa katika shauri hili. Aidha mahakama imeona pia kuwa haifungwi na kilichazungumziwa katika maamuzi hayo kwa sababu ni maamuzi ya Mahakama Kuu na mazingira ya kesi hizo ni tofauti na mazingira ya kesi iliyoko mbele ya mahakama hii. Kwa kusema hivyo mahakama inaona hakuna uthibitisho wa kuwa utaratibu wa kisheria uliopo katika kanuni ya 13 (1) ya Tangazo la Serikali Na. 42 la 2007 kuhusu usikilizaji wa shauri la nidhamu na usitishaji wa ajiri ya mjibu maombi ulikiukwa na mleta maombi. Kuhusiana na nafuu ambazo wadaawa wanastahili katika shauri hili mahakama imeona kwamba mjibu maombi aliomba katika CMA Fl 15 kuwa arejeshwa kazini na alipwe malimbikizo ya mishahara ya mwezi Mei hadi Agosti, 2017 pamoja na likizo za mwaka 2016 na 2017 na Tume ilimkubalia ombi lake la kurejeshwa kazini. Kwa kuwa mahakama imejiridhisha kuwa usitishwaji wa ajira ya mjibu maombi ulikuwa kwa sababu inayokubalika kisheria na taratibu za kisheria zilizingatiwa katika kusitisha ajira yake, mahakama inaona kuwa amri ya kuwa mjibu maombi arejeshwa kazini haiwezi kuwa tena nafuu ya haki anayostahili mjibu maombi. Kwa sababu hizo tajwa hapo juu, mahakama imeridhika kuwa maombi ya mleta maombi yana mashiko na yanastahili kukubaliwa. Kwa hiyo tuzo iliyotolewa na Tume inatenguliwa na amri ya kuwa mjibu maombi arejeshwe kazini inatenguliwa. Mahakama hii anaagiza kama mjibu maombi hakulipwa malimbikizo ya mishahara yake ya mwezi Mei CMA Fl alipwe stahili hizo. Imasainiwa hapa Dar es salaam leo tarehe 20 mwezi Agosti, 2021. I. ARUFANI JAJI 20/08/2021 16 Mahakama: Hukumu hii imesomwa leo tarehe 20 mwezi wa Agosti, 2021 akiwepo Luciana Benedict, Mwakilishi wa Mleta Maombi ni akiwepo Mjibu Maombi mwenyewe. Haki ya kukata rufaa kwenda Mahakama ya Rufani imeelezwa kwa wawakilishi wa wadaawa. 17