registered trustees of evangelical lutheran church in tanzania morogoro diocese vs simoni h loko and wengineo 2021 tzhcld 136 4 juni 2021
The employees' joint claim was properly instituted as per the applicable regulations. The employer failed to prove that the termination was substantively and procedurally fair, as the employees were terminated before the expiry of the period given to comply with the employer's directive, and disciplinary procedures...
Source-derived case information.
- Citation
- registered trustees of evangelical lutheran church in tanzania morogoro diocese vs simoni h loko and wengineo 2021 tzhcld 136 4 juni 2021
- Parties
- Applicant: The Registered Trustees of Evangelical Lutheran Church in Tanzania, Morogoro Diocese; Respondent 1: Simoni H. Loko; Respondent 2: William Mitimingi; Respondent 3: Japhet Gogo; Respondent 4: Peter Makala; Respondent 5: Hosea Mmbaga; Respondent 6: Ezekiel Lukanda
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2021
- Procedural Posture
- Labour Revision (consolidated) / Judgment After Hearing of Consolidated Revision Applications
- Outcome
- Partly allowed; revision applications granted to the extent discussed.
- Legal Topics
- Unfair Termination, Procedural Fairness in Dismissal, Remedies for Unfair Dismissal, Representative Suits in Labour Disputes, Internal Dispute Resolution Procedures
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
The Registered Trustees of Evangelical Lutheran Church in Tanzania, Morogoro Diocese
Applicant
Simoni H. Loko
Respondent 1
William Mitimingi
Respondent 2
Japhet Gogo
Respondent 3
Peter Makala
Respondent 4
Hosea Mmbaga
Respondent 5
Ezekiel Lukanda
Respondent 6
Procedural Posture
Labour Revision (consolidated) / Judgment After Hearing of Consolidated Revision Applications
Legal Issues
- 1 Whether the representative suit by employees was properly instituted before the Commission
- 2 Whether the termination of employment was substantively and procedurally fair
- 3 What remedies are appropriate for each party
Ratio Decidendi
The employees' joint claim was properly instituted as per the applicable regulations. The employer failed to prove that the termination was substantively and procedurally fair, as the employees were terminated before the expiry of the period given to comply with the employer's directive, and disciplinary procedures were not followed. The appropriate remedy is compensation for unfair termination, not reinstatement, due to the breakdown of the employment relationship. The award of 14 months' salary was improper and is set aside; other awards remain.
Court Disposition
Partly allowed; revision applications granted to the extent discussed.
Orders
- Award of 14 months' salary set aside.
- Awards of 24 months' salary as compensation, severance pay, and one month's salary in lieu of notice upheld.
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ILIYOKETI MOROGORO SHAURI LA MAREJEO LILILOUNGANISHWA NA. 28 NA 36 LA 2020 BAINA YA THE REGISTERED TRUSTEES OF EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA, MOROGORO DIOCESE......................... MLETA MAOMBI NA SIMONI H. LOKO............................................................... MJIBU MAOMBI NA. 1 WILLIAM MITIMINGI........................................................ MJIBU MAOMBI NA. 2 JAPHET GOGO..................................................................... MJIBU MAOMBI NA. 3 PETER MAKALA.................................................................. MJIBU MAOMBI NA. 4 HOSEA MMBAGA................................................................MJIBU MAOMBI NA. 5 EZEKIEL LUKANDA............................................................ MJIBU MAOMBI NA. 6 HUKUMU Tarehe ya mwisho ya Amri: 25/05/2021 Tarehe ya Hukumu: 04/06/2021 A.E. MWIPOPO, J. The Registered Trustees of Evangelical Lutheran Church in Tanzania, Morogoro Diocese (Wadhamini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Morogoro) (ambaye katika shauri hili atajulikana kama mwajiri) na Simon H. Loko, William Mitimingi, Japhet Gogo, Peter Makala, Hosea Mmbaga na Ezekiel Lukanda (ambao katika shauri hili watajulikana kama waajiriwa) wameleta mashauri ya Marejeo kuomba Mahakama irekebishe uamuzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi katika mgogoro wa kik'azi Na. i CMA/MORO/66/2019 wa tarehe 25 Mei, 2020, uliotolewa na Mhe. Kiobya Z., Muamuzi. Simon H. Loko, William Mitimingi, Japhet Gogo, Peter Makala, Hosea Mmbaga na Ezekiel Lukanda waliajiriwa katika nafasi ya Uchungaji na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Morogoro. Mnamo tarehe 06 Aprili, 2019 ajira yao ilisitishwa na mwajiri kwa sababu za kinichamu. Waajiriwa hao hawakuridhika na kuachishwa kazi, hivyo walifikisha mgogoro wao Mbele ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (hapa itajulikana kama Tume). Tume iliona uachishwaji kazi wa Wajibu Maombi haukuwa halali na wa haki. Uamuzi huo wa Tume haukuwaridhisha pande zote na kila mmoja alifungua shauri la marejeo mbele ya Mahakama hii. Mwajiri alifungua shauri la marejeo namba 28 la 2020 na waajiriwa walifungua shauri namba 36 la 2020. Kufuatia maombi ya pande zote mbili kuwa mashauri hayo yaunganishwe ill yasikilizwe kwa pamoja, Mahakama illtoa amri ya kuyaunganisha mashauri haya ili yasikilizwe pamoja mnamo tarehe 25 Mei, 2021. Katika shauri Na. 28 la 2020 mwajiri alikuwa na hoja 6 za kuomba marejeo zilizotokana na uhahidi. Hoja hizo ni kama zifuatazo:- 1. Iwapo Muamuzi alikuwa sahihi kuamua kuwa kulikuwa na shauri la uwakilishi lililo sahihi mbele ya Tume. 2 2. Iwapo Muamuzi alikwa sahihi kuona kuwa ana mamlaka ya kusikiliza mgogoro wa kidini kabla ya waajiriwa hawajamaliza taratibu za ndani. 3. Iwapo Muamuzi alikuwa na mamlaka ya kisheria ya kutoa tuzo ambazo hazikuwa zimeombwa katika fomu Na. 1 ya Tume, hazikuwahi kusuluhishwa na hazikuwa sehemu ya hoja zinazobishaniwa zilizotengenezwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi na Tume. 4. Iwapo Muamuzi alikuwa sahihi kuwapa waajiriwa tuzo ya malipo ya mishahara ya miezi 14 ya wakati ambao shauri lilikuwa linaendelea kusikilizwa mbele ya Tume baada ya kuwa aliwapa fidia ya miezi 24 kwa uachishwaji kazi usio halali. 5. Iwapo Muamuzi alikuwa sahihi kukokotoa tuzo kwa kuegemea katika mishahara ambayo haikuthibitishwa kwa ushahidi mbele ya Tume. 6. Iwapo Muamuzi aliuchambua vizuri ushahidi uliopo katika rekodi ill kufikia hitimisho kuwa sababu na taratibu za uachishwaji kazi zilikuwa sio halali na za haki. Katika shauri Na. 36 la 2020 waajiriwa walikuwa na hoja 5 za kisheria za kuomba marejeo zilizotokana na ushahidi. Hoja hizo ni kama zifuatazo:- 3 i. Kwamba, Muamuzi alikosea kisheria na kiushahidi kwa kushindwa kutoa nafuu ya kurudishwa kazini kama ilivyoombwa na waajiriwa katika fomu Na. 1 ya Tume. ii. Kwamba, Muamuzi alikosea kisheria na kiushahidi kwa kushindwa kutolea uamuzi juu ya hoja ya udhalilishaji na ubaguzi ambazo zilikuwa miongoni mwa hoja zinazobishaniwa ziliyotengenezwa na Tume kama hoja Na. 3 na 4. ill. Kwamba, Muamuzi alikosea kisheria na kiushahidi kwa kushindwa kurekodi vizuri na kuchambua ushahidi kuhusiana na malipo ya mwezi ya waajiriwa. iv. Kwamba, Muamuzi alikosea kisheria na kiushahidi kwa kushindwa kuzingatia muda uliobaki kutoka tarehe waliyoachishwa kazi hadi tarehe kila mmoja aliyotarajia kustaafu kabla ya kutoa amri ya kulipwa fidia kwa miezi 24 tu. v. Kwamba, Muamuzi alikosea kisheria na kiushahidi kwa kushindwa kutoa amri kwa waajiriwa kulipwa shilingi 1,581,467,000/= ambayo ni sawa na malipo yao kwa miezi 98, 167, 87, 274, 353 na 237 kwa ajili ya mwajiriwa wa kwanza hadi wa sita kwa mpangilio huo. Wakati wa usikilizwaji wa shauri hili lililounganishwa, pande zote mbiii zilikuwa zinawakilishwa na mawakili. Mwajiri alikuwa anawakilishwa na Bw. 4 Marwa Masanda, Wakili, na waajiriwa walikuwa wakiwakilishwa na Bw. Baraka Lweyeka, Wakili. Akifanya mawasilisho ya kuunga mkono marejeo Na. 28 la 2020 Wakili wa mwajiri alieleza kwamba Tume ilikosea kuona mgogoro uliokuwa mbele ya Tume unakidhi vigezo vya uwakilishi kwa sababu ulikiuka masharti ya kifungu cha 86(1) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini, Sura ya 366 kama ilivyorejewa mwaka 2019. Alieleza kuwa sheria inaelekeza mashauri yote yafunguliwe kwa kupitia fomu na. 1 ya Tume lakini Fomu iliyowasilishwa mbele ya Tume ilikuwa na jina moja tu la Simon H. Loko. Aidha, fomu hiyo haikuonyesha majina ya watu wengine. Kanuni ya 5(2) na (3) ya Kanuni za Taasisi ya Kazi (Uamuzi na Usuluhushi), Tangazo Na. 64 la 2007 inaelekeza kwamba kama mwajiriwa zaidi ya mmoja hajaridhika na uamuzi wanaweza kumpa kibali mmoja wao kufungua shauri kwa niaba yao. Katika fomu Na. 1 kuna kiambatisho kilichosainiwa na waajiriwa wengine ambacho kimeondoa maneno awe mwakilishi wetu. Kwa sababu hiyo, waajiriwa wengine walimruhusu Simon Loko kuweka sahihi katika nyaraka za kufungua mgogoro na sio kuwawakilisha. Kwa kuwa hakuna kibali cha moja kwa moja cha kuwawakilisha waajiriwa wengine haikuwa sahihi kwa Tume kusikiiiza na kupokea ushahidi wa waajiriwa wengine. Hivyo, hakukuwa na shauri la s uwakilishi lililofunguliwa. Hata tuzo zilizotolewa hazikuwa halali kwani hawakuwa na mgogoro walioufungua mbele ya Tume. Wakili wa mwajiri alieleza kuwa hoja yao ya pili ya Marejeo ni kuwa Msuluhishi alikosea kuendelea na usuluhishi wakati taratibu za ndani za utatuzi wa mgogoro hazikuwa zimekamilika. Pamoja na kuwa sio lazima kukamilisha taratibu za ndani, lakini pale zinapokuwepo taratibu hizo ni vizuri zikafuatwa kwanza. Mgogoro huu unahusisha taasisi ya kidini kati ya kanisa na wachungaji wake. Waumini wanatarajia wapate muongozo kutoka kwa viongozi na haitarajiwi kuwepo kwa mgogoro baina yao. Uwepo wa mgogoro unapunguza uaminifu wa waumini kwa kanisa. Kama Dayosisi bado kulikuwa na nafasi kwa mkutano mkuu kumaliza mgogoro huo, pamoja na msajili wa vyama vya kijamii. Hivyo wanaona mgogoro ulifunguliwa mapema kabla ya kumaliza taratibu zilizopo za usuluhishi. Katika hoja ya tatu ya marejeo, Wakili wa mwajiri aliwasilisha ya kwamba Tume haikuwa sahihi kutoa tuzo ambazo hazikuombwa katika fomu Na. 1 ya Tume. Katika fomu hiyo, waajiriwa waliomba kurudishwa kazini bila masharti, kulipwa haki za kiutumishi na kulipwa fidia. Tume iliwapatia waajiriwa hao tuzo ya fidia ya kuachishwa kazi isivyo halali, mshahara wa miezi 14, malipo ya taarifa ya kuachishwa kazi, na kiinua mgongo. Hivyo vyote havipo katika fomu Na. 1 ya Tume. Tuzo zilizotolewa hazikuwa zimesuluhishwa na usuluhishi wa malipo hayo haukushindikana. 6 Tuzo hizo pia hazikuwa sehemu ya viini vya mgogoro mbele ya Tume. Hivyo, tuzo hizo zilitolewa kimakosa na Tume. Mahakama ilikuwa na msimamo kama huo katika kesi ya Barclays Bank (T) Ltd dhidi ya Jacob Muro, Rufaa ya Madai Na. 357 ya 2019, Mahakama ya Rufaa, iliyoketi Mbeya. Pale ushahidi utakaotolewa ukiwa kinyume na nyaraka za wadaawa (pleadings) basi ushahidi huo haupewi uzito na unafutwa. Tume ilitakiwa ijielekeze katika maelezo yaliyotolewa katika nyaraka zao (pleadings) na si vinginevyo. Wakili wa mwajiri alieleza katika hoja ya nne ya marejeo kuwa Muamuzi alikosea kutoa tuzo ya mshahara wa miezi 14 ya kipindi kesi ilikuwa mbele ya Tume wakati ameshawapa fidia ya miezi 24. Hivyo ni wazi Muamuzi alitafsiri vibaya kifungu cha 40 cha sheria ya Ajira na Mahusiano kazini, Sura ya 366 ya Sheria kama Ilivyorekebishwa mwaka 2019. Kifungu hiki kinampa mamlaka ya kutoa tuzo kwa mwajiriwa aliyekuwa anadai wakati akiwa katika utumishi wake lakini mishahara ya miezi 14 inalipwa baada ya ajira yao kuwa imesitishwa. Malipo haya sio sahihi kwa kuwa tayari walishapewa fidia ya miezi 24. Hivyo tuzo hii haikuwa halali. Sababu ya tano ya marejeo ni kuwa Muamuzi alitoa fidia ya mshahara kwa kigezo cha mshahara ambao haukuwasilishwa au kuthibitishwa mbele ya Tume. Wakili wa mwajiri alielezea kuwa hakuna shahidi aliyeeleza mishahara ya waajiriwa. Kiasi cha mishahara yao 7 kinaonekana wakati wa maswali ya dodoso ya Muamuzi ambayo yaliulizwa baada ya mwajiri kuwa ameshauliza maswali yao ya dodoso. Maswali hayo hayakuwa sahihi na kinyume cha sheria kwa kuwa yalileta ushahidi mpya ambao haupo katika ushahidi wa msingi au maswali ya dodoso. Muamuzi alitakiwa kupata ufafanuzi wa hoja zenye utata. Wakili alirejea Kesi ya Barclays Bank (T) Ltd dhidi ya Jacob Muro ambayo imenukuliwa. Sio kazi ya Mahakama kufanya uchunguzi wa ushahidi ambao haujatolewa. Mahakama ilitakiwa iwaeleze wadaawa washinde kwa hoja na ushahidi. Hivyo, Tume ilikuwa na upendeleo katika Uamuzi husika kwani Mwajiri hakusikilizwa katika jambo hilo la Mshahara. Sababu ya mwisho, Wakili alieleza kuwa ushahidi uliotolewa mbele ya Tume unathibitisha kuwa kulikuwa na sababu za msingi za kuwaachisha kazi Wajibu Maombi na taratibu zilifuatwa. Ushahidi unaonyesha kuwa waajiriwa wote walisema kuwa hawapo tayari kufanya kazi na Askofu ambaye ndiye mkuu wao wa kazi. Na wakasisitiza kuwa lazima ajiuzulu kwa sababu hawayatambui mamlaka yake. Mazingira hayo yalikuwa hayawezi kuwafanya warudi kazini kwa kuwa mgogoro ungeendelea. Hivyo, Tume ilikuwa sahihi kuona kuwa suala la kuwarudisha kazini lisingewezekana kwa kuwa walitaka Askofu ajiuzulu na hawakuwa tayari kufanya naye kazi. Aliendelea kueleza kuwa taratibu za kuwaachishwa kazi waajiriwa zilifuatwa na hivyo Muamuzi alikosea kuona kuwa taratibu hazikufuatwa. 8 Waajiriwa walipewa nafasi ya kufuta kauli yao kuwa hawapo tayari kufanya kazi na askofu lakini walikataa. Hivyo wanaona kuwa mwajiri alithibitisha sababu za kuwaachisha kazi na taratibu zilifuatwa. Wakili wa Mwajiri aliomba Mahakama iyakubali Marejeo haya na kutupilia mbali mwenendo na uamuzi wa Tume. Akijibu mawasilisho ya mwajiri, Wakili wa waajiriwa alieleza kuwa kanuni ya 5(2) na (3) ya Kanuni za Taasisi za Kazi (Usuluhishi na Uamuzi), Tangazo la Serikali Na. 64 la 2007, inaeleza kuwa waajiri wanaweza kufungua kwa pamoja shauri mbele ya Tume. Hivyo, shauri la pamoja sio sawa na shauri la uwakilishi (representative suit) katika Sheria ya Mwenendo wa Madai. Hakuna sehemu yoyote waajiriwa walieleza kuwa wana shauri la uwakilishi. Kanuni tajwa zinatoa fursa kwa mtu au watu wenye maslahi yanayofanana kusaini nyaraka kwa niaba ya wenzake. Sharti linalowekwa katika kanuni ni kuwa wanaosainiwa wanapaswa kuweka majina yao kuonyesha kuwa wamempa kibali mmoja wao kufungua shauri la pamoja. Sharti la pili ni kuwa orodha hiyo iwekwe pamoja na fomu na. 1 ya Tume. Waajiriwa walitekeleza vigezo vyote hivyo. Majina yalikuwepo na yalisainiwa na orodha hiyo iliambatanishwa pamoja ya fomu ya CMA Na. 1 pia upande wa pili walipewa. Ukurasa 6 wa Fomu Na. 1 inaonyesha majina ya waajiriwa wote na tarehe zao za kuajiriwa. 9 Hivyo vyote vimetosha kuthibitisha kuwa waajiriwa walifungua shauri la pamoja. Wakili alieleza kuwa maneno yaliyokatwa kuhusu kuwakilishwa ni kwa sababu walimpa Simon Loko mamlaka ya kusaini nyaraka zao na sio kuwawakilisha mbele ya Tume. Hivyo walitumia haki yao kutafuta mwakilishi wanayemtaka katika shauri hilo. Mwajiri sio kazi yake kuwapangia nani wa kuwawakilisha waajiriwa. Kuhusu hoja ya pili ya mwajiri, Wakili wa waajiriwa alieleza kuwa hakuna sheria au kitu chochote kinachoelezwa kuwa ni lazima wamalize taratibu za ndani za kanisa. Biblia ambayo ni kielezo Cl kinatambua uwepo wa Mahakama na waumini wanafundishwa hivyo. Waajiriwa walimaliza taratibu zote za ndani za kanisa katika kudai haki zao. Waliachishwa kazi na Halmashauri Kuu ya Dayosisi ambacho ni chombo cha juu Kabisa kama katiba ya Dayosisi - kielelezo C2 na mwongozo wa utendaji wa kanisa - kielelezo C3 vinavyoonyesha. Kanuni ya XI C (3) na (14) ya kielelezo C2 inaeleza kuwa Halmashauri Kuu itapokea rufaa kutoka katika Halmashauri ya Utendaji. Na kuwa Halmashauri Kuu itafanya Uamuzi kwa niaba ya Mkutano Mkuu. Kifungu cha 10(7) (b) cha kielelezo C3 kinaeleza kuwa maamuzi ya Halmashauri Kuu katika masuala ya ajira ndio maamuzi ya mwisho. Hivyo hakukuwa na nafasi nyingine yoyote ya kukata rufaa kwa io mjibu wa taratibu za kanisa. Hili liliungwa mkono na shahidi DW - Katibu Mkuu wa Dayosisi. Kuhusu hoja ya tatu ya Mleta Maombi kuwa nafuu zilizotolewa Tume hazikuombwa, Wakili alieleza katika fomu Na. 1 ya Tume waajiriwa waliomba pamoja na kulipwa fidia ya kuachishwa kazi waliomba walipwe haki za kiutumishi. Nafuu zote zilizotolewa na Tume ni haki za kiutumishi. Hivyo Tume ilikuwa sahihi kuzitoa. Na sio kweli kuwa wadaawa hawakuwapata nafasi ya kusikilizwa au katika ushahidi wao kusema mshahara wa waajiriwa ni shilingi ngapi. Msimamo wa kisheria uliopo katika kesi ya Barclays Bank (T) Ltd ambayo mwajiri ameinukuu kuwa wadaawa hubanwa na nyaraka zao (pleadings) ni sahihi lakini mazingira ya shauri hilo hayaendani na mazingira ya shauri hili. Kuhusu hoja ya nne ya mwajiri, Tume ilikuwa sahihi kutafsiri kifungu cha 40(2) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Sura 366 ya Sheria. Muamuzi alizingatia uzito wa makosa ya kimaudhui na kiutaratibu yaliyofanywa na mwajiri. Hivyo Tume ilikuwa sahihi kutoa tuzo hiyo, ingawa ombi la msingi la Wajibu Maombi ni kurudishwa kazini na bado wanaomba warudishwe kazini. Hoja ya tano ya mwajiri ni kuwa mishahara iliyotumika kupigia hesabu tuzo walizopewa haikutolewa ushahidi. Wakili alieleza kuwa hoja hiyo sio sahihi kwa sababu ushahidi ulitolewa kama rekodi inavyoonyesha. ii Muamuzi hakuwa na upendeleo na hoja hii haijawahi kutolewa mbele ya Tume au katika kiapo cha mwajiri. Hivyo anaomba hoja hiyo ya upendeleo ipuuzwe. Kuhusu mawasilisho kuwa Muamuzi alishindwa kuwarudisha kazini kwa sababu hawawezi kufanya kazi na Askofu, Wakili alieleza kuwa waajiriwa walieleza sababu kwanini hawapo tayari kufanya kazi na Askofu na kutaka Askofu ajiudhuru. Tuhuma walizotoa waajiriwa dhidi ya Askofu hazijawahi kukanushwa. Shahidi pekee wa mwajiri alikubali kuwa tuhuma hizo ni sahihi. Hivyo waleta maombi wapo tayari kufanya kazi na mamlaka halali. Hivyo hoja hii nayo haina mashiko. Kuhusu hoja ya sita iliyotolewa na mwajiri, Wakili alieleza hakukuwa na sababu yoyote iliyothibitishwa ya kuwaachisha kazi Waajiriwa. Barua za kuwaachisha kazi zilipokelewa kama kielelezo C4, C9, C14, C17, C20 na C23. Barua hizi zinaonyeshwa kuwa sababu ya kuwaachisha kazi ni kuvunja maadili. Na hakuna sababu nyingine inayoweza kuletwa baada ya hizi barua za kuachishwa kazi. Kuhusu utaratibu wa kuachishwa kazi, Wakili alieleza kuwa kanuni ya 13 ya Kanuni za Ajira na Mahusiano Kazini (Kanuni za Utendaji Bora) Tangazo la Serikali Na. 42 la 2007 inaeleza utaratibu unaotakiwa kufuatwa. Kanuni ya 13(1), (2), (3), (4), (5), (7), (8), (10) na (12) hizo hazikufuatwa kabisa na mwajiri. Shahidi wa mwajiri ambaye ni DW1 amekubaliana na 12 hayo kuwa hawakuwahi kupewa hati ya mashtaka wala onyo lolote. Waajiriwa walitakiwa kupelekwa kwanza katika Halmashauri ya wachungaji kwa mujibu wa kielelezo Cl ambayo ilipewa mamlaka ya kutunza (handle) mashauri yote ya watumishi wa kiroho. Pia adhabu za waliokuwa wanatenda kosa zilizotolewa kiubaguzi kwa kuwa katika waraka wa Baraza la Maaskofu wa Tanzania - kielelezo C8 Askofu wa Morogoro alikuwa mmojawapo ya maaskofu waliotia saini waraka huo na hawakuwahi kuchukuliwa hatua ambazo walichukuliwa Wajibu Maombi. Aidha, waajiriwa wengine ambao walishiriki kuandaa waraka huo hawakuchukuliwa hatua kama za waajiriwa hawa. Hivyo Wakili wa waajiriwa anaona kuwa mwajiri alishindwa kuthibitisha uhalali wa sababu na taratibu za kuwaachisha kazi. Baada ya kunaliza kujibu hoja za mwajiri, Wakili wa waajiriwa aliendelea kuwasilisha hoja za waajiriwa zilizopo katika Marejeo Na. 36 ya 2020. Katika hoja ya kwanza alieleza kuwa Muamuzi alikosea kutowarejesha waajiriwa kazini baada ya kuona kuachishwa kazi kwao hakukuwa kwa sababu halali na utaratibu haukufuatwa kinyume na kifungu cha 40(1) (a) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini. Kifungu cha 40(3) cha sheria hiyo kinatoa nafasi kwa mwajiriwa kuamua kumrudisha mfanyakazi kazini au kulipa fidia. Hivyo, Muamuzi alikosea kuamua kuwa kuwarejesha kazini kwa kuwa mazingira ya kazi yalikuwa yanaruhusu kwa waajiriwa kurudishwa kazini kwani hawakuwa na shida na mamlaka ya 13 mwaajiri na bado kulikuwa na uwezekeno wa mgogoro kutatulika. Hivyo wakili aliomba waajiriwa warejeshwe kazini na tuzo ya Tume irekebishwe. Katika hoja yao pili waajiriwa walieleza kuwa Tume haikutolea Uamuzi masuala ya udhalilishaji na ubaguzi. Tume iliona kuwa masuala haya yanafanywa na mtu binafsi hivyo haiwezi kuvitolea maamuzi. DW 1 hakueleza kuwa matendo hayo ni binafsi hivyo wanaomba suala hilo liangaliwe na kufanyiwa uamuzi. Hoja ya mwisho ya waajiriwa ni kuwa iwapo Mhakama haitatoa amri ya kurejeshwa kazini basi itoe fidia ya zaidi ya miezi 24 kuendana na uachishwaji kazi usio halali ambao ulifanyika. Waajiriwa walikuwa na mikataba ya kudumu na bado walikuwa na muda mrefu wa kufanya kazi kama kielelezo C2 na C3 vinavyoonyesha. Hivyo wanaomba walipwe fidia ya mishahara ya miezi iliyobakia hadi kustaafu kwao ambayo jumla yake ni shilingi 1,581,467,000/= ambayo itagawanywa kwa miezi iliyobakia kabla ya kustaafu kwa kila mmoja. Akifanya mawasilisho ya nyongeza, Wakili wa mwajiri alirudia mawasilisho yake ya msingi (submission in chief). Aidha, alisisitiza kuwa kielelezo C2 katika kanuni ya X(c)(4) kinaipa Mkutano Mkuu mamlaka ya kusikiliza rufaa zote zitakazowasilishwa. Na hivyo hivyo katika kielelezo C3 kanuni ya 10(6) inasema rufaa itakatwa kwenda ngazi ya juu. Kuhusu kutokuwa tayari kufanya kazi na Askofu na kuwa Askofu hayupo kihalali 14 halikuwa jambo lililowasilishwa kwa Uamuzi mbele ya Tume. Aidha, kuhusu utaratibu wa mgogoro wa viongozi wa kiroho kusuluhishwa kwanza na Halmashauri ya wachungaji wakili alieleza kuwa huo sio utaratibu sahihi kwa kuwa katiba ya Kanisa na Mwongozo wa Utawala unaeleza kuwa majukumu ya Halmashauri ya Wachungaji ni kutunza mashauri na sio kusuluhisha. Wakili wa mwajiri akaendelea kujibu hoja zilizowasilishwa na waajiriwa kuwa Muamuzi alikuwa sahihi kuona kuwa haiwezekani kuwarudisha kazini waajiriwa kwa sababu hawako tayari kufanya kazi na Askofu. Kuhusu kifungu cha 40(3) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini kifungu hiki kinatumika pale ambapo tayari Tume au Mahakama inaamuru arudishwe kazini na mwajiri hayupo tayari kuwarejesha. Aidha kuhusu udhalilishaji na ubaguzi kutofanyiwa kazi na Tume, Wakili alikuwa na maoni kuwa waajiriwa waliomba kusikilizwa kwa udhalishaji wa fidia yake ambazo sio masuala ya kazi. Hivyo, Tume haina Mamlaka ya kusikiliza mashauri ya udhalilishaji. Na kuhusu kuomba fidia ya miezi iliyobaki ya mikataba yao, wakili alieleza kuwa hakuna ushahidi wa kuonyesha kuwa mikataba yao ya ajira ilikuwa ya kudumu. Hakuna ushahidi kuonyesha ajira yao ilianza lini na itaisha lini. Hivyo, hakuna msingi wa kujua muda wao wa kustaafu au mwisho wa mkataba wao. 15 Akifanya mawasilisho ya nyongeza ya waajiriwa, Wakili alieleza Tafsiri ya kifungu cha 40(3) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Sura ya 366 Marekebisho ya 2019 ni kuwa sio jukumu la Muamuzi kuamua kuwa mazingira ya kumrudisha kazini mwajiriwa yanaruhusu au la. Aidha, Tume ilikuwa na mamlaka ya kusikiliza na kuamua masuala ya udhalilishaji na ubaguzi. Fomu Na. 1 inaonyesha kuwa Tume inaweza kushughulikia suala hilo pale linapotokea kwenye mazingira ya kazi. Mwisho Wakili alieleza ya kwamba, kuhusu hoja ya kwamba waajiriwa walikuwa katika ajira ya kudumu au la hili lipo katika ushahidi wa DW1. Tarehe ya kuanza ajira inaonyeshwa katika fomu Na. 1 ya CMA. Umri wa kustaafu wa waajiriwa unaonyeshwa kwenye vielelezo C2 na C3. Hivyo, hesabu ya muda uliobakia inaweza kufanyika. Baada ya kusikiliza Mawasilisho ya pande zote naona kuwa hoja tatu zinazobishaniwa katika Marejeo haya ambazo Mahakama inabidi izitolee uamuzi. Hoja hizo ni kama zifuatazo; - i) Iwapo shauri la uwakilishi (representative suit) la waajiriwa lilikuwa limefunguliwa kwa usahihi mbele ya Tume. ii) Iwapo uachishwaji kazi wa waajiriwa ulikuwa halali na wa haki kisababu na kiutaratibu. iii) Nini ni nafuu za kila upande. 16 Katika kujibu hoja ya kwanza, wakili wa mwajiri alieleza kuwa Tume ilikosea kwa kuona shauri hili linakidhi vigezo vya uwakilishi kwa sababu lilikiuka masharti ya kifungu cha 86(1) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini, Sura ya 366 ya Sheria, kama ilivyorejewa ya 2019. Wakili alieleza kuwa sheria inaelekeza mashauri yote yafunguliwe kwa kupitia fomu na. 1 ya Tume lakini fomu iliyowasilishwa mbele ya Tume ilikuwa na jina moja tu la Simon H. Loko. Aidha, fomu hiyo haikuonyesha majina ya watu wengine. Kwa upande wa waajiriwa, wao walieleza kuwa Kanuni ya 5(2) na (3) ya Kanuni za Taasisi ya Kazi (Uamuzi na Usuluhushi), Tangazo la Serikali Na. 64 la 2007 inaelekeza kwamba kama mwajiriwa zaidi ya mmoja hajaridhika na Uamuzi, walio wengi wanaweza kumpa kibali mmoja wao kufungua shauri kwa niaba yao. Nimeangalia fomu Na. 1 ya Tume iliyowasilishwa mbele ya Tume na waajiriwa. Fomu hiyo imejazwa na Simon H. Loko na kusainiwa naye. Katika sehemu B (part B) ya fomu hiyo katika eneo la kuanza kwa ajira imejazwa tarehe ya kuanza kazi kwa waajiriwa wengine. Fomu hiyo imeambatishwa na orodha ya majina ya waajiriwa wengine ambayo wameisaini. Utaratibu wa kufungua shauri la pamoja ambalo kwa maoni yangu ni sawa na shauri la uwakilishi (representative suit) mbele ya Tume linaongozwa na sheria yake mahsusi. Na sheria hiyo ni kanuni ya 5 ya Tangazo la Serikali Na. 64 la 2007. Kanuni hiyo inatoa nafasi kwa nyaraka 17 za mgogoro kusainiwa na mhusika au mtu mwingine anayestahili wa kumwakilisha katika shauri. Kanuni inaruhusu mwajiriwa zaidi ya mmoja kuanzisha shauri la pamoja na nyaraka zao kuwekwa saini na mmoja wao waliyempa mamlaka na waambatishe orodha ya majina yao iliyo na saini zao. Kanuni hiyo inaeleza kama ifuatavyo, nanukuu:- 5.-(l) Nyaraka itatiwa saini na mhusika au mtu mwingine yeyote anayestahili, chini ya sheria au kanuni hizi, kumwakilisha mhusika huyo. (2) Pale ambapo mashauri yameanzishwa au kupingwa kwa pamoja na mwajiriwa Zaidi ya mmoja, nyaraka zinaweza kutiwa saini na mwajiriwa ambaye amepewa mamlaka na waajiriwa wengine kufanya hivyo. (3) kwa kuzingatia kanuni ndogo ya (2) orodha ya maandishi ya waajiriwa ambao wamempa mamlaka mwajiriwa mahsusi kutia saini kwa niaba yao iazima iambatishwe kwenye nyaraka. Orodha iazima itiwe saini na waajiriwa ambao majina yao yameorodheshwa ndani yake. Ni maoni yangu kuwa kanuni tajwa hapo juu inaruhusu mwajiriwa mmoja kufungua shauri la pamoja na waajiriwa wengine na kuweka saini kwa niaba yao iwapo watampa kibali. Kinachotakiwa ni mwajiriwa au waajiriwa hao waambatishe orodha yenye majina yao na ambayo wameitia saini. Kanuni inaruhusu nyaraka za shauri la pamoja kutiwa saini na mwajiriwa ambaye amepewa mamlaka na waajiriwa wengine. Hata fomu Na. 1 ya Tume haitoi nafasi kwa mwajiriwa zaidi ya mmoja kujaza taarifa zake. Kwa sababu hiyo naona kuwa hoja ya mwajiri kuwa mgogoro wa waajiriwa haukuwa sawa mbele ya Tume haina mashiko. 18 Hoja ya pili inahusu uhalali wa sababu ya kuwaachisha kazi Wajibu Maombi. Kifungu cha 37 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Sura ya 366 ya Sheria kama ilivyorekebishwa mwaka 2019 ndicho kinachoongoza uachishwaji kazi usio halali. Kifungu cha 37(1) cha sheria hiyo kinaeleza kuwa itakuwani kinyume cha sheria kwa mwajiri kumuachisha kazi mwajiriwa isivyo halali. Na kifungu kidogo cha (2) cha kifungu hicho kinaeleza kuwa mwajiri atakuwa amemwachisha kazi mwajiriwa isivyo halali iwapo atashindwa kuthibitisha kuwa sababu za kumwachisha kazi zilikuwa za haki na halali na taratibu za kumwachisha kazi zilikuwa halali. Hivyo, jukumu la kuithibitishia Mahakama ya kwamba uachishwaji kazi ulikuwa halali ni la mwajiri kama inavyoelekezwa katika kifungu cha 39 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini. Mahakama hii katika kesi ya Tanzania Railway Limited dhidi ya Mwajuma Said Semkiwa, Marejeo Na. 239 ya 2014, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, iliyokaa Dar Es Salaam, ilieleza kuwa ni msimamo wa kisheria kwamba Hi uachishwaji kazi uonekane ni halali ni lazima utokane na sababu halali na taratibu halali za kuachishwa kazi. Kwa maneno mengine kuwe na uhalali wa sababu za kuachishwa kazi na uhalali wa taratibu za kuachishwa kazi. Katika shauri hili waajiriwa wanakili kuandika waraka - Kielelezo D-3 (waraka wa Askofu) ukimtaka Askofu ajiuzuru kwa tuhuma mbalimbali ikiwa ni pamoja na uvunjifu wa katiba ya Dayosisi, matumizi mabaya ya 19 madaraka, ubaguzi na upendeleo, kuwa mtu wa maendeleo, kukosa usikivu na kutendea kazi mambo ya kusikia, kushiriki mambo ya kimila na uchochezi wa migogoro ya wakulima na wafugaji. Kwa mujibu wa Kanuni ya 10(8) (b) ya Mwongozo wa Utumishi wa Kanisa inamtaka mtumishi mwenye malalamiko kuyafikisha kwa mkuu wake wa kazi kwa njia ya maandishi. PW1 katika ushahidi wake ameeleza kuwa waliandika waraka huo na kuuwasilisha kwa viongozi wa Dayosisi kama kumbukumbu ya kupokea barua - kielelezo C6 kinavyoonesha. Kwa upande wa shahidi wa mwajiri ambaye ni DW1 yeye alieleza kuwa kuandika waraka ni kinyume cha kanuni ya 10(8) (a)-(d) ya Mwongozo wa Utumishi wa Kanisa. Na kuwa hata baada ya kupewa barua ya onyo kali - kielelezo C7 na kutakiwa kuukana waraka huo na kuwa na imani na Askofu Mameo bado hawakufanya hivyo. Nimezipitia kanuni hizo na kuona kuwa hakuna kosa lililofanywa na waajiriwa kwa kuwa wameeleza kuwa waraka huo wa maandishi uliwasilishwa kwa viongozi wa dayosisi na ushahidi huo haujapingwa. DW1 alichoonesha katika ushahidi wake ni kuwa malalamiko yaliyokuwa katika waraka hayakuwa ya kweli. DW1 alieleza kuwa hata baada ya kuambiwa waukane waraka huo bado waajiriwa walikaidi. Kwa sababu hiyo walitenda kosa la nidhamu. PW1 ameeleza kuwa barua ya onyo ilieleza kuwa kosa lao 20 ni kutofuata utaratibu wa kuwasilisha malalamiko na kuwa wao waliwasilisha waraka wao kwa maandishi. PW1 aliendelea kueleza kuwa barua ya kuwaachisha kazi - kielelezo D8 inasema kosa lao ni kukaidi maagizo ya Halmashauri Kuu. Nimeisoma barua ya kuwaachisha kazi waajiriwa. Baua inaeleza kuwa Halmashauri Kuu ilikaa tarehe 06/04/2019 na kuwapa onyo kali waajiriwa na kutakiwa ndani ya siku 7 wafute tamko lao katika waraka la kutokuwa na Imani na Askofu. Barua hiyo ya kuwataarifu Uamuzi wa Halmashauri Kuu walipewa tarehe 25/04/2019. Lakini tarehe 30/04/2019 kabla ya hizo siku 7 kukamilika mwajiri aliamua kuwafuta kazi. Ni kweli kuwa waajiriwa hadi wanaachishwa kazi walikuwa hawajafuta tamko lao. Lakini pia ni wazi kuwa muda waliopewa wa kufuta tamko ulikuwa haujakamilika hivyo mwajiri aliwaachisha kazi kabla ya siku 7 alizowapa za kukana waraka hazijamalizika. Hii inaonesha kuwa walikuwa bado hawajakaidi maelekezo ya Halmashauri Kuu. Hivyo, ni maoni yangu kuwa sababu hiyo ya kuwaachisha kazi haionekani kuwa ni ya haki. Kuhusu taratibu za kuachishwa kazi kwa makosa ya kinidhamu, ill taratibu hizo ziwe halali Mwajiri hana budi kuzingatia taratibu zilizoainishwa katika Kanuni ya 13 ya Kanuni za Ajira na Mahusiano Kazini (Kanuni za Utendaji Bora), Tangazo la Serikali Na. 42 la 2007. Katika Marejeo haya Tume iliona ya kwamba taratibu za uachishwaji kazi hazikufuatwa kwa 21 kuwa hakuna Taarifa yoyote ya uchunguzi iliyofanywa mwajiri. Ushahidi unaonesha waajiriwa wakipewa taarifa ya kuitwa katika mkutano wa Halmashauri Kuu kwa ajili ya kujadili tuhuma zilizopo katika waraka. Baada ya majadiliano walipewa barua ya onyo kali na kutakiwa kukana waraka huo. Lakini baada ya hapo haionekani kama kulikuwa na kikao kingine cha Halmashauri Kuu kilichokaa kuamua kuwaachisha kazi. Hivyo ni wazi kuwa hakuna uchunguzi uliofanyika kuhusu tuhuma zinazowakabili, hakuna kamati ya nidhamu iliyokaa, hakuna mashahidi waliosikilizwa kuhusiana na tuhuma hizo, waajiriwa hawakupewa nafasi ya kuwahoji mashahidi, kanuni dhidi ya upendeleo hazikuzingatiwa kwa watu wanaowatuhumu waajiriwa kuwa wajumbe wa kikao kilichowajadili na kuamua wapewe barua za onyo kali zikiwataka waukane waraka, na watu hao ni Askofu na DW1. Katika kesi ya Mbeya- Rukwa Auto Parts and Transport dhidi ya Jestina Mwakyoma [2003] T.L.R. 251, Mahakama ilikuwa na msimamo kuwa kuwa ni kanuni ya haki za asili (natural justice) kuwa mtu yoyote asiadhibiwe bila kusikilizwa. Aidha, Mahakama hii ilikuwa na msimamo kama huo katika kesi ya Abbas Sherally na Mwenzake dhidi ya Abdul Sultan Haji Mohamed Fazalboy, Maombi ya Madai Na. 33 ya 2002. Kitendo cha waajiriwa kunyimwa taarifa ya uchunguzi ni sawa na kuwanyima haki yao ya kuwasikliza kama ilivyoeleza Mahakama ya Rufani 22 katika kesi ya Severo Mutegeki na Mwenzake dhidi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA), Rufaa ya Madai Na. 343 of 2019, Mahakama ya Rufani, iliyokaa Dodoma. Mahakama ya rufaa pia ilikuwa na msimamo kama huo kwa mwajiriwa kunyimwa haki ya kuwahoji kwa maswali mashahidi wa mwajiri wakati wa kikao cha nidhamu ni sawa na kuwanyima haki yao ya kusikilizwa katika kesi ya Hamisi Jonathan John Mayage dhidi ya Board of External Trade, Rufaa ya Madai Na. 37 of 2009 Mahakama ya Rufani ya Tanzania, (haijaripotiwa). Pia katika maombi haya ni wazi ya kwamba mgogoro wa Wajibu Maombi ulishughulikiwa na Halmashauri Kuu kabla ya kupitishwa Halmashauri ya Utendaji kinyume na Kifungu cha 10(7)(b) cha Mwongozi wa Utumishi. Hivyo hoja ya Mleta Maombi ya kwamba Waleta Maombi hawakufuata taratibu za ndani kabla ya kufungua Maombi yao Tume inakosa nguvu kwani chombo kilichoshughulikia mgogoro ndio chombo cha mwisho cha masuala ya kinidhamu ya watumishi katika Dayosisi. Hivyo Mahakama hii inaona kuwa waajiriwa waliachishwa kazi bila sababu halali na pasipo kufuata utaratibu halali za kuwaachisha kazi. Hoja ya mwisho katika shauri hili nini ni stahiki za kila upande. Tume ilitoa amri kuwa mwajiri awalipe waajiriwa mishahara ya miezi 24 kama fidia ya kuachishwa kazi, mishahara ya miezi 14 ya wakati wa usikilizwaji 23 wa mgogoro mbele ya Tume, mshahara wa mwezi mmoja kama taarifa ya kuachishwa kazi na kiinua mgongo. Waajiriwa wanaomba warudishwe kazini bila masharti (reinstatement) au walipwe shilingi milioni 1,581,467,000/= kama fidia ya kuachishwa kazi isivyo halali. Upande wa mwajiri ameeleza kuwa Tume ilikosea kuwapa tuzo ya mishahara ya miezi 14 baada ya kuwapa fidia ya mishahara ya miezi 24. Kwa mujibu wa kanuni ya 32(2) (b) ya Kanuni za Taasisi za Kazi (Mwongozo wa Usuluhishi na Uamuzi), Tangazo la Serikali Na. 67 la 2007, Muamuzi anatakiwa atoe amri ya kurudishwa kazi pale ambapo mazingira ya uachishwaji kazi yanaruhusu kuendelea kwa mahusiano ya kikazi. Katika shauri hili Muamuzi aliona kuwa hawezi kuwarudisha kazini waajiriwa kwa sababu waajiriwa walitoa ushahidi kuwa wao hawamkubali Askofu Jacob Mameo Paulo ambaye ndiye kiongozi wa Dayosisi. Hivyo, nakubaliana na Muamuzi kuwa kuwarudisha kazini ni kuruhusu migogoro katika taasisi hiyo ya dini iendelee. Hivyo, nafuu inayostahili katika mgogoro huu ni wa fidia kwa kuachishwa kazi isivyo halali kama Tume ilivyoamua kwa usahihi. Wakili wa waajiriwa aliomba walipwe milioni 1,581,467,000/= kama fidia. Hata hivyo maombi yake hayana uhalisia na hayana mchanganuo wa malipo hayo na hivyo Mahakama haiwezi kuyakubali. Kuhusu malipo ya mshahara wa miezi 14 nakubaliana na maoni ya wakili wa mwajiri kuwa Muamuzi hakuwa sahihi kutoa tuzo hiyo kwa kuwa waajiriwa hawakuwa 24 wakidai mishahara hiyo. Kifungu cha 40(2) cha Sura ya 366 ya Sheria, kinaeleza kuwa malipo ya fidia ni nyongeza ya malipo mengine anayostahili mwajiriwa. Kwa kumlipa fidia ya kuachishwa kazi ndio malipo ambayo waajiriwa wanastahili kwa kuachishwa kazi isivyo halali. Kwa kuwa hawakuwa wakifanya kazi kipindi mgogoro ukiwa mbele ya Tume waajiriwa hawastahili malipo ya madeni mengine ambayo hawakuwa wanadai. Hivyo, naifuta tuzo hiyo ya mshahara wa miezi 14. Kuhusu ushahidi mishahara ya waajiriwa, ushahidi pekee unaoonesha mishahara wa waajiriwa ni maelezo yao wakati wakiulizwa maswali na Tume. Kwa ajili ya kupata malipo wanayostahili kulipwa na kwa nia ya kutenda haki, naona kuwa Tume ilikuwa sahihi kuona kuwa mishahara ya waajiriwa ni hiyo waliyoitaja. Hivyo, Tume ilikuwa sahihi kuitumia katika kufanyia hesabu za malipo yao. Malipo ya kiinua mgongo na mshahara wa mwezi mmoja badala ya taarifa kuachishwa kazi yanabaki kama yalivyo. Kwa sababu hiyo, uamuzi wa Tume kuhusu malipo ya shilingi 65,736,000/= ya fidia ya kuachishwa kazi, malipo ya shilingi 7,376,114/= ya kiinua mgongo na malipo ya shilingi 2,739,700/= ya taarifa ya kuachishwa kazi yanabaki kama yalivyo. Kuhusu malipo ya fidia kutokana na kashfa (udhalilishaji), sijaona ushahidi wowote uliotolewa mbele ya Tume kuonesha kuwa waajiriwa walidhalilishwa. Hivyo hoja hii haina msingi. 25 Hivyo maombi ya marejeo katika shauri Na. 28 la 2020 na shauri la marejeo Na. 36 la 2020 yamekubaliwa kwa kiasi nilichojadili na kueleza hapo juu. Kwa kuwa hili ni shauri la kikazi, kila upande utabeba gharama za kuendesha shauri hili. 04/06/2021 26