unitrans t limited vs gibson weston kachingwe na wenzake 631 2021 tzhcld 144 4 juni 2021
The Commission for Mediation and Arbitration lacked jurisdiction to quantify and confirm the High Court's decision in Labour Dispute No. 15 of 2010, as such authority is reserved for the Labour Court unless specifically referred. The Commission's proceedings and decision were null and void.
Source-derived case information.
- Citation
- unitrans t limited vs gibson weston kachingwe na wenzake 631 2021 tzhcld 144 4 juni 2021
- Parties
- Applicant: UNITRANS (T) Limited; Respondent: Gibson Weston Kachingwe na wenzake 631
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2021
- Procedural Posture
- Labour Revision / Final Judgment
- Outcome
- application allowed
- Legal Topics
- Jurisdiction of Arbitration Commission, Interpretation of Court Orders, Execution of Judgments, Standing of Parties
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
UNITRANS (T) Limited
Applicant
Gibson Weston Kachingwe na wenzake 631
Respondent
Procedural Posture
Labour Revision / Final Judgment
Legal Issues
- 1 Whether the Commission for Mediation and Arbitration had jurisdiction to quantify and confirm the High Court's decision in Labour Dispute No. 15 of 2010
- 2 Whether the Commission acted unlawfully in hearing and deciding the respondents' application
- 3 Whether the respondents were identifiable and had standing in the application before the Commission
Ratio Decidendi
The Commission for Mediation and Arbitration lacked jurisdiction to quantify and confirm the High Court's decision in Labour Dispute No. 15 of 2010, as such authority is reserved for the Labour Court unless specifically referred. The Commission's proceedings and decision were null and void.
Court Disposition
application allowed
Orders
- Proceedings and decision in MISC.APPL/CMA/MOR/23/2019 before the Commission are set aside
- Each party to bear its own costs
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DIVISHENI YA KAZI ILIYOKAA MOROGORO SHAURI LA MAREJEO NA. 29 LA 2020 KATI YA UNITRANS (T) LIMITED................................................... MLETA MAOMBI NA GIBSON WESTON KACHINGWE NA WENZAKE 631...... WAJIBU MAOMBI HUKUMU Tarehe ya Amri Ya Mwisho: 26/05/2021 Tarehe ya Hukumu: 04/06/2021 A.E MWIPOPO, J. Shauri hili la marejeo limefunguliwa kupinga uamuzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Ofisi ya Morogoro katika Maombi Namba MISC/APPL/MOR/23/2019 yaliyotolewa tarehe 8 Mei, 2020 na Mhe. Z.B. Mgombozi, Msuluhishi. UNITRANS (T) Limited ambaye ni Mleta Maombi anaiomba Mahakama mambo yafuatayo:- 1. Kwamba, Mahakama hii ikipendezwa iliitishe, ifanye marejeo ya mwenendo na kuuweka pembeni (set aside) uamuzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Ofisi ya Morogoro katika Maombi Namba MISC/APPL/MOR/23/2019 yaliyotolewa tarehe 8 Mei, 2020 na Mhe. Z.B. Mgombozi, Msuluhishi. 2. Kwamba Mahakama hii ikipendezwa itoe tamko kuwa uamuzi huo wa kukokotoa na kuthibitisha katika Maombi Na. i MISC/APPL/MOR/23/2019 yaliyotolewa tarehe 8 Mei, 2020 haukupatikana kihalali na ulikuwa kinyume cha sheria na umejaa makosa. 3. Kwamba, Mahakama hii ikipendezwa itoe amri nyingine yoyote au zozote itakazoona ni za haki na zenye usawa (equitable). Shauri hili la marejeo linaungwa mkono na kiapo cha Gaspary Mwakatuma, ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa Mleta Maombi. Kiapo hicho kina hoja sita za kisheria katika aya ya nne (4) ambazo Mleta Maombi anaona zinatokana na maelezo muhimu ya mgogoro huo. Hoja hizo ni kama zifuatazo:- i. Kwamba Msuluhishi alikosea kisheria na kiushahidi katika mwenendo wa mgogoro kwa kukokotoa na kuthibitisha Hukumu na Amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi bila kuwa na Mamlaka. ii. Kwamba Msuluhishi alikosea kisheria na kiushahidi kwa kuendelea na ukokotoaji na uthibitishaji wa Hukumu na Amri (Decree) bila kuwepo kwa Amri (Order) yoyote ya kuwasilisha au kukokotoa kutoka Mahakama Kuu. iii. Kwamba Msuluhishi alikosea kisheria na kiushahidi kukokotoa na kuthibitisha Amri ya Mgogoro wa Kazi Na. 15 wa 2010 kwa kuwapendelea Wajibu Maombi ambao walikuwa ni wageni na sio wadaawa katika mgogoro husika. 2 iv. Kwamba Msuluhishi alikosea kisheria na kiushahidi kwa kuendelea na usikilizwaji wa shauri ambalo lilikuwa tayari limeshasikilizwa na kutolewa uamuzi (res judicata) na wakati huo huo shauri kama hilo likiwa linaendelea kusikilizwa na Mahakama yenye mamlaka (res subjudice). v. Kwamba Msuluhishi alikosea kisheria na kiushahidi kwa kuendelea na shauri ambalo liliwasilishwa kimakosa na Waleta Maombi ambao hawatambuliki na ambao hawana maslahi na shauri husika. vi. Kwamba Msuluhishi alikosea kisheria na kiushahidi kukokotoa na kuthibitisha Amri kwa kuwapendelea Wajibu Maombi wote na kwa miaka hadi mwaka 2019 wakati akijua kuwa baadhi ya Wajibu Maombi walikuwa wameshalipwa kiwango cha chini cha mshahara, wengine walikuwa wameachishwa kazi, wengine walikuwa wameshalipwa, wengine walishastaafu kutoka katika kuajiriwa na Mleta Maombi na wengine wameshafariki na hakuna kumbukumbu za wawakilishi wao binafsi wa kisheria (personal legal representative). Maelezo ya mgogoro huu kwa ufupi ni kuwa mwaka 2010 Chama cha Wafanyakazi wa Mashambani (Tanzania Plantation and Agriculture Workers Union - TPAWU) walifungua mgogoro wa kazi Na. 15 wa 2020 kwa niaba ya waajiriwa dhidi ya Mleta Maombi kwa ajili ya kudai malipo ya 3 mishahara ya wanachama wake na masharti mengine ya kazi yawe kama yalivyo kwa sekta ya usafirishaji na mawasiliano. Mahakama hii ilitoa hukumu tarehe 6 Juni, 2011 ambapo ilitoa amri kuwa Mleta Maombi awalipe waajiriwa wake kama waajiriwa wa sekta ya usafirishaji kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Namba 223 la 2007 kwa kipindi husika na baada ya tarehe 01/05/2010 kwa masharti ya Tangazo la Serikali Namba 172 la 2010. Wajibu Maombi katika shauri hili walifungua shauri la utekelezaji wa hukumu ya mgogoro wa kazi Na. 15 wa 2010 ambalo lilisajiliwa kama shauri la utekelezaji Na. 325 la 2014 hapa Mahakamani kwa jina la TPAWU ambapo namba ya Waleta Maombi katika shauri hilo ilikuwa ni 481 dhidi ya Mleta Maombi. Shauri hilo la utekelezaji wa hukumu lilitupiliwa mbali (struck out) na Mhe. Naibu Msajili tarehe 23/10/2015 kufuatia pingamizi lililowekwa na Mleta Maombi. Ndipo Wajibu Maombi wakafungua shauri la maombi Na. No. CMA/MOR/23/2019 mbele ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi kuomba Tume ifanye ukokotoaji na uthibitishaji wa Amri ya Mahakama (Decree) katika mgogoro wa kazi Na. 15 wa 2010 ya Mhe. Jaji Rweyemamu (kama alivyokuwa). Na baada ya kuwasikiliza pande zote, Tume ilitoa uamuzi wake tarehe 08/05/2020. Mleta Maombi hakuridhika na uamuzi huo ndipo akafungua shauri hili la marejeo hapa Mahakama. Wakati wa usikilizwaji wa shauri hili, Mleta Maombi aliwakisishwa na Bw. Danstan Kaijage, Wakili, na kwa upande wa Wajibu Maombi 4 alikuwepo Gibson Kachingwe ambaye alieleza kuwa atawasilisha yeye mwenyewe kwa niaba ya Wajibu Maombi. Akitoa mawasilisho ya kuunga mkono marejeo, Wakili wa Mleta Maombi alieleza kuwa Uamuzi wa Tume ulitolewa bila kufuata utaratibu na umejaa makosa. Katika ukurasa wa 12 wa Uamuzi uliotolewa na Mhe. Mkombozi, Z.B, Msuluhushi wa tarehe 08/05/2020 tunaona kuna maneno yameongezwa kwa pembeni (commitment) jambo ambalo linaonyesha kuwa kuna uwezekano wa Uamuzi huo kuandikwa na mtu mwingine. Mamlaka ya Msuluhishi yapo katika Kanuni ya 5(1) ya Kanuni za Taasisi za Kazi (Mwongozo wa Usuluhishi na Uamuzi), Tangazo la Serikali Na. 67 la 2007. Mamlaka hayo ni kaona namna usuluhishi utakavyoendeshwa. Kwa bahati mbaya hakuna usuluhishi wowote ambao ulifanyika. Badala yake, msulushi alijibadilisha kuwa Muamuzi na kutoa uamuzi. Wakili anaendelea kueleza kuwa waliweka pingamizi juu ya uhalali wa mgogoro kufunguliwa katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi kwa kuwa haina Mamlaka ya Kusikiliza maombi ya kukokotoa (quantify) na kuthibitishe uamuzi wa Mahakama Kuu. Kwa sababu uamuzi wa Mahakama Kuu huwa utekelezaji wake unafanywa na Mahakama Kuu yenyewe. Kama ingekuwa kuna tuzo ya Tume na Muamuzi hakutoa hesabu ya malipo basi huwa shauri linaweza kurudishiwa Tume na Mahakama kwa ajili ya kufanya mahesabu hayo. Na utaratibu ni kwamba pande zote zitaitwa na kutoa ushahidi. Mgogoro wa Kazi Na. 15 wa 2010 5 uliokuwa mbele ya Jaji Rweyemamu kati ya TPAWU na UNITRANS haukuwa na malipo. Ulikuwa ni uamuzi wa matamko. Hakuna amri ya Mahakama iliyorudisha shauri hilo Tume kwa ajili ya kufanyia Mahesabu (ukokotoaji wa malipo). Pamoja na kuieleza Tume haya yote Tume iliendelea kusikiliza shauri hilo na kulitolea Uamuzi. Hivyo, Uamuzi wote wa Tume ulikuwa ni batili na kinyume cha Sheria. Wakili aliendelea kueleza kuwa Shauri Na. 15 la 2010 mbele ya Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi lilikuwa kati ya TPAWU na UNITRANS. Wajibu Maombi hawakuwa sehemu ya Maombi hayo na walifungua maombi mbele ya Tume na kusikilizwa. Hivyo walikuwa ni wageni, hawakuwa sehemu ya Shauri la msingi lililokuwa mbele ya Mahakama, hivyo Tume haikutakiwa kuwasikiliza. Shauri hilo pia lilikuwa tayari mbele ya Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi kama Maombi Na. 759 ya 2019 na hivyo kuendelea na shauri hilo haikuwa sahihi, lakini bado Muamuzi aliendelea kulisikiliza. Shauri hilo la Maombi lilihusu wadaawa hawahawa na maombi yalikuwa yanashabihiana. Kwa sasa shauri hilo limeshatolewa Uamuzi na wamekata rufaa kwenda Mahakama ya Rufani. Hivyo alitakakiwa kufuata kanuni ya kutoendelea kwa mashauri mawili mbele ya Mahakama yenye mamlaka kuhusu wadaawa walewale na madai yaleyale kwa wakati mmoja (res subjudice). Mleta Maombi aliendelea kueleza kuwa Wajibu Maombi hawakuwa wakijulikana. Na Katika shauri hili na hata mbele ya Tume wajibu maombi 6 hawajawahi kuleta watu 231 wakathibitishwa. Kuna watu kati ya Wajibu Maombi ambao wanajulikana kuwa tayari wamefariki na utaratibu wa kufuata ili kupata haki zao haujafanyika. Baadhi ya wafanyakazi waliachishwa kazi mwaka 2010 lakini Uamuzi wa msuluhishi umewapa malipo ya mpaka mwaka 2019. Msuluhishi alielekeza wajibu maombi walipwe billion 4.7 na Mleta maombi. Mleta Maombi anaona kuwa nafuu hii ni ya kumkomoa ili afunge biashara kitu ambacho ni kinyume cha ustawi wa kijamii na kiuchumi kwa inavyoelezwa na kifungu cha 3 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini. Aidhaz hakuna mfanyakazi hata mmoja aliyefika mbele ya Tume kwa ajili ya kuthibitisha madai yake. Mleta Maombi aliitaarifu tume kuwa tayari alishalipa waajiriwa wake na wahusika wa Mgogoro wa kazi namba 15 wa 2010 tayari walishawasilisha hati ya makubaliano ya kumaliza mgogoro (deed of settlement) mbele ya Mahakama na mbele ya Tume. Mleta Maombi anaomba Mahakama ifanye marejeo ya uamuzi wa Tume na kuona kuwa Msuluhishi alitoa uamuzi kinyume cha Sheria na hivyo uamuzi huo utenguliwe. Akijibu mawasilisho ya Mleta Maombi, Bw. Gibson Kachengwe alieleza kuwa kuhusu uamuzi wa pingamizi la awali yaliyotolewa na Msuluhishi ni maoni yake kuwa pande zote mbili hazikuomba marejeo dhidi ya uamuzi huo mdogo kama uamuzi mdogo wa Tume ulivyoeleza. Hivyo basi pande zote mbili zilikubali kubanwa na uamuzi huo. Bw. 7 Kachengwe aliendelea kueleza kuwa Msuluhishi alimtaka Mleta Maombi atoe maelezo kwa ajili ya kuthibitisha malipo yao lakini hawakuwasilisha mahesabu ili Tume iweze kupima (kukokotoa) malipo yaliyoamriwa na Mahakama. Uhalali wa Mgogoro kuwa mbele ya Tume ni kuwa wakati wa kukazia hukumu TPAWU waliwasilisha Mahakamani shauri la ukaziaji hukumu (execution application) Na. 325 la 2014 na shauri hilo lilitupiliwa mbali kutokana na kutojulikana tarehe ya amri ya Mahakama (Decree date). Hivyo ukaziaji hukumu haukuendelea kwa sababu tarehe ya amri ya Mahakama haikujulikana. Naibu Msajili alieleza kuwa Wajibu Maombi walitakiwa wawasilishe maombi ya madai yao baada ya kuonekana kuwa wanaangukia katika sekta ya kilimo na sio sekta ya usafiri. Baada ya amri hiyo ya Naibu Msajili, Wajibu Maombi waliwasilisha Maombi Mahakama Kuu ambapo tarehe 17/01/2019 Msajili wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, alikataa kusajili shauri hilo na kuelekeza kuwa kama tuzo haikukokotoa malipo warudi tena Tume kwa ajili ya ukokotoaji. Kutokana na maelekezo ya Msajili, Wajibu Maombi walifungua shauri lao mbele ya Tume. Suala la Mamlaka ya Tume halipo kwa kuwa Mahakama ilielekeza ukokotoaji wa malipo ufanywe mbele ya Tume. Kuhusu Wajibu Maombi kuwa si sehemu ya wadaawa katika uamuzi wa Mahakama Kuu katika Mgogoro wa Kazi Na. 15 wa 2010, Bw. Kachengwe alieleza kuwa shauri hili lilifunguliwa mbele ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi na wafanyakazi wakiongozwa na yeye mwenyewe 8 kama mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi (TPAWU) wa tawi. Tume iliupeleka mgogoro katika Mahakama ya Kazi kwa kuwa lilihusu tafsiri ya sheria na ndipo TPAWU wakachukua kuliendesha shauri hilo. TPAWU walitakiwa wasajili shauri hili kama TPAWU kwa niaba ya wafanyakazi wa UNITRANS (T) Limited lakini walisajili kuwa TPAWU ndiye Mleta Maombi. Kwa hivyo kulikuwa na Uhusiano Mkubwa kati ya TPWU na Waleta Maombi. Kanuni ya 49(2) ya Kanuni za Mahakama ya kazi inaeleza kuwa Mshinda deni tuzo, mtu mwenye maslahi, mnufaikaji anaweza kuomba kukazia hukumu ya Uamuzi au tuzo ya Tume au mtu mwingine yeyote anayehusika au bodi kama amri ya Mahakama inavyoelekeza. Hivyo ukaziaji wa hukumu katika shauri la utekezaji Na. 325 la 2014 haukufanyika kwa kuwa lilifutwa (struck out). Anaendelea kueleza kuwa mwaka 2016 TPAWU waliingia makubaliano na Mleta Maombi (deed of settlement) ambayo hayakuwa halali. Sababu ni kuwa kipengele E kilichopo katika ukurasa wa 2 wa Makubaliano hayo inaonyesha kuwa sasa UNITRANS imebadili leseni yake na kuwa katika Sekta ya kilimo wakati hukumu ya Mahakama ilishaeleza kuwa wapo katika sekta ya usafirishaji. Pia makubaliano hayo yalisainiwa na mwenyekiti wa tawi wa TPAWU ambaye hakuwa na uelewa wa kiingereza hivyo hakujua jambo alilolisaini. Aidha kiwango cha malipo kilichokubaliwa kuwa kitalipwa katika hati ya makubaliano (deed of settlement) ni shillings milioni 839,144,068.00 ambazo zingelipwa ndani ya 9 miezi 12 na hazijawahi kulipwa. Tunaona hati ya makubaliano iliona wanaostahili kulipwa ni wale waliokuwa na mishahara ya kima cha chini. Aidha, Mleta maombi alilipa wafanyakazi tu waliokuwa wanalipwa chini ya kiwango cha kima cha chini. Na hakuna uthibitisho kuwa watu 540 waliorodheshwa na Mleta Maombi kama walilipwa. Mleta Maombi hakuwa sahihi kuona kuwa baadhi ya wafanyakazi walipwe na wengine wasilipwe wakati wote wanafanya kazi katika sekta moja. Kuhusu hoja ya Mleta maombi kuwa Wajibu Maombi kuwa hawajulikani, Bw. Kachengwe alieleza Mleta Maombi anadai Wajibu Maombi hawajulikani lakini wakati huo huo anatoa orodha ya watumishi wanaostahili kulipwa na wasiostahili kulipwa. Hii inaonyesha kuwa anawajua wafanyakazi wote ambao ni Waleta Maombi. Aidha, watu 631 walisaini nyaraka za maombi mbele ya Tume. Kuhusu mwajiriwa ambaye alifariki, huyo alisainiwa na nduyu yake bila kuonyesha kuwa anayesaini ni msimamizi wake wa mirathi. Mwajiriwa huyo hatakiwi kupoteza haki zake sababu amefariki. Pia orodha hiyo iliandaliwa mwaka 2013 na sio mwaka 2018 kama walivyodai waleta maombi. Kuhusu wafanyakazi kuendelea kulipwa hadi mwaka 2019, Bw. Kachengwe alieleza kuwa hii sio kweli kwa sababu kila mwajiriwa alifanyiwa hesabu ya hadi tarehe yake ya kuachishwa kazi na hesabu hizo hazina riba kwa sababu Tume iliondoa riba kwa kuwa shauri hilo ni shauri la kazi. Hivyo kiasi kilichothibitishwa ni shilingi bilioni 4.3. Kiasi hicho sio io tatizo kwa kuwa ni haki yao kwa mujibu wa sheria. Mchanganuo wa malipo ulitolewa mbele ya Tume hivyo sio kweli kama mchanganuo haukutolewa. Ni wazi kuwa waleta maombi hawakusema malipo waliyoyafanya yamefikiwaje na kikokotoo ni kipi. Kuna suala jipya katika aya ya 3.4 ya kiapo cha Mleta Maombi kuwa amewalipa jumla ya watu 1,280 katika Hati ya makubaliano lakini mbele ya Tume walisema kuwa wamelipa watu 540. Mjibu Maombi anaona hili sio sehemu ya rekodi za Tume na naomba liondolewe. Katika orodha ya waliolipwa na wasiolipwa Adam Skonda alionekana kuwepo kote lakini mshahara wake ni wa kima cha chini na alistahili kulipwa. Zabron Daudi hajawahi kulipwa tokea mwaka 2008 hadi 2014. Hivyo taarifa ya Mleta Maombi ina makosa kuonyesha kuwa kuwa watu wamelipwa wakati hawajalipwa. Bw. Kachengwe aliomba Mahakama ione kuwa Uamuzi wa Tume ulikuwa sahihi na shauri hili litupiliwe mbali (dismissed). Katika mawasilisho ya nyongeza (rejoinder submission), Wakili wa Mleta Maombi alirudia mawasilisho yake ya msingi. Aidha, alifafanua kuwa kanuni ya 49(2) ya Kanuni za Mahakama ya Kazi, Tangazo la Serikali Namba 106 la 2007 (Labour Court Rules, G.N. No. 106 of 2007) inaongelea mnufaika wa Tuzo ya Tume sio ya uamuzi wa Mahakama Kuu. Kuhusu kupinga Hati ya makubaliano, Wakili wa Mleta Maombi alieleza kuwa Wajibu Maombi hawajawahi kuipinga hati hiyo ya makubaliano na ii amri ya Mahakama kuhusu Hati hiyo ya makubaliano. Wote waliostahili kulipwa katika Mgogoro wa kazi namba 15 la 2010 mbele ya Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi wamelipwa. Hakuna mtu ambaye hajalipwa. Na orodha iliyoletwa na Mleta Maombi ya watu waliostahili kulipwa ipo sahihi na watu walilipwa. Kutokana na mawasilisho ya wadaawa, ninaona kuna hoja 3 ambazo Mahakama inatakiwa izitolee uamuzi. Hoja hizo ni kama zifuatazo:- 1. Iwapo Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ilikuwa na mamlaka ya kusikiliza maombi ya kukokotoa na kuthibitisha uamuzi wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi katika Mgogoro wa Kazi Na. 15 wa 2010. 2. Iwapo Tume ilisikiliza na kutoa uamuzi katika maombi ya Wajibu Maombi kinyume cha sheria. 3. Na Iwapo Wajibu Maombi hawatambuliki na hawana maslahi na shauri lililokuwa limewasilishwa mbele ya Tume. Nikianza kuingalia hoja ya kwanza iwapo Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ilikuwa na Mamlaka ya kusikiliza maombi ya kukokotoa na kuthibitisha uamuzi wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi katika Mgogoro wa Kazi Na. 15 wa 2010, sheria inayoongoza tafsiri ya hukumu, amri au uamuzi wa Mahakama hii ni kanuni ya 48(8) ya Kanuni za Mahakama ya Kazi, Tangazo la Serikali Na. 106 la 2007. Kanuni hiyo inaeleza kuwa, nainukuu:- 12 "4(8) Where any question arises as to the interpretation of any decision of the Court, or the Labour Commissioner, or the Commission, any party to the decision may apply to the Court for a decision on such a question, and the Court shall decide the matter after hearing the parties and the decision of the Court shall be notified to the parties and shall be deemed to form part of and shall have the same effect in all respect as the main decision." Kwa tafsiri isiyo rasmi, kanuni hiyo inaeleza kuwa pale ambapo kutakapotokea swali kuhusu tafsiri ya uamuzi wa Mahakama, au Kamishna wa Kazi, au Tume, mdaawa yeyote katika uamuzi huo anaweza kuwasilisha maombi Mahakamani kwa ajili ya uamuzi kuhusiana na swali husika, na Mahakama itaamua suala hilo baada ya kuwasikiliza wadaawa wote na taarifa ya uamuzi wa Mahakama itapelekwa kwa wadaawa wote na itachukuliwa kuwa ni sehemu na itakuwa na matokeo sawa na uamuzi wa msingi (main decision) katika hali zote. Aidha, tafsiri ya neno Mahakama katika kanuni ya 2(2) inaeleza kuwa neno Mahakama litakuwa na maana ya Mahakama ya Kazi. Kutokana na kanuni tajwa hapo juu ni wazi kwamba pale kunapokuwa na maswali kuhusu tafsiri ya uamuzi wa Mahakama ya Kazi basi tafsiri hiyo itatolewa na Mahakama ya Kazi yenyewe. Katika shauri hili la marejeo, Mleta Maombi alieleza kuwa waliweka pingamizi juu ya uhalali wa mgogoro kufunguliwa katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi kwa kuwa haina Mamlaka ya Kusikiliza maombi ya kukokotoa (quantify) na kuthibitisha uamuzi wa Mahakama Kuu. Mgogoro wa Kazi Na. 15 wa 2010 uliokuwa mbele ya Jaji Rweyemamu kati ya 13 TPAWU na UNITRANS haukuwa na malipo na ulikuwa ni uamuzi wa matamko. Hakuna amri ya Mahakama iliyorudisha shauri hilo Tume kwa ajili ya kufanyia Mahesabu (ukokotoaji wa malipo). Pamoja na kuieleza Tume haya yote Tume iliendelea kusikiliza shauri hilo na kulitolea Uamuzi. Upande wa Wajibu Maombi walieleza kuwa uamuzi wa pingamizi la awali ulitolewa na Muamuzi na pande zote mbili hazikuomba marejeo dhidi ya uamuzi huo mdogo. Hivyo basi pande zote mbili zilikubali kubanwa na uamuzi huo. Uhalali wa Mgogoro kuwa mbele ya Tume ni kuwa wakati wa kukazia hukumu TPAWU waliwasilisha Mahakamani shauri la ukaziaji hukumu (execution application) Na. 325 la 2014 na shauri hilo lilitupiliwa mbali (struck out) kutokana na kutojulikana tarehe ya amri ya Mahakama (Decree date). Naibu Msajili alieleza kuwa Wajibu Maombi walitakiwa wawasilishe maombi ya madai yao baada ya kuonekana kuwa wanaangukia katika sekta ya kilimo na sio sekta ya usafiri. Wajibu Maombi waliwasilisha Maombi Mahakama Kuu ambapo tarehe 17/01/2019 Msajili wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, alikataa kusajili shauri hilo na kuelekeza kuwa kama tuzo haikukokotoa malipo warudie tena Tume kwa ajili ya ukokotoaji. Kutokana na maelekezo ya Msajili Wajibu Maombi walifungua shauri Tume. Suala la Mamlaka ya Tume hawakuliona kwa kuwa Mahakama ilielekeza ukokotoaji wa malipo ufanywe mbele ya Tume. Kutokana na mawasilisho hayo ya Wajibu Maombi, sababu ya kuwasilisha maombi ya kukokotoa na kuthibitisha uamuzi wa Mahakama 14 Kuu, Divisheni ya Kazi katika Mgogoro wa Kazi Na. 15 wa 2010 ni maelekezo ya Msajiri wa Mahakama Kuu Divisheni ya kazi baada ya kukataa kupokea na kufungua maombi yao ya kupata mahesabu na kuthibitishwa kwa malipo katika mgogoro tajwa kuwa wawasilishe maombi hayo Tume ya Usuluhishi na Uamuzi. Nimeangalia pia uamuzi mdogo wa Tume uliotolewa 17/11/2019 na J.R. Katto, Msuluhishi, ambapo ameeleza kuwa Tume haiwezi kukosa mamlaka ya kupiga mahesabu (kukokotoa) na kuthibitisha uamuzi wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi kwa sababu Mgogoro huo uliwahi kupita mikononi mwake ambapo ulipewa Na. RF/CMA/MOR/325/2015. Ni maoni yangu kuwa uamuzi huo wa Tume sio sahihi kuwa Tume inayo mamlaka ya kufanya mahesabu (kukokotoa) na kuthibitisha uamuzi Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi. Mgogoro uliokuwa mbele ya Tume ni tofauti na mgogoro uliokuwa mbele ya Mahakama Kuu. Mbele ya Mahakama Kuu kulikuwa na Mgogoro wa Kazi Na. 15 wa 2010. Hivyo ni mgogoro tofauti na mgogoro uliowahi kuwa mbele ya Tume. Vilevile, Tume haina mamlaka ya kukokotoa au kuthibitisha uamuzi wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi isipokuwa pale ambapo Mahakama Kuu imetoa amri kuwa Tume ifanye ukokotoaji na uthibitishaji. Katika shauri hili, Wajibu Maombi wameeleza kuwa sababu ya kuuwasilisha maombi ya kukokotoa na kuthibitisha uamuzi wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi ni maelekezo ya Msajili wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi alioutoa tarehe 17/01/2019 baada ya kukataa kusajili shauri la 15 maombi ya kukokotoa uamuzi wa Mahakama katika mgogoro wa kazi Na. 15 wa 2010. Hata hivyo, maelezo haya hayapo katika kiapo Kinzani cha Wajibu Maombi na pia hayakuwa sehemu ya mawasilisho ya Wajibu Maombi wakati wa kujibu pingamizi kama uamuzi mdogo wa tume uliotolewa tarehe 17/11/2019 unavyoonesha katika aya 3 na 4 zilizopo katika ukurasa wa 4. Kuhusu hoja ya Mjibu Maombi kuwa Mleta Maombi na Mjibu Maombi wanabanwa na Uamuzi mdogo wa Tume sababu hawakuomba marejeo, hoja hiyo haina msingi kwa kuwa uamuzi mdogo wa Tume haukuwa unamaliza shauri lililokuwa mbele ya Tume. Hivyo, pande zote zilikuwa haziruhusiwi kisheria kuomba marejeo dhidi ya uamuzi huo kwa mujibu wa kanuni ya 50 ya Kanuni za Mahakama ya Kazi, 2007. Baada ya shauri la msingi kumalizika ndipo pande zote zinaweza kuomba marejeo. Hivyo, ni maoni yangu kuwa Tume haikuwa na Mamlaka ya kufanya mahesabu (kukokotoa) na kuthibitisha uamuzi wa Mahakama Kuu uliowasilishwa na Wajibu Maombi. Hivyo, nafuta mwenendo wa shauri Na. MISC.APPL/CMA/MOR/23/2019 lililosikilizwa na Tume pamoja na uamuzi wake kwa kuwa Tume ilisikiliza shauri hilo ikiwa haina mamlaka. Kwa sababu hoja hii inamaliza shauri hili, sitaendelea kuzitolea uamuzi hoja zilizobaki. 16 Hivyo, shauri hili la marejeo limekubaliwa. Kwa kuwa shauri hili linahusu mgogoro wa kazi, kila upande utagharamia gharama zake za kuendesha shauri lake. 04/06/2021 17