victor mtole 4 others vs walt ul asr education center another 2022 tzhcld 928 2 septemba 2022
The application was fatally defective for combining distinct requests under different legal provisions and for improper affidavit procedure, warranting dismissal.
Source-derived case information.
- Citation
- victor mtole 4 others vs walt ul asr education center another 2022 tzhcld 928 2 septemba 2022
- Parties
- Applicant: Victor Mtole; Applicant: Ester Charles; Applicant: Mohamed Issa; Applicant: Twanzi Mkalacha; Applicant: Hadija Hassan; Respondent: Walt-ul-Asr-Education Center; Respondent: Wali-ul-Asr-Seminary
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2022
- Procedural Posture
- Labour Application / Ruling on Preliminary Objections
- Outcome
- application struck out
- Legal Topics
- Representation, Extension of Time, Procedural Defects
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Victor Mtole
Applicant
Ester Charles
Applicant
Mohamed Issa
Applicant
Twanzi Mkalacha
Applicant
Hadija Hassan
Applicant
Walt-ul-Asr-Education Center
Respondent
Wali-ul-Asr-Seminary
Respondent
Procedural Posture
Labour Application / Ruling on Preliminary Objections
Legal Issues
- 1 Whether the applicants can be represented by one among them
- 2 Whether the applicants are entitled to extension of time to file review applications
- 3 Whether the application is properly constituted
Ratio Decidendi
The application was fatally defective for combining distinct requests under different legal provisions and for improper affidavit procedure, warranting dismissal.
Court Disposition
application struck out
Orders
- The application is struck out for procedural defects.
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
KATIKA MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DIVISHENIYA KAZI PAR ES SALAAM MAOMBI YA ANUAI NA. 153 YA MWAKA 2022 KATI YA VICTOR MTOLE........ ............. ............. MLETA MAOMBI 1 ESTER CHARLES ................................................. MLETA MAOMBI 2 MOHAMED ISSA...................... MLETA MAOMBI 3 TWANZI MKALACHA................ MLETA MAOMBI 4 HADIJA HASSAN ............................................................... MLETA MAOMBI 5 DHIDI YA WALT - UL - ASR - EDUCATION CENTER.........................MJIBU MAOMBI 1 (WALI-UL-ASR-EDUCATION CENTER) WALI-UL-ASR-SEMINARY ............ ...................................... MJIBU MAOMBI 2 UAMUZI S. M. MAGHIMBL J. Waleta maombi wameleta maombi haya mbele ya mahakama chini ya Kanuni ya 24(1), 24(2)(a)(b)(c)(d)(e)(f), 24(3)(a)(a)(b)(c)(d), 36(1) 44(l)(2)(3)v vya Kanuni za Mahakama ya Kazi, Tangazo la Serikali Na. 106 la Mwaka 2007 pamoja na vifungu vingine vya sheria vinavyohusiana. Maombi haya yameambatanishwa na kiapo cha pamoja cha waleta maombi kilichoapwa tarehe 18/11/2021. Wajibu maombi walipinga vikali maombi haya kwa kuleta kiapo kinzania i kilichothibitishwa tarehe 15/05/2022 na Bi. Saida Mavumbi, Afisa Mkuu wa wajibu maombi. Waombaji wanaiomba mahakama amri zifuatazo:- i. Kwamba mahakama itoe kibali kwa mmoja wa waleta maombi ambaye ni Victor Ntore awe muwakilishi wa waleta maombiambao ni Ester Charles, Mohamed Issa, Twanzi Mkalachaka na Hadija Hassan. ii. Kwamba mahakama tukufu itoe kibali cha kuongeza muda kwa waleta maombi ili waongezewe muda wa nyongeza waweze kufungua maombi ya kufanya marejeo na kutengua uamuzi wa aina mbili tofauti uliotolewa na Tume ya Kibaha wa mgogoro wa kazi Na.KBC/PWN/816/2020 na mgogoro wa kikazi Na.KBC/PWN/0015/2020 ulioamuriwa na Tume ya Kibaha kwasababu sio wan amba halisi ya faili la mgogoro wa kikazi waliofungua waleta maombi mbele ya Tume ya Kibaha Na.KBC/PWN/05/2020. iii. Amri nyingine ambayo mahakama itakaona inafaa. Shauri hili limeendeshwa kwa njia ya maandishi. Mbele ya Mahakama hii waleta maombi waliwakilishwa na Bw. Daudi Maziku 2 Maduki, mwakilishi binafsi ilihali Bw. Saiwello TJ. Kumwenda kutoka kampuni ya mawakili iitwayo KUMWENDA. Katika mawasilisho yake Bw. Madiku aliiambia mahakama kuwa wajibu maombi wote kwapamoja hutumia majina hayo kwa masuala ya elimu ya kiislamu huko wilayani Kibaha mkoani Pwani na huduma za ujenzi wa maeneo ya huduma zao. Alieleza kuwa waleta maombi waliajiriwa na wajibu maombi kwa mikataba ya kudumu na walipatiwa huduma za mikopo walipokuwa kazini japokuwa hawakupewa mikataba. Katika mawasilisho yake Bw. Madiku alieleza kwakirefu mahusiano ya kiajira kati ya waleta maombi na wajibu maombi ambapo naona mawasilisho hayo hayana mantiki katika shauri hili. Mahakama imezingatia mawasilisho ya pande zote mbili na yatajadiliwa katika kutoa maamuzi. Akijibu mawasilisho ya waleta maombi Wakili Kumwenda aliibua hoja ambazo mahakama inaona izishughulikie kwanza kabla ya kutatua msingi halisi wa kesi. Hoja hizo ziliibuliwa pia katika kiapo kinzani cha wajibu maombi ambazo ni:- i. Kwamba hakuna kanuni waliyoitaja ambayo inawapa nguvu ya kuomba mmoja wao aombe kuwakilisha wengine na maombi haya kufanywa kwa kujitegemea na siyo kuyachanganya na maombi makubwa. 3 ii. Kwamba waleta maombi wanaomba mahakama iwaongezee muda ili walete maombi ya marejeo ili kutengua maamuzi ya aina mbili lakini ombi hilo haliko sawa kwakuwa hawajataja kifungu gani cha sheria kinawapa nguvu ya kuomba ombi kama hilo lakini pia hawajatoa sababu kwanini walichelewa kuingiza marejeo wakati siku ya Tuzo kule Tume walikuwepo. Japokuwa waleta maombi walikuwa na nafasi ya kujibu hoja hizo katika kiapo cha nyongeza lakini hawakufanya hivyo. Hata hivyo wangeweza pia kujibia hoja hizo katika mawasilisho ya nyongeza lakini wameshindwa pia kufanya hivyo. Mahakama baada yakupitia maombi haya, imeona kuwa waleta maombi wanaaina mbili ya maombi mbele ya mahakama hii kama yalivyoainishwa hapo juu. Ombi la kwanza ni kuwa Bw. Victor Ntole awe mwakilishi wa waleta maombi na ombi la pili ni ongezeko la muda ili waweze kufanya maombi ya marejeo. Kama ambavyo imepingwa na wakili Kumwenda ni kweli kuwa maombi haya hayakupaswa kuchanganywa kwa Pamoja kwakuwa hata vifungu vya kisheria vinavyotumika kwa maombi hayo ni tofauti. Maombi ya uwakilishi hufanywa chini ya kifungu cha 44 cha Kanuni za Mahakama ya Kazi ambacho kimenukuliwa katika maombi haya. Lakini maombi ya 4 ongezeko la muda hufanya chini ya 56 ya Kanuni za Mahakama ya Kazi ambayo haijanukuliwa na waleta maombi katika maombi haya. Hivyo ni wazi kuwa maombi haya yanamapungufu mbele ya mahakama hii kwakuwa yamelekwa kwa Pamoja kimakosa. Pamoja na mapungufu hayo hata kiapo cha waleta maombi kilichopo mbele ya mahakama hii kinamakosa kwakuwa mleta maombi wa kwanza na wa pili wameapa kwaniaba ya waleta maombi wengine jambo ambalo sio sahihi kwani idhini ya mahakama ya kuwaruhusu kufanya hivyo hakuna. Hivyo basi kama kweli waleta maombi wanayo nia ya kuendelea na shauri hili wanatakiwa kuleta maombi ambayo ni sahihi mbele ya mahakama. Hivyo basi, kutokana na mapungufu yaliyoainishwa hapo juu shauri hili linaondolewa mbele ya mahakama hii kwa kuwa lina mapungufu kisheria. Imeamriwa hivyo. Imesainiwa leo Tarehe 02 Mwezi Septemba, Mwaka 2022 m .... L S.t4j^AGHIMBI J AJI 5