MAREJEO NA
The applicant failed to prove he was suspended from employment as alleged. There was no written evidence of suspension, and the evidence showed he stopped attending work after a disciplinary meeting. The CMA properly analyzed the evidence and reached a correct decision.
Source-derived case information.
- Citation
- MAREJEO NA
- Parties
- Applicant: Yahaya Amiri M Kwizu; Respondent: Imperial Security Company Limited
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2024
- Procedural Posture
- Labour Revision / Judgment
- Outcome
- Application dismissed
- Legal Topics
- Suspension From Employment, Procedural Fairness, Burden of Proof, Employment Contract, Disciplinary Proceedings
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
Yahaya Amiri M Kwizu
Applicant
Imperial Security Company Limited
Respondent
Procedural Posture
Labour Revision / Judgment
Legal Issues
- 1 Whether the applicant was suspended from employment by the respondent
- 2 Whether the applicant is entitled to salary during the alleged suspension period
- 3 Whether the Commission for Mediation and Arbitration (CMA) properly analyzed the evidence
Ratio Decidendi
The applicant failed to prove he was suspended from employment as alleged. There was no written evidence of suspension, and the evidence showed he stopped attending work after a disciplinary meeting. The CMA properly analyzed the evidence and reached a correct decision.
Court Disposition
Application dismissed
Orders
- Application is dismissed for lack of merit
- Decision of the Commission for Mediation and Arbitration is upheld
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
KATIKA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA DIVISHENI YA KAZI DAR ES SALAAM MAREJEO NA. 27790 YA MWAKA 2024 REFERENCE NA. 20231215000027790 YAHAYA AMIRI M KW IZU.................................................... MLETA MAOMBI DHIDI YA IMPERIAL SECURITY COMPANY LIMITED........................... MJIBU MAOMBI HUKUMU Tarehe ya amri ya Mwisho: 13/03/2024 Tarehe ya Hukumu: 09/ 04/2024 MLYAMBINA, J. Kabla ya kuwasilisha mgogoro huu mbele ya Mahakama, Mlalamikaji alifungua malalamiko yake katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (ambayo itajulikana kama Tume), akidai kuendelea kulipwa mishahara yake kutokana na maamuzi ya Mjibu Maombi kumsimamisha kazini (suspension) kwa muda kupisha majlbu ya kikao cha nidhamu walichokifanya kutokana na utendajl kazi wa Mleta Maombi. Ni madai ya Mleta Maombi kuwa, kusimamishwa kazi huko kulikuwa kwa njia ya mdomo, hali iliyompelekea kudai barua ya kusimamishwa kazi ili kujua amesimamishwa kwa muda gani pamoja na kuendelea kulipwa mishahara yake kwa kipindi chote atakachokuwa amesimamishwa kazi. Mieta Maombi alidai kuwa licha ya kwamba Mjibu Maombi alimuandikia barua Mlalamikiwa (Kilelezo Y3) akiomba kupatiwa barua ya kusimamishwa kazi na kuweza kufahamishwa kuwa amesimamishwa kwa muda gani, lakini Mjibu Maombi hakujibu barua hiyo. Aliendelea kueleza kuwa, jambo hilo lilipelekea Mleta Maombi kupeleka malalamiko yake mbele ya Tume. Baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili, Tume iliamua ya kuwa Mleta Maombi hakuslmamishwa kazi hivyo madai yake yakatupiliwa mbali. Mleta Maombi hakuridhika na maamuzi hayo ya Tume. Hivyo basi ameleta tena madai yake mbele ya Mahakama hii ili iweze kusahihisha maamuzi ya Tume. Hoja kuu ya Mleta Maombi mbele ya Mahakama h ii n i kuwa Tume Hishindwa kuchambua ushahidi uiiowasiiishwa mbele yake Hi kufikia uamuzi wa haki. Shauri hili liliendeshwa kwa njia ya maandishi na pande zote mbili ziliwasilisha mawasilisho yao kama ilivyoamuriwa na Mahakama. Mbele ya Mahakama hii Mleta Maombi alijiwakilisha mwenyewe ilihali wakili Erick Mwanri, alimwakilisha Mjibu Maombi. Mleta Maombi alieleza kuwa alisimamishwa kwa njia ya mdomo lakini aliona sio njia sahihi ya kumsimamisha kazi bila kuwa na uthibitisho wa barua hivyo, alichukua uamuzi wa kumuandikia barua Mlalamikiwa na kumuomba ampatie maandishi ya barua ya kile anachokidai kuwa amemsimamisha kazi kwa muda (Kielelezo Y3). Alieleza kuwa hata baada ya kupokea barua hiyo Mjibu Maombi alikaa kimya na kutojibu chochote. Mleta Maombi alieleza kuwa, sheria ipo wazi katika Kanuni ya 27(1) na (2) ya Kanuni ya Ajira na Mahusiano Kazini (Kanuni za Utendaji) GN. Na. 42 ya 2007 inamtaka Mwajiri afafanue muda wa kumsimamisha mwajiriwa na sababu ya kumsimamisha Mwajiriwa kwa maandishi. Pia sheria ipo wazi kwamba endapo Mwajiri atachukua uamuzi wa kumsimamisha kazi Mwajiriwa, basi atalazimika kumlipa mishahara yake kwa kipindi chote atakachokuwa amesimamishwa. Alinukuu kanuni hiyo inayoeleza ifuatavyo: 27(1) Pale ambapo tuhuma kali za mwenendo mbaya au kukosa uwezo mwajiri anaweza kumsimamisha kazi mwajiriwa kwa kumpatia mshahara kamili wakati tuhuma zinapochunguzwa na kusubiri hatua zitakazofuata. (2) Mwajiriwa aliyesimamishwa kazi atapewa barua kwa maandishi ya kusimamishwa kazi, inayoeleza sababu za kusimamishwa kazi na masharti yoyote ya kusimamishwa Mleta Maombi alieleza kuwa katika shauri hili Mjibu Maombi alishindwa kulitolea maelezo suala la kumsimamisha Mleta Maombi na badala yake kuanza kukataa kwa kuibua hoja mpya za kusainiwa kwa mkataba. Aliongeza kuwa hata hivyo Mjibu Maombi hakuweza kutoa 3 ushahidi wowote wakati anakanusha madai hayo mbele ya Tume. Aliendelea kueleza kuwa pale ambapo Mwajiriwa amesimamisha malalamiko juu ya Mwajiri, jukumu la kuthibitisha kuwa madai hayo ni sahihi au la linahamia kwa Mwajiri kulingana na Kifungu cha 39 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano KaziniNamba 6 ya Mwaka 2004. Kinachosema: Katika mwenendo wowote unaohusiana na usitishwaji wa ajira usiokuwa wa haki mwajiri atatakiwa kuthibitisha kuwa usitishwaji huo ulikuwa wa haki Kuyapa nguvu zaidi maelezo yake, Mleta Maombi alirejea shauri la Hamidu Abdalah Mbekae na Wenzake dhidi ya Be Forward Tanzania Co. Ltd, Rufaa Na. 380 ya mwaka 2019 iliendelea kuelezwa kuwa katika kuzumgumzia suala la mkataba mpya ambao Mlalamikiwa anadai ndio sababu ya mgogoro, ni dhahiri kwamba mkataba huo haukuwa na mgogoro wowote kwani licha ya kwamba walichelewa kumsainisha mkataba mpya lakini waliendelea kumtumia katika kazi zao na kumlipa mshahara wake wa mwezi kama wafanyakzi wengine. Allifafanua kuwa mkataba wa awali uiifikia kikomo mwezi September 2022 lakini Mlalamikaji aliendelea kwenda kazini na Mlalamikiwa aliendelea kumlipa mshahara wake wa mwezi wa kumi, kwahiyo hakukuwa na shaka kwamba mkataba baina ya Mwajiri na Mwajiriwa uliendelea, kama ilivyoelezwa katika hukumu ya Tume kuwa Mwajiri alikiri kuendelea kufanya nae kazi na hata mshara wa mwezi wa kumi alimpatia. Mleta Maombi alisisitiza kuwa kiini cha mgogoro ni kusimamishwa kazi (suspension) na sio kuachishwa kazi (Termination), na stahiki zilizodaiwa ilikuwa ni mlalamikaji kulipwa mishahara yake kwa kipindi chote atakachokuwa amesimamishwa kazi. Lakini Tume ilishindwa kuchambua kiini cha mgogoro na badala yake kuanza kujikita kuchambua kama Mlalamikaji ni Mwajiriwa wa Mlalamikiwa au la jambo ambalo halikuwahi kubishaniwa. Kupitia maombi haya ya marejeo, Mlalamikaji anaiomba Mahakama kupitia uamuzi wa Tume pamoja na ushahidi uliotolewa na pande zote mbili na kuweza kuyakubali marejeo haya na kuutupilia mbali uamuzi wa Tume kwakuwa haukuchambua vizuri kile kilichokuwa kiini cha mgogoro. Mjibu Maombi alianza kwa kuelezea mahusiano yake na Mleta maombi. Alieleza kuwa alimwajiri Mleta Maombi kama Mlinzi, ambapo walimpa mkataba wa majaribio wa miezi 6. Kwamba, mkataba wa kwanza ulikuwa wa miezi 3 ulifanyika na kusainiwa na pande zote mbili tarehe 16 mwezi wa 3 mwaka 2022 ulifikia kikomo tarehe 5 mwezi wa 6 mwaka 2022 kwa malipo ya mshahara wa TZs 160,000/= kwa mwezi kama ambavyo kielelezo A1 kinavyoonekana. Alieleza kuwa licha ya Mleta Maombi kukataa kusaini mkataba mpya lakini bado alipokea mshahara wa mwezi wa 10. Hivyo basi inashangaza tena Mleta Maombi pale anaposema amesimamishwa kazi wakati alipewa mkataba mpya na alikataa kusaini na kupokea mshahara wa mkataba mpya kwa kuwa mkataba wake ulikua umefikia kikomo. Wakili Mwanri aliendelea kueleza kuwa kulingana na Kanuni ya 10(3) ya GN Na. 42 ya mwaka 2007 inatoa umuhimu wa muda wa majaribio pasina kuzidi miezi kumi na mbili kwa mfanyakazi ambapo ni pamoja na mwajiri kukagua na kujua kama mwajiriwa ana uwezo na mahiri kufanya kazi hiyo kama anafaa kuajiriwa kwenye nafasi ya kazi hiyo. Wakili alielezea kwa kina nafasi ya Mwajiriwa aliepo katika kipindi cha majaribio kama ilivyoelezwa katika kesi mbalimbali ikiwa ni pamoja na David Nzaligo v. National Microfinance Bank Pic, Civil Appeal No.61 of 2016, Karosso, J.Ana kesi ya Commercial Bank of Africa (F) Ltdv. Nikodemus Musa Igogo, Labour Revision, No. 40/2012. Ilielezwa kuwa kwa kuzingatia taratibu za kisheria mwajiri ana uwezo wa kusitisha au kuvunja mkataba ikiwa bado mwajiriwa yupo ndani ya muda wa majaribio ya kazi ilikuona uwezo na umahiri wa mfanyakazi kama anafaa au la. Aliongeza kuwa hoja ya Mleta maombi kwamba Mjibu maombi alimsimamisha kazi bila kumpa sababu za kimaandishi haina mashiko kwa kuwa Mleta Maombi baada ya mkataba wa majaribio kuisha alipewa mkataba mpya wa mwaka mmoja ili athibitishwe(confirmed) kazini lakini aiikataa kusaini biia ya sababu. Licha ya jitihada zilizo fanywa na Mjibu Maombi kumtaka asaini ila yeye aiiamua kukataa kusaini mkataba huo kwasababu anazozijua wewe. Na bado alipokea mshahara ingawa hakuwa anaingia kazini tokea tarehe ya kikao cha nidhamu. Viievile Wakiii aiikanusha vikali madai ya Mieta Maombi kuwa hakuthibitisha maelezo yake mbele ya Tume. Alieleza kuwa maelezo yalithibitishwa na DW1 ambaye nio afisa rasilimali wa Mleta Maombi. Katika hoja yake kuwa Mwajiri ana jukumu la kuthibitisha kuwa madai hayo ni sahihi au la kwa mujibu wa Kifungu cha 39 cha sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Wakiii Mwanri elieleza kuwa hoja hiyo haina mashiko kwani kifungu tajwa kinahusu kuachishwa kazi (proceedings of unfair termination) na kwenye shauri hili Mjibu Maombi hakufukuzwa kazi. Aliongeza kuwa hata hivyo kifungu hicho hakimuhusu yeye kwakuwa alikuwa bado chini ya majaribio na ni sahihi kuwa wakati huu hakuwa na mkataba na Mjibu Maombi. Kuyapa nguvu maelezo yake alirejea kesi ya Stella Temu v. Tanzania Revenue Authority (supra). Itiendelea kuelezwa kuwa baada ya kipindi cha majaribio kumalizika, Mjibu Maombi aliridhishwa na utendaji wa Mleta Maombi na kuamua kumpa mkataba wa mwaka mmoja ili asaini na hatua zingine ziendelee. Jambo la kushangaza Mleta Maombi alikataa kusaini mkataba huo pasipo sababu yoyote. Kutokana na hali elezwa hapo juu Mjibu Maombi aliamua kumuita Mleta Maombi kwenye kikao cha nidhamu kupitia barua ya tarehe 27 mwezi wa 10 mwaka 2022. Barua hiyo ilimtaka afike na msaidizi wake wa kisheria siku ya kikao. Kwamba siku hiyo ya kikao Mleta Maombi hakwenda na msaidizi wake wa kisheria kulingana na takwa la barua bali alienda na mdhamini wake hivyo, kulingana na umuhimu na lengo mahususi la kikao hicho, wajumbe wa mkutano hawakuona umuhimu wa mdhamini na kuomba atoke nje ya kikao hicho kwani kikao kilimtaka msaidizi wa kisheria na sio mdhamini. Jambo la ajabu na lakushangaza mleta maombi naye aliamua kuondoka katika kikao hicho na kukataa kusaini nyaraka za kikao. Wakili Mwanri alieleza kuwa kuanzia tarehe ya kikao cha nidhamu Mleta Maombi hakuwahi kufika kazini mpaka tarehe 29 mwezi 12 mwaka 2022 Mjibu Maombi alipopata taarifa ya kufunguliwa shauri la mgogoro wa kikazi mbele ya Tume. Alisisitiza kuwa Mleta Maombi alikuwa muda wa majaribio. Hivyo basi, aliiomba Mahakama itupilie mbali maombi haya na kuendelea kushikilia maamuzi ya Tume. Mahakama imezingatia mawasilisho ya pande zote mbili. Ni madai ya mleta maombi kuwa alisimamishwa kazi na Mjibu Maombi. Ameeleza hayo kwa kina mbele ya Tume na hata mbele ya Mahakama hii. Mleta Maombi anadai ya kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 39 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ni wajibu wa mwajiri kuthibitisha madai dhidi ya Mwajiriwa. Kifungu rejewa kimetafsiriwa kwa usahihihi na wakili Mwanri. Kifungu hicho hutumika pale ambapo mwajiri amemuachisha Mwajiriwa kazi na kupitia kifungu hicho mwajiri anajukumu la kuthibitisha endapo uachishwaji kazi huo ulikua halali kwa sababu za msingi na kufuata taratibu za kisheria. Lakini katika shauri hili, kama ambavyo mawasilisho ya pande zote mbili yanajieleza, mgogoro mbele ya Tume ulikuwa ni kusimamishwa kazi (suspension) na sio kusitishwa kazi (termination of employment). Mleta Maombi ameeleza tu kuwa alisimamishwa kazi kwa njia ya mdomo hivyo hakuna barua yoyote yakuthibitisha madai yake. Lakini pia Mleta Maombi amesisitiza kuwa alisimamishwa kazi na alimuandikia barua Mjibu Maombi yakutaka kumueleza amemsimamisha kwa muda gani. Barua hiyo ilipokelewa kama kielelezo Y3. Katika barua hiyo mleta maombi ameeleza kuwa alisimamishwa kazi mnamo tarehe 01/11/2022 na Operation Manager aitwaye Bakari Rashid Ally. Hivyo basi kupitia barua hiyo alimuomba Mjibu Maombi ampatie barua rasmi yakumsimamisha kazi lakini pia aeleze amemuachisha kazi kwa muda gani. Mjibu Maombi hakujibu barua hiyo na katika utetezi alieleza kuwa walipokuwa kwenye mchakato wakujibu barua husika walipokea fomu ya malalamiko kutoka Tume hivyo wakaona barua hiyo wataijibu mbele ya Tume. Kumbukumbu zinaonesha na hakuna ubishi kuwa siku ya tarehe 01/11/2022 Mjibu Maombi aliendesha kikao cha nidhamu dhidi ya Mleta Maombi. Ilielezwa yakuwa licha ya kwamba mleta maombi aliitikia wito wa kuhudhuria kikao husika hakufanikiwa kukaa kwenye kikao hicho mpaka mwisho. Kwamba, katika taarifa ya kuhudhuria kikao (kielelezo Y2) alielekezwa aende na mwanasheria wake lakini yeye akahudhuria na mdhamini wake. Hivyo basi kwakuwa wajumbe wa kikao husika hawakuona umuhimu wa mdhamini kwakuwa mambo yaliyotakiwa kujadiliwa yalikuwa ya kisheria, mdhanini huyo hakuruhusiwa kushiriki katika kikao hicho. Baada ya mdhamini kutoruhusiwa na mleta maombi naye aliondoka na hakuhudhuria katika kikao hicho. Katika fomu ya kuanzisha shauri mbele ya Tume (CMA FI) Mleta Maombi ameeleza kuwa mgogoro huu umezuka tarehe 02/11/2022. Ni wazi kuwa alimaanisha siku hiyo ndiyo siku aliyosimamishwa kazi. Lakini katika Ushahidi wake mbele ya Tume Mleta Maombi aleleza kuwa alisimamishwa kazi tarehe 01/11/2022 baada ya Mleta Maombi kumaliza kikao cha nidhamu kilichoendeshwa bila yeye kuwepo. Ushahidi huo wa mleta maombi ni wazi kuwa unakinzana na kile alichoelezea katika CMA FI. Sasa Mahakama inajiuliza endapo Mleta Maombi asimamishwa kazi tarehe 02/11/2022 kama alivyoelezea katika CMA FI je aliasimamishwa kwa njia gani? Alipigiwa simu au la? Mkanganyiko huo Pamoja na Ushahidi uliotolewa na upande wa Mjibu Maombi Mahakama inaona kuwa madai ya Mleta Maombi yameshindwa kuthibitishwa. Mjibu Maombi pia ameyapa nguvu maelezo yake kwa kutoa kielelezo Y2 ambacho ni hati ya malipo ya mshahara wa Mleta Maombi aliopokea tarehe 04/11/2022. Ni wazi kuwa mpaka tarehe hiyo aliruhusiwa kwenda kazini na baada ya kupokea mshahara wake kwasababu anazozijua mwenyewe aliamua kutokwenda kazini. Hivyo basi Mahakama inaona ya kuwa maombi haya hayana mantiki. Ni wazi kuwa Tume ilipitia na kuchanganua ushahidi uliotolewa mbele yake kwa ufasaha na kufikia maamuzi sahihi kuwa Mleta Maombi li hakusimamishwa kazi kama alivyodai. Hivyo basi madai yake yameshindwa kuthibitishwa. Shauri hili linatupiliwa mbali. Imeamriwa hivyo. YJ. Mlyambina JAJI 09/04/2024 Hukumu hii imesomwa na kutolewa leo tarehe 09/04/2024 mbele ya Mleta Maombi pekee. Haki ya kuata Rufaa ipo wazi. YJ. MlyamBma JAJI 09/04/2024