yapi merkeziinsaat sanayi anonim sirketi vs yakob amir jongo 2022 tzhcld 717 11 agosti 2022
The applicant failed to provide sufficient and timely reasons for non-appearance before the CMA. The applicant's conduct showed lack of diligence, and the right to be heard was not violated as the applicant was given opportunities but failed to utilize them. Therefore, there were no grounds to set aside the ex parte...
Source-derived case information.
- Citation
- yapi merkeziinsaat sanayi anonim sirketi vs yakob amir jongo 2022 tzhcld 717 11 agosti 2022
- Parties
- Applicant: YAPI MERKEZIINSAAT SANAYI ANONIM SIRKETI; Respondent: YAKOB AMIR JONGO
- Court
- TANZLII
- Jurisdiction
- Tanzania
- Judgment Date
- 1 January 2022
- Procedural Posture
- Labour Revision / Judgment on Application to Set Aside Ex Parte Award
- Outcome
- Application dismissed
- Legal Topics
- Setting Aside Ex Parte Award, Right to Be Heard, Procedural Fairness
- Source Language
- en
Source-derived case record
Summary, issues, holding and outcome
More case intelligence is available
Unlock the full research layer for this judgment.
Parties
YAPI MERKEZIINSAAT SANAYI ANONIM SIRKETI
Applicant
YAKOB AMIR JONGO
Respondent
Procedural Posture
Labour Revision / Judgment on Application to Set Aside Ex Parte Award
Legal Issues
- 1 Whether the applicant provided sufficient grounds to set aside the ex parte award of the Commission for Mediation and Arbitration (CMA)
- 2 Whether the applicant was denied the right to be heard before the CMA
Ratio Decidendi
The applicant failed to provide sufficient and timely reasons for non-appearance before the CMA. The applicant's conduct showed lack of diligence, and the right to be heard was not violated as the applicant was given opportunities but failed to utilize them. Therefore, there were no grounds to set aside the ex parte award.
Court Disposition
Application dismissed
Orders
- Each party to bear its own costs
Full Case Text
Judgment text and source record
1 paragraphs
MAHAKAMA KUU YA TANZANIA DIVISHENI YA KAZI PAR ES SALAAM MAREJEO NA. 160 YA 2022 YAPI MERKEZIINSAAT SANAYI ANONIM SIRKETI ..... ....... MLETA MAOMBI DHIDIYA YAKOB AMIR JONGO....................... ...... MJIBU MAOMBI (Kutokana na Uamuzi wa Tume ya Ushuluhishi na Uamuzi kanda ya DSM- Pwani) (Lyimo: Muamuzi) Tarehe 20. 04. 2022 < katika CMA/PWN/KBH/MISC APP/05/2021 | HUKUMU 06. 07 & 11.08. 2022 Rwizile J Mleta maombiameleta maombi haya akipinga maamuzi ya Tume ya Usuluhishi nd. Uarriuzi ('Tume') akilomba mahakama itengue maamuzi hayo. Katika hati ya Taarifa ya maombi mleta maombi ameomba amri zifuatazo:- i. Kwamba, iipendeze mahakama hii tukufu kuitisha taarifa za nyaraka, kurejea, kutengua na kuweka kando uamuzi wa upande mmoja wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Na. CMA/PWN/KBH/MISC APP/05/2021 ambao ulitolewa mnamo tarehe 20.04.2022 kwa mkono wa Mheshimiwa Joyce Lymo, Muamuzi na kupokelewa na mleta maombi mnamo tarehe 09.05.2020. ii. Kwamba, Mahakama hii tukufu iweze kutoa amri nyingine yoyote ambayo itaona inafaa kutolewa. Maombi haya yameambatana pamoja na kiapo cha Bv^ana Benedict Katare, Afisa sheria wa mleta maombi. Mjibu maombi kwa upande wake aiipinga vikali maombi haya kwa kuwasilisha kiapo kinzani. Katika hati ya kiapo mleta maombi ameeleza kuwa anaiomba mahakama itengue maamuzi ya Tume kutokana na hbja zifuatazo:- i. Kwamba iwapo ilikuwasahihi kisheria kwa Muamuzi kutoa Tuzo ya gharama za madhara kiujumla bila uthibitisho wowote. ii. Kwaqiba,, iwapo nl. sahihi kwa Muamuzi kuanisha kwamba mleta maoijibi hajawahi kufika wala kuhudhuria kikao chochote tangu mgogoro huu ulipofunguliwa mbele ya Tume. iii. Kwamba, iwapo ilikuwa sahihi kisheria kwa Muamuzi kuendelea kusikiliza mgogoro upande mmoja hata baada ya kupokea taarifa na uthibitisho wa wito kutoka Mahakama Kuu iliyowasilishwa na mleta maombi. iv. Kwamba, iwapo ilikuwa sahihi na halali kisheria kwa Muamuzi kutoa amri na kuendelea kusikiliza mgogoro upande mmoja bila kutoa taarifa kwa wadaawa. v. Kwamba, uamuzi uliotolewa na Muamuzi ulikuwa ni kinyume cha sheria ambapo ni kosa kwenye kumbukumbu za kisheria. vi. Kwamba, iwapo mwakilishi wa mlalamikiwa alikuwa na mamlaka kisheria kumwakilisha mjibu maombi. vii. Kwamba, Mwamuzi alikosea katika hoja na sheria kwa kushindwa kuangalia kwa makini vielelezo vilivyowasilishwa mbele ya Tume kama mkataba wa ajira na kufikia Kutoa maamuzi yanayo kinzana na mkataba huo unaozifunga pande zote mbili. Mawasilisho katika shauri hili yalifanywa kwa njia ya mdomo. Mbele ya Mahakama hiUm^ aliwakilishwa na wakili Ceasor Kabisa ilihali wakili Fredrick Msumaii alimwakilisha mjibu maombi. Wakati wa^kufanya mawasilisho yake wakili Kabisa aliomba kiapo cha mleta maombi kizingatiwe. Wakili huyo alitupilia mbali baadhi ya hoja na kubakiza hoja ya tatu na tano tu. Katika hoja ya tatu wakili Kabisa alieleza kuwa kuna taarifa zilizowasilishwa mbele ya Muamuzi tarehe 30.06.2021, ambazo ni wito kutoka Mahakama Kuu kitengo cha kazi katika Marejeo Na. /' 3 11/2021 iliyopangwa kusikilizwa mbele ya Mhe. Jaji Mwipopo. Alieleza kuwa taarifa hiyo ilifikishwa mbele ya Tume na afisa Rasilimali watu lakini mwamuzi aliikataa kwa madai kuwa ilichelewa. Alieleza kuwa hoja hiyo ilikuwa ni sababu tosha kuairisha shauri. Katika hoja ya tano wakili Kabisa alieleza kuwa maamuzi yana kasoro kwakuwa Muamuzi alienda kinyume na sheria na utaratibu kwa kutoa fidia inayozidi na iliyo kinyume na sheria. Alisema kuwa Muamuzi alitoa fidia ya madhara kiujumla (General damage) ya milioni kumi (10) bila uthibitisho wowote jambo ambalo lilishakataliwa na Mahakama katika kesi ya Tanzania Ports Authority Vs. Erick Kataro, Revision No. 670/2019 Mahakama Kuu, Dar es Salaam. Wakili huyo aliomba maamuzi ya Mahakama hii yaongozwe na Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano^va Tanzania/ 1977. Mwisho, alihisihi mahakama ikubali maombi haya. 1 :■:? 'O' Akijibu hoja wakili Msumali nae aliomba kiapo kinzani cha mjibu maombi kiwe sehemu ya mawasilisho yake. Kuhusu hoja ya tatu alieleza kuwa aliyoeleza wakili Kabisa ni tofauti na yale aliyoeleza wakati wa kusikilizwa kwa maombi yake mbele ya Tume. Alieleza kuwa Tume ilikataa maelezo yake kama inavyoonekana katika ukurasa wa 5 wa maamuzi ya f4 Tume. Wakili Msumali aliendelea kueleza kuwa hati ya wito aliyopewa tarehe 28.06.2022 iliwasilishwa mbele ya tume kupitia maombi ya kutengua uamuzi wa upande mmoja. Alieleza kuwa wito huo haukuifikia Tume siku shauri linaitwa kusikilizwa shauri la msingi hivyo hapakuwa na sababu ya msingi kwa Tume kumruhusu. Kwa mazirigira hayo alieleza kuwa mleta maombi alipewa nafasi ya kusikilizwa. Kuhusu hoja ya tano alieleza kuwa hoja hiyo ni mpya mleta maombi hakuisema katika maelezo yake mbele ya Tume. Aliongeza kuwa hata kwenye kiapo chake mbele ya Tume; hoja, zake hazikuwa na mashiko. Kwamba Tume ilitoa uamuzi kwa kuzingatia ushahidi wote. Hivyo wakili Msumali aliomba Mahakama Itupilie mbali shauri hili pamoja na kuangalia kasoro zilizopo katika kiapo kinachounga mkono maombi haya. Katika^ mawasilisho ya nyongeza wakili Kabisa hakuwa na chakuongeza, Baada ya kupitia mawasilisho ya pande zote mbili mahakama inaona inatakiwaWtatua hoja ya msingi ya endapo mleta maombi alieleza sababu za msingi za kuweza kutengua maamuzi ya upande mmoja. Katika shauri hili kumbukumbu zinaonesha kuwa Tume iliendelea kusikiliza shauri upande mmoja baada ya mleta maombi kushindwa Z 5 kuhudhuria siku ambayo shauri lilipangwa kusikilizwa. Katika maelezo yake mbele ya Tume mleta maombi alieleza kuwa alikuwa na taarifa kuwa shauri lao lilipangwa tarehe 08.06.2021 lakini alishindwa kuhudhuria hivyo alitoa hudhuru hivyo shauri lilihairishwa hadi tarehe 30.06.2021. Aliendelea kueleza kuwa tarehe 30.06.2021 ambapo shauri lilikuwa limepangwa kusikilizwa wakili wa mleta maombi alikuwa na kesi katika Mahakama Kuu ambayo ni Marejeo Na. 11/2021 kati ya Kearsey Travel & Tours Vs. Halidi Kiponza mbeie ya Mheshimiwa A. MWipppo. Kwamujibu wa vielelezo vilivyopo mbele ya Mahakama hii hakuna ubishi kuwa mnamo tarehe 30.06.2021 wakili wa mleta maombi alikuwa na shauri katika mahakama hii. Jambo ambaio Tume inaona sio sawa ni kitendo cha wakili wa mleta maombi kuppkea wito wa mahakama kuu tokea tarehe 28.06.2024 lakini ^kashlnda kutoa taarifa mapema mbele ya Tume kwamba atashindwa kuendelea na shauri siku hiyo pangwa. jambo hilo linaopesha |abisa wakili huyo hakuwa makini katika kuzingatia shauri lililokuwambele ya Tume. Lakini hata hivyo kutokana na mwenendo wa mleta maombi kushindwa kuhudhuria Tume bila sababu za msingi tarehe ya nyuma ambapo shauri hilo lilipangwa kinaonesha wazi hakuwa na / 6 mwenendo mzuri mbele ya Tume. Hivyo basi kwa mazingira hayo naona kuwa Tume ilikuwa sahihi kuendelea na shauri upande mmoja. Vilevile, kama ambavyo imeelezwa na wakili wa mjibu maombi nakala ya wito wa Mahakama Kuu mleta maombi aliiwasilisha wakati akifanya maombi ya kutengua maamuzi ya upande mmoja na sio siku arpbayo shauri lilipangwa kusikilizwa. Hivyo basi endapo wito huo wa mahakama Kuu ungekuwa umewasilishwa siku ya kusikijga shauri Tume Muamuzi angeuzingatia na shauri lingeweza kuhairishwa mpaka tarehe nyingine. Pamoja na hayo ifahamike kuwa mleta maombi ni kampuni ambayo ina wafanyakazi wengi hivyo kama angekuwa anazingatia uwepo wa shauri hilo mbele ya Tume mmoja wa wafanyakazi angeteuliwa na kwenda kutoa taarifa ya wakili kutohddhuria. Kama kumbukumbu zinavyoonesha hilo pia halikufanyika. Mahakama inaona kuwa mleta maombi alipewa haki ya kusikilizwa,kikamilifu lakini yeye mwenyewe alishindwa kutumia haki yake kw^kudha|§y| kuhudhuria Tume bila ya sababu zozote za msingi. Mwenendo huo wa mleta maombi hauwezi kuvumiliwa na mahakama kwakuwa ndio unaokwamisha upatikanaji wa haki kwa wakati. Kutokana na sababu zilizoelezwa hapo juu ni wazi kuwa mleta maombi ameshindwa kueleza sababu za msingi za kuifanya Mahakama itengue maamuzi ya Tume. Hivyo basi, kwakuwa mleta maombi ameshindwa kueleza sababu za msingi kwanini alishindwa kuhudhuria Tume, Mahakama inaona maombi haya hayana mashiko na yanatupiliwa mbali. Kila upande utajilipia gharama. A.K. Rwizile JAJI 11.08.2022