Download PDF

Tanzania Judgment

TANZLII

MAOMBI YA MAREJEO NA 277 OF 2023 JUMA MOSHI LUGELO VRS TAN CHOICE LTD

On this page

Professional case brief

Research organized from the available case record

Source document

01

Holding and result

The applicants' persistent absenteeism, evidenced by attendance records and repeated warnings, constituted a valid and sufficient ground for dismissal. The disciplinary process and sanction were appropriate and lawful under the cited legal provisions and precedents.

Court disposition

Application dismissed

Orders

  • Application for revision is dismissed
  • Decision of the Commission for Mediation and Arbitration is upheld
  • Each party to bear its own costs

02

Material facts

Parties

Juma Moshi Lugelo

Applicant Counsel: Edward Simkoko

Ikiwani Udodo Hassan

Applicant Counsel: Edward Simkoko

Tan Choice Ltd

Respondent Counsel: Ceasor Kabisa

Amounts and remedies

  • Claimed Compensation: TZS 5,023,537

03

Procedural history

  1. Posture

    Labour Revision / Judgment

04

Questions and positions

Legal issues

Party arguments

Applicant
Applicants argued there was no valid reason for dismissal as their absence was only for two days, and that the employer's decision contravened Rule 12 of GN No. 42 of 2007, which requires consideration of alternative penalties. They cited case law stating absence for less than five days is not a sufficient ground for dismissal.
Respondent
Respondent argued the dismissal was justified due to habitual absenteeism, which affected operations and caused losses, and that the applicants had been repeatedly warned. Cited case law supports that persistent absenteeism, even if not consecutive, is a valid ground for dismissal.

05

Court’s reasoning

  1. 01

    Section 39 of the Employment and Labour Relations Act, Cap 366 (R.E. 2019)

    Employer must prove validity of termination.

  2. 02

    Rule 12(4)(b) of GN No. 42 of 2007

    In disciplinary matters, prior warnings and records may be considered in determining appropriate sanction.

  3. 03

    Bulyamhulu Gold Mine Ltd v. George Allen Gwabo, Revision No. 48 of 2015

    Persistent absenteeism, even if not consecutive, is sufficient ground for dismissal.

06

Ratio, limits and disposition

Ratio decidendi

The applicants' persistent absenteeism, evidenced by attendance records and repeated warnings, constituted a valid and sufficient ground for dismissal. The disciplinary process and sanction were appropriate and lawful under the cited legal provisions and precedents.

Court disposition

Application dismissed

  • Application for revision is dismissed
  • Decision of the Commission for Mediation and Arbitration is upheld
  • Each party to bear its own costs

Source and reliance status

TANZLII · 1 January 2023

This page organises the available record for research. Confirm quotations, current status, and subsequent treatment against the official source before relying on the case.

Judgment reading view

Judgment text

The complete available source text.

Source document

TANZLII

Judgment· 1 January 2023

MAOMBI YA MAREJEO NA 277 OF 2023 JUMA MOSHI LUGELO VRS TAN CHOICE LTD

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAHAKAMA KUU YA TANZANIA

DIVISHENI YA KAZI

ILIYOKETI DAR ES SALAAM MAOMBI YA MAREJEO NA. 277 YA 2023 (Marejeo yanatokana na uamuzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ya PWN iliyoketi Kibaha, Tarehe 14 Septemba 2023 katika Mgogoro wa Kazi Na. CM A/PW N/KBH/87/2022/28/2022)

BAIN A YA JUMA MOSHI LUGELO.......................................................MLETA MAOMBI N A .l IKIWANI UDODO HASSAN.......................... ......... .....MLETA MAOMBI NA.2 NA TAN CHOICE LTD........................................................................ MJIBU MAOMBI

HUKUMU Tarehe ya mwisho ya Amri; 4/4/2024 Tarehe ya Hukumu: 31/5/2024 OPIYQ. J. Marejeo haya yanatokana na uamuzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi katika Mgogoro wa Kazi Na. CMA/PWN/KBH/87/2022/28/2022. ju m a m oshi lu g e lo n a m w e n za k e ambao ni waleta maombi wanaomba Mahakama hiii ipitie na kutengua, na mara baada ya kutengua imuamuru mjibu maombi kuwalipa waleta maombi fidia isiyopungua kiasi cha fedha Tsh 5,023,537/= na kutoa nafuu nyingine yoyote ambayo waleta maombi wanastahili kupata. Historia fupi ya shauri hili ni kwamba waleta maombi waliajiriwa kwa nyakati tofauti kwa kufanya kazi ya kuchinja na kutunza wanyama aliajiriwa kwa mkataba wa mwaka mmoja. Mahusiano ya kiajira yalikoma tarehe 23/11/2023 baada ya mwajiri/mjibu maombi kusitisha ajira ya waleta maombi kwa madai ya utovu wa nidhamu unaotokana na utoro kazini. Waleta Maombi hawakuridhika na maaumuzi hayo, hivyo kupelekea kufunguliwa kwa mgogoro wa kazi mbele ya Tume. Hata hivyo Tume ilitupilia mbali madai ya waleta maombi kwa kuona uachishwaji kazi ulikuwa wa haki na kisheria, hivyo kupelekea kufunguliwa kwa maombi haya. Maombi haya, yaliambatana na kiapo cha Pamoja cha waleta maombi, ambacho kikielezea mtririko mzima wa mgogoro huu uliopelekea maombi haya kama ilivyoelezwa hapo juu, ambapo waleta maombi wanadai muamuzi alikosea kimantiki na kisheria kwa kuamua kwamba mjibu maombi alikuwa na sababu za

msingi za kuwaachisha kazi, kwa kutumia kumbukumbu za nyuma ambazo hazikuwahi kufanyiwa uchunguzi. Shauri hili lilisikilizwa kwa njia ya maandishi, ambapo waleta Maombi waliwakilishwa na Bw. Edward Simkoko, Mwakilishi Binafsi. Wakati mjibu maombi aliwakilishwa na Bw. Ceasor Kabisa, wakili. Mahakama hii imezingatia mawasilisho ya pande zote mbili, ambayo yatatumika katika uamuzi huu. Hata hivyo hoja bishaniwa katika shauri hili ni je palikuwapo na sababu ya msingi ya uachishwaji kazi inayoendana na adhabu ya uachishwaji kazi na je mjibu maombi alikuwa sahihi kuwaachisha kazi waleta maombi kwa kutumia kumbukumbu za nyuma ambazo hazikufanyiwa utafiti. Kuhusu hoja ya kwanza ya kwamba je palikuwapo na sababu ya msingi ya uachishwaji kazi inayoendana na adhabu ya uachishwaji kazi, Bw. Simkoko alieleza kwamba hapakuwepo na sababu ya msingi ya kuwaachisha kazi waleta maombi kwa kutohudhuria kazini kwa muda wa siku mbili, alieleza ya kwamba maamuzi ya mjibu maombi yanaenda kinyume na msimamo wa sheria ikiwepo Kanuni ya 12 ya T.S Na.42 la 2007 inayomtaka muamuzi katika makosa ya nidhamu kuzingatia adhabu mbadala na siyo kuachisha kazi. Katika kuipa nguvu hoja yake alirejea kesi Constantine Victor John v. Muhimbili National Hospital, Maombi ya Madai Na.188/01 ya 2021 na kesi ya Sunder Chemical Fiber Limited v. Judith Thadey Mrosso, Marejeo Na.432 ya 2023 ambazo zimetoa msimamo ya kwamba

kutofika kazini kwa siku zisizozidi (5) tano, siyo sababu ya msingi kumwachisha mfanyakazi kazi. Kwa upande wa mjibu maombi alieleza ya kwamba muamuzi alikuwa sahihi kwa kuamua ya kwamba palikuwepo na sababu ya msingi ya uachishwaji kazi kutokana na ushahidi uliotolewa, kwani waleta maombi walikuwa na mazoea ya utoro kazini jam bo lililopelekea kuathiri shughuli za utendeji na hasara kwani mjibu maombi kuna wakati ilibidi awaajiri vibarua wa muda ili wafanye kazi za waleta maombi. Aliendelea kwa kueleza ya kwamba kutokana na uasili wa kazi ya mwajiri waleta maombi hawakutakiwa kuwa watoro kazini. Katika kutilia mkazo hoja yake alirejea kesi ya Bulyamhulu Gold Mine Ltd v. George Allen Gwabo, Marejeo Na. 48 ya 2015, Mahakama kuu, Divisheni ya Kazi ambayo ilitoa msimamo wa kisheria ya kwamba utoro uliokithiri japokuwa sio mfulilizo ni sababu tosha ya kumwachisha mwajiriwa kazi. Katika kujibu hoja ya uwepo wa sababu ya uachishwaji kazi ni wazi ya kwamba kwa mujibu wa K/F cha 39 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini, Sura ya 366 Marekebisho ya 2019, kinamtaka mwajiri kuthibitisha uhalali wa uachishwaji kazi. Katika shauri hili kielelezo D9 (rejista ya mahudhurio) inaonyesha baadhi ya siku ambazo waleta maombi hawakufika kazini pasipokuwa na kibali cha ruhusa. Pia hakuna ubishi ya kwamba ni mara nyingi waleta maombi wamekuwa hawafiki Hata hivyo kwa mujibu wa Kanuni ya 12(4)(b) T.S

Na. 42 la 2007 ni wazi inatamka kwamba katika kuamua kama uachishwaji kazi ni adhabu sahihi, mwajili ataangaiia vitu vingi ikiwepo taarifa za nyuma za mwajiriwa, jam bo ambaio iimejidhihiiisha katika shauri hili ambapo Kielelezo D7(onyo la mdomo) na D8 (onyo la maandishi) vinaonyesha waleta maombi, kila mmoja ameonywa zaidi ya mara moja juu ya tabia ya utoro na hivyo kwa mtizamo wa Mahakama hii inaona ni utoro uliokithiri, hivyo kuikubali hoja ya mjibu maombi kama ilivyojadiliwa katika Kesi tajwa hapo juu, kesi ya Buiyamhulu Gold Mine Ltd v. George Allen Gwabo, Marejeo Na. 48 ya 2015, Mahakama kuu, Divisheni ya Kazi ambayo ilitoa msimamo wa kisheria ya kwamba utoro uliokithiri japokuwa sio mfulilizo ni sababu tosha ya kumwachisha mwajiriwa kazi. Kutokana na msimamo wa kisheria hapo juu ni wazi ya kwamba muamuzi wa tume alikuwa sahihi si tu kwa kuamua ya kwamba palikuwapo na sababu ya msingi bali adhabu ya uachishwaji kazi ilikuwa sahihi, kwa sababu walete maombi walikwishaipata nafuu nyingine baada ya mwajiri kuwapa onyo mara kwa mara pasipokuwepo mabadiliko. Katika msimamo huu hoja ya pili ya waleta maombi kwamba hapakuwa na uchunguzi inakosa mashiko kwani hakuna ubishi ya kwamba wamekuwa na tabia ya kutofika kazini kulingana na rejista ya mahudhurio katika kielelezo D9. Katika mazingira haya nayakataa maombi haya ya Marejeo kwa kuwa hayana mashiko kisheria, na kushikilia maamuzi ya Tume. Kila upande Utabeba gharama zake katika shauli hili. Amri hii irnetolewa leo.

Source wording is retained. Consult the source document for its original formatting and pagination.

Authorities

Authorities used by the court

Cases, legislation, regulations, and constitutional provisions identified in the available record.

Constantine Victor John v. Muhimbili National Hospital, Labour Application No. 188/01 of 2021

Case cited

Sunder Chemical Fiber Limited v. Judith Thadey Mrosso, Revision No. 432 of 2023

Case cited

Bulyamhulu Gold Mine Ltd v. George Allen Gwabo, Revision No. 48 of 2015

Case cited

Employment and Labour Relations Act, Cap 366 (R.E. 2019)

Legislation

Legislation referenced in the available case record.

GN No. 42 of 2007

Legislation

Legislation referenced in the available case record.

Case-aware research

Ask AI about this case

The judgment and available research above are public. New questions open in a separate private conversation grounded in this case.

About this LexChat collection

This page organizes the available case record for research. Verify quotations, current status, and subsequent treatment against the source document. Corrections can be reported to hello@esheria.ai.

Legal information, not legal advice. Research summaries do not replace the judgment.